Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 1-1] Utangulizi katika Kitabu cha Warumi Sura ya 1

“Waraka wa Paulo Mtume kwa Warumi” unaweza kuchuliwa kuwa ni hazina ya Biblia. Inahusika zaidi na namna ya mtu awezavyo kupata haki ya Mungu kwa kuiamini Injili ya maji na Roho. Ukilinganisha Waraka kwa Warumi na ule Waraka wa Yakobo, wapo wanaouelezea huu wa kwanza kama “maneno mfano wa mrija wakufyonzea” Hata hivyo Yakobo ni neno la Mungu kama ilivyo Warumi.Tofauti pekee ni kwamba, katika Warumi ni wathamani kwa sababu unatoa mtazamo wa kijumla katika biblia, hali Yakobo uthamani wake nao upo katika neno ambalo linalowawezesha wenye haki kuishi kwa mapenzi ya Mungu.
 

Paulo ni mtu wa namna gani?
 
Hebu tusome Warumi 1:1-7, “Paulo mtumwa wa Kristo Yesu aliyeitwa kuwa mtu, na kutengwa ahubiri Injili ya Mungu ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu yaani habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu, ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo kwa wote walioko Rumi wapendwao na Mungu walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.”
Ujumbe huu unaweza kusemekana kama ni “salamu za Paulo kwa Wakristo wa Rumi.” Paulo anawasalimu akiwa kama mtumwa wa Yesu Kristo aliye haki ya Mungu.
Mstari wa 1 unazungumzia juu ya swali “Paulo ni nani?” Alikuwa ni Myahudi aliye kutana na Bwana mfufuka akiwa njiani kuelekea Dameski na ambaye alichaguliwa kama chombo cha Bwana (Matendo 9:15) katika kueneza Injili kwa watu wa Mataifa.
 

Paulo alieneza Injili ya kweli iliyo katika msingi wa mpangilio wa sadaka ya dhambi na unabii wa Agano la kale.
 
Katika mstari wa 2 Paulo Mtume alikuwa akieneza Injili iliyo na msingi wa maneno ya Agano la kale. Alielezea kuwa ni “Injili ya Mungu” ikiwa ndiyo “Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu” kwa kupitia mistari hii tunaweza kuona kwamba Paulo alichaguliwa kutenda kazi ya Injili.
Msemo “kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu” yanamaanisha ahadi za Mungu katika kumtuma Yesu Kristo aliye kuja akiwa katika mwonekano wa mpangilio wa sadaka ya dhambi au unabii wa Agano la kale. Manabii wote wa Agano la Kale akijumuishwa Musa Isaya Ezekiel, Jeremiya na Danieli walishuhudia ya kwamba Yesu Kristo atakuja ulimwengunguni na kufa msalabani baada ya kubeba dhamba za dunia.
Je! ni injili gani ambayo mtume Paulo alitoa? Alihubiri injili ya maji na Roho iliyozungumza juu ya Mwana wa Mungu, Yesu Kristo.
Baadhi ya watu husema ya kwamba maneno ya Agano la Kale yalifikia ukomo wake kwa wakati huo na kusisitiza usemi huo huku wakinukuu Mathayo 11:13 kama ushahidi. Baadhi ya wainjilisti mashuhuri wamefikia hata kudharau sehemu hii ya Agano la Kale.
Hata hivyo Mungu aliweka ahadi nasi kupitia Agano la Kale na tayari amekwisha itimiza ahadi hii kwa njia ya Yesu Kristo katika Agano Jipya. Hivyo katika ulimwengu wa imani, Agano la Jipya halitoweza kuwepo pasipo Agano la Kale na ndivyo ilivyo hata kwa Agano la Kale pia haliwezi kuwepo pasipo Agano Jipya na hata kutimizwa.
Paulo Mtume alichaguliwa kwa ajili ya Injili ya Mungu. Sasa basi, swali ni hili, “Aina gani ya Injili aliyo ihubiri?” Alihubiri ukweli ule wa Yesu Kristo kuja duniani na kutuokoa kwa dhambi zetu zote kupitia Injili ya maji na Roho ambayo msingi wake ni Agano la Kale. Hivyo kila tunapo ihubiri Injili ya maji na Roho yatupasa pia kufanya hivyo kwa msingi wa unabii na mpangilio wa sadaka ya dhambi ulio kuwa nyakati za Agano la Kale. hapo ndipo watu watakapo amini kwamba Injili ya maji na Roho ni ya kweli na pia kwamba Agano Jipya ni kutimia kwa maneno ya ahadi za Agano la Kale.
Tokea mwanzo wa Agano la Kale, tunaweza kuona kwamba mkazo ulitiliwa katika ubatizo wa Yesu alio upokea kwa Yohana na damu yake msalabani. Huku ikiwa kiini cha Agano la Kale palikuwemo mpangilio wa sadaka ya dhambi ambayo ni ukombozi wa wenye dhambi. Mtu mume au mke ilimpasa aweke mikono yake juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi na kumwaga damu yake kwa kifo cha kuchinjwa shingo ili aweze kusamehewa dhambi.
Sasa ikiwa palikuwemo na kuwekewa mikono na damu ya sadaka za wanyama kwa ajili ya ondoleo la dhambi wakati huo wa Agano la Kale, Nini kilicho kuwemo katika Agano Jipya? Palikuwemo na ubatizo wa Yesu alioupokea na damu yake msalabani. Zaidi ya haya Kuhani iliyetajwa katika Agano la Kale (Walawi 16:21) Linalinganishwa na Yohana Mbatizaji katika Agano Jipya.
Mstari wa 3 na 4 unazungumzia swali juu ya “Yesu alikuwa ni mtu wa namna gani?” Mstari unazungumzia juu ya wasifu wake kiujumla. Yesu Kristo alikuwa ni wa uko wa Daudi kimwili kwa Roho Mtakatifu, alifahamika akiwa kama mwana wa Mungu kwa nguvu ya ufufuko wake toka kifoni. Hivyo basi, akawa Mwokozi kwa kuleta maji na damu kwa wale wote wenye kumwamini akiwa Mfalme wa Wafalme na Kuhani Mkuu wa milele Mbinguni kwa wenye kuamini.
Katika baadhi ya theologia za Kikristo Uungu wa Yesu umekuwa ukikataliwa kabisa. Theolojia hizi husema “Alikuwa mfano mzuri wa kijana”. Zaidi ya hayo kulingana na theologia ya Kisasa, husema “upo wokovu katika dini zote” Hivyo katika seminari za kileo, watu husisitiza ya kwamba imewapasa pia kuamini matendo ya kuagua mashetani, dini ya Kibudha, dini ya Kikatoliki na nyingi nyinginezo katika ulimwengu huu. Hiki kinachoitwa theologia ya Kileo au theologia Mpya husema kwamba kila jambo ni lazima liheshimiwe na kukubalika na hivyo wanadamu wote imewapasa kuungana na kuwa “wamoja”.
Hata hivyo ilikwisha semwa kwa uwazi katika Biblia kwamba hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Sasa basi Mungu huyu ni nani? Ni Yesu Kristo, Jina “Kristo” maana yake, “yeye aliye pakwa mafuta kichwani kwake”. Katika Agano la Kale mfalme au nabii ndiye aliye pakwa mafuta kichwani na Kuhani Mkuu. Hivyo basi Yesu anasemekana kuwa ndiye Mfalme wa Wafalme. Mtu akataaye kuwa Yesu ni Mungu huyu si muumini wa Mungu.
Siku hizi imani za watu ulimwenguni pote zimegeuka kuwa ni za kimu ungano wa kimadhehebu ya aina mbali mbali (ecumenicalism) yaliyo katika msingi wa wingi wa kidini. Husifu na kuabudu huku wakichanganya mambo ya aina mbali mbali toka dini za kigeni kama vile za Kibudha (Buddhism) na Kunfusia (cunfucianism). Katika wakati fulani mkusanyiko huabudu kwa njia za kibudha, na wakati mwingine hufanya kwa njia za kikristo. Labda paweza pakawa na muunganiko wa mlo, hata hivyo inapokuja swala la imani, basi ile iliyo halisi ni muhimu zaidi.
Hivyo jibu ni kwamba kwa swali la mstari wa 3 na 4 “Yesu ni nani?” yeye ndiye pekee aliye kubalika akiwa mwana wa Mungu kwa nguvu ya ufufuko wake toka kifoni. Kristo amekuwa Bwana na Mwokozi kwetu.
Mistari ya 5 na 6 inazungumzia namna Paulo alivyo kuja kuwa Mtume kupitia Mungu. Akawa mshuhudiaji katika kuihubiri Injili kwa watu wa Mataifa ili nao waweze kupokea wokovu kwa kumwamini Yesu Kristo.
 

