Search

Masharti ya Kibiblia

Maelezo Mafupi ya Baadhi ya Masharti ya Kibiblia

Imehusishwa na Injili ya Maji na Roho

 • 1. Dia

  Kutolewa kwa mali au mtu kwa kulipia thamani inayodaiwa. Thamani au malipo ya fedha yanayodaiwa kutolewa. Mara nyingi hutumika kama uwakilishi wa moja kwa moja katika ukombozi (mfano Kutoka 21:30; kiasi cha fedha; Hesabu 35:31-32, Isaya 43:3 “dia’’). Katika Agano Jipya, Mathayo 20:28 na Marko 10:45 yaeleza kafara kama “malipo ya fedha.”

 • 2. Patana, Upatanisho

  Tendo la ibada katika kutwika dhambi za wanadamu wote kwa Yesu. Katika Agano la Kale upatanisho ulikuwa ni kutwika dhambi zote kwa sadaka ya mnyama kwa kuwekea mikono juu ya kichwa cha mnyama huyo. Katika Agano Jipya, maana yake ni ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatizaji. Kwa Kiebarania na Kigiriki neno hili humaanisha kutwika dhambi juu ya Yesu Kristo ili wenye dhambi waweze kuingia kwenye haki ya mahusiano na Mungu. Agano Jipya linaeleza juu ya kutolewa sadaka kwa upatanisho kwa uwazi; ubatizo wa Yesu na Kifo chake Msalabani.
  Katika Agano la Kale: Neno “upatanisho” limetumika zaidi ya mara 100 na mara zote limeelezea kama (Walawi 23:27, 25:9, Hesabu 5:8) ‘kaphar’ Kiebrania (kila mara huandikwe kama “kufanya upatanisho”) Upatanisho ni tafsiri ya neno la Kiebrania lenye maana kamili ya kutwika dhambi kwa kuwekewa mikono juu ya kichwa cha mbuzi na kuzitamka juu yake maovu yote ya waisraeli (Walawi 16:20).
  Katika Agano Jipya: Upatanisho unahusishwa katika Karamani ‘Kpr’ ikiwa na maana ‘kufunika’. Maana yake upatizo wa ukombozi wa Yesu katika Agano Jipya. Yesu alikuja ulimwenguni na kubatizwa akiwa na umri wa miaka 30 ili kutimiza ukombozi wa wanadamu wote.

 • 3. Upatanisho wa Kibiblia

  A. Katika Agano la Kale, upatanisho kwa kawaida ulipatikana kwa kupitia mnyama wa sadaka (Mf. Kutoka 30:10, Walawi 1:3-5, 4:20-21, 16:6-22).
  B. Katika Agano Jipya maana ya sadaka ya upatanisho katika Agano la Kalle ilikuwa ni msingi uliwekwa, lakini ukombozi wa wanadamu ungeweza kukamilishwa tu endapo mwili wa Kristo Yesu ungetolewa kwa kufa kwa ajili ya dhambi zetu (1 Wakorintho 15:3).
  Neno upatanisho halikutumika tu katika kumaanisha kifo cha Kristo kulipia dhambi ya asili, bali ilikuwa pia kubeba dhambi zote za wanadamu. Baada ya ubatizo ambao dhambi zote za ulimwengu zilitwikwa kwake Yesu (Mathayo 3:15), aliokoa wanadamu wote kwa kuitoa damu yake msalabani. Walawi 1:1-5, Yahana 19:30).
  Mtume Paulo ameelezea katika 2 Wakorintho 5:14 kwamba “mmoja alikufa kwa ajili ya wote” ndipo basi katika mstari ufuatao wa 21 inaelezea kwamba ilikuwa “ni kwa ajili yetu”. Ni mistari michache katika Agano Jipya hufananisha na Yesu kama Sadaka (mf. Waefeso 5:2); Yohana 1:29, 36 (Mwanakondoo – Yohana Mbatizaji) na 1 Wakorintho 5:7 (pasaka wetu – Mtume Paulo).
  Hata hivyo, Paulo ameweka bayana kwamba ubatizo wa Yesu katika mto Yordani ulikuwa ni upatanisho wa dhambi zote za ulimwengu. Ameelezea katika Warumi 6 kwamba dhambi zote za ulimwenguni alitwikwa Yesu kwa kupitia ubatizo wake na Yohana Mbatizaji.
  Ameendelea kuelezea juu yake kusulubiwa kwa Yesu kuwa ni hukumu na fidia kwa dhambi zetu na ya upatanisho ilitolewa kwa roho za watu wote.
  Kifo cha Yesu kilikuwa ni utambulizi wa mpango wa Mungu unao onyeshwa katika sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale. Kuwekea mikono katika Agano la Kale na ubatizo wa Yesu katika Agano Jipya ni kulingana na sheria ya Mungu. (Isaya 53:10, Mathayo 3:13 –17, Waebrania 7:1-10, 18 1 Petro 3:21).
  Agano Jipya haliishii hapo tu na ubatizo na kifo cha Yesu, bali linakwenda zaidi kwa kutuelezea juu ya kutimizwa kwa wokovu kwa kubatizwa kwetu katika Kristo, ambapo kunatuwezesha sisi binafsi kufa na Yesu (Warumi 6:3-7, Wagalatia 2:19-20).
  Inatuelezea kuwa Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu Kristo ili kubeba dhambi zetu zote za ulimwengu na kwa matokeo hayo alisulubiwa. Yesu Kristo kwa kupitia ubatizo wake na damu yake si pia alitakasa dhambi za ulimwengu, bali pia aliokoa kila mmoja wetu toka nguvu za shetani na kuturudisha katika nguvu za Mungu kwa kukubali adhabu na kuvumilia maumivu kwa niaba ya wanadamu wote.
  Hivyo ukombozi wa Yesu umesuluhisha tatizo la dhambi lililoweka kizuizi kwa wanadamu kutoweza kuwa karibu na Mungu. Tendo hili la kihistoria la muda limerudisha amani na utulivu kati ya wanadamu na Mungu kwa kuleta wokovu, furha (Warumi 5:11), uzima (Warumi 5:17-18) na ukombozi (Mathayo 3:15, Yohana 1:29, Waebrania 10:1-20, Waefeso 1:7, Wakolosai 1:14) katika wakati mmoja.

