Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 1-3] Mwenye haki ataishi kwa Imani (Warumi 1:17)

(Warumi 1:17)
“Kwa maana haki ya Mungu inadhihishwa ndani yake toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa Mwenye haki ataishi kwa imani.”
 

Yatupasa kuishi kwa Imani
 
Je, wenye haki huishi kwa namna ipi? Kwa imani. Wenye haki huishi kwa imani. Ukweli ni kwamba neno “Imani” ni la kawaida, lakini ni neno kuu na muhimu katika Biblia. Wenye haki huishi kwa imani tu. Natumaini tutaweza kupata mwanga toka katika kifungu hiki kwa sababu tuna mwili na Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu. Tunajaribu kutafsiri maandiko mengi kwa mawazo yetu pasipo kujua maana kamili iliyo fichika katika Biblia ingawa tunaweza kuelewa katika hali ya kawaidia. Kwa pamoja tuna mwili na Roho. Hivyo, Biblia inasema kwamba sisi wenye haki tutaishi kwa imani kwa sababu tunaondoleo la dhambi.
 

Lakini tatizo ni kwamba, mwili hautoweza kutenda jema.
 
Lakini tatizo ni kwamba tuna mwili pia. Hivyo, kila wakati, tuna pima mambo kwa mwili. Wakati mwingine, tunapima au kuhukumu jambo fulani tukiwa na mawazo ya kimwili yasiyo badilika, na hivyo hatuamini kabisa neno la Mungu pale inapokuja imani. Hata hivyo Biblia inasema kwamba mwenye haki ataishi kwa imani tu. Hii inamaana gani? Unaweza kudhani “wenye imani gani wasioishi kwa imani? Kwa nini unasisitiza juu ya mstari huu? Je ni mstari huu pekee katika maandiko?”
Leo hii, napenda kuwaeleza juu ya mstari huu Yatupasa kuishi kwa imani. Hatugundui kutofahamu kwetu hadi pale tutakapo jaribu kuelezea kwa kina jambo fulani ingawa tunadhani kuwa tunafahamu vyema juu ya hili kwa mawazo yetu. Mwenye dhambi anakabaliwa na mapambano gani? Mtu asiye zaliwa upya hupambana kwa mawazo yake pamoja na mwili wake. Aliye zaliwa upya kupambana na nani? Mwili na roho ndani ya mtu hupambana dhidi ya kila moja. Unaweza kushangaa kwa nini nimebaki kurudia kile ambacho tayari kimekwisha eleweka, lakini napenda kuelezea hili mara kwa mara kwa sababu ni jambo la maana.
Hata kwa mtakatifu aliyezaliwa upya mwili wake na roho yake huendelea kupambana kila moja kwa sababu bado wana mwili. Ipo sehemu mahususi katika mwili inayo pendelea kuishi kwa anasa, ikijaribu kuishi kwa ubora wajuu pasipo makosa yoyote ambapo ni kinyume kulingana na imani Mungu atuelekezayo kuishi.
Hivyo mwili wa mwenye haki nao pia hutaka kufikia ukamilifu hata kwa kazi za kiroho, huku ukijaribu kujishughulisha na kila aina ya tatizo la kiroho kwa ukamilifu na kutarajia kufikia ukamilifu wa kimwili kwa wakati mmoja. Je, lakini mtu aweza kuishi maisha ya imani kwa kutegemea mwili? Kama Paulo alivyo sema “Kwa maana lile jema nilipendalo silitendi bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo” (Warumi 7:19). Hapa mwili kamwe hauwezi kutenda jema. Tunatabia fulani katika mwili ambayo mara zote hutamani kuishi kiukamilifu mbele ya Mungu ingawa mwili huo kamwe hautoweza zaidi ya kutenda uovu.
 

