Mahubiri

Somo la 1: Dhambi

[1-1] (Marko 7:8-9, 20-23) Yatupasa Kwanza Kutambua Dhambi Zetu Ili Tuweze Kukombolewa

(Marko 7:8-9)
“Ninyi mwaiacha amri ya Mungu na kuyashika mapokeo ya wanadamu. Akawaambia, vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.”
 
(Marko 7:20-23)
“Akasema, kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu; Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.”
 

Kwanza ningependa kufafanua nini maana ya dhambi. Kuna dhambi zilizoelezwa na Mungu na nyingine kuelezewa na mwanadamu. Neno dhambi kwa Kigiriki ‘hamartia’ maana yake ni ‘kukosea katika kulenga shabaha”. Kwa maneno mengine, ni kufanya jambo pasipo usahihi. Ni dhambi kutotii maelekezo ya Mungu. Hebu na tuangalie kwa awali maana ya dhambi kwa mtizamo wa mwanadamu.

Nini maana ya dhambi?
Ni kutotii maelekezo 
ya Mungu.

Twagundua dhambi zetu kupita dhamira zetu. Ingawa kiwango cha ubinadamu hutofautiana kulingana na jamii anayotoka, hali ya kimawazo, katika mazingira na dhamira.
Hivyo, maana ya dhambi inatofautiana kati ya jamii na jamii. Kitendo cha aina moja chaweza au kisiweze kuchukuliwa kama dhambi endapo kila jamii itakuwa na aina yake ya vipimo. Ndiyo maana Mungu ametupa vipengele vya sheria 613 ili vitumike kama vipimo halisi vya dhambi.
Mchoro ufuatao unatuelekeza dhambi za mwanadamu.

Sheria ya Mungu
Dhamira ya Mwanadamu,
Uongofu na kanuni za kijamii
Sheria ya kitaifa,
Sheria ya kiraia

Hatupaswi kamwe kuweka viwango vya dhambi kwa kutumia dhamira iliyowekwa kwa kanuni zetu za kijamii.
Dhambi za dhamira siyo zitokanazo na jinsi ile Mungu anavyoelezea nini maana ya dhambi. Hivyo tusizisikilize dhamira zetu, bali tulinganishe viwango vya dhambi zetu na amri za Mungu.
Kila mmoja ana wazo lake juu ya nini maana ya dhambi. Wengine huchukulia ni udhaifu hali wengine hudhani kwamba ni kutokana na kilema cha tabia.
Mathalani, katika nchi ya Korea, watu hujengea makaburi ya wazazi wao kwa kupanda nyasi na kuyatunza hadi wenyewe wanapofariki. Lakini kwa kabila Fulani duni katika ncha Papua New Guinea, wanawatukuza wazazi wao waliofariki kwa kufanya sherehe ya kuila miili yao wakiwa na ndugu wa familia (sina uhakika sana endapo huipika kwanza kabla ya kula). Naimani hupenda kuizuia miili hiyo isiliwe na funza. Utamaduni huu ni kielelezo cha mtazamo wa kibinadamu kuhusiana na dhambi ulivyo na utofauti.
Matendo ya kistarabu katika jamii moja yanaweza kuchukuliwa kwa jamii nyingine kuwa yasiyo ya kistaarabu na kinyama. Ingawa Biblia inatueleza kwamba dhambi ni kutotii maelekezo ya Mungu. “Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo yenu” (Marko 7:8-9). Muonekano wetu wa nje ni muhimu mbele za Mungu kwa kuwa yeye huangalia kina cha mioyo yetu.
 

Kanuni za mtu ni dhambi mbele za Mungu

Dhambi ipi iliyo hatari zaidi?
Ni kupuuzia Neno la Mungu.

