Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 1-4] Mwenye haki huishi kwa Imani (Warumi 1:17-18)

(Warumi 1:17-18)
“Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani kama ilivyoandikwa, mwenye haki ataishi kwa imani. Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.”
 

Inatulazimu kuishi kwa Imani
 
Imeandikwa “Mwenye haki ataishi kwa imani” Je, tunaishi kwa imani au la? Njia pekee ya mwenye haki kuishi ni kwa imani. Imani ndiyo imwezeshayo mwenye haki kuishi. Twaweza kuishi na kuendelea na mambo yote pale tu, tutakapo mwamini Mungu. Wenye haki tu ndio wawezao kuishi kwa imani. Neno “tu” maana yake hakuna zaidi ya yeyote awezaye kuishi kwa imani ila mwenye haki. Sasa, vipi kuhusu wenye dhambi? Wenye dhamba kamwe; hawatoweza kuishi kwa imani Je, wewe unaishi kwa imani? Inatulazimu kuishi kwa imani.
Inachukua muda mrefu kujifunza imani ya kweli. Kile kitupasacho kuelewa ni kwamba tunaishi ikiwa tunamwamini Mungu na kufa endapo hatumwamini Mungu. Yatupasa tuelewe ya kwamba ni hatima ya mwenye haki kuishi kwa imani.
Ndege wanambawa lakini ikiwa hawatozitumia watakamatwa na kuuwawa na wanyama watambaao ardhini. Hivyo wenye haki ndiyo wenye hatima ya kuishi kwa imani. Mungu ameweka hatima ya wenye haki katika kuishi kwa imani. Ikiwa watashindwa basi roho zao zitakufa.
Maisha ya Mkristo na njia ya kweli huanza kwa imani. Mwenye haki atawezaje kuendana na jamii baada ya kuzaliwa upya kwa maji na Roho? Yatupasa kujua kwamba njia pekee ni kwetu kuishi kwa imani.
Je, unaelewa? Ni uhai kwa mwenye haki. Pasipo imani tutakufa na kukosa nguvu ya kuendana na magumu. Ikiwa mtu asiye ishi kwa imani au hata kutumia imani atapitia magumu, na hatimaye atakufa. Ikiwa mtu atakuwa na imani juu ya Mungu na kukiri “Bwana ninakuamini wewe”, basi mtu huyo ataweza kuishi, ingawa ataweza kuwa ni dhaifu na mwenye kushindwa. Ataweza kuishi kwa kuwa na imani kwa Mungu. Mungu husaidia mtu na kuenenda kwa kwa kadiri mtu awezavyo kumwamini yeye.
 

Tunapo gundua kikomo chetu, ndipo basi tunapo jifunza juu ya imani.
 