Hatuto weza kuishi maisha ya Imani kwa kutegemea mwili
 
Kwa msisitizo nasema kujaribu kuishi kwa njia ya kujitoa maishani kimwili ni kinyume na kuwa na imani iliyo sahihi. Tuna mawazo yanayo pingana na tabia dhidi ya Mungu kalingana na mtazamo wa kibiblia. Kuwa mkamilifu kimwili na kuishi maisha ya imani pasipo tatizo lolote kimwili ni jambo lisilo wezekana. Mwili wa mwanadamu ni mfano wa mavumbi. Biblia inasema “Kwa maana yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sisi ni mavumbi” (Zaburi 103:14). Vilevile ni mfano wa mvuke au ukungu wa maji unaotokea kwa muda mchache na kutoweka kwasababu ya kutokuwa wakamilifu.
Je wote wawili, mwili wa mtu aliyezaliwa upya mara ya pili na yule asiye zaliwa upya mara ya pili wanauwezo wa kutenda dhambi? Je, mtu aliye zaliwa upya mara ya pili aweza kujizuia kutotenda dhambi? Hatuhitaji kamwe kuishi kwa imani ikiwa mwili utaweza kuendelea pasipo kutenda dhambi, Je, hatimaye tutaweza kuishi kwa kutegemea nguvu ya miili yetu? Hakika tunafahamu kwamba ni vigumu tatizo si kuelewa au kutoelewa kwetu kwamba ingawa sivyo au ndivyo tumezaliwa upya mara ya pili, hivyo pia mwili bado ni dhaifu unao endelea kutenda uovu.
Je, twajuaje kwa kiasi juu ya miili yetu? Twajuaje kuhusiana na nafsi zetu? Unaweza kudhani kuwa unajifahamu vyema asilimia mia moja 100% lakini utambulisho wa nafsi yako ni kinyume na tabia yako ya kweli kwasababu huamini kwamba ama kwa hakika wewe ni mwingi wa dhambi. Je ni kwa kiasi gani cha asilimia unachodhani kuwa unajua juu ya nafsi yako? Hata 50% itakuwa ni nyingi sana. Kwa kawaida watu hutambua nafsi zao kwa kiasi kidogo tu cha 10% au 20%, ingawa hudhani kuwa wana fahamu kwa asilimia mia moja. Wanapo dhani kuwa wametenda uovu mwingi ndipo wanapo fedheeka na hatimaye kuacha kumfuata Bwana ndipo hujiuliza ikiwa kama wataweza au kutoweza kuendelea na imani hata mwisho, na matoke yake kuishia kuona kuwa ni vigumu.
Maji machafu na taka hutoka nje na kuelea toka bomba la mawazo ya kimwili. Inaonekana kuwa ni vigumu kwao kuishi maisha ya kujitolea kwa imani “Oh! Nadhani kamwe haito wezekana kumfuata Bwana, nafikiri mwili wangu utakuwa na nafuu pale dhambi zangu zitakapofutwa mara moja na kwa wakati wote, lakini mwili huu bado ni dhaifu na wenye mapungufu, ingawa ni muda mrefu sasa” Hatui juu ya nafsi zetu hata kidogo na hasa pale tusipo kubali makosa ya miili yetu pia. Hivyo matokeo yake ni kwamba hatuwezi kuishi kwa uaminifu pale tunapo ona mawazo mengi ya kimwili yanapo jitokeza toka mwilini. Hatutoweza kamwe kuishi maisha ya imani kwa kutegemea mwili. Mwili wa mwanadamu ni nini basi? Je, mwili huo wa mwanadamu utaweza kutakasika kwa viwango hatua kwa hatua na hivyo kuishi kwa ukamilifu mbele ya Mungu ikiwa utazoeshwa vyema kwa majaribio? Hakika hii haitowezekana kamwe na mwili hautoweza kujizuia kutenda dhambi hata siku ya pumzi ya mwisho.
 

Sasa basi wenye haki huishije?
 
