Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 1-2] Haki ya Mungu iliyo dhihirishwa katika Injili (Warumi 1:16-17)

(Warumi 1:16-17)
“Kwa maana siionei haya Injili kwa sababu ni uwezo wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza na kwa Myunani pia. Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, mwenye haki ataishi kwa imani.”
 

Yatupasa kuipokea haki ya Mungu.
 
Paulo Mtume hakuionea haya Injili ya Kristo. Alitamka juu ya Injili. Hata hivyo, moja ya sababu ambayo watu wengi hulia ingawa wanamwamini Yesu ni kwa sababu ya dhambi. Pia ni kutokana na upumbavu wao katika kushindwa kuikubali haki ya Mungu. Tutaweza kuokolewa kwa kuamini haki ya Mungu na kuachana na haki zetu binafsi.
Kwa nini Paulo Mtume hakuionea haya Injili? Kwanza kabisa, ni kwa kuwa haki ya Mungu ilikuwa imedhihirishwa ndani yake.
Injili, “euaggelion” kwa Kiyunani maana yake “habari njema” Yesu alipozaliwa Bethelehemu, Malaika wa Mungu aliwatokea wachungaji walio kuwa wakilinda wanyama wao usiki na kuwa ambia “Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia” (Luka 2:14). Ilikuwa ni habari njema ya “amani kwa watu aliowaridhia” Injili ya Bwana ilituokoa toka dhambini kote na kutusafisha na dhambi ya ulimwengu. Yesu alisafisha dhambi zetu zote. Yeye mwenyewe alizisafisha dhambi za wale wato walio kuwa wakisota kama funza katikati ya rundo la kinyesi na walio katika tope la dhambi.
Kwanza Paulo Mtume alisema kwamba haki ya Mungu ilidhihirishwa katika Injili. Haki ya Mungu ilidhihirishwa katika Injili iliyo futa dhambi zetu zote. Haki ya Mungu imeruhusu tuwe watakatifu na kuhesabiwa haki. Pia imeruhusu kutuletea uzima wa milele na kutufanya tusiwe na dhambi.
Haki ya wanadamu ni ipi? Sisi wanadamu tunapenda kujionyesha mbele za Mungu pale tunapo kuwa na cha kujidai, tukiondoa gamba la majivuno kwa kutenda mambo mema ambako ndiko kutengeneza haki ya kibinadamu. Hata hivyo tendo la haki ya Yesu lililotuokoa kwa dhambi zetu zote ndilo linalo ruhusu haki ya Mungu kudhihirishwa katika Injili. Hii ni haki ya Mungu.
Siku hizi, wakristo wengi huihubiri Injili pasipo kuelewa juu ya Injili ya haki ya Mungu wakisema “mwamini Yesu na utaokoka na hivyo utabarikiwa kwa utajiri!” hata hivyo, haya si mafundisho ya Injili ya haki ya Mungu. Injili hii inaonekana kuwa maarufu kuliko chochote, lakini watu karibia wote hawana ufahamu na hawaielewi Injili ya kweli. Ni sawa na ukweli kwamba, Biblia ni kitabu kilicho uzwa zaidi lakini bado watu hawafahamu kile kilichomo ndani yake. Jambo lililo na thamani na lenye manufaa katika dunia hii ni Injili ambayo Mungu ametupatia.
“Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani.” Injili ya Mungu ni mfano wa chemchemi katika jangwa (oasis). Yesu alikuja kwa wale wote wenye dhambi walio kosa kwa uovu mwingi na hivyo kuwasafisha kabisa. Hata hivyo, baadhi yao wanaikataa zawadi ya haki yake ambayo imesafisha dhambi ya ulimwengu huku wakijaribu kuanzisha haki zao binafsi. Watu wanao jibidisha kwa juhudi zao binafsi, (mfano huduma, kujitolea, ukereketwa, matoleo ya sadaka, sala za toba, sala za kufunga kula, kuitunza siku ya Bwana, kutafsiri maneno ya Mungu kwa vitendo na kadhalika) na kuikataa zawadi ya Mungu, ni wale wanao ikataa haki ya Mungu. Mtu hatoweza kuipokea haki ya Mungu mpaka pale tu atakapo iacha haki yake binafsi.
 

Wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
 
Katika Mwanzo 3:21 imeandikwa “Bwana Mungu akawafanyia Adamu na Mkewe mavazi ya ngozi akawavika”.
Mtu wa kwanza Adamu alitenda dhambi dhidi ya Mungu kwa kuanguka katika mtego wa Shetani. Kile walichofanya Adamu na Hawa baada ya kutenda dhambi ilikua ni kushona majani ya mti wa aradali na kujifanyia nguo. Nguo hiyo iliyo fumwa kwa majani ilikuwa mfano wa kitamba kilicho tokana na ngozi. Ilikuwa ni tofauti kati ya “haki ya mwanadamu” na “haki ya Mungu.” Mwanzo 3:7 inasema “Wakashona majani ya mtini wakajifanyia nguo.” Je ulikwisha wahi kusuka mkeka kwa majani ya mgomba? Sisi Wakorea hukwanyua majani fulani ya mboga na kuyasukia masuke ya majani ya mchele ili yakauke. Wakati wa kipindi cha baridi tunapika mchuzi wa maharage na kuyachanganya na mboga hizo. Nitamu mno!
Adamu na Hawa walishona majani ya mtini, wakajifanyia nguo baada ya kutenda dhambi. Aina hii ya matendo mema, kujitolea, yote haya hujenga haki ya kibinadamu. Ni haki ya kibinadamu na si ile haki Mungu. Sababu ya kushona majani ya mti inaonyesha dhambi ya majivuno kwa kujaribu kuficha dhambi zao kwa matendo mema mbele ya Mungu—kujitengenezea haki binafsi—kujitolea kwa mtu, sadaka kujihukumu, kuhudumu, sala za toba kuvaa vazi na kujifunika dhambi kwa fikra ni kujitukuza ambako huleta majivuno mbele ya Mungu.
Je tunaweza kweli kuficha dhambi zetu ndani ya mioyo yetu mbele ya Mungu kwa kushona vazi la majani? Je tunaweza kuficha dhambi zetu kwa matendo mema? Kamwe hapana, kwani majani yataanza kunyauka na kuanguka wakati wa mchana na baada ya siku 3 yote yataanguka na mwishowe vazi lililofanyizwa kwa majani ya mboga haliwezi kukaa muda mrefu. Watu wenye kushona majani ya mti kuwa vazi, yaani wale wote wanaojaribu kuwa wenye haki kwa kumtumikia Mungu vyema kwa matendo yao hawatoingia Ufalme wa Mbinguni. Hatuwezi kupata msamaha wa dhambi kwa haki za matendo yetu mema.
Wakati Adamu na Hawa walipojaribu kuzificha dhambi zao kwa kushona vazi la majani ya mti, ndipo Mungu alimwita Adamu, “Uko wapi Adamu” Huku akijificha katikati ya miti ya bustanini aliitika akisema “Nalisikia sauti yako bustanini nikaogoopa kwa kuwa mimi ni uchi nikajificha” Mtu mwenye dhambi huogopa na kujificha katikati ya miti ya bustani. Miti kibiblia ina maanisha watu. Aliye na dhambi moyoni hujaribu kijificha katikati ya watu. Hujaribu kukaa nafasi za katikati. Si kukaa mbali sana au karibu mbeleni mwa viti vya kanisa ambamo watu hukusanyika kwa pamoja. Je, kwa nini? Kwa sababu hutaka kujificha miongoni mwa watu.
Hata hivyo hawezi kujificha mbele ya Mungu. Imempasa mtu huyu apokee msamaha mbeli za Mungu kwa kuziacha dhambi na haki zake binafsi na kwa kuamini haki ya Bwana. Wale walio na imani haba na hawataki kuukubali ukweli nao pia hupenda kuingia Ufalme wa Mbinguni wakijificha katikakati ya watu wanao fanana na hilo, lakini mwishowe watakwenda motoni. Na wale wapendao kuficha dhambi zao kwa matendo mema, ni wenye dhambi mbele za Mungu na inawapasa wawekwe bayana kuwa ni waovu na nilazima wajitoe mbele ya Mungu.
Mungu alimwambia Adamu aliyeshona vazi la majani ya mti, “Kwa nini ulikula tunda? Nani aliyekudanganya?” “Oh, Mungu ni mwanamke huyu uliyenipatia ndiye aliyenipa tunda ni kala” “Hawa kwa nini umetenda hivyo?” “Ni nyoka ndiye aliyenilaghai na kula” Ndipo Bwana Mungu akwamwambia nyoka “Kwa kuwa umetenda hivi umelaaniwa kuliko wanyama wote mwituni na kuliko hayawani wote walioko mwituni kwa tumbo utakwenda na mavumbi utakula siku zote za maisha yako” Na pia Mungu alimwambia Adamu na Hawa “Nanyi pia mmetenda dhambi Ninyi mlio kubali kudanganywa kutenda dhambi na huyo aliyeshiriki nanyi nyote pia.” Siku hizi manabii wa uongo huubiri Injili potofu wakisema “Pokea moto!” wale wanao danganywa nao pia wata pokea sawa nao kwenda motoni.
 

