Livros cristãos gratuitos para estudos bíblicos sobre salvação, o Espírito Santo, o Tabernáculo e o Apocalipse de João

HOME  |  MAPA DO SITE  |  CONTATO  |  AJUDA    
 Livros impressos absolutamente grátis
- Edição em Swahili # 8

 


JE, NYAKATI ZA MPINGA KRISTO, KUFIA-DINI, KUNYAKULIWA NA UFALME WA MILENIA ZINAKUJA? ( II )

- Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo

 

Dokezo

Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo

Maelezo ya Kina

Wakristo wengi siku hizi wanaiamini nadharia ya kunyukuliwa kabla ya dhiki. Kwa kuwa wanaiamini nadharia hii potofu, inayowaeleza kuwa watanyakuliwa kabla ya kuja kwa ile Dhiki Kuu ya miaka saba, ndio maana wanaendelea kuishi maisha ya kidini ya kivivu yanayojengwa katika haki binafsi.
Lakini kunyakuliwa kwa watakatifu kutatokea baada ya mapigo yatakayotokana na tarumbeta la saba, yaani hadi pigo la sita litakapokuwa limemiminwa- yaani, kunyakuliwa kutatokea baada ya kuonekana kwa Mpinga Kristo katikati ya machafuko ya kidunia, wakati ambapo watakatifu waliozaliwa tena upya watakuwa wameuawa kwa kuifia-dini, na wakati ambapo tarumbeta la saba litakapokuwa limeshapigwa. Ni wakati huo ndipo Yesu atakaposhuka toka mbinguni, na hapo ndipo ufufuo na kunyakuliwa kwa waliozaliwa tena upya kutakapotokea (1 Wathesalonike 4:16-17).
Siku hii, kila mtu katika ulimwengu huu atakuwa amesimama katika njia panda kuhusiana na hatma yake ya milele. Watakatifu waliozaliwa tena upya kwa kuamini katika "injili ya maji na Roho" watafufuliwa na kunyakuliwa, kisha watakuwa warithi wa Ufalme wa Milenia na Ufalme wa Mbinguni wa milele, lakini wenye dhambi ambao hawakuweza kushiriki katika ufufuo huu wa kwanza watakutana na adhabu kuu ya mabakuli saba yatakayomiminwa na Mungu na kisha watatupwa katika moto wa milele wa kuzimu.
Hivyo, ni lazima sasa uachane na nadharia potofu za kidini pamoja na tamaa na miiko potofu ya ulimwengu huu, na kisha uingie katika Neno la Mungu la kweli. Ninatumaini na kuomba ili kwamba kwa kusoma mfululizo wa vitabu vyangu juu ya injili ya maji na Roho, basi ninyi nyote mtabarikiwa kwa dhambi zenu zote kuoshelewa mbali, na kisha kuupokea ujio wa Bwana wetu mara ya pili pasipo hofu.

Kutoka kwa Mchapishaji

Katika toleo la kwanza juu ya Kitabu cha Ufunuo, mwandishi aliandika kuwa Mungu amezipanga nyakati saba katika Majaliwa yake, na kwamba wakati wa farasi wa kijivujivu utatujia kwa haraka sana, na kwamba watu watateseka sana chini ya ukatili wa Mpinga Kristo; lakini watakatifu waliozaliwa tena upya wataweza kumshinda huyo Mpinga Kristo na kisha kuupata Ufalme wa Milenia na Mbingu na Nchi Mpya kwa kupitia imani yao sahihi iliyotolewa na Mungu.
Sasa, kwa kupitia toleo hili linalofuata, utaweza kuutambua ufahamu sahihi wa Neno hasa kuhusiana na sehemu zilizobakia za Kitabu cha Ufunuo, kuanzia sura ya 8 hadi ya 22.
Mwandishi anakushauri kuwa na imani imara katika ukweli kwamba unabii wote wa Kitabu cha Ufunuo utakuja kutimia: Hivi punde kutatokea mapigo ya matarumbeta saba; Mpinga Kristo atatokea, mauaji makubwa ya Mpinga Kristo kwa watakatifu wakiifia-dini; ufufuo na kunyakuliwa kwa watakatifu waliozaliwa tena upya katikati ya Dhiki Kuu; mapigo ya mabakuli saba yakimiminwa juu ya maadui wa Mungu; kuja kwa Ufalme wa Milenia; ufufuo wa pili wa wenye dhambi kwa ajili ya adhabu yao ya milele; watakatifu kuishi pamoja na Mungu katika Ufalme wa Mbinguni wa milele.
Miongoni mwa mambo haya yatakayokuja, kunyakuliwa kwa watakatifu kunapaswa kuwa ni jambo la kuzingatia kwa Wakristo wote. Je, unyakuo huu utatokea lini, na ni nani atakayeshiriki katika baraka hii?


 
Free Christian Books
    Lista dos livros impressos
    Edição Swahili 8
 
 • Sobre este livro
 •  
 • Tabela de conteúdos
 •     Sobre o serviço de livros gratuitos
      Como pedir os livros gratuitos?
      FAQ
  Ver
  cesta
   

  Bookmark
     
  Copyright © 2001 - 2019 The New Life Mission. ALL RIGHTS reserved.