“Tena mtakapokosa msiyashike maagizo hayo yote Bwana aliyo mwambia Musa tangu siku hiyo Bwana aliyoleta maagizo, na baadaye katika vizazi vyenu; ndipo itakapo kuwa kama ni kosa lililofanywa pasipo kujua, wala mkutano haukuwa na fahamu ndipo wote utasongeza ng’ombe dume mmoja mdogo kuwa sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana pamoja na sadaka ya unga, na sadaka yake ya kinywaji kama amri ilivyo, na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi. Naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya mkutano wote wa wana wa Israeli nao watasamehewa maana lilikuwa ni kosa nao wamekwisa leta matoleo yao sadaka iliyo songezwa kwa Bwana kwa moto, na sadaka yao ya dhambi pia wanaileta mbele za Bwana kwa ajili ya kosa lao, nao makutano wote wa wana wa Israeli wataasamehewe, na mgeni akaaye kati yao; maana katika habari zao hao wote jambo hilo lilitendeka pasipo kujua. Tena kama mtu mmoja akifanya dhambi pasipo kujua, ndipo atasongeza mbuzi mmoja mke wa mwaka wa kwanza kuwa sadaka ya dhambi. Naye kuhani atafanya upatanisha kwa ajili ya huyo mtu akosaye, atakapo fanya dhambi pasipo kuja mbele za Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atasamehewa. Mtakua na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lolote pasipo kujua kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao” (Hesabu 15:22-29). 
“Tena mtakapo kosa, msiyashike maagizo hayo yote Bwana aliyomwambia Musa.” Yapo maelezo mengi ya neno “msiyashike maagizo” pasipo kusudio katika Biblia. Mwili huyaacha maagizo wakati mwingine pasipo kusudio na hivyo kufanya kile kisicho ruhusiwa kutendwa. Nauliza ikiwa yawezekana kwako kwa mwili wako kuwa mkamilifu, lakini umeshindwa hata baada ya kuwa na ukombozi. Lakini ukweli ni kwamba haitosaidia kwetu kujitambua na badala yake kujificha. Mwili huchujika uchafu na dhambi wakati wote. Mwili wakati wote hutenda dhabi ambazo Mungu huzichukia. Je mwili hautendi dhambi zisizo na idadi? Je, mwili mara zote kuishi vile Mungu apendavyo. Mwili hutenda dhambi pasipo kujizuia mara zote.
Sheria ya Mungu imejumuisha Amri kumi za Mungu na vipengele vya aina mbali mbali 613, “Usiwe na miungu wengine zaidi yangu. Usijifanyie na kujitengenezea sanamu. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, Ikumbuke siku ya Sabato na uitakase. Waheshimu baba na mama yako, Usiue, usizini, usiibe, usimshuhudie jirani yako uongo, usitamani nyumba ya jirani yako” Amri 4 za kwanza ni maelekezo ambayo yanatuhitaji kuwa na mahusiano na Mungu. Zilizo salia kuanzia ya 5 hadi 10 ni amri ambazo imetupasa kuzifuata kati yetu wanadamu. Lakini Je, Mwili uko radhi kutii amri hizi?
Katika barabara zipo alama za mistari kwa ajili ya waendao kwa miguu ili kuvuka kwa usalama barabarani. Lakini mwili kamwe hauko radhi kufuata sheria za barabarani. Watu huzifuata pale tu wanapo hisi kuwa wanaonekana na wengine. Ukweli ni kwamba hawako radhi kuzifuata sheria hizi. Huvuka barabara huku wakipuuzia alama za barabarani pale wasipo onekana.
Bila kupenda mwili hutenda dhambi. Watu wanapo kuwa wame elimika bara bara, itawapasa kufuata alama za usalama barabarani bila kujali ikiwa kama kuna anaye waangalia. Hata hivyo wataheshimika kwa mwili. Hatupendi kuvuka barabara kulingana na alama za usalama bara barani na hivyo tunajaribu kutotii kwa jinsi tuwezavyo.
