Mahubiri

Somo la 1: Dhambi

[1-2] (Marko 7:20-23) Wanadamu Wamezaliwa Wakiwa Wenye Dhambi

(Marko 7:20-23)
“Akasema kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. 
Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.”
 

Watu wamechanganyikiwa na kuishi kwa hisia potofu

Ni yupi hasa anayeweza
Kuokolewa?
Ni yule mwenye kujiona ni 
Mwenye dhambi zaidi.

Kabla ya yote, napenda kukuuliza swali. Binafsi unajionaje? Je, unafikiri wewe ni mwema au mwovu? Unafikiri vipi?
Kila mtu anaishi kwa hisia zake potofu. Waweza kuwa si mwovu kama udhaniavyo au si mwema kama ujionavyo. 
Au unafikiri wewe binafsi si mwema? Jibu la mwisho ndilo, kwamba wewe ni mwovu?
Hebu nikuulize swali jingine. Ni yupi aliye na nafasi zaidi ya kukombolewa – yule aliyetenda uovu zaidi au yule aliyetenda uovu kidogo tu? Yule aliye kubali kwamba ametenda dhambi zisizo na idadi ana nafasi zaidi ya kukombolewa kwa sababu mtu huyo amekubali kuwa yeye ni mwenye dhambi zaidi. Mtu huyu ni rahisi zaidi kuamini neno la ukombozi kwa ajili yake toka kwa Yesu.
Hakika tunapojichunguza nafsini mwetu tunashuhudia kwamba ni wenye dhambi nyingi Mwanadamu ni nani? Ni mtu aliye “mbegu ya uovu” Isaya 59, inasema kwamba kuna aina za maovu ndani ya moyo wa mwanadamu. Kwa maana hiyo ni wazi kwamba wanadamu ni wenye wingi wa dhambi Ikiwa tutasema wanadamu ni wenye wingi wa dhambi, wengi watakataa. Lakini ukielezea kwamba mtu ni “mbegu ya uovu” ni maelezo yaliyo sahihi Tukijichunguza wenyewe kwa uaminifu, ni wazi na kweli kwamba tu viumbe waovu. Wale wote walio wakweli katika nafsi zao watakubaliana na hili.
Ingawa inaonekana kwamba wengi wenu watakataa kukubaliana na jambo hili kwamba ni wenye wingi wa dhambi. Wengi huishi kwa amani kwa sababu hawajali kwamba wao ni wenye dhambi nyingi. Kwa kuwa sisi ni waovu tumeunda ustaarabu wa madhambi. Kama isinge kuwa hivyo, basi tungeona haya kutenda dhambi Ingawa wengi wetu hatuoni aibu tena tunapotenda madhambi.
Hata ikiwa dhamira zetu zinajua. Kila mmoja ana dhamira inayomshuhudia “ni aibu.” Adamu na Hawa walijificha baada ya kutenda dhambi. Na leo hii wenyedhambi hujificha nyuma ya pazia la utamaduni – utamaduni wetu wa uovu. Wanajificha kati ya watenda dhambi wenzao kuzuia hukumu ya Mungu.
Watu wengi wamedanganywa na hisia zao potofu. Wamefikiri kwamba ni waadilifu zaidi ya wengine. Hivyo wanapopata taarifa mbaya za wengine, hupayuka na kusema “Ni kwa vipi huyu mtu ametenda haya? Inawezekanaje mtu kutenda hili? Ni kwa namna gani mwana kuwatendea wazazi wake?” Huku wakiamini kwamba wao hawawezi kuyafanya mambo haya.
Rafiki zangu, ni vigumu kwako kujitambua nafsi yako. Ili uweze kuitambua nafsi yako katika kweli, tunapaswa kwanza kupata ondoleo la madhambi. Inatuchukua muda mrefu kwetu kupata ufahamu wa kweli juu ya asili yetu ya uanadamu, na wapo wengi kati yetu kamwe hawatagundua hili hadi pale watakapofikwa na mauti.
 