Kushindwa kuishi katika mapenzi ya Mungu ni dhambi. Ni sawa na kutoamini neno lake. Mungu alisema, ni dhambi kuishi kama Wafarisayo ambao walikataa sheria ya Mungu kwa kukazia zaidi msisitizo wa mafundisho ya desturi zao. Yesu aliwachukulia kuwa ni wanafiki.
“Ni Mungu yupi unayemwamini? Je, unaniheshimu na kunitukuza? Unajivunia juu yangu, lakini je unaniheshimu?” Mara nyingi watu huangalia umbo la nje na kupuuzia neno la Mungu ndani ya nafsi zao. Je wajua hilo?
Matendo ya kuvunja sheria chanzo chake yametokana na udhaifu ambao ni maovu. Makosa tuyafanyayo na upotovu tuutendao kutokana na kutokuwa wakamilifu siyo dhambi kuu ndani yetu bali ni kuanguka katika usahihi. Mungu ametofautisha kati ya dhambi na uovu. Wale wote wenye kulidharau neno lake ni wenye dhambi, hata ikiwa hawana makosa. Ni wenye dhambi zaidi mbele ya Mungu. Na hii ndiyo maana Yesu aliwakemea Mafarisayo.
Katika nyakati za Agano la Kale, kitabu cha mwanzo hadi kumbukumbu la Torati ziliwekwa sheria zilizotaja nini cha kutenda na nini cha kutotenda. Ni maneno ya Mungu Sheria yake. Haitowezekana kwetu kuzitekeleza katika asilimia mia moja, lakini yatubidi kuzikubali kama ni sheria za Mungu. Alitupatia hapo mwanzo na yatupasa kuzikubali kuwa ni Maneno ya Mungu.
“Hapo mwanzo palikuwepo na Neno, naye Neno alikuwepo kwa Mungu, naye Neno alikuwa ni Mungu” (Yohana 1:1) Naye alisema “Na uwepo mwanga na ukawepo” Aliumba vyote. Na baadaye, akaiweka Sheria.
Na baadaye “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu” (Yohana 1:1, 14). Ni kwa namna gani basi Mungu alijidhihirisha kwetu? Alijidhihirisha kwetu kupitia sheria kwa maana Mungu ni Neno na Roho. Sasa je, Biblia inaitwa nini? Tunaita Neno la Mungu.
Imesemwa hapa “Ninyi mwaiacha amri ya Mungu na kuyashika mapokeo ya wanadamu” vipo vipengele 613 katika sheria ya Mungu. Fanya hivi na usifanye vile waheshimu wazazi wako… nakadhalika. Katika kitabu cha Mambo ya Walawi imetajwa ni kwa namna gani mwanamume na mwanamke wanapaswa kuenenda na nini kifanyike endapo mifugo ikitumbukia shimoni… Hivi ni baadhi ya vipengele 613 katika sheria.
Kwa kuwa haya si maneno ya mwanadamu, tunapaswa kuyatafakari nyakazi zote. Ingawa tutashindwa kutekeleza sheria yote, tunapaswa kwa kiasi Fulani kuzitambua na kumtii Mungu.
Je, kuna kifungu hata kimoja cha maneno ya Mungu yasiyo sahihi? Mafarisayo waliziacha sheria za Mungu na kuzifuata taratibu za mafundisho ya wanadamu dhidi ya sheria ya Mungu. Maneno ya wakuu wao yalichukua nafasi ya uzito wa juu dhidi ya yale ya Mungu Yesu alipokuwa duniani, haya ndiyo aliyoshuhudia, na ndicho kilicho umiza moyo wake zaidi kwa kuona Neno la Mungu likipuuziwa na wanadamu.
Mungu ametupa vipengele 613 vya sheria ili tuweze kuzitambua dhambi zetu na kutuonyesha kuwa yeye ni mkweli na mtakatifu kwetu. Kwa kuwa sisi sote ni wenye dhambi mbele yake, tunapaswa basi kuenenda kwa imani na kumwamini Yesu kuwa ndiye aliyeletwa na Mungu kwa upendo kwetu. 
Wenye kuweka neno lake kando na kutoamini watakuwa ni wadhambi. Wenye kushindwa kuenenda katika neno lake pia ni wadhambi, ingawa kuweka kando neno lake ni hatari zaidi. Wenye kutenda dhambi hii wataishia motoni. Kutoamini Neno lake ni dhambi iliyo hatari zaidi mbele za Mungu.
 