Bwana alitengeneza vazi la ngozi kwa ajili ya Adamu na mkewe.
 
Bwana aliwaza “Sito waacha Adamu na Hawa waliotenda dhambi kwa kudanganywa na Shetani kwa jinsi walivyo. Toka asili nilikwisha amua kuwaumba kwa mfano wangu na kuwafanya kuwa watoto wangu, hivyo nitawaokoa ili kukamilisha mpango wangu” Mpango huu ndiyo aliokuwa nao Mungu. Hivyo Mungu alimtwika mnyama dhambi zao, akamchinja shingo na kumuua mnyama huyo, akimchuna ngozi na kufanyiza ngozi yake kuwa vazi la Adamu na Hawa. Alifanya hivi kuwa ndiyo alama ya wokovu. Ukweli ni kwamba, lile vazi la majani lisingeliweza kukaa muda mrefu na ilipaswa lifanyiwe matengenezo kila mara. Mungu alimvika Adamu na Hawa, “njooni kwangu, tayari nimekwisha wafanyia upya vazi la ngozi ya mnyama la kuwavika. Ni ngozi ya mnyama aliye kufa kwa ajili yenu.” Bwana alimvika Adamu na Hawa kwa vazi la ngozi ya baraka ya Haki ya Mungu ili aweze kuwapa wote uzima mpya. Bwana Mungu alifanya vazi la ngozi kwajili ya Adamu na mkewe na kuwavika, kama vile Mungu alivyo wavika wale wote wanao amini wokovu vazi la haki yake.
Hata hivyo, wokovu wa mwanadamu ambao ni vazi la mmea litokanalo na majani yake nitofauti na wokovu wa Mungu. Mungu alituvika kwa vazi la ngozi, ambalo ndiyo haki ya Mungu Bwana ametuvisha ondoleo la dhambi kwa haki ya Mungu ambapo ametupatia mwili wake na damu yake. Alizichukua dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo wake na kusulubiwa ili apokee hukumu badala yetu. Mungu ametupatia msamaha wa dhambi pale tunapo iamini haki yake kwa njia ya Injili ya ubatizo na damu ya Yesu. Ni Injili yenye kuokoa wenye dhambi.
Wapo watu wengi wenye kujaribu kutengeneza haki zao binafsi huku wakiikataa haki ya Mungu hapa duniani. Imekupasa kuitupilia mbali haki yako. Katika Warumi 10:1-4 “Ndugu zangu nitakayo sema moyoni mwangu na dua yangu ni mwombayo Mungu ni kwa ajili yao, ili waokolewe. Kwa maana nawashuhudia kwamba wanajuhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe hawa kujitia chini ya haki ya Mungu. Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria ili kila aaminiye ahesabiwe haki.”
Waisraeli walikuwa wakisisitizia matendo ya sheria ili waweze kujiwekea haki zao wenyewe huku wakiipuuzia haki ya Mungu. Mungu aliwapa wanadamu sheria ili waweze kufahamu dhambi. Watu hutambua dhambi kwa njia ya Amri kumi za Mungu na hivyo kupokea msamaha wa dhambi kwa kuamini haki yake ya wokovu ambayo huwaokoa toka dhambini kwa njia ya mpangilio wa sadaka ya hemani. Hivyo sadaka ya dhambi itolewayo hemani inamaanisha juu ya Yesu kama mwakilishi wa Mungu katika Agano Jipya. Hata hivyo Waisraeli hawakuifahamu haki ya Mungu.
 

Kwa nini Yesu alibatizwa?
 
Kwa nini Yesu alibatizwa? Yohana Mbatizaji alimbatiza Yesu ili kusafisha dhambi zote za dunia hii. Yesu alimwambia Yohana Mbatizaji kabla ya kubatizwa “Kubali hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15). Hii ndiyo sababu ya ubatizo wa Yesu. Alibeba dhambi za ulimwengu kwa njia ya ubatizo “Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29) Alibeba dhambi zote na kusulubiwa ili aweze kuzilipia. Hata hivyo Waisraeli hawakumwamini Yesu kuwa ndiye Mwokozi wa kweli kwa wenye dhambi.
Waisraeli hawaja ikubali haki ya Mungu, lakini Yesu ndiye mwisho wa sheria ya haki kwa kila aaminiye. Mwisho wa sheria maana yake ni pale Yesu aliposafisha dhambi zote za dunia. Kristo alihukumiwa akiwa laana ya sheria. Yesu aliwakomboa watu wote kwa dhambi zao. Yesu alibatizwa ili kusafisha dhambi zote za wanadamu. Alibeba dhambi zote za ulimwengu kwa kutoa mwili wake kwa Yohana ili ubatizwe na kujitwika dhambi zote za dunia juu ya mwili huo. Ndipo alipo okoa watu wote kwa dhambi zao. Alihitimisha hukumu ya laana ya sheria kwa kuzichukua dhambi za dunia kwa njia ya ubatizo wake na kusulubiwa kwake. Alituokoa kwa njia iliyo sahihi toka hukumuni na laana ya sheria.
Ilikuwa ni mwisho wa sheria na mwanzo wa haki ya Mungu kwa wokovu. Kwa usahihi Yesu alizichukua dhambi zetu ulimwenguni kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji na hatimaye kwenda msalabani. Sasa basi itawezekanaje mtu awe na dhambi moyoni ingawa mtu huyo anaiamini haki ya wokovu wa Yesu kwa hakika? “Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani.” Ubatizo na damu ya Yesu ndivyo vyote haki ya Mungu. Kuamini haki ya Mungu ni kuamini ubatizo na damu yake. 
Zaidi ya yote hukumu ya haki ya Mungu ilikuwa ni kusulubiwa kwa Yesu. “Kristo ni mwisho wa sheria” Hukumu ya Mungu itakuja kwa wale wote ambao bado hawaja hukumiwa huku sheria ikiendelea kuwepo. Sheria ya Mungu ndiyo ifunuayo dhambi na kuithibitisha kwamba mshahara wa dhambi ni mauti, yaani laana na moto wa jehanamu. Hivyo ubatizo wa Yesu ulibeba dhambi zetu zote na kuhitimisha sheria ili kutimiza haki yote.
 

Wale walio kuwa wapumbavu walizitwaa taa zao wasitwae na mafuta pamoja nao.
 
Hebu na tuangalie Mathayo 25:1-13 Hapa upo mfano wa wanawali kumi walio kuwa wakimsubiri bwana harusi, kuja kwake Bwana. Tuone nini maana ya haki ya Mungu kwa kupitia maandiko.
“Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi waliotwaa taa zao, wakataka kwenda kumlaki bwana harusi. Watano wao walikuwa wapumbavu na watano wenye busara. Wale walio kuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao, bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana harusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manene pakawa na kelele, haya bwana harusi, tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawambia wenye busara, tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema sivyo, hayatatutosha sisi na ninyi, afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao mkajinunulie. Na hao walipokuwa wakienda kununua bwana harusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye harusini, mlango ukafungwa, halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana utufungulie, Akajibu akasema Amini nawaambia siwajui ninyi. Basi kesheni kwa sababu hamjui siku wala saa” (Mathayo 25:1-13).
Imeandikwa ya kwamba Ufalme wa Mbinguni umefanana na wanawalikumi walio beba taa zao na kwenda kumpokea bwana harusi. Ni nani watakao ingia ufalme wa Mbinguni? Kati ya wale wanawali ni wapi walio ingia Ufalme wa Mbinguni? Kwa nini baadhi yao hawakuweza kuingia Ufalme wa Mbinguni? Ingawa walikuwa wakimwamini Yesu kuwa ni Bwana walikuwa wapumbavu, na wengine watano walikuwa werevu. Wapumbavu walichukua taa zao bila mafuta. Taa husimama badala ya makanisa. Ukweli ni kuwa walizibeba taa zao lakini hazikuwa na mafuta, hii inamaanisha kwa wale waendao kanisani pasipo Roho Mtakatifu (mafuta maana yake Roho Mtakatifu kibiblia).
Wale walio wapumbavu walifanya nini? Walibeba taa zao bila mafuta. Mtu asiye zaliwa upya mara ya pili ingawa anamwamini Yesu, anaweza kujitolea kuhudhuria kanisani. Kila mtu utakuta akisema “kanisa langu ndilo halisi” kila mtu ulimwenguni husema hivyo. Watu hujigamba juu ya waanzilishi wa makanisa yao na tabia na utaratibu na dhehebu lao. Wale walio kuwa wapumbavu walibeba taa zao pasipo mafuta, lakini wale walio waerevu walibeba mafuta.
Mwanadamu ni nani? Mwanadamu ni kama chombo mbele ya Mungu. Ni mavumbi. Ameumbwa kwa mavumbi. Hivyo yeye ni kama chombo ambacho Mungu hukaa ndani yake. Waerevu walibeba taa zao na mafuta katika vyombo vyao.
 

