Mahubiri

Somo la 4: Kutatua Dhambi za Kila Siku

[4-1] (Yohana 13:1-17) Injili Ya Upatanisho Ulio Kamilifu

(Yohana 13:1-17)
“Basi kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapedna upeo. Hata wakati wa chakula cha jioni naye Ibilisi amekwesha kumtia Yuda mwana wa Simoni Iskariote moyo wa kumsaliti Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na yakuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu aliondoka chakulani, akaweka kando mavazi yake akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuufuta kwa kile kitambaa alichojifunga. Hivyo yuaja kwa Simoni, Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia kama nisipo kutawadha huna shirika nami Simoni Petro akamwambia Bwana, si miguu yangu tu hata na mikono yangu na kichwa changu pia. Yesu akamwambia Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote, nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote. Kwa maana alimjua yeye atakaye msaliti; ndiyo maana alisema, si nyote mlio safi. Basi alipokwisha kuwatawadha miguu na kuyatwaa mavazi yake na kuketi tena akawaambia Je, mmeelewa na hayo niliyowatendea? Niny mwaniita, Mwalimu na Bwana, nanyi mwanena vema; maana ndivyo nilivyo. Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu nimewatawadha miguu imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa nimewapa kielelezo ili kama mimi nilivyo watendea; nanyi mtende vivyo Amin, amin, nawaambia ninyi, mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliye mpeleka; mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda. Sisemi habari za ninyi nyote, nawajua wale niliowachagua, lakini andiko lipate kutimizwa aliyekula chakula changu amenunulia kisigino chake.”
 

Kwa nini Yesu alimwosha miguu Petro siku moja kabla ya sikuu ya Pasaka? Punde kabla ya kumsafisha miguu Yesu alisema “Nifanyalo wewe hujui sasa lakini utalifahamu baadaye.” Petro alikuwa wa pekee zaidi kwa Yesu kati ya wanafunzi wote. Aliamini kwamba Yesu alikuwa ni Mwana wa Mungu na alishuhudia kwamba ndiye Kristo. Wakati Yesu alipokuwa akisafisha miguu yake, palikuwa na sababu maalumu ya kufanya hivyo. Petro alipo kiri imani yake kwamba Yesu alikuwa Kristo, maana yake alimwamini Yesu kuwa ni Mwokozi aliye mwokoa na dhambi zake zote.

Kwa nini Yesu aliwaosha
Miguu wanafunzi wake kabla
Ya kusulubiwa kwake?
Kwa sababu alitaka wajue kwamba
Yeye ndiye wokovu hakika.

Kwa nini aliosha miguu ya Petro? Yesu alijua kwamba Petro angelimkana punde mara tatu na angeliendelea kutenda dhambi.
Ikiwa baada ya Yesu kupaa mbinguni, Petro angeliendelea kuwa na dhambi moyoni asingeweza kuungana na Yesu. Lakini Yesu alikua juuu ya udhaifu wa wanafunzi wake wote kila mmoja, na hakupenda dhambi ikae kati yake na wanafunzi wake. Hivyo, alihitaji kuwafundisha ya kwamba uovu wao wote alikwisha usafisha. Hii ndiyo sababu aliwaosha miguu wanafunzi hao. Kabla ya kufa kwake, alitaka kuhakikisha ya kwamba wamesimama imara katika Injili ya ubatizo na pia msamaha kamili wa dhambi za maisha yao yote.
Yohana 13 inazungumzia juu ya wokovu kamili aliotimiza Yesu kwa wanafunzi wake alipokuwa akiwaosha miguu, Yesu aliwaambia juu ya hekima ya Injili ya Ubatizo wake kupitia hivyo watu wote walitakaswa kwa makosa yao yote.
“Usidanganyike na shetani wakati mwingine. Nimekwisha zichukua dhambi zenu zote kwa ubatizo wangu katika mto Yordani na nitabeba hukumu badala yenu msalabani. Na baadaye nitafufuka katika wafu na kutimiza wokovu wa kuzaliwa upya kwenu nyote. Ili kuwafundisha juu ya haya kwamba nimekwisha safisha vile vile hata zile dhambi zenu zijazo, sasa nawaosha miguu kabla ya kusulubiwa. Hii ni siri ya Injili ya kuzaliwa upya. Yawapasa nyote kuamini hili.”
Yatupasa wote kuelewa ni sababu ipi iliyo mfanya Yesu aoshe miguu yya wanafunzi wake na kujua ni kwa nini alisema “Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.” Hii pekee itatuwezesha kuamini juu ya Injili ya kuzaliwa upya na kutufanya sasa kuzaliwa upya maishani mwetu.
 

Yesu alisema katika Yohana 13:12

Ni yapi makosa yetu?
Ni dhambi tutendazo kila siku
Kutokana na udhaifu wetu.

Kabla ya kufa msalabani, Yesu aliandaa karamu ya Pasaka kwa wanafunzi wake na kuwathibitishia juu ya Injili ya ondoleo la dhambi kwa kuwaosha miguu kwa mikono yake.
“Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na yakuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu aliondoka chakulani akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa, lakini utalifahamu baadaye” (Yohana 13:3-7).
Aliwafundisha wanafunzi wake Injili ya ubatizo na msamaha wa dhambi kupitia ubatizo wake.
Kwa muda Petro alipokuwa mwaminifu kwa Yesu hakuweza kuelewa sababu ya Yesu aliye Bwana kumwosha miguu. Na baadaye alipoelewa sababu halisi Yesu kumfanyia haya ghafla alibadilika kwa namna anayomfahamu kuwa yeye ni nani. Yesu alitaka kuwafundisha juu ya ondoleo la dhambi juu ya maji ya ubatizo wake.
Alitia shaka juu ya Petro asingeweza kuja kwake kutokana na dhambi atakazotenda hapo baadaye, kwa maneno mengine dhambi za mwilini zijazo; Yesu aliwaosha miguu ili shetani asipate kuchukua imani ya wanafunzi wake. Baadaye, Petro alikuja kuelewa sababu yake.
Yesu alikuja kutayarisha njia ili kila amwaminiye katika maji ya ubatizo wake na damu yake aweze kukombolewa kwa dhambi zake zote daima.
Katika Yohana 13, maneno aliyokuwa akisema wakati akiwasafisha miguu wanafunzi wake yamewekwa kama kumbukumbu. Ni maneno muhimu ambayo waliozaliwa upya tu wataweza kuyaelewa kiundani.
Sababu ya Yesu kuosha miguu ya wanafunzi wake kabla ya Pasaka ilikuwa ni kusaidia kuelewesha ya kwamba alikisha safisha dhambi zao zote katika maisha yao. Yesu alisema “Nifanyalo wewe hujui sasa, lakini utalifahamu baadaye.” Maneno haya kwa Petro yaliondolea kuwa kweli ya ukombozi wa milele kwake.
Yatupasa kuelewa na kuamini juu ya ubatizo wa Yesu ambao ulitakasa dhambi zetu zote na uovu wake. Ubatizo wa Yesu katika Yordani ilikuwa ni Injili ya kutwisha dhambi kwa kuwekea mikono. Yatupasa pia kuamini maneno ya Yesu alibeba dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake na kukamilisha ondoleo la dhambi kwa kuhukumiwa kifo msalabani. Yesu alibatizwa ili kuwaachanisha watu wote na dhambi zao.
 

Ondoleo la makosa yetu yote ya maishani lilitimizwa kwa ubatizo na kwa damu ya Yesu

Ni upi “mtego” wa shetani
Dhidi ya wenye haki?
Shetani hujaribu kulaghai wenye
Haki ili kuwafanya wawe 
wadhambi tena.

Yesu alikwisha elewa vyema, baada ya kusulubiwa kwake, kufufuka na kupaa mbinguni, shetani na wa wahamasishaji wa imani ya uongo watajitokeza na kujaribu kuwalaghai wanafunzi wake. Tunaweza kuona katika ushuhuda wa Petro “Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai” ya kwamba anamwamini Yesu. Lakini bado Yesu alipenda kumkumbusha Petro kwa mara nyingine kuishika Injili ya ondoleo la dhambi moyoni mwake. Injili hiyo ilikuwa ni ya ubatizo wa Yesu kupitia hiyo alichua dhambi zetu zote ulimwenguni. Alipenda kumkumbusha tena Petro, wanafunzi wengine na hata sisi leo hii. “Nifanyalo wewe hujui sasa lakiniutalifahamu baadaye.”
Kila wanafunzi wa Yesu wanapotenda dhambi shetani hujaribu kuwahukumu kwa kuseama “Tazama ikiwa bado unaendelea na dhambi utasema vipi kuwa huna dhambi? Bado hujaokoka; Bado wewe ni mwenye dhambi tu.” Ili kuzuia aina hiyo ya maambukizo, Yesu aliwaambia kuwa imani yao katika ubatizo wake ilikwisha safisha dhambi zao zote za maishani za kale, wakati uliopo na ujao.
“Nyote mwafahamu nilibatizwa! Sababu ya kubatizwa Yordani ilikuwa ni kusafisha dhambi zenu zote maishani pamoja na ile dhambi ya asili ya mwanadamu. Je, unaweza kuelewa sasa kwa nini nilibatizwa na kwa nini nilisulubiwa na kufa msalabani?” Yesu aliwaosha wanafunzi wake miguu kuwaonyesha yeye alikwisha zichukua dhambi zao zote za kila siku kupitia ubatizo wake na ataichukua hukumu msalabani.
Sasa wewe na mimi tumekombolewa toka dhambi zetuzote kwa imani zetu katika ubatizo wa Yesu na damu yake ambayo imetuwezesha kupokea ondoleo la dhambi zetu zote. Yesu alibatizwa na kusulubiwa kwa ajili yetu. Ametakasa dhambi zetu zote kwa ubatizo na damu na kwa yeyote wenye kuelewa na kuamini katika Injili ya ondoleo la dhambi na wenye kuamini ukombozi wa kweli toka dhambini huokolewa.
Sasa wale waliozaliwa upya yawapasa kufanya nini baada ya kuokolewa? Yawapasa kukiri dhambi zao za kila siku na kuamini katika wokovu wa ubatizo na damu ya Yesu injili ya upatanisho kwa dhambi zote. Injili ya ondoleo la dhambi ndiyo itupasayo sisi wote tuliozaliwa upya tupasayo kuidhihirisha ndani ya mioyo yetuu kwa undani sana.
Ikiwa utatenda dhambi tena, ina maana wewe ni mwenye dhambi? La! Sivyo kwa kujua kwamba Yesu alichukua dhambi zako zote, utaweza vipi tena kuwa mwenye dhambi? Ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ilikuwa injili ya ondoleo la dhambi zote. Kwa yeyote anayeamini katika Injili hii halisi ya ondoleo la dhambi ataweza kuzaliwa upya, bila kikwazo, “kama mwenye haki.”
 

Wenye haki hawawezi kuwa wenye dhambi tena

Kwa nini wenye haki 
hawawezi Kamwe kuwa
wenye dhambi tena?
Kwa sababu Yesu alikwisha 
jitoa kwa Dhambi zao
zote maishani mwao.

Ikiwa utaamini Injili ya ondoleo la dhambi kwa maji na kwa Roho lakini bado unahisi wewe ni mwenye dhambi kwa sababu ya makosa ya kila siku, basi yakupasa uende Yordani alipobatizwa Yesu ili kuondoa dhambi zako zote ikiwa utakuwa ni mwenye dhambi tena baada ya kupokea ondoleo la dhambi ina maana Yesu anapaswa kubatizwa tena. Yakupasa uwe na imani katika ondoleo la dhambi litokanalo na Injili ya ubatizo wa Yesu. Yakupasa uzingatie moyoni kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu zote kwa wakati mmoja na kwa wakati waote wa maisha yetu kwa ubatizo wake. Yakupasa uwe na imani isiyo yumba na kukengeuka kuwa Yesu Kristo, ndiye Mwokozi.
Kumwamini Yesu kama Mwokozi maana yake ni kuamini ubatizo wa Yesu; ambao ulizichukua dhambi zetu zote maishani. Ikiwa kweli utaamini ubatizo wa Yesu msalabani, kifo na ufufuko wake, hakika kamwe huwezi kuwa mwenye dhambi tena, bila kujali aina gani ya dhambi ulitenda. Umekwisha kombolewa kwa dhambi zako zote kwa maisha yako yote kwa Imani.
Yesu Kristo alisafisha hata dhambi zijazo tutakazo tenda kutokana na udhaifu wetu. Kwa kuwa alisisitiza umuhimu wa ubatizo wake, aliwaosha wanafunzi wake miguu kwa maji kuonyesha juu ijili ya msamaha wa dhambi ambao ni ubatizo wake. Yesu Kristo alibatizwa akasulubiwa akafufuka na kupaa mbinguni ili kutimiza ahadi ya Mungu ya upatanisho kamili wa dhambi za ulimwengu na wokovu wa wanadamu kwa matokeo haya wanafunzi wa Yesu waliweza kuhubiri Injili ya upatanisho wa dhambi ubatizo wa Yesu, msalaba na ufufuko mwanzao kabisa hadi mwisho wa maisha yao.
 

Udhaifu wa kimwili wa Petro

Kwa nini Petro alimkana Yesu?
Kwa sababu alikuwa dhaifu.

Biblia inatueleza kwamba Petro alikumbana na Mtumishi wa Kayafa Kuhani Mkuu akimtuhumu kuwa naye pia alikuwa mfuasi ya Yesu, alikana mara mbili kwa kusema “si mimi.” Na ndipo kwa mara ya tatu aliapa kwa hasira kutomtambua Yesu.
Hebu tusoma kifungu toka Mathayo 26:69. “Na Petro alikuwa ameketi nje behewani, kijakazi mmoja akamwendea, akasema wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya. Akakana mbele ya wote akisema sikui usemalo, Naye alipotoka nje hata ukumbini, mwanamke mwingine alimwona akawaambia watu walikuwako huko, huyu alikuwapo pamoja Yesu Mnazareti. Akakana tena kwa kiapo, simjui mtu huyu. Punde kidogo wale waliohudhuria wakamwendea wakamwambia Petro hakika wewe nawe ni mmoja wao; kwa sababu hausemi wako wakutambulisha. Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo. Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilosema kabla ya kuwika jogoo utanikama mara tatu. Akatoka nje; akalia kwa majonzi” (Mathayo 26:69-75).
Ukweli ni kwamba, Petro alikuwa akimwamini Yesu na kuwa mfuasi mwaminifu. Aliamini ya kwamba, Bwana Yesu alikuwa Mwokozi na “nabii ajaye”. Lakini Yesu alipofikishwa mbele ya Mahakama ya Pilato na ikawa hatari kwake kuonyesha uhusiano wake na Yesu kwa mamlaka, alimkana na kumlaani mbele yao.
Petro hakujua kwamba angeweza kumkana Yesu lakini Yesu alifahamu hilo kabla. Alifahamu udhaifu wake kwa undani zaidi. Hivyo, Yesu alisafisha miguu ya Petro kusimika Injili ya wokovu katika ushuhuda wake kama ilivyoandikwa katika Yohana 13, “utatenda dhambi baadaye kwa nyakati zijazo, lakini nimekwisha kutakasa dhambi zako zote za nyakati zijazo.”
Hakika Petro alimkana Yesu alipoona maisha yake yamo hatarini, lakini ilitokana na udhaifu wwa kimwili uliomfanya kutenda hayo. Hivyo kwa Yesu kuweza kuwaokoa wanafunzi wake kwa dhambi zao za nyakati zijazo ilimbidi awasafishe miguu yao kabla.
“Nitaziondoa dhambi zenu zote zijazo pia. Nipo karibu kusulubiwa kwa kuwa nilibatizwa na kuchukua dhambi zenu zote nitalipia zote ili niwe mwokozi wenu wa kweli kwa wote. Mimi ni Mungu wenu, Mwokozi wenu, nitazilipia zote na nitakuwa Mchungaji kwenu kwa ubatizo wangu na damu yangu. Mimi ndiye Mchungaji wa wokovu wenu.”
Ili kupandikiza imani hii mioyoni, Yesu aliwaosha miguu baada ya karama ya Pasaka. Hii ndiyo Injili iliyo kweli na hakika.
Kwa kuwa kimwili tu dhaifu hata baada ya kuzaliwa upya tutaendelea kutenda dhambi. Hata hivyo hatupaswi kutenda dhambi, lakini tunapokutana na matukio ya kutisha kama Petro, tunajikuta bila kutarajia tukianguka. Tunaishi katika mwili, hivyo nyakati nyingine tunapelekwa kati kwa kuangamizwa na dhambi zetu. Mwili utaendelea kutenda dhambi ikiwa tutaendelea kuishi katika mazingira ya ulimwengu huu, lakini Yesu amekwisha ondoa dhambi zote kwa ubatizo na damu yake msalabani.
Hatuwezi kumkana Yesu kuwa ni Mwokozi wetu, lakini tunapo ishi katika mwili, bado tutaendelea kutenda dhambi kinyume na mapenzi ya Mungu. Ni kwa sababu tumezaliwa na mwili.
Yesu alijua yote haya, alipoishi katika mwili, hivyo akawa Mwokozi wetu kwa kulipia dhambi zetu zote kwa ubatizo na damu yake. Amezifuta dhambi za wale sote wenye kuamini wokovu na ufufuo wake.
Na ndiyo maana Injili zote nne huanzia na ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji. Lengo la maisha ya ubinadamu wake lilikuwa ni kutimiza Injili ya kuzaliwa upya, Injili ya wokovu.

Ni mpaka lini tutaendelea
Kutenda dhambi katika mwili?
Tutaendelea hivyo mpaka
Mwisho wa maisha yetu.

Petro alipomkana si mara moja wala mbili, bali mara tatu kabla ya kuwika jogoo, ni kwa maana gani iliumiza moyo wake! Alijisikia aibu namna gani? Alikwisha apa mbele za Yesu ya kwamba hatomkana. Alitenda dhambi kwa sababu ya udhaifu wa mwili lakini ni kwa kiasi gani alifedheheka moyoni alipodhoofika katika udhaifu na kumkana Yesu si tu mara moja bali mara tatu? Ni fedheha ya namna gani aliyo isikia Yesu alipomwangalia kwa huruma tena?
Lakini Yesu alikwisha yajua yote hayo na zaidi Hivyo alisema “Najua utaendelea kutenda tena na tena. Lakini nimekwisha kuzichukua dhambi zako zote katika ubatizo wangu, usikubali dhambi zako zikukwaze na kuwa tenda mwenye dhambi, usije shindwa kurudi kwangu. Nimekuwa mwokozi wako kikamilifu kwa kubatizwa kwangu na kuhukumiwa kwa dhambi zako zote. Nimekuwa Mungu wako, Mchungaji wako. Amini Injili ya ondoleo la dhambi zako. Nitaendelea kukupenda ingawa utaendelea kutenda dhambi katika mwili nilikwisha kutakasa kwa makosa yako yote. Injili ya ondoleo la dhambi linatenda kazi milele. Upendo wangu kwako na wa milele.”
Yesu alimwambia Petro na wanafunzi “kama nisipo kutawadha huna shirika nami.” Sababu ya kuongea Injili hii katika Yohana 13 ilikuwa ni muhimu kwa watu kuzaliwa upya katika maji na kwa Roho. Je, unaamini hili?
Katika mstari 9 “Simon Petro akamwambia Bwana si miguu yangu tu hata na mikono yangu na kichwa changu pia, Yesu akamwambia yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote.”
Ndugu wapendwa je, utaweza kuja tenda tena “dhambi za mwili” tena au hapana? Hakika utaendelea kutenda. Lakini Yesu alisema kwamba alikwisha kutakasa hata zile dhambi za nyakati zijazo katika maisha yako duniani makosa yote ya mwili kwa ubatizo wake na kwa damu yake na kukufanya kuwa safi kupitia maneno aliyowaeleza mitume wake yaliyo ya kweli, Injili ya upatanisho kabla ya kusulubiwa.
Kwa kuwa tunaishi katika mwili ulio na udhaifu wa aina zote, hatuwezi kujizuia kutenda dhambi. Yesu alitakasa dhambi za ulimwengu wote kwa ubatizo wake. Hakusafisha vichwa vyetu tu na miili yetu, bali pia miguu yetu yaani dhambi zetu zijazo maishani. Hii ni Injili ya kuzaliwa upya, ubatizo wa Yesu.
Baada ya Yesu kubatizwa, Yohana Mbatizaji alishuhudia “Tazama, huyu ndiye mwanakondoo wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu!” (Yohana 1:29) Inatubidi kuamini kwamba dhambi zote za ulimwengu zilitakaswa kwa kutwikwa Yesu wakati wa ubatizo wake.
Tunapoishi katika ulimwengu huu wenye uovu, hatuwezi kujizuia kutenda dhambi. Huu ni ukweli usiofichika. Inapotokea udhaifu wa miili yetu, yatupasa kujikumbusha kwamba Yesu alikwisha tutakasa kwa dhambi zetu zote ulimwenguni kupitia Injili ya ondoleo na malipo kwa damu yake. Yatupasa kutoa shukrani kwake toka moyoni mwetu. Hebu na tukiri kwa imani kwamba Yesu ni Mwokozi na Mungu wetu. Bwana asifiwe!
Kila mmoja ulimwenguni hawezi kujizuia kutotenda dhambi mwilini watu wataendelea kutenda dhambi katika miili yao na kufa kwa dhambi hizo.
 

Mawazo ya Uovu ndani ya mioyo ya Watu

Nini kimtiacho najisi mtu?
Dhambi za aina mbalimbali
Na mawazo ya uovu.

Yesu anasema katika Mathayo 15:19-20. “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wivu, ushuhuda wa uongo na matukano hayo ndiyo yamtia ya mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.” Kwa sababu ya aina za dhambi mbaya ya mioyo ya watu huwatia najisi na kuwafanya wasiwe safi.
 

Yampasa mtu kugundua asili ya uovu wake

Nini kulichopo ndani
Ya moyo wa kila mtu?
Aina kumi na mbili za Dhambi 
(Marko 7:21-23).

Yatupasa kuwa na uwezo wa kusema “Hizo aina kumi na mbili za dhambi zimo ndani ya moyo wa kila mwanadamu. Mimi ninazo zote ndani ya moyo wangu. Ninazo aina kumi na mbili za dhambi ndani yangu zilizo ainishwa katika biblia.” Kabla ya kuzaliwa upya katika maji na Roho, yatupasa kukiri kwamba dhambi asili yake ni mioyoni. Yatupasa kukubali sisi ni wenye dhambi kabisa mbeli ya Mungu, lakini mara nyingi hatufanyi hilo. Wengi wetu hujikosha kwa kusema “sikuwa na mawazo haya moyoni, nilijikuta tu nikitumbukizwa bila kupenda.”
Lakini Yesu alisema nini juu ya wanadamu? Kwa ufasaha alisema kile kinachotoka moyoni mwa mwanadamu ndicho “kimtiacho najisi” yeye. Alitueleza kwamba watu wamejawa na mawazo maovu ndani yao. Unafikiri nini? Wewe ni muovu au mwema? Je, unajua kwamba kila mtu anayo mawazo ya uovu? Ndiyo kila mtu anayo!
Miaka michache iliyopita hapa Seoul, palikuwa na ajali ya kuanguka kwa jingo la maduka Familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao ziliingia katika kipindi kigumu cha majonzi na machungu, lakini watu wengi walikimbilia kwenda kushuhudia jambo hili likiwa kama ni tukio la kupendeza machoni pao.
Wengine walisema mioyoni mwao “wangapi wamekufa? 200? Ah! Kumbe wachache tu! 300? Labda? Ingukuwa jambo la ajabu na la kushangaza kama wangekufa kama elfu moja hivi…” Hii ndiyo mioyo ya watu inavyo ongea kwa ndani uovu wake. Inatubidi tukubali haya ni heshima mbaya kwa walio adhirika na jambo hili. Ni kwa namna gani jambo hili limekuwa la kukatisha tamaa kwa ndugu wafiwa! Wengine walipoteza fedha na mali.
Wapita njia wengi hawakusikitika “ingekuwa labda watu wengi wamekufa ingekuwa jambo la kushangaza, lakini hawa tu. Ah! Wachache. Inashangaza! Ni vipi kama ingekuwa uwanja wa mpira? Maelfu wengelifunikwa na vifusi? Ah, ndiyo, labda ingekuwa tukio la kwanza kutokea!” Inawezekana wengi waliwaza namna hii mioyoni. Mawazo kama haya yanaweza kusikika katika ajali ya gari. Wakereketwa wenye kupenda mambo ya ajali ya gari. Wakereketwa wenye kupenda mambo ya ajali husikika wakisikitika kwamba ilikuwa ni ajali ndogo tu.
Wote tunafahamu ni kwa namna gani tulivyo waovu wakati mwingine. Tunaweza kutoa kauli zetu na kuelezea masikitiko yetu tunapo ona ajali, lakini kwa siri mioyoni mwetu tunapenda kuona kama ni jambo la kuburudisha. Tunapenda kuona majanga makubwa ya ajali ambapo maelfu ya watu wamepoteza maisha yao, ili mradi haiendani kinyume na mapenzi yetu. Hii ndiyo namna ya mioyo yetu inavyofanya kazi. Wengi wetu tulikuwa namna hii hapo mwanzo.
 

Mauaji ndani ya kila moyo wa Mwanadamu

Kwa nini tunatenda Dhambi?
Ni kwa sababu tunayo mawazo
Ya uovu ndani ya mioyo yetu.

Mungu ametuambia ya kwamba ipo dhambi ya mauaji ndani ya kila moyo wa mwanadamu. Lakini wengi watakataa hili mbele ya Mungu “utasema vipi hivyo! Unawezaje kunifananisha na mtu wa aina hivyo! Unawezaje kunifananisha na mtu wa aina hiyo!” Iliwapasa kukubali juu ya hili mioyoni mwao. Wao hufikiri anayefanya mauaji ni wa kizazi kingine tufauti yao. 
“Yule muuaji katika habari siku zile, aliyewaua watu wengi kwa kuwachoma katika chumba cha chini ni yule mtu aliye na dhambi ya mauaji moyoni mwake! Yule ni kizazi kingine! Siwezi kuwa kama yeye! Sithubutu kama yeye! Muuaji!” Wanakuwa wageni katika uhalifu na kupiga kelele “wale waliozaliwa na mbegu ya uovu walipaswa kufutwa kabisa juu ya uso wa dunia! Walipaswa kuhukumiwa kifo!”
Lakini kwa bahati mbaya mawazo ya kuua yamo ndani ya mioyo ya wale wenye hasira, navile vile katika mioyo ya wale wanye matukio ya mauaji ya mfululizo na wenye kuua katika tukio moja. Mungu anatuambia yakwamba ndani ya mioyo ya watu, yapo mawazo ya uuaji. Yatupasa kukubaliana na Neno la Mungu ambaye yeye aweza kuyaona mambo yaliyo fichika ndani ya fikara zetu. Kwahilo, yatubidi tukubali kwa kusema “Mimi ni mwenye dhambi niliye na mawazo ya uuaji ndani ya moyo”.
Ndiyo, Mungu ametueleza ya kwamba yapo mawazo ya uovu ndani mioyoni mwetu, ikiwa ni pamoja na uuaji ndani ya kila mwanadamu. Hebu basi na tulikubali neno la Mungu. Kwajinsi kizazi hiki cha wanadamu kinavyo zidi kuwa kiovu, kila aina ya vifaa vya kujilinda vinazidi kuwa ni nyenzo za kuua. Hii ni matokeo ya uuaji nadani ya mioyo yetu. Waweza kuua katika kiwango cha hasira au woga. Sisemi ya kwamba kila mmoja wetu ataweza kuua katika maana halisi ya tendo la kuua, bali tunafikra hizi hata ndani ya mioyo yetu.
Tumezaliwa tukiwa na mioyo yenye uovu mioyoni mwetu. Wengine hutenda kabisa na kuua, si kwa sababu wamezaliwa mahususi kuwa wauaji, bali kwa sababu sisi sote tuna uwezo wa kuwa wauaji mioyoni mwetu. Hii ni kweli. Hakuna awezaye kukwepa ukweli huu.
Hivyo, njia sahihi yetu ya kuchukulia jambo hili ni kulikubali neno la Mungu na kulitii. Tunatenda dhambi hapa ulimwenguni kwa sababu tuna mawazo yaliyo maovu ndani ya mioyo yetu.
 

Uzinzi ndani ya mioyo yetu

Mungu anasema kwamba upo uzinzi ndani ya kila moyo wa mtu. Je, unaamini hilo? Je, unakubali kwamba wewe una uzinzi moyoni mwako? Ndiyo, upo uzinzi katika kila moyo wa mwanadamu.
Na hii ndiyo maana ukahaba na uhalifu unao andamana na matendo ya ngono umestawi katika jamii zetu. Ni njia mojawapo ya hakika katika kujitengenezea kipato kirahisi katika kila vipindi vya historia ya mwanadamu Biashara nyingine mathalani zaweza kutetereka kiuchumi, lakini aina hii za biashara kamwe hazianguki kirahisi kwa sababu uzinzi bado unadumu na kuweka makazi ndani ya mioyo ya kila mtu.
 

Tunda la Mwenye kutenda dhambi ni Dhambi

Mwanadamu anaweza
Kufananishwa na nini?
Mwanadamu ni mfano wa mti
Utoao matunda ya dhambi.

Kama ulivyo mti wa mtufaha utoao matunda ya tufaha, mti wa mtende utoao tende, mti wa mzabibu utoao zabibu, sisi tuliozaliwa na aina 12 za dhambi mioyoni mwetu, hatuwezi kujizuia bila kutoa matunda ya dhambi hizi.
Yesu alisema kile kinacho toka moyoni mwa mtu ndicho kimtiacho najisi. Unaamini? Tunaweza kukubali kwa maneno tu haya “Ndiyo, sisi ni kizazi cha dhambi waovu. Hakika ni kweli Bwana.” Ndiyo, yatupasa kukubali uovu wetu. Yatupasa kukubali ukweli mbele za Mungu.
Kama ilivyo kwake Yesu Kristo alipotii mapenzi ya Mungu; yatupasa pia uasi kulikubali neno la Mungu na kulitii. Hii ndiyo njia pekee tutaweza kuokolewa toka dhambini kwa kupitia maji na Roho. Hii ndiyo zawadi toka kwa Mungu.
Nchini mwangu tumebarikiwa kwa aina nne za misimu. Misimu hii inapo kuwepo, aina mbalimbali za miti huzaa matunda. Kwa mfano huu dhambi 12 ndani ya mioyo yetu zimeshikana ndani yetu hivyo kendelea kutuongoza kutenda dhambi. Hii leo yaweza kuwa tumetingwa na dhambi ya uuaji mioyoni mwetu na kesho yaweza kuwa uzinzi.
Baadaye, siku inayofuata, mawazo ya uovu, baadaye tamaa mbaya, wizi, ushuhuda wa uongo…na kadhalika. Tunaendelea kutenda dhambi mwaka hadi mwaka, kila mwezi, kila siku, kila saa. Hakuna siku isiyopita bila kutenda dhambi ya aina Fulani. Tunaendelea kujilaumu na kuahidi kutorudia lakini hatuwezi kwa sababu tumezaliwa hivyo.
Je, umewahi kuona mti wa tufaha kukataa kubeba tunda la tufaha kwa sababu tu haupendi? “sipendi kubeba tunda la tufaha!” Hata ikiwa mti umeghairi na kukubali bado utabeba tunda lake bila pingamizi kipindi cha masika, na tunda litakuwa tayari kuliwa wakati wa kiangazi.
Hii ni matokeo ya asili, na maisha ya mwenye dhambi vile vile huwa kama hivi. Wenyedhambi hawawezi kujizuia kubeba matunda ya dhambi maishani mwao.
 