 • 4. Siku ya Upatanisho

  Kiebrania ni umaanisho wa siku ya “kufunika au “kusuluhisha”. Sehemu muhimu ya siku ya Wayahudi ilikuwa ni siku ya Upatanisho katika siku ya kumi ya mwezi wa saba (Walawi 23:27, 25:9). Tunaweza kuona katika walawi 16 kwamba hata Kuhani Mkuu hakuruhusiwa kuingia Patakatifu pa Patakatifu isipokuwa katika ibada iliyo tengwa katika siku hiyo.
  Upatanisho pia ulihitajika kabla ya kuingia patakatifu pa patakatifu, na pia ulihitajika kwa Wana wa Israeli; kwa njia hii, ndipo Kuhani mkuu aliweza kutoa sadaka ili aweze kutwisha dhambi kwa kuwekea mikono juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka. Waisraeli walfikiri juu ya utakatifu wa Mungu na juu ya dhambi zao katika Siku hiyo ya Upatanisho.
  Katika muda huo, kwa kiasi cha sadaka 15 (ikijumuishwa na Azazeli) 12 sadaka ya kuteketezwa na 3 sadaka ya upatanisho walitolewa kwa Mungu (Walawi 16:5-29, Hesabu 29:7-11). Ikiwa tutahesabu “mwana kondoo mwingine” aliyetajwa katika Hesabu 28:8 zipo sadaka 13 za kuteketezwa na 4 za upatanisho.
  Siku Waisraeli waliyokuwa wakitoa sadaka ya upatanisho kwa dhambi za mwaka ilikuwa ni siku ya kumi katika mwezi wa saba. Kwa jinsi hiyo hiyo siku ya upatanisho wa dunia ilikuwa ni siku ile Yesu alipobatizwa na Yohana Mbatizaji. Hakika ilikuwa ni siku ya upatanisho wa wanadamu. Ilikuwa ni siku ya Mungu kutakasa dhambi zote za wanadamu ulimwenguni (Mathayo 3:13-17). Ilikuwa ni siku ya Upatanisho ambayo Mungu “alitimiza haki zote.”

 • 5. Sadaka ya Upatanisho

  Katika Agano la Kale: kama ilivyo sadaka nyenginezo, sadaka ya utakaso wa Waisraeli wote ilitolewa katika madhabahu Kuhani Mkuu alijitakasa yeye binafsi kwanza na kuvaa vazi lile takatifu badala ya vazi lile la kawaida la ibada, alichagua ndama dume kwa sadaka ya dhambi na kondoo dume kama sadaka ya kuteketezwa kwa matoleo yake binafsi na nyumba yake (Walawi 16:3-4). Kuhana Mkuu aliweka mikono yake juu ya kichwa cha kila mmoja wa sadaka hizi ili kutwika dhambi za mwaka za watu wake.
  Kuwekea mikono kulikuwa ni jambo muhimu katika siku ya upatanisho. Kama isingefanyika matoleo ya sadaka hizo yasingeweza kufanyika kwa kuwa upatanisho wa dhambi usingekamilika bila kuwekewa mikono, hivyo ndivyo kutwika dhambi za mwaka za Waisraeli juu ya sadaka ya dhambi.
  Katika Walawi 16:21 “Na haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi kasha atanipeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.”
  Alichukuwa mbuzi wawili na kondoo dume kama sadaka ya kuteketezwa kwa watu (Walawi 16:5). Na ndipo aliwatoa mbele za Bwana katika malango ya madhabahu na kupiga kura ili kuchagua moja wa Bwana na mwingine kuwa Azazeli.
  Yule mmoja wa Bwana alitolewa akiwa hai mbele za Bwana kupatanisha kwa dhambi za mwaka za Waisraeli na kupelekwa jangwani (Walawi 16:7-10).
  Dhambi za Israeli zilipaswa kutwikwa kwa azazeli kwa kuwekewa mikono na Kuhani Mkuu ndipo azazeli aliyebeba juu yake dhambi zote za Israeli alipopelekwa jangwani kwa kusulihisha watu na Mungu. Hivi ndivyo dhambi za mwaka zilivyotakaswa.
  Katika Agano Jipya: kwa namna hiyo, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji (kwa kuwekewa mikono katika Agano la Kale) na kubeba dhambi zote za ulimwengu akiwa kama mwanakondoo wa sadaka ili kutimiza wokovu wa Mungu (Walawi 20:22, Mathayo 3:15, Yohana 1:29, 36).
  Katika Agano la Kale kabla ya kupiga kura Haruni alimchinja ndama dume kama sadaka ya dhambi kwa ajili yake na nyumba (walawi 16:11). Na baadaye kuchukua chetezo kilichojaa makaa ya moto toka altare mbele ya Bwana huku mikononi akiwa amebeba uvumba wa kunukia, uliosagwa na kuwa laini, na kuchukua nyuma ya pazia. Baadaye aliweka uvumba huo juu ya chetezo yenye makaa ya moto mbele ya Bwana ili wingu la moshi wa uvumba liweze kutanda juu ya kiti cha rehema. Pia alichukua kiasi cha damu ya ndama dume na kunyunyizia kwa vidole vyake juu na mbele ya kiti cha rehema mara saba (Walawi 16:12-19).
  Katika siku ya upatanisho, kuwekea mikono kwa Haruni juu ya kichwa cha sadaka kusingeweza kuachwa. Haruni aliweka mikono juu ya kichwa cha mbuzi na kumtwika dhambi zote na uovu wote wa Israeli juu ya kichwa chake. Na ndipo mtu aliye tayari atamchukua mbuzi huyo jangwani na kumwachia huko. Mbuzi huyo wa Azazeli atatangatanga huko jangwani na dhambi za Israeli haki kufa mwishowe. Huu ndiyo mpango halisi wa sadaka ya upatanisho katika Agano la Kale.
  Ni sawa sawa kama ilivyo katika Agano Jipya isipokuwa mbuzi huyo alikuwa badala ya Yesu Kristo beba dhambi zote za ulimwengu juu yake kwa ubatizo wake, na kutokwa damu na kufa msalabani kwa ajili yetu sote.
  Hivyo leo, wokovu toka dhambini hauwezi kuletwa bila ya ubatizo na kusulubiwa kwa Yesu Kristo, Kuhani wa mbinguni aliye mkuu. Hitimisho hili ni la wokovu wa kuzaliwa upya katika maji na Roho.

 • 6. Ibada ya kuwekea mikono

  Huu ulikuwa ni mpango ulioletwa na Mungu kwa ajili ya kutwika dhambi juu ya sadaka ya dhambi katika nyakati za Agano la Kale (Walawi 4:29, 16:21). Katika siku hizo za Agano la Kale, Mungu aliruhusu watu kupatanishwa kwa dhambi zao kwa kuwekea mikono sadaka za dhambi ndani ya madhehebu. Ilikuwa ni kuonyesha jinsi ya ubatizo wa Yesu utakao kuja katika Agano Jipya.

 • 7. Ubatizo

  Ubatizo maana yake ①kusafishwa ② kuzikwa (kuzamishwa) na maana ya kiroho ③ kutwika dhambi kwa kuwekea mikono, kama ilivyofanywa katika Agano la Kale.
  Katika Agano jipya, ubatizo wa Yesu na Yohana Mbatiizaji ulikuwa ni kusafisha dhambi za ulimwengu. “Ubatizo wa Yesu” una maana ya kuchukua dhambi za wanadamu zote, kutakaswa kwa dhambi zote za ulimwengu.
  Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu na Kuhani Mkuu katika uzao wa Haruni, na kubebeshwa dhambi zote za ulimwengu juu yake. Hii ni dhumuni halisi la ubatizo.
  Maana ya kiroho neno “ubatizo” ni “kutwika, kuzikwa”. Hivyo “ubatizo wa Yesu” maana yake dhambi zote alitwikwa Yesu na kuhukumiwa badala yetu. Ili kuokoa wanadamu Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kufa kwa dhambi hizo.
  Yote haya, kifo chake na pia kifo chako na changu wenye dhambi wote ulimwenguni na ufufuko wake ni ufufuo wa watu wote. Kujitoa kwake sadaka ni wokovu wa wenye dhambi na ubatizo ni ushuhuda halisi katika kutusafisha dhambi zetu zote sisi walimwengu.
  Biblia inatueleza “upo mfano wa mambo haya, ambao sasa ni ule ubatizo” (1 Petro 3:21). Ubatizo wa Yesu ni njia ya haki ya kuokoa wanadamu kwa kutakaswa dhambi zetu.
  Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji, mwakilishi wa wanadamu na Kuhani Mkuu katika uzao wa Haruni, na kubebeshwa dhambi zote za ulimwengu juu yake. Hii ni dhumuni halisi la ubatizo.

 • 8. Dhambi

  Kila jambo liendalo kinyume na Mungu ni dhambi. Hii inamaanisha dhambi zote, ikijumuishwa dhambi ya asili na makosa ambayo tutendayo siku zote za maisha yetu kwa jumla.
  Dhambi ni “hamartia” kwa Kigiriki. Na kwa maana ya msemo ni “hamartano” yaani “kukosea kulenga” Hivyo moja ya hatari ya dhambi ni kukosa kumwamini Yesu na hivyo kukosa kuwa na uwezo wa kuokoka. Kutojua au kutoamini ukweli ni kutenda dhambi ya uasi na kuna kufuru Mungu.
  Ikiwa kweli hatupendi kutenda dhambi aina hii mbele ya Mungu yatupasa kuelewa Neno lake na kutambua ukweli kuwa Yesu ni Mwokozi.
  Yatupasa kuamini ubatizo wa Yesu na Msalaba wake kupitia maneno ya Mungu. Ni dhambi kutokubali Neno la Mungu, kupindisha ukweli, na kuamini kanuni potofu.
  Biblia inatuelezea kwamba dhambi iliyo hatari zaidi, “dhambi iletayo kifo” (1 Yohana 5:16) ni kutoamini kwamba Mungu alitakasa ulimwengu wote kwa dhambi. Yatupasa kuamini kuzaliwa kwa Yesu, katika kutusafisha dhambi zetu kupitia ubatizo wake, na katika kutoa maisha yake kwa damu yake pale msalabani. Ni dhambi ikiwa mtu hatoamini maandiko ya neno la Mungu kwamba Yesu alibatizwa, alikufa msalabani na alifufuliwa ili kutuweka huru kwa dhambi zetu zote.

