Search

VITABU VILIVYOCHAPISHWA BURE,
VITABU NA VITABU VYA AUDIO

HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA: Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo (Ⅰ)
  • ISBN8983147571
  • Kurasa414

Kiswahili 9

HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA: Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo (Ⅰ)

Rev. Paul C. Jong

YALIYOMO
 
Dibaji 
1. Wokovu wa Wenye Dhambi Uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-21) 
2. Bwana Wetu Aliyeteseka Kwa Ajili Yetu (Isaya 52:13-53:9) 
3. Yahwe God Aliye Hai (Kutoka 34:1-8) 
4. Sababu Iliyomfanya God Amuite Musa Kwenda Katika Mlima Sinai (Kutoka 19:1-6) 
5. Jinsi Ambavyo Waisraeli Walianza Kutoa Sadaka Katika Hema Takatifu la Kukutania: Msingi wa Kihistoria (Mwanzo 15:1-21) 
6. Ahadi ya God Iliyothibitishwa Katika Agano Lake la Tohara Bado Inafaa na Ni Muhimu Kwetu (Mwanzo 17:1-14) 
7. Vifaa vya Ujenzi vya Hema Takatifu la Kukutania Vilivyoweka Msingi wa Imani (Kutoka 25:1-9) 
8. Rangi ya Lango la Ua wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-19) 
9. Imani Inayodhihirishwa Katika Madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa (Kutoka 27:1-8) 
10. Imani Iliyodhihirishwa katika Birika la Kunawia (Kutoka 30:17-21) 
11. Shuhuda za Wokovu 
 
 
Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na ya Roho Mtakatifu tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili.
Kwa kweli, rangi za bluu, Zambarau, na nyuzi nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo.
Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho Mtakatifu, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika rangi za bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania.
Kupakua kitabu mtandaoni
PDF EPUB
Kitabu cha Sauti
Kitabu cha Sauti

Vitabu vinavyohusiana na kichwa hiki