Nataka ufikiri juu yako ikiwa umekwisha ishi kwa imani au la. Mtu hawezi kuanza kuishi kwa imani pale tu anapo zaliwa upya. Huishi kwa kutegemea na mazingira kwanza hivyo hajifunza kuishi kwa imani. Kwa nini? Kwa sababu mtu ataweza kuishi hapa duniani akifanya kipato cha fedha kwa mikono na miguu yake; hivyo kutokuwa na umuhimu wa imani katika Mungu. Lakini hatimaye tunaweza kuhisi vikomo vyetu, pale tunapo anza kushangaa na kujiuliza ikiwa tutaweza kuishi kwa kutumaini nguvu na juhudi za kimwili. Hapo ndipo tunapo ona kwamba haitowezekana. Sasa basi tutaweza kuishi vipi? Yatupasa kutumia imani. Hatutoweza kamwe kuishi ikiwa hatutotumia imani na kumwamini Mungu.
Yatupasa kuishi kwa imani hata kwa mambo madogo huku tukisema “Bwana! Nakuamini tafadhali nisaidie”. Tunapo mwamini Mungu hata kwa mambo madogo, huku tukisema “Bwana! Nakuamini, naamini kwamba umenisaidia, Nakuamini”, hapa tunaweza kuthibitisha kwamba tunaweza kuishi kwa imani hata kwa yale mambo madogo.
Tutaweza kuona vile tunavyo kuwa imara na kuwa na matarajio ya mambo yatakayo tokea pale tu tatakapo amini. Hata hivyo, ikiwa hatutomwamini Mungu hatutoweza kuelewa kwamba Mungu ameruhusu yatendeke, na hivyo kupoteza tumaini kwa kuwa hatuyaoni kwa imani. Hatutoweza kutatua matatizo ingawa suluhisho laweza kuwa ni rahisi kwa imani. Kuishi kwa imani ni vyema kwa kila njia, hivyo yatupasa kujifunza kuishi kwa imani.
Watu katika Agano la Kale waliishi kwa imani na hivyo ni sawa pia kwa watu katika Agano Jipya kuokolewa kwa imani. Tunakuaje na uhakika wa wokovu wetu? Je tumekuwa wenye haki kwa kuamini kile Yesu Kristo alichofanya? Ndiyo. Mungu hutusaidia pale tunapo ishi kwa kumwamini yeye. Kabla ya yote mwamini Mungu na uombe chochote utakacho ndipo Mungu atakusaidia. Mungu hutupatia mambo mengi kwa jinsi ile atupavyo wokovu. Imani imo katika sehemu zote za maisha yetu. Ni uhai.Uhai kwa wenye haki ni imani. Imani ni uhai. Ni sawa na damu katika mwili. Mtu aliyezaliwa upya asipokua na imani, roho yake hufa kama vile mwili usipokuwa na damu. Yatupasa kumwamini Mungu na kukiri “Mungu nakuamini. Naamini kwamba unanisaidia na kutatua matatizo yangu.”
Ni imani ndiyo itafutayo ufalme wa Mungu kwanza kabla ya kutafuta kile tunacho hitaji kimwili na kuamini kwamba bila shaka Mungu atajibu sala zetu. Yatupasa kuishi kwa kuamini. Kile tulicho nacho katika mwili wakati fulani kitageuka kuwa ni bure tunapo ishi hapa duniani. Hivyo tutakutana na hatari au hali isiyo zuilika hapo baadaye. Katika wakati huo jambo lililo la muhimu linalo hitajika ni imani katika Mungu; yaani kuamini kwamba Mungu alikwisha tuokoa, kutusaidia na kuwa yeye ni mwema.
Zaidi ya yote tunahitaji imani ya kwamba Mungu hutupatia yote tuomabayo na tutafutayo ikiwa yanafaa mbele yake. Imani hutuongoza katika kuishi kwa neema yake pale kile tulicho nacho kimwili kinapo fika kikomo, yaani uwezo na nguvu zetu kimwili. Imani katika Mungu hugeuka na kuwa ni kichocheo cha nguvu kwetu katika kukamilisha kile tunacho tumaini mbele ya Mungu.
 

Yatupasa kutumia imani hata kwa mambo madogo pia.
 