Mamlaka gani Paulo Mtume alikuwa nayo?
 
Kama ilivyo andikwa mstari wa 7 Paulo Mtume alikuwa na mamlaka kubariki waumini katika Yesu kwa jina la Mungu. Mamlaka ya Mtume maana yake ni nguvu za kiroho za kuweza kubariki watu wote kwa njia ya jina la Yesu Kristo.
Kwa hivyo, Paulo angeweza kusema, “Neema na iwe kwako kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.”
Hapa ningependa kutafakari kidogo zaidi juu ya hizi baraka. Inaonekana ya kwamba Paulo Mtume alikuwa na mamlaka za kufanya baraka kwa watu. Nasi kila tumalizapo ibada siku za Jumapili tunahitimisha kwa kusema “Bwana akubarikie na kukulinda,Bwana akuangazie nuru za uso wake na kukufadhili, Bwana akuinulie uso wake na kukupa amani”. Mungu anatamani kutoa aina hii ya baraka kwa watakatifu. Asili ya maneno ya baraka ni kama ifuatavyo.
Hebu tuanze na Hesabu 6:22 “Kisha Bwana akanena na Musa na kumwambia, Hivi ndivyo mtakavyo wabariki wana wa Israeli mtawaambia, Bwana akubarikie na kukulinda, Bwana akuangazie nuru za uso wake na kukufadhili, Bwana akuinulie uso wake na kukupa amani.”
Haruni Kuhani Mkuu na wana wake waliambiwa “Hivi ndiyvo mtakavyo wabariki wana wa Israeli”. Ikiwa wange wabariki Waisraeli namna hii, Mungu angewabariki kama ilivyo andikwa katika maandiko. Tunapo angalia nyaraka zote za Paulo tunaweza kuona mara kwa mara akisema “Neema ya Bwana iwe juu yenu” Hii inaonyesha kwamba hakuwa yeye binafsi aliyeweza kutoa baraka bali alikuwa ni Mungu aliyefanya hivyo. Hivyo, Paulo Mtume mara zote alitoa baraka kwa watakatifu kila alipomaliza nyaraka zake.
Paulo alikuwa na mamlaka kutoa baraka kwa watu wa Mungu. Mamlaka hii haikupewa kwa wahudumu wote wa Kikristo. Badala yake ilitolewa kwa watumishi wa Mungu pekee. Mtumishi wa Mungu anapofanya baraka akisema kwamba awatakia baraka, ndipo hapo Mungu anatoa baraka hizo kulingana haswa na baraka.
Mungu ametoa mamlaka za kimbingu si kwa watumishi wake tu, bali pia kwa watakatifu wote walio zaliwa upya mara ya pili. Mungu husema “Wowote mtakao waondolea dhambi, wameondolewa, na wo wote mtakao wafungia dhambi wamefungiwa” (Yohana 20:23). Ametoa aina hii ya mamlaka kwa wale wote wenye haki. Hivyo, mtu imempasa awemwangalifu katika kukabilana na mtakatifu aliye zaliwa upya, kwa sababu ni sawa na kukabiliana na Mungu mwenyewe. Mungu ametoa mamlaka ya kubariki na kulaani kwa wale Mitume pamoja pia na watumishi na wenye haki.
 

Paulo Mtume mwenye kupenda kugawa vipawa vya kiroho kwa Watakatifu.
 
Tusome Warumi 1:8-12 “Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inahubiriwa katika dunia nzima kwa maana Mungu ni mwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake, nishahidi yangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma sikuzote katika sala zangu, ni kiomba nije kwenu hivi karibuni, Mungu akipenda kuifanikisha safari yangu kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya rohoni ili mfannye imara yaani tufarijiane mimi na nyinyi kila mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.”
Kwanza kabla ya yote, Mtume Paulo alikuwa akimshukuru Mungu kwa ajili ya nani? Alimshukuru Mungu kwa ajili ya Wakristo wa Roma kwa sababu walikuwa wakimwamini Yesu na kwa kupitia wao Injili ilihubiriwa kwa watu wote.
Katika mstari wa 9 na 10 mtu angeliweza kuuliza swali, “Kwa nini Paulo Mtume alitaka kwenda Roma wakati wa safari za huduma yake?” Sababu yake ilikuwa ni kwamba endapao Injili ya maji na Roho ingelihubiriwa Roma kwa wakati huo ingeliweza kusambaa ulimwenguni pote. Kama Amerika, kwa nyakati hizi, Roma ilikuwa ndiyo kitovu cha ulimwengu kama ilivyo ule usemi usemao “Barabara zote huelekea Roma.”
Tunafanya juhudi kubwa kuihubiri Injili hii Amerika. Tutakapo ihubiri Injili hii ya maji na Roho Mtakatifu kule Amerika, wamisionari wengi watachipuka na kwenda ulimwenguni hata kuihubiri Injili njema kwa wengine. Ndiyo maana Paulo alipenda kwenda Roma.
 

