Search

Mahubiri

Somo la 6: Wazushi

[6-1] Ukristo Bandia na Uzushi Ndani ya Ukristo (Isaya 28:13-14)

(Isaya 28:13-14)
“Kwa sababu hiyo neno la Bwana kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni, huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma na kuvunjwa na kunaswa na kuchukuliwa. Basi lisikieni neno la Bwana enyi watu wenye dharau mnao watawala watu hawa walio ndani ya Yerusalemu.”
 

MAANA YA UZUSHI KIBIBLIA

Biblia inatafsiri vipi 
maana ya neno “uzushi”?
Biblia inatafsiri uzushi kama moja ya 
dhambi ndani ya moyo wa mtu 
Ingawa anamwamini Yesu.

Wapo waandishi bandia wa makala nyakati hizi hasa katika nchi zilizoendelea. Hujifanya kuwa waandishi wa makala huku wakiwa na nia ya kujipatia vipato toka kwa walengwa wa makala hizo, kwa kuwatishia kutoboa siri zao. Neno bandia maana yake ni kitu au jambo lenye kuonekana kuwa ni halisi hali si kweli. Kwa maneno mengine, lina maana kwa kitu au jambo ambalo ukweli wake ni tofauti na mwonekano wa nje.
Neno “uzushi” na “Bandia” yanatumika mara nyingi katika nukuu za makanisa ya kikristo.
Zipo tafsiri chache halisi za maana ya uzushi na nini maana ya kuwa “bandia” pia wapo wachache wenye kufundisha juu ya mada hizi katika hali iliyo makini kibiblia.
Katika mazingira hayo mimi binafsi nafikiri ninalo jukumu la kuweka wazi vile biblia inavyotafsiri “uzushi” na kutilia mkazo juu ya somo hili. Pia ningependa kutaja mambo kadhaa ya mifano ya uzushi katika maisha yetu ya kawaida kila siku na kwa jinsi hiyo itatuwezesha kufikiri kwa pamoja juu ya hili. Yeyote amwaminiye Mungu yampasa kuwaza juu ya uzushi angalau mara moja katika maisha.
Tito 3:10-11, inaeleza maana ya uzushi kama wadanganyaji, wenye kulaghai na kujihusisha na uovu, wenye hukumu ndani yao. Mzushi ni mtu mwenye kujihukumu binafsi ndani yake kuwa ni mwenye dhambi. Hivyo wale wote wenye kumwamini Yesu hali ndani ya mioyo yao wanashuhudiwa dhambi hao ni wazushi mbele ya Mungu.
Yesu alichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake. Lakini wazushi hukataa kuamini juu ya injili hii halisi yenye kuleta wokovu kwa wale wote walio na dhambi na hivyo kujihukumu wenyewe kwa kujiunga na daraja la waovu.
Je, nawe ni mzushi? Yatupasa kufikiri juu ya hili ikiwa tunataka kuishi kwa uadilifu na maisha ya uaminifu.
Je wewe haujihukumu mwenyewe kuwa ni mwenye dhambi ingawa unamwamini Yesu huku ukiwa hujawahi kusikia injili ya maji na Roho? Unapojiona mwenyewe kuwa ni mwenye dhambi basi unafanya huduma ya Yesu kuwa batili kwa kushusha hadhi wokovu ule ulio kamili na injili ya maji na Roho pia.
Kwa kujiita mwenye dhambi mbele ya Mungu ni kujiona kuwa si mtoto wa Mungu. Wale wenye kukiri mbele za Yesu “Bwana mimi ni mwenye dhambi” inawapasa kuangalia upya imani zao.
Itawezekana vipi kumuamini Yesu na kuendelea kudai kuwa ni mwenye dhambi ikiwa Yesu alibeba dhambi zote za ulimwengu na kukuokoa kabisa na hukumu ile ya milele? Utaweza vipi kuikana zawadi bure ya wokovu wake na kujiita mwenye dhambi hali Yesu alizichukua dhambi zako zote kwa ubatizo wake na kuhukumiwa ipasavyo msalabani?
Watu wa aina hii ni wazushi kwa sababu hujitolea kuwa wenye dhambi kinyume na neno la Mungu. Yakupasa ujue Injili ya maji na Roho ili kukwepa kutenda uzushi mbele ya Mungu.
Yeyote mwenye kumwamini Yesu hali akiwa hajazaliwa upya mara ya pili ni mzushi kwa kuwa bado anayo dhambi moyoni.
Kwa kuwa Mungu alizichukua dhambi zote ulimwenguni, pamoja na zako basi tutaweza kuwa wazushi mbele zake ikiwa tutadharau baraka hii ya wokovu. Kwa sababu Mungu ni mtakatifu sisi tutaweza kuwa wazushi ikiwa tunadhambi mioyoni mwetu.Ikiwa kweli tunapenda kuwa wenye haki, yatupasa basi kuamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
 

CHANZO CHA MZUSHI KATIKA BIBLIA


Hitaji gani muhimu lenye kumpa 
mtu sifa ya ukuhani?
Inampasa azaliwe upya 
mara ya pili.


Hebu na tuone katika kitabu cha 1Wafalme 12:25-26 “ndipo Yeroboamu akajenga Shekemu katika milima ya Efraimu akakaa huko. Akatoka huko akajenga Penuel. Yeroboamu akasema moyoni mwake basi ufalme utairudia nyumba ya Daudi.”
Yeroboamu alikuwa mmoja wa wasaidizi wa Sulemani. Sulemani alipotenda dhambi katika siku zake za mwanzo, Yeroboamu aliamua kumsaliti mfalme na baadaye kuwa mfalme wa kabila kumi na mbili za Israel katika kipindi cha utawala wa Rehoamu mwana wa Sulemani.
Nia ya kwanza kabisa ya Yeroboamu kuwa mfalme wa Israeli kwa sababu watu wake wangeliweza kurudi Yuda ambako ndiko kulipokuwa na hekalu.
Hivyo, akaja na wazo la kuzuia jambo hili lisitokee. Alitengeneza ndama wawili katika Betheli na Dani na kuweka amri kwa watu wote kuwaabudu. 1Wafalme 12:28 inasema “kwahiyo mfalme akafanya shauri akafanyiza ng’ombe wawili wa dhahabu” Mmoja akamuweka Betheli na mwingine Dani na kuwaambia watu waabudu ingawa hii ilikuwa ni dhambi kubwa sana. Kwa ridhaa yake aliamua kuteua makuhani kuongoza ibada hiyo.
“Baada ya hapo Yeroboamu hakuiacha njia yake mbovu lakini akafanya tena makuhani wa mahali pa juu wa watu wowote” (1Wafalme 13:33). Huu ulikuwa ni mwanzo wa uzushi.
Hata sasa wazushi huteua nafasi za ukuhani kwa yeyote yule ajitoleaye kufanya kazi ya Mungu. Yeyote aliyehitimu chuo cha theolojia ataweza kuwa mtumishi, mwinjilisti,mmisionari au mzee wa kanisa hata kama hajazaliwa upya kwa maji na Roho.
Itawezekana vipi mtu ambaye hajazaliwa upya mara ya pili kuweza kushika nafasi ya utumishi? Ikiwa mtu huyo atateuliwa kama kuhani, kanisa lenye kufanya uteuzi huo litakuwa ni kiwanda chenye kuzalisha wazushi.
Hebu tufikiri tena juu ya chanzo cha uzushi. Kwanza Yeroboamu alibadilisha ndama wa dhahabu kuwa badala ya Mungu ili kulinda nguvu za kisiasa. Pili alimsimika yeyote aliyejitolea kuwa kuhani kwa maneno mengine aliwasimika watu wa kawaida kuwa makuhani. Hata leo mambo hayo hutokea.
Historia ya uzushi inaendelea kustawi baada ya Yeroboamu. Wale ambao hawajazaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho kamwe hawatoruhusiwa kuwa makuhani.
Je, itawezekana kweli mtu aliyehitimu shule ya theolojia tu kuweza kuwa mtumishi wa Mungu hata kama hajapata kibali cha Mungu? Kamwe. Ni wale tu waliokubalika na Mungu ndiyo wanaruhusiwa kuwa watumishi wake. Watu hawa ni wale waliozaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Imeandikwa katika 1Wafalme 12:25-26 na 1Wafalme sura 13 kwamba dhambi ya Yeroboamu alileta hasira ya Mungu. Yatupasa sote kuelewa habari hii, na ikiwa mtu hatofahamu juu ya hili yampasa basi arudi katika biblia na kutafuta.
Hebu chunguza ikiwa nawe unaweka ndama wa dhahabu badala ya Mungu katika huduma yako. Je, kwa namna yoyote unaweka msisitizo kwenye baraka za kidunia ili wafuasi wako wasiweze kurudi katika injili ya kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho?
Je, unawaeleza wafuasi wako kwamba wataweza kupokea uponyaji wa magonjwa yao kwa kumuamini Yesu? Je, unawaambia watabarikiwa kwa utajiri wa mali? Je, unawateua wale ambao hawajaokoka kuwa watumishi au wafanyakazi katika kanisa lako na kudai kwamba dhehebu lako ndilo halisi? Ikiwa ndivyo, unatenda dhambi ya Yeroboamu mbele ya Mungu na kuleta hasira yake.
 