Ijue Nafsi yako

Wasiotambua nafsi zao 
Huishi vipi?
Huishi katika unafiki kwa kujaribu
Kuficha uovu wao.

Wakati mwingine tunakutana na watu wa aina hii ambao kwa kweli hawazitambui nafsi zao. Ndugu mmoja alisema, “Itambue nafsi yako.” Ingawa, wengi wetu hatujui mioyoni mwetu kuna: uuaji, wizi, tamaa ya mali, madhaifu, hila, tamaa ya mwili, jicho la husuda na mengine mengi.
Yule asiyejitambua ana sumu ya nyoka katika kinywa chake ingawa hunena mema. Sababu yake ni kwamba, mtu huyu hajaweza kujitambua ya kwamba amezaliwa kuwa mwenye dhambi asiye zuilika.
Wapo wengi wa aina hii wasiojua asili yao wamejipotosha wenyewe na kuishia katika maisha yaliyo vishwa uongo wa nafsi zao. Hawatambui kwamba wanajiingiza wenyewe kwenye jehanam kwa kujidanganya nafsi zao.
 

Dhambi huendelea kuchafua watu Kwa maisha yao yote

Kwa nini wanakwenda 
motoni?
Kwa sababu hawazitambui
Nafsi zao.

Tuone katika Marko 7:21-23 “Kwa maana ndani ya mioyo ya watu, hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.” Mioyo ya watu imejawa na mawazo ya uovu tangu kutungwa mimba katika matumbo ya mama zao.
Hebu na tufikiri kwa mfano huu, ya kwamba moyo wa mwanadamu uwe umeundwa kwa vioo na kujazwa kwa wingi kwa maji machafu yanayoitwa dhambi. Je, itatokea nini ikiwa mtu atazunguka hapa na pale? Maji haya machafu yatamwagika na kuchafua kila pahala. Na kila mtu huyu atakapopita dhambi hizo ziturudi kumwagika mahali pote.
Kwa jinsi hii sisi ni wenye dhambi kupindukia, tunao ishi kwa namna hii maishani mwetu pote. Tunapaka madoa ya dhambi kilatuendapo. Tutaendelea kutenda dhambi sikuzote za maisha yetu kwa sababu sisi ni wenye dhambi kupindukia.
Taabu yetu ni kuwa, hatujatambua sisi ni wenye dhambi kupindukia, au kwa maneno mengine tu mbegu za dhambi. Ni wenye dhambi kupindukia na wenye dhambi mioyoni mwetu toka siku tulipozaliwa
Wingi wa dhambi umefikia kikomo na kumwagika nje. Ingawa watu hawaamini hili kwamba ni warithi wa dhambi, wanafikiri kwamba wao huongozwa na wengine kutenda dhambi na hivyo, wao binafsi si waovu.
Ingawa watu wanapotenda dhambi, hufikiri kwamba kinachohitajika katika kusafisha na kuwaweka wasafi tena ni kwa dhambi hizo kuzifuta katika kumbukumbu zao (kujisahihisha) Hujutia kwa kulia mara zote wanapotenda dhambi, na kujiona kwamba haikuwa kosa lao. Je tunapojitakasa wenyewe, yatupasa basi kuendelea na uchafu mwingine? Basi ina maana tutaendelea kujuta na kulia siku zote.
Bilauri inapojaa dhambi itaendelea kumwagika na kuchafua. Hakuna sababu ya kulia na kujutia kwa nje. Haijalishi na kwa mara ngapi tutalia na kujutia kwa tabia zetu mbovu ni bure ikiwa bilauri itaendelea kujaa dhambi.
Tumezaliwa na wingi wa dhambi mioyoni mwetu hapatakuwa patupu ingawa ni kwa kiasi gani zitajaa na kumwagika pahala pote tuendapo. Hivyo tunatenda dhambi maishani mwetu hadi mwisho.
Yeyote asiyetambua hili, huendelea kificha asili yake. Dhambi hukaa ndani ya mioyo ya watu na haitaweza kutoka kwa kulia ili itakaswe. Tunapochafua kwa dhambi kidogo tunasafisha kwa tambaa safi na baadaye kwa tambaa chafu na kuendelea ingawa utakuwa safi bado utaendelea kuchafua tena na tena!
Itaendelea hivi mpaka lini? Hadi pale mtu atakapo kufa. Watu hutenda dhambi hadi mwisho wa siku za maisha yao. Na hii ndiyo maana yatupasa kumwamini Yesu ili tukombolewe. Ili tuweze kukombolewa yatupasa kwanza kuzitambua nafsi zetu.