Sasa basi nini sababu ya Mungu kutupatia sheria? Sheria hutuwezesha kuelewa dhambi (Warumi 3:20). Kwa sheria ndipo tunapo gundua kwamba tu wadhambi ambao wakati wote hatutii Amri kumi. Tunatenda dhambi nyakati zote. Sheria siku zote hutuhitaji kutenda mema na si uovu. Hata hivyo bado miili yetu mara zote hutenda dhambi kwa sababu ya udhaifu wa kutofuata sheria. Biblia inasema kwamba wenye haki wataishi kwa imani. Hata hivyo, wenye haki walio na miili hii watawezaje kuishi kwa imani? Nao hawawezi kuishi kwa sheria, katika miili yao sasa watafanyaje? Wataishi kwa imani.
Roho hutaka kufuata mapenzi ya Mungu lakini mwili wakati wote hutenda dhambi, kutotii vipengele vyote vya Amri kumi za Mungu, matokeo ya dhambi za mwili ni kutenda hili na lile leo na kesho. Zipo dhambi ambazo mwili hupendelea kutenda zaidi ya nyingine. Mwili wa mwanadamu hutenda dhambi siku zote maishani. Je hivi ndivyo au la?
Hebu tuichunguze ile amri ya tano “Waheshimu baba na mama yako” Hakika hii ni sawa na watu kujaribu kufuta ingawa kwa kiasi hawawezi kwa muda wote kutekeleza. Sasa hebu tuiruke katika kuizungumzia. Inayofuata ni “Usiue” Sisi sote hufanya mauaji katika mawazo yetu huku wachache wetu tu wakiua kimwili. Hata hivyo hii nayo tuiruke kwa sababu ni dhambi mbaya sana. Inayo fuata ni “Usizini” na “Usiibe” Dhambi hizi ni rahisi kuzitenda katika maisha ya kila siku: baadhi ya watu walifanya kuwa ni tabia kwao kutenda dhambi aina hizi. Je, hawatamani mali za wenzao pia? (Biblia inasema kutamani mali ya mtu ni dhambi pia). Pia ni wepesi kusogeza hata mali za wengine mahala pake (kuiba) Mwili hutenda aina hizi za matendo maovu pindi unapotaka.
Hebu, kwa mfano tunatenda dhambi moja au mbili kati ya hizi aina kumi Je, kwa hili tutaweza kuwa wenye haki mbele ya Mungu? —Hapana haitufanyi.— Sisi si wenye haki mbele ya Mungu kwa kupitia mwili kwa sababu hata dhambi iliyo ndogo bado ni dhamni tu. Mwili hutenda dhambi mara kwa mara hadi mwisho wa kifo. Mwili hauwezi kujizuia kutenda dhambi mbele ya Mungu hadi siku ya kifo. Hivyo basi, umekwisha kuwa safi na kutakasika mbele ya Mungu hata leo? Hebu tuangalie mwili huu huku tukiutenga mbali na Roho. Je haujawahi kumtendea Mungu dhambi kwa sababu ya ukamilifu wako katika mwili? Hata dhambi moja ukiwa usingizini, utakuta unapendelea kuangalia picha zisozofaa hata ndotoni huku ukiwaza juu ya umbo la mwana mke mrembo. Wote tunatenda dhambi.
Mwili hutenda kile Mungu aelekezacho tusitende na hautendi kile aelekezacho kutenda. Mwili kubaki kuwa ni ule ule hata baada ya dhambi kufutwa. Tutawezaje kuwa wakamilifu? Hata hivyo inawezekana kwa njia ya Yesu Kristo tu. 
Sisi ndiyo tulio tenda dhambi hizo. Je hatukumtendea Yesu? —Ndiyo tumemtendea.— Je, hata sasa tunatenda au la? —Ndiyo tunatenda.— Je tunaendelea kutenda au la? —Ndiyo tunaendelea.— Tutaendelea kutenda dhambi hadi siku yetu ya kifo ikiwa bado tutakuwa na mwili. Sisi ni viumbe wenye dhambi ambao hatuwezi kuacha hata siku ya mwisho wa pumzi zetu. Kwanza ikiwa bado hujazaliwa upya mara ya pili, inakupasa kukiri kwamba wewe ni mwenye dhambi mbele ya Mungu ambaye atafutilia mbali dhambi hizo. Baada ya kukombolewa tunahitajika kukiri kwamba tumetenda dhambi pale tunapo kosa. Yatupasa kukiri hivyo baada ya kujichunguza kwa kupitia sheria pale tuangukapo ingawa wakati mwingine tunatenda mema kwa miili yetu huku tukujifananisha kuwa ni wema. Yatupasa kuikubali dhambi kuwa ni dhambi.
 