Karama ya rohoni ambayo Paulo alikuwa akiizungumzia
 
Katika mstari wa 11 imeandikwa “Kwa maana ninatamani sana kuwaona nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara.”
Paulo Mtume alikua akimaanisha nini juu ya kutoa karama ya rohoni ili watu wafanywe imara? Karama ya Rohoni aliyokuwa akiizungumzia ni ile Injili ya maji na Roho ambayo nasi twaihubiri. Katika mstari wa 12 imeandikwa “yaani, tufarijiane mimi na nyinyi kila mtu kwa imani ya mwezake yenu na yangu”. Kwa usemi wa kwamba karama ya roho zitawekwa juu ya watu ili kuwawezesha kuwa imara na kuwatia moyo katika imani moja kati yao wao na Paulo ilkuwa ni kwa sababu ya kuipeleka Injili ya maji na Roho. Kwa yeye alipenda kuona watu wakitulia na kufanyika wakipokea baraka hatimaye kuwa na ushirika ndani ya imani hii ya aina moja.
Usemi wa Paulo Mtume kutaka kufanyika pamoja kwa njia ya imani moja unaonyesha jinsi ile anavyo tamani kuendelea kuihubiri Injili ya maji na Roho Mtakatifu kwa mara nyingine katika kanisa la Roma. Sasa washirika wote wa kanisa letu wanaelewa na kuamini kwa dhati katika Injili ya maji na Roho, ingawa kunaonekana na baadhi ya Wakristo wa majina wasio amini bado injili hii ya kweli kuwa ujumbe ulipo kuwa si chochote kwao. Kwa namna hii kanisa la Roma litaweza kuhitaji Injili upya.
Hivyo Paulo Mtume alisema kwamba angeliweza kutiwa moyo kwa imani ya pamoja. Hakika tunapata faraja mbele ya uwepo wa Mungu na mioyo yetu yaweza kupumzika kwa amani kwa shukrani ya imani iliyo katika Injili ya maji na Roho. Tusingeliweza kamwe kupumzika pasipo injili ya maji na Roho.
Zaidi ya yote imeandikwa “nipate kuwapa karama ya rohoni ili mfanywe imara”. Karama hii ya rohoni ndiyo Injili ya maji na Roho. Mtu aweza kuwa mtoto wa Mungu na kupokea baraka ikiwa tu ataamini Injili ya maji na Roho.
Hata hivyo kuna faida gani watu kuishi kiuadilifu au kwa uaminifu kwa kuacha mambo kama uvutaji wa tumbaku, kunywa pombe na kuepuka kutenda mabaya ikiwa hawaifahamu Injili ya maji na Roho ingawa wanamwamini Yesu kwa namna yoyote? Matendo yao hayana maana mbele ya haki ya Mungu. Haki ya Mungu ni kuu zaidi ya hii ya mwanadamu Ni rahisi kuwavuta watu kanisani lakini ni muhimu kuihubiri injili ya maji na Roho kwa waumini wapya ili waweze kusamehewa dhambi zao zote na kuwa watoto wa Mungu kwa kuvikwa karama ya rohoni ambayo ndiyo baraka toka Mbinguni.
Paulo Mtume alipenda watakatifu wa Roma waweze kutiwa moyo kwa njia ya imani yake. Hivyo alisema “yaani tufarijiane mimi na nyinyi kila mtu kwa imani ya mwenzake yenu na yangu” kwa hiyo, Paulo Mtume ilimlazimu aihubiri Injili kwa jumuia nzima ya kanisa ili waweze kuwa na imani hatimaye wafanywe imara kwa imani yake katika maji na Roho, ilimlazimu awape waumini wa kanisa la Roma Injili ya maji na Roho Mtakatifu na kuwafundisha jinsi ile ilivyo kwa undani.
Hii ndiyo iliyomfanya Paulo Mtume kuwa tofauti na wainjilisti wengine wa nyakati hizi hapa ulimwenguni. Katika Waraka wa kanisa la Roma Paulo Mtume alisema kwamba alipenda watu waweze kufarijika kwa imani ya pamoja, kati yao na yeye. Hivi ndivyo wahubiri wa nyakati hizi waliomo makanisani wanapaswa kujifunza toka kwa Paulo Mtume. Paulo Mtume alizoea kuihubiri Injili ya maji na Roho ambayo mtu angeliweza kutambua kati ya ndugu wa kweli na wa uongo kiimani.
Nyakati hizi, makanisa huwafanya makundi ya waumini wapya kupokea kwanza kanuni za mafundisho kwa miezi 6, na kwa mwaka mzima hatimaye kuwabatiza. Hivyo hubatizwa pasipo kujali ikiwa wameelewa Injili ya maji na Roho au la ambayo Yesu ameikamilisha, kwa maneno mengine, ingawa watu watakuwa washirika wa kanisa bado hawajaweza kuwa watoto wa Mungu waliopokea haki yake. Kile watumishi wa nyakati hizi wanachoweza kuwafanyia waumini wapya ni kuwafundisha namna ya kuhifadhi akilini Amri kumi na kanuni ya Imani za Mitume. Waumini hao wanapo hitimu kwa kufaulu kuweka kichwani ndipo huulizwa “Sasa je, utaacha kuvuta sigara, kunywa pombe? Je, utakuwa mwaminifu kwa kulipa asilimia kumi ya mapato yako? Utaishi maisha ya uadilifu?”
Sababu ya makanisa katika Ulaya, Asia na ulimwenguni pote kuwa mbali na haki ya Mungu ni kwamba wao hafukuzia haki ya mwanadamu. Siku hizi hata hapa Korea au kwa jinsi inavyo fahamika kwa jina “Jerusalemu ya Asia” idadi ya Wakristo inashuka. Kwasasa imefikia hali ambapo hakuna yeyote apendaye kuja kanisani ikiwa hakuna tukio la maana litakalo fanyika kama vile matamasha ya nyimbo za kusifu au onyesho la nyimbo. Hata ikiwa watu watakuja bado kunakuwemo na semina na makongamano juu ya uadilifu na ustaarabu wapewayo vijana yenye vichwa vya habari kama vile “usivute sigara uwe mwangalifu, ikumbuke na kuitunza siku takatifu ya Jumapili na kujitolea kwa kazi za Mungu” ambayo yote haya hayana lolote mbele ya haki ya Mungu.
Kwa kuwa mwanadamu ni rahisi kwake kuiendea dhambi na si rahisi kuiacha, imempasa basi kumtegemea Bwana. Hivyo watu wanapo kuja katika kanisa la Mungu imetupasa kuwapa Injili ya maji na Roho ili kwamba waweze kupokea haki ya Mungu. Kwanza imetupasa kuwapa haki ya Mungu isemayo kwamba mimi na wewe tumetakaswa dhambi zote ingawa bado tu dhaifu mwilini.
Uwe na uhakika wa kuweka katika kumbukumbu za akili yako. Mtu aweza kuishi kulingania na mapenzi ya Mungu ikiwa ametakaswa kwa njia ya kuamini haki ya Mungu. Mtu aweza kuihubiri Injili ikiwa tu tatizo la dhambi zake limetatuliwa.
Ilisemekana kwamba Paulo Mtume kwa hakika aliwapa karama ya rohoni watu. Karama hii ambayo Paulo anaizungumzia si zile zisemekanazo kama vile kunena kwa lugha au uponyaji ambao huzungumziwa na vuguvugu la Wapentekoste katika ukristo wa siku hizi. Wakristo wengi huchukulia matukio ya siyo ya kawaida kama vile maono, unabii, kunena kwa lugha au kuponywa magonjwa vyote na vingine kama hivi kuwa ndiyo karama.
Hata hivyo mambo haya si karama ya rohoni toka mbinguni. Kuona maono wakati wa maombi bila shaka si karama ya rohoni. Kwa mtu kupiga mayowe au kupata kupagawa kila anaposikika sauti za ajabu huku akishindwa kupata usingizi usiku kwa siku kama tatu, yote haya si karama ya Mungu. Anaye dai kuwa anaweza kunena kwa lugha na kuanguka kwa kukosa fahamu baada ya kupiga mayowe nakunena lugha za ajabu “la-la-la” akichezesha ulimi hii si namna ya mtu kumpokea Roho Mtakatifu. Badala yake ni sawa na kurukwa akili kwa hali ya kupagawa. Hata hivyo wapo wanao jiita “Wanauamsho wa Karismatiki” ambao husisitiza kwamba kwa lugha au namna ya kumpokea Roho Mtakatifu. Hufanya jambo la makosa sana, na imani waliyonayo hakika si sawa.
Maji ya uzima ya Roho Mtakatifu hububujika toka mioyoni pale tunapo kuwa waaminifu kwa kazi za kiroho wa Mungu na kumfuata Bwana. Maji ya Roho Mtakatifu yatafurika ndani ya mioyo yetu pale tutakapo achana na matendo ya mwili na kufuta matendo ya kiroho badala yeke.
Wakristo inawapasa kutafuta na kupata karama ya rohoni ya ondoleo la dhambi kwa kuamini Injili ya maji na Roho. Baadhi husema kwamba idadi kubwa ya Wakristo kwa sasa wanaelekea karibu na motoni kutokana na nafasi za makanisa ya wakati huu. Hii inaonyesha ya kwamba makanisa ya nyakati hizi huchochea zaidi haki ya kibinadamu baada ya waumini wao kuhudhuria kanisani kwa muda mrefu. 
Hii haimaanishi kwamba mtu huyo aweza kupokea karama ya Rohoni kwa matendo ya aina hii. Yatupasa kuichukulia haki ya Mungu moyoni mwetu kwa imani katika Injili ya maji na Roho ili tuweze kupokea karama ya rohoni.
Hebu turudie ile mistari ya 13 hadi 17 “Lakini ndugu zangu sipendi msiwe na habari ya kuwa mara nyingi nalikusudia kuja kwenu nikazuiliwa hata sasa ili nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine, Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani, nawiwa na wenye hekima na wasio na hekima, Kwa hiyo kwa upendo wangu, mimi ni tayari kuihubiri Injili hata na kwenu ninyi mnao kaa Rumi,Uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza na Myunani pia. Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani ilivyo andikwa Mwenye haki ataishi kwa imani.”
Paulo Mtume alipendelea kwenda Roma. Hata hivyo hakuweza kutimiza hilo kwa sababu aliwekewa kikwazo. Hivyo ilimbidi asali kuomba mlango wa huduma yake ufunguliwe. Hata nasi pia yatupasa kufanya maombi ya aina hii tukiwa tunaihubiri Injili ulimwenguni kwa njia ya huduma za vitabu. Tutakapo sali tu ndipo moyo wa Mungu utakubaliwa na pale Mungu atakapo fungua mlango na njia yetu itakuwa rahisi kupeleka Injili ya maji na Roho duniani
 

