Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 1-5] Waipingao kweli kwa uovu (Warumi 1:18-25)

(Warumi 1:18-25)
“Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na ouvu wa wanadamu waipingao kweli kwa ouvu. Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayo julikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyo onekana na tangu kuumbwa ulimwenguni yanaonekana na kufahamika kwa kazi zake, yaani uweza wake wa milele na Uungu wake, hata wasiwe na udhuru, kwa sababu walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru, bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu na ya ndege na ya wanyama na ya vitambaavyo. Kwa ajili hiyo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, wafuate uchafu, hata wakavunjia na heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anaye himidiwa milele. Amina.”
 

Je, ni kwa nini ghadhabu ya Mungu Imedhihirishwa?
 
Tunaweza kuona kwamba Paulo Mtume alihubiri Injili ile ile ambayo nasi leo tunaihubiri. Je, ni kwa nini ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa? Hukumu ya Mungu imedhihirishwa kwa waasi wote waipingao kweli kwa uovu, ikimaanisha kwa wale wote wenye dhambi na kuzuia ukweli kwa mawazo yao.
Paulo Mtume kwa bayana anasema kwamba ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kwanza kabisa kwa wale wenye kuzuia ukweli kwa uongo. Hawa ndiyo watakao hukumiwa na Mungu. Ghadhabu ya Mungu ita fanana je? Ghadhabu ya Mungu itadondoshwa juu yamiili na roho ndani ya jehanamu.
Tusidhani kwamba ni miili tu ndiyo itakayo hukumiwa kwa sababu watu pia nao wanaroho. Hivyo Mungu atahukumu vyote kea pamoja, yaani mwili na roho zao. Wapo wanao kwenda kinyume na haki, wakiwa na dhambi. Ghadhabu ya Mungu na hukumu yake imedhihirishwa kwao wote wenye dhambi walio ifanya mioyo yao kukwa migumu, wale wasio mwogopa Mungu.
Paul Mtume anasema katika Warumi 1:17, “Waadilifu wataishi kwa imani.” Pia anasema kuwa hukumu na ghadhabu ya Mungu hufunuliwa kwa wale ambao huzuia ukweli na dhambi zao.
 

Wasio amini wako chini ya ghadhabu ya Mungu.
 
Kwa ushawishi mkuu Mungu ameupa ulimwengu wokovu wa kweli. Ukweli na upendo wa Mungu umewekewa ushawishi ulimwenguni. Hivyo basi, hakutokuwa na sababu ya kuupuuzia ukweli na upendo wake. Mungu atauhukumu ulimwengu wa watu wasio amini Injuli ya kweli na kwa wale wote wasiyo iamini.
Hebu basi tufikiri juu ya watu ambao wao bado hawajapokea upendo wa ukweli wa Injili. Tunaona vile Mungu alivyo umba, kile kiitwacho maji, nyasi, miti, anga, ndege, nk. Ni kwa vipi vitu vyote hivi vimeweza kuwepo pasipo uumbaji wa Mungu? Biblia inasema “maana kila nyumba imetengenezwa na miti, ila yeye aliye vitengeneza vitu vyote ni Mungu” (Waebrania 3:4). Je, si kosa kwao kuto amini juu ya Mungu na neno la kweli litokalo kwake?
Hivyo, ipo sababu kwa watu wasio amini neema ya Mungu ya msamaha wa dhambi katika kuhukumiwa na Mungu. Wao husisitiza kanuni za kihistoria juu ya kuwepo kwa mwanadamu wa kwanza atokanaye na sokwe. Wao hushikilia kwamba ulimwengu kwa asili ulijitokea wenyewe tu, kwa kanuni iliyoitwa “mlipuko mkuu”, (Big Bang) zaidi ya miaka bilioni 15 iliyo pita, na ndipo basi aina fulani ya viumbe vilijitokeza na kuanza kuishi. Husema asili ya ukweli wa uhai ulibadilika na kuingia hatua ya samaki, wanyama na hatimaye binadamu. Ikiwa kanuni hii ni kweli, basi wanadamu hatimaye wengeliweza kubadilika na kufikia hatua nyingine tena ya maisha kwa maumbo mengine baada ya miaka elfu 1 au 2.
“Kwa sababu mambo yake yasiyo onekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana na kufahamika kwa kazi zake, yaani uweza wake wa milele na Uungu wake, hata wasiwe na udhuru” (Warumi 1:20). Watu hubisha na kukataa kuwepo kwa Mungu, ingawa huweza kubainisha kwamba Mungu yupo pale wanapo kumbana na maajabu na mambo ya kushangaza yahusuyo mazingira ya asili. Wasio amini wako chini ya ghadhabu ya Mungu. Wengi hawamtukuzi Mungu au hata kumshukuru, hivyo kupotea kwa uzushi wao. Mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza, wakijinenea kuwa wenye hekima wakipumbazika na kuubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu na ya ndege na ya wanyama na ya vitambaavyo. Kwa sasa ghadhabu ya Mungu inawasubiri watu hawa wale wote ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili wapo chini ya hukumu ya Mungu haijalishi ikiwa wana mwamini Yesu kwa namna zao au la.
 

