Search

Uhakiki wa Vitabu

Watu ambao wamesoma vitabu vyetu wametuma hakiki zifuatazo. Ni matumaini yetu kwamba kupitia wao, nyote mtashirikiana kila mmoja neema ya Mungu ambayo imetuwezesha kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Chapisho lako litaonekana tu baada ya kuidhinisha.

Tuma ujumbe
Jumla 2
 • Nambari 2

  kuomba vitabu

  Mimi ni liokoka lakini sikuwahi kuona Mtu yeyote ambaye alinifundisha na kuninyesha ukweli na kufungua ukweli mwanzo sikuelewa Mpaka pale nilipo Kutana na vitabu vya Paul c jong ambavyo vilifanya badiliko kubwa lakini kiu yangu ilikuwa kupata vitabu vingine box 201 Tanzania mkoa Mara wilaya tarime naomba munitumie asante 

  • Elisha Samweli
  • Tanzania, United Republic of
  • 05/05/2021109
 • Nambari 1

  Book review-TYhe Love o f God Revealed through Jesus,The only begotten Son(I)

  Kuna falsafa moja ya Kiswahili isemayo " Kwa mantiki hiyo basi, kitabu hiki ni cha msingi sana kutoka na na ukweli kwamba mafundisho yake yanafunua mpango wa Mungu wa upendo kwa wanadamu wote wakaao juu ya uso wa dunia.    Hakuna mtu aliyemwamini Yesu akashindwa kumjua Mungu na mapenzi yake kwa binadamu, mataifa, na hata viumbe wengine.Kwa maelezo mengine ni kwamba tukitaka kumtambua mungu ni lazima kwanza tumtambue na kumwamini yesu kama Bwanna mwokozi wetu aliye tuonyesha pendo lake la dhati kwa kutufilia msalabani na kufufuka toka kwa wafu. Hii ni kanuni ya kibiblia isiyopaswa kupingwa ama kutiliwa mashaka na mtu awaye yote anayeujua na kuuthamini upendo wa Mungu kikwekikweli.   Kitabu hiki kupitia Rev. Paul C.Jong kimetoa fafanuzi ambazo zinakubalika na mazingira ya kitabu hiki cha Yohana kilipoandikwa ikiwa ni pamoja na mwandishi, wapokeaji,hali halisi ya mambo ilivyokuwa, siasa, lugha na utamaduni. Pia kinahusisha mazingira ya watu wa sasa kwa kutambua kuwa yesu ni uzima wa waaminio bila kujali taifa , lugha elimu au kabila.    Kumwamini Yesu Kristo kuwa ndiye Bwana, masiha mwana wa Mungu aliye hai aliyekuja kwa Maji na Roho ndiyo sharti ya kuupokea upendo wake Mungu usio na kifani uliofunuliwa kwetu kupitia Yesu Kristo.Hata hivyo napenda kutanabaisha kuwa, japokuwa yesu alizaliwa na kuonekana kama mwanadamu bado anabaki kuwa Mungu kutokana na ushahidi tunaoupata kunpitia (Yohana 1:1)Katika kusoma kitabu kiki nimebaini kuwa pendo la Mungu kwa wanadamu lina umuhimu wa aina tatu: 1.Ni msingi wa wokovu wa mwanadamu 2.Ni njia ya kumtambua Yesu na Mungu  3.Ni sababu ya Mungu kusamehe dhambi za wanadamu 4.kuthihirisha thamani ya mwanadamu mbele za Mungu na Ulimwengu 5.Kutangaza haki na hukumu ya Mungu kwa wanaokaidi kumwamini yesu katika pendo lake kupitia injili ya Maji na Roho.   Ni dhahiri kuwa hakuma mwanadamu mwenye dhambi anayeweza kumfikia Mungu bila kupitia Yesu kristo. Hivyo basi ni jukumu letu sote tulioijua kweli kupitia injli ya Maji na Roho kumtangaza Yesu kristo kwa mataifa yote kuwa yeye ndiye ufunuo halisi wa Mungu; kwa pendo lake wanaomwamini katika kweli hawatapotea kamwe.  Nawatakia wasomaji wote baraka na uvuvio wa Mungu mnapoendelea kusoma kitabu hiki hakika mtazidi kuyajua mapenzi ya Mungu kuwa mpo hai leo duniani, kwa ajili ya Yesu aliye ufunuo na chapa halisi ya Mungu. Yatupasa kueneza ukweli huu kwa wengine tukianza na familia zetu, jamii tunazoishi, nchi zetu na adui wanaoupinga ukweli huu.  Bwana na azidi kuitwa Ebenezer-Amen  James A. makulla  NLM Tanzania phone + 2550712673222

  • James Anthony M.loya
  • Tanzania, United Republic of
  • 05/01/2021103