 • 9. Toba

  Ikiwa mtu aliyetengwa mbali na Mungu amegundua hilo juu ya dhambi zake na kumshukuru Yesu kwa kusafishwa na dhambi hizo na kurudi kwa Mungu, hii ni toba.
  Sote sisi tumejawa na dhambi. Toba ya kweli ni kukubali kufuata kweli; kwamba sisi ni wenye dhambi mbele ya Mungu, na hivyo hatuwezi kujizuia kutenda dhambi maishani mwetu na kwenda jahanamu tutakapo kufa hivyo yatupasa kumkubali Yesu kama mwokozi wetu kwa kuamini kwamba alikuja ulimwenguni kutuokoa sisi wenye dhambi na hivyo alibeba dhambi zetu (kupitia ubatizo), akafa na alifufuliwa kutuokoa. Toba ya kweli ni kuacha fikra zetu na kumrudia Mungu (Matendo 2:38).
  Toba ni kukiri dhambi zetu na kulirudia neno la Mungu kukubali wokovu katika maji na kwa damu kwa moyo wetu wote (1 Yohana 5:6).
  Toba ya kweli ni kukubali wenyewe kwamba sisi ni wenye dhambi kabisa na kumwamini Yesu, Mwana wa Mungu kama Mwokozi wetu aliye tuokoa na dhambi zetu zote. Ili tuweze kuokolewa na kusafishwa dhambi zetu zote, yatupasa kuacha kujaribu kujitakasa kwa kupitia matendo ya sheria, na kukiri kwamba sisi ni wenye dhambi mbele ya Mungu na sheria yake, sisi basi yatupasa kukubali kweli ya wokovu wa Yesu, Injili ya maji na Roho, ambayo Yesu alituachia kwa ubatizo na damu yake.
  Mwenye dhambi yampasa kuacha mawazo yyake na kumrudia Yesu kikamilifu. Tutaokolewa pale tutakapo amini ubatizo wa Yesu uliozichukua dhambi zetu zote kwake.
  Kwa maneno mengine, ubatizo wa Yesu, kusulubiwa kwake, na ufufuko wake umetimiza haki ya Mungu wokovu wa wenye dhambi. Yesu alikuja katika mwili, alibatizwa na kusulubiwa ili kutusafisha kwa dhambi zetu zote. Kwa kuwa na imani iliyo kamili katika yote haya na kuamini kwamba Yesu alifufuka ili awe Mwokozi wa wote wenye kumwamini katika toba ya kweli na imani ya halisi.

 • 10. Wokovu

  Wokovu katika Ukristo maana yake ni “ukombozi toka kwenye nguvu au adhabu ya dhambi.” Tunapokea wokovu pale tunapokiri kwamba hatuna uwezo kujizuia kwenda motoni na kumwamini Yesu ametuokoa sisi sote toka dhambi zetu zote kwa kupitia kuzaliwa wake, ubatizo na damu yake msalabani.
  Wale wasio na dhambi kwa kuamini wokovu wa Yesu, ubatizo na damu ya Yesu huitwa “walio okoka, waliozaliwa upya, wenye haki.”
  Tunaweza kutumia neno “wokovu” kwa wale wote walio okolewa tokana na dhambi zao, pamoja na hata zile za asili na zile za kila siku, kwa kumwamini Yesu. Kama alivyo mtu aliyejongea kwa Mungu, yule ajongeaye dhambi za ulimwengu atakuwa ameokolewa kwa kumwamini Yesu kama mwokozi, kwa kuamini ubatizo na damu, maneno ya kweli ya kiroho.

 • 11. Kuzaliwa upya

  Maana yake “kuzaliwa mara ya pili” Mwenye dhambi atazaliwa upya na kuwa mwenye haki ikiwa ataokoka kiroho kwa kuamini ubatizo wa Yesu na Msalaba wake. Tutaweza kuzaliwa upya kiroho kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu, waliozaliwa upya ni wale wote aliosafishwa kwa dhambi zao zote na “atatokea mara ya pili pasipo dhambi kwa hao wamtazamiao kwa wokovu” (Waebrania 9:28).

 • 12. Ondoleo la dhambi

  Hili ni jambo muhimu na pia kumaanisha kusamehewa dhambi. Dhambi husamehewa pale tunapotakaswa kwa dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote kupitia Injili ya maji na kwa Roho. Imani katika Injili ya maji na kwa Roho ni kuamini mlolongo wa kweli. Uungu wa Yesu Kristo, hufanywa Mwana wa Mungu, ubatizo wake na kusulubiwa kwa ajili ya wokovu wetu wote na kufufuliwa kwake.
  Ukombozi wa Yesu aliotupa waweza kuwa wetu kupitia imani katika ubatizo na damu kama ulivyo unabii uliotolewa katika Agano la kale, Yesu mwenyewe aliokoa watu wote toka dhambini. Ukombozi katika Biblia unalenga sehemu ya kusafishwa dhambi kupitia imani katika ubatizo wa Yesu na Damu yake. Dhambi zote alitwikwa, Yesu, hivyo kamwe hakuna dhambi mioyoni kwa wanadamu.
  Twaweza kujiita tuliokombolewa na wenye haki pale tu dhambi zetu zote zinapotwikwa kwa Yesu kupitia imani kwa ubatizo wake.