Mungu amewaacha wafuate uchafu.
 
“Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana na heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa Amina. Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu hata wanawake wakabadili matuizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili, wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi yamke ya asili wakawakiana tamaa wanaume wakayatenda yasiyo pasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao” (Warumi 1:24-27).
Kifungu hiki kinatueleza nini? Mungu huwaacha watu kuabudu na kutumikia viumbe wakitenda dhambi watakavyo. Pia akiwaachia kwa shetani. Mungu huumwacha shetani afanye atakalo. Hivyo yatupasa kumwamini Mungu na kuokolewa hara ipasavyo. “Hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili, wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke ya asili wakawakiana tamaa.” Hii ni sawa na kupinga juu ya Mungu na ndicho kisababishacho UKIMWI.
Mungu ameweka matumizi ya asili. Mwanamume kuishi na mwanamke. Hata hivyo, ukweli ni kwamba wanaume wana uhusiano wakijinsia na wanaume wenzao, na wanawake kwa wanawake kuonyesha kwamba wamepingi matumizi ya asili ambayo Mungu amewapa. Kitabu cha Warumi kiliandikwa takribani miaka 1900 iliyo pita. Paulo Mtume alitabiri kwamba wale watakao acha matumizi ya kawaida ya kujamiiana watalipia adhabu kwa tendo hilo lisolofaa. Maneno ya Mungu yanapatikana na katika ukweli huo kwa nyakati hizi. Twajua ya kwamba UKIMWI umetapakaa hasa kati ya wanao jamiiana wa jinsia moja.
Ni sawa kwao kulipia gharama ya adhabu kwa tendo hilo la kujamiiana. Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa dhidi yao watu wenye kubadilisha matumizi ya asili katika tendo la kujamiiana. Wanastahili kupokea adhabu ya UKIMWI. Gonjwa hili hakika limesababishwa pamoja na mambo mengine ni kuto kumwamini Mungu zaidi. Mungu aliwaachia wasio na imani akili isiyo ya kistaarabu. Kwa maneno mengine, hakika hii ni laana ya Mungu mwenyewe.
 

Wako kinyume na haki ya Mungu.
 
Watu wasiopenda juu ya Mungu katika fikra zao ni kama ifuatavyo; “Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wemejawa na husuda na uuaji, na fitina na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasio watii wazazi wao; wa siona ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema, ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao” (Warumi 1:29-32).
Ni mambo gani “wanakubaliana nao wayatendao”? Watu walio kinyume na Mungu huwatendea nini watu wenye haki? Huwashitaki wenye haki kwa kusema “Ninyi ni wazushi” Wenye haki hushitakiwa kwa sababu ya haki zao baada ya kumwamini Yesu. Wao ni watu wenye heri.
Watu huwasikitikia wale wanao tanga tanga kimwili. Hata hivyo twaweza kuona wakikanusha na kuwazuia wengine kumwamini Yesu na kuwa wenye haki kwa njia ya msamaha wa dhambi. Hii ni sawa na kuishi wakiwa mfano wa watumishi wa dhambi kwa sababu hawamwamini Mungu wala kutii neno la kweli.
Kwa hivyo, wasio amini na shetani hutuambia kwamba si lazima kuwa mkamilifu kiutakaso au hata kusamehewa kiukamilifu dhambi, ingawa kwa upende mwingine wao huku elekeza kumwamini Yesu Kristo. Wasio amini na wasio tii hufikiri na kusema kwamba imewapasa kumwamini Yesu huku wangali na dhambi moyoni mwako. Na hii hatimaye watakwenda jehanamu. Watu hufarijika pale wanapo ona wana mwamini Yesu wakiwa ni wenye dhambi. Wale wasio fahamu huku wakiendelea kumwamini Mungu, ingawa nao ni Wakristo, hawatoweza kumpokea Mungu kwa kupitia ufahamu wao na kupinga kwao. Wao huwapinga wale wenye haki wa Mungu. Humwabudu shetani na dhambi zake zote. Wale ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili, ingawa wana mwamini Yesu ndivyo walivyo kwa jinsi hiyo. Wanao mwamini Yesu huku wakiwa na dhambi mioyoni mwao ndiyo wasiotii neno la kweli la Mungu na hivyo kuwapinga wale Wakristo wote walio zaliwa upya mara ya pili, ambao wamepata ondoleo la dhmbi na kupokea utakaso kwa njia ya kuamini ukweli wa Yesu Kristo.
 