WAZUSHI HUABUDU MUNGU WA NDAMA WA DHAHABU

Hata nyakati hizi wapo wazushi wengi wanaoabudu ndama wa dhahabu. Husema kwamba Mungu alimbariki Sulemani pale alipomtolea maelfu ya sadaka za kuteketezwa kwa Mungu. 1Wafalme 3:3-5 “Suleimani naye akampenda Bwana, akienda katika amri za Daudi babaye ila hutoa dhabihu na kufukizia uvumba katika mahali pa juu. Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko, kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Suleimani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile. Na huko Gibeoni Bwana akamtolea Suleimani katika ndoto ya usiku, Mungu akamwambia omba utakalo nikupe.”
Hutapeli fedha za waumini wao kwa ahadi za kibadhilifu za “sadaka elfu za kuteketezwa zilitolewa na Sulemani” Wale waumini wapumbavu fedha zao hufujwa. Na wale wenye kuabudu ndama wa dhahabu kama Mungu hupoteza fedha zao ambazo hutumika kama michango ya kujenga majengo makubwa ya kanisa. Hii si kwa sababu makanisa yao ni madogo sana bali kwa sababu wanapenda kuiba fedha kwa waumini wao kwa kigezo hicho.
Kumweka ndama wa dhahabu mbele ya washarika ili aweze kuabudiwa ni uzushi ulio letwa ili kufanya ubadhilifu wa fedha za waumini hao. Sisi tunaomwamini Mungu kamwe tusikubali kupumbazwa. Unapotoa fedha yako kwa nia ya kumwabudu ndama wa dhahabu si sadaka kwa Mungu unatoa bali huishia kwenye mifuko ya makuhani bandia ambao wamejawa na tamaa kama Yeroboamu. Usikubali kuangukia katika mitego ya wazushi wa aina hii.
Sasa basi, kwa nini Mungu alifurahishwa na maelfu ya sadaka za kuteketezwa alizotoa Sulemani? Kwa sababu Suleimani alikwisha tambua dhambi zake, alijua ya kuwa ilimpasa afe kwa ajili ya dhambi hivyo kutoa sadaka kulingana na imani. Alitoa maelfu ya sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya shukrani ya wokovu wa Mungu. Sulemani alitoa maelfu ya sadaka za kuteketezwa kila siku akifikiri juu ya ukombozi wa maji na Roho.
Sasa yakupasa ukumbuke maana halisi ya uzushi ili usije ukadanganywa na makuhani bandia.
 

WALE WOTE WANAOTOA HUDUMA PASIPO KUZALIWA UPYA MARA YA PILI NI WAZUSHI

Wazushi husema nini juu ya 
kuzaliwa upya mara ya pili?
Wao husingizia kuwa wameokoka baada ya 
kupata maono, ndoto na aina nyinginezo 
za matukio wanayo elezewa 
kuwa ni ya kiroho.

Wapo wale wenye kufundisha wengine ili waokoke hali wao wenyewe hawajaokoka kwa imani. Ni wazushi. Huwaambia watu waokoke hali wao hawana uwezo ndani yao wa kumfanya mtu aokoke kwa kuwa hajui injili ya maji na Roho. Watu kama hawa tunawacheka!
Makuhani bandia huubiri injili potofu, kwa kupotosha injili ya maji na Roho. Huwaambia watu kutakasa dhambi zao kwa toba za kila siku.
Husema “Nenda ukafanye maombi mlimani, jaribu kufunga, jitolee kwa kazi ya Mungu, fanya maombi jioni, kuwa mtiifu, toa michango ya ujenzi wa kanisa lakini uwe mwangalifu na dhambi zako.”
Siku moja nilisikia mtu fulani akitoa ushuhuda jinsi alivyookoka. Alisema kuwa aliota kuwa amesimama kwenye mstari na ndipo zamu yake ilipokuja Yesu akamwita jina lake. Akasema huo ndio ushuhuda wake alipookoka. Lakini je, huku kukata shauri kwa namna hii kulikuwa ni sawa? Sidhani kama Yesu alisema hivyo?
Katika Yohana 3 Yesu anasema “mtu asipo zaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu”. Hapa Mungu anasisitiza ya kuwa ni wale tu watakaozaliwa upya kwa maji na kwa Roho ndiyo wataweza kuwa makuhani. Yeyote anaye amini habari za ndoto, mashamshamu, furaha za kiroho au kwa sala za toba za kila mara ni mzushi.
Nyakati hizi, watu wengi hawaamini maandiko ya neno la Mungu na kushikilia mafundisho ya madhehebu yao badala ya kuzaliwa upya mara ya pili. Ikiwa maji na kwa Roho vyaokoa, basi wale wanaokataa kuhubiri injili ya wokovu wa maji na Roho ni Wakristo bandia na wazushi.
 

WANAMAGEUZI NA UKRISTO WA SASA

Ni lini Injili ya kweli ilianza 
kuchanganywa na kupotoshwa huku 
ikilinganishwa na dini nyinginezo?
Kuanzia kipindi cha Mtawala wa Kirumi aitwaye 
Constantine alipo toa tamko la Milan katika 
mwaka 313 Baada ya Kristo.

Madhehebu ya Kikristo yalianza lini? Ni lini aina za madhehebu kama vile Presbyterian, Methodist, Baptist, Lutheran, Holiness na Full Gospel yalianza? Mageuzi haya yalianza baada tu ya miaka 500 iliyopita. 
Wakristo wa mwanzo walikuwa ni wafuasi wa Yesu alipokuwa duniani. “Wakristo maana yake wale wote wenye kumfuata Yesu Kristo”.
Wakristo wa kwanza walikuwa ni mitume na wafuasi wao. Mitume na wakuu wa makanisa walifuata injili ya kweli hadi kufikia miaka 313 BK (Baada ya Kristo). Hata hivyo baada ya Tangazo la ilani huko Milan la Constantine Mkuu, wakristo na watu wa mataifa walianza kuchanganyikana. Matokeo yake ni kipindi cha giza ambacho kilidumu takribani zaidi ya miaka 1000.
Baadaye mwanzoni mwa karne ya 16, Martin Luther alitangaza Mageuzi kwa kusema “wenye haki wataishi kwa imani”(Warumi1:17). Baadaye kidogo kati ya mwaka 1500-1600 wanamageuzi kama vile John Calvin na John Knox waliongoza vuguvugu toka ukatoliki. Na hii ndiyo mafanikio ya Mageuzi.
Mageuzi yalikuwa ni jitihada tu za kuanzisha makanisa mapya tofauti na kanisa la Katoliki la Roma. Wanamageuzi hao hawakuweza kuweka bayana mambo ya msingi katika kuukataa ukatoliki wenyewe.
Sababu zao hazikuwa ni kuanzisha imani ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho, bali zilikuwa ni kujiweka huru tokana na ukandamizaji wa udhalimu wa Kanisa Katoliki la Roma. Kanisa Katoliki la Roma waliita vuguvugu hilo kuwa Uprotestanti (Protestantism) yaani uasi au waasi.
Kwa wakati huo, Kanisa Katoliki la Roma liliwaasa watu kununua vitu vilivyotolewa au kutengenezwa na kanisa kama vile, tasbihi, picha za watakatifu, sanamu na vipande vya nguo zao kwa thamani kubwa kwa ahadi ya kuwawezesha wafu wao kuingia mbinguni. Luther hakujua kimsingi ukatoliki ulikuwa makosa. Bali yeye alichojaribu ni kusimamisha kanisa Katoliki la Roma kuuza vitu hivyo kwa ajili ya kuliwezesha kifedha katika ujenzi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
Matokeo yake tunaweza kuona mabaki ya ukatoliki hata ndani ya makanisa ya waprotestant wa nyakati hizi; kubatiza watoto wachanga, sala za toba ambazo ni sawa na ungamo la dhambi ndani ya kanisa Katoliki la Roma, sakramenti takatifu, kusimika wale waliohitimu shule za theolojia, makanisa mazuri na makubwa. Haya yote ni mabaki ya Kanisa Katoliki la Roma ndani ya Uprotestanti.
Kwa kuangalia tangu mageuzi mwanzoni mwa miaka takribani 1500 historia ya Uprotestanti ni kiasi cha umri wa miaka 500. Mwaka huu mageuzi haya yanaadhimisha mwaka 481 tangu kutokea na kuanzishwa. Unaweza usigundue kwamba Martin Luther alihasi kanisa lake mama miaka 481 tu iliyopita. Uprotestanti hauwezi kamwe kudai uhalali wa kuwa wazi kwa sababu tu ya upya wake. Mageuzi katika Ukristo bado yanaendelea na yataendelea.
Hata hivyo jambo moja inapaswa kuzingatia. Kamwe tusisahau kwamba wale tu watakao zaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho ndiyo watakaoingia ufalme wa mbinguni. Hebu na tuhubiri hivyo! Je, wewe unahubiri injili ya Yesu, injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho? Ikiwa hapana, basi wewe si mtumishi wa Mungu. Ni injili hii ambayo Mungu ametuhitaji kuiamini. Ndiyo hiyo Yesu aliyomfundisha Nikodemo katika Yohana sura ya 3.
Je, biblia huzungumzia juu ya injili ya wokovu wa maji na Roho tu au pia huzungumzia mambo kama vile kutenda matendo mema kwa jamii na kuishi maisha matakatifu? Bila shaka jambo la mwisho kati ya haya ni muhimu pia. Ingawa utaweza kulitekeleza katika ile kweli ikiwa tu utakuwa umezaliwa upya katika maji na kwa roho. Mapenzi ya Mungu kwetu ni kuiamini injili.
 
 
MAFUNDISHO YA WAZUSHI

Mzushi ni nani?
Ni yule mwenye kuendelea kuwa 
mwenye dhambi ingawa 
anamwamini Yesu.

Ni lini wakristo bandia, imani ya wazushi ilipoanza kumea hapa duniani?
Watu wa Israel walimwabudu Mungu mmoja hadi pale walipogawanywa na kuwa makundi mawili ya dola katika utawala wa Yeroboamu kama ilivyoandikwa katika 1Wafalme 12-13. Kuanzia kipindi hicho kabla ya Kristo kuja duniani, imani ya uzushi ilianza kustawi. Zipo imani nyingi za uzushi zitendazo kazi nyakati hizi.
Biblia inazungumzia juu ya mafundisho ya Ukristo bandia katika Isaya sura ya 28 na Tito 3:10-11. Biblia inasema kwamba wazushi ni wale wote wenye kumuamini Yesu huku hali wanadhambi mioyoni mwao. Yeyote aliye namna hii ni mzushi.
Hufundisha kama ilivyosemwa katika Isaya 28:9-10 “Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nanihabari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini? Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa na kunaswa na kuchukuliwa.”
Wazushi huongeza amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni. Hii inamaana gani? Maana yake “uwe mwangalifu, uwemwangalifu sana na wale wenye kujifanya kuwa wamezaliwa upya mara ya pili kwa imani katika Yesu” wanakwambia uwe mwangalifu tu hata iwe vipi. Watakwambia usiwasikilize, usiambatane ili usije anguka kwenye wazushi.
Kwa jinsi hiyo ikiwa wanajigamba wao ndio wenye imani halisi, kwa nini basi hawaondolei mbali wale wenye kusema imani zao ni tofauti na neno la Mungu? Inasikitisha. Wanadai kuwa wao ndiyo Wakristo halisi, lakini hawana ushahidi wa hicho wanachokiita uzushi. Mkristo wa kweli ataweza kumshinda mzushi kwa neno la Mungu.
Nyakati hizi zimekuwa kwamba wale wajiitao wakristo halisi huwakana wale waliozaliwa kwa maji na kwa Roho na kuwaita ni “wazushi” kwa sababu tu imani zao zinatofautiana nao. Tunaweza vipi kuwa wazushi ikiwa tunaamini injili ya maji na Roho?
Ikiwa wale wenye kuitwa wazushi wanahubiri injili ya maji na Roho, basi hao ndiyo Wakristo halisi. Kwa upande mwingine ikiwa watakuwa wakristo halisi wasio hubiri injili ya maji na Roho bila shaka watakuwa wazushi.
Tofauti kati ya wakristo halisi na wazushi ipo katika kuhubiri injili ya maji na Roho na kumuamini Yesu hali wakiwa na dhambi miyoni. Wataweza vipi kuwa wazushi ikiwa wanaamini neno la Mungu na kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho?
Je, ni uzushi kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani na kutakaswa kabisa na dhambi? Je, ni “Ukristo halisi” kutoamini injili ya maji na Roho?
Wapo watu wengi wa madhehebu walio iacha Biblia huku wakidai kuwa ni wakristo “halisi” wameacha kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho kama ilivyoainishwa katika Biblia kwa sababu wanahubiri juu ya damu katika msalaba tu, kuukana ubatizo wa Yesu (Maji).
Nini tofauti kati ya Kanisa Katoliki la Roma na Kanisa la Kiprotestant nyakati hizi? Kama ilivyo wanamageuzi walioasi kanisa Katoliki la Roma, kama jinsi ile walivyojitoa toka Kanisa Katoliki la Roma na kuanzisha Protestanti, nasi pia yatupasa kuasi Ukristo usio na mwelekeo na makuhani bandia. Hapo ndipo tutaweza kufunguka macho kwenye injili ya kweli, kuwa na imani ya kweli na kuokolewa kwa ukamilifu kupitia injili ya maji na Roho.

Yatupasa kufanya nini ili 
kuzuia kutokuwa wazushi?
Yatupasa kuzaliwa upya mara ya 
pili kwa maji na kwa Roho.

Biblia inatueleza kwamba ni wale tu wenye kuamini injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ndiyo wenye kufuata imani ya kweli. Yesu alisema haya pia kwa Nikodemo katika Yohana 3:1-12.
Wazushi mara nyingi huwaasa wafuasi wao kujitolea kwenye imani yao. Huwaasa kufanya maombi usiku kucha na kujibidisha katika matendo. Hii ni sawa na kumwambia kipofu akimbie.
Haijalishi ni kwa kiwango gani unasali, haina maana yoyote, ikiwa hujazaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Tunaposema kwamba wale ambao waliozaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho ni wenye haki, wazushi hutoa shutuma kupitia Warumi 3:10 “hakuna mwenye haki hata mmoja” kwa kutumia kifungu hiki huwaita wenye kuamini kuwa ni wazushi.
Hata hivyo ukweli wa mambo yao ndiyo wazushi. Maana halisi ya kifungu hiki si rahisi kueleweka kama inavyosomeka. Wazushi hawa hajaisoma bibli ipasavyo Mtume Paulo alisema kwamba hakuna mwenye haki duniani. Alikuwa akinukuu kifungu hiki toka Agano la Kale ambalo linasema hakuna mwenye haki duniani kabla ya Yesu kuja na kuwakomboa wanadamu kwa dhambi zao kupitia wokovu wa Mungu. Hata hivyo wale waliookolewa na Yesu ndiyo tu walio na haki.
Tunaweza kuona ukweli ikiwa tutaweza kusoma sura nzima katika kifungu hicho. Wazushi wanachofanya ni kuwaonya wafuasi wao kuwa waangalifu dhidi ya wale walio na imani tofauti na yao. Huwakataza waumini wao kuabudu mahala pengine kama si katika makanisa yale wanayoyaona ndiyo halisi kwao.
Hivyo usharika hauthubutu kamwe kuingia kwenye makanisa yenye kuhubiri injili ya maji na Roho.
Hatimaye huwa viziwi dhidi ya injili ya kweli na kushindwa kuzaliwa upya. Haya ni mafundisho ya viongozi waongo ambao kwakweli hujenga jamii ya kuzimu. Watahukumiwa na Mungu kwa hilo. Wazushi wamemhasi Mungu.
Wazushi ni watu gani? Je, ni wale waliokombolewa kwa kuamini injili ya maji na Roho, au ni wale wenye kudai kumwamini Yesu hali wameshindwa kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho?
Tito 3:11 inasema wale wenye kumwamini Yesu huku wakibaki na “mioyo yenye hukumu ya hatia” hao ndiyo wazushi.
Huwaasa wafuasi wao kutohudhuria mikutano ya uamsho ambayo injili ya kuzaliwa upya mara ya pili huubiriwa kwa kuwaambia ni hatari. Ni kwa namna gani wanaojiita wakristo halisi kuogopa migongano ya kiimani? Wanaogopa kwa sababu hawana imani iliyo ya kweli ndani yao. Kwa sababu ya “amri juu ya amri”. Mafundisho ya wazushi ni kama haya.
Makuhani wazushi hunukuu kidogo toka kitabu hiki, kidogo kwenye kitabu kile, maneno ya wanafilosofia toka vitabu vya fasihi na kuchanganya vyote na mawazo yao kwa kufanya viwe wito wa maana kwa watu.
Huamini kuwa wafuasi wao ni mbumbumbu na wanahitaji kuelimishwa juu ya mambo ya dunia. Kanisa la kweli hujikita kuhubiri neno la Mungu na kuwaelimisha waumini wake kwa neno la Mungu. Watu hawahudhurii ibada makanisani ili waweze kuelimishwa juu ya mambo ya dunia, bali huja ili waweze kusikia mambo ya mbinguni ambayo kamwe hawawezi kuyapata au kusikia duniani. Huja kusikiliza neno la Yesu.
Watu huingia kwenye makanisa yao wakiwa wenye dhambi wakitumaini kuibuka wakiwa wenye haki wasio na dhambi. Sasa nini makuhani hawa bandia huwafundisha? Huwaambia wafuasi wao wasihudhurie mikutano ya uamsho ambapo watumishi wa Mungu huubiri injili ya kweli. Huwazuia wafuasi wao kutokuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Huu ni upumbavu mkubwa! Kwa namna yoyote wataweza kuwalaghai wafuasi wao lakini kamwe hawataweza kumlaghai Mungu.

Je, makuhani bandia wataweza 
kuwafanya waumini kuzaliwa upya 
kwa maji na kwa Roho?
Kamwe!Ni wale tu waliozaliwa upya mara 
ya pili ndiyo watakaoweza kufanya 
wengine kuzaliwa upya.

Wewe mzushi, ikiwa kweli wewe ni mtumishi wa Mungu, je, huoni Roho akikuonya? Yakupasa ugeuke. Acha kuwakwaza wafuasi wako kuhudhuria mikutano ya uamsho ambamo watumishi wa Mungu huubiri injili ya kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho.
Wazushi huwaelimisha wafuasi wao na maneno ya theolojia pekee, inapotokea kukabiliwa na kanuni ngeni kwao hushindwa kihoja. Inasikitisha sana. Makuhani bandia ni wepesi kuhudumu pasipokutumia neno la Mungu. Huubiri, kutoa nasaha na kuhudumu neno kwa kutegemea fikra zao potofu. Wale wote wenye kuhuduku neno na kuhubiri pasipo neno la Mungu ni wazushi na watu wa mshahara (Yohana 10:13).
Makuhani bandia ni wazushi kwa sababu dhamira zao na matendo yao ni tofauti. Watu wengine hudhani kwamba makanisa yasiyoweza kuwa na madhehebu makubwa ni makanisa ya wazushi. Hata hivyo makanisa haya kiukweli yasingependa kuwa chini ya madhehebu yale yaliyo rasmi kwa sababu makanisa yao huendesha mafundisho yaliyokinyume na Biblia.
Wazushi huwaasa wafuasi wao kuweza kukombolewa hali wao binafsi hawajaweza kumaliza tatizo la dhambi ndani yao. Wanatenda dhambi ya Yeroboamu. Ikiwa yupo yeyote ambaye bado mwenye dhambi ndani ya moyo wake huku akijaribu kumtumikia Mungu inapasa kuelewa ya kwamba dhambi zake na utakatifu wa Mungu ni mambo yasiyochangamana kabisa. Yampasa kujua yeye ni mzushi.
Kwa hivyo, ikiwa mtu yeyote anayehubiri au kufanya kazi kanisani bado ni mwenye dhambi, anapaswa kutambua kuwa yeye ni mwovu. Yeye ni mwovu kwa sababu hajui injili ya wokovu wa Kristo, injili ya kuzaliwa mara ya pili kwa maji na Roho. ikiwa mtu anajifunza Bibilia kutoka kwa mzushi na kuwafundisha wengine kwa njia hiyo hiyo, yeye huwa mzushi
Twajua mti kupitia matunda yake. Wale walio na haki kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake ndiyo tu watakaoweza kuwa na haki hali wale wote ambao bado ni wenye dhambi wataangamia kwa dhambi. “Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri na mti mwovu huzaa matunda mabaya” (Mathayo 7:17).
 

