Swahili 9

  • ㆍISBN : 8983147571
  • ㆍPages : 414

HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA: Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo (Ⅰ)

Paul C. Jong

Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na ya Roho Mtakatifu tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili.
Kwa kweli, rangi za bluu, Zambarau, na nyuzi nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo.
Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho Mtakatifu, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika rangi za bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania.

AUDIOBOOK
SW/09/Ch01_Wokovu wa Wenye Dhambi Uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania.mp3
Due to COVID-19 and disruption to international mail service
we have temporally suspended our ‘Free Print Book service’.
In the light of this situation we are not able to mail you the books at this time.
Pray that this pandemic will end soon and the resumption of the postal service.