Mahubiri

Somo la 2: Sheria

[2-1] (Luka 10:25-30) Ikiwa Tutaenenda Kwa Sheria, Je, Itatuokoa?

(Luka 10:25-30)
“Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu akisema Mwalimu, nifanye nini ili nirithi uzima wa milele? Akamwambia, imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama nafsi yako. Akamwambia, umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. Naye akitaka kujidai haki; alimwuliza Yesu na jirani yangu nani? Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao wakimwacha karibu kufa.”
 

Je, tatizo kuu la
Mwanadamu ni lipi?
Wanaishi kwa wingi wa 
fikra potofu.

Luka 10:28, “fanya hivi nawe utaishi.” 
Watu wengi huishi kwa fikra potofu. Inaonekana kwamba jambo hili huwafadhaisha sana. Huonekana kwamba ni wenye uerevu lakini rahisi kudanganyika na mwisho kutokujua wapo kwenye upande wa maovu. Tumezaliwa bila ya kutambua nafsi zetu, lakini tunadhani tunazijua. Ikiwa basi watu hawazitambui nafsi zao, Biblia inarudia kutueleza kwamba sisi sote ni wenye dhambi.
Kwa kawaida watu huongea habari za dhambi zao. Inaonekana kwamba watu hawana uwezo ndani yao wakutenda mema, ingawa wao wamejiundia tabia ya kujiona ni wema. Hujigamba kwa matendo mema ambayo wametenda ingawa hukubali kwa kushuhudia kwa vinywa vyao kuwa ni wenye dhambi.
Hawajui ya kwamba labda wanayo mazuri ndani mwao au hawana uwezo wa kutenda mema na hivyo kujaribu kudanganya wengine na kwa nyakati nyingine kijidanganya wenyewe. “Tazama hatuwezi kuwa si wema kabisa! Kuna mambo kiasi ambayo ni mazuri ndani yetu.”
Kwa yote haya watu wa aina hii huwaona wengine na kusema “Lo! Sikudhani kama angeweza kufanya hivi. Ingekuwa ni vema kama asingefanya hili. Angeweza kufanya vizuri zaidi kama asingetenda jambo hili. Ingekuwa vizuri zaidi kama angesema hivi. Nafikiri ingekuwa vizuri kama angehubiri Injili namna hii. Ameokoka kabla yangu, hivyo nadhani alipaswa kutenda mambo kama aliyeokoka zaidi yangu. Nimeokoka hivi karibuni, lakini najua mengi na nitafanya vizuri zaidi yake.”
Humo makali ya mioyo pindi wanapojeruhiwa “subiri, utaniona mimi si kama wewe. Unaweza kudhani wewe ni zaidi yangu, lakini utaona. Imeandikwa kwenye biblia wale walio wa mwisho watakuwa wa kwanza. Najua itakuwa kwangu. Subiri nitakudhihirishia.” Watu hujidanganya nafsi zao.
Ingawa angeweza kujibu mashambulizi ya maneno haya kama angekuwa ni yeye mwenye kuambiwa haya, bado ataendelea kutoa hukumu. Anaposimama madhabauni hujikuta akipata kigugumizi kwa kuwa dhamira yake inamhukumu. Swali linapokuja mbele za watu ikiwa wanao uwezo wa kutenda mema, wengi husema hawana uwezo wowote. Lakini ndani ya nafsi zao wanazo fikra kwamba wao wanao uwezo huo. Hivyo hujaribu kutenda mema hadi wanapo kufa.
Hufikiri wanayo mazuri ndani ya mioyo yao na wanao uwezo wa kutenda mema. Na huamini kuwa wao ni wema wa kutosha. Ukiachilia mbali ni kwa muda gani wamekuwa wenye kushika dini, hasa wale ambao waliopata mafanikio makubwa katika kazi za Mungu, hufikiri “Mmeweza kufanya hivi na vile kwa ajili ya Bwana.”
Je, ikiwa tutamweka Bwana kando ya maisha yetu, tutaweza kweli kutenda mema? Kuna mema kweli ndani ya utu wetu? Tutaweza kweli kuishi kwa kutenda mema? Wanadamu hawana uwezo binafsi wa kutenda mema. Wanapojaribu kwa nafsi, hujikuta wakiishia kutenda dhambi. Wengine humweka Yesu kando baada ya kumwamini kwa kujaribu kutenda mema kwa kutegemea nafsi zao. Hakuna la zaidi bali ni uovu kwetu na hivyo kutenda dhambi tu. Kwa wote (hata waliookoka) tunaweza kutenda dhambi. Ni ukweli wa miili yetu.

Mara nyingi tunatenda yapi?
Mabaya au mazuri?
Mabaya!

Katika kitabu chetu cha nyimbo za kusifu “Lisifuni jina la Yesu” kuna wimbo Fulani huimbwa “♪Bila Yesu tumekwama. Hatuna thamani kama vile merikebu ipitavyo bahari kuu bila nahodha. ♪” Bila Yesu, tutaweza kuanguka dhambini tu! Sisi ni viumbe waovu. Tutaweza kutenda mema pale tu tutakapookolewa.
Mtume Paulo alisema “Kwa maana lile jema nilipendalo silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo” (Warumi 7:19). Kama mtu akiwa ndani ya Yesu, haijalishi hili, ingawa atakapo jaribu kutenda mema bila Mungu wakati wote atajikuta akiishia kutenda dhambi.
Hata mfalme Daudi aliwahi kuwa mwenye asili hii. Wakati ufalme wake ulipostawi na kuwa wenye amani, siku moja aliamka na kwenda juu ya dari la nyumba yake kupunga hewa. Hapo aliona kushawishi na kuanguka kwenye tamaa ya mwili. Alikuwa vipi alipo msahau Bwana? Alikuwa mwovu! Alifanya tendo la zinaa na Basheba na kumuua Uria, mumewe na hakuuona uovu wake. Badala yake alijitetea kwa matendo yake.
Ndipo siku moja, nabii Nathari alipomjia na kusema “Palikuwa na watu wawili katika mji mmoja; mmoja wao alikuwa tajiri, wapili maskini, Yule tajiri alikuwa na kondoo na ng’ombe wengi sana; bali yule maskini hakuwa na kitu, ila mwanakondoo mmoja, mdogo ambaye amenunua na kumlea; naye akakuwa pamoja naye na pamoja na wanawe, hula sehemu ya posho lake, na kukinyanyua kikombe chake na kulala kifuani mwake akawa kwake kama binti. Hata msafiri mmoja akamfikia yule tajiri, naye akaacha kutwaa moja ya kondoo zake mwenyewe, au moja ya ng’ombe zake mwenyewe, ili kumuandalia yule msafiri aliyemfikia, bali alimnyang’anya yule maskini mwanakondoo wake, akamwandalia yule mtu aliyemfikia” (2 Samweli 12:1-4).
Daudi akasema “mtu aliyetenda jambo hili, hakika yake astahili kufa!” Hakika hasira yake ilimpanda na kusema “Alikuwa na mifugo yake mingi na yakutosha; ilimpasa kuchukua moja wapo. Badala yake alichukua kondoo wa masikini kwa matayarisho ya chakula cha mgeni wake. Yampasa kufa!” Ndipo Nathani alipomwambia “Wewe ndiwe mtu huyo” kama hatumfati Yesu na kuwa naye, hata yule aliyeokoka aweza fanya kama haya.
Ndivyo ilivyo kwa watu wote, hata wale waaminifu mara nyingi huanguka kwa kutenda uovu bila Yesu. Hivyo yatupasa tushukuru sana nyakati hizi kwamba Yesu ametuokoa, ingawa ndani yetu hatuna lililo jema. “♪Naam tena mtulie chini ya kivul cha Msalaba. ♪” Miyoyo yetu imetulia chini ya kivuli cha ukombozi wa Kristo, lakini ikiwa tutakiacha na kutafuta wenyewe, hakika hatutapata pumziko.
 

Mungu ametupatia Haki kwa Imani katika sheria

Ni ipi inapaswa kuwa ya kwanza
Imani au Sheria?
Imani.