Tunatakaswa kwa imani.
 
Je tunachukiaje tatizo la dhmbi hasa baada ya kulikiri? Je, tulitakaswa baada ya kuamini kwamba Yesu alizibeba dhambi zetu zote kwa kubatizwa kwake na Yohana Mbatizaji na kuhukumiwa msalabami ili kutuokoa? —Ndiyo.— Tulitakaswa kwa kuamini kwamba dhambi zetu zote zitokanazo na mwili zilitwikwa juu yake Yesu pale alipobatizwa. Hivyo basi kifungu kisemacho mwenye haki ataishi kwa imani kina maana gani?
Kuwa na imani ni kumwamini Roho, si mwili. Kumwamini Mungu tu, neno lake, sheria yake na ukombozi wake ndiko kutakako tutakasa. Na tutakuwa wakamilifu baada ya kuwa wenye haki kwa kuwa na imani juu ya Yesu. Je, hivi ndivyo au sivyo? Ndivyo. Mwili bado ni dhaifu na si mkamilifu hadi pale tunapo kuwa wakamilifu kwa kupokea ondoleo la dhambi. Biblia inasema “kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa kukiri hata kupata wokovu” (Warumi 10:10). Lakii mwili wakati wote ni dhaifu na usiomkamilifu, kama ule wa Mtume Paulo. Hivyo hatutaweza kamwe kuwa wenye haki au hata kufikia kiwango cha haki hatua kwa hatua kwa kuutegemea mwili. Mwili kamwe hautoweza kuishi maisha ya haki.
Njia pekee ambayo wenye haki wataweza kuishi ni kwa kumwamini Mungu, ambako ndiko kukubali ondoleo la dhambi na baraka ambayo alitupatia. Tutaweza kutakaswa na kubaki wenye haki huku tukitegemea haki ya Mungu milele, amabayo tuliipokea toka kwa Mungu na kuishi milele kwa imani zetu juu yake. Maisha yetu hutegemea zaidi imani juu ya Mungu. Hivyo Biblia inasema kwamba mwenye haki ataishi kwa imani. Tunatakaswa kwa imani na kuendelea kuwa na haki ya Mungu kwa kuwa na imani na kuendelea kuishi nayo. Ingawa mwili si wenye haki. Ni upumbavu kujaribu kutakaswa hatua kwa hatua kwa sababau haiwezekani. Tutaweza kuishi pale tu tunapo pokea msaada wa Mungu kwa kumwamini yeye kuwa ndiye Mungu wetu, Bwana wetu na Mchungaji wetu.
Hivyo Mtume Paulo anasema “mwenye haki ataishi kwa imani” akiwa amenukuu katika Habakuki ndani ya Agano la Kale pia anasema “kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake (Injili) toka imani hata imani.” Haki ya Mungu ndiyo nini? Je, ni sawa na ile ya wanadamu? Je, kwa kupunguza dhambi kidogo kidogo kwa njia ya utakaso wa hatua kwa hatua ndiko hutatutakasa kabisa? Je, sisi ni wakamilifu kwa kuwa tu hatutendi dhambi tena baada ya kumwamini Yesu au baada ya kuwa na imani?
Ni katika Injili tu ambamo haki ya Mungu ilidhihirishwa na ndiyo yenye kututakasa kikamilifu kwa ondoleo la dhambi kwa sababu kamwe hatutoweza kuwa wenye haki kwa miili yetu. “Kwa maana haki ya Mungu inadhihishwa ndani yake toka imani hata imani.” Maana yake ni kwamba tunakuwa wenye haki kwa imani. Mwenye haki ataishi kwa kuwa ana imani katika Mungu baada ya kuwa mwenye haki. Wenye haki huendelea na haki hiyo ya Mungu na kupokea baraka zake zote kwa kupitia imani.
 

Yatupasa kuishi kwa imani.
 
