Swahili 15

  • ㆍISBN : 9788928239177
  • ㆍPages : 383

Mfululizo wa Paul C. Jong Juu ya Ukuaji wa Kiroho Kitabu cha 4 - Waraka wa Kwanza wa Yohana (Ⅱ)

Paul C. Jong

Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi unapaswa kuufahamu upendo wa Mungu kwa uhalisia kuliko kuufahamu kwa nadharia tu. Wale wanaomfahamu na kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wao ni lazima waufahamu upendo wa Mungu kwa uthabiti hasa kuhusiana na ondoleo la dhambi zao ambalo lilitimizwa kupitia Neno la injili ya maji na Roho. Ili tuweze kuufahamu upendo wa Mungu kwa kina basi tunapaswa kuwa waamini tunaoamini katika injili hii ya kweli. Upendo wa Mungu unajidhihirisha kwa kina na kwa uthabiti katika injili hii ya kweli. Kama tutaufahamu upendo wa Mungu, basi ufahamu wetuni lazima utokane na upendo thabiti wa Mungu kwetu sisi ambao umefunuliwa katika Ukweli wa injili ya maji na Roho. Ni hapo ndipo tunapoweza kuwaongoza wengine kuuendea upendo wa kweli wa Mungu.
Mtume Yohana anashuhudia kuwa Yesu Kristo, aliyekuja kwa maji, kwa damu, na kwa Roho Mtakatifu, ni Mungu Mwokozi mwenyewe. Kiini cha ushuhuda wake ni ule Ukweli wa ondoleo la dhambi, ambao unapatikana katika maji, damu, na Roho Mtakatifu.
Kama ilivyoandikwa katika Neno la Mungu, maji yana maanisha ni ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji, na damu ina maanisha ni hukumu ambayo Yesu aliipokea kwa ajili ya dhambi zetu zote. Pia, ushahidi wa wokovu wetu unajikita katika Roho Mtakatifu, maji, na damu (1 Yohana 5:8). Huduma za maji, damu, na Roho Mtakatifu ni za Mungu na ambazo kwa hizo amewakomboa wenye dhambi toka katika dhambi zao zote.

AUDIOBOOK
undefined
Due to COVID-19 and disruption to international mail service
we have temporally suspended our ‘Free Print Book service’.
In the light of this situation we are not able to mail you the books at this time.
Pray that this pandemic will end soon and the resumption of the postal service.