Search

VITABU VILIVYOCHAPISHWA BURE,
VITABU NA VITABU VYA AUDIO

Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo - JE, NYAKATI ZA MPINGA KRISTO, KUFIA-DINI, KUNYAKULIWA NA UFALME WA MILENIA ZINAKUJA? (Ⅰ)
  • ISBN8983141689
  • Kurasa351

Kiswahili 7

Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo - JE, NYAKATI ZA MPINGA KRISTO, KUFIA-DINI, KUNYAKULIWA NA UFALME WA MILENIA ZINAKUJA? (Ⅰ)

Rev. Paul C. Jong

YALIYOMO 
 
Dibaji 

SURA YA 1 
1. Lisikie Neno la Ufunuo wa God (Ufunuo 1:1-20) 
2. Ni Lazima Tuzifahamu Nyakati Saba 

SURA YA 2 
1. Barua Kwa Kanisa la Efeso (Ufunuo 2:1-7) 
2. Imani Inayoweza Kukubaliana na Kuifia-dini 
3. Barua Kwa Kanisa la Smirna (Ufunuo 2:8-11) 
4. Uwe Mwaminifu Hadi Kifo 
5. Ni Nani Aliyeokolewa Toka Katika Dhambi? 
6. Barua Kwa Kanisa la Pergamo (Ufunuo 2:12-17) 
7. Wafuasi wa Fundisho la Imani ya Wanikolai 
8. Barua Kwa Kanisa la Thiatira (Ufunuo 2:18-29) 
9. Je, Umeokolewa Kwa Maji na Roho? 

SURA YA 3
1. Barua Kwa Kanisa la Sardi (Ufunuo 3:1-6) 
2. Wale Ambao Hawakuyachafua Mavazi Yao Meupe 
3. Barua Kwa Kanisa la Filadelfia (Ufunuo 3:7-13) 
4. Watumishi na Watakatifu wa God Wanaoufurahisha Moyo Wake 
5. Barua Kwa Kanisa la Laodikia (Ufunuo 3:14-22) 
6. Imani ya Kweli kwa Maisha ya Ufuasi 

SURA YA 4
1. Mtazame Yesu Anayeketi Katika Kiti cha Enzi cha God (Ufunuo 4:1-11) 
2. Yesu ni God

SURA YA 5 
1. Yesu Aliyetawazwa Kuwa Mwakilishi wa God Baba (Ufunuo 5:1-14) 
2. Mwana-Kondoo Aketiye Katika Kiti cha Enzi 

SURA YA 6
1. Nyakati Saba Zilizopangwa na God (Ufunuo 6:1-17) 
2. Nyakati za Mihuri Saba 

SURA YA 7
1. Ni Nani Atakayeokolewa Wakati wa Dhiki Kuu? (Ufunuo 7:1-17) 
2. Hebu Tuwe na Imani Inayopigana Vita 
 
 
Baada ya mashambulio ya kigaidi ya tarehe 11 mwezi Septemba kulitokea msongamano katika tovuti hii "www.raptureready.com," ambayo ni tovuti inayotoa habari juu ya nyakati za mwisho, iliripotiwa kuwa watumiaji wa tovuti hiyo walizidi zaidi ya milioni 8. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa ushirikiano kati ya kituo cha CNN na kile cha TIME ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 59 ya Wamarekani wanaamini katika mafundisho ya siku za mwisho.
Akijibu masuala hayo ya nyakati, mwandishi anatoa ufafanuzi wa mada kuu za kitabu cha Ufunuo, zikiwemo mada za kuja kwa Mpinga-Kristo, Kufia-Dini, yaani kufa kwa watakatifu kwa ajili ya dini, Kunyakuliwa, Ufalme wa Milenia, na Mbingu na Nchi Mpya, zote zikitoka katika mazingira ya maandiko yote na chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.
Kitabu hiki kinatoa maelezo katika mfumo wa komentare wa aya kwa aya toka katika Kitabu cha Ufunuo huku aya hizo zikiongezewa nguvu na mahubiri ya kina toka kwa mwandishi. Yeyote atakayesoma kitabu hiki atakuja kuifahamu mipango ambayo God anayo kwa ulimwengu huu.
Sasa ni wakati wako kutambua juu ya hitaji kamilifu la kuamini katika injili ya maji na Roho ili uweze kuipata hekima inayoweza kukukomboa toka katika majaribu na taabu zote za nyakati za mwisho. Kwa kupitia vitabu hivi viwili na kwa kuamini katika injili ya maji na Roho utaweza kuyashinda majaribu na taabu zote zilizotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo. 
Kupakua kitabu mtandaoni
PDF EPUB

Vitabu vinavyohusiana na kichwa hiki