Search

VITABU VILIVYOCHAPISHWA BURE,
VITABU NA VITABU VYA AUDIO

Waraka wa Kwanza wa Yohana

Mfululizo wa Paul C. Jong Juu ya Ukuaji wa Kiroho Kitabu cha 3 - Waraka wa Kwanza wa Yohana (Ⅰ)
  • ISBN9788928239122
  • Kurasa333

Kiswahili 14

Mfululizo wa Paul C. Jong Juu ya Ukuaji wa Kiroho Kitabu cha 3 - Waraka wa Kwanza wa Yohana (Ⅰ)

Rev. Paul C. Jong

Yaliyomo
 
Dibaji 

SURA YA 1
1. Yesu Kristo ni God (1 Yohana 1:1-10) 
2. Je, Ni Kweli Kuwa Una Ushirika na God? (1 Yohana 1:1-10) 
3. Aina Mbili za Ungamo (1 Yohana 1:8-10) 
4. Ungamo Katika Kweli (1 Yohana 1:8-10) 

SURA YA 2
1. Yesu Kristo ni God wa Kweli (1 Yohana 2:1-5) 
2. Bwana Wetu Aliyefanyika Kuwa Mwombezi Wetu (1 Yohana 2:1-17) 
3. Je, Unaishi Kwa Kuzifuata Amri za God? (1 Yohana 2:7-11) 
4. Msiipende Dunia Wala Vitu Vilivyomo Ndani Yake (1 Yohana 2:15-17) 
5. Maadui wa Kristo ni Akina Nani? (1 Yohana 2:18-29) 
 
 
Mtume Yohana ni mmoja kati ya viongozi wakuu wa kiroho katika Ukristo. Nyaraka zote tatu alizoziandika bado zinaushuhudia Ukweli mkuu wa kiroho kwa watakatifu katika Kanisa la God. Lakini kuna baadhi ya vifungu ambavyo ni vigumu kwetu kuvielewa na kuvifafafanua vizuri.
Tunaweza kuangalia 1 Yohana 1:8 kama moja kati ya vifungu vigumu katka Nyaraka za Yohana: "Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu." Kifungu hiki ni kigumu sana kuweza kukifahamu, hasa pale tunapokitumia kwa waamini wanaoamini katika injili ya maji na Roho.
Mfano wa pili ni kifungu kinachopatikana katika 1 Yohana 1:9, "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote." Kifungu hiki ni kati ya vifungu ambavyo vimekuwa vikinukuliwa mara kwa mara na wenye dhambi wanapojaribu kutoa msingi wa kibiblia kuhusiana na sala zao za toba. Je, kifungu hiki kina maanisha kwamba wenye dhambi wanapaswa kuziungama dhambi zao ili waweze kusamehewa kutokana na dhambi walizozitenda? Au, je, kifungu hiki kina maanisha kwamba wenye haki wanaoamini katika injili ya maji na Roho wanapaswa kuziungama dhambi zao? Tunapaswa kukiamini kifungu hiki kwa mujibu wa ufafanuzi toka kwa Roho Mtakatifu, toka kwa Mwandishi wa Biblia, na kwa kuzingatia nia aliyokuwa nayo Mtume Yohana.
Mfano wa tatu kuhusiana na vifungu vigumu ni ule unaotoka 1 Yohana 2:22, "Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana." Kifungu hiki kinazungumzia juu ya maadui wa God. Kifungu hiki kinaweka bayana kwamba maadui wa God ni wale wasioamini kwamba Yesu ni God. Na kwa kufanya hivyo maadui hao wanakana kwamba God si Baba wa Yesu Kristo.
Mfano wa nne unatoka 1 Yohana 3:6 ambapo aya hii inasema, "Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua." Katika kifungu hiki tunapooma maneno yanayosema "Kila akaaye ndani yake," basi tunatambua kwamba kifungu hiki kimetolewa kwa ajili ya wenye haki walioasafishwa dhambi zao zote kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Wenye haki hawawezi kuikana imani yao katika hali yoyote ile, hii ni kwa sababu wanaiamini injili ya kweli. Je, inawezekana wakawepo baadhi ambao hawatendi dhambi kwa miili yao? Ukweli ni kuwa kila mmoja anatenda dhambi. Lakini waamini wa injili ya maji na Roho hawawezi kufanya dhambi ya kuikana injili ya kweli.
Kupakua kitabu mtandaoni
PDF EPUB

Vitabu vinavyohusiana na kichwa hiki