Swahili 14

  • ㆍISBN : 9788928239122
  • ㆍPages : 333

Mfululizo wa Paul C. Jong Juu ya Ukuaji wa Kiroho Kitabu cha 3 - Waraka wa Kwanza wa Yohana (Ⅰ)

Paul C. Jong

Mtume Yohana ni mmoja kati ya viongozi wakuu wa kiroho katika Ukristo. Nyaraka zote tatu alizoziandika bado zinaushuhudia Ukweli mkuu wa kiroho kwa watakatifu katika Kanisa la Mungu. Lakini kuna baadhi ya vifungu ambavyo ni vigumu kwetu kuvielewa na kuvifafafanua vizuri.
Tunaweza kuangalia 1 Yohana 1:8 kama moja kati ya vifungu vigumu katka Nyaraka za Yohana: "Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu." Kifungu hiki ni kigumu sana kuweza kukifahamu, hasa pale tunapokitumia kwa waamini wanaoamini katika injili ya maji na Roho.
Mfano wa pili ni kifungu kinachopatikana katika 1 Yohana 1:9, "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote." Kifungu hiki ni kati ya vifungu ambavyo vimekuwa vikinukuliwa mara kwa mara na wenye dhambi wanapojaribu kutoa msingi wa kibiblia kuhusiana na sala zao za toba. Je, kifungu hiki kina maanisha kwamba wenye dhambi wanapaswa kuziungama dhambi zao ili waweze kusamehewa kutokana na dhambi walizozitenda? Au, je, kifungu hiki kina maanisha kwamba wenye haki wanaoamini katika injili ya maji na Roho wanapaswa kuziungama dhambi zao? Tunapaswa kukiamini kifungu hiki kwa mujibu wa ufafanuzi toka kwa Roho Mtakatifu, toka kwa Mwandishi wa Biblia, na kwa kuzingatia nia aliyokuwa nayo Mtume Yohana.
Mfano wa tatu kuhusiana na vifungu vigumu ni ule unaotoka 1 Yohana 2:22, "Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana." Kifungu hiki kinazungumzia juu ya maadui wa Mungu. Kifungu hiki kinaweka bayana kwamba maadui wa Mungu ni wale wasioamini kwamba Yesu ni Mungu. Na kwa kufanya hivyo maadui hao wanakana kwamba Mungu si Baba wa Yesu Kristo.
Mfano wa nne unatoka 1 Yohana 3:6 ambapo aya hii inasema, " Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua." Katika kifungu hiki tunapooma maneno yanayosema "Kila akaaye ndani yake," basi tunatambua kwamba kifungu hiki kimetolewa kwa ajili ya wenye haki walioasafishwa dhambi zao zote kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Wenye haki hawawezi kuikana imani yao katika hali yoyote ile, hii ni kwa sababu wanaiamini injili ya kweli. Je, inawezekana wakawepo baadhi ambao hawatendi dhambi kwa miili yao? Ukweli ni kuwa kila mmoja anatenda dhambi. Lakini waamini wa injili ya maji na Roho hawawezi kufanya dhambi ya kuikana injili ya kweli.

AUDIOBOOK
undefined
Due to COVID-19 and disruption to international mail service
we have temporally suspended our ‘Free Print Book service’.
In the light of this situation we are not able to mail you the books at this time.
Pray that this pandemic will end soon and the resumption of the postal service.