Kuishi kwa imani ni kama ifuatavyo. Wanadamu huporomoka kirahisi kama nyumba ya tope, haijalishi kwa namna gani ni madhubuti. Mtu aweza kusema “Nitafanya hivi na vile Bwana.” Hata hivyo, mwili hushindwa. Tunaishi kwa imani katika Bwana na neno la ukombozi toka dhambini na sheria baada ya kupokea ondoleo la dhambi. Je, mwili utaweza kubadilika na kuwa wenye afya njema, mrefu na safi ikiwa tutaishi maisha ya imani kwa muda mrefu? Kamwe sivyo. Hivyo kuishi kwa imani ni kumwamini Mungu ipasavyo. Tunakuwa wenye haki kwa kuwa na imani kikamilifu juu ya Injili na kuishi kwa kupokea baraka zote za Mungu kwa imani juu yake.
Mwenye haki ataishi kwa imani. Hii ni kuiishi kwa imani yetu juu ya Mungu. Je una amini hivyo? —Ndiyo.— Je, inatokea wakati mwingine unakuwa na matarajio yatokanayo na mwili? Je hutokea ukawaza, “natumaini 20% mwili wangu bado ni bora kwa sehemu hii, ingawa mwili wangu huu bado si mkamilifu kwa sehemu iliyo baki?” Hata hivyo Biblia inasema kwamba, mwenye haki ataishi kwa imani. Mungu anasema kwamba, mtu hatoweza kuishi kwa kuutegemea mwili, hata kwa 0.1% Je unawazo la kuifuata imani hata siku Bwana atakapo rudi tena huku ukiacha kutotenda dhambi ya kuutumaini mwili hata kwa kiwango kidogo?
Tunakuwa wenye haki kwa imani katika Yesu hata kama ni kwa kiasi gani twaweza kuwa tumetenda dhambi. Sisi ni wenye dhambi kimwili ikiwa hatutoweza kumwamini Yesu ingawa ni kwa kiasi fulani tu wema. Tunatakaswa pale tunapo mwamini Yesu 100%, lakini tunakuwa wenye dhambi pindi tusipo mwamini yeye kwa 100%. Je, Mungu huridhishwa japokuwa tunatena dhambi kwa kiasi kidogo? Je, inampendezesha Mungu ikiwa tunakuwa wenye haki kwa kuitegemea miili?
 

Haki ya Mungu ilitufanya kuwa wenye haki.
 