“Ubatizo na msalaba wa Yesu” ulikuwa ni kwa ajili ya upatanisho wa wenye dhambi

Nini maana ya upatanisho
wa Yesu?
Ni malipo ya mshahara wa dhambi
kwa ubatizo wake (kuwekewa mikono)
na kumwaga damu 
yake msalabani.

Hebu na tusome kifungu hiki katika Biblia ili tuone ni kwa namna gani wenye dhambi, kizazi cha uovu wameweza kupatanishwa kwa dhambi zao mbele ya Mungu na kupata maisha ya furaha. Hii ni Injili ya upatanisho wa dhambi.
Katika Walawi 4, inasema “Na mtu awaye yote katika watu wa nchi akifanya dhambi pasipo kusudia kwa kufanya neno lolote katika hayo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe naye akapata hatia akijulishwa hiyo dhambi yake aliyofanya, ndipo atakapoleta mbuzi mke mkamilifu, awe matoleo yake kwa ajili ya dhambi yake aliyofanya naye ataweka mkono wake kichwani mwake hiyo sadaka ya dhambi na kumchinja sadaka ya dhambi, mahali hapo pa sadaka ya kuteketezwa kasha kuhani atatwaa katika hiyo damu yake kwa kidole chake na kuitia katika pembe za madhabahu ya kuteketeza na damu yake yote ataimwaga chini ya madhabahu. Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani kasha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu iwe harufu ya kupendeza kwa Bwana na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake naye atasamehewa” (mambo ya Walawi 4:27-31).
Katika kipindi cha Agano la kale, watu walipatanushwa vipi kwa dhambi zao? Waliwekea mikono yao juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi ambayo ni mbuzi, na kumtwisha mbuzi huyo dhambi zao zote.
Imeandikwa katika Walawi pia “Nena na Wana wa Israeli, uwaambie, mtu wa kwenu atakapomtolea Bwana matoleo, mtatoa matoleo yenu katika wanyama wa mifugo, katika ng’ombe na katika kondoo. Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng’ombe, atatoa ng’ombe mume mkamilifu, ataleta mlangoni pa hema ya kukutania ili akubaliwe mbele ya Bwana kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake” (Walawi 1:2-4).
Mtu wa kipindi hicho anapogundua dhambi ndani ya moyo wake, ilimpasa kutayarisha sadaka ya dhambi ambayo itatumika katika kumpatanisha kwa dhambi. Ilimpasa “kumwekea mikono” juu ya kichwa cha yule mnyama wa sadaka ili kumtwisha dhambi alizotenda ndani ya ukumbi wa hekalu takatifu, palikuwa na altare ya kuteketezea dhabihu. Lilikuwa ni sanduku la muundo wake, kubwa kiasi zaidi ya meza ya madhabahu, na katika kila kingo zake palisimikwa pembe. Watu wa Israeli walipatanishwa kwa dhambi zao kwa kuwekea mikono juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi na nyama yake kuchomwa juu ya altare ya kutekelezea sadaka.
Mungu aliwaambia watu katika kitabu cha Walawi “ataleta mlangoni pa hema ya kukutania ili akubaliwe mbele ya Bwana.” Dhambi zao zilitwikwa kwa yule mnyama wa sadaka walipo mwekea mikono kichwani, na wenye dhambi walichinja koo lake na kumtoa damu yake kwa kuimimina katika zile pembe nne katika kingo za altare ya kutekeleza kwa moto.
Baada ya hapo, mwili wa sadaka hiyo ulitolewa kwa kusafisha viungo vya ndani na nyama yake ilikatwa vipande na kuchomwa hadi majivu juu ya altare hiyo. Na ndipo harufu ya kupendeza ya nyama ile itatolewa kwa Mungu kwa ajili ya upatanisho wao naye. Hivi ndivyo walivyopatanishwa kwa dhambi za kila siku.
Mungu aliruhusu pia sadaka ya upatanisho kwa dhambi za mwaka. Hii ilikuwa na tofauti na ile ya dhambi za siku. Kwa hili, Kuhani Mkuu ndiye pekee aliyeruhusiwa kuwekea mikono sadaka ya dhambi kwa niaba ya watu wa Israeli na kunyunyizia damu upande ule wa Mashariki wa kiti cha Rehema mara saba. Pia kuwekea mikono juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai kulifanyika mbele ya watu wote wa Israeli katika siku ya kumi ya mwezi wa saba kila mwaka (Walawi 16:5-27).

Nani ni mfano wa
Sadaka ya dhambi
Katika Agano la Kale?
Yesu Kristo

Hebu sasa na tuangalie mfumo wa matoleo au kafara ulivyobadilika katika Agano Jipya na kwa vipi hadhi ya umilele wa Mungu ilivyobaki kwa miaka yoote hii bila kubadilika.
Kwa nini Yesu ilimbidi afe msalabani? Alikosa nini ulimwenguni hapa hadi Mungu kuruhusu afe msalabani? Ni nani aliye mshurutisha afe kifo hicho? Wakati wenye wote ulimwenguni, yaani sisi wote, tulipoanguka dhambini Yesu alikuja duniani kutuokoa.
Alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani na kubeba hukumu msalabani kwa dhambi zetu zote na kwa niaba yetu wote sisi wanadamu. Kwa njia aliyobatizwa na kwa njia ile pia iliyotoa damu yake msalabani inafanana na sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale, kuwekea mikono sadaka ya dhambi na kutoa damu yake.
Hii ndiyo njia iliyofanyika katika Agano la Kale. Mwenye dhambi aliweka mikono juu ya sadaka ya dhambi na kutaja dhambi zake, kwa kusema “Bwana, nimetenda dhambi. Nimeua na kuzini.” Na ndipo dhambi hizo zinapotwikwa sadaka hiyo ya dhambi.
Kama ilivyo mwenye dhambi hiyo anapo mchinja koo sadaka yule wa dhambi na kumtolea kwa Mungu, Yesu alitolewa kwa namna hii ili kutupatanisha sisi sote kwa dhambi zetu. Yesu alibatizwa na kutoa damu yake pale msalabani ili kutuokoa na kutupatanisha kwa dhambi zetu zote kwa kujitoa kwake.
Ukweli ni kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu. Tunapofikiri hili, ilikuwa na maana gani juu ya matoleo ya wanyama hawa, wasio na doa kama kafara za dhambi zetu zote za watu? Je, wanyama hawa wote walikuwa wanaelewa nini maana ya dhambi? Hawajui juu ya dhambi. Walitolewa pasipo kuwa na doa.
Kama ilivyo kwa wanyama hao wasivyo na doa, ndivyo ilivyo pia kwa Yesu asiye na dhambi. Ni Mungu Mtakatifu, Mwana wa Mungu na hakutenda dhambi. Hivyo, alibeba dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake katika Mto Yordani katika umri wa miaka 30.
Yesu alikufa msalabani kwa sababu ya dhambi alizo beba kwa niaba yetu. Ilikuwa ni huduma yake ya wokovu katika kutakasa dhambi za wanadamu.
 

Mwanzo wa Injili ya Upatanisho wa dhambi

Kwa nini Yesu alibatizwa na
Yohana Mbatizaji Mto Yordani?
Kutimiza haki zote.

Imeandikwa katika Mathayo 3, “Wakati huyo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akakubali” (Mathayo 3:13-15).
Yatupasa kujua na kuelewa sababu ya ubatizo wa Yesu katika umri wa miaka 30. alibatizwa ili kutupatanisha kwa dhambi zetu zote na kutimiza haki zote za Mungu. Kuokoa watu wote kwa dhambi zao, Yesu Kristo, Yeye yule asiye na doa alibatizwa na Yohana Mbatizaji. 
Hivi ndivyo Yesu alivyochukua dhambi za ulimwengu na kujitoa nafsi yake ili kupatanisha wanadamu wote ili uweze kuokolewa toka dhambini, yatupasa kujua kweli yote na kuiamini. Ni hiyari yetu kuamini wokovu wa Yesu na kuokolewa.
Ubatizo wa Yesu una maana gani? Ni sawa na kuwekea mikono katika Agano la Kale. Katika kipindi hicho, dhambi za watu wote zilibebeshwa kichwani pa yule mnyama wa sadaka ya dhambi na Kuhani Mkuu ndiye aliyewekea mikono. Kwa mfano huo, katika Agano Jipya, Yesu alizichukua dhambi za ulimwengu kwa kujiweka yeye kuwa sadaka ya dhambi kwa kubatizwa na Yohana.
Yohana Mbatizaji alikuwa ni mkuu kati ya wanadamu wote kwa kuwa mwakilishi aliyeteuliwa na Mungu. Akiwa mwakilishi wa wanadamu, Kuhani Mkuu wa wanadamu aliweka mikono juu ya kichwa cha Yesu na kumtwisha dhambi zote za ulimwengu kwake. “Ubatizo” humaanisha “kutwika, kuzikwa na kutakaswa.”
Je, unajua ni kwa nini Yesu alikuja ulimwenguni na alibatizwa na Yohana Mbatizaji? Je unaamini katika Yesu kwa kuelewa maana ya ubatizo wake? Ubatizo wa Yesu ulikuwa ni wa kuzichukua dhambi zetu zote; sisi uzao wa uovu, tulizo tenda kwa miili yetu kwa maisha yetu yote. Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu ili kuitimiza ile Injili halisi ya ondoleo la dhambi zetu zote.
Katika Mathayo 3:13-17 inaanza na maneno “Wakati huo,” na kuonyesha muda Yesu alipobatizwa, ndiyo wakati dhambi za ulimwengu zilipotwikwa juu yake.
“Wakati huo” Yesu alizibeba dhambi zote za wanadamu kufa msalabani baada ya miaka mitatu na alifufuka siku ya tatu. Ili kutakasa ulimwengu kwa ajili ya wote, alikufa mara moja na kwa wote. Alikufa mara moja kwa wote na alifufuka kutoka kifoni mara moja kwa wote. Kwa wale wenye kuhitaji kukombolewa kwa dhambi zao mbele ya Mungu, Yesu alikwisha chukua dhambi za ulimwengu na kutuokoa mara moja na kwa wote.
Kwa nini Yesu ilipaswa kubatizwa? Kwa nini ilimpasa kuvaa taji la miiba na kuhukumiwa mbele ya mahakama ya Pilato kama mhalifu wa kawaida? Kwa nini alihukumiwa msalabani kwa kutoka damu hadi kufa? Sababu ya hayo yote hapo juu ni kwamba, alizibeba dhambi zote za ulimwengu, zangu na zako, katika ubatizo wake. Kwa dhambi zetu ilimpasa afe msalabani.
Yatupasa kuamini neno la msalaba ambalo Mungu ametuokoa na kushukuru yeye. Bila ya Ubatizo wa Yesu, Msalaba wake, na ufufuo wake hakika pasingekuwepo na wokovu wetu.
Yesu alipobatizwa na Yohana ili kubeba dhambi za ulimwengu, alizibeba dhambi hizo na hivyo kutuokoa sisi wale tu wenye kuamini Injili ya wokovu. Wapo watu wenye kufikiri kwamba “Yesu alizichukua dhambi zile za asili tu.” Hakika watu wa aina hii wamepotoka kwa aina hii ya imani katika mafundisho ya aina hii.
Imeandikwa kwa uwazi kabisa ndani ya Biblia kwamba Yesu alizibeba dhambi zote za ulimwengu mara moja na zote pale alipobatizwa dhambi zetu zote, ikiwa zile za asili nazo, zimetakaswa kabisa. Yesu anasema katika Mathayo 3:15 “kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki zote.” Kutimiza haki zote maana yake, dhambi zote pasipo kuchagua ziliondolewa kwetu sisi sote.
Je, Yesu ametakasa dhambi zote katika maisha yetu, pia? Ndiyo ametakasa. Hebu na tuone uthibitisho wa maandiko katika kitabu cha Walawi kwanza. Inatueleza juu ya Kuhani Mkuu na sadaka ya Siku ya Upatanisho.
 

Sadaka ya Upatanisho wa dhambi za mwaka mzima za Waisraeli wote

Je, Waisraeli waliweza 
kutakaswa Mara moja na kwa wakati 
wote Kwa sadaka ya dhambi 
itolewayo Duniani?
Kamwe.

“Na Haruni atamtoa yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi aliye kwa ajili ya nafsi yake na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake kisha atatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za Bwana mlangoni pa hema ya kukutania. Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili, kura moja kwa ajili ya Bwana, na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli. Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Bwana, na kumtoa awe sadaka ya dhambi Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za Bwana ili kunganyia upatanisho, ili kumpelekea jangwani kwa ajili ya Azazeli” (Walawi 16:6–10). Hapo Haruni alichukuwa mbuzi wawili mbele ya lango la hema la kukutania kwa matoleo ya dhambi za mwaka za Israeli.
“Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili, kura moja kwa ajili ya Bwana na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli.”
Mnyama wa Sadaka alihitajiwa kwa sheria ya ondoleo la dhambi za kila siku ili kumtwika dhambi za wenye dhambi kwa kuwekewa mikono juu ya kichwa chake. Lakini kwa dhambi za mwaka za Waisraeli, Kuhani Mkuu kwa niaba ya watu wote, alitwika dhambi za mwaka juu ya sadaka ya dhambi katika siku ya kumi ya mwezi wa saba kwa kila mwaka.
Katika Walawi 16:29-31 imeandikwa “Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba siku ya kumi ya mwezi, mtajitaabisha roho zenu msifanye kazi ya namna yoyote, mzalia na mgeni akaaye kati yenu, kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa, nanyi mtatakaswa na dhambi zetu zote mbele za Bwana Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele” (Walawi 16:29-31).
Katika Agano la Kale, watu wa Israeli walileta sadaka ya dhambi ili kupatanishwa na dhambi za kila siku na kumtwisha dhambi hizo juu ya kichwa chake kwa kuungama “Bwana nimetenda dhambi kadhaa….kadhaa…. Nakusihi unisamehe.” Baadaye ata mchinja koo mnyama yule na kumpa Kuhani damu yake, na kwenda nyumbani akiwa na imani kwamba alikuwa huru kwa dhambi katika yote haya, sadaka ile ya dhambi hufa kwa niaba ya mwenye dhambi aliye itoa ikiwa na dhambi zake juu yake. Mnyama huyu wa kafara alitolewa kufa kwa niaba ya mwenye dhambi. Katika Agano la Kale sadaka ya dhambi aliweza kuwa mbuzi dume, ndama dume au ng’ombe dume, na hao walikuwa ni wanyama wa kafara ambao Mungu aliwatofautisha.
Mungu kwa rehema yake isiyo na mwisho, aliruhusu maisha ya wanyama hawa kutolewa kafara kwa niaba ya wenye dhambi ili wafe kwa niaba yao.
Kwa jinsi hii katika Agano la Kale, wale wenye dhambi waliweza kupatanishwa kwa dhambi zao kupitia sadaka ya upatanisho. Makosa ya wenye dhambi waliweza kupatanishwa kwa dhambi zao kupitia sadaka ile ya dhambi kwa kuwekewa mikono, na damu yake alipelekwa Kuhani ili kuzifuta dhambi zao.
Ingawa hivyo; ilikuwa si rahisi kupatanishwa kwa dhambi za kila siku. Na matokeo yake, Mungu aliruhusu Kuhani Mkuu kufuta dhambi za mwaka mzima katika kila siku ya kumi ya kila mwezi wa saba katika mwaka kwa niaba ya watu wa Israeli.
Hivyo nini ilikuwa nafasi ya Kuhani Mkuu katika siku ya upatanisho? Kwanza, Aruni, Kuhani Mkuu aliweka mikono juu ya kichwa cha yule sadaka wa dhambi, kutubu dhambi za watu wote, “Bwana, watu wa Israeli wametenda dhambi kadhaa wa kadhaa, waliua, walizini, walifanya uasherati, wizi, walishuhudia uongo, walikufuru…”
Na ndipo humchinja koo mnyama yule, kuchukua damu yeke na kunyunyizia mara saba katika kiti cha rehema ndani ya Madhabahu takatifu (Kibiblia namba 7 huchukuliwa kama namba kamili.)
Ilikuwa ni kazi yake kila mwaka kufanya yote haya katika kutoa sadaka ya upatanisho ya dhambi za mwaka.
Kwa sababu Mungu ni mwenye haki, katika kuwaokoa watu wote kwa dhambi zao, iliruhusu sadaka hii ya dhambi kufa kwa niaba ya watu kwa kuwa yeye ni mwingi wa rehema, aliruhusu watu kuyatoa maisha ya wanyama hawa wa sadaka kwa niaba yao. Kuhani Mkuu alinyunyizia damu yake mnyama hiyo upande wa mashariki ya kiti cha rehema na kwa haya yote msamaha ulitolewa kwa watu wote katika siku ya upatanisho kwa siku ile ya kumi katika mwezi wa saba.