Paulo anaye wiwa na watu wote
 
Ni watu gani Paulo Mtume anasema wanamdai, na ni deni gani analo maanisha katika mstari wa 14 na 15? Ana sema ya kwamba amekuwa ni mdaiwa kwa Wayunani na wasio Wayunani na kwamba anadaiwa kuihubiri Injili ya maji na Roho. Kwa nyongeza anasema amekuwa mdaiwa kwa wenye hekima na wasio na hekima. Hivyo anatamani kuihubiri Injili kwa wale walio Roma vile awezavyo kwa kiwango cha juu.
Kwahiyo, dhumuni la Paulo Mtume kuwaandikia kanisa ilikuwa ni kutuma Injili ya kweli. Amekuta pia hata katika mioyo ya watu ndani ya kanisa la Roma Injili ya maji na Roho haikua imara, na hivyo kuiweka kuwa ni karama ya rohoni. Kwa hiyo aliihubiri Injili ya maji na Roho hata kwa wale walio ndani ya kanisa pia na hata wale wote wa ulimwengu. Alisema kwamba amekuwa mdaiwa kwa walio na hekima na wasio na hekima Wayunani na wasio Wayunani.
Aina gani ya deni Paulo analodaiwa? Anadaiwa deni la kuihubiri Injili ya maji na Roho Mtakatifu kwa watu wa ulimwengu. Alitilia mkazao wa kulipa deni lake lote kwa watu wote ulimwenguni. Kwa mfano huu pia, watu wote hata sasa tulio ipokea Injili ya maji na Roho tunadaiwa katika kuifanya ijulikane pia. Deni tunalo paswa kulilipa ni injili ya maji na Roho kwa ulimwengu wote katika muda huu.
Kimakosa watu hudhani damu ya msalabani ndiyo wokovu wote. Hata hivyo Injili ya mbinguni biblia inayoishuhudia ni Injili ya maji na Roho ambayo Paulo Mtume aliishuhudia pia, hivyo katika Warumi sura ya 6 Paulo alisema kwamba yeye alibatizwa katika Kristo Yesu kwa mauti yake. Kwa kuwa wamo pia Wakristo wa majina ndani ya kanisa la Roma wenye kuamini damu ya msalabani tu, Paulo alipenda kuwapelekea siri iliyofichika ya ubatizo wa Yesu alio upokea. Kwa jinsi hii pia nasi imetupas kuihubiri Injili ya maji na Roho kwa wale wote ambao bado hawaja isika, ingawa kwa muda mrefu wamo ndani ya kanisa.
Wakati Wakristo wanapo ulizwa ikiwa wanadhambi au la, hudhani swali hili pekee kuwa lisilo na maana na la kupuuzia utu wao. Hata hivyo, swali hili hakika ni lenye umuhimu mkuu na lenye thamani ya juu. Ikiwa wanadamu hatima yao ni motoni kutokana na dhambi ni nani basi aliyepo wa kuuliza aina hii ya swali na kuleta mwafaka juu yake? Ni mtu yule tu asiye na dhambi moyoni baada ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa Injili ya maji na Roho ndiye awezaye kuthubutu kuuliza swali la aina hii na pia kutoa jibu sahihi kwa watu. Ni yule tu aliye zaliwa upya mara ya pili, ndiye awezaje kuwaongoza wenye dhambi kuzaliwa upya mara ya pili kwa kuwapa Injili ya maana ambayo ni Injili ya maji na Roho Mtakatifu ambayo wenye dhambi wote hawajaisikia.
Ndugu zangu hata ikiwa mtu anamwamini Yesu lakini bado hajazaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho Mtakatifu, basi hakuna awezaye kuingia Ufalme wa Mungu. Hivyo basi inakupasa uwe na shukrani kila ukutanapo na watu wenye kuwezesha wenye dhambi kupokea ondoleo la dhambi kwa njia ya kuihubiri Injili ya maji na Roho. Utapokea baraka kuu.
 

Injili ambayo Paulo hakuionea haya.
 