Hebu natuone Warumi 3:1-8 “Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwa faa nini? Kwa faa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. Ni nini basi ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je, kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo kama ilivyo andikwa ili ajulikane kuwa una haki katika maneno yako, ukashinde uingiapo katika hukumu. Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je, Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu) Hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu? Lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ni ngali nahukumiwakuwa ni mwenye dhambi? Kwa nini tusiseme (kama tulivyo singiziwa na kama wengine wanavyo kaza kusema ya kwamba ya twasema) Natufanye mabaya ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki” (Warumi 3:1-8).
Mtume Paulo alisema “Lakini ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu tuseme nini Je, Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu?” Je, Mungu ni dhalimu na mkosaji kwa neema yake? Kile Mtume Paulo alichokuwa akikiuliza kwa kuwajibu wale walio mletea fedheha ni kwamba “kiasi cha udhaifu wetu kinapo ongezeka ndicho kiasi kikubwa cha haki ya Mungu kituokoacho dhambi zetu zote kitakacho kuwepo”. Mtumwe Paulo hunena na wale wenye kushangaa vile mwanadamu wanavyo tenda dhambi kwa maisha yao yote watakavyo weza kutakaswa. Anasema kwamba udhaifu wa mwanadamu ndiyo wenye kuweka wazi haki ya Mungu. Wanadamu, ambao miili yao haiwezi kuacha kutenda dhambi hadi siku ya mwisho wa pumzi, huonyeshe ukuu wa haki ya Mungu kwa kupitia udhaifu wao.
Haki ya Mungu haimaanishi chochote ikiwa mtu ataweza kuwa mwenye haki binafsi kwa juhudi zake pamoja na haki ya Mungu, ikiwa mtu ataweza kuokolewa kwa 97% kwa msaada wa Mungu na asilimia 3% kwa juhudi zake binafsi. Paulo anasema kwamba Mungu mwenyewe kwa ukamilifu ndiye aliye waokoa wale wote wenye kuendelea kutenda dhambi hadi siku ya kifo kwa kupitia Yesu. Hivyo basi uovu wetu huonyesha jinsi ile ya utajiri wa Mungu ulivyo mkuu. Mwili hautoweza kuacha kutenda dhambi hata siku ya mwisho wa kifo; hivyo hautoweza kuwa mkamilifu hata kwa siku moja, Ukweli wa kwamba Yesu alituokoa kiukamilifu sisi tulio wenye dhambi toka hukumuni, huonyesha jinsi ile ya haki ya Mungu ilivyo kuu. Hivyo Mtume Paulo anasema “Kwa nini tusiseme (kama tulivyo singiziwa, na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba kuhukumiwa kwao kuna haki” (Warumi 3:8).
Je, tutaweza kuwa wenye haki kwa kutegemea mwili? Je, mwili utaweza kuwa mkamilifu baada ya kupokea msamaha wa dhambi? Kamwe hautoweza. Je mimi na wewe na watu wote walio hai duniani tukiwapa swali hili kuwa, wataweza kuwa wenye haki kwa kutegemea miili yao? —Hapana.— Je Bwana wetu alituokoa kiukamilifu au la? —Ndiyo.— Bwana alituokoa kiukamilifu kutokana na dhambi zetu zote. Je, bado tunadhambi ikiwa tuna mwamini Yesu kwa mioyo yetu yote? —Hapana.— Hatuna tena dhambi hata ikiwa twaweza kuwa wakosaji.
Bwana alisema, “Tena mmesikia watu wa kale walivyo ambiwa, Usiape uongo ila mtimizie Bwana nyapo zako, lakini mimi nawaambia, usiape kabisa; hata kwa mbingu kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. Wala usi ape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. Bali maneno yenu yawe ndiyo, ndiyo; siyo, siyo kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwevu” (Mathayo 5:33-37). Kuapa tu ni dhambi kwa sababu hutoweza kutimiza kile unacho apa. Hivyo usiape au kuweka ahadi ya kutenda jambo baadaye. Amini neno la Mungu ndipo utakapo, kuwa hai Waweza kuwa mwenye haki ikiwa utaamini haki yake na Bwana atakusaidia ikiwa utamwamini yeye tu.
Zipo aina nyingi za ndoto. Tunapitisha hukumu ya kimwili na kuamua kimwili kwa sababu ya huo mwili. Hivyo, yupo mhukumu ndani yetu asiye shikamana na imani ya neno la Mungu. Wapo wahukumu wawili ndani yetu. Mmoja wapo ni nafsi zetu na mwingine ni Yesu. Hivyo wote wawili hujaribu kuchukua nafasi ya utawala ndani yetu. Tunajaribu kufanya sheria za mwili na kutoa hukumu yake kwa kuwa tuna mwili. Mwili hutuambia “wewe ni mwema ingawa unaendelea kutenda dhambi; Nitakupitisha kuwa mwenye haki ingawa mwili wako si 100% mwenye haki” Hukumu ya mwili siku zote hunena namna hii.
Ingawa hukumu ya haki ya Mungu hutuhitaji tuwe 100% tusio wenye dhambi, Mungu ni Mtakatifu. Tutaweza kuwa wenye haki ikiwa tu kwa kupokea ondoleo la dhambi kwa kupitia imani zetu. Hivyo basi wanao amini Injili ya Mungu tayari wamekwisha ifikia haki ya Mungu. Tayari tumekwisha kuwa wenye haki wenye kumwamini Mungu na hakika tuta ishi kwa imani. Maana yake ni kwamba wasio amini na wale wote waishio kwa kutegemea mwili hawato ishi kwa imani. Narudia tena kuwaambia na kuwaelezea maana ya undani huu, kwa jinsi ile ya mfano wa kuchemsha mifupa zaidi na zaidi hadi mchuzi unapo geuka na kuwa mweupe.
 

Twahitaji imani.
 