Mtume Paulo alisema kwamba, Mungu ametupatia haki kwa imani toka mwanzo. Alimpatia Adamu na Hawa, Kaini na Abeli, Sethi na Enoki, Nuhu, Abrahamu, Isaka na mwisho Yakobo na watoto wake kumi na wawili. Hata pasipo sheria, walifanywa kuwa wenye haki mbele za Mungu kupitia haki itokanayo na Imani ya Neno lake. Walibarikiwa na walipata pumziko kupitia imani ya Neno lake.
Muda uliopita wakati uzao wa Yakobo uliishi Misri kama watumwa kwa miaka 400 kwa sababu ya Yusufu. Ndipo Mungu alipowaongoza kutoka kupitia Musa kuelekea Kanaani, pamoja na kuwa watumwa kwa miaka 400, walisahau haki katika Imani.
Ndipo Mungu alipowaongoza kupita kati ya Bahari ya Shamu kwa muujiza na kuwaongoza jangwani walipofika jangwa la dhambi, akawapa sheria katika Mlima Sinai. Aliwapa sheria ambazo zilikuwamo Amri kumi na vipengele 613. Mungu aliahidi “Ndimi Bwana Mungu wako, Mungu wa Abraham, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Musa apande na kuja katika mlima Sinai na nitawapa sheria.” Ndipo alipowapa Waisraeli Sheria.
Aliwapa Sheria ili waweze “kutambua dhambi” (Warumi 3:20). Ilikuwa ni kuwafahamisha juu ya anachotaka na asichotaka na kuweka wazi haki yake na utakatifu.
Watu wote wa Israeli waliokuwa utumwani Misri kwa miaka 400 walipita kati ya Bahari ya Shamu. Hawakuwahi kukutana na Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. Hawakumjua.
Walipokuwa wakiishi kama watumwa kwa kipindi hicho cha miaka 400, walisahau haki ya Mungu katika muda huo hawakuweza kuwa na kiongozi Yakobo na Yusufu walikuwa viongozi hapo awali inaonekana Yusufu alishindwa kuirithisha Imani hiyo kwa watoto wake wa kiume, Manase na Efraimu.
Hivyo, walihitaji kumtafuta Mungu tena na kukutana naye kwa kuwa waliisahau haki yake. Tunapaswa kuweka akilini kwamba Mungu aliwapa haki kwa imani mwanzo na kuwapa sheria baada ya kuisahau Imani. Aliwapa Sheria ili waweze kumrudia.
Kuiokoa Israeli na kuwafanya kuwa wana wake, aliwaambia kwamba aliwalazimu kutahiriwa.
Nia ya kuwaita ilikuwa ni kuwafanya watambue kwamba alikuwa kati yao ili kuanzisha Sheria na pili, kufanya watambue walikuwa ni wenye dhambi mbele zake. Mungu alitaka waje mbele zake na kuwa watu wake kwa kukombolewa kwa mfumo wa sadaka ambayo aliyokuwa amewapa. Na aliwafanya kuwa watu wake.
Wana wa Israeli walikombolewa kupitia mfumo wa sadaka wa Sheria kwa kumwamini Masiya ajaye. Lakini mfumo huu ulipitwa na wakati. Na tuangalie hii, ilikuwa ni lini.
Katika Luka 10:25 mwanasheria mmoja alitajwa kumjaribu Yesu. Alikuwa ni Mfarisayo. Mafarisayo walikuwa ni wenye kuyashika mafundisho bila kukubali kubadilika kwa kufanya jitihada zao binafsi kuishi kwa kufuata neno la Mungu; Walijaribu kuzilinda sheria za nchi kwanza kwa kuishi kadiri ya maandiko ya sheria. Walikuwa ni wakereketwa (kwa lugha ya kisasa) ambao walihamasisha na fanya ghasia za kuvunja sheria ili kufanikisha malengo ya maono yao juu ya uhuru wa Waisraeli toka kwa Warumi.

Yesu alitaka kukutana 
Na watu gani?
Wenye dhambi wasio na 
Mchungaji.

Kuna baadhi yao hata nyakati hizi wamo kwenye dini tuzionazo. Huongoza harakati za kijamii kwa usemi kama vile “Okoa wanaogandamizwa duniani!” Huamini Yesu alikuja kuokoa maskini na wanaogandamizwa. Hivyo baada ya kujifunza theologia katika seminari, huchukua nafasi katika mambo ya kisiasa na kujaribu kuwakomboa wanaonyanyaswa katika kila sehemu ya jamii.
Ndiyo wenye kushinikiza kwa kusema “Hebu na tuishi kwa sheria na rehema ya sheria takatifu. Tuishi kwa sheria, kwa neno la Mungu.” Lakini hawatambui hakika ya ukweli wa Sheria. Hujaribu kuishi kwa sheria iliyoandikwa bila kufahamu na kupata ufunuo wa Mungu juu ya Sheria hiyo.
Kwa maana hiyo tunaweza kusema kwamba hapakuwepo na manabii, watumishi wa Mungu katika Israeli kwa kipindi hicho cha miaka 400 kabla ya Kristo. Kwa sababu hii basi, walikuwa ni kundi la kondoo wasio na Mchungaji.
Hawakuwa na sheria wala Kiongozi wa kweli. Mungu hakujidhihirisha mwenyewe kwa hao walio kuwa ni viongozi wa dini zao walio wanafiki. Nchi ilitawaliwa na Dola ya Warumi. Hivyo Yesu aliwaambia watu hawa wa Israeli walio mfuata jangwani kwamba hawatarudishwa kutoka kwake wakiwa na njaa. Alijawa na huruma juu yao waliokama kundi la wanakondoo wasio na Mchungaji kwani wengi wao walikuwa kwenye mateso makubwa.
Wanasheria na wale wengine walio na nafasi za uongozi walikuwa ndiyo wenyewe tu wenye kunufaika. Mafarisayo walikuwa ni kizazi cha “Judaism” na walikuwa ni wenye majivuno sana.
Mwanasheria huyu alimwuliza Yesu katika Luka 10:25 “nifanye nini niweze kurithi uzima wa milele?” Alionekana kufikiri kwamba yeye ni bora zaidi kati ya watu wa Israeli. Hivyo mwanasheria huyu (ambaye hajakombolewa) alimwuliza Yesu kwa kusema “nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?”
Mwanasheria huyu anasimama badala yetu leo. Alimwuliza Yesu swali hili, naye akajibu “imeandikwa nini katika Torati? Wasomaje?” 
Naye akajibu “mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote na akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.”
Naye akamjibu “umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.”
Alijaribu kumtia changamoto Yesu bila ya kufahamu yeye alikuwa ni mwenye dhambi, asiyeweza kutenda mema. Hivyo Yesu alivyomwuliza, “imeandikwa nini katika Torati, wasomaje?”