Kwa namna gani yatupasa kuishi? Yatupasa kuomba kwa mfano, “Mungu nakuamini, nimepungukiwa na kutokuwa na hiki na kile, hivyo nisaidie Bwana” Hapa sizungumzii juu ya udhaifu wetu wa asili. Hebu na tuishi kwa imani, huku tukisema “nahitaji hili na lile katika maisha yangu ya kila siku. Tafadhali nisaidie Bwana. Naamini utanifanyia” Mtu anayeishi kwa imani yampasa kumtafuta Mungu kwa kuanzia maswala hata yaliyo madogo. Mfano “Bwana sina dawa ya kusukutulia meno. Tafadhali nipatie. Nakuamini wewe” Hivyo basi, tunaweza kuyaona majibu ya Mungu pale tunapo mwamini yeye na kumtafuta.
Kwa namna gani wenye dhambi huishi? Wenye dhambi hushi kwa kutumaini juhudi zao wenyewe, lakini wenye haki huishi kwa imani. Tunaweza kutumia imani zetu katika maisha yetu pale tunapo jua ya kwamba wenye haki huishi kwa imani. Hatuishi kwa kile tulicho nacho bali kwa imani. Je, unaona? “Mwenye haki ataishi kwa imani” Kile mwenye haki anacho hitaji hasa ni imani lakini tunakuja kuitumia imani pale tunapofikia mwisho wa yale tunayo hodhi kimwili.
Tunakuja kutumia imani pale uwezo wetu wote na vile tunavyo vihodhi vinapo kwisha. Hata hivyo yatupasa kutambua kwamba kuishi kwa imani ni jambo la hakika na kweli katiaka amri ya Mungu, ambalo msimgi wake ni ahadi za Mungu ambazo bila shaka tunazihitaji katika maisha yetu. Ishi kwa imani. Mwamini Mungu na umtafute. Ndipo utakapo pokea na kupata kile unacho kihitaji. Yatupasa tujifunze namna ya kuishi kwa imani toka yale yaliyo madogo na ndipo hatua kwa hatua tutaweza kuwa na imani madhubuti.
Daudi alimuua Goliathi kwa mawe madogo 5 kwa imani. Ali muua Goliathi kwa imani ya kwamba Mungu alikuwa upande wake, huku akiwaza “Mungu na kuamini, kumuua Goliathi ni mapenzi yako” Na kumshinda Goliathi “Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, wewe unanijia mimi na upanga na fumo na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi Mungu wa majeshi ya Israeli ulio watukana” (1 Samweli 17:45) kwa imani Abrahamu alipoitwa alitii kwa kutoka nje ya makao yake na kwenda sehemu nyingine ambayo angerithishwa, na kwenda huku asijue ni wapi.
Mwenye haki ataishi kwa imani. Katika Injili yapo matamko yafananayo na “Ishi kwa imani”. Hata hivyo wapo wangapi wanaojua kwamba kuishi kwa imani ni maisha ya mwenye haki yaani maisha ya Mkristo? Hapa sijasema kwamba kuishi kwa kuziacha kabisa juhudi zetu za kimwili na mali tulizo nazo kwa kuzitegemea. Kile ni nacho kushauri kuacha kutumaini kwa akili yako yale yaliyo duniani kwa kuishi kwa imani. Sasa niaminije? Mwamini Mungu. Mungu hutenda kazi pale tunapo mwamini na kutafuta kile tunacho hitaji. Mwamini kuwa ndiye anaye jibu maombi na uwaamini viongozi wa kanisa pia. Jiunge na kanisa lake na umtumikie Bwana. Je unaamini? Yatupasa kuishi kwa imani kwa sababu ni wenye haki kwa binafsi.
Yatupasa kuachana na kile tunacho tumaini kwa mioyo yetu. Yatupasa tumwamini Mungu kutafuta na kupata bila kujali ugumu wa kazi yenyewe. Yatupasa kuishi kwa imani na kuwa naye. Ndipo hapo tutakapo tawala na Bwana na siyo kudhihakiwa na watu wa dunia. Mungu anasema kwamba “Waandaa meza mbele yangu machoni pa watesi wangu” (Zaburi 23:5). Kuwa na fidia kuu ni kuweza kubarikiwa mbele ya Mungu. Si kuishi kwa kulingana na maendeleo ya mazingira bali kwa imani.
Je, ulikwisha ishi kwa imani? Watu wengi wasio na idadi hawaja wahi kamwe kuishi kwa imani, lakini wapo wale walio kwisha onja matunda ya Mungu pale walipo sali na kuomba. Yatupasa kuona haya ya kiwepo katika maisha yetu mara kwa mara. Hii ndiyo njia ya mwenye haki impasayo kuishi. Tusitegemee vitu vya duniani, bali tumwamini Mungu. Ni maisha ya mwenye haki. Tuishi namna hiyo, ni kwa imani tu ndipo tutaishi na kupata baraka zote toka kwa Mungu.
 

Kile tunacho hitaji hasa mbele ya Mungu ni Imani.
 
Kuwa na imani inaweza kuonekana kuwa ni vigumu lakini ukweli ni kuwa, hili ni rahisi mno. Hakuna kinacho hitajika zaidi ya kumwamini Mungu. Yatupasa kumwamini Mungu tu. Watu hufikiri kwamba ni vigumu kumwamini Mungu, lakini si vigumu namna hiyo. Namwita baba yangu “Baba” na kuamini kuwa ni baba yangu kwa sababu yeye ndiye baba yangu wa kweli. Kwa yeye kuwa ni baba hakutegemei vile ilivyo imani yangu. Imani katika Mungu huanza kwa sehemu hiyo. Namwamini Mungu kwa nini? Kwa sababu Mungu wakati wote husimama na wenye haki akiwapenda na hata kuwa Baba kwao na Mwokozi. Pili ikiwa tuta mwamini yeye tutaweza kuomba tutakacho kama ilivyo mtoto amuombapo Baba yake atakacho. Mwisho Mungu Baba husikia na kujibu tutakacho. Kumwamini Mungu msingi wake hutokana na kuanza kwa uhakika wa mambo madogo kama hayo.
Yatupasa kuishi kwa imani kwa sababau Mungu ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Maisha yetu yote yanategemea imani zetu. Tunaokolewa kwa imani na kutunzwa na Mungu kwa njia ya imani. Ni imani ambayo ndiyo inayo turuhusu kusema “Bwana, ninakuamini Nitunze na tafadhali unihifadhi” Tutafanyaje ikiwa pale tutakuwa wadhaifu na hata kumwogopa shetani na vitisho vyoke? Yatupasa tumwamini Mungu huku tukisema “Bwana ninakuamini” Tunaweza kudhani visivyo na matokeo yake kunaswa na hata kushindwa na shetani. Kwa jambo hilo kwa kuwa tunaomba na kumwamini Mungu hukutukisema “Bwana tafadhali nihifadhi. Ninakuamini hakika.” Na kwa kuwa Mungu ndiye Baba yetu, yeye hututunza, Mungu kwa vyovyote yeye ndiye atutunzaye hata pale tunapo fanya maombi yasiyo faa mbele zake, kwa sababu yeye hutufahamu vyema. Jambo muhimu hapa ni kumwamini yeye. Ni rahisi. Hebu tumia imani Mungu akupayo na ndipo atakapo kuongoza toka imani hata imani. Ni upotofu ikiwa hatoamini, hata kuwepo kwa Mungu Tunaweza kuanza kuishi kwa imni ikiwa tunamwamini Mungu.
 

