Search

VITABU VILIVYOCHAPISHWA BURE,
VITABU NA VITABU VYA AUDIO

Waraka wa Paulo Mtume kwa Wagalatia

Mahubiri kupitia Wagalatia - KUTOKA TOHARA YA MWILI HADI MAFUNDISHO YA TOBA (I)
  • ISBN9788928239382
  • Kurasa449

Kiswahili 16

Mahubiri kupitia Wagalatia - KUTOKA TOHARA YA MWILI HADI MAFUNDISHO YA TOBA (I)

Rev. Paul C. Jong

Yaliyomo
 
Dibaji 

SURA YA 1
1. Bwana Ametukomboa Toka Katika Ulimwengu 
2. Huu Wenye Uovu (Wagalatia 1:1-5) 
3. Pengine Imani Yako Ni Kama ya Wanatohara? (Wagalatia 1:1-5) 
4. Bwana Ametukomboa Kikamilifu Mara Moja na Kwa Wote (Wagalatia 1:3-5) 
5. Hakuna Injili Nyingine Zaidi ya Injili ya Maji na Roho (Wagalatia 1:6-10) 
6. Wale Ambao Mioyo Yao Imeandaliwa Kama Watumishi wa God (Wagalatia 1:10-12) 
7. Imani ya Mtume Paulo na Maonyo Yake Kwa Wanatohara (Wagalatia 1:1-17) 
8. Maisha ya Kiimani ya Kisheria Huleta Laana Tu (Wagalatia 1:1-24) 

SURA YA 2
1. Ni Kwa Nini Mtume Paulo Aliwapuuza Waishio Kisheria? (Wagalatia 2:1-10) 
2. Kiini cha Imani ya Paulo (Wagalatia 2:20) 
3. Je, Sisi Tumekufa na Kufufuka Pamoja na Yesu Kwa Imani Katika Mwana wa God? (Wagalatia 2:20) 
4. Mtu Hahesabiwi Haki Kwa Matendo ya Sheria Bali Kwa Imani Katika Injili ya Maji na Roho (Wagalatia 2:11-21) 
5. Tunahesabiwa Haki Kwa Imani Safi Tu (Wagalatia 2:11-21) 

SURA YA 3
1. Wakati Wote Uishi Maisha Yako Kwa Imani Katika Injili Ya Maji na Roho (Wagalatia 3:1-11) 
2. Ni Wakati Gani Ambapo Utupu wa Mioyo Yetu Unapotoweka? (Wagalatia 3:23-29) 
3. Sasa Hatupaswi Kuwa Chini ya Laana ya Sheria (Wagalatia 3:1-29) 
 
 
Mafundisho ya Toba Yanatosha Kukufanya Upate Ugonjwa wa Kiroho.

Ulimwenguni kote watu wanaogopa virusi kama vile vya SARS kwa kuwa wanaweza kufa kutokana na kuambukizwa na virusi hivyo visivyoonekana.
Vivyo hivyo, Wakristo wengi siku hizi ulimwenguni kote wanakufa kimwili na kiroho kutokana na kuathiriwa na mafundisho ya toba. Ni nani ambaye alifahamu jinsi mafundisho ya toba yalivyo potofu kiasi hicho?
Unafahamu ni nani aliyewafanya Wakristo kuangukia katika mkanganyo wa kiroho? Ni Wakristo wenye dhambi wenyewe ambao wanaendelea kutoa sala za toba kila siku ili waweze kuzisafisha dhambi zao binafsi huku wakidai kuwa wanamwamini Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wao.
Hivyo unapaswa kupokea ondoleo la dhambi zako kwa kuliamini Neno la injili ya maji na Roho ambalo kwa asili ndilo ambalo God alitupatia. Haupaswi kuipoteza nafasi hii yenye baraka ya kuweza kuzaliwa tena upya. Sisi sote tunapaswa kukombolewa toka katika mkanganyo wa kiroho kwa kuuamini Ukweli wa injili ya maji na Roho. Tunapaswa kuiangalia nuru ya Ukweli ambayo ilikuja kupitia injili ya maji na Roho, na nuru hiyo ilikuja baada ya kuyatoroka mashimo ya mkanganyo wa kiroho.
Kupakua kitabu mtandaoni
PDF EPUB

Vitabu vinavyohusiana na kichwa hiki