Sababu ya Mungu kutupatia Sheria

Kwa sababu zipi Mungu 
alitupa sheria?
Ni kutufanya tuzitambue dhambi zetu na 
Hukumu juu yake.

Sababu ipi Mungu alitupatia Sheria? Ilikuwa ni kutufanya kuzitambua dhambi zetu na kumrudia kwake kwa toba. Alitupatia vipengele 613 vya sheria ili tuweze kuzitambua dhambi zetu na kuweza kukombolewa kupitia Yesu Kristo. Na hii ndiyo maana ya Mungu kutupatia sheria.
Warumi 3:20 inasema “kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya Sheria.” Hivyo twajua kwamba sababu ya Mungu kutupatia sheria ilikuwa si kutulazimisha kuenenda nayo.
Kwa namna hii sasa, tunapata kujua nini juu ya Sheria? Ni hivi, sisi tu wadhaifu kwa kuitimiza sheria yote na ni wenye dhambi sana. Tunatambua nini juu ya vipengele hivyo 613 vya Sheria? Tunang’amua mapungufu yetu na kushindwa kwetu kuifuata Sheria yake. Tunatambua yakwamba sisi ni viumbe wa Mungu, tulio dhaifu, na wenye dhambi mbele zake. Ilitupasa sisi sote kutupwa motoni kwamujibu wa Sheria ya Mungu.
Tunapo tambua dhambi zetu na kushindwa kwetu kuishi kwa kuzifuata sheria, sasa, na tufanye nini? Je tunajaribu kuishi kwa ukamilifu wenyewe? Hasha! Yatulazimu kukubali kuwa sisi ni wadhambi, tumwamini Yesu ili tukombolewe kupitia wokovu wake katika Maji na Roho na kumshukuru yeye.
Sababu ya Mungu kutupa sheria ilikuwa ni kutufanya tuzitambue dhambi zetu na kujua adhabu yake juu ya dhambi hizo. Hivyo, itatufanya kuelewa kuwa hakuna njia ya kuokolewa toka motoni pasipo Yesu ikiwa tutamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi, tutakombolewa. Mungu alitupa sheria ili ituongoze kuelekea kwa Mwokozi Yesu.
Mungu alizifanya sheria ili kutufanya tuweze kutambua ni kwa namna gani tulivyo wenye dhambi na kuhitaji wokovu wa roho zetu kutoka kwenye dhambi hizo. Alitupa sheria na kumtuma mwana wake wa pekee, Yesu, kutuokoa kwa kuzibeba katika ubatizo wake. Kumwamini Yeye kutatufanya tuokolewe.
Sisi ni wadhambi tusio na tumaini lolote, yatulazimu kumwamini Yesu ili kuwa huru kutoka dhambini, kuwa watoto wa Mungu na kuurudisha utukufu wake.
Yatupasa tuelewe, kufikiri na kuamua kupitia neno lake kwa kuwa yeye ni asili ya yote. Yatupasa tuikubali kweli ya wokovu kupitia Neno lake. Hii ni Imani ya Haki na kweli.
 

Nini kilichomo ndani ya Moyo Wa Mwanadamu

Natufanye Nini Mbele 
za Mungu?
Tunapaswa tuzikubali dhambi
zetu na kumwomba Mungu
atuokoe. 