Wale ambao hawajazaliwa upya ndiyo wanao wapinga walio zaliwa upya.
 
Paulo Mtume anasema katika Biblia ya kwamba, “ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kwa watu wote waipingao kweli kwa uovu.” Pia anasema kwamba “hukumu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu.” Yote yanafanyika kulingana na ukweli. Ukweli ni ule wa Bwana aliye zifuta dhambi zetu zote. Hukumu ya Mungu imedhihirishwa kwa wale wote walio kinyume na ukweli huo huku wakiuziwa. Tunajifunza kwa njia ya neno la Mungu ya kwamba wote wenye kumwamini Yesu, ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili wata kuja kuhukumiwa na Mungu. Mungu atakuja kuwahukumu wale wote ambao hawajaokoka ingawa wanamwamini Yesu kwa njia zao.
Wanaoamini huku wakiwa bado hawajaokoka huupendelea kuwasengenya na kuwazushia wale ambao wamezaliwa upya mara ya pili, huku wakiwa na mioyo iliyo jawa na chuki dhidi yao. Hawa watakwenda jehanamu. Mungu atawafutilia mbali kwa kwenda motoni. Wenye dhambi wanao wateta wenye haki walio samehewa dhambi wata hukumiwa. Je, unaona ninachosema? Imetupasa kuwasikitikia wanao mpinga Mungu kwa dhambi zao, huku wasijue ya kwamba wako kinyume naye, huku waki teta “inashangaza kwa hawa kusema hawana dhambi. Ni jambo la ajabu.”
Hukumu ya Mungu imedhihirishwa kwa wale walio kinyume naye kwa uovu wao. Watu hawa huyafurahia mambo hayo wayafanyayo. Wao hukubaliana katika kuteta na kusingizia, na huona kuwa ni vyema Wakristo ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili kuwashutumu wenye haki. Ni wanafiki wawachukiao wenye haki wakijigamba na kupanga uovu kwa pamoja. Je, wajua jinsi ile wanavyo panga uovu? Hutenda movu kwa njia ya kuungana wao kwa wao. Huwapinga wenye haki kwa kauli mbiu zenye maneno mazuri kama vile “Hebu na tumwamini Yesu kwa njia iliyo sahihi. Tuwe na aina nzuri ya imani. Tuwe nuru kwa ulimwengu.” Hutenda dhambi hizi kwa kuungana wao kwa wao kwa sababu si ajabu kutenda dhambi.
Hivyo, Mungu anasema katika Zaburi 2:4 “Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka” kwa sababu wafalme wa dunia wako kinyume na Mungu. Husema “Oh! Inachekesha sana. Hakuna kitakacho nitokea haijalishi vile unavyo nipinga. Ninyi watu mnanilazimisha kunihonga ili Mungu anitie hukumuni.” Mungu anasubiri muda wa hukumu kwa kuwa ni siku ya dhihaka.
 

Wanao wahukumu wenye haki wata hukumiwa na Mungu.
 
Wale walio kinyume na ukweli wa Mungu na ambao bado hawajazaliwa mara ya pili hutenda dhambi. Wale ambao wamezaliwa upa mara ya pili wao pia wana mapungufu katika miili yao. Ingawa upo utofauti wa ki msingi kati ya watu hawa. Tuna mwamini Mungu na kweli tumekwisha pokea msamaha wa dhambi kwa kupitia Mungu. Wengine hawamwamini Mungu kabisa. Watu hawa walio kinyume na haki ya Mungu na ukweli wa Mungu, “Kwa hiyo wewe mtu uwaye yote uhukumuye huna udhuru, kwa maana katika hapo umhukumuyo mwingine waji hukumu mwenyewe kuwa na hatia kwa maana wewe uhukumuye unajifanya yale yale” (Warumi 2:1).
Paulo Mtume aliwaambia Wayahudi na Wakristo ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili huku waki shikilia sheria. Huwahukumu wengine huku waki sema “Usiue, usizini, usiibe, na umtumikie Mungu pekee hali huku wao wenyewe hawaifuati sheria.” Ni Mungu pekee ndiye mwenye hukumu ya haki na pi watoto wake walio zaliwa upya mara ya pili ndiyo watakao toa hukumu kulingana na neno la Mungu.
Watu aina hii ndiyo imewapasa kuhukumiwa kwa sababu wao huwahukumu wenye haki vile isivyo. Mungu atawahukumu hawa wote ambao bado hawaja zaliwa upya mara ya pili, hii ni kusema kwamba ni Wayahