VITABU VILIVYOCHAPISHWA BURE,
VITABU NA VITABU VYA AUDIO

Waraka wa Kwanza wa Yohana

  • ISBN9788928239177
  • Kurasa383

Swahili 15

Mfululizo wa Paul C. Jong Juu ya Ukuaji wa Kiroho Kitabu cha 4 - Waraka wa Kwanza wa Yohana (Ⅱ)

Rev. Paul C. Jong

Yaliyomo
 
Dibaji 

SURA YA 3
1. Mungu Wetu Aliyekuja Kwetu Kwa Upendo wa Agape (1 Yohana 3:1-8) 
2. Ni Aina Ipi ya Dhambi Ambayo Hatupaswi Kuitenda 
3. Mbele za Mungu? (1 Yohana 3:9-16) 
4. Yeye Anayezishika Amri za Mungu Anakaa Ndani Yake (1 Yohana 3:17-24) 

SURA YA 4
1. Zijaribuni Roho Ikiwa Zinatokana na Mungu (1 Yohana 4:1-6) 
2. Kuanzia Sasa na Kuendelea Tunapaswa Kuishi Vipi? (1 Yohana 4:7-13) 
3. Tunapaswa Kukaa Katika Upendo wa Mungu (1 Yohana 4:16-21) 

SURA YA 5
1. Ni Ukweli Upi Unaotuweka Huru Toka Katika Dhambi Zetu Zote? (1 Yohana 5:1-4) 
2. Ni Nani Aliyezaliwa na Mungu? (1 Yohana 5:4-8) 
3. Je, Tunaamini Nini? (1 Yohana 5:1-11) 
4. Ni Ukweli Upi Uliotukomboa Toka Katika Dhambi Zetu Zote? (1 Yohana 5:1-12) 
5. Ushahidi Thabiti Unaotuokoa Toka Katika Dhambi Zetu Zote (1 Yohana 5:8-13) 
6. Kama Ndugu Anafanya Dhambi Isiyoleteleza Mauti, Mwombe Mungu Autunze Uhai Wake (1 Yohana 5:16-19) 
7. Yesu Ni Mungu wa Kweli na Uzima wa Milele (1 Yohana 5:20) 
8. Ingawa Tunaweza Kuwa na Mapungufu Wakati Wote, Upendo wa Mungu Mkamilifu Umetukomboa Toka Katika Dhambi za Ulimwengu (1 Yohana 5:1-21) 
 
Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi unapaswa kuufahamu upendo wa Mungu kwa uhalisia kuliko kuufahamu kwa nadharia tu. Wale wanaomfahamu na kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wao ni lazima waufahamu upendo wa Mungu kwa uthabiti hasa kuhusiana na ondoleo la dhambi zao ambalo lilitimizwa kupitia Neno la injili ya maji na Roho. Ili tuweze kuufahamu upendo wa Mungu kwa kina basi tunapaswa kuwa waamini tunaoamini katika injili hii ya kweli. Upendo wa Mungu unajidhihirisha kwa kina na kwa uthabiti katika injili hii ya kweli. Kama tutaufahamu upendo wa Mungu, basi ufahamu wetuni lazima utokane na upendo thabiti wa Mungu kwetu sisi ambao umefunuliwa katika Ukweli wa injili ya maji na Roho. Ni hapo ndipo tunapoweza kuwaongoza wengine kuuendea upendo wa kweli wa Mungu.
Mtume Yohana anashuhudia kuwa Yesu Kristo, aliyekuja kwa maji, kwa damu, na kwa Roho Mtakatifu, ni Mungu Mwokozi mwenyewe. Kiini cha ushuhuda wake ni ule Ukweli wa ondoleo la dhambi, ambao unapatikana katika maji, damu, na Roho Mtakatifu.
Kama ilivyoandikwa katika Neno la Mungu, maji yana maanisha ni ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji, na damu ina maanisha ni hukumu ambayo Yesu aliipokea kwa ajili ya dhambi zetu zote. Pia, ushahidi wa wokovu wetu unajikita katika Roho Mtakatifu, maji, na damu (1 Yohana 5:8). Huduma za maji, damu, na Roho Mtakatifu ni za Mungu na ambazo kwa hizo amewakomboa wenye dhambi toka katika dhambi zao zote.
Kupakua kitabu mtandaoni
PDF EPUB