Katika mstari wa 16, ni Injili gani Paulo Mtume hakuionea haya? Ilikuwa ni Injili ya maji na Roho kwa sababu Injili ni nguvu ya Mungu kwa wokovu wa kila aiaminiye, ambayo yeye aliipa jina “Injili yangu” (Warumi 2:16, 16:25) nakuichukilia kuwa ni ya kujivunia na kuu kwake badala ya kuionea haya. Sababu ya kutoionea haya Injili ya maji na Roho ni kwa kuwa Injili hii huwafanya watu wasiwe tena na dhambi moja kwa moja na kwa wakati wote, hivyo kuondoa kizuizi cha dhambi kinacho watenga wanadamu na Mungu.
Je, utakaso wa dhambi ungeliwezekana kwa watu kuiamini Injili ya damu ya msalabani pekee? Inaonekana kwamba yawezekana kuwasafisha dhambi zilizo tendeka hadi sasa kwa aina hii ya imani, lakini haitowezekana kutakasa zile zijazo mbeleni. Hivyo watu walio na aina hii ya iamani hujaribu kutakasa dhambi zao kwa kusali sala za toba kila siku. Hukiri kwamba mioyo yao imefurika kwa dhambi hivyo bila kujizuia wao ni wenye dhambi. Wakristo hawa wenye dhamba hawawezi kuzungumzia juu ya Injili kwa uaminifu juu ya wengine kwa sababu “Injili” kwao si “habari njema” tena.
Injili kwa Kiyunani ni “evaggelion” kwa maneno mengine Injili yenye uwezo wa kufutilia mbali dhambi zote ulimwenguni. Injili pekee ya kweli inafananishwa na baruti. Injili ya kweli ndiyo iwezayo kuondolea mbali dhambi ya ulimwengu. Hivyo basi mtu kama Pulo aliye amini Injili ya maji na Roho, aliyo na uwezo wa kuondolea mbali dhambi hakuionea haya. Nyakati hizi hata Wakristo wanaonekana kuione haya kuiihubiri. Hata hivyo wale wenye haki ya Mungu ni watu wenye kusimama na hadhi na utukufu wanapo ihubiri Injili.
Paulo Mtume hakuwa hata na chembe ya haya kwa Injili ya maji na Roho. Ingawa Injili pekee ya msalaba lazima iwe na haya, Injili ya maji na Roho kamwe haito onewa haya kamwe, bali ni ya maana na yenye nguvu imiminikayo pamoja na sifa ikiwa na hadhi. Yeyote anaye amini Injili hii hupokea ujazo wa Roho Mtakatifu kwa imani kiasi kwamba kumfanya awe mtoto wa Mungu. Nasema tena kwako kwamba Injili njema ya maji na Roho Mtakatifu kamwe haiwezi kuonewa haya. Hata hivyo Injili yenye kuamini damu ya msalabani ndiyo iletayo haya.
Je ninyi ni wakristo mlio na haya kila mnapo ihubiri Injili ya damu ya msalaba pekee? Mnaona aibu mnapo isambaza na kuiamini Injili ya damu ya msalaba pekee ambayo ndani yake haumo ubatizo wa Yesu. Kwa kuwa mliona haya kuihubiri Injili hiyo isiyo ya thamani, iliwapasa kila wakati kumlilia Bwana au kufanya maombi ya hisia za mashamshamu kwa kunena kwa lugha ili kupandisha mori kabla ya kutoka na kuelekea barabarani kwa ajili ya kupaza sauti na kuhubiri “Mwamini Yesu.Mwamini Yesu!”
Hili ni jambo ambalo mtu aweza kulitenda akiwa amejawa na hisia kali na si awezalo kulifanya akiwa na ufahamu wa kweli. Na ndiyo maana wale wote wenye kuamini damu ya msalaba pekee hupiga kelele na kusababisha usumbufu kila wanapofanya uinjilisti mitaani wakiwa na vipaza sauti karibu na midomo yao, huku wakipiga kelele kwa maneno “Wa Yesu mbinguni, wasio amini motoni” Ingawa wanao amini injili ya maji na Roho hupeleka injili yao kwa ustaarabu wakiwa wanazifungua biblia zao huku wakiburudika kwa chai na kujadiliana na wengine.
Kwa hivyo, injili ina nguvu sawa kwa kila mtu ikiwa ni pamoja na Wayahudi na Wagiriki. Injili ya maji na Roho inaruhusu wokovu sawa kutoka kwa dhambi kwa kila mtu anayemwamini Yesu wakati injili inapohubiriwa kwao. kwa upande mwingine, wakati mtu atatoa kitu kingine isipokuwa injili ya maji na Roho, atapokea hasira ya Mungu. Kwa hivyo Paulo alisema, “Lakini hata kama sisi, au malaika kutoka mbinguni, akihubiri injili nyingine yoyote kuliko ile ambayo tumekuhubirieni, na alaaniwe” (Wagalatia 1:8). Paul Mtume alisema wazi kuwa kuna injili tu ya maji na Roho ambayo ni kweli kutoka kwa injili zingine zote.
Bila kujali kama mtu ni Myunani au Myahudi, au ikiwa mtu anaamini katika Uisilamu, Ukomunisti, Ubuddha, Taoism, mungu wa jua au kitu kingine chochote, kila mtu anapata nafasi ya kusikia injili. zaidi ya hayo, injili hii ya maji na Roho Mtakatifu inawapa nafasi ya kuokolewa kutoka kwa dhambi zao zote. kwa hivyo, tunapaswa kusema kwamba Yesu Kristo ni Mungu, kwamba ndiye aliyeumba ulimwengu, kwamba alikuja ulimwengu huu kwa mfano wa mwili wa mwanadamu kutuokoa, kwamba alichukua dhambi zetu zote kwa kubatizwa na Yohana, na kwamba alipokea. hukumu ya dhambi zetu kwa kufa Msalabani.
Kwa hivyo, mtume Paulo hakuwa na aibu na injili ya maji na Roho. Hata ingawa injili tu ya Msalaba lazima iwe injili ya aibu, injili ya maji na Roho haiwezi kuwa ya aibu hata kidogo; lakini injili nzuri na yenye nguvu inayojaa kiburi na hadhi. Yeyote anayeamini injili hii anapokea utimilifu wa Roho Mtakatifu kwa imani kwa ukweli kwamba yeye ni mtoto wa Mungu. Tena ninawaambia kwamba injili nzuri ya maji na Roho Mtakatifu haiwezi kamwe kuwa injili ya aibu. Walakini, injili inayoamini katika damu ya Msalaba ni aibu tu.
Wakristo, je! Ulikuwa na aibu wakati wowote ulipaswa kuhubiri injili ya damu ya Msalaba tu? Ulijisikia aibu wakati unaokoa na kuamini injili ya damu tu ambayo haina ubatizo wa Yesu. Kwa sababu ulikuwa na aibu kuhubiri injili isiyo na maana, ilibidi kila mara ulilie kwa ajili ya Bwana au kutoa sala zenye nguvu kwa lugha zingine ili kujaza hisia zako kabla ya kwenda barabarani kupiga kelele “Mwamini Yesu. Mwamini Yesu!”
Hili ni jambo ambalo mtu anaweza kufanya tu na hisia zinazozidi lakini kitu ambacho mtu hataweza kufanya na akili timamu. Ndio sababu wale wanaoamini katika damu ya Msalaba wanapiga kelele na kusababisha usumbufu wakati wowote wanapokuwa barabarani kwa uinjilishaji. wakiwa na megaphone karibu na vinywa vyao, wanapiga kelele tu maneno, “Yesu, Mbingu, ukafiri, kuzimu.” Walakini, mwamini katika injili ya maji na Roho hutoa injili kwa mtindo wa kiungwana sana; wakati anafungua bibilia yake, anakunywa chai na kuzungumza na mwingine
 

Nini kisemwacho juu ya Injili ya haki ya Mungu?
 