Ni lazima imani ianze kwa neno la Mungu, kwa kuliamini. Ikiwa sivyo, basi tutaanguka katika makosa. Itakuwa katika makosa na imani isiyo ya kweli.
Wakati Mafarisayo na Wanasheria walipomwona Yesu akila na wanafunzi wake mikate huku mikono ikiwa michafu, wasingeweza kusahihisha hilo ikiwa wangeliweka katika mtazamo wa neno la Mungu. Neno latuambia chochote kinachoingia ndani mwa mtu tokea nje, hakimtii najisi kwa kuwa huenda moja kwa moja kupitia tumboni na kutoka nje, na hakiuharibu moyo.
Kama isemavyo Marko 7:20-23 “Akasema kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.” Yesu alisema watu ni wadhaifu kwa kuwa wamezaliwa na dhambi ndani mwao.
Je, waelewa maana yake? Tumezaliwa wadhambi kwa kuwa sisi ni uzao wa Adamu lakini hatuwezi kuiona kweli kwa sababu hatujakubali na kuamini maneno ya Mungu. Hivyo, nini kilichomo ndani ya moyo wa mwanadamu?
Ujumbe uliopo hapo juu unasema “ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.” Aina zote za uovu hutoka ndani ya mioyo ya wanadamu na kuwatia unajisi.
Imeandikwa katika Zaburi “Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha, mtu ni kitu gani hata umkumbuke. Na mwanadamu hata umwangalie” (Zaburi 8:3-4).
Kwa nini Mungu mwenyewe ametutembelea? Anatutembelea kwa sababu anatupenda, alituumba na kutuonea huruma kwa kuwa tu wadhambi. Alizifuta dhambi zetu zote na kutufanya watu wake “Bwana, Bwana wetu Ni kwa namna gani jina lako ni lakuheshimiwa duniani pote, na Mbinguni!” (Zaburi 8:1) Mfalme Daudi aliimba Zaburi hii katika kitabu cha Agano la Kale alipotambua kwamba Mungu atakuja kuwa Mwokozi wa wenye dhambi.
Katika Agano Jipya, Mtume Paulo alirudia maneno hayo. Ni jambo la kushangaza sana, viumbe wa Mungu kuweza kuwa watoto wa Mungu. Hili hufanyika kupitia huruma yake tu. Huu ni upendo wa Mungu.
Tunapaswa tuelewe kuwa, tunapo jaribu kuishi kwa sheria ya Mungu ni ujasiri ulio wa hatari kwake. Na pia ni ujeuri utokanao na upumbavu. Si vyema kuishi nje ya upendo wake huku tukijitahidi kufuata sheria wenyewe na kusali pasipo na matumaini katika maisha yetu ni mapenzi ya Mungu tujitambue kwamba tu wadhambi katika sheria na kuamini ukombozi kupitia maji na damu ya Yesu.
Neno lake limeandikwa katika Marko 7:20-23, “Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani ya moyo nayo yamtia mtu unajisi.”
Yesu alisema kile kitokacho ndani ya mwanadamu dhambi ya ndani, humtia najisi kamwe chakula kisicho safi toka kwa Mungu hakiwezi kututia najisi. Viumbe wote ni safi, isipokuwa kile kitokacho ndani ya mwanadamu nayo ni dhambi humtia najisi. Sote ni wazawa wa Adamu. Hivyo, tumezaliwa na nini? Tumezaliwa na dhambi kumi na mbili ndani yetu. Je hii si kweli?
Je, twaweza kuishi bila kutenda dhambi? Tutaendelea kutenda dhambi kwa kuwa tumezaliwa wenye dhambi. Twaweza kuacha kutenda dhambi kwa kuwa twaielewa sheria? Twaweza kuishi kwa kuifuata sheria? Hasha!
Kwa kiasi tunapo jaribu kuishi kwa kufuata sheria ndivyo itakavyo kuwa ngumu kuifuata. Tunapaswa kutambua mwisho wetu na kuachilia matendo yetu ya awali na kwa unyenyekevu wa ufahamu wetu, twaweza kukubali ubatizo na damu ya Yesu, ambao hutuokoa.
Vipengele vyote 613 vya sheria ni vyenye haki na vyema. Lakini watu ni wadhambi toka tumboni mwa mama zao. Tunapo tambua ya kwamba Sheria ya Mungu ni njema lakini sisi wanadamu tumezaliwa wenye dhambi hatutoweza kuwa wenye haki kwa juhudi zetu binafsi, tutagundua kuwa tunahitaji rehema ya huruma ya Mungu na ukombozi wa Yesu katika Injili ya maji, damu na Roho. Tunapogundua vikomo vyetu – kwamba hatutoweza kupata haki kwa uwezo wetu na tutakwenda motoni kwa dhambi zetu – basi yatupasa kutegemea ukombozi wa Yesu.
Tunaweza kuponywa. Tunapaswa kuelewa kwamba, tumeshindwa kuwa wenye haki na wema mbele za Mungu kwa juhudi zetu wenyewe. Sasa basi tunapaswa kukubali mbele za Mungu kwamba sisi ni wenye dhambi ambao mwisho wetu ni jehanamu, na tuweze kuomba huruma yake, “Mungu uniokoe kutoka dhambini na unihurumie.” Ndipo Mungu hakika atakutana nawe kwa Neno lake. Katika njia hii tutaweza kuponywa.
Natuone basi sala ile ya Daudi. “Nimekutenda dhambi wewe peke yako, Na kufanya uovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo na kuwa safi utoapo hukumu” (Zaburi 51:4).
Daudi alitambua yeye ni mwenye wingi wa dhambi na muovu wa kutupwa motoni, lakini alikubali mbele za Mungu, “Bwana ukiniita kuwa mwenye hakika ni mwenye dhambi mimi. Ukiniita mwenye haki, hakika ni mwenye haki mimi. Ukiniokoa, nitaokoka na ukinitupa motoni, nitaishia motoni.”
Hii ni imani sahihi na njia ya kuokolewa. Hivi ndivyo tunavyopaswa tuwe, ikiwa tunatumaini la wokovu katika Yesu.
 