Ni yupi kwa shukrani zaidi
Hupokea upendo wa Yesu?
Ni yule mwenye kukubali Kwamba
ametenda wingi wa makosa 
maishani.

Na tuseme kwa mfano, kuna watu wawili wenye kufananishwa na bilauri mbili zilizojaa maji machafu. Bilauri zote zimejaa dhambi mmoja wao akisema “Oh, mimi ni mwenye dhambi” na hivyo kwenda kumtafuta mtu wa kuweza kumsaidia.
Lakini yule mwingine mwenye kufikiri kwamba yeye si mwenye dhambi, hatoweza kuona wingi wa uovu ndani yake na kufikiri kwamba yeye ni mwema. Maishani mwake huendelea kusafisha uchafu unaomwagika. Atasafisha pande moja hadi nyingine kwa haraka.
Wapo wengi wa aina hii wenye kuishi maisha ya kusafisha dhambi ili kujizuia kuchafua upya tena. Na kwa kuwa bado wanazo dhambi ndani ya mioyo yao, je itasaidia nini? Kuwa waangalifu kwa kutumia juhudi zao haitosaidia kuwa karibu na mbingu. Uangalifu wa aina hii huwaongoza katika njia ya kwenda motoni zaidi.
Rafiki wapendwa “kuwa waangalifu kwa juhudi zetu! Hutupeleka motoni. Na tuchukue fundisho hili kwa dhati mioyoni mwetu. Ingawa unapokuwa mwangalifu na kutochafua kwa dhambi bado wewe ni mwenye dhambi!
Nini kilicho ndani ya moyo wa mwanadamu? Dhambi? tamaa mbaya? Ndiyo! Mawazo potofu? Ndiyo! Wizi? Ndiyo! Majivuno? Ndiyo!
Hatuwezi kujizuia, bali tukubali kwamba sisi ni wadhambi hasa pale tunapojiona kwamba tunatenda dhambi na kuwa dhaifu bila hata kuambiwa. 
Tunaweza tusitambue hili tunapokuwa bado ni vijana. Lakini tunapoendelea kuwa watu wazima inakuaje? Tunapo kuwa shule, hadi vyuoni na zaidi, tunakuja kugundua kwamba kila tulicho nacho ndani yetu ni dhambi tupu! Je hii si kweli? Kwa uwazi na uaminifu, ni vigumu kuficha asili zetu za dhambi sawa? Hatuwezi kuacha kuwa na dhambi ndani yetu kama si nje! Hujutia na kusema “Oh, nilipaswa nifanye hivi” Kamwe tunaona ni vigumu kubadilika. Kwa nini ipo hivi? Kwa sababu kila mmoja wetu amezaliwa na wingi wa dhambi mioyoni mwake.
Hatuwezi kuwa safi kwa kuwa waangalifu tu. Tunachohitaji kujua ni kwamba tumezaliwa tukiwa na wingi wa dhambi ndani yetu ili tuweze kukombolewa kabisa. Ni wale tu wenye kukubali ukombozi ulioletwa na Yesu ndiyo watakao okolewa.
Wenye kufikiri kwamba hawajatenda dhambi nyingi, awamwamini Yesu kwamba alizichukua dhambi zao zote na wataishia motoni. Tunapaswa kujua kila mmoja wetu anazo hizi dhambi nyingi ndani yake kwa kuwa tumezaliwa nazo.
Ikiwa mtu atafikiri kwamba “Sijatenda maovu mengi, hivyo sihitaji ukombozi wa dhambi hizi ambazo ni chache sana.” Je, atakuwa huru hapo baadaye? Hili si jambo la maana.
Anayekombolewa hutambua ni mwingi wa dhambi. Hutambua hakika Yesu alizichukua dhambi zote kwa ubatizo katika mto Yordan na pia alizilipia dhambi pale alipokufa msalabani.
Haijalishi tumekombolewa au la, bado tutaendelea kuishi na kusumbuliwa na fikra potofu. Sisi ni wenye wingi wa dhambi. Na hii ndivyo tulivyo. Tunaweza kukombolewa endapo tukimwamini Yesu kwamba, alizichukua dhambi zetu zote.
 