Unasoma nini juu
ya sheria?
Sisi ni wenye dhambi tusioweza
kufuata sheria. 

“Wasomaje” kwa kifungu hiki Yesu anauliza, ni kwa namna gani mimi na wewe tunaijua na kuielewa sheria.
Kwa jinsi hii wengi wetu nyakati hizi ndivyo tulivyo. Mwanasheria huyu alifikiri kwamba Mungu alikusudia kuweka sheria ili zifuatwe. Hivyo alijibu kupitia maandiko “mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote na jirani yako kama nafsi yako.”
Sheria haikuwa na kasoro. Alitupa sheria iliyo kamilifu. Alituambia tumpende Bwana kwa moyo na kwa roho na kwa nguvu na akili na kuwapenda majirani zetu kama nafsi zetu. Ni haki tumpende Mungu kwa moyo wetu wote na kwa nguvu zetu zote, lakini hii ni amri takatifu isiyoweza kutimizwa kwa nafsi zetu.
“Wasomaje?” Hii ina maana sheria ni kamilifu na sawa lakini je, wewe unaelewa nini juu yake? Mwanasheria alifikiri kwamba Mungu alileta sheria hii ili aweze kuitii. Ingawa Sheria ya Mungu imeletwa kwetu ili tuweze kuziona nafsi zetu na upungufu ndani yake kwa kuukubali udhaifu wetu uliowazi kabisa mbele za Mungu. “Umetenda dhambi, umeua hali nilikuambia usiue. Kwa nini hukunitii.” Ndivyo Mungu akuulizavyo.
Sheria huweka wazi madhambi ya watu ndani ya mioyo yao. Hebu na tufikiri kwa mfano nilipokuwa nikitembea, nikaona tunda zuri na tamu ililoiva katika shamba la mtu. Mungu amenionya kwa sheria, “usichume tunda hilo katika shamba. Itaniaibisha mimi ukitenda hilo.” “Ndiyo Baba.” “Shamba hili ni la ndugu fulani, hivyo usichume.” “Ndiyo Baba.”
Tunaposikia hivyo tusichume, tunahisi msukumo ndani yetu wa kuchuma. Tunapochukua hatua ya kujizuia inashindikana. Na hii ndivyo ilivyo katika dhambi za za watu.
Mungu ametuonya tusitende dhambi. Aweza kusema hivi kwa kuwa yeye ni mtakatifu, mkamilifu na mwenye uwezo wote. Kwa upande mwingine hatuwezi “kamwe” kutotenda dhambi na “kamwe” hatuna utakatifu. Hatuna mazuri ndani ya mioyo yetu. Sheria inatuhukumu na neno “kamwe.” Kwa nini? Kwa sababu watu husukumwa na tamaa ndani ya mioyo yao. Hatuwezi kujizuia bila kufuata tamaa. Tunatenda dhambi ya uzinzi kwa kuwa tunayo dhambi ya uzinzi ndani ya mioyo yetu.
Tunapaswa kusoma biblia kwa makini. Niliposoma niligundua maneno haya. Nilisoma kwamba Yesu alikufa msalabani kwa ajili yangu na nilishindwa kujizuia machozi yalinitoka. Hakika nilikuwa mwingi wa dhambi hata kumfanya afe kwa ajili yangu… Moyo wangu ulipondeka sana hata kumwamini. Na ndipo nilipowaza “ikiwa nitamwamini, basi nitaliamini neno lake.”
Niliposoma kitabu cha Kutoka 20, Biblia inasema “usiwe na miungu wengine zaidi yangu.” Niliomba toba kutokana na amri hii. Nilitafuta katika kumbukumbu za akili yangu ikiwa hapo awali niliwahi kuwa na miungu wengine zaidi yake, kulitaja jina lake bure, au kuabudu miungu wengine. Niligundua kwamba niliabudu miungu wengine mara nyingi wakati nilipotoa kafara kwa heshima ya mababu zangu walio kufa. Nilitenda dhambi ya kuwa na miungu wengine.
Hivyo niliomba kwa kutubu, “Bwana, nimeabudu miungu wengine. Imenipasa kuhukumiwa kwa hilo. Nakusihi unisamehe dhambi zangu. Sinto tenda tena.” Na baadaye, dhambi moja itaonekana kuondolewa.
Hapo tena jaribu kukumbuka ikiwa niliitia jina la Mungu bure. Nagundua ya kwamba nilipo anza kumwamini Mungu, nilikuwa nikiendelea kuvuta sigara. Rafiki zangu walinieleza, “Huoni yakuwa unamwaibisha Mungu kwa kuvuta kwako sigara? Itawezekanaje kwa Mkristo kuvuta sigara?”
Hii ni sawa na kuliitia jina lake bure. Hivyo nikaomba tena “Bwana nimeliita jina lako bure, Naomba unisamehe. Nitaacha kuvuta.” Hivyo nilijaribu kuacha kuvuta lakini nilishindwa na kuendelea na kuacha kwa muda tofauti katika kipindi cha mwaka mzima. Hakika ilikuwa ni vigumu kwangu na ilifikia kutowezekana kuacha kuvuta sigara. Lakini mwishowe niliweza kabisa nilidhani hii ilikuwa tayari dhambi niliyoweza kuidhibiti.
Nyingine ilikuwa, “Kuitakasa siku ya Sabato.” Hii ina maana kwamba nisifanye shughuli yeyote siku ya Jumapili, kazi au kutafuta fedha… Na niliweza kuacha hili pia.
Ndipo ilipokuja “Waheshimu baba na mama yako.” Niliwaheshimu nilipokuwa mbali nao, lakini nilipokuwa karibu nao nilikuwa na machungu juu yao. “Oh! Nimetenda tena dhambi mbele ya Mungu. Naomba unisamehe” niliomba toba.
Lakini sikuweza kuwaheshimu kwani wote walikwisha fariki kwa wakati huo. Nifanye nini sasa? “Bwana, naomba msamaha mimi mwenye dhambi nisiye na thamani, ulikufa msalabani kwa ajili yangu” nilishukuru sana!
Njia hii ndiyo niliyo itumia kushughulikia dhambi zangu moja hadi nyingine. Palikuwa na sheria nyingine kama vile usiue, usizini, usitamani mpaka nilipokuja gundua sikuweza kufuata hata moja, niliomba usiku kucha! Je, wajua ya kwamba kuomba na toba haifurahishi kabisa. Hebu tuangalie hili.
Nilipo waza juu ya kusulubiwa kwa Yesu, niliona uchungu uliokuwepo. Alikufa kwa ajili yetu na ni nani asiye taka kuishi kwa neno lake. Nililia usiku mzima na kuwaza ni upendo wa namna gani juu yangu na nilimshukuru kwa kunipa faraja ya kweli.
Katika mwaka wangu wa kwanza kuhudhuria kanisani ulikua kwa ujumla ni rahisi, lakini miaka ilipozidi kuendelea ikawa ni vigumu kwangu kulia kwa kuomba toba kwani ilibidi nifikiri sana ili niweze kulia kwani nilikwisha kuwa na mazoea.
Machozi yalipoacha kunitoka, niliamua kuomba milimani na kufunga siku hadi 3. Ndipo machozi yalipo toka. Yalinilenga tena nilipo kuja mbele ya kanisa nililia.
Walio nizunguka waliniambia “Oh! Umekuwa mtakatifu sana kwa sala zako za milimani.” Lakini baadaye yalikauka tena. Ikawa vigumu tena katika mwaka wa tatu. Nilijaribu hata kufikiri mabaya niliyotenda kwa rafiki zangu na ndugu katika Kristo ili niweze kutoka machozi Haikuwezekana kabisa!
Baada ya miaka 5, sikuweza kulia ingawa nilijitahidi kwa namna zote na hata kutokwa na makamasi. Baada ya miaka kadhaa katika hili, sikupata amani ndani yangu. Na ndipo Mungu alinifanya niirudie tena Biblia.
 