 
Tunapaswa tuelewe ni zipi dhambi zetu halisi

Kwa kuwa sisi tu uzao wa Adamu, basi sote tuna tamaa mbaya ndani ya mioyo yetu Hivyo, Mungu anasemaje katika hili? Anatueleza tusitende uzinzi ingawa mioyoni mwetu tuna dhambi ya uzinzi. Tuna uuaji ndani ya mioyo yetu, lakini Mungu anasemaje? Anatueleza tusiwe tunadharau wazazi wetu mioyoni mwetu lakini anatueleza tuwaheshimu. Tunapaswa kutambua kwamba neno lake ni kweli na jema, lakini ndani yetu mioyoni kuna dhambi.
Je hii si sawa? Hakika ni kweli. Hivyo yatupasa tufanye nini mbele za Mungu? Tunapaswa kukubali kwamba sisi ni wenye wingi wa dhambi tusio na matumaini. Hatupaswi kudhani kuwa sisi ni wenye haki jana kwa kuwa hatukutenda dhambi siku hiyo ya jana. Tumezaliwa wenye dhambi chochote tufanyacho tutaendelea kuwa wenye dhambi. Na hii ndiyo maana tunahitaji ukombozi kupitia imani katika ubatizo wa Yesu.
Sisi si wenye dhambi kutokana na matendo yetu kama vile uzinifu, uuaji, wizi… bali tu wenye dhambi kwa kuwa tumezaliwa wenye dhambi ndani yetu. Tumezaliwa ndani yetu tukiwa na aina kumi na mbili za madhambi, hivyo kwa kuwa tu wadhambi mbele ya macho ya Mungu kamwe hatutoweza kuwa wema kwa uwezo wetu binafsi. Twaweza kujifanya kuwa wema kwa muda tu.
Ikiwa tumezaliwa wenye nia zenye dhambi katika nafsi zetu, ni kwa namna gani basi twaweza kuwa wenye dhambi ikiwa hatutotenda dhambi? Hatuwezi kuwa wenye haki mbele za Mungu kwa kutegemea nafsi zetu. Ikiwa tutajifanyia haki yetu tutakuwa wanafiki. Yesu aliwaita mafarisayo na wanasheria kuwa “sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki” (Matayo 23:23) Wanadamu wamezaliwa wakiwa wadhambi na hutenda dhambi katika kipindi chote cha maisha yao hapa duniani.
Anayedai kwamba hana dhambi ambaye hajapigana au kumpiga yeyote au kuiba hata sindano kwa yeyote kwa maisha yake yote anadanganya kwa kuwa wanadamu wamezaliwa na dhambi ndani yao. Mtu huyo ni mwongo, mdhambi na mnafiki. Hivi ndivyo Mungu amuonavyo.
Kila mmoja ni mdhambi toka tumboni mwa mamae. Ingawa hata tusipotenda dhambi hata moja, bado tumepangiwa kwenda motoni. Haitajalisha ni kwa kiwango gani umefuata sheria na amri za Mungu, bado wewe ni mwenye dhambi ndani yako na hukumu ile ya motoni ina kusubiri.
Sasa, natufanye nini juu ya huu mwisho wa hukumu ya motoni? Tunapaswa kuomba huruma ya Mungu na kumtegemea yeye kwa wokovu wa dhambi hizo. Tusipokubali kuokolewa naye, basi ni wazi tutakwenda motoni huu ni mwisho wetu.
Ni kwa wale tu watakao likubali neno la Mungu kwamba wao ni wenye dhambi. Na wajue na kuelewa kuwa watafanywa kuwa wenye haki kwa imani tu. Hivyo kufahamu kwamba, kudharau na kuweka kando neno la Mungu bila ya kulitambua ni dhambi iliyo hatari zaidi. Watakao likubali neno lake ni wenye haki, ingawa hapo nyuma walikuwa ni wenye dhambi. Wamezaliwa upya kwa Neno lake na kwa neema, na ndio pekee waliobarikiwa.
 