Ni nani mwanakondoo wa
Sadaka kulingana na Agano
la kale?
Yesu asiye na doa.

Kuhani Mkuu alitoa mbuzi wawili katika siku ile ya upatanisho kwa ajili ya watu wa Israel. Mmoja wao aliitwa Azazeli; maana yake “kutoa” Na kwa njia hiyo, Azazeli wa Agano la Jipya ni Yesu. “Kwa maana hii jinsi Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwana wake wa pekee ili kila yule amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).
Mungu ametupa Mwana wake kama mwana kondoo wa sadaka. Akiwa kama mwanakondoo wa sadaka kwa wanadamu wote, alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kuwa Mwokozi, Masia wa dunia. Yesu maana yake “Mwokozi” na Kristo “Mfalme aliyepakwa mafuta.” Hivyo Yesu Kristo maana yake “Mwana wa Mungu alikuja kutuokoa sisi sote.”
Kama ilivyo dhambi zote za watu wote katika mwaka mzima zilivyo futwa katika siku ile ya Upatanisho katika Agano la Kale, Yesu Kristo katika miaka 2000 iliyopita, alikuja duniani ili kubatizwa na kutoa damu yake kwa kifo cha msalabani ili kikamilishe Injili ya ondoleo la dhambi zetu.
Katika jambo hili, hebu na tusoma kifungu katika Walawi. “Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi kasha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote mpaka nchi isiyo watu naye atamwacha mbuzi jangwani” (Walawi 16:21-22).
Imeandikwa ya kwamba dhambi za Waisraeli wote zili twikwa juu ya kichwa cha mbuzi kama ilivyo katika Walawi 1. “uovu wao wote” inamaana dhambi zote zilizo tendwa ndani ya mioyo yao na kwa miili yao. Na “uovu wao wote” ulitwikwa juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi kwa kuwekewa mikono na Kuhani Mkuu.
 

Kwa sheria ya Mungu, yatupasa kuwa na ufahamu wa kweli wa Dhambi zetu zote
 
Kwa nini Mungu 
Alitupatia sheria?
Ili tuweze kuzifahamu
Dhambi zetu.
 
Sheria ya Mungu imeundwa kwa vipengele 613 vya amri. Ukweli na kwamba, tunapo waza juu yake, tunafanya vile anavyosema juu ya sheria za kufanya na kutofanya anachohitaji tufanye.
Hivyo, sisi ni wenye dhambi. Imeandikwa katika Biblia kwamba Mungu alitupa sheria hizo ili tuweze kuzitambua dhambi zetu (Warumi 3:20). Hii ina maana kwamba alitupa sheria zake na amri ili kutufundisha sisi wenye dhambi. Hakutupa kwa sababu tungeweza kuzifuata bali ili tuweze kutambua dhambi zetu.
Hakutupa ili tuzifuate. Huwezi kutegemea mbwa kuishi kama mwanadamu. Kwa njia hiyo pia hatuwezi kuishi kwa kufuata sheria ya Mungu, bali tutaweza kupitia sheria hizo kugundua dhambi zetu kupitia amri zake.
Mungu alitupa kwa kuwa tuna wingi wa dhambi ingawa mara nyingi hatugundui hili. “Wewe ni muuaji, mzinzi, mtenda maovu.” Mungu hutuambia kwa namna hii kupitia kwa kuzingatia amri za sheria yake. Anatuambia tusiwe, lakini bila kizuizi tunaua ndani ya mioyo yetu na wakati mwingine kwa matendo kimwili.
Hata hivyo, kwa kuwa imeandikwa katika Sheria ya kwamba tusiwe, tunajua ya kwamba ni wauaji kwa kusema “Ah, nilikosea tu! Mimi ni mwenyedhambi kwa kuwa nimefanya nisicho takiwa kufanya. Nimetenda dhambi.”
Ili kuokoa watu wa Israeli kwa dhambi zao Mungu aliruhusu Haruni kutoa sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale na ilikuwa ni yeye pekee aliye patanisha watu kwa dhambi za kila mwaka mara moja.
Katika Agano la Kale, sadaka za dhambi zilihitajika kutolewa kwa Mungu katika siku ya upatanisho. Moja ilitolewa mbele za Mungu wakati ile nyingine ilitumwa jangwani baada ya kuwekwa mikono kwa kubeba dhambi zote za mwaka mzima za watu wote. Kabla ya mbuzi huyo kupelekwa jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari, Kuhani Mkuu aliweka mikono juu ya kichwa cha mbuzi huyo akiwa hai na kutaja dhambi kwa kutubu.
Nchi ya Palestina ni jangwa. “Azazeli” ndiko walipo pelekwa huko, jangwa lisilo na mwisho na kutangatanga hadi kufa. Wakati azazeli akipelekwa jangwani, watu wa Israeli husimama na kushuhudia hadi kutokomea mbali, na hivyo kuamini kwamba dhambi zao zimetokomea na azazeli huyo. Na ndipo watu wanapopata amani juu ya yote haya, na azazeli huyo baada wa kutangatanga jangwani akiwa na dhambi hufikia kikomo na kufa.
Kwa namna hii, Mungu hupatanisha watu wake wote kwa dhambi zao kwa kupitia mwana kondoo wake, Yesu Kristo. Dhambi zetu zote zilitakaswa kabisa kupitia ubatizo wa Yesu na kwa damu yake Msalabani.
Yesu ni Mungu na Mwokozi. Ni mwana wa Mungu aliye kuja kuokoa wanadamu wote na dhambi zao zote. Ni muumba aliyetufanya kwa mfano wake na alikuja ulimwenguni kutuokoa toka dhambini.
Si dhambi za kila siku tu tuzitendazo kwa miili yetu ndizo alitwikwa Yesu, bali hata pia zile zijazo katika maisha yetu, zile katika mioyo yetu na kwa miili yetu pia. Kwa hiyo, ilimpasa abatizwe na yohana Mbatizaji ili kutimiza haki ya Mungu, upatanisho kamili kwa dhambi zote za ulimwengu.
Miaka mitatu kabla ya Yesu hajasulubiwa, alipoanza huduma yake ya uwazi, alibeba dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake mto Yordani. Ubatizo huu ndio mwanzo wa upatanisho kwa mmmwanadamu.
Katika mto Yordani, ambapo ni sehemu ya kina cha maji yafurikayo kiunoni, aliweka mikono yake juu ya kichwa cha Yesu na kumzamisha kwenye maji. Ubatizo huu ni sawa na kuwekea mikono kwa Kuhani Mkuu juu ya sadaka ya dhambi.
Kuzamishwa maana yake ni kufa na kuibuka maana yake kufufuka. Yote haya, kwa kubatizwa na Yohana, Yesu alitimiza na kubainisha viungo vile vitatu katika mpango wake; kubeba dhambi zote, kusulubiwa na kufufuka.
Tutaweza kuokolewa ikiwa tu tutatii maneno yale ya Yesu yaliyo tuokoa toka dhambini. Mungu amekwisha amua kutuokoa kupitia Yesu, na agano aliloweka katika Agano la Kale limekwishatimia kwa kupitia tendo hili, Yesu alikwenda msalabani akiwa na dhambi zetu zote juu ya kichwa amezibeba.

Amekwisha futa dhambi 
Zetu zote? Nini kilichobaki kwa
Upande wetu ikiwa Yesu?
Kile kitupasacho ni kuwa na Imani 
katika Maneno ya Mungu.

Katika Yohana 1:29 imeandikwa “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yohana Mbatizaji alishuhudia hili. Dhambi za wanadamu wote alibeba Yesu alipobatizwa mto Yordani. Amini hili! Ndipo utakapo barikiwa kwa ondoleo la dhambi zako zote.
Yatupasa kuwa na Imani ya neno la Mungu tuweke kando mawazo yetu na ugumu wa mioyo na tutii Neno la Mungu lililoandikwa inatulazimu kuamini katika kweli hii kwamba Yesu alichukua dhambi za ulimwengu huu.
Kusema kwamba Yesu alibeba dhambi zote za ulimwengu huu na kuseama pia alitimiza haki zote za Mungu kwa kutupatanisha kwa dhambi ni jambo sawa na moja katika maana. “Kuweka mikono” na “ubatizo” pia ni kitu kimoja katika tafsiri.
Haijalishi ikiwa tutasema “yote” “kila kitu” au “kwa jumla” tafsiri inabaki kuwa ni ile ile maana ya “kuwekea mikono” katika Agano la kale inabaki ile ile katika Agano Jipya, isipokuwa neno “ubatizo” ndilo hutumika badala yake.
Huja katika maana rahisi iliyo ya kweli kwamba Yesu alibatizwa na kuhukumiwa msalabani ili kutupatanisha kwa dhambi zetu zote. Tutaweza kuokolewa pale tutakapo amini Injili hii halisi.
Biblia inaposema Yesu “alichukua dhambi za ulimwengu” (Yohana 1:29) nini maana ya “dhambi za ulimwengu”? Maana yake ni dhambi zile zote tulizozaliwa nazo mioyoni, mawazo machafu, wizi, uasherati, ulafi, udhaifu, uhasi, majivuno na upumbavu yote haya hukaa akilini mwetu. Pia inahusu makosa na maovu tutendayo kwa miili na ndani ya mioyo yetu.
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana” (Warumi 6:23). “Na katika torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo” (Waebrania 9:22). Kama ilivyo katika mistari hii, dhambi zote hulipiwa gharama. Yesu Kristo, ili kuokoa wanadamu kutoka dhambini, aliyatoa maisha yake na kulipia gharama ya dhambi mara moja kwa wakati wote.
Hivyo, ilikuwa huru toka dhambini, yatupasa kuamini Injili ile halisi – ubatizo wa Yesu, Damu yake na Umungu wake (akiwa ni Roho).
 

Upatanisho wa Dhambi za Kesho.

Je, ipo haja ya kutoa sadaka
Kwa ajili ya dhambi zetu tena?
Kamwe hatupaswi.

Dhambi za kesho, siku baada ya kesho, na zile tutakazo tenda hadi siku tutakapo kufa; pia nazo zimejumuishwa katika “dhambi za ulimwengu” kama zile za leo, jana na keshokutwa pia zimo katika “dhambi za ulimwengu.” Dhambi ya asili na za maishani zote zimejumuishwa katika “dhambi za ulimwengu” na kila moja alitwikwa Yesu katika ubatizo wake. Hivyo majumuisho yote haya yamechukuliwa toka kwetu, hatuna tena dhambi.
Jambo pekee ni kuamini Injili hii (habari njema) iliyo halisi, maandiko ya Mungu, na kutii ukweli ili tuokolewe. Yatupasa kuweka kando hisia zetu ili tukombolewe toka dhambini. Unaweza kuuliza “itawezekana vipi achukue dhambi ambazo sijatenda?” Nami nitakuuliza “Ina maana Yesu inambidi arudi tena ulimwenguni kila tunapotenda dhambi na kutoa damu yake tena na tena?”
Ndani ya Injili ya kuzaliwa upya, ipo sheria ya upatanisho wa dhambi na “pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo” (Waebrania 9:22). Ikiwa yeyote atataka kukombolewa toka dhambini kwa siku hizo za Agano la Kale, ilimbidi azitwike dhambi kwa kuwekea mikono sadaka ya dhambi (mnyama), nayo sadaka hiyo itakufa kwa kuchunjwa koo kwa niaba yake na dhambi zake.
Kwa kiasi hiki ni sawa na Mwana wa Mungu ialiyeshuka ulimwenguni kuokoa wanadamu. Alibatizwa ili kubeba dhambi zote za ulimwengu, alitoa damu yake msalabani kwa kusema “yamekwisha”. Alifufuka toka kuzimu baada ya siku 3 na ameketi kuume kwa Mungu kwa haya yote, amekuwa Mwokozi wetu daima.
Ili kuondolewa kabisa dhambi zetu, yatupasa kuondokana na fikra zilizonasa akilini mwetu na kuachana na mafundisho ya udini yanayotueleza kwamba tujikomboe kwa sala za toba kila siku. Ili dhambi za wanadamu ziweze kufutwa, sadaka halali inapaswa kutolewa mara moja na kwa wakati wote. Mungu wa Mbinguni alimtwika mwana wake dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo na kuruhusu asulubiwe kwa ajili yetu. Kwa ufufuo wake toka kifoni wokovu wetu ulikamilika.
“Bali aliyejeruhiwa kwa makosa yetu. Alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake. Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona … Na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.” Katika Isaya 53 imesema kwamba makosa na maovu yetu yote ulimwenguni ya wanadamu wote alibebeshwa Yesu Kristo.
Katika Agano Jipya, Waefeso 1:4 umeandikwa “kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.” Hii inatuambia kwamba Mungu alituchagua tuwe wake kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Kabla hata ya ulimwengu haujaumbwa. Mungu alikwisha amua kutufanya kuwa watu wake, wenye haki bila doa; katika Kristo chochote tungeliweza kuwaza kabla, yatupasa sasa kuamini na kutii Neno la Mungu, neno la maji, damu na Roho.
Mungu ametueleza Mwanakondoo wake, Yesu Kristo, alichukua dhambi za ulimwengu na kutupatanisha wanadamu wote. Katika Waebrania 10:1 “Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayo kuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wowote kuwakamilisha wakimbiao.”
Hapa inasema kwamba, kwa jinsi ile iliyokuwa ikitolewa mara kwa mara katika mwaka hadi mwaka, kamwe haitoweza kuwafanya kuwa wakamilifu. Sheria ni kivuli cha mema yatakayokuwa na si sura yenyewe ya mambo. Yesu Kristo, Masia aliyekuja, ametufanya kuwa kamili kwa mara moja na wakati wote (kama ilivyo dhambi za mwaka za Israeli walivyopatanishwa mara moja na wakati wote wa mwaka mzima) kwa ubatizo na kusulubiwaili kutupatanisha kwa dhambi zetu zote.
Hivyo, Yesu ametuelezea katika Waebrania 10, “ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo nemepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi, ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu, tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa na Roho Mtakatifu naye amshuhudie kwa maana, baada ya kusema hili ni agano nitakalo agana nao baada ya siku zile, anena Bwana niitatia sheria zangu mioyoni mwao na katika nia zao nitaziandika ndipo anenapo. Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa, Basi ondoleo la hayo likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:9-18).
Tunaamini kwamba Yesu ametuokoa kutoka dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo na damu yake msalabani.
 