MAKUHANI WAZUSHI WANAFUNDISHA NINI KATIKA MAHUBIRI YAO

Makuhani 
wazushi wanafundisha nini
katika mahubiri yao?
Theolojia za dunia hii na mawazo 
ya kibinadamu.

Makuhani waongo huwa waangalifu sana. Kwa nini? Inawapasa kuwa waangalifu ili wasijekugundulika kwa uongo wao kwa sababu hawana imani thabiti ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Wazushi hunukuu hapa na pale kidogo. Huwalaghai watu na kuwafundisha hali wasiijue maana ya injili ya kweli. 
“amri juu ya amri, amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni, huku kidogo na huku kidogo” (Isaya 28:13).
Kanuni juu ya kanuni, husema “neno hili maana yake ni kadhaa wa kadhaa kwa Kirumi na kadhaa wa kadhaa kwa Kiebrania. Na kuna kanuni kadhaa wa kadhaa” Pia huwaonya watu kuwa waangalifu pale wanapokabiliwa ana kwa ana kwa kanuni za wokovu zenye kuelezea kwa namna ya uwazi kabisa. Husema Martin Luther alisema hivi, John Calvin alisema vile wakati John Knox alisema hivi na vile, nasisi tunafikiri wote ni sahihi kwa njia zao.
Hawajui hata waliongealo au hata waliaminilo. Yule mwenye imani ya kweli huelezea imani yake kwa namna ya uwazi mtupu. Waumini wa kweli huweza kutofautisha kwa uwazi kati ya wale walio zaliwa upya mara ya pili na wale wasio zaliwa upya mara ya pili. Sisi tunahubiri uwazi injili ya kuzaliwa upya mara ya pili katika maji na Roho.
Lakini wazushi wapo katika ulimwengu wa machafuko. Imani zao ni kama popo. Kama alivyo popo hupendelea kuishi mapangoni nyakati za mchana na kutoka nje nyakati za usiku tu, wazushi hupenda namna hii ya maisha kwa kuamini hili na lile. Hawajui ile kweli.Kuhani mzushi anapokwenda motoni, wafuasi wake hufuata nyuma kwenye mwisho wa machungu. Hivyo wengi huishia motoni kwa kuwa wamewaamini manabii wa uongo.
Je, kiongozi wako wa kiroho amezaliwa upya kwa maji na kwa Roho? Je, anahubiri maneno ya injili ya kuzaliwa upya kwa maji na kwa roho kama ilivyoandikwa katika biblia? Kama ndivyo hakika wewe ni mwenye bahati, lakini kama sivyo basi utaangamia. Kama hujazaliwa upya mara ya pili yakupasa kusikia injili ya maji na Roho, soma vitabu vyenye kuelezea juu ya hili na uzaliwe upya.
Wazushi hawapendi injili ya kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho. Wao huubiri kwamba “Yesu Kristo amekuja kuondoa dhambi zetu, na ni hilo tu alilofanya. Na anaendelea kufanya hivyo kila siku katika kutuondolea dhambi na ataendelea kufanya hivyo hata maishani”. Hii inaweza vipi kuwa kweli. Husema wao ni wenye haki lakini wanaendelea kutenda dhambi. Wanakuwa wenye haki kwa muda fulani na baadaye kuwa wenye dhambi.
Hii ndiyo theolojia potofu. Ni uongo. Yeyote aliye wa haki sasa, na baadaye mwenye dhambi ni mzushi, nabii muongo. Yeyote anayeihukumu nafsi yake ni sawa na yule anayejihukumu mwenyewe.
 

LAANA YA MUNGU IMEACHILIWA KWA WOTE WALIO WAFWazushi hutilia mkazo 
mambo gani?UASI WA WAZUSHI

Matendo mema.

Wazushi hawana msimamo. Hivyo si rahisi kuongoza wafuasi kuweza kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho hasa pale waumini wao wanapowakabili kwa maswali ya utafiti juu hili. Badala yake huwapa waumini mawaidha ya ajabu kwa kuwaambia mtu ataweza kuzaliwa upya kwa mashamushamu na haipaswi kuelewa pale unapozaliwa upya mara ya pili. Hakika hili ni jambo la kuchekesha sana.
Yesu alisema katika Yohana 3 kuwa “mtu asipozaliwa upya kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu”. Nyakati hizi wale wenye haki waliozaliwa upya mara ya pili badala yake ndiyo huitwa wazushi wasiofaa.
Makuhani wazushi husema hawawezi kujiita wenye haki kwa kuwa wajinyenyekeza. Huwaambia wafuasi wao “msihudhurie mikutano ile ya uamsho ambayo wahubiri wamepanga kuzungumzia baraka ya kuzaliwa upya mara ya pili, mtaweza kuja kuwa pia wazushi. Utafukuzwa na kanisa. Kama unapenda kuendelea kuwa hapa nasi basi ukiri wewe ni mwenye dhambi na Mungu atakufanya mwenye haki siku itakapokuja” Hivyo ndivyo wasemavyo. Hapa humaanisha kuwa ni jukumu lako kuamua kuwa mlokole au la!
Wazushi huwaambia wafuasi wao “inakubidi uwe nasi lakini swala la ulokole ni jukumu lako. Kwahivyo jaribu mwenyewe. Kama jinsi ulivyosasa utakapokwenda mbele ya Mungu muda utakapowadia, hivyo utakuja kuelewa ukweli. Binafsi sijui kitakachotokea baadaye hapa. Lakini ulipo ndipo kanisa halisi, hivyo inakubidi uendelee kuwepo nasi” Unadhani haya ni kweli?
Makuhani hawa wazushi hunukuu kidogo hapa na pale na kujiundia kanuni zao binafsi. Na ndipo inapokuwa kweli kwa ajili yao. Hawajui juu ya neno la Mungu linalotueleza juu ya maji na Roho.
Wazushi hutafsiri biblia kulingana na fikra zao. Yatupasa kuitafsiri biblia kulingana na neno kama lilivyo, lakini wao huitafsiri kwa namna wazionazo wao. Na hii ndiyo maana wapo wanatheolojia na madhehebu mengi katika Ukristo.
Kwa kuwa wapo wazushi wengi wa madhehebu na theolojia ipo idadi isiyo na mwisho ya vitabu vya uzushi. Makuhani bandia husoma kidogo hapa na pale wanapohubiri. Kuhani wa kweli siku zote huubiri kwa kutumia Biblia pekee.
Wazushi hufuja fedha kwa wafuasi kwa njia ya ulaghai wa kila aina. Wao hula na kuishi maisha mazuri duniani na kuishia motoni kwa sababu walishindwa kuzaliwa upya mara ya pili. Hii ni hatima Mungu aliouweka kwa ajili yao.
Tangu hapo awali Mungu amewavumilia. Lakini wale wenye mioyo migumu kupokea baraka yake ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho atawatupa motoni.
Mungu atawahukumu wazushi wote. Wazushi humuamini Mungu kwa jitihada binafsi na kutumia wingi wa hoja na kanuni za kithiologia tangu mwanzo. Lakini kidogo kidogo huanza kuhubiri kulingana na kanuni za kiutu ili wafuasi wao wasiweze kuzaliwa upya mara ya pili.
Wazushi hujaribu pia kuwekea mkazo juu ya matendo yao ya kimwili. Mtumishi yeyote asiyehubiri injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho ni mzushi mbele ya Mungu.
Huwabana wafuasi wao pasipo kukoma. Huwashinikiza kuhudhuria maombi kwa siku 40 usiku kucha siku 100 za maombi ya asubuhi mapema, kupanda milimani kwa maombi, kufunga kula mara kwa mara, kufanya michango ya ujenzi wa majumba ya kanisa, maelfu ya sadaka za kuteketezwa, michango ya mikutano ya uamsho... Huthubutu hata kutengeneza michoro ya chati ili kuonyesha kwa kila mchangiaji ni kiasi gani ametoa mchango. Kwa kuangalia matunda ya kazi zao, tutaweza kuona jinsi walivyo wazushi.
Laana ya Mungu huwaangukia wafuasi wao pia. Watumishi wenye kuhubiri pasipo kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho wao pamoja na wafuasi wote wapo kwenye laana ya Mungu.
 

WAZUSHI HUJARIBU KUZISOMA AKILI ZA WAFUASI WAO

Kwa nini wazushi hujaribu 
kuzisoma akili za wafuasi wao?
Kwa kuwa hawajazaliwa upya, bali hufanya 
huduma kwa unafiki na pasipo 
Roho Mtakatifu ndani yao.

Makuhani wazushi hulalamika kila siku. Inawapasa kuwa na uhakika ikiwa wanawaridhisha mashemasi wakuu, wazee wa kanisa na mashemasi wa kawaida pamoja na watu wa kawaida. Ndiyo walivyo kila siku.
Wanakuwa na tabia ya unafiki kila siku “watakatifu na wenye huruma” ni wenye dhambi nyingi lakini hujifanya kuzungumza mambo matakatifu hivyo kuwa wanafiki zaidi siku hadi siku.
Muhubiri mmoja aliwahi kusema “ni laana kufanya utumishi pasipo n Roho ndani yako” maana yake ni kwamba ni uzushi kufanya kazi ya Mungu pasipo kukombolewa; ni maisha ya laana. Ikiwa wewe ni mmoja kati ya wazushi, basi yakupasa uzaliwe upya kwa maji na kwa Roho.
Anayemwamini Yesu pasipo kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho ni mzushi. Kwa nyongeza, wote tunapaswa kuirudia injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Wenye hili tu ndio waliozaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho ndiyo watakao hubiri injili kwa wengine.
 