Wenye kujaribu kukombolewa kwa kupitia Matendo yao bado ni wenye dhambi

Ni yupi mwenye dhambi hata
baada ya kumwamini Yesu?
Ni yule mwenye kujaribu kukombolewa 
kupitia matendo yake.

Hebu na tusome Wagalatia 3:10 na 11 “Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana: maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye. Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa Imani.”
Imesemwa “Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati ayafanye” Wale wenye kufikiri kuwa wana mwamini Yesu, hali wakitaka haki kupitia matendo yao, wamelaaniwa. Wapo wapi wenye kujaribu kuwa wenye haki? Wapo chini ya laana ya Mungu.
Kwa nini Mungu ametupa Sheria? Ametupa sheria ili tuweze kuzitambua dhambi zetu (Warumi 3:20). Na pia alitaka tujue kwamba sisi ni wenye dhambi na mwisho wetu ni jehanamu.
Amini ubatizo wa Yesu, Mwana wa Mungu na uzaliwe upya kwa maji na kwa Roho. Ndipo utakapo okolewa dhambini, kuwa mwenye haki, kupata uzima wa milele na kwenda mbinguni. Uwe na Imani moyoni mwako.
 

Dhambi kuu ya Majivuno Duniani

Ni ipi iliyo dhambi kuu ya
Majivuno Duniani?
Ni kujaribu kuishi 
Kwa matendo ya Sheria

Tumebarikiwa kwa kuwa na Imani ya baraka zake. Mungu huwaokoa wale wote wenye Imani kwa Neno lake.
Leo hii kati ya wale wenye kuamini, wamo Wakristo wenye kujaribu kuenenda katika matendo ya sheria. Imewapasa kuishi kwa matendo ya sheria, lakini je, yawezekana?
Tunapaswa tuelewe kwamba ni kwa namna gani itakuwa ni upumbavu kujaribu kuishi kwa matendo ya sheria. Tutakapojaribu sana na ndivyo itakapo kuwa ngumu zaidi. “Imani huja kwa kusikia, na kusikia ni neno la Mungu” (Warumi 10:17) Yatupasa tutupilie mbali majivuno yetu ili tuweze okolewa.
 

Yatupasa tuache vipimo tujiwekeavyo ili tuweze kuokolewa

Tunapaswa tufanye nini basi,
ili tupate okolewa?
Yatupasa tuache kujiwekea
vipimo vyetu.