Wokovu katika kuzaliwa upya kwa Maji na kwa Roho umeandikwa katika mioyo yetu na katika nia zetu

Je, sisi ni wenye haki
kwa kutotenda tena dhambi?
Hapana sisi ni wenye haki kwa sababu 
Yesu alizichukua dhambi zetu zote 
na tunamwamini yeye.

Je, wote mpo katika imani kamilifu ya wokovu? – Amen – Je, mnatii kwa imani maneno ya Mungu kwamba Yesu Kristo alibatizwa na kutoa damu yake pale msalabani ili kutuokoa? Yatupasa kuwa na imani na Neno lake ili tuweze kuzaliwa upya. Tutaweza kuokolewa ikiwa tu, tutaamini kwamba Yesu Kristo, kupitia Injili ya ondoleo la dhambi, alitutakasa dhambi zetu zote pamoja na dhambi za ulimwengu.
Hakika hatuwezi kuwa watakatifu kwa kutii sheria ya Mungu bali tutaweza kuwa wakamilifu kupitia imani yetu juu ya kazi ile aliyo ifanya Yesu (Kazi ya ukombozi kamili) Yesu Kristo alichukua dhambi zetu kwa ubatizo wake mto Yordani, na akateswa kwa hukumu na kuadhibiwa kwa dhambi zetu zote msalabani kwa kuamini Injili hii kwa moyo wetu wote tutaweza kwa hakika kukombolewa na dhambi zetu zote na kuwa wenye haki daima. Je unaamini hili?
Ubatizo wa Yesu, kusulubiwa kwake na ufufuko wake ni ondoleo la dhambi zote za wanadamu na sheria ya Wokovu inayohusu upendo wa Mungu usio na mwisho wala masharti. Mungu anatupenda kama tulivyo na ni mwenye haki, hivyo alitufanya kuuwa haki kwanza. Alitufanya kuwa haki kwa kumtwika dhambi zetu zote Yesu kwa ubatizo wake.
Ili kututakasa kwa dhambi zetu zote, Mungu alimtuma mwana wake, Yesu kuja ulimwenguni kwa ajili yetu. Aliruhusu Yesu azichukue dhambi za ulimwengu kupitia ubatizo wake na kumuhukumu. Alitufanya kuwa wana wenye haki kwa kupitia wokovu kwa maji na kwa damu, upendo wa kimungu wa agape
Imeandikwa katika Waebrania 10:16 “Nitalia sheria zangu mioyoni mwao na katika nia zao mtaziandika.”
Ndani ya mioyo yetu na nia zetu je, ni wenye dhambi mbele ya Mungu au wenye haki? Ikiwa tunaimani na Neno la Mungu, basi ni wenye haki Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu zote na alihukumiwa kwa ajili yake. Yesu Kristo ni Mwokozi wetu. Unaweza kudhani “Kwa sababu tunatenda dhambi kila siku itakuwa upi ni wenye haki? Hakika sisi ni wenye dhambi.” Lakini unapo amini neno la Mungu, kama vile Kristo Yesu alivyomtii Baba, tunakuwa wenye haki pia.
Bila shaka, kama nilivyokwisha sema hapa mwanzo, tuna dhambi mioyoni mwetu kabla ya kuzaliwa upya. Baada ya kuikubali Injili ya ondoleo la dhambi mioyoni mwetu kabla ya kuzaliwa upya. Baada ya kuikubali Injili ya ondoleo la dhambi mioyoni mwetu, tumeokolewa na dhambi zetu zote. Kabla hatujafahamu hili tulikuwa wenye dhambi. Sasa tumekuwa wenye haki tunapo anza kuamini wokovu wa Yesu na kuwa wenye haki ndiyo Mtume Paulo aliyo kuwa akiiongelea sana. Imani ya Injili ya ondoleo la dhambi imetufanya muwa “wenye haki.”
Si Mtume Paulo, wala Abrahamu na hata mababu zetu wa imani hawakuwa wenye haki kwa matendo ya sheria, bali kwa kuwa na imani ya Neno la Mungu, maneno ya baraka zake katika ondoleo la madhambi.
Katika Waebrania 10:18 “Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.” Kama ilivyoandikwa, Mungu ametuokoa ili tusiweze kufa kwa dhambi zetu. Je, unaamini hilo? – Amina –
Katika Wafilipi 2 “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yu namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu, tena alipoonekana ana umbo kama mwanadamu alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni na vya duniani na vya chini ya nchi na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba” (Wafilipi 2:5-11).
Yesu Kristo, aliyejawa na utukufu wa Mungu na ni Mungu halisi (Wafilipi 2:6) hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho. Bali alijifanya kuwa mtumwa, na kuja kwa mfano wa mwanadamu. Alijishusha na kuwa mtiifu hadi kufa ili kutuokoa.
Hivyo tumsifu Yesu “ndiye Mungu wetu, Mwokozi wetu na Mfalme kwetu.” Sababu ya kumtukuza na kumsifu Yesu ni kwamba yeye alitii mapenzi ya Baba yake hadi mwisho kama asinge yatii, tusinge mtukuza mwana wa Mungu leo hii. Lakini kwa sababu Mwana wa Mungu alimtii Baba yake hata kufa, viumbe na watu wote hapa duniani watamtukuza, na watafanya hivi milele.
Yesu Kristo alikuwa ni Mwanakondoo wa Mungu aliyechukua dhambi za ulimwengu, na imeandikwa kwamba alizichukua kwa ubatizo wake sasa ni miaka zaidi ya 2000 imepita tangu alipozichukua dhambi za ulimwengu. Mimi na wewe tumeishi duniani hapa tangu kuzaliwa kwetu, na dhambi zetu zote pia zimejumuishwa katika dhambi za ulimwengu.

Je, tutaweza kuwa wenye
Dhambi Ikiwa tutatenda 
dhambi kesho?
Hapana, kwa sababu Yesu alikwisha
Chukua dhambi zetu zote zile za siku
Za nyuma, sasa na wakati ujao.
 
Bila kutenga dhambi ya sili toka makosa ya maishani petu, Je, hatukuwa wa dhambi toka kuzaliwa kwetu? – Ndiyo – sisi ni wadhambi.
Yesu alikwisha jua kwamba tutatenda dhambi kuanzia siku ile tuliyozaliwa hadi siku ya kufa. Hivyo alichukua dhambi hizo kabla. Je, waweza kuona sasa? Ikiwa tulipaswa kuishi umri wa miaka 70, dhambi zetu zingekuwa nyingi kiasi cha lori 100 za taka! Lakini Yesu alizichukua zote hizi mara moja kwa ubatizo wake na kuzipeleka msalabani kwa malipo.
Ikiwa Yesu angelichukua dhambi ya asili tu, hakika sisi wote tungelikufa na kwenda motoni. Hata ikiwa hatuhisi kwamba Yesu hakuchukua dhambi zetu zote, kamwe haiweze kubadilisha ukweli wa Yesu kufuta dhambi zetu zote.
Ni kiasi gani cha dhambi tunachotenda hapa ulimwenguni? Dhambi zote tutendazo zimejumuishwa katika dhambi za ulimwengu.
Wakati Yesu alipomwambia Yohana ambatize alikuwa akimaanisha juu ya kubeba dhambi za ulimwengu. Yesu alishuhudia ya kwamba yeye alikwisha chukua dhambi zote za ulimwengu. Mungu alimtuma mtumishi huyu Yohana mbele ya Yesu ili ambatize Yesu. Kwa kubatizwa, na Yohana ambaye ni mwakilishi wa wanadamu, Yesu aliinamisha kichwa chake mbele yake ili abatizwe ili azichukue dhambi zote za ulimwengu.
Dhambi zetu zote tokea umri wa miaka 20 hadi 30 na 40 na zaidi hata zile za watoto wetu zimejumuishwa katika dhambi za ulimwengu ambazo Yesu alibeba kwa ubatizo wake.
Ni nani awezaye kusema zipo dhambi zilizobaki Ulimwenguni? Yesu Kristo alichukua dhambi zote za ulimwengu huu na tunaweza wote kuokolewa kwa kuamini kwa moyo wetu wote, bila kivuli cha shaka juu ya nini Yesu aliyofanya katika kuleta upatanisho wa dhambi zetu yaani ubatizo na kutoa damu yake ya thamani.
Wengi huishi maisha ya kuchanganyikiwa yaliyo funikwa kwa fikra binafsi, wakizungumzia juu ya maisha yao tu, wakidhani kwamba yalikuwa ni muhimu sana. Lakini wapo wengine wanaishi maisha magumu. Wengine wameishi maisha ya kuchanganyikiwa. Hata mimi niliwahi kuishi kabla ya kuzaliwa upya, yaani kuokoka utawezaje kukataa kuelewa na kuto kukubali juu ya Injili ya ondoleo la dhambi katika ubatizo wa Yesu na damu yake?
 

Wokovu wa wenye dhambi ulikwisha kamilishwa

Sababu gani Yesu aliosha
Miguu ya Petro?
Alitaka Petro awe na Imani madhubuti,
Ukweli Yesu alikwisha takasa tayari
Dhambi zake zote zijazo 
kwa ubatizo wake.

Hebu tusome Yohana 19 “Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania Golgotha. Wakamsulubisha huko na wengine wawili pamoja naye, moja huku na mmoja huku, na Yesu kati kati. Naye Pilato akaandika anwani akaiweka juu ya msalaba imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposhulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji, nayo iliandikwa kwa kiebrania, na Kirumi na Kiyunani” (Yohana 19:17-20).
Ndugu wapendwa, Yesu Kristo alichukua dhambi zote za ulimwengu akahukumiwa na kusulubiwa mbele ya Pilato. Hebu sasa tufikirie juu ya tukio hili pamoja.
Kwa kuanzia mstari wa 28. “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe akasema, Naona kiu. Kulikuako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo Wakampelekea kinywani. Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki kinywani. Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki alisema imekwisha. Akainama kichwa akisalimu roho yake” (Yohana 19:28-30).
Yesu alisema “Yamekwisha” na baadaye alikufa pale msalabani. Baada ya siku tatu, alifufuka toka kifoni na kupaa mbinguni.
Ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji na kifo chake msalabani ni mambo mawili yasiyoweza kuachanishwa moja halina sababu ya kuwepo pasipo jingine. Hivyo, tumsifu Bwana wetu Yesu kwa kutuokoa kupitia Injili yake ya ondoleo la dhambi.
Mwili wa mwanadamu mara nyingi hufuata matakwa yake ya kimwili, hivyo hatuwezi kujizuia kutotenda dhambi kwa miili yetu. Yesu Kristo ametupa ubatizo wake na damu yake ili kutuokoa na dhambi za mwili. Alituokoa na dhambi za mwili kwa Injili yake wale walio na ondoleo kamili la dhambi ndiyo watakaoweza kuingia katika Ufalme wa Mbinguni wakati wowote kwa kumwamini Yesu, aliyezaliwa Bethlehemu, alibatizwa Yordani na kufa Msalabani na alifufuliwa baada ya siku tatu. Tuna msifu Bwana na kulitukuza Jina lake milele.
Sura mwisho katika Injili ya Yohana, Yesu alikwenda kwa Petro na kumwambia “Je, Simon wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa?” naye Petro akamjibu “Ndiyo Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda.” Ndipo Yesu akamwambia “lisha kondoo zangu.”
Petro alielewa kila kitu juu ya Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake, ondoleo la dhambi. Hivyo, kuamini Injili ya maji na damu ambayo ilimpatia ondoleo la dhambi zake zote na pia kwa nini Yesu alimwosha miguu, ndiko kulikofanya Imani yake katika Yesu iwe madhubuti.
Hebu tusome Yohana 21:15 tena “Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simon Petro, Je! Simon wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda Akamwambia, lisha wana kondoo wangu.” Aliweza kumkabidhi wana-kondoo wake Petro kwa kuwa alikuwa ni mwanafunzi wake aliye okoka kikamilifu na kwa kuwa Petro alikuwa mwenye haki na mtumishi kamilifu wa Mungu.
Ikiwa Petro angerudia tena kuwa mdhambi kwa makosa ya kila siku, Yesu asingeweza kumwambia ahubiri Injili ya upatanisho wa dhambi tena, kwa kuwa yeye na wenzake wasingeweza kujizuia bila kutenda dhambi kila siku katika mwili. Hivyo Yesu aliwaambia wahubiri Injili ambayo ailiyofuta kabisa dhambi zao zote kwa sababu ndiyo waliyo iamini kwa ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, Injili ya upatanisho wa dhambi.
 

“Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda”

Utakuwa mwenye dhambi
tena ikiwa utatenda dhambi?
Hapana Yesu alikwisha zichukua dhambi
zako zote zijazo mbeleni 
pale Yordani.

