Swahili 8

  • ㆍISBN : 9788928209972
  • ㆍPages : 471

Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo - JE, NYAKATI ZA MPINGA KRISTO, KUFIA-DINI, KUNYAKULIWA NA UFALME WA MILENIA ZINAKUJA? (Ⅱ)

Paul C. Jong

Wakristo wengi siku hizi wanaiamini nadharia ya kunyukuliwa kabla ya dhiki. Kwa kuwa wanaiamini nadharia hii potofu, inayowaeleza kuwa watanyakuliwa kabla ya kuja kwa ile Dhiki Kuu ya miaka saba, ndio maana wanaendelea kuishi maisha ya kidini ya kivivu yanayojengwa katika haki binafsi.
Lakini kunyakuliwa kwa watakatifu kutatokea baada ya mapigo yatakayotokana na tarumbeta la saba, yaani hadi pigo la sita litakapokuwa limemiminwa- yaani, kunyakuliwa kutatokea baada ya kuonekana kwa Mpinga Kristo katikati ya machafuko ya kidunia, wakati ambapo watakatifu waliozaliwa tena upya watakuwa wameuawa kwa kuifia-dini, na wakati ambapo tarumbeta la saba litakapokuwa limeshapigwa. Ni wakati huo ndipo Yesu atakaposhuka toka mbinguni, na hapo ndipo ufufuo na kunyakuliwa kwa waliozaliwa tena upya kutakapotokea (1 Wathesalonike 4:16-17).
Siku hii, kila mtu katika ulimwengu huu atakuwa amesimama katika njia panda kuhusiana na hatma yake ya milele. Watakatifu waliozaliwa tena upya kwa kuamini katika "injili ya maji na Roho" watafufuliwa na kunyakuliwa, kisha watakuwa warithi wa Ufalme wa Milenia na Ufalme wa Mbinguni wa milele, lakini wenye dhambi ambao hawakuweza kushiriki katika ufufuo huu wa kwanza watakutana na adhabu kuu ya mabakuli saba yatakayomiminwa na Mungu na kisha watatupwa katika moto wa milele wa kuzimu.
Hivyo, ni lazima sasa uachane na nadharia potofu za kidini pamoja na tamaa na miiko potofu ya ulimwengu huu, na kisha uingie katika Neno la Mungu la kweli. Ninatumaini na kuomba ili kwamba kwa kusoma mfululizo wa vitabu vyangu juu ya injili ya maji na Roho, basi ninyi nyote mtabarikiwa kwa dhambi zenu zote kuoshelewa mbali, na kisha kuupokea ujio wa Bwana wetu mara ya pili pasipo hofu.

AUDIOBOOK
SW/08/Ch8-1_Matarumbeta Yanayoyatangaza Mapigo Saba.mp3
Due to COVID-19 and disruption to international mail service
we have temporally suspended our ‘Free Print Book service’.
In the light of this situation we are not able to mail you the books at this time.
Pray that this pandemic will end soon and the resumption of the postal service.