Sheria ni kwa ajili ya kuzifahamu dhambi

Tunagundua nini juu 
ya Sheria?
Kamwe hatuwezi kuzifuata 
Sheria. 

Katika Warumi 3:20 tunasoma “Kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” Mwanzo kabisa nilichukulia kifungu hiki kuwa ujumbe binafsi kwa Mtume Paulo na kuamini maneno niliyopendelea. Lakini baada ya machozi yangu kukauka hakika sikuweza kuendelea na maisha yangu ya imani ya kidini.
Hivyo niliendelea na dhambi na kufikia hatua ya kugundua nina dhambi ndani ya moyo wangu na kushindwa kuishi kwa sheria. Sikuweza kuvumilia ingawa sikuweza kuachana na sheria kwa kuwa niliamini ilikuwepo ili niweze kuitii. Hatima yake nikawa mwanasheria kama walionyeshwa katika maandiko hapo awali. Ikawa ni vigumu kwangu kuendelea na maisha ya imani.
Nilikua na dhambi nyingi hata kufikia kila ninapo soma sheria naanza kugundua dhambi hizo kila ninapozivunja amri 10 ndani ya moyo wangu. Ikumbukwe kuwa na dhambi moyoni ni sawa kutenda dhambi tu! Sikuweza kufahamu kwamba nilikuwa tayari muumini wa sheria.
Nilipofuata sheria nilifarijika. Lakini nilipoanguka nilikua mnyonge, mwenye hasira na huzuni. Na wakati huo nikawa mwenye kukosa matumini kwa yote. Ingeweza kuwa rahisi ikiwa hapo awali ningefundishwa ukweli juu ya sheria kama vile “Hapana, siyo hivi! Ipo maana nyingine ya sheria nayo ni kama taa kuonyesha dhambi zako kama vile wewe unapenda fedha, kupenda jinsia tofauti na vitu vizuri vya kuonekana.Una vitu unavyovipenda kuliko upendavyo Mungu. Unapenda sana kufuata mambo ya dunia. Sheria iliwekwa kwako si nifuate bali uweze kugundua nafsi yako kama mwenye dhambi aliye na uovu moyoni.”
Ikiwa mtu yoyote angeweza kunifundisha hivi basi nisingeweza kuteseka kwa miaka 10 namna ile. Hivi ndivyo nilivyo weza kuishi kwa sheria kwa miaka 10 kabla ya kuja kugundua hili.
Amri ya nne inasema “Ikumbuke siku ya Sabato na uitakase.” Hii ina maana kwamba tusifanye kazi siku ya jumapili.Tunafundishwa tufanye kazi, sio kutembea mwendo wa mbali katika safari kwa siku ya jumapili.Nilidhani ilikuwa ni sahihi na niheshima kutembea sehemu nilizo hitaji kuhubiri. Hata hivyo nilitaka kuhubiri sheria. Na nihisi ilinipasa kutenda yale nihubiriyo. Ikawa ni vigumu na kushindwa.
Kama ilivyo hapo mwanzo “wasomaje?” sikuelewa swali hili na kuteseka miaka 10. mwanasheria hakuelewa vema hili.Alifikiri ya kwamba ikiwa ataheshimu sheria na kuishi kwa uangalifu mkubwa atakuwa amebarikiwa na Mungu.
Lakini Yesu alimwambia “wasomaje?” Naye akajibu kwa imani itokanayo na sheria. Naye akamjibu “umejibu vema, unaichukua kama ilvyoandikwa. Jaribu kuifuata. Utaishi ikiwa utweza na utakufa ukishindwa. Mshahara wa dhambi ni mauti. Hakika ukishindwa utakufa.” (kinyume cha kuishi ni kufa,sivyo?)
Lakini mwanasheria huyu hakugundua hili. Mwanasheria ni mfano wetu sisi leo, mimi na wewe. Nilijifunza theologia (elimu ya dini) kwa miaka 10. Nilijaribu kila namna, kusoma kila kitu na kutenda kila jambo; kufunga kula, kuwa na maono, kunena kwa lugha… Nilisoma Biblia kwa miaka 10 kwa kutegemea nitahitimisha jambo fulani mbeleni. Lakini kiroho nilikuwa bado kipofu!
Na ndiyo maana mwenye dhambi huitaji mtu fulani atakayefungua macho yake, na huyu ni Bwana wetu Yesu Kristo. Ndipo mtu hugundua “Ahaa! Hatuna uwezo wa kufuata sheria. Haijalishi ni kwa bidii gani tutaweza kujaribu kuifuata tutaishia kufa tukikosa matumaini. Lakini Yesu alikuja kutuokoa kwa maji na kwa Roho! Haleluya!” Kwa maji na kwa Roho tutaweza kukukombolewa Ni neema, zawadi ya Mungu. Na tumsifu Bwana.
Nilikuwa mwenye bahati ya pekee kuhitimu toka kwenye njia ya kukosa matumaini katika sheria, naamini wengi huchukua muda mrefu zaidi katika maisha yao kusoma theologia katika njia panda na bila kugundua ukweli hadi umauti. Wengine huamini kwa mioyo mingi, kizazi hadi kizazi na hawazaliwi upya.
Tunahitimu kutokuwa wadhambi pale tu tunapogundua hatuna uwezo wa aina yeyote binafsi wa kufuata sheria na kusimama mbele ya Yesu kwa kukubali kuisikiliza Injili ya kwa maji na kwa Roho. Tunapokutana na Yesu tunahitimu kutoka kwenye hukumu na jehanamu. Sisi ni wenye wingi wa dhambi, lakini tunafanyizwa haki kwa sababu Yesu ametuokoa katika maji na damu yake.
Yesu amesema hatuwezi kuishi katika mapenzi yake. Alimwambia mwanasheria, lakini haelewa hili. Hivyo alimpa mfano huu.

Nini kimfanyacho Mwanadamu 
kuanguka tokakwenye 
maisha ya imani? 
Dhambi.

“Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha wakaenda zao,wakamwacha karibu kufa” (Luka 10:30 ). Yesu alimpa Mwanasheria mfano huu ili kuamsha dhamira yake kwakua kuteseka kwa maisha yake yote kama jinsi Mtu yule aliyepigwa na wanyang’anyi karibu kufa.
Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko. Yeriko inawakilisha dunia hii ya sasa, hali Yerusalemu inawakilisha mji wa kidini, mji wa imani uliojawa na majigambo ya sheria. Mfano huu hutuelezea ikiwa tutamwani Kristo kwa njia udini tutaangamia.
“Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko akangukia kati ya wanyang’anyi, wakamvua nguo wakamtia jeraha wakenda zao wakimwacha karibu kufa.” Yerusalemu ulikuwa ni mji mkubwa ukiwa na wakazi wengi. Kulikuwa na Kuhani Mkuu, Jeshi la Makuhani Walawi na wengi wa Wakuu mashuhuri wa dini. Palikuwepo na wengi wenye kuelewa sheria vema. Na walijaribu kuishi kwa sheria, lakini walishindwa na kukimbilia Yeriko wakangukia duniani (Yeriko) na kushindwa kuzuia kukutana na wanyang’anyi.
Mtu huyu pia alikutana njiani na wanyang’anyi toka Yerusalemu kwenda Yeriko wakamvua nguo. “Kuvuliwa nguo” maana yake kupoteza haki. Ni vigumu kwetu kuishi kwa kufuata sheria, kuishi kwa sheria Mtume Paulo amesema katika Warumi 7:19-20 “Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi, bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilipendalo si mimi nafsi yangu nilitendalo, bali ni ile dhamiri ikaayo ndani yangu.”
Ningetamani kutenda mema na kuishi katika Neno lake Mungu. Lakini ndani ya moyo wa mwanadamu umefurika mawazo mabaya, uasherati,wivi, uuaji, unzizi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu (Marko 7:21-23).
Kwa kuwa haya ndiyo yaliyomo ndani ya mioyo yetu, basi tunafanya yale tusiyopaswa na hatufanyi yale yatupasayo kufanya. Tunaendelea kurudia maovu haya ndani ya mioyo yetu. Hivyo shetani huitaji kukuhamasisha kwa kiasi kidogo tu ili uweze kutenda dhambi.
 
 
Dhambi zilizo ndani ya moyo wa kila mwanadamu

Je tutaweza kuishi
Kwa sheria?
Hapana!

Imeandikwa katika Marko 7:20 “kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.”
Yesu anatueleza kwamba yapo mawazo mabaya uasherati, wivi, uaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu katika moyo wa mwanadamu.
Wote tunauuaji ndani ya mioyo yetu. Hakuna asiyefanya mauaji. Mama hukemea watoto zao “Usifanye hivi. Nilikuambia usifanye, ole wako. Nilikueleza mara nyingi. Sasa nitakuua ukirudia tena.” Hii ni sawa na kuua! Unaweza kumuua mtoto wako katika mawazo yako kwa maneno yasiyo na fikara kama haya.
Imewapasa watoto wetu kuwa wepesi kutuepuka kwa kutukimbia; kwani pasipo hivyo tungeweza kuwashukia kwa vipigo vya hasira na hata kufikia hatua ya kuwaua. Wakati mwingine tunaingiwa hofu na kusema “Oh Mungu wangu! Kwanini nimefanya hivi?” Tunaanza kuona alama za uvimbe baada ya kuwapiga watoto wetu na kudhani yakuwa tulikuwa wendawazimu kwa kutenda hayo. Hatuwezi kujizuia kutenda haya kwa sababu ndani ya mioyo yetu kuna uuaji.
Hivyo “Ninatenda nisilo taka” maana yake tunatenda uovu kwa kuwa tuna uovu ndani yetu. Ni rahisi kwake shetani kutujaribu kutenda dhambi.