Hebu natufikiri juu ya maneno ya Yesu kwa Petro “Je, Simon wa Yohana wewe wanipenda kuliko hawa?” “Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda.” Kukiri kwake kwa upendo kulikuwa ni kwa ukweli ulio chupuka kwa imani itakanayo na Injili ya upatanisho wa dhambi.
Ikiwa Yesu asingemfundisha Petro na Mitume wake juu ya Injili ya ondoleo la dhambi kwa kuwaosha miguu asingeweza kukiri upendo wao kwa namna hiyo. 
Badala yake Yesu alipokuja na kumuuliza “wanipenda kuliko hawa?” Petro angeweza kujibu “Bwana mimi ni mtu asiye mkamilifu. Mwenye dhambi asiyeweza kukupenda kuliko vingine. Nakusihi uniache tu.” Naye angetoweka, kwa kujificha mbele ya Yesu.
Lakini hebu tufikiri, juu ya jibu hili la Petro. Hakika alikuwa amebarikiwa kwa Injili ile ya ondoleo la dhambi, ubatizo wa Yesu na damu yake ambayo ni wokovu wa wanadamu wote.
Hivyo Petro alikuwa na uhakika kwa kusema “Naam, Bwana wewe wajua kuwa nakupenda,” kukiri upendo kulikuja kwa imani katika Injili ya ondoleo la dhambi, ambayo Yesu alichukua dhambi zote za ulimwengu. Hii ni pamoja na zile zijazo, ambazo watu wamefungwa kuzitenda kwa sababu ya udhaifu na upungufu wa miili yao.
Petro aliamini kwa dhati katika Injili ya ondoleo la dhambi na kwa kuwa pia aliamini kwamba Yesu alikuwa ni Mwana kondoo wa Mungu hivyo kuweza kumjibu Bwana bila kughairi. Wokovu wa Yesu ulikuja kutoka Injili (habari njema) ya ondoleo la dhambi, na hivyo Petro aliokolewa toka dhambi za kila siku pia. Petro aliamini wokovu kupitia Injili ya ondoleo la dhambi zote za ulimwengu.
Je, na wewe u kama Petro? Je, waweza kumpenda na kumtumaini Yesu aliyezichukua dhambi zako zote kwa Injili ya ondoleo la dhambi, kwa njia ya ubatizo na damu yake? Waweza vipi kutoamini au kutompenda? Hakuna njia nyingine.
Ikiwa Yesu alichukua dhambi zako za siku za nyuma na zile za wakati uliopo tu, hakika tusingeweza kumsifu kama tufanyavyo sasa. Kwa nyongeza ya hili, na hakika tungeishia motoni tu. Hivyo yatupasa tukiri kwamba Injili hii ya ondoleo la dhambi imetuokoa.
Siku zote mwili umelazimika kutenda dhambi, hivyo tutaendelea kutenda dhambi bila hiyari. Hivyo yatupasa kukiri kwa kuamini Injili ya upatanisho kamili wa dhambi zetu ambao ametupatia Yesu, Injili ya ubatizo na damu ya Yesu, umetuokoa.
Ikiwa hatutaamini Injili hii hakuna atakaye okolewa kutoka katika dhambi maishani mwake kwa nyongeza, ikiwa tutakombolewa na dhambi zetu zote maishani kwa kukiri na kutubu kila mara, bila shaka tungekuwa wazembe kuendelea kuwa wenye haki na kuendelea kuwa dhambi mioyoni mwetu siku zote.
Kama ingekuwa namna hii, tungerudi kuwa wenye dhambi na tusinge mpenda Yesu au hata kuwa karibu naye. Pia tusingeweza kuamini wokovu wa Yesu na kumfuata hadi mwisho wa maisha yetu. 
Yesu ametupatia Injili ya ondoleo la dhambi na kutuokoa sisi sote wenye kuiamini. Amefanyizwa kuwa Mwokozi kamili na kututakasa makosa yetu ya kila siku ili tuweze kuwa huru kumpenda.
Sisi wenye kuamini hatuwezi kujizuia kupenda Injili ile ya ubatizo na damu ya Yesu, ondoleo la dhambi zetu zote. Wenye kuamini wote watampenda Yesu milele na kushikwa kwa pendo la wokovu kupitia Injili ya ondoleo la dhambi ambalo Yesu mwenyewe ametuachia.
Wapendwa! Ikiwa Yesu amebakiza hata dhambi ndogo, hakika tusingeweza kumwamini, au hata kuwa mshuhudiaji wa Injili hii. Usingeweza pia kutembea kama Mtumishi wa Mungu.
Lakini ikiwa utaamini Injili hii ya ondoleo la dhambi kwa kweli utaokolewa na dhambi zako zote. Ameachilia uokolewe toka dhambi zako zote pale utakapo fahamu ukweli wa Injili ya ondoleo la dhambi, iliyomo katika Neno la Yesu.
 

“Wanipenda kuliko hawa?”

Jambo gani litufanyalo kupenda 
Yesu zaidi ya chochote?
Upendo wake kwetu kupitia ubatizo wake
uliotutakasa dhambi zetu zote hata zile
za nyakati zaijazo.

Mungu alimwaminisha mwana kondoo wake kwa wale watumishi walio ikubali Injili ya ondoleo la dhambi kwa uaminifu. Yesu aliuliza mara tatu “Je! Simon wa Yohana wewe wanipenda kuliko hawa?” naye Petro akamjibu kwa mara zote “Naam Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda,” sasa hebu tufikiri juu ya jibu la Petro. Tunaweza kuona huu ulikuwa si utashi wake binafsi bali imani iliyokuwa ndani yake juu ya ondoleo la dhambi.
Tunapo mpenda mtu, na ikiwa upendo huo unatokana na hiyari yetu, utaweza kushindwa tutakapo kuwa dhaifu. Lakini upendo utokanao na nguvu ya upendo wa Mungu huo utakuwa usio na mwisho wala mipaka. Upendo wa Mungu, uliosheni upatanisho wa dhambi zetu zote, wokovu kwa maji ya ubatizo wa Yesu na Roho ndivyo ulivyo.
Imani yetu katika Injili ya ondoleo la dhambi ni lazima uwe ndiyo msingi na upendo wetu na matendo yetu kwa Bwana. Ikiwa tunampenda Yesu kwa hiyari yetu tutakwazika baadaye na kuishia kujeruhiwa kwa maovu yetu. Ijapokuwa Yesu ametutakasa kabisa na madhambi yetu yote; yale ya asili, yale ya kila siku, kwa wakati uliopita, uliopo na ujao katika maisha yetu yote hapa ulimwenguni. Hukumwacha yeyote katika wokovu huu.
Yote haya ni ukweli mtupu. Ikiwa upendo wetu na imani zetu itategemeana na hiyari na maamuzi binafsi, tutapotoka kiimani. Lakini ikiwa upendo wetu na imani zetu itategemeana na Injili ya ondoleo la dhambi Yesu alilotupa, tutakuwa tayari ni watoto wa Mungu, wenye haki. Hivyo tukiamini wokovu katika maji na Roho, tutakuwa hatuna dhambi.
Kutokana na ukweli kwamba wokovu ulikuja si katika namna ya kimungu ndani yetu, bali kwa upendo wa Mungu na sheria yake ya wokovu wa kweli katika ondoleo la dhambi, sisi ni wenye haki ingawa ni kwa namna gani hatujakamilika na kwa kuwa dhaifu kimwili maishani mwetu. Tutaingia ufalme wa Mbinguni na kumsifu Mungu milele. Je, unaamini hili?
1 Yohana 4:10 inasema “Hili ndilo pendo la Mungu, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bale kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.” Yesu alituokoa kwa maji na Roho, hivyo yatupasa kuamini Injili ya ondoleo la dhambi ubatizo wa Yesu na damu yake.
Ikiwa Mungu hajatuokoa kwa Injili hii, tusinge okoka, bila kujali ni kwa kiasi gani tunamwamini. Lakini Yesu alitutakasa na dhambi zetu zote tulizotenda moyoni na katika mwili.
Ili tuweze kuwa wenye haki, yatupasa kuwa na uhakika na wokovu wetu kupitia imani katika maneno ya maji na Roho, Injili ya upatanisho, Injili ya ondoleo la dhambi za ulimwengu imeundwa kwa ubatizo wa Yesu na Damu yeke. Injili ya ondoleo la dhambi ni mjumuiko wa Imani ya kweli, msingi wa wokovu wa kweli na ni ufunguo wa kuingia Ufalme wa Mungu.
 

Yatupasa kuachana na Imani ya utashi wetu

Imani iliyo ya kweli 
huja toka wapi?
Huja toka juu kwa Bwana aliye 
kwisha takasa dhambi zetu 
za nyakati zijazo.

Imani na upendo wa mtu utokanao na utashi wake si imani na upendo wa kweli. Wapo wengi katika dunia hii waliomwamini Yesu kwa mara ya kwanza kwa utashi mzuri, na baadaye waliacha imani zao kwa sababu ya uchungu wa dhambi zao moyoni.
Lakini yatupasa kuelewa kwamba Yesu alikwisha takasa dhambi zote za ulimwengu; si zile tuzionazo ndogo tu bali hata zile kuu tuzifanyazo kwa kutoelewa.
Katika Yohana 13, ili kuwafundisha wanafunzi wake namna gani wokovu wake ulivyo wa kutumainiwa na wakuendelea kuwepo milele, Yesu aliwakusanya wanafunzi wake pamoja kabla kusulubiwa kwake Alipokuwa nao kwa chakula cha jioni, alinyanyuka na kuanza kuwakosha miguu ili kusisitiza juu ya ukweli wa wokovu uliokamilifu ndani ya mioyo yao. Nasi sote yatupasa kufahamu na kuamini juu ya Injili ya ondoleo la dhambi ambayo Yesu alitufundisha wanafunzi wake kwa kukosha miguu yao.
Mwanzo Petro alikataa kumruhusu Yesu kuosha miguu yake “Wewe hutanitawadha miguu kamwe.” Na huu ndiyo uhalisi wa imani itokanayo na utashi binafsi. Lakini Yesu alimwambia “Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utafahamu baadaye.”
Hivyo sasa kwa Injili ya maji na Roho tutaweza kuelewa maneno ya Biblia ambayo yalikuwa kinyume na ufahamu wetu. Ni neno la kweli; injili ya maji na Roho, ondoleo la dhambi limfanyalo mwenye dhambi kuwa mwenye haki kwa kuamini kwa moyo wako wote.
Petro alikwenda kuvua samaki na wanafunzi wengine, kama ilivyo kawaida yao kabla ya kukutana na Yesu. Ndipo Yesu alipowatokea na kuwaita kwake. Yesu alikuwa ametayarisha kifungua kinywa kwa ajili yao, na walipokuwa wakishiriki, Petro aligundua maana ya maneno Yesu aliyokuwa akiwaelezea hapo awali. “nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utafahamu baadaye.” Hatimaye aligundua kile Yesu alichokuwa akimaanisha kwa kuosha miguu yao hapa awali.
“Bwana aliosha dhambi zangu zote. Dhambi zote nilizo tenda kwa udhaifu wangu, zikiwa pamoja na zile zote nitakazo tenda hapo awali pia.” Petro aliacha ile imani yake itokanayo na utashi wake na fikra zake na kuanza kusimama imara katika ubatizo na damu ya Yesu, Injili ya ondoleo la dhambi.
Baada ya kifungua kinywa Yesu alimuuliza Petro, “Je, wanipenda zaidi ya hawa?” Kwa kuimarisha imani katika upendo wa Yesu Petro alikiri “Ndiyo Bwana; wewe wajua kwamba nakupenda.” Yamkini Petro angeweza kujibu kwa kusema “utajua baadaye” alikuwa na nafasi ya kukiri imani yake ya kweli, imani katika ubatizo na damu ya Yesu, Injili ya ondoleo la dhambi.
 

Na baadaye, alikuwa Mtumishi wa kweli wa Mungu

Baada ya uzoefu, Petro na wanafunzi wengine walihubiri Injili hadi mwisho wa pumzi yao. Hata Paulo aliyewatesa na kuwaua bila huruma Wakristo, alishuhudia Injili katika vipindi hivyo vya utawala wa Dola ya Warumi.

Je, waweza kuwa vipi
mtumishi wa Mungu?
Kwa kuamini upatanisho wa milele
wa dhambi zangu zote

Kati ya wanafunzi wale kumi na wawili wa Yesu Yuda aliye muuza Yesu na baadaye kujinyonga. Alikuwa Paulo ndiye mtume aliyechukua nafasi yake. Wanafunzi wa Yesu walimchagua Mathiasi kati yao, lakini Mungu alimteua Paulo, hivyo akawa Mtume wa Yesu na kuhubiri Injili ya ondoleo la dhambi pamoja na wanafunzi wengine.
Wengi wa wanafunzi hawa walikufa wakiwa mashahidi wa Mungu. Hata pale walipotishiwa kuuawa hawakuikana imani na kuendelea kuhubiri Injili ile halisi.
Yamkini wangehubiri kwa namna hii “Yesu Kristo alizitakasa dhambi zetu zote za mwili kwa ubatizo na damu yake na kwa hivyo, kwa injili ya ondoleo la dhambi yeye alizibeba dhambi zetu zote kwa kubatizwa kwake mto Yordani na kubeba hukumu yetu msalabani. Amini Injili ya Yesu katika ubatizo na damu yake msalabani ili muokolewe.”
Kwa kusikia Injili hii halisi na kuiamini hakika kila mtu ataokolewa. Ni nguvu ya imani katika Injili ya ubatizo wa Yesu, damu yake na Roho.
Mitume walihubiri Injili ya maji na Roho kwa kusema “Yesu ni Mungu na Mwokozi.” Ni kwa sababu walikwisha shuhudia juu ya Injili hii ya Yesu kwamba ni Mwokozi na kuokolewa dhambini. Kwa sababu ya upendo wa Mungu usio na mwisho na wokovu kamili toka kwa Yesu sote tumekuwa wanafunzi wa Yesu.
Je, wote mnaamini hivyo? Yesu alitupenda sote kwa upendo mkuu hata kutupa Injili ya maji na Roho, ondoleo la dhambi na kuwa wenye haki wanafunzi wa Yesu. Ili kutufundisha Injili ya kweli ya ondoleo la dhambi, Yesu aliosha miguu ya wanafunzi wake.
Yesu alisafisha miguu ya wanafunzi wake ili kuwafundisha wao na hata sisi leo hii kwamba dhambi zote za ulimwengu, zikiwa zile tuzifanyazo maishani mwetu pote na hata zile zijazo za nyakati, yeye alikwisha zitakasa kwa ubatizo wake na damu yake msalabani. Tunamshukuru Yesu kwa upendo wake na kwa Injili ya ondoleo la dhambi.
Yesu alitufundisha mambo mawili kwa kuosha miguu ya wanafunzi wake.Kwanza ilikuwa ni kama alivyo alisema “Nifanyalo huwezi kufahamu sasa utalifamu baadaye,” ya kwamba dhambi zetu zote alizitakasa kwa injili ya ondoleo la dahmbi, ubatizo wa Yesu wa damu yake.
Pili,somo lingine litakuwa ni kujishusha yeye mwenyewe ili kuokoa wenye dhambi na kuwafanya wenye haki, sisi tulio zaliwa upya yatupasa kuwatumikia wengine kwa kuhubiri injili ya undoleo la dhambi. Ni haki yetu sisi tulio amini awali kutumikia wanao kuja.
Sababu mbili hizi ndizo zilizomfanya Yesu kuosha miguu ya wanafunzi wake katika siku ile ya pasaka na ndiyo sababu zilizo wazi hadi hivi leo katika kanisa lake.
Mwanafunzi hawezi kuwa zaidi ya mwalimu, hivyo tuna hubiri injili duniani na dunia iokolewe kama tupasavyo kumtumikia Yesu sisi tulio okolewa hapo awali yatupasa tuwatumikie wali wajo nyuma yetu.Kwa kufundisha haya Yesu aliosha miguuu ya wanafunzi wake.Kwa nyongeza kwa kuosha miguu ile ya Petro alituonyesha kwamba yeye ndiye Mwokozi wa kweli hivyo tusiwe kudanganywa na shetani tena.
Wote mtaweza kuokolewa kwa kuamini injili ile ya indoleo la dhambi maji na Roho. Yesu alitutakasa na dhambi zetu zote kwa ubatizo wake kusulubiwa kwake na kwa ufufuo wake. Ni wale tu watakao amini injili yake ndiyo watako okolewa kwa dhambi zote za ulimwengu huu milele.
 