Mungu Hakuwakomboa wale wenye “dhambi chache”

Ni yupi amdanganyae Bwana?
Ni yule mwenye kuomba msamaha
wa dhambi za kila siku.

Mungu hawakomboi wale wenye “dhambi chache” Mungu hawezi kuwatazama wale wenye kusema “Mungu, tazama mimi ninadhambi chache sana” Anao waonea huruma ni wale tu wenye kusema “Mungu, nitaokolewa ikiwa utaniokoa. Siwezi kamwe kuomba toba tena kwa sababu nafahamu siwezi kujizuia kuacha kurudia kutenda dhambi. Naomba uniokoe”
Mungu huwaokoa wale tu wenye kumtegemea yeye pekee. Hata mimi nilijaribu kuomba sala za toba kila siku lakini hazikuniacha huru. Hivyo nilipiga magoti mbele za Mungu na kuomba “Mungu nakusihi unihurumie na uniokoe kwa dhambi zangu.” Na aombaye namna hii huokolewa na kuamini katika ukombozi wa Mungu na ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji. Wataokolewa.
Mungu huwaponya wale tu wenye kujitambua ndani ya nafsi yao kwamba ni wenye wingi wa dhambi, kidogo tu, hivyo naomba unisamehe” bado ni wenye dhambi na Mungu hawezi kuwaokoa. Mungu kuwaokoa wale tu wenye kuzikubali dhambi zao kuwa ni nyingi.
Katika Isaya 59:1-2 imeandikwa, “Tazama mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia, lakini maovu yenu yamewafarakisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimewaficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”
Kwa kuwa tumezaliwa na wingi wa dhambi; Mungu hawezi kututazama kwa kuvutiwa nasi. Si kwa sababu mkono wake ni mfupi, macho yake ni mazito au hawezi kusikia tunapo omba msamaha.
Mungu anatuambia “maovu yenu yamewafarakisha ninyi na Mungu wenu na dhambi zimewaficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” Kwa kuwa tunadhambi nyingi ndani ya mioyo yetu hatuwezi kamwe kuingia mbimbuni, hata ikiwa milango itafunguliwa na kuwa wazi zaidi.
Ikiwa sisi tulio na wingii wa dhambi tukiomba msamaha kila tunapotenda dhambi, Ingempasa Mungu kurudia mara kwa mara kumsulubisha Mwana wake kwa ajili ya toba hizo za kurudiwa. Hakika Mungu hapendezwi kufanya njia hii. Anasema “Usije kwangu kila mara na kila siku kwa dhambi zako. Nilimtuma Mwanangu kuwakomboa na dhambi zenu zote. Inawapasa kuelewa ni kwa namna gani alizichukua dhambi zenu zote na kuamini hili ni la kweli. Hivyo amini Injili kwa maji na kwa Roho ili muokolewe. Huu ni upendo mkuu niliowapa watu wangu.”
Hivi ndivyo atuambiavyo “Mwamini Mwana wangu na mpokee ondoleo la dhambi Mimi Mungu wako nilimtuma Mwana wangu wa pekee kuwapatanisha na maovu yenu yote kwangu. Mwamini Mwana wangu ili muokolewe.”
Wale wote wasiojitambua kuwa wenye wingi wa dhambi huenda mbele zake bila kuelewa hatari ya wingi wa dhambi zao na kuomba tafadhali, “Bwana nisamehe dhambi hizi tu ambazo ni chache.”
Wanajaribu kumlaghai Mungu kwa maombi ya namna hii. Hatutendi dhambi mara moja tu, bali tunaendelea kutenda hadi kifo. Kwa hili tungepaswa basi kuendelea kuomba msamaha mara zote hadi mwisho wa maisha yetu, kwa sababu hatuwezi kuzuia kutenda dhambi, na miili yetu ipo chini ya sheria ya kutenda dhambi hadi kufa.
Kusamehewa dhambi chache si suluhisho la tatizo la dhambi kwa sababu tutaendelea kutenda dhambi nyingine tena pasipo idadi. Hivyo njia pekee ya kutuacha tuwe huru ni kuzitwika dhambi zetu zote kwa Yesu.