Wanawali wapumbavu ambao wana taa tu bila mafuta kuchoma hisia zao
 
Biblia inatuambia ya kwamba wapo wanawali wapumbavu kati ya watu wanao mwamini Yesu. Hubeba taa zao pasipo mafuta. Hii maana yake hawajazaliwa upya mara ya pili. Je utambi usipo kuwa na mafuta utawaka muda mrefu? Vile itupasavyo kujua hapa ni kwamba taa pasipo mafuta huwaka muda mchache, haijalishi kama utambi ni mzuri. Waumini ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili ingawa wana upendo kwa Bwana hapo mwanzo, haichukui muda mrefu kati ya miaka 4 au 5 ndipo upendo huo hufutika. Yawapasa kugundua kwamba hawana ondoleo la dhmbi. 
Wale ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili au hawana mafuta (Roho Mtakatifu) hunena mambo kama vile “Hapo mwanzo nilikuwa ni mtu mwenye imani sana lakini sivyo tena kwasasa. Agalia na wewe utakuja kuwa kama mimi”. Watu wa aina hii ni manabii wa uongo na watakatifu waongo ambao wao huishi maisha ya kiudini pasipo kuzaliwa upya. Imewapasa wawe na imani ya wokovu kwa sababu imani zao ziko katika msingi wa hisia. Imewapasa kupokea wokovu kwa kuamini maji na damu ya Yesu Kristo na hivyo kupata mafuta ya Mungu kama zawadi. Utambi humaanisha moyo wa mwanadamu.
Wanawali walimsubiri bwana arusi katika kifungu hicho cha juu. Hapa imetupasa kuelewa msingi wa utamaduni wa Waisraeli. Sherehe za harusi hufanyika nyakati za usiku na huanza pale bwana arusi ajapo. Hivyo bibi harusi humsubiri. Hivi ndivyo ilivyo katika sherehe ya harusi kwa Waisraeli.
“Hata Bwana harusi alipo kawia, wote wakasinzia wakalala usingizi” pakawa na ukelele “haya bwana harusi tokeni mwende kumlaki” nao wakaondoka wale wanawali wote wakizitengeneza taa zao.” Wanawali hawa kumi walipokuwa wakimsubiri bwana harusi andiko linasema pakatokea ukelele “Haya bwana harusi, tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zinazimika.” Wapumbavu hawa mara zote ndiyo wajinga. Iliwapasa kutayarisha mafuta kabla ya kuja bwana harusi. Haijalishi ikiwa utambi wa taa kuwa dhaifu lakini ukiwa na mafuta ya kutosha hauwezi kamwe kuzimika.
Wanawali wapumbavu waliokuwa na taa zisizo na mafuta walizichoma tambi zao tu. Hii inamaanisha kwamba ni mioyo ndiyo iliyokuwa ikiungua tu. “Inanipasa kuzaliwa upya na kuishi maisha ya mtu aliye zaliwa upya na kujazwa Roho Mtakatifu” Waliiunguza mioyo yao kwa namna hii. Wakati wa utoto wetu, taa za mafuta zilitumika kuwasha mwanga katika vyumba nyakati za giza. Tukichoma karatasi litateketea kwa muda mchache kufumba nakufumbua. Moto wake utakuwa mkubwa na mkali wenye mwanga sana, lakini utazimika muda mchache tu.
Wanawali wapumbavu wenye kwenda motoni ni wale wenye kuiunguza mioyo yao (kwa hisia) pasipo mafuta na moto huo wa imani zao huzimika pale inapo wapasa kukutana na Bwana. Hawana Roho Mtakatifu ndani yao. Hudhani kuwa wanaamini vile ipasavyo ingawa ndani yao hawana Roho Mtakatifu. Huimba “♬uje Roho wa moto, uje♬” Huwa katika hali ya kuhaha. Ndipo wanawake wapendao kucheza muziki, huita “kucheza muziki wa Roho Mtakatifu” huku wakiruka ruka na kusema “njoo tunakusii ushuke!” Hawa ni wajinga na wenda wazimu. Tutakuwa wajinga ikiwa bado tunadhambi mbele ya Mwokozi, tunakuwa wanawali wapumbavu ikiwa bado tunadhambi mioyoni mwetu, ingawa bado tunamwamini Yesu. Usiwe mwanamwali mpumbavu.
 