Uwe na imani katika injili ile itakasayodhambi zetu zote za kila siku

Tunaondolea mbali ulaghai wa shetani kwa kuamini injili ya ondoleo la dhambi, maneno ya maji na Roho. Nirahisi kwa watu kudanganywa na shetani na shetani huyo kuendelea kuwanong’oneza katika masikio yao. Je, kwa kujua yakwamba miili ya wanadamu wakati wote itaendelea kutenda dhambi duniani, ni kwa vipi basi wanadamu hao hawatoweza kuwa na dhambi? Watu wote ni wenye dhambi. 
Hivyo basi tunafahamu jibu lake “kwa kutambua yakwamba Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake. Je, nikwanamna gani basi mwenye kuamini aweza kuwa si mwenye dhambi tena? Je, Yesu amelipa mshahara wote kwa dhambi zote, na hivyo hakuna kilicho baki kwetu kukilipia?
Ikiwa hatuta amini injili ya maji na damu maneno ya ibilisi yanaweza kuwa yenye sababu, lakini ikiwa tutakuwa na injili kwa upendo wetu tutaweza kuwa imani isiyo tikisika ktatika neno la Mungu lilo la kweli.
Yatupasa kuwa imani katika inji ya kuzaliwa upya kwa maji na damu.imani ya kweli ni katika injili ya ubatizo wa Yesu damu yake pale msalabani, kifo chake na ufufuo wake.
Je umeshakwisha una picha ya umbile la madhabahu takatifu? Ni nyumba ndogo ya turubai.ilivyo gawanyika katika sehemu kuu mbili, eneo la inje ni eneo takatifu na sehemu ya ndani ni patakatifu madhabahuni, ambapo kile kiti cha nehema kilimo.
Zipo jumla ya nguzo 60 zilizo zunguka wima sehemu ya nje ya madhabahu takatifu pa patakatifu zime zungukwa na kuta 48. yatupasa tuweke ndani ya mawazo yetu mtazamo wa mdhabuhu takatifu ndani yafukaa zetu ili tuweze kuelewa maana ya maneno ya Mungu.
 

Je malango ya ukumbi wa madhabahu yalitengenezwa kwa namna gani?

Malango ya ukumbi wa
madhabahu hayo yaliundwa
kwa nini?
Chandarua ya kufumwa rangi ya Samawati
Zambarau na nyekundu na 
kitani ya kusokotwa.

Lengo la ukumbi wa Madhabahu umeelezewa katika kitabu cha cha Kutoka 27:16 “Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa na ya rangi ya zambarau na nyekundu na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshona taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na matako yake manne.” Vitu hivi vilivyo tumika kutengenezea lango hili la ukumbi wa madhabahu vilikuwa samawati, zambarau na kitani ya kufumwa nyekundu ilifumwa na kuwa na rangi ya kuvutia.
Mungu alimwamuru Musa kupamba lango kwa rangi za kuvutia za samawati, zambarau na nyekundu na kitani ya kusokotwa ili iwe ni rahisi kwa kila mmoja kuweza kuuona mlango kwa urahisi. Lango hili lililo fumwa kwa rangi hizo katika kitani cha kufumwa lilining’inizwa kati ya pembe nne za minara.
Vitu hivi vinne vina simama badala ya mpango wa wokovu wa Mungu, ambao atawaokoa wale woto wenye kumwamini mwana wake, kwa kupitia ubatizo na kwa damu ya Yesu, na kwa kupitia hali yake ya kuwa yeye ndiye Mungu.
Kila kifaa kilicho tumika kujengea hema hii kilikuwa na maana yake ya pekee na vyote viliwakilisha Neno la Mungu na mipango yake katika kuwaokoa wanadamu kupitia Yesu.
Kila kimoja ya vitu hivi vilivyo tumika kujenga madhabahu takatifu? Aina nne tofauti zilitumika! Samawati, zambarau, nyekungu na kitani ya kufumwa; vitu hivi vinene vilikuwa na umuhimu katika kuimarisha imani zetu katika Injili ya kuzaliwa upya. Kama havikuwa muhimu habari hii isingewekwa kwa kumbukumbu katika Biblia kwa maelezo ya kina kama haya.
Vitu vyote vilivyotumika katika lango la ua wa madhabahu takatifu vina maanisha umuhimu wa tafsiri katika wokovu wetu. Hivyo Mungu alimfunulia Musa na kumwambia jinsi ile ya kufanya kama aelezwavyo.
 

Nini maana ya nguo ya samawati, zambarau nyekundu na kitani ya kufumwa katika Injili ya Mungu?

Vitu vyote hivi vilivyo
tumika viliashiria nini?
Wokovu wa Yesu kupitia ubatizo 
wake na damu yake. 

Ndani ya madhabahu takatifu kitambaa cha samawati, zambarau na nyekunda na kitani ya kufumwa vilitumika kwa ajili ya pazia lililo tundikwa kati ya pahala patakatifu na patakatifu pa patakatifu. Vitu vya namna hiyo pia vilitumika kumvika Kuhani mkuu ambaye alipaswa kuingia patakatifu pa patakatifu mara moja kwa mwaka. 
Kitambaa cha samawati kinaashiria ubatizo wa Yesu katika 1 Petro 3:21 inasema “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unao waokoa ninyi siku hizi.” Petro anahakikisha juu ya ubatizo wa Yesu kupitia kwake dhambi zote za ulimwengu alizibeba kwa mstari huu kama mfano ya wokovu katika ondoleo la dhambi. Dhambi zetu zote alibebeshwa Yesu kupitia ubatizo wake. Hivyo kitambaa cha samawati, ubatizo wa Yesu ni moja kati ya sehemu muhimu ya Neno la wokovu.
Kitambaa chekundu kinamaanisha damu ya Yesu na kitambaa cha zambarau nacho ni Uungu wake – hadhi ya Yesu kama Mfalme na Mungu. Rangi hizo tatu zilikuwa muhimu kwa ajili ya imani yetu katika Yesu na wokovu wake.
Vazi lile la nje, maridadi avaalo Kuhani Mkuu liliitwa kifuko cha kifuani, na kamba ya kusokotwa iliyo samawati. Kuhani mkuu alivaa kilemba kilicho bandikwa kwa bamba la dhahabu safi na kuandikwa juu yake, mfano wa kuchorwa kwa mhuri “MTAKATIF KWA BWANA.” Ulitiwa mkanda wa rangi ya samawati ili kulifunga katika hicho kilemba upande wa juu.
 

Ukweli utokanao na maana ya kitambaa c ha rangi ya Samawati

Nini kinachowakilishwa 
na kitambaa cha rangi 
ya samawati?
Ubatizo wa Yesu.

Nilitafuta maana ya rangi ya kitambaa cha Samawati katika Biblia. Biblia inasema juu ya rangi ya samawati? Yatupasa kuelewa maana ya rangi ya samawati, zambarau, na nyekundu katika kitambaa.
Kitambaa cha samawati kinawakilisha “maji” nao ni ubatizo wa Yesu. Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji ili aweze kubeba dhambi zote za ulimwengu (Mathayo 3:15).
Ikiwa Yesu hakuzichukua dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake, leo hii tusingeweza kutakaswa mbele za Mungu. Hivyo Yesu Kristo alipasa aje ulimwenguni na kubatizwa na Yohana Mbatizaji katika mto Yordani ili aweze kuchukua dhambi za ulimwengu.
Sababu na maana ya kuwepo kwa rangi ya samawati katika kitambaa kilichopo malangoni mwa ukumbi wa madhabahu takatifu ilikuwa ni kwamba tusingeweza kutakaswa pasipo ubatizo wa Yesu.
Kitambaa chakundu kinawakilisha damu ya Yesu, kifo chake msalabani. Zambarau inawakilisha Uungu wa Yesu, hadhi ya Yesu kama “yeye alihimidiwa, mwenye uweza peke yake mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana” (1 Timotheo 6:15).
Ukweli ni kwamba kitambaa cha rangi nyekundu kinawakilisha damu ya Kristo, iliyotoka pale msalabani kulipia mshahara wa dhambi zote za wanadamu. Yesu Kristo alikuja ulimwenguni katika mwili ili kubeba dhambi zote za wanadamu juu yake kwa ubatizo wake na kulipia mshahara wa dhambi kwa kujitoa kwake msalabani. Ubatizo na damu ya Yesu ndiyo Injili ya kweli kwa ondoleo la dhambi lenye unabii kupitia rangi za kitambaa cha pazia lililotumika katika lango la madhabahu takatifu kipindi cha Agano la Kale.
Nguzo za madhabahu zilitokana na mbao za mti wa mshita, viunganishi vyake vilitokana na shaba iliyo pakwa utepe wa fedha juu yake wenye dhambi wote walihukumiwa kwa makosa yao kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti. Kabla ya mtu yeyote hajabarikiwa na Mungu ili kupata maisha mapya, yampasa kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zake za siku kwa nyakati hizo za Agano la Kale.
Kwa jinsi hiyo basi, ubatizo wa Yesu kipindi cha Agano Jipya unawakilishwa na rangi ya Samawati katika madhabahu takatifu iliyo beba dhambi zetu zote msalabani, alitokwa na damu na kuhukumiwa kwa ajili yake ili kwa hayo ametuokoa sisi sote wenye kuamini Injili ya ondoleo la dhambi. Yeye ni mfalme wa falme na Mungu mtakatifu.
Wapendwa Wakristo, ubatizo wa Yesu ulikuwa ni wokovu toka kwake, ulio tuokoa sisi sote kwa kuzibeba dhambi zetu zote. Yesu yeye aliye Mungu alishika ulimwengu ni katika mwili (kitambaa cha rangi ya zambarau); Alibatizwa ili kubeba dhambi zetu zote ulimwenguni (kitambaa cha rangi ya samawati); Alisulubiwa na kutokwa damu pale msalabani ili kuikubali hukumu kwa niaba yetu (kitambaa cha rangi nyekundu). Ubatizo wa Yesu bila shaka unatufundisha kwamba yeye amekuwa Mwokozi wa kweli kwa wanadamu.
Tunaweza kuona pia katika rangi zilizopakwa katika malango ya madhabahu takatifu. 
Kufumwa kwa kitambaa cha malango ya madhabahu takatifu kwa rangi ya samawati zambarau na nyekundu kwa nyuzi nzuri za heriri ni ishara tosha inayotueleza bayana ukweli wa wokovu wa Mungu. Nyuzi nzuri za hariri hapa zinatuonyesha kwamba ameniokoa pasipo kuzuizi cha dhambi zetu. Ilikuwa hakika ni muhimu katika wokovu wa upatanisho wa dhambi zetu zote.
Tunaweza kuona toka katika vitu vingine vilivyotumika kwa malango ya madhabahu takatifu jinsi ile Yesu Kristo asivyo chagua kuokoa sisi wenye dhambi bila kuweka mpangilio. Alitii mpango makini wa Mungu alibatizwa akasulubiwa na kufufuka toka kifoni ili kukamilisha wokovu wa wanadamu kwa rangi ya samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa, hii ndiyo malighafi iliyo tengeneza Injili ya ondoleo la dhambi ambayo Yesu alituokoa, sisi sote wenye kuamini wokovu wake.
 

Birika la Shaba katika Agano la Kale ni mfano wa ubatizo katika Agano jipya

Sababu gani makuhani 
waliosha mikono na miguu kabla ya
kuingia sehemu takatifu?
Iliwapasa kusimama mbele ya
Mungu pasipo na dhambi Yeyote.

Birika lilitengenezwa kwa shaba. Shaba inawakilisha hukumu aliyopata Yesu kwa ajili yetu. Maji katika birika hilo yanawakilisha neno la Injili, linalo tueleza juu ya kutakasa kwa uovu wetu wote.
Hutuonyesha jinsi ile dhambi za kila siku zilivyoweza kutakaswa. Dhambi za kila siku za wanadamu ziliweza kutakaswa kwa kupitia imani katika maneno ya ubatizo wa Yesu. 
Altare ya sadaka ya kuteketezwa inawakilisha hukumu. Maji ya Yesu, ambayo ni Samawati ni Injili ya ondoleo la dhambi kwa wenye dhambi wote, kwa maneno mengine, ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji (Mathayo 3:15, 1 Yohana 5:5-10). Ni neno la ushuhuda la Injili ya wokovu kupitia ondoleo la dhambi.
Katika 1 Yohana 5 imeandikwa “Na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu – hiyo imani yetu. Kisha wako watatu washuhudiao duniani, Roho, maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja.” Inatueleza pia kuwa Yeye amwaminie Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake katika maji, damu na Roho.
Mungu alituruhusu sisi tuweze kutakaswa kwa kupitia imani katika Injili ya upatanisho na kuingia madhabau takatifu. Hivyo tunaweza sasa kuishi katika imani, kulishwa neno la Mungu, kubarikiwa naye na kuishi maisha ya haki ilikuwa watu wa Mungu maana yake ni kuokolewa kwa imani katika Injili ya upatanisho na kuishi ndani ya hekalu takatifu.
Watu wengi hivi leo husema inatosha tu bila hata ya kufikiri na kujua juu ya maana ya rangi ya samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa kilicho, malangoni pa madhabau takatifu. Ikiwa mtu atamwamini Yesu bila kujua juu ya vitu hivi imani yake haitoweza kuwa ya kweli kwa sababu ataendelea kuwa na dhamira ya dhambi moyoni mwake. Hii itatokana na kutoamini ukweli wa kuzaliwa upya kupitia injili ya ondoleo la dhambi katika maji, damu na Roho.
Ikiwa mtu alipaswa kumtathmini mtu Fulani ambaye asiye mfahamu na ikiwa atataka kumfurahisha msikilizaji atasema “Ndiyo namwamini mtu huyu. Bila shaka sijakutana naye kabla lakini namwamini hata hivyo.” Je, unadhani msikilizaji ataridhika kusikia hilo? Labda baadhi yenu mtaweza kuwa na tabia hii ya kibinadamu lakini hii si tabia ya Mungu anayo hitaji toka kwetu.
Mungu anatutaka kuamini Injili ya ondoleo la dhambi Wokovu wa Yesu kupitia samawati (ubatizo wa Yesu), zambarau (Uungu wa Yesu) nyekundu (damu ya Yesu) katika kitambaa. Yatupasa kujua kabla ya kuwa na imani katika Yesu jinsi alivyotuokoa kwa dhambi zetu zote.
Tunapo mwamini Yesu yatupasa kuelewa jinsi alivyo tuokoa toka dhambini kupitia maji (ubatizo wake) damu (kifo chake) na Roho (Yesu aliye Mungu).
Tunapoelewa kwa uhakika, tutaweza kuona ukweli na imani iliyo kamili. Imani yetu haitokamilika bila kuelewa ukweli huu. Imani ya kweli huja tu kwa kuelewa ushuhuda wa wokovu wa Yesu, Injili ya ondoleo la dhambi na Yesu kuwa Mwokozi wa kweli kwa wanadamu.
Nini basi imani ya anayemdhihaki Yesu ilivyo? Hebu na tuone.
 

Imani ya dhihaka kwa Yesu

Nini tunachohitaji 
katika Imani?
Kujua kwa uhakika juu ya 
Ubatizo wa Yesu.

Unapasa kuelewa kwamba kumwamini Yesu pasipo kwa undani ni sawa na kumdhihaki. Ukidhani ya kwamba “naona ni vigumu kuamini, na kwa kuwa yeye ni Mungu na ni Mwana wa Mungu inanilazimu kuamini hata hivyo” hapo ndipo unapo mdhihaki Yesu. Ikiwa unahitaji kuokoka kwa uhakika, huna uchaguzi zaidi ya kuamini ubatizo na damu ya Yesu, Injili ya ondoleo la dhambi.
Kumwamini Yesu pasipo kujua juu ya Injili ya ondoleo la dhambi ni hatari zaidi kuliko kutomwamini kabisa. Kuhubiri Injili ya damu ni kufanya kazi ya bure pasipo kuelewa ukweli.
Yesu haitaji mtu yeyote azunguke na kuhubiri juu ya kumwamini yeye kijuu juu, au kuwa na imani pasipo na sababu. Anatutaka tumwamini kupitia kujua Injili ya ondoleo la dhambi. 
Tunapomwamini Yesu yatupasa kukubali ya kwamba Injili ya ondoleo la dhambi ndiyo ubatizo na damu ya Yesu tunapomwamini Yesu, yatupasa kuelewa vyema Injili hii kupitia Neno lake na kujua kwa makini namna alivyo zisafisha dhambi zetu zote.
Yatupasa pia kujua nini maana ya rangi za samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa kilicho matangoni mwa madhabau takatifu inasimama badala ya nini. Hapo ndipo tutakapo weza kuwa na imani ya kweli ambayo itadumu milele maishani.
 