Na tuseme hivi kwa mfano, mtu ambaye hajakombolewa akae katika kibanda kwa miaka 10, akielekeza uso wake ukutani akiwazia kama Sungchol, kuhani wa dini ya Kijadi Korea. Ni vyema akiwa ameketi akielekeza uso wake ukutani, lakini itabidi mtu kumletea chakula na kufanya usafi mahala pale.
Itampasa awe na mawasiliano na mtu. Haitakuwa ni tatizo ikiwa atakuwa ni mwanaume kama yeye, lakini hebu tuseme akiwa ni mwanamke. Ikiwa atamwona kwa bahati, basi muda wote aliokaa utakuwa ni bure. Anaweza kuwaza moyoni “hainipasi kutenda uzinzi; lakini ninao moyoni; na inanibidi niuache. Niutoe. Hapana! Ondoka kwenye akili yangu!”
Lakini lengo lake litayeyuka pale tu atakapomuona mwanamke huyo. Baada ya mwanamke huyo kutoka, ataangalia ndani ya moyo wake. Miaka 5 ya jitihada zake zitageuka kuwa ni bure na vyote kwa ukorofi.
Ni rahisi shetani kuteka haki ya mtu. Kile alichonacho shetani ni kuweka msukumo mdogo tu! Mtu anapohangaika kutotenda dhambi bila ya kukombolewa kwanza ni rahisi na haraka zaidi kuanguka kwenye dhambi. Mtu huyo anaweza kuwa ni mtoaji mzuri wa zaka kila Jumapili, mfungaji kwa siku 40, mwenye kujitoa kwa maombi ya siku 100, lakini shetani hufanikiwa kumshawishi na kumdanganya kwa mambo mazuri ya maisha.
“Nitakupa nafasi bora ya cheo katika shirika, lakini wewe ni Mkristo usiyefanya kazi Jumapili, Vipi utaweza? Hii ni nafasi kubwa. Utaweza kufanya kwa muda wa wiki 3 za Jumapili na iliyobaki moja katika mwezi unaweza kwenda Kanisani. Na hakika utaifurahia nafasi hii nzuri yenye malipo manono. Unaonaje?” kwa hili mpendwa kati ya watu 100, watu 100 wangelikubali tu.
Kama halifanyi kazi hili, shetani atarudia mchezo mwingine kwa wale wenye tamaa ya ngono. Shetani atamleta mwanamke mbele yake na ataanguka kumtamani, na kumsahau Mungu mara moja! Na hivi ndivyo haki ya mtu inavyovuliwa.
Ikiwa tutajaribu kuishi kwa kuifuata sheria, mwisho wetu siku zote ni majeraha ya dhambi, maumivu na ufukara wa kiroho; tutapoteza haki zote. “Alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaanguka kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu kufa.”
Hii ina maana kwamba tunaweza kujaribu kukaa Yerusalemu kwa kuishi katika mapenzi ya Mungu Matakatifu, tutajikwaa kila wakati kwa sababu ya udhaifu na mwisho kuangamia.
Yaweza kuwa unaomba toba kwa Mungu, “Bwana nimetenda dhambi. Naomba unirehemu; sitotenda tena. Naahidi kwako kwamba hili litakuwa ni mwisho. Nakusihi unisamehe hili tu!”
Lakini haichukui muda. Watu hawawezi kuishi katika ulimwengu huu bila kutenda dhambi. Wanaweza kujizuia kwa kiasi cha muda fulani, lakini haiwezekani kutotenda kabisa. Hivyo hatuwezi, ila tutaendelea kurudia kutenda dhambi tu! “Bwana, naomba unisamehe” ukiendelea hivi, watalihama Kanisa na kuacha dini kabisa. Watamwacha Mungu kwa kuwa na dhambi na kuishia jehanamu.
Kushuka kwenda Jeriko ni sawa na kuangukia katika ulimwengu wa sasa; kuwa karibu na dunia mbali na Yerusalemu. Hapo mwanzo, Yerusalemu ilikuwa karibu na kwa kadiri ya mzunguko wa dhambi na kuungama ulivyorudiwa tunajikuta tukisimama katikati ya mji wa Yeriko; kuanguka kabisa duniani.