WAZUSHI HUIMIZA JUU YA AMANI TU

Makuhani wazushi huwaridhisha 
vipi wafuasi wao?
Mara nyingi huimiza amani kwa kuwaambia 
wafuasi wao wataweza kuingia ufalme 
wa mbinguni japokuwa wana 
dhambi mioyoni mwao.

Isaya 28:14-15 inasema “Basi lisikieni neno la Bwana enyi watu wenye dharau, mnaowatawala watu hawa walio ndani ya Yesrusalemu. Kwa sababu mmesema tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu, pigo lifurikalo litakapopita halitatufikia sisi, kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyokweli.”
Wenye dharau ni watu gani? Ni wale wote wenye kuhubiri neno la Mungu kwa kuchanganya imani zao potofu. Aina yoyote ya mawazo ya mhubiri, theoligia asemazo inampasa kutoa tafsiri ya kweli kibiblia. Lakini makuhani wazushi huubiri kwa Biblia kwa jinsi waonavyo wao binafsi inafaa. Hawa ni wapuuzaji.
“Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu, pigo lifurikalo litakapopita halitatufikia sisi” wazushi husema kuwa pigo halitawafikia wao, huwaambia wengine wasiwe na wasiwasi. Uharibifu wa kuzimu vimewasubiri, lakini wao husema hakuna wasiwasi, uharibifu wa kuzimu havitokuwepo kwao. Hivyo uwe mbali nao ikiwa unapenda kuishi.
Wazushi husema kuwa haina haja ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Je, hii ni kweli? Hapana, sivyo kabisa. Huwezi kuingia ufalme wa mbinguni kama hujazaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Ni sawa kutoingia ufalme wa mbinguni? Hii ni sawa na kuuliza ikiwa ni sawa kwenda motoni? Huitaji kusema majibu yote mawili siyo. Hebu basi wote tuamini injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho na kuingia Mbinguni pamoja.
Makuhani wazushi huwashawishi watu kwa kusema kuwa kwa sababu wanamwamini Yesu, ni sawa tu kwao kuwa wenye dhambi bali hawatokwenda motoni.
Je, Yesu anahangaika na wewe ikiwa unadhambi? Mwenye dhambi ataweza kweli kwenda mbinguni? Je, utaweza kukwepa kwenda motoni ingawa unadhambi? Je, imeandikwa katika biblia kwamba haupaswi kwenda motoni ikiwa unamwamini Yesu ingawa unadhambi moyoni?
Wazushi husema kwamba wameweka mapatano na kifo, hivyo hakitoweza kuwapata. Wanasema kuwa mwenye kuamini ataweza kuzuia hukumu ya motoni ingawa anadhambi moyoni. Unafikiri inaweza kuwa hivyo?
Wazushi huwavuta watu na kuwapa uhakika, kwa kuwaeleza kifo na ahera haviwasubiri wao. Kuhani mzushi huteua wasiozaliwa upya mara ya pili kuchukua nafasi za ushemasi, uzee wa kanisa na utumishi. Lakini hawafahamu hatima yao ni motoni kwa kutoamini injili ya maji na Roho. Walichopaswa kufanya ni kutilia mkazo wafuasi wao kuamini injili ya maji na Roho.
Je, waumini wakiwa ni wenye dhambi, wataweza kutambuliwa kuingia mbinguni? Mwenye dhambi ataweza kuingia mbinguni? Kamwe! Je, yupo mwenye haki aliye na dhambi? Hapana. Haya ni mafundisho ya wazushi na wanatheologia bandia.
Biblia inasema “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Ni sheria ya Mungu ndiyo huwatupa wenye dhambi moja kwa moja motoni. Kwa upande mwingine wale wote waliozaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho hupokelewa mbinguni.
“Pigo lifunikalo litakapopita halitatufunika sisi kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli” Makuhani wazushi husema maneno mara moja na kuamni kwa dhati kwamba hawatokwenda motoni ingawa wanadhambi moyoni. Kwa sababu hujificha nyuma ya uongo na theologia zisizo za kweli, hivyo Mungu hawezi kufanya chochote kuwasaidia. Huamini juu ya theologia zao tu. Kwa kuwa wanaamini theologia zao badala ya neno la Mungu, basi ni wazushi na wenye dhambi waendao motoni. Ni namna gani inavyosikitisha kwa jinsi walivyo wengi wa aina hii.
 

WAZUSHI HUTAMANI FEDHA TU

Lengo la kuhani 
mzushi ni lipi?
Kufuja fedha nyingi wawezavyo 
tokakwa waumini wao.

Wazushi na makuhani bandia hupendelea fedha. Ni wenye tamaa. “Ni kiasi gani cha fedha mtu huyu atatoa ikiwa atajiunga na kanisa langu?” Huwaza juu ya zaka atakayotoa. Hii ni sawa na kuabudu ndama wa dhahabu. “Tafadhali nifanye kuwa na mafanikio, nifanye kuwa na fedha nyingi Bwana” Makuhani bandia hufundisha watu kuomba namna hiyo.
Husema, “Ikiwa utamwamini Yesu utapata fedha nyingi, utapata mimba ikiwa ulikuwa tasa na utakuwa na mafanikio katika biashara yako.”
Hivyo wengi hudanganyika na hawa makuhani bandia na fedha zao hufujwa na kuishia motoni na matatizo yao. Hii si haki hata kidogo! Ikiwa mtu fulani aliyetokea katika mazingaombwe ya uzushi akizinduka atashangaaa kukuta ni kiasi gani cha fedha alichochangia walaghai wake. Atajuta mwenyewe kwa ujinga wake kwa kuwafuata na kuwafanyia kazi kwa bidii.
Wazushi hupendelea kuonekana kuwa wao ndiyo wenye dhehebu rasmi, wafuasi wao hujitolea kuomba asubuhi na mapema, kuomba milimani, kutoa michango maalumu, zaka, sadaka ya wiki, zipo sababu nyingi ili kuwafanya waumini wao kuchangia fedha.
Wafuasi wao hujibidisha kwa matendo ya sheria, lakini bado wangali na dhambi mioyoni mwao kwa kuwa hakuna yeyote aliye wafundisha juu ya injili ya maji na Roho. Wengine huuliza maswali lakini hawapati majibu ya moja kwa moja. Yeyote ambaye hajazaliwa upya kwa maji na kwa Roho ni mzushi.
 

WAZUSHI NA WAFUASI WAO WANASIKITISHA

Ni watu gani wenye kusikitisha 
zaidi hapa ulimwenguni?
Ni wale wenye kuhudumu kazi ya Mungu 
pasipo kuzaliwa upya mara ya pili 
kwa maji na kwa Roho.

“Enyi wazushi mnasikitisha! Iliwapasa kutafuta ukombozi wenu kwanza! Ishara kuu ya imani bandia ni kuabudu ndama wa dhahabu wa Yerusalemu. Jambo la kwanza wazushi walifanya katika nyakati za Agano la Kale ilikuwa ni kujenga hekalu na kusimika ndama wa dhahabu ndani yake” (1Wafalme 12:25-33).
Nyakati hizi, hujenga makanisa makubwa na kufuja fedha toka kwa wafuasi wao. Huwaambia wafuasi wao kuchukua mikopo katika mabenki ili kuchangia ujenzi wa makanisa mazuri na makubwa. Huamsha hamasa za washirika na kupitisha vikapu vya michango. Fedha, pete za vito vya thamani, saa za dhahabu hujazwa vikapuni mara moja. Hivi ndivyo wazushi hufanya. Makanisa yote ya wazushi hufanya namna hii.
Kwa nje huonekana wanajali sana mambo ya kiroho, lakini kiukweli wanajali zaidi fedha. Nawashauri muwe mbali kabisa na makanisa ya aina hii yenye kujali fedha tu. Nakusihi msiende kwenye makanisa haya ambamo matajiri wa mali na fedha ndiyo wenye kuheshimiwa zaidi. Si vyema kutaja kiasi cha kila sadaka ya mshirika kwani kwa kutaja hivyo wazushi huvutia zaidi wachangiaji.
Wazushi husema maneno ya kuwavutia wafuasi wao. “Utabarikiwa ikiwa utamwamini Bwana Yesu.” 
“Jitolee kwa kazi ya Mungu. Kiasi utakacho jitolea zaidi ndivyo utakavyobarikiwa zaidi.”
“Ukitumika kama mzee wa kanisa utabrikiwa kwa mali.”
Matokeo yake, wafuasi hushindana wao kwa wao ili kuwa wazee wa kanisa. Ikiwa kama kulikuwepo na fidia ni nani angekubali kuhudumu kama mzee wa kanisa? Wazee wa kanisa ndiyo wanao tegemewa kutoa michango ya fedha zaidi.
Je huteuliwa kwa kigezo cha namna wanavyoamini kwa dhati mafundisho na kanuni za dhehebu lao, walivyotegemewa katika jamii na kiasi gani wanachoweza kuchangia makanisani? Hii ni kweli.
Wazushi huendekeza zaidi fedha. Hujali kujenga makanisa makubwa. Hawajali ikiwa wafuasi wao wataenda motoni ikiwa wanatoa michango ya fedha nyingi.
Wazushi ni wale wenyekufanya kazi kwa mshahara. Huwatega watu wao kwa kuwapa vyeo vya bandia. Hutoa vyeo kwa wafuasi wao bila uangalifu (Ezekieli 13:17-19). Hii ni kuwafunga wawe makanisani mwao na kuongeza utajiri. Wazushi hawahubiri injili ya maji na Roho. Wao hujitahidi kujineemesha wenyewe.
Hata yule aliyehudhuria kanisa kwa miezi michache ataweza kupewa cheo cha ushemasi. Zaidi ikiwa atazifata kanuni na mafundisho ya kanisa hilo na kuwa na uwezo wa kifedha, hupandiswa na kuwa mzee wa kanisa. Hii yote ni katika tabia ya aibu ya dhambi ya Yeroboamu aliyemweka ndama wa dhahabu badala ya Mungu.
Wazushi huabudu ndama wa dhahabu. Hawasaidii watu kuokoka. Huchukua fedha kwa wafuasi wao tu kwa kuwashawishi na ahadi za baraka za kidunia. Hawajali ikiwa waumini wao watahukumiwa kwenda motoni ikiwa kama kanisa lao lipo katika hali nzuri ya kifedha.
Wazushi hupendelea kusema “labda” “yawezekana” “huenda” mara nyingi kwa sababu hawana uhakika juu ya wanalosema. Hawana imani ya neno la Mungu na hawaamini kweli wanachokihubiri. Mpangilio wa imani zao haumo kwenye imani ya neno la Mungu. Husema “huenda itawezekana kusema hivi…….” Kamwe hawazungumzi bayana na hakika. Ingekuwa ni vyema kama wasingefundisha wafuasi wao chochote kuliko kuwafundisha uongo.
Wazushi kamwe hawawezi kuwaongoza watu kuweza kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho zaidi wanawahukumu watu kwenda motoni.
 