Bwana atamu wao vipi mwanamwali mpumbavu?
 
Bwana ni Mungu Mtakatifu, Bwana harusi ni Mungu na Mwana wa Mungu asiye na dhambi. Hata hivyo utawezaje kukutana na Mungu huku ukiwa na dhambi? Je, ungependa kukutana na Mungu huku ukiwa na dhambi moyoni mwako? Hakika huu utakuwa upumbavu na ujinga kwako kufanya hivyo.
Yesu, Bwana harusi wetu alikuja ulimwenguni na kumweka bibi harusi katika hali ya utakaso. Aliwaweka wanawali kuwa watu wenye haki kwa kusafisha dhambi zao kwa njia ya ubatizo, aliwachagua kuwa wanawali kwake. Muda ulipo wadia wale watano wakasema “Tafadhali njoo”. Hata hivyo, watawezaje kuingia katika tafrija ya harusi wakiwa na nyuso zenye giza? Bwana harusi alitoka na kuwauliza “Mlikuwa wapi?” Sura zao zilikuwa na giza kwa sababu ya dhambi, walikuwa na uchungu mkuu kwa sababu ya dhambi zao zilizo ndani ya mioyo yao.
Bwana atamwoaje mwanamwali anaye lia kwa sababu ya dhambi zake? “Nakushukuru Bwana, kwa kunitakasa kwa jinsi hii.” Aina hii ya mtu ndiye atakaye kuwa mwenye furaha akiwa na bwana harusi wake wa kiroho ingawa bado ni dhaifu kwa kuwa bwana harusi anampenda na alimsafisha dhambi zake zote na udhaifu wake.
Bwana harusi humrekebisha bibi harusi katika kujipamba akimpatia vazi jema na manukato ya hali ya juu pamoja na vipodozi. Ndipo bibi harusi huvaa vazi na kujiweka mapambo yote ili awe tayari kukutana na bwana harusi. Bwana wetu alitumwa ulimwenguni sisi tukiwa kama bibi harusi ili atuongoze katika kukutana na bwana harusi. Ametoa kwetu mwili wake kwa ondoleo la dhambi pale mto Yordani. “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli” (Yohana 1:14). Bwana mwenyewe ndiye aliyebeba dhambi zetu zote ili tuwe na neema tele, kweli na msamaha wa dhambi kwa kumwamini yeye. Bwna harusi alibeba dhambi zote za bibi harusi pale mto Yordani. Bwana alimwokoa bibi harusi kwa dhambi zake kwa kuhukumiwa kwa niaba yake msalabani.
 

Je, tutaweza kweli kumnunua Roho Mtakatifu kwa fedha na kwa kujitoa?
 