Katika mstari wa 17 nini kisemwacho kuwa kimefunuliwa katika Injili ya Kristo? Inasema kwamba “Haki ya Mungu” imefunuliwa katika Injili ya kweli. Hivyo ilisemekana kwamba haki ya Mungu ilifunuliwa ndani yeke toka imani hata imani kwa hiyo wenye haki wataishi kwa imani tu. Injili itokanayo na damu ya msalabani haina haki ya Mungu.
Ndugu kama ilisemekana kwamba mtu imempasa kufanya sala za toba kila siku kwa ajili ya dhambi zake za kila siku ingawa zile za asili zimekwisha samehewa na hivyo ataweza kutakaswa kwa awamu katika viwango hadi kufikia mwenye haki kamili, basi je, aina hii ya imani itaweza kuwa na haki ya Mungu ndani yake? Hapa hakuna haki ya Mungu ifunuliwayo. Kile kinachofunua haki ya haki ya Mungu huzungumzia mambo yaliyo kamili. Injili ya maji na Roho Mtakatifu huzungumzia juu ya Injili iliyo kamili toka mwanzo hadi mwisho.
Ninyi watu hufanya sala za toba kwa sababu mnaendelea kutenda dhambi kila siku, na hivyo inakuwa kama kujifunika upya na majani ya mti wa aradali ili kutunza upande wa aibu kila siku, au labda kila juma na mwezi. Mtu anaye rudia kuwa mwenye dhambi kwa kusali sala za toba ni kama kujifunika aibu yake kwa majani ya mti wa aradali. Na hii ndiyo hali halisi ya maisha ya kidini kwa wale wote waaminio Injili ya damu ya msalabani tu. Ni wapumbavu wasio tamani kujivika ngozi aliyo toa Mungu bure na badala yake hufanyiza vazi la majani ya mti wa aradali.
Damu ya Yesu msalabani ni matokeo ya ubatizo na si kumwaga damu msalabani ndiko kuliko mwezesha Yesu kubeba dhamba zetu. Alibeba dhamba zetu pale alipo batizwa na ndipo alipo kwenda msalabani akiwa tayari amekwisha beba dhambi hizo zote za ulimwengu hatimaye kufa ili kuleta upatanisho wa dhambi za ulimwengu. Hivyo msalaba ni matokeo ya ubatizo alio upokea Yesu kwa kuwa Yesu alikwisha beba dhambi zetu kwa njia ya ubatizo wake, kumwaga damu msalabani ndiko hitimisho la kuelekea upatanisho wa dhambi zetu zote. Yesu alibeba laana zetu zote za dhambi kuelekea msalabani kwa sababu alikwisha upokea ubatizo.
Sasa basi, ni kwa maana gani tutaweza kupata haki ya Mungu? Tutaweza kuipata kwa kujua na kuamini Injili ya maji na Roho. Utaweza kuniuliza “Je wewe nawe ni mwenye kuamini Injili ya maji na Roho?” Ndipo nitakapo jibu haraka na kwa uwazi “Ndiyo” kwa swali hili. Siri ya kupokea haki ya Mungu ni kuiamini Injili ya maji na Roho.
Sababu ya hili ni kwamba Injili ya maji na Roho ni ukweli na hivyo basi kwa kuwa Injili hii ina jumuisha ondoleo la dhambi Mungu alilowapa wanadamu bure, ni njia ya kuwapa watoto wake, baraka ya uzima wa milele ambapo mtu hupokea Roho Mtakatifu na pia baraka za kimwili na kiroho hapa duniani.
Paulo Mtume alisema haki ya Mungu ilidhihirisha wazi katika Injili ya maji na Roho aliyo hubiriwa. Hivyo kujivika haki ya kibinadamu pasipo kuijua haki ya Mungu ni kama kutenda dhambi mbele ya Mungu. Zaidi ya yote, Injili ya kuamini damu ya msalabani pekee ambamo hakuna haki ya Mungu ni batili.
Haki ya Mungu humaanisha Injili ya kweli ya maji na Roho ambayo Mungu alitupatia. Agano Jipya na la Kale yote mawili yametuokoa dhambini. Agano Jipya pia limetimiza maneno ya ahadi yaliyo kuwepo katika Agano la Kale. Mungu alituokoa toka dhambini kwa kutupatia Injili ya kweli ambamo haki yake ilidhihirishwa bayana. Kwa njia hii alituokoa kwa dhambi zetu zote.
Sasa hivi ulimwengu unapaswa kuirudia Injili ya maji na Roho. Injili pekee inayoweza kuokoa watu kwa dhambi zao ni Injili halisi ya maji na Roho. Ndugu zangu ulimwengu wote inabidi mrudie Injili ya maji na damu. Inabidi mrudie Injili hii iliyo na haki ya Mungu.
Sababu ya hili ni kwamba, injili ya maji na Roho ndiyo ukweli pekee uwezao kuokoa watu na dhambi zao. Injili pekee iliyo na haki ya Mungu ndiyo iwezayo kutuokoa kutufanya tusio na dhambi na kutuweka kuwa watoto wa Mungu. Zaidi ya yote, Roho Mtakatifu ndani ya mioyo yetu huwakinga watu wa Mungu na pia kutuombea kutubariki, kukaa ndani yetu wakati wote na hatimaye kutupatia uzima wa milele kama zawadi.