WAZUSHI HUFANYA KAZI YA MANABII WA UONGO
 

Mathayo sura ya 7 inatuambia juu ya wale wenye kumuamini Yesu hali wakiishia motoni. Wazushi watampinga Mungu hata siku ile ya mwisho. Kama ilivyoandikwa katika biblia “wengi wataniambia siku ile Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndiponitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu” (Mathayo 7:22-23).
Hawa hawaamini kwamba Yesu alisafisha dhambi za watu wote; hawaamini injili ya maji na Roho.
Ni watenda maovu. Hii ni maana gani? Maana yake huwaambia watu wamwamini Yesu huku wakiwa na dhambi mioyoni mwao. Utaweza kushangaa kuwa hili ni kosa gani, lakini ni dhambi hatari mbele ya Mungu.
Mwenye dhambi anapowahubiria watu umuhimu wa kumwamini Yesu, hawezi kuwaongoza kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Kwahiyo wazushi huzalisha wenye dhambi wenye kumwamini Yesu. Ni dhambi kubwa dhidi ya Roho kutenda uovu huu.
Wazushi hawaamini neno la Mungu wala kuhubiri injili kama ilivyoandikwa. Wanachofanya ni kufuja fedha za wafuasi wao. Ni wenye dhambi ingawa wanamwamini Yesu. Hujaribu kuwaongoza wengine hali wao binafsi hawajazaliwa upya. Kwa njia hii, hutenda uovu.
 

WAZUSHI SI CHOCHOTE BALI HUJIFANANISHA KUWA WENYE HAKI.

Tunawezaje kutofautisha kati ya 
waliozaliwa upya na wale wasiozaliwa 
upya mara ya pili?
Tunaweza kuwatofautisha kwa kuwaangalia 
kama wanadhambi mioyoni 
mwao au hawana.

Usije ukadanganywa na hawa wahubiri bandia wenye kukiri kuwa wao ni wenye dhambi. Usiwape fedha zako. Usije ukawapa fedha ulizozitolea jasho hao wenye dhambi.
Kwa nini uwape fedha zako hao wahubiri wasioweza kukusaidia wewe kwa dhambi zako? Ukitaka kutoa fedha zako kama sadaka, angalau jaribu kwanza kusubiri hadi pale dhambi zako zitakapofutwa kupitia injili ya maji na Roho.
Kama ilivyo vitu vya bandia katika sanaa, pia vipo katika maisha. Kwa mfano zipo dini bandia zisizoweza kuongoza katika utakaso wa dhambi moyoni.Utaweza kuzigundua vipi dini bandia? Kitu kilichobandia hufanana na kile kilichohalisi kwa nje lakini kiukweli ni tofauti kabisa na kile cha halisi.
Yakupasa uamue mwenyewe. Ni yupi mhubiri wa kweli? Ni yupi mzushi? Ni ipi imani halisi? Wenye imani halisi ni wanaomuamini Yesu na nguvu yake ya ukombozi. Watu hawa hawana dhambi mioyoni mwao. Lakini wale wazushi wanadhambi mioyoni mwao.
Je, watu wote wa aina hii ni wazushi? Inaweza kabisa kuwa hivyo. Ingawa, hebu twende katika biblia. Yeyote amwaminiye Yesu hali hajazaliwa upya mara ya pili ni mzushi. Ni wazi kwamba waliozaliwa upya mara ya pili ndiyo wenye imani halisi. Hivyo wale wasiozaliwa upya mara ya pili ni wazushi. Ni wale wenye kumuamini Yesu huku wakiwa na dhambi mioyoni.
Wazushi nibandia mbele ya wenye haki. Wanaweza kujua njia ya utakaso ni kumwamini Yesu lakini kwa bahati mbaya bado wanadhambi mioyoni mwao. Huamini kuwa wao bado ni wenye dhambi. Hata hivyo hudai kuwa wataingia mbinguni na hudai kumwabudu Mungu. Inaonekana kuwa ni wenye haki, lakini tusidanganyike na ubandia huo.
 

HUKUMU YA MUNGU INAWASUBIRI WALE WOTE WAZUSHI

Kwa nini injili halisi ilibadilishwa?
Kwa sababu makuhani waongo na wazushi 
walichanganya imani potofu za 
wanadamu na injili halisi.

“Kwahiyo, asema Bwana, Bwana wa majeshi, mwenye enzi wa Israel. Nitapata faraja kwa hao wanipingao nitatwaa kiasi kwa adui zangu, nami nitakuelekezea wewe mkono wangu na kukutakasa takataka zako kabisa na kukuondolea bati lako lote, nami nitarejeza upya waamuzi wako kama walivyokuwa hapo kwanza na washauri wako kama walivyokuwa hapo mwanzo, baada ya hayo utaitwa Mji wa haki mji Mtakatifu! Sayuni itakombolewa kwa hukumu na waongofu wake kwa haki. Lakini kuharibika kwao wakosao nao wenye dhambi kutatokea wakati mmoja, nao wamwachao Bwana watateketezwa. Kwa maana watatajirika kwa sababu ya mialoni mlioitamani nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua. Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka na kama bustani isyo na maji. Na mtu hodari atakuwa kama makumbi, na kazi yake kama cheche ya moto, nao watawaka pamoja wala hapana atakayewazimia” (Isaya 1:24-31).
Mungu anatuambia ya kwamba ikiwa tutawaamini walimwengu tutaibiwa kwa sababu wao ni wanadamu. Anatuambia ya kwamba tutaaibika kwa sababu ya kanisa tulilolichagua, na aibu hii itakuwa kama mti ambao majani yake yamenyauka kwa sababu bustani haina maji.
Anatueleza kuwa makuhani waongo pamoja na wafuasi wao wenye kuamini kanuni za kibinadamu wakiliacha neno la Mungu watakuwa kama makumbi na cheche ya moto. Wote wataungua motoni. Wahubiri waongo na wazushi ambao hawajakombolewa pamoja na wenye dhambi ni maadui wa wenye haki watahukumiwa kwa moto wa Mungu.
Kanisa litengenezwalo kwa theologia pekee laweza kuonekana ni kubwa kwa nje lakini ni tupu ndani yake. Kanisa lolote ambalo halijajengwa katika msingi wa imani ya neno la Mungu na injili ya kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho ni sawa na bustani isiyo na maji.
Yaweza kuwa ni mti, lakini umekufa na kushindwa kuzaa matunda. Kisima kinapokuwa hakina maji si kisima tena.
“Na mtu hodari atakuwa kama makumbi, na kazi yake kama cheche ya moto, nao watawaka pamoja wala hakuna atakayewazima.” Wale wote wasio na Roho wanaweza kuonekana wenye nguvu dhidi ya wengine, lakini machoni pa Mungu ni kama makumbi yaliyowekwa kwa ajili ya moto wa kuzimu.
Bwana anauliza “Ee mlinzi habari gani za usiku?” (Isaya 21:11). Wenye haki ambao ni wauzima wa milele imewapasa kuhubiri injili ya maji na Roho katika kiza cha usiku.
Mungu ni nuru na shetani ni kiza. Mungu huongoza watu kwenye haki na shetani huongoza watu kwenye mahekalu ya machafuko na theologia za uongo.
Katika nyakati za nabii Isaya, imani za watu zilikuwa katika machafuko kama ilivyo nyakati hizi. Walichanganya neno la Mungu na theologia na kanuni za kibinadamu. Ziliwapotosha watu wa Israel kwa matokeo machafu ya wanadamu hata kufikia Mungu kutowataka kabisa.
“Na kukuondoa bati lako lote. Nami nitarejeza upya waamunuzi wako kama walivyokuwa hapo kwanza” Sadaka isiyo kubalika kamwe kwa Mungu ni kama bati, mchanganyiko wa ukweli wa Mungu na kanuni za wanadamu.
Mungu haruhusu kamwe sadaka zilizochanganywa. Zaweza kuonekana safi kwa macho ya kibinadamu lakini ikiwa zimechanganywa na imani potofu za kibinadamu zimechanganywa na takataka na hivyo kutokukubaliwa na Mungu aliyeonyesha hasira yake kwa watu wa Israel, hasa wazushi, wahubiri bandia na wenye dhambi.
Ikiwa tutasoma Kutoka au Hesabu tunaweza kuona kuwa Mungu hakuwakasirikia hapo mwanzo. Mungu aliwasaidia watu wa Israeli na kuwapa baraka. Lakini baada ya kifo cha Yoshua, kuanzia Waamuzi, watu wa Israeli walivamiwa.
Ingawa walichagua kwenda njia zao, Mungu alimtuma nabii Yeremia na kuwaeleza watu wa Israeli kujisalimisha kwa Babeli. 
Hii inamaana ya kiroho, inamaanisha kuwa wenye haki kuwaambia wanao wafuata wazushi kujisalimisha kwenye injili ya maji na Roho.
 

MUNGU HUWAONYA WAZUSHI

Kwa nini Mungu huwaonya wazushi?
Kwa sababu hutumikia sanamu 
badala ya Mungu.