Hata hivyo, wanawali wapumbavu waliwaomba wale walio na hekima kuwagawia mafuta, kwa kuwa taa zao zilikuwa zinazimika alipokuwa akiingia bwana harusi. Je, tutaweza kumgawana Roho Mtakatifu? Je tutaweza kununua msamaha wa dhambi kwa matendo mema, kujitoa au fendha? Wale wenye hekima waliwaelekeza kwenda kumnunua Roho Mtakatifu toka kwa wahubiri wa uamsho. Wapumbavu hawa walidhani walikuwa nao wamekwisha nunua huko. Walifikiri kuwa wangeweza kununua kwa fedha mafuta hayo. Walikuwa wakiishi maisha ya ukereketwa wa kidini, wa kidhani yakuwa kwa kutoa kwao sadaka kubwa na huduma zao, kuhudhuria kanisa la asili na kusali mara kwa mara kutawapa chochote kitu.
Lakini haijalishi chochote hakuna awezaye kununua msamaha wa dhambi ambao Bwana alitupatia kwa gharama yoyote hapa ulimwenguni. Wapumbavu hujaribu kupasha moto hisia zao hadi pale wanapo taka kusimama mbele za Bwana. Wale wanawali watano wapumbavu huku wakiwa na maisha ya kidini wakisema “Nitakufuata wewe tu, nitapanda hata mlimani kwa maombi ya kutubu. Twendeni tukamtumikie Bwana tuende hata nchi za mbali kuihubiri Injili.”
Bwana harusi alikuja mwishowe na shangwe kuu. Wale walio wapumbavu walitaka kwenda kununua mafuta alipo kuwa akiingia ila wale walio kuwa na msamaha wa dhambi na huku wakiwa tayari na mafuta (Roho Mtakatifu) waliingia katika sherehe ya harusi baada ya kutayarisha kila kitu. Ndipo akafunga mlango. Yesu hakuwachagua kwa bahati nasibu hawa wanawali watano. Namba tano maana yake “neema” kibiblia. Wanawali watano husimama badala ya wale wote walio na msamaha wa dhambi kwa neema na kuamini neema hiyo na matendo ya haki. Waligundua kile bwana harusi alicho watendea na kuiamini haki ya Bwana, ambayo ndiyo iwafanyayo kuwa wenye haki. Hata hivyo wale walio salia, wanawali wapumbavu hatimaye alisema “Bwana bwana utufungulie” akawajibu akasema “Amin nawaambia siwa jui ninyi”.
 

Twaweza kupokea zawadi ya Roho Mtakatifu pale tu dhambi zetu zitakapo futwa.
 
Wale wote wasio tayarisha mafuta ya taa zao kamwe hawato weza kukutana na Bwana. Bwana atawachukua wale tu wenye kuiamini haki yake na kuusubiri Ufalme wa Mbinguni na wale walio na ondoleo la dhambi mioyoni mwao, katika ufalme wa Mbinguni. Bwana alinena ahadi “Tubani mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Hapa nini kinacho fuata baada ya ondoleo la dhambi ni “kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo 2:38). Ikiwa mtapokea Injili ya haki ya Mungu dhambi ndani ya mioyo yenu zita futwa kwa hakika na ndipo Roho Mtakatifu atawajia. Kimwili au kihisia hatuwezi kuhisi uwepo wa Roho Mtakatifu wa Mungu ingawa, Roho Mtakatifu yupo. Twaweza kusema hatuna tena dhambi kwa sababu tunaye Roho Mtakatifu na neno la Mungu limo mioyoni mwetu. Yeye yule apokeaye haki ya Mungu huwa ni mtu mwenye haki ingawa aweza kuwa ni dhaifu. Hata hivyo yeye yule asiye na haki na Bwana, ataendelea kuwa ni mwenye dhambi.
 