Nani awezaye Kuokolewa?
Wale watakao acha
Kujitafutia haki.

Alikutana na nani njiani alipokuwa akienda Yeruko? Alikutana na wanyang’anyi. Yeyote yule asiyetambua, na kuishi kwa sheria maisha yake yanafananishwa na mbwa aliyetelekezwa. Hula na kunywa na kwenda haja mahala popote. Mbwa wa aina hii huamka asubuhi nyingine na kunywa na kula tena. Huweza hata kula kinyesi chake. Ndiyo maana mtu huyu hufananishwa na mbwa. Hula na kunywa lakini huomba toba asubuhi inayofuata na kurudia yale yale kwa mara zote.
Ni sawa na mtu aliyekutana na wanyang’anyi akienda Yeriko. Akaachwa akiwa amejeruhiwa karibu ya kifo. Ina maana kwamba kuna dhambi ndani ya moyo. Na hii ndivyo ilivyo kwa mwanadamu.
Watu humwamini Yesu na kujaribu kuishi kwa sheria katika Yerusalemu, jamii ya dini, lakini wanaachwa na dhambi ndani ya mioyo yao. Kile wanachoweza kuonyesha katika maisha yao ya udini ni majeraha ya dhambi. Wale wenye dhambi mioyoni mwao hakika siku za mwisho watakwenda motoni. Wanajua hili, lakini hawajui lakufanya. Je ni kweli hata wewe upo katika mji huo wa dini? Ndiyo. Hata sisi tulikuwepo.
Mwanasheria aliyeshindwa kuielewa sheria ya Mungu angehangaika maishani pote, lakini angeishia motoni kwa majeraha. Ni sisi kati yetu, mimi na wewe.
Yesu pekee aokoa. Wapo watu wengi wenye uerevu kati yetu na kila mara kupayuka wanayoyajua. Wote hawa hujifanya kwa kuishi katika sheria ya Mungu na hawapo kweli nafsini mwao. Hawawezi kuita beleshi kuwa ni beleshi, mara zote hizificha nafsi zao kwa nje ili kuonekana waaminifu.
Kati yao ni wenye dhambi kuelekea Yeriko, wale waliopigwa na waovu na kuachwa karibu kufa. Tunapaswa kuelewa vile tusivyo imara, wepesi wa kuumizwa mbele za Mungu.
Yatupasa tukiri mbele zake “Bwana, hakika nitaishia motoni ikiwa hutoniokoa. Naomba uniokoe. Nitakufuata popote, ikiwa ni penye kimbunga au dhoruba, ikiwa tu nitaweza kusikia Injili. Ukiniacha peke yangu, nitakwenda motoni. Nakusihi niokoe!”
Wale wenye kugundua kuwa wapo karibu na jehanamu na kujaribu kutenda matendo ya kujitafutia haki wakiwa wanaambatana na Bwana ndiyo pekee watakaookolewa. Hatuwezi kuokolewa kwa juhudi zetu binafsi.
Yatupasa kuelewa kwamba, tutafananishwa na mtu yule aliye angukia katika mikono ya wanyang’anyi.