Kwa nini watumishi wa Mungu walionyesha hasira kwa watu wa Israeli? Kwa sababu walibadilisha mpangilio wa utoaji sadaka, kwa kuwateua watu wa kawaida kuwa makuhani na kubadilisha tarehe za utoaji sadaka.
Waliibadilisha siku ya upatanisho kutoka siku ya kumi ya mwezi wa saba kwenda siku ya tano ya mwezi wa nane na kuwateua makuhani nje ya kabila la Walawi. Hivyo walizuia njia ya kuzaliwa upya mara ya pili.
Mungu huchukizwa na wahubiri waongo. Wale wenye kumtumikia ndama wa dhahabu badala ya Mungu, ndiyo makuhani wazushi.
Ukweli ni kwamba Mungu alichukizwa nao kwa sababu tu walimwabudu ndama wa dhahabu. Je, wewe na mimi wakati mwingine hatuabudu sanamu pia? Tunatenda dhambi mara nyingi, lakini uovu wetu hauchukuliwi kuwa ni dhambi ya hatari kwa sababu tupo katika neema ya Mungu. Lakini kumweka ndama wa dhahabu kuchukua nafasi ya Mungu ni dhambi isiyo sameheka. Ndivyo hivyo pia inapoelekea kubadilisha mpangilio wa utoaji sadaka na kuwateua watu wa kawaida kuchukua nafasi ya ukuhani.
Ni jinsi gani ilivyo dhambi ya hatari! Ni dhambi mbaya zaidi. Mtu ataweza vipi kusamehewa kwa kumbadilisha Mungu na ndama wa dhahabu! Imeandikwa katika biblia kwmaba ilikuwa ni dhambi ya Yeroboamu ndiyo iliyoleta hasira ya Mungu.
Kama vile Mungu alivyoonyesha hasira yake katika kipindi cha Agano la Kale, leo hii anawaangamiza wenye dhambi walioko kinyume naye. Mungu aliwaambia waisrael kwamba atawalaani wale wote ambao hawakuacha kuabudu ndama wa dhahabu.
 

WAZUSHI HUTOA SADAKA KINYUME NA SHERIA

Yatupasa kufanya nini kabla 
ya kumtumikia Mungu?
Kwanza tupate utakaso wa 
dhambi zetu zote.
 
Wafalme na makuhani wazushi katika Israel walikwenda kinyume na Mungu na waliteua wale walio puuzia mpangilio wa utoaji sadaka wa kikuhani. Yeroboamu, mfalme aliye dhalimu, aliteua mtu ambaye hakutokea katika nyumba ya makuhani Walawi.
Ni wale tu waliotokea katika nyumba ya Walawi wangeweza kuwa makuhani na kufanya kazi hemani. Kwa uhakika zaidi, makuhani walipaswa wawe toka nyumba ya Haruni. Hii ilikuwa ni sheria ya Mungu milele. Lakini Yeroboamu aliteua makuhani nje ya nyumba ya Walawi na kutoa sadaka kwa ndama wa dhahabu. Yatupasa kujua ni vipi hili jambo lilileta hasira ya Mungu.
Hata leo, wale ambao hawajazaliwa upya mara ya pili wataweza kuwa wahudumu wa neno, wazee wa kanisa, mashemasi ndani ya Kanisa. Hii ni kinyume na sheria ya Mungu na huleta hasira yake. Je, Mungu hufurahishwa na sadaka za waovu? Wazushi imewapasa kuharibu ndama wa dhahabu na kumrudia Mungu waweze kuzaliwa upya mara ya pili.
Isaya 1:10-17 inasema “Lisikieni neno la Bwana enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora. Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea unafaida gani? Asema Bwana nimejaa mafuta ya kafara za kondoo waume na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng’ombe wala ya wana-kondoo, wala ya mbuzi waume. Mjapo ili kuonenkana mbele zangu ni nani aliyetaka neno hili mikononi mwenu kuzikanyaganyua zangu? Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na Sabato, kuita makutano, siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada. Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa nafsi yangu yazichukia, mambo hayo yanielemea nimechoka kuja kuchukua. Nanyi mkunjuapo mikono yenu, mtaficha macho yangu nisiwaone, naam mwombapo maombi mengi, sitasikia mikono yenu imejaa damu. Jiosheni, jitakaseni ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu acheni kutenda mabaya. Jifunzeni kutenda mema takeni hukumu na haki, wasaidieni walioonewa mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.”
Tunaposoma kifungu hiki kwa makini, tunaweza kuona vile viongozi wa kidini wa Israeli walivyo kuwa wakijitolea, ingawa katika kujitolea huko, walikuwa wakiangamia kwa sababu walitoa sadaka isiyo njema na kutoitii sheria ya Mungu.
Tunaweza kuona kwamba hawakuifuata sheria ya Mungu walipokuwa wakitoa sadaka na pia hawakuwa waangalifu kulifuata neno la Mungu. Viongozi hawa walikuwa ni watu wa kujitoa kwa sadaka zisizo na idadi mbele ya Mungu.Biblia inatuambia damu ilitiririka kama mto ndani ya Hema.
Hata hivyo Mungu alipoangalia walichokuwa wakikifanya, alisema kuwa hii ilikuwa ni kama dhambi ya Gomora tu. Aliona kwamba walikuwa wakitoa sadaka mbele yake, lakini ukweli ni kwamba walikuwa wakitenda dhambi tu. Alisema kuwa ingekuwa ni vyema zaidi kutokuleta sadaka hizo kabisa. Hakuhitaji kuzipokea kabisa.
Walipokuwa wakitoa sadaka mbele ya ndama wa dhahabu, Mungu hakuweza kuwasamehe. Hakuweza kuvumilia kabisa. Aliwaeleza kuwa walipaswa kutoa sadaka kulingana na amri yake. Ikiwa sivyo basi ingekuwa vyema kwao kutotoa sadaka hizo kabisa.
Sadaka hazikutolewa kwa Mungu katika namna iliyosahihi, matokeo yake, makuhani walikuwa wakitenda dhambi mbele ya Mungu. Yakupasa kujua kwamba kumtumikia Mungu na kutenda kazi yake pasipo kutakaswa dhambi, ni dhambi iliyo kuu mbele zake.
 

WAZUSHI HUFANANISHWA NA WAALIMU WA SHULE

Wazushi hufundisha 
juu ya nini?
Hufundisha juu ya maadili mema 
na siyo namna ya kuzaliwa 
upya mara ya pili.

Wazushi huonekana watakatifu kwa nje. Wanaposimama madhabahuni, huvutia wengi na kudanganya tokana na kuonekana kwao. Huonekana kuwa wa kweli. Na mara nyingi huitimisha mahubiri yao kwa kuwaasa watu kuwa wema. Haya ni mahubiri ya namna gani? Nini tofauti kati ya mahubiri yao na masomo ya walimu wa shule?
Kanisa la Mungu ni mahala ambamo wale wote waliozaliwa upya huja pamoja kumwabudu Mungu. Hili ndilo kanisa pekee na la kweli la Mungu. Kanisa la kweli la Mungu halijaribu kufundisha namna ya kuwa na tabia njema mbele ya Mungu. Wahubiri wa kanisa la kweli huubiri injili ya maji na Roho. Haijalishi jinsi ulivyo mdhaifu, Mungu amekutakasa kwa dhambi zako zote.
Wahubiri wazushi huwaambia wafuasi wao “Fanya hivi na usifanye vile”, huweka mzigo mzito juu yao, lakini wao hawana uwezo wa kuonyesha hata kidole kubeba.
Wahubiri wazushi huwanunulia watoto wao vifaa vya mziki,gari na kuwapeleka watoto wao ng’ambo kwa masomo. Kuhani anauwezo gani wa kufanya hivyo?Anapata wapi fedha? Kama kweli anayo fedha kiasi hicho kwa nini asiitumie katika kuhubiri injili? Je, mhubiri imempasa kuendesha gari gharama? Imempasa kuendesha gari ya anasa ili kujipatia hadhi? Muhubiri anayeendesha gari ya anasa ni mwizi! Wakati wafuasi wake hawawezi kugharamia hata kununua gari ya hali ya chini kabisa, itakuwa ni sawa kweli kwake kuwa na gari ya kifahari? Tunaweza kugundua wahubiri wazushi kwa kuangalia matendo yao.
Mhubiri mzushi hudai kulipwa kiasi kikubwa cha fedha. Makanisa mengine hulipa wahubiri kiasi cha dola 10,000 kwa mwezi. Na hii ni malipo rasmi. Hupewa ada za shule, ada za vitabu, ada ya matunzo ya watoto, fedha za ujio wa wageni, kwa uchache nimetaja.
Na bado wengi hulalamika kwamba hawakulipwa kiasi kinachotosha. Hupokea dola 10,000 kwa mwezi na kudai zaidi. Je, dola 10,000 kwa mwezi ni mshahara mdogo kweli? Mhubiri imempasa kuridhika kwa kupokea kiasi anachopata akiwa mhubiri wa injili ya maji na Roho.
Mhubiri wa kweli hupata faraja na amani kwa Mungu. Lakini mhubiri mzushi asiye na amani hudai nyongeza ya fedha. Wahubiri namna hii kweli huabudu ndama wa dhahabu.
Kanisa la Mungu mara nyingine huitwa Sayuni. Hakuna kanisa zuri kama Sayuni. Kanisa la Mungu mahala ambapo injili ya maji na Roho hu hubiriwa.
Isaya 1:21 inasema “Mji huu uliokuwa mwaminifu umekuwaje kahaba! Yeye aliyejaa hukumu ya haki; haki ilikaa ndani yake bali sasa wauaji!” Isaya analielezea kanisa la Mungu kwa kusema haki ilikaa ndani yake.
Mungu ni wa haki na msawa. Kwa kuwa sisi si wakamilifu kutokana na kuwa uzao wa Adamu, hivyo kuzaliwa tukiwa wenye dhambi Yesu alikuja duniani kututakasa na dhambi zetu kwa maji na kwa Roho. Huu ndiyo usawa wa Mungu.
Katika Agano la Kale, watu walipogundua kuwa si wakamilifu walikwenda mbele ya Mungu na kutoa sadaka. “Nimetenda kosa kadha wa kadha. Nilikosea” ndipo waliposamehewa dhambi zao za kila siku na pia kupata msamaha wa dhambi zote za mwaka mzima mara moja katika siku ile ya upatanisho.
Pia katika Agano Jipya, Yesu Kristo alikuja duniani na kubatizwa hivyo kuwa sadaka ili kutakasa dhambi za wanadamu mara moja na kwa wakati wote.
Lakini katika ibada ya siku ya mwaka mpya utakuta watu wanalia na kutubu “Mungu wangu tafadhali nisamehe kwa dhambi nilizotenda mwaka uliopita. Na tafadhali nibariki tena mwaka huu”. Watu hawa ni wazushi.
Hivyo basi, nini maana ya ukweli wa kuzaliwa kwa maji na kwa Roho? Yesu alikuja duniani takribani miaka 2000 iliyopita, alitakasa dhambi za wanadamu mara moja na kwa wakati wote kwa hivyo alituokoa milele. Alituokoa kwa dhambi zetu zote za dunia kwa maji na kwa damu. Lakini ikiwa tutaomba kusamehewa kila siku yeye atajibu nini? 
“Mji huu uliokuwa mwaminifu umekuwaje kahaba! Yeye aliyejaa hukumu ya haki, haki ilikaa ndani yake bali sasa wauaji” Yeyote anayejiita ni mwenye dhambi ni mzushi.
 