 • 13. Yesu Kristo

  YESU: “Mwokozi aliye okoa watu wote kwa dhambi zao zote na kuadhibiwa nazo” Yesu humaanisha Mwokozi aliye wa pekee mwenye kuokoa watu wote toka dhambini.
  KRISTO: “Mpakwa mafuta” Palikuwapo na watu watatu walioruhusiwa kupakwa mafuta mbele ya Mungu kwa kuteuliwa ① Wafalme ② Manabii ③Na Makuhani. Yesu alikamilika kwa haya yote.
  Yesu Kristo alikuwa yote haya. Alifanya kazi katika yote haya. Yatupasa kuamini kuwa Yesu Kristo ni Mfalme, Nabii na kuhani aliyeleta ukombozi na wokovu. Kwa yote haya tutamwita “Yesu Kristo.” Alikuwa ni Kuhani wa mbinguni aliyetuokoa toka dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo na damu.
  Hivyo, yeye ni Mfalme wa wote wenye kumwamini. Hutufanya kuelewa dhambi zetu pale tunapo kuja mbele zake. Alitufundisha kwamba sisi ni wenye dhambi toka kizazi cha mababu zetu na kwa matokeo haya, tupo chini ya hukumu ya Mungu.
  Yeye pia ametufundisha ya kwamba tumesafishwa dhambi zetu kupitia ubatizo wake na damu. Aliyafanya yote haya kwa ajili yetu sisi wenye dhambi.

 • 14. Sheria ya Mungu. Amri kumi

  Vipo vipengele 613 vya sheria ya Mungu vinavyohusu maisha yetu ya kila siku. Lakini iliyo kuu kati ya hii ni Amri kumi ambazo yatupasa kuzifuata mbele ya Mungu. Yapo maelekezo na maonyo kama vile “Ufanye hivi” na “Usifanye hivi.” Na huu ndiyo mwongozo wa maisha, na amri za Mungu tulizopewa ili tuweze kutambua dhambi zetu. Kupitia Amri zilizo andikwa na Mungu tutaweza kutambua ni kwa kiasi gani tumeacha utii kwake (Warumi 3:19-20).
  Sababu Mungu kutupatia amri zake ilikuwa ni kutufanya tugundue na kuziona dhambi zetu kamwe hatutoweza kuzishika Amri zote, hivyo yatupasa kunyenyekea kwa kukubali ukweli kwamba sisi ni wenye dhambi mbele yake kabla ya kumwamini Yesu. Sisi sote ni wenye dhambi na Mungu anajua kwamba kamwe hatutoweza kuishi kwa kufuata sheria yake. Hivyo, alishuka ulimwenguni kama mwanadamu, alibatizwa na kuhukumiwa msalabani. Kujaribu kuishi kwa sheria ya Mungu ni dhambi ya kiburi. Hatupaswi kufanya hivyo.
  Sheria yatuonyesha ni kwa vipi Mungu alivyo mkamilifu na Mtakatifu na kwa upande mwingine ni kwa jinsi gani mwanadamu alivyo dhaifu. Kwa msemo mwingine, utakatifu na ukamilifu wa Mungu umefunuliwa katika sheria ya Mungu.

 • 15. Mto Yordani, ndipo Yesu alipobatizwa

  Mto Yordani humwagika kuelekea bahari ya chumvi (Dead sea) kina cha Bahari ya chumvi ni takribani mita 400 pungufu usawa wa bahari. Hivyo, maji ya Bahari ya chumvi hayawezi kumwagika sehemu nyingine; yamesimama hapo katika Bahari ya chumvi.
  Chumvi chumvi ya bahari hiyo ni mara 10 zaidi ya ladha ipatikanayo bahari nyingine za kawaida na hivyo hakuna kiumbe chochote chenye kuishi ndani yake. Hivyo ndivyo ilivyoitwa Bahari ya Chumvi (Dead sea). Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika mto wa kifo (Yordani). Hii inawakilisha wanadamu wote, isipokuwa tu wale wasio na dhambi mioyoni mwao, watapatwa na laana ya milele kwa dhambi zao mwishoni.
  Hivyo basi Mto Yordani ni mto wa kusafisha dhambi, mto ambao wenye dhambi hufa. Kwa kifupi, ni mto wa ukombozi ambao dhambi zote za ulimwengu zilisafishwa hapo kwa ubatizo wa Yesu, kubebeshwa kwa dhambi Yesu.
  Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji katika mto wa kifo (Yordani).