" Freely you have received, freely give " (Matthew 10:8)

HOME  |  SITEMAP  |  CONTACT US  |  HELP    
 Absolutely FREE Printed Book
- Swahili edition # 7

 


JE, NYAKATI ZA MPINGA KRISTO, KUFIA-DINI, KUNYAKULIWA NA UFALME WA MILENIA ZINAKUJA? ( I )

 

Dokezo

Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo

Maelezo ya Kina

Baada ya mashambulio ya kigaidi ya tarehe 11 mwezi Septemba kulitokea msongamano katika tovuti hii "www.raptureready.com," ambayo ni tovuti inayotoa habari juu ya nyakati za mwisho, iliripotiwa kuwa watumiaji wa tovuti hiyo walizidi zaidi ya milioni 8. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa ushirikiano kati ya kituo cha CNN na kile cha TIME ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 59 ya Wamarekani wanaamini katika mafundisho ya siku za mwisho.

Akijibu masuala hayo ya nyakati, mwandishi anatoa ufafanuzi wa mada kuu za kitabu cha Ufunuo, zikiwemo mada za kuja kwa Mpinga-Kristo, Kufia-Dini, yaani kufa kwa watakatifu kwa ajili ya dini, Kunyakuliwa, Ufalme wa Milenia, na Mbingu na Nchi Mpya, zote zikitoka katika mazingira ya maandiko yote na chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.
Kitabu hiki kinatoa maelezo katika mfumo wa komentare wa aya kwa aya toka katika Kitabu cha Ufunuo huku aya hizo zikiongezewa nguvu na mahubiri ya kina toka kwa mwandishi. Yeyote atakayesoma kitabu hiki atakuja kuifahamu mipango ambayo Mungu anayo kwa ulimwengu huu.

Sasa ni wakati wako kutambua juu ya hitaji kamilifu la kuamini katika injili ya maji na Roho ili uweze kuipata hekima inayoweza kukukomboa toka katika majaribu na taabu zote za nyakati za mwisho. Kwa kupitia vitabu hivi viwili na kwa kuamini katika injili ya maji na Roho utaweza kuyashinda majaribu na taabu zote zilizotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo.


Kutoka kwa Mchapishaji

Mwandishi amekuwa akiihubiri injili ya maji na Roho kwa nafsi zilizopotea katika ulimwengu huu kwa takribani miongo miwili sasa.
Kama mwanzilishi wa Huduma ya Utume wa Maisha Mapya (The New Life Mission), kwa sasa anawaelekeza na kuwatia moyo wanafunzi wengi wa Yesu katika shule ya kimissionari ya Utume wa Maisha Mapya (The New Life Mission School).
Baada ya kuanzisha makanisa ya kimissionari, kwa sasa anaieneza injili kwa kupitia kazi zake za kiuandishi.
Kwa sasa vitabu vyake vimetafsiriwa na vinasomwa katika zaidi ya lugha kuu 52 ulimwenguni.


 
Free Christian Books
    Printed Book List
    Swahili edition 7
 
 • About this book
 •  
 • Table of Contents
 •     About free book service
      How to request free books?
      FAQ
  View
  Basket
   
  Partner's Zone

  register as a coworker
  Bookmark
     
  Copyright © 2001 - 2019 The New Life Mission. All Rights Reserved.