Nini asili ya Mwanadamu?
Mwingi wa dhambi.

Biblia inatoa idadi ya dhambi za wanadamu; “Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli, hutumaini ubatili, hunena uongo, hupata mimba ya madhara na kuzaa uovu. Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa na hilo livunjwalo hutoka nyoka nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao, kazi zao ni kazi za uovu na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao. Miguu yao hukimbilia mabaya nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao. Njia ya amani hawajui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo yao; wamejifanyizia njia zilizo potoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani” (Isaya 59:3-8).
Mikono ya watu ina najisi ya uovu na yote, wayatendayo maishani mwao ni dhambi tu! Kila watendalo ni dhambi. Na ndimi zetu zimenena uongo. Kila litokalo kinywani ni udanganyifu. 
“Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo” (Yohana 8:44). Wale ambao hawajazaliwa upya husema “Ninakueleza kweli … hakika kweli. Ninachosema ni kweli…” Ingawa kila alichosema si kweli. Ni kama ilivyoandikwa Shetani “asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe.”
Watu huweka imani yao palipo na maneno matupu na kusema uongo. Watu hubeba dhambi na kuzaa uovu. Huatamia mayai ya fira na kusuka wavu wa buibui. Mungu anasema “yeye alaye mayai yao hufa, la hilo livunjwalo hutoka nyoka.” Anasema kuna mayai ya fira moyoni mwako. Mayai ya nyoka! Kuna uovu ndani ya moyo wako. Na ndiyo maana tunapaswa kukombolewa kwa kuamini Injili kwa maji na kwa damu.
Ninapoanza kuongea juu ya Mungu, wapo wenye kusema “Oh, mpendwa, usinizungumzie juu ya huyu Mungu, kwani kila ninapojaribu kutenda jambo, dhambi hutoka ndani mwangu. Inafurika nje. Siwezi kuchukua hatua bila ya kutenda dhambi mahala popote. Sina msaada! Nimejawa na dhambi. Sina matumaini. Hivyo usinizungumzie juu ya Mungu huyu Mtakatifu.”
Mtu wa aina hii ni mwenye hakika kwamba ni mwingi wa dhambi lakini hajafahamu kwamba Mungu amekwisha mwokoa kwa ukamilifu wote wa Injili ya upendo wake. Ni wale tu wenye kuzitambua nafsi zao kuwa na wingi wa dhambi ndiyo wenye kuokolewa.
Kwa hakika kila mtu yupo namna hii. Kila mtu huendelea kutokwa dhambi mahala pote aendapo. Dhambi hufurika na kumwagika kwa kuwa watu ni wenye wingi wa dhambi. Njia pekee kwetu ya kuokolewa kutoka mazingira ya aina hii ni kwa kupitia uweza wa Mungu. Je huoni ni rahisi na ajabu? Wote wale wenye kujikuta wakitenda dhambi mara zote husononeka, kukosa furaha ingawa utulivu wao hupatikana kwa Bwana Yesu Kristo alikuja kutuokoa.
Kwa ukamilifu, alizifuta dhambi zetu zote. Kubali tu kwamba wewe ni mwingi wa dhambi ili uokolewe.