Kwa namna gani mtu ataokolewa? Itawezekana pale tu mtu huyo atakapo tambua yeye binafsi kwamba ni mwenye dhambi. Wapo wengi ambao awajakombolewa kwa sababu awataki kuacha Imani potofu na juhudi zao binafsi.
Mungu anasema kwa wale wenye kuzishika sheria wamelaaniwa. Wale wenye kuamini kuwa wataweza kuwa wenye haki kutoka hatua hadi hatua kwa kujaribu kuishi kwa matendo ya sheria baada ya kumwamini Yesu, wamelaaniwa wanamwamini Mungu lakini bado wanafikiri kwamba wanapaswa kuishi katika sheria ili kuendelea katika wokovu.
Ndugu zangu, twaweza vipi kuwa wenye haki kupitia matendo yetu? Tunakuwa wenye haki pale tu tunapo amini Neno la Yesu; na ndilo pekee lenye kuokoa. Imani katika ubatizo wa Yesu, damu yake, na Mungu Mkuu ndivyo pekee viokoavyo.
Na ndiyo maana Mungu alileta kanuni ya Imani kwetu ili iwe njia ya kuwa wenye haki mbele zake. Ukombozi katika maji na katika Roho hauhitaji matendo ya sheria ya mtu, bali ni Imani juu ya Neno la Mungu. Mungu ametukomboa kwa imani na huu ndiyo mpango ulio kamilika katika wokovu kwetu.
Kwa nini wale walio mwamini Yesu hawakukombolewa? Kwa sababu hawakukubali neno la wokovu kupitia maji na katika Roho lakini sisi wale tusiokamili ndani yetu kama walivyo wao, tumekombolewa kupitia Imani katika Neno la Mungu.
Ikiwa watu wawili watafanya kazi katika jiwe la kusagia nafaka, atakaye achwa upande mmoja akifanya kazi ataendelea hali yule mwingine atanyakuliwa. Aliyeachwa akiendelea anafananishwa na yule asiyekombolewa. Kwa nini basi mmoja anyakuliwe na mwingine kuachwa?
Sababu ni kwamba yule mmoja alisikiliza na kuamini Neno la Mungu, hali mwingine alifanya kwa bidii kutenda matendo ya sheria na kutupwa jehanamu. Mtu huyu alikuwa akitambaa kuelekea mbele za Mungu lakini alitupwa pembeni kama mdudu mchafu amtambaaye mtu. Ikiwa mtu anajaribu kutambaa ili kumfikia Mungu kwa matendo ya sheria hakika atatupwa motoni.
Na ndiyo maana tunapaswa kukombolewa kwa Imani katika maji na katika Roho. 
“Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa. Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria, kwa sababu mwenye haki ataishi kwa Imani” (Wagalatia 3:10-11, Warumi 1:17).
Usipoamini Neno la Mungu ni dhambi mbele zake. Na kwa kuongezea, vilevile ni dhambi kulipuuzia kwa kujiwekea vipimo binafsi. Mwanadamu hawezi kuishi kwa kuifuata sheria ya Mungu kwa kuwa amezaliwa na asili ya dhambi ndani yake na ataendelea kutenda dhambi maishani mwake. Tunatenda dhambi hapa leo na kesho pale kidogo hadi kufikia mahala pote tunapokwenda. Yatupasa kuelewa kwamba sisi tu ndani ya mwili usioweza kuacha kutenda dhambi.
Mwanadamu amefananishwa na ndoo iliyofurika mbolea ambayo ikibebwa huvuja na kumwagika kila pahala ipitishwapo Ndivyo tulivyo. Tunamwagika dhambi kila pahala tupitapo. Je, waona hiyo?
Je, unaweza kuendelea kusema kuwa wewe ni mtakatifu? Ikiwa utajigundua hivyo binafsi, hutojaribu tena pasipo na matumaini kujitafutia utakatifu ila kwa kuamini kwa maji na kwa damu ya Yesu.
Wale ambao awajazaliwa upya yawapasa kutupilia mbali mioyo yao migumu na kukubali kwamba wao ni wadhambi mbele za Mungu. Na ndipo wanapopaswa kulirudia Neno la Mungu na kugundua kwamba aliwaokoa kwa maji na kwa Roho.