Swahili 5

  • ㆍISBN : 8983143045
  • ㆍPáginas : 373

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (Ⅰ)

Paul C. Jong

Injili ya maji na Roho ni haki ya Mungu!

Maneno katika kitabu hiki yatatosheleza kiu ya moyo wako. Wakristo wa nyakati hizi wanaendelea kuishi pasipo kufahamu suluhisho halisi la dhambi za kila siku watendazo kila kukicha.
Je, unafahamu juu ya haki ya Mungu? Nadhani utajiuliza mwenyewe juu ya swali hili na hatimaye kuamini juu ya haki ya Mungu ambayo imedhihirishwa kupitia kitabu hiki.
Haki ya Mungu imekuwa ikiandamana na Injili ya maji na Roho. Hata hivyo kama ilivyo hazina yenye thamani imekuwa ikifichwa mbali na macho ya wafuasi wa washika dini wengi kwa miongo kadhaa. Namatokeo yake watu wengi wamekuwa wakitegemea na kujigamba juu ya haki zao binafsi badala ya ile haki ya Mungu. Kwa hiyo kanuni za Kikristo zisizo na maana zimetawala imani katika mioyo ya waumini wengi huku wakidhani kwamba ndizo zenye haki ya Mungu.
Kanuni za kuchaguliwa toka asili, kuhesabiwa haki na utakaso wa awamu kwa viwango, ni mojawapo ya kanuni kuu za mafundisho ya wakristo ambayo yameleta tafrani za kimawazo na utupu ndani ya nafsi za waumini.
Lakini sasa, wakristo wengi imewapasa kurudi na kuelewa upya juu ya Mungu, kujifunza juu ya haki yake na hatimaye kuendelea na imani iliyo na uhakika.
"Bwana wetu aliye haki ya Mungu" atakupatia nafsi yako uelewa mkuu na kukuongoza katika amani. Mwandishi anapenda uhodhi baraka ya kuifahamu haki ya Mungu.
Baraka ya Mungu iwe nanyi.

Audiolivro
SW/05/Ch1-1_Utangulizi katika Kitabu cha Warumi Sura ya 1.mp3
Devido ao COVID-19 e à interrupção do Serviço de Correio Internacional,
suspendemos temporariamente o nosso 'Serviço de Impressão Gratuita de Livros'.
Diante dessa situação, não podemos enviar os livros para você neste momento.
Ore para que esta pandemia termine em breve e retorne o serviço postal.