Search

Ujumbe kutoka kwa Wafanyakazi Wenza

Ikiwa wewe ni mfanyakazi mwenzangu na ungependa kutuma ujumbe na picha kwa "Ujumbe kutoka kwa Wenzako", bonyeza kitufe cha "Tuma ujumbe", na uingie. Chapisho lako litaonekana tu baada ya kuidhinisha

Tuma ujumbe
Jumla 1
 • Nambari 1

  INJILI YA MAJI NA ROHO IMEFUNGUA MACHO YANGU YA KIROHO;

  Nimekuwa nikitamani sana kujua ukweli wa wokovu wa mwanadamu,na uhakika kuurithi ufalme wa Mungu.Kama ilivyokawaida ya Mkristo yeyote anayemwabudu na kumtumikia Mungu,Nilijitahidi sana kwa juhudi nyingi na maarifa ya kibinadamu ili angalau kumfanya Mungu wangu anione nikiwa safi mbele zake.Lakini kila nilipojaribu hayo yote,nilijikuta bado ninamapungufu mengi sana,Na hata kufikia kukata tamaa na kuona hakuna haja ya kusali,Kweli nilijiona mimi sifai kabisa kila mara.Mwaka wa 2007 nikiwa katika kibanda cha huduma za kimtandao nikituma barua pepe kwa rafiki yangu,Nilikutana na tovuti hii ya www.bjnewlife.org na baada ya kuifungua niliona nuru ya ajabu sana,macho yangu yalifunguliwa na kugundua kuwa kumbe Tayari Yesu alikwisha beba dhambi zangu zote kupitia Ubatizo alioupokea katika mto Yordani kupitia kwa Yohana Mbatizaji,na kisha kufa msalabani,Hakika hili ni Pendo kuu mno.Ninamshuku Mungu kwa baraka hizi ambazo ametupatia,Ahsante pia kwa Mchungaji Paul C.Jong kwa mafundisho mazuri ambayo yamenifanya huru kweli kweli.Mungu awabariki nyote na awatunze siku zote mbawani mwake.Ndimi katika Shamba la BwanaEllys Mpanilehi, Tanzania( Sema Biblia Ministries)

  • Ellys Mpanilehi
  • Tanzania, United Republic of
  • 10/31/202167