Ina staajabisha sana kuona kwamba wapo watu wengi ambao hawatilii maanani Injili hii. Natumaini kila mmoja aweze kuiamini Injili ya maji na Roho Mtakatifu kwa kuwa na ufahamu bayana juu ya ubatizo wa Yesu. Ubatizo Yesu alio upokea toka kwa Yohana si jambo ambalo Yesu aliliafiki kwa sababu tu ya kuwa mfano. Sababu ya yeye kubatizwa ni ili aweze kubeba dhambi zote za ulimwengu. Yohana ambaye alikuwa ni mkuu kati ya wanadamu walio zaliwa na wanawake alimwekea Yesu mikono juu ya kichwa chake wakati akimbatiza. Aina hii ya tendo linafanana na lile ambalo Kuhani Mkuu alipo kuwa akiweka mikono yake juu ya kichwa cha mnyama wa sadaka asiye na doa wakati wa Agano la kale (Walawi 16:21) kifo cha Yesu msalabani kilikuwa ni matokeo ya kubeba dhambi juu ya mwili wake na inakwenda sambamba kwa mfano wa sadaka ya dhambi kwa kumwaga damu na kufa baada ya kuwekewa mikono.
Kwa sababu Injili hii ya maji na Roho Mtakatifu ilikuwa ikitajwa katika Agano la Kale na Jipya yeyote anaye amini Injili nyingine huku akiondoa sehemu yoyote ya asili yake, basi mtu huyu alikuwa na imani potofu isiyo ya kweli. Sehemu muhimu na jambo la kwanza ambalo Yesu alilifanya alipo kuja ulimwenguni lilikuwa ni kubatizwa na Yohana. Ni makosa makubwa kuamini kwamba ubatizo wa Yesu ni alama tu na kudhani kwamba Yesu alibatizwa ili awe mfano.
Mtu mzushi ni wa aina gani? Katika Tito 3:10-11 imeandikwa “Mtu aliye mzushi baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili mkatae ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka tena atenda dhambi maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.” Mwenye kujihukumu maana yake ni yule anaye kiri na kutubu kwamba yeye ni mwenye dhambi. Hivyo, Mkristo asemaye “mimi ni mwenye” ni mtu mzushi. Imeandikwa, “Kataa mtu mgawanyiko baada ya shauri la kwanza na la pili.”
Kwa kuwa aina hii ya Wakristo ni watu wasio wakawaida na walio hovyo, basi mtu mtakatifu haimpasi kuwa karibu na mzushi huyu. Ni mtu anayejihukumu kwa sababu imani yake na maisha yake ya kidini yameoza. Mtu atendaye dhambi isiyo samehewa mbele ya Mungu ni yule asiyependa kuwa mwenye dhambi kwa kuamini Injili ya maji na Roho na badala yake huendelea na dhambi ya kuukataa wokovu halisi mbele ya Mungu huku akisema kwamba yeye bado ni mwenye dhambi lakini anamwamini Yesu. Basi ni mwenye dhambi na hivyo kujiita ni mwanye dhambi, atakuwa ni mzushi anaye elekea motoni.
Baadhi ya Wakristo hubandika vipeperushi katika magari yao vilivyo andikwa. “Ni makosa yangu” Hii inaonekana na kwamba labda mtu huyo ni mkarimu au muungwana na mnyenyekevu inapoonekana na baadhi ya watu, lakini ukweli ni kwamba maana yake ni kwamba, kwa kuwa ni kosa la mtu mambo kama vile kwenda motoni kwa mzushi, kutukana namengine ya aina hii ni kosa lake. “Ni kosa langu” ni neno linalo onekana ni la kweli lakini sivyo vile mtu awezavyo kuishi pasipo kukosa. Hata hivyo, kwa kusema kwamba wanao unga mkono kauli hii huku wakidhani kwamba wataweza kuishi wakiwa wema ni moja kwa moja kuyakana maneno ya Mungu yanayo sema wanadamu ni mbegu ya uovu. Wenye kuendekeza aina hii ya mawazo ya kibinadamu hatimaye watapokea aina zote za laana.
Je yupo yeyote kwa nafasi yoyote kati ya watu wenye kujihukumu? Ndipo tena imekupasa usikilize kwa uanglifu Mahubiri yangu katika Warumi sura ya 3 yanayosema kwamba ondoleo la dhambi halimaanishi kuwa ni Fundisho la Kanuni ya kufanywa haki. Warumi inazungumiza juu ya hili kwa undani zaidi. Paulo Mtume alikwisha jua kabla kile watakacho sema mbeleni na hivyo kuanza kutaadharisha kwamba kutokuwa na dhambi ni kuwa hakika kutokuwa na dhambi na si kumuita mwenye dhambi ni mwenye haki. Pia kwa uwazi alishuhudia kwamba ni Injili ya maji na Roho ndiyo iliyo ya kweli. Hivyo ni asili kwamba wale wenye kuamini damu ya Yesu pekee msalabani watakuwa wapumbavu na bubu wanapo soma Warumi.
Waraka wa Paulo Mtume kwa Warumi ni andiko kuu kwa sababu linashuhudia Injili ya maji na Roho. Mtu imepasa awe mwenye haki baada ya kumwamini Yesu ingawa kwa asilia alikuwa ni mwenye dhambi aliye beba dhambi moyoni mwake. Hivi ndivyo mtu awezavyo kuwa na imani ya kweli.
Natumaini kwamba ingawa hata sasa imani za watu hazija kamilika, imani zao hatimaye zitafikia ukamilifu huku wanapo yasikia maneno ya maji na Roho kwa kupitia kanisa la walio zaliwa upya mara ya pili. Tafadhali naomba ujifunze zaidi juu ya Injili ya maji na Roho kupitia mahubiri na kuthibitisha, maneno ya kweli.
Naamini kwamba Mungu atatukirimia utajiri wa baraka za mbinguni.