Ndimo haki ya Mungu imedhihirika
 
Bwana alikuja kwa maji na damu. Alituokoa toka dhambini kwa ubatizo wake. Alibeba dhambi zetu pale alipo batizwa na kupokea adhabu kwa niaba yetu kwa sababu ya dhambi zetu zote kwa kumwaga damu yake. Je Mitume Yohana, Petro na Paulo wanasema nini juu ya hili? Wao kwa pamoja huzungumzia juu ya mwili wa Yesu na damu yake. Huzungumzia juu ya mwili wa Yesu na damu yake msalabani. Mathoyo 3:13-17 huzungumzia bayana juu ya ubatizo wa Yesu. Yesu alibatizwa ili kuweza kuwafanya wenye dhambi kuwa watakatifu na kuwasafisha kabisa kwa dhambi ya dunia katika mto Yordani.
Hebu natuangalie katika 1 Petro 3:21 Petro alishuhudia kwamba mfano wa waokovu ni ubtatizo wa Yesu. “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo unao waokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili bali jibu safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu amekwenda zake mbinguni malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake” (1 Petro 3:21-22).
Imeandikwa “mfano wa mambo haya ni ubatizo unao waokoa ninyi pia siku hizi, kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.” Ubatizo wa Yesu ulio beba dhambi zetu zote katika mwili wake, umekuwa ni uthibitisho wa wokovu wetu. Ukweli wa kumwaga damu yake ni uthibitisho wa kuhukumiwa kwake kwa ajili ya dhambi zetu. Je, unaona ninacho elezea? Hivyo Biblia inatamka kwamba Yesu ndiye pekee aliye kuja kwa maji, damu na Roho Mtakatifu (1 Yohana 5:6-9) Yesu aliletwa ulimwenguni akiwa na mwili wa mwanadamu kubeba dhambi zetu zote kwa namna ile ambayo Kuhani Mkuu Haruni alipo weka mikono yeke juu ya sadaka ya mnyama na kumtwika dhambi za watu.
Maji ni mfano unao tuokoa; yaani ubatizo. Imeandika kwamba si kuondolea mbali uchafu wa mwilini. Hii haimaanishi ya kwamba hauto endelea kutenda dhambi tena baada ya ondoleo la dhambi. Tunapokea msamaha wa dhambi kwa kuamini ubatizo wa Yesu. Je, hatutondelea kutenda dhambi kwa miili yetu? Ndiyo tunaendelea? Wengi wanaelewa visivyo juu ya ondolea la dhambi na kusema “kama huna dhambi moyoni, basi hutoweza kutenda dhambi” Hii haikueleweka Biblia inasema “Bila shaka hakuna mwandadamu mwenye haki hapo duniani ambaye afanya mema asifanye dhambi” (Mhubiri 7:20). Mwili ni dhaifu bado. Nidhaifu hata mwisho. Hutenda dhambi; hata siku ya mwisho wa kifo. “Siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu.” Dhamiri zetu hubadilika na kuwa dhamiri njema mbele ya Mungu kwa kupitia imani zetu katika ubatizo na damu ya Yesu. Dhamira hizi zaweza kumwita Mungu Bwana wetu na Mwokozi wa imani zetu katika ukweli kwamba Bwana alibeba dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo wake.
 

Ustawi wa mioyo yetu hutegemea Ubatizo wa damu ya Yesu.
 
Ustawi wa moyo ni ubatizo na damu ya Yesu. Ustawi wa moyo na mfano wa kile kisafishacho dhambi ni ubatizo wa Yesu. Kwa hiyo, Petro Mtume alisema kwamba ubatizo ni mfano unao tuokoa sisi.
Hebu natuone katika 1 Petro 1:22-23 “Mkisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia, upendano wa ndugu usio na unafiki basi jihatahidini kupendana kwa moyo. Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.” Amina.
Tumezaliwa upya mara ya pili na kupokea msamaha wa dhambi zetu zote kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu. Tunazaliwa upya mara ya pili “kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumula hata milele”. Haleluyah! Kuzaliwa upya mara ya pili hutokea kwa kupitia neno la uzima lenye kudumu hata milele ndani yako. Neno la Mungu hufananishwa na upawa ambao ni wa kupimia. Neno ni kifaa cha kupimia wokovu. Kipimo cha wokovu wa Mungu hakibadiliki.
Yohana Mbatizaji alisema katika Yohana 1:29 “Tazama! Mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya duniani.” Mwanakondoo wa Mungu aliyebatizwa mto Yordani ndiye mkate wa kweli wa uzima ambaye alituokoa kwa mwili na damu yake vyote.
Tunatakaswa na kuokolewa kwa kuamini neno la Mungu. Biblia inasema “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusika huja kwa neno la Kristo” na pia inasema “Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani kama ilivyoandikwa mwenye haki ataishi kwa imani” (Warumi 10:17, 1:17). Twaweza kuwa wenye haki kwa kuiamini Injili.
Je, umekwisha takaswa? —Amina.— Je, una dhambi ndani ya moyo wako tena? Ni Injili, habari njema, ‘euaggelio’ kwa Kiyunani. Haki ya Mungu ni ipi? Ni ule ukweli wa Bwana kusafisha dhambi zetu zote kwa kuutoa mwili wake na damu yake kwa ajili yetu sote. Haki ya Mungu hutuwezesha kutakaswa. Kubeba dhambi ya dunia na kusulubiwa kwa ajili ya wenye dhambi. Ni maji, ubatizo wa Yesu huzichukua dhambi za dunia kwa ubatizo na kusulubiwa. Haki ya Mungu imejumuishwa na ubatizo na kifo, ambapo msalaba ni mfano wa hukumu yetu. Hii ndiyo hasa haki ya Mungu ambayo imedhihirishwa ndani ya Injili.