Hatutoweza kuzaliwa upya bila ya kumwamini Yesu, Ukweli wa Samawati, Zambarau na nyekundu katika kitambaa

Makuhani walifanya nini kabla
Ya kuingia pahala patakatifu?
Walisafisha mikono na miguu kwa
Maji yaliyomo katika
Birika la shaba.

Bwana wetu Yesu alituokoa. Hatuna budi zaidi ya kumsifu Bwana pale tunapo ona namna aliyo tuokoa kwa ukamilifu. Yatupasa kuangalia katika madhabau takatifu. Ametupatia maneno ya Injili ya ondoleo la dhambi kupitia Samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa cha madhabau takatifu na kutuokoa kwa hayo. Tumshukuru na kumsifu Bwana. 
Wenye dhambi wasingeweza kuingia mahala patakatifu bila ya kupitia hukumu ya kutisha. Ni vipi mtu angeingia mahala patakatifu bila ya kuhukumiwa dhambi zake? Hii isingewezekana. Ikiwa mtu huyo angeingia sehemu iliyo katazwa angepatwa na kifo mahala hapo na wakati huo. Ingekuwa angamizo kubwa. Mwenye dhambi asingeweza kuingia mahala patakatifu na kuweza kuishi tena.
Bwana wetu ametuokoa kwa kupitia ificho wa siri katika malango ya madhabau takatifu. Kwa rangi za kitambaa cha samawati, zambarau na nyekundu na nyuzi za hariri zilizo fumwa, hakika alituokoa sisi sote. Alitueleza siri ya wokovu kupitia vitu hivi.
Je, mimi na wewe hatukuokolewa kupitia hivyo? Ikiwa hatutoamini maneno yatokanayo na samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa, hapatakuwa na wokovu mwingine tena kupitia Injili ya ondoleo la dhambi. Rangi ya samawati haiwakilishi Mungu; inasimama badala ya ubatizo wa Yesu pekee. Ni ubatizo wa Yesu ambao ulio zichukuwa dhambi zetu zote.
Mtu ataweza kuingia katika madhabau ya sadaka za kutekelezwa bila ya kuamini kitambaa cha samawati. Isipokuwa hawezi kuingia pahala patakatifu alipo kaa Mungu.
Hivyo kabla ya kuingia malangoni pa mahala patakatifu pa madhabau yatupasa kuamini katika rangi ya samawati katika kitambaa (ubatizo wa Yesu) kitambaa chekundu (Damu yake msalabani) na zambarau (Uungu wa Yesu na mwana wa Mungu). Ikiwa tu tutaamini tutakubalika naye na kukubalika kuingia kupitia pazia la mahala patakatifu pa patakatifu.
Wengine huingilia ukumbi wa nje na kufikiri kwamba wamo ndani. Lakini huu si wokovu. Namna gani inatupasa tuokolewe? Yatupasa kuwa na uwezo wa kuingia patakatifu pa patakatifu.
Ili kuweza kuingia pahala pa patakatifu pa patakatifu yatupasa kupitia katika birika la shaba. Birika la shaba linawakilisha ubatizo wa Yesu na yatupasa kusafisha dhambi zetu za kila siku kwa ubatizo wa Yesu na kutakaswa ili tuingie pahala patakatifu.
Katika Agano la Kale, kuhani ilimpasa kujisafisha kabla ya kuingia patakatifu na katika Agano Jipya, Yesu alisafisha miguu ya wanafunzi ili kuonesha kuwa alikwisha safisha makosa yao yote katika maisha yao.
Sheria ya Mungu inanena “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23). Mungu humhukumu mtu kwa dhambi pasipo msamaha, lakini alipitisha dhambi hizo kwa Mwana wake na kumhukumu yeye badala yetu. Huu ndiyo upendo wa Mungu, wokovu wake. Wokovu wa kweli hupatikana tu pale tunapoamini Injili ya ondoleo la dhambi linalo jumuisha ubatizo, damu, kifo na ufufuo wa Yesu.
 

Ili uweze kuzaliwa Upya, yakupasa kutodhihaki ukweli wa kibiblia, Injili ya ondoleo la dhambi

Nini kilicho baki 
kwetu kufanya?
Ni kuamini Injili, neno la 
maandiko ya Mungu.

Sikuwahi kumdhihaki mtu. Ikiwa mtu Fulani atazungumza juu ya jambo Fulani ambalo silielewi, nitauliza kwa unyenyekevu ili amuelezee kwa undani. Lakini niulizapo juu ya matumizi ya madhabau takatifu, hakuna aliyewahi kunipa jibu.
Hivyo nifanye nini? Ndipo ilinibidi kuirudia biblia. Katika biblia ni wapi imeelezewa juu ya jambo hili? Imeelezewa kwa undani katika kitabu cha kutoka. Ikiwa mtu atasoma kitabu hiki kwa makini, ataweza kuelewa maana yake kupitia neno la maandiko ya Mungu.
Rafiki wapendwa, hauwezi kamwe kuokoka kwa kuamini pasipo uangalifu juu ya Yesu. Huwezi kuokoka kwa kuhudhuria mara kwa mara ibada za kanisa. Tunaelewa kwamba Yesu alimwambia Nikodemo “Amin, amin nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu, Je! wewe u mwalimu wa Israeli na mambo haya huyafahamu” (Yohana 3:5, 10).
Wote wamwaminio Yesu yawapasa kuamini juu ya kitambaa cha samawati (dhambi zote za ulimwengu alitwikwa Yesu alipobatizwa). Kitambaa rangi nyekundu (kifo cha Yesu kwa dhambi zetu zote) na zambarau (Yesu ni mwokozi, Mungu na mwana wa Mungu).
Yatupasa kuamini kwamba Yesu ni mwokozi wa wote wenye dhambi ulimwenguni. Bila imani hii, mtu hawezi kuzaliwa upya hata kuingia mahala patakatifu katika ufalme wa Mungu mtu vile vile hawezi kuishi kwa uaminifu hapa ulimwenguni bila haya.
Je, ingekuwa ni rahisi vipi ikiwa mtu atazaliwa upya kwa kuwa na imani na Yesu? – Ndiyo upo wimbo usemao “♫Umeokolewa, nimeokolewa sote tumeokolewa. ♫” Ni vyema! Lakini wapo walio na imani kwa Yesu bila ya kuokolewa kwa kuzaliwa upya.
Yatupasa kujua ukweli katika Biblia pamoja na kuwa na imani na Yesu. Yatupasa kuelewa juu ya Injili ya ondoleo la dhambi katika biblia na maana ya rangi za samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa ili tuweze kuingia madhabau takatifu na kuwa na Mungu katika ulimwengu wa imani. Ndani ya madhabau ya imani, tutaweza kuishi kwa furaha hadi muda ambao Yesu atakapo kuja tena kutupeleka katika ufalme wake. Ni muhimu kwetu kumwamini Yesu katika njia sahihi.
 

Injili halisi ilianza kwa utakaso wa kitambaa cha rangi ya samawati

Nini sharti lisilo kwepeka 
katika wokovu wetu zaidi 
ya msalaba wa Yesu?
Ubatizo wa Yesu.

Watu kufikiri kwamba wataweza kuishi kwa ukamilifu pasipo kutenda kosa. Ingawa kwa kujibidisha huko kutenda mema, ndipo kwa kiasi hicho hugundua udhaifu wao zaidi. Wanadamu hawana ukamilifu na hivyo si rahisi kwao kutotenda dhambi. Kwa namna hiyo basi Yesu alituokoa kwa rangi ya samawati, zambaru na nyekundu katika kitambaa, Injili ya upatanisho ili tuweze kutakaswa na kuingia patakatifu pa Mungu.
Ikiwa Mungu asingetuokoa kwa rangi hizo tusingeweza kamwe kuingia pahala patakatifu kwa uwezo wetu. Nini sababu ya hili? Ikiwa kwa wale pekee wenye kuishi kimakini katika mwili wangeweza kuingia patakatifu, basi pasingekuwepo hata mmoja angeweza kuhitimu. Ikiwa mtu atamwamini Yesu bila kufahamu ukweli wa Injili, basi ataongeza dhambi juu ya moyo wake.
Yesu alituokoa kwa ubatizo wake ulio makini katika mpango wa wokovu, wokovu wa Samawati zambarau na nyekundu katika kitambaa na nyuzi nzuri za hariri zilizofumwa. Alisafisha dhambi zetu zote Je, unaamini hilo? – Ndiyo – Je, unao ukweli juu ya Injili ya ondoleo la dhambi ndani ya moyo wako na kuwa na ushuhuda juu ya hilo? – Ndiyo –
Ikiwa utakuwa na ushuhuda wa injili utaweza kuwa katika paji la uso vibao vya dhahabu visemavyo “MTAKATIFU KWA BWANA” na kujiunga na “Makuhani wakuu” (1 Petro 2:9). Na ikiwa tu, utaweza kusimama mbele ya watu na kuwalezea kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu, ufanyaye kazi kama kuhani mkuu.
Kilemba cha Kuhani Mkuu kilikuwa na vibao vya dhahabu na vilifungwa kwa kamba za samawati. Kwa nini samawati? Kwa sababu Yesu alituokoa kwa Injili ya ondoleo la dhambi lililochukua dhambi zetu zote na kutufanya tusio na dhambi kwa ubatizo wake. Ubatizo katika Agano Jipya ni sawa na kuwekea mikono katika Agano la Kale.
Haijalishi ni kwa namna gani ya uangalifu na uaminifu tuaminivyo katika Yesu tusingeweza kupata tuzo ile iliyo andikwa kwa kugongwa muhuri “MTAKATIFU KWA BWANA” bila ya kugundua siri ya maneno katika rangi za samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa.
Ni kwa namna gani tunakuwa wenye haki? Imeandikwa katika Mathayo 3:15 “Yatupasa kuitimiza haki yote.” Yesu alibatizwa na kutuokoa sisi sote toka dhambini. Kwa ubatizo wake, alibeba dhambi zetu zote, nasi wenye kuamini tumefanywa wenye haki.
Ni vipi basi tutaweza kusema hatuna dhambi ikiwa hapajakuwepo ubatizo wa Yesu? Hata ikiwa tunamwamini Yesu na kupiga kelele tukidhani kwa kufikiri juu ya kiffo chake pale msalabani, machozi yote ya ulimwengu yasingeweza safisha dhambi zetu zote. Kamwe Haijalishi na kwa kiasi gani tutaweza kulia na kutubu, dhambi zetu zitabaki nasi.
“MTAKATIFU KWA BWANA.” Ikiwa Yesu amebeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na damu Bwana ameturuhusu dhambi zetu zote sisi kuweza kutwikwa juu yake na kuwa neno la wokovu liliwekwa kumbukumbu katika Biblia, tumekuwa wenye haki kwa imani, bila kujali makosa yetu na udhaifu.
Hivyo, tunaweza kusimama mbele za Mungu. Tutaweza sasa kuishi kama wenye haki na kuhubiri Injili ulimwenguni upo wimbo usemao “♫Nimeokolewa, umeokolewa, sote tumeokolewa.” Tumeokolewa kutokana na rehema za Mungu katika mpango wake.
Bila neno la Injili ya ondoleo la dhambi ndani ya moyo, hakuna wokovu, haijalishi bidii utakayo jaribu. Ni sawa na wimbo Fulani wa Korea mashuhuri usemao “Oh moyo wangu unadunda haraka bila ya sababu kila nimwonapo, kila wakati nipo karibu naye. Bila shaka mtakuwa mwenye upendo usio tulia.” Moyo wangu unadunda haraka, bali si wake. Upendo haurudishwi. Kwa bahati mbaya, wapo wakristo wengi bado wanao upendo usiotulia mbele ya Mungu.
Watu hudhani wokovu huja katika njia mbali mbali toka kwa watu mbalimbali. Huuliza “Kwani uje kwa Injili ya ubatizo pekee?” Lakini usingeweza kuwa wokovu ulio kamilika ikiwa usingekuwepo Injili ya ubatizo wa Yesu. Ni njia pekee tuwezayo kupata haki mbele za Mungu kwa sababu ni njia pekee ituwezeshayo kutakaswa na dhambi zetu zote.
 
 
Ni wokovu gani wa Samawati ambao Yesu ametupatia?

Nini kilicho tufanya
Kuwa wenye haki?
Injili ya Samawati, zambarau 
na nyekundu katika
kitambaa.

Wokovu kupitia Injili ya Samawati, zambarau na nyekundu katika kitambaa ni zawadi ya Mungu kwa wanadamu wote. Zawadi hii imetufanya sisi tuweze kuingia madhabau takatifu na kuishi maisha ya amani. Imetufanya kuwa wenye haki na kutuwezesha kuishi ndani ya Kanisa na kuwa chini ya mafundisho ya maandiko matakatifu kupitia Kanisa.
Tunapo kwenda mbele za Mungu kila mara, katika sala, Injili hii hutubariki katika upendo wa Mungu. Na hii ndiyo maana wokovu ni wenye thamani kwetu. Yesu anatueleza tujenge nyumba ya imani “juu ya mwamba.” Mwamba huo ni Injili ya ubatizo wa Yesu. Yatupasa sote tuokolewe kuishi na wokovu, kwenda mbinguni, kupata maisha ya milele na kuwa wana wa Mungu.
Rafiki wapendwa kwa sababu ya Injili hii ya upatanisho tumeweza kuwa na uwezo wa kuingia madhabau takatifu kwa imani. Kwa kuwa tumesafishwa dhambi zetu zote (ubatizo wa Yesu) na hukumu ile msalabani, basi tumeokolewa kwa Imani katika Injili ya ubatizo wa Yesu.
Utele wa upatanisho wa dhambi zetu zote, ubatizo wa damu ya Yesu, ni Injili iliyosafisha dhambi zetu zote. Je, unaamini hili? Injili ya kweli ni Injili itokayo mbinguni kwa upatanisho uliosafisha kwa ukamilifu dhambi zetu zote.
Tumezaliwa upya kwa kuamini Injili ya upatanisho, Yesu ametupa Injili hii iliyosafisha dhambi zetu zote za kila siku na hata zile zijazo. Bwana asifiwe. Haleluya!
Injili ya maji na Roho (Injili ya maji na damu) ni Injili ya kweli iliyokamilika na kuhubiriwa na Yesu Kristo. Kitabu hiki kiliandikwa kubainisha siri ya Injili ya Yesu, Injili ya maji na Roho.
Kwa kuwa watu wengi humwamini Yesu bila kujua kikamilifu ukweli, sasa leo hii hujigamba kwa nafsi zao kuwa ni wenye ukereketwa au wenye udini katika ulimwengu wa thiologia za Kikristo (wenye kuitwa wanafilosofia wa kitheologia) kwa ufupi, huishi kwa taabu na kuchanganyikiwa. Hivyo yatupasa kurudi hatua nyuma na kuamini Injili ya kweli. Bado hujachelewa! 
Nitakwenda kwa undani zaidi katika kitabu cha pili kwa wale wenye maswali juu ya Injili ya kuzaliwa upya katika maji na Roho.