Toka imani hata imani
 
Warumi 1:17 inatuamba “Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani.” Tunapo itumia imani yetu mara kwa mara ndipo tunapo kuwa watu wa imani. Nataka uelewe hili, Mungu hawezi kuwepo kwetu ikiwa hatumwamini hata ikiwa yeye yupo. Unafikia imani hata imani pale unapo mwamini kwa dhati kwamba Mungu yupo na alituokoa.
Unapokuwa mtu wa imani, mambo yote ya Mungu huwa ni yako kwa imani. Kile Biblia inachosema katika Warumi 1:17 ni kwamba mwanzo na mwisho wa imani ni imani “Kwa maana haki ya Mungu imedhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani.” Hivyo tutaweza kuokolewa na kuwa watu wa imani pia ikiwa tutamwamini kuwa Mungu ndiye aliye tuokoa kamwe hatutoweza kuwa wana wa imani ikiwa hatutokuwa na imani. Mungu hujibu pale tunapo tafuta kwa dhati kile tunacho hitaji maishani huku tukimwamini yeye.
Kile Mtume Paulo alichokuwa akisema katika Warumi 1:17 ndiyo muhimu ingawa ni kwa ufupi Je, unaelewa sasa namna ya mwenye haki anavyoishi? “Mwenye haki ataishi kwa imani.” Imani bila shaka ni muhimu kwa mwenye haki, si kwa wenye dhambi.
Jambo la kwanza linalohitajika kwa wenye dhambi ni kuamini kwamba Yesu ni mwokozi. Hata hivyo sisi tulio zaliwa upya mara ya pili tunaweza kuwa na imani maishani. Je, tunahitaji jambo moja au mambo mawili tunapo ishi? Hapana yapo mambo mengi ya kufanya ikiwa ni kwa makini au kwa urahisi. Mwenye haki ataishi kwa imani kwa mambo yote. Je, unaelewa hili? Yatupasa kuishi kwa imani. Tumeokolewa kwa imani na kututunza dhidi ya hatari kwa imani. Tunapo omba kwa imani, Mungu hujibu. Yatupasa kuishi kwa imani na kuomba hata pale tunapo kuwa dhaifu. Kwa mambo yote, toka ndoa hata kuihubiri Injili. Tunahitaji imani. Tunapo ihubiri Injili kwa mtu fulani, imani hutuwezesha kusali kama vile “Mungu naamini umekwisha uokoa nafsi ile” Tunafanya yote kwa imani.
Hatutoweza kuihubiri Injili pasipo imani. Tutaweza kuihubiri Injili kwa imani tu. Watu huokolewa pale tunapo ihubiri Injili kwa imani. Je umekwisha wahi kuishi kwa imani? Watu huishi, pasipo imani huku wasijue ya kwamba imewapasa kuishi kwa imani hivyo kujikuta wakigonga mwamba wanapokutana na magumu. Huanza kutafuta pale wanapo ishiwa nguvu, hivyo mwishowe hukosa yote. Hawana uhakika na imani na hawako tayari kuishi huku wakikiri kuwa “siko tayari kuishi kwa sababu siwezi kuishi.”
Lakini mwenye haki ataishi kwa imani kwa pamoja na kwa hakika; pale anapo amini, kutafuta na kupata majibu. Mawazo yasiyo ya maana na kutoamini hutawala punde ikiwa hatutokuwa na imani. Ndipo tunaposhindwa kwenda pamoja na kanisa. Ni kwa namna gani tutaweza kutembea na Bwana bila imani? Je, kunalolote la kuamini katika mwili? Hakuna Tutaaminije? Hatutoweza kuwa na imani ikiwa hatumwamini Mungu. Twaweza kulifuata kanisa pale tunapo ishi kwa imani na kuishi huko ni kutokana na imani. Je unaona hilo? Je, unamwamini Mungu?. Sasa basi tafuta utakacho Mwamini Mungu na ndipo yote yata kwenda salama. Tatizo pekee ni kuelewa kwamba inatupasa kuishi kwa imani.
Namshukuru Mungu aliyetuongoza katika maisha yaetu yaliyo baki kwa imani.