MAKUHANI WAZUSHI HAWAHUBIRI INJILI YA KUZALIWA UPYA MARA YA PILI KWA MAJI NA KWA ROHO.

Je, Mungu husikiliza sala 
za wenye dhambi?
Hapana. Hawezi kusikiliza kwa sababu 
dhambi zao zimewatenganisha 
na Mungu.

Mungu wetu huwaona wale wenye kumuamini na kuomba msamaha wa dhambi zao kama wauaji. Ikiwa wanatubu na pia kujiita wenye dhambi, je, wanategemea Yesu atarudi na kufa tena kwa ajili ya dhambi zao? Ubatizo wa Yesu na msalaba wake ni wokovu wa kweli.
Katika 1Petro 3:21 inasema kwamba, ubatizo wa Yesu ni mfano wa mambo ya wokovu. Yesu Kristo alikufa mara moja ili kuwaokoa wandamu wote kwa dhambi zao. Alitakasa dhambi zote za wanadamu mara moja na kwa wakati wote na kufufuka siku ya tatu. Ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 
Yesu Kristo alibatizwa mara moja na kufa mara moja msalabani kutuokoa dhambini milele. Alibatizwa na Yohana Mbatizaji alipofikisha umri wa miaka 30. Alikufa mara moja kutuokoa na dhambi zote ulimwenguni. Je, hukumu hii haikutolewa kwa wakati wote?
Ikiwa wazushi husema wao bado wenye dhambi basi wanamwita Yesu ashuke mara ya pili na kusulubiwa tena. Ukweli ni kwamba, maana yake ingempasa kuendelea kuja kufanya hivyo kila mara wanapo omba toba.
Wale wote wenye kuamini injili ya maji na Roho kwa moyo wao wote ndiyo waliookolewa toka dhambini daima, na kuwa wenye haki na kwenda mbinguni kupokea baraka ya Mungu na uzima wa milele. Yeyote akutanaye na walio haki ataweza kuokoka kupitia injili ya maji na Roho na kuwa kati ya watu wa Mungu waliobarikiwa. Mtu yeyote atakayewauliza waliohaki juu ya wokovu atabarikiwa mbele ya Mungu.
Hebu tusome Isaya 1:18-20 “haya njooni tusemezane asema Bwana, dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi, bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.”
Mungu anatuambia kuwa ikiwa tutakuwa watiifu kwa injili ya maji na Roho, tutakula mema ya nchi, bali ikiwa tutakataa na kuiasi tutaangamia kwa upanga.
Mungu wetu alisema “Haya njooni tusemezane. Je, wewe ni dhaifu? Si mwenye haki? Unaipenda nafsi yako kupita kiasi? Huwezi kufuata amri zangu? Huwezi kufanya vile sheria inavyoamrisha? Unaelewa lakini huwezi kutenda mema? Sasa basi, njoo kwangu. Ingawa dhambi zako zijapokuwa nyekundu zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa kama sufu.” Maana yake ni kwamba, Mungu amewaokoa wenye dhambi kwa stahiki na kuwafanya wenye haki.
Hapakuwa na dhambi hapo mwanzo Mungu alipowaumba Adamu na Hawa. Lakini mara shetani alipotokea. Aliwajaribu ili wasimtii Mungu na kuwafanya wanadamu wote kuwa wenye dhambi, kwa kushawishi kwa dhambi shetani alisababisha wanadamu kuanguka. Mwanzo Adamu na Hawa hawakuwa wenye dhambi mbele ya Mungu. Waliishi na Mungu bustanini Edeni. Lakini wakawa wenye dhambi. Hivyo sasa Mungu anatuita sisi. Haya njooni, tusemezane!
“Dhambi ngapi unatenda duniani? Na ni ngapi utakazoendelea kutenda hadi mwisho wa kifo chako?”
“Ah, Mungu. Si rahisi kwangu kutotenda dhambi, hatuwezi kutakasika hata tukijitahidi vipi.”
“Sawa, ni dhambi ngapi umekwisha tenda hadi sasa?”
“Ndiyo, Bwana, siwezi kukumbuka kila kitu, lakini ni chache zilizo katika kumbukumbu siku ile? Unajua ninachosema…na pia kuna siku moja, unajua...”
Ndipo Mungu atasema “sasa nieleze, unadhani ni hizo tu? Unajua ngapi zaidi ya hizi? Hata hivyo dhambi unazokumbuka, zile ulizosahau na hata zile utakazotenda mbeleni, nazitakasa zote milele. Lakini si zako tu bali hata za kizazi chako na warithi wako. Mimi ni Mungu wa haki. Nimetakasa dhambi zako mara moja kwa wakati wote na kwa wote.”
Mungu aliyetakasa dhambi zote za wanadamu tokea dhambi ya Adamu hadi mwanadamu wa mwisho duniani, ndiye Alpha na Omega, mwanzo na mwisho.
“Mimi ni mwokozi na mwenye enzi Mungu.”
“Mimi ni Yehova Mungu anayesamehe.”
“Nitakuwa na msamaha kwa wenye kustahili kusamehewa na nitakuwa na huruma kwa wenye kustahili huruma.”
Tunapoomba msamaha na kuwa wakweli kwake, tutaweza kupata huruma yake. Baba yetu anataka kutubariki sisi sote. Anataka sisi sote kuwa wenye haki. Kwa upendo na huruma yake, anataka kutufanya sisi sote kuwa watoto wenye haki.

Mungu anatuhitaji tufanye 
nini baada ya kuzaliwa upya?
Anatuhitaji kuihubiri injili 
ulimwenguni pote.

Anatuhitaji tutakasike tuwe kama theluji. Yesu ametakasa dhambi za wanadamu mara moja kwa wakati wote kupitia ubatizo na damu. Ikiwa kanisa halitoweza kusuluhisha tatizo la dhambi na uzima kwa waumini wake kamwe halitoweza kuitwa kanisa la Mungu.
Watu huenda kwa wachungaji na kuwauliza “Nina dhambi, hivyo nifanyeje? Nimetubu na kutubu mara nyingi lakini bado ninadhambi. Siwezi kuendelea. Sidhani kama nitaweza kuendelea tena na maisha ya dini.” Ikiwa mchungaji hatoweza kumpa mtu huyu jibu sahihi la tatizo lake, ni mzushi. Ataweza kusema “shauri lako. Kafanye maombi mlimani. Jaribu siku 40 kufunga.”
Makuhani wazushi au viongozi wa dini wamejaa uchafu kiasi cha hata kutofahamu injili ya maji na Roho. Hawajui kama roho zao zitaishia motoni au mbinguni.
Wale walio wazee wa kanisa hawana haki mbele ya Mungu. Ni wakristo bandia na wazushi. Huonekana kama wanamwamini Yesu kwa nje lakini moyoni wamejaa uovu. Hawajatakaswa na dhambi zao. Hawawezi kuhubiri injili ya maji na Roho yenye kuleta utakaso. Hebu na tusidanganywe nao.
Tito 3:10-11 huwaeleza wazushi kuwa “mtu alioyemzushi baada ya kumwonya mara moja ya kwanza na mara ya pili, mkatae, ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotea, tena atenda dhambi maana amejihukumu yeye mwenyewe.” Kwa sababu wanamwamini Yesu lakini hawajazaliwa upya mara ya pili hujihukumu wenyewe kuwa ni wenye dhambi. Hupuuza na kuchezea injili ya maji na Roho kwa kudai kuwa ni wenye dhambi watakao kwenda motoni.
Ni wazushi katika ukristo. Yeyote amwaminiye Yesu hali anabaki kuwa na dhambi ni mzushi. Mzushi hutofautiana na Mungu. Mungu ni Mtakatifu. Lakini wao si watakatifu. Wale wote wenye kuamini injili ya maji na Roho hutakaswa dhambi zao zote. Hivyo anayemwamini Yesu lakini bado anadhambi ni mzushi. Yatupasa kuwa mbali nao.
Hebu na tuhubiri injili kwa wale wote ambao hawajisikia bado na wale wote wenye kutaka kuiamini lakini hawaijui. Tuwasaidie kuzaliwa upya mara ya pili. Tuwakemee wale wenye kusimama kinyume na injili ya maji na Roho.
Yatupasa kuhubiri injili ya kuzali upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho ulimwenguni pote. Amina.