Ni muhimu kuielewa Biblia, ingawa nikiasi gani tunaielewa ndicho kilicho muhimu zaidi. Baadhi ya watu huamini uumbaji wa Mungu tu katika Maandiko. Baadhi nao huamini yote mawili, Mungu Kuumba mbingu na nchi, na vile Yesu kusafisha dhambi zetu za asili. Hawa huamini kwamba dhambi zao za kila siku zinapasa kutakaswa kila siku. Hujiwekea hukumu yao binafsi kulingana na sheria ya mwili. Je, ni kwa kiasi gani tunaamini? Wenye haki wataishi kwa imani tu, kuanzia mwanzo hadi mwisho tuna hitaji imani katika Mungu.
Hivyo ni kwa kiasi gani basi unaamini? Je, inatokea kwako kujipima jinsi utakavyo, huku ukiweka mawazo binafsi ukidhani—ni safi, mwili wangu ni barabara au mimi ni dhaifu kushindwa kumwamini Mungu- Je inatokea kujipa alama ya 80% leo na 95% siku inayo fuata, lakini 5% baadhi ya siku huku ukidhani —Ningeliweza kuwa nafuu zaidi kwangu endapo nisinge zaliwa— Je, unawaza namba hii? —Ndiyo.— Hata mimi pia.
Nasema kweli hata mimi. Hata pale ninapo jigundua mwenyewe, huwaza, “ingelikuwa ni afadhali kwangu nisingeli mfahamu Bwana na kumwamini. Inaonekana kuwa ni vigumu kuishi maisha ya kujitolea kiimani. Imekuwa ni ngumu hata sasa. Niko njia panda kwa kuona hatima yangu mbeleni na kurekebisha yaliyo pita. Nina stahili kupata sifa kwa kuishi maisha ya imani kwa kiasi hadi sasa, lakini sintoweza kuendelea kuishi na Bwana toka sasa. Nimekuwa mwepesi sana kuelewa dhambi kwa sababu nina mjua Mungu. Mawazo mengi na hukumu yamekuja toka ndani yangu tangu nilipo kujua Bwana. Nimekufuata bure Bwana, si kwa jinsi nikujuavyo sasa lakini, sina uhakika na nafsi yangu katika kukufuata wewe tena. Kwa nini? Kwa sababu nafahamu Mungu Mtakatifu na mkamilifu. Ah! Bwana, siwezi kukufuata tena. Sina uhakika.”
Hivyo Mungu hutuambia tuishi kwa imani kwa sababu yeye anajua jinsi ile tulivyo. “Yakupasa uendelee kuwa mwenye haki na kuweza kubarikiwa kwa imani. Dhambi zako zote zilitwikwa juu yake Yesu Kristo kwa njia ya ubatizo wake wewe hutenda dhambi kila ninapo wianisha mwili wako na Sheria. Hivyo basi ukiri kwamba hutoweza kuacha dhambi. Je, Mwokozi wako hakuzibeba dhambi zako zote au la?               —Alizibeba.— Je, dhambi zako zote hazikuitwika juu yake Mwokozi au la? —Ndiyo.— Sasa basi je, unadhambi bado     —Hapana.— Je, Bwana hakukuokoa au la? —Ndiyo.— Wingu na siku ya giza vitageuka kuwa nuru ya mchana kama vile wimbo wa tenzi za rohoni usemao “Kuna nuru ya Jua ndani ya Nafsi yangu leo.”
 

Kwamwe hatutoweza kuwa wenye dhambi tena.
 
Unaweza kukata tamaa pale unapowaza juu ya wakati ujao, lakini ni kweupe na ni mchana pale tunapo mwangalia Bwana kwa imani. Hivyo Mungu anasema kwamba mwenye haki ataishi kwa imani Je, unaimani hiyo? —Ndiyo.— Je, utaweza kuendelea kuwa na haki ya Mungu kwa kuushurutisha mwili vyema? —Hapana.— Je, haki ya Mungu hubadilika pale mwili unapotenda maovu? Je, tunakuwa wenye dhambi?        —Hapana.—
Mtume Paulo anasema katika Wagalati 2:18 “Maana nikija jenga tena yale niliyoyabomoa naonyesha ya kuwa mimi mwenyewe ni mkosaji.” Mtu anaye amini kwamba dhambi zake zote zilitwikwa juu ya Yesu Kristo kwa njia ya ubatizo wake kamwe hawezi tena kuwa mwenye dhambi kwa sababu dhambi zake zote zilitwikwa juu ya Yesu na hawezi tena kuwa mwenye dhambi kwa mara nyingine. Unaelewa? —Ndiyo.—
Mungu amekwisha tuokoa na ni Bwana wetu siku zot na ni Baba. Wakati wote Mungu hutusaidia na yuko pamoja nasi hata siku ya mwisho wa dunia. Na hii ndiyo sababu husema, “Ishi kwa imani Nita kusaidia ikiwa utaendelea kuniamini mimi.” Malaika ni watumishi kati yetu na Mungu. Humwambia Mungu kila kitu juu yetu. Mungu ametufanya kuwa watoto kwake. Tulikuwa wenye dhambi kwa asili. Kamwe hatutoweza kuwa wenye haki kwa imani.
Tunashukuru Bwana Bwana amekuwa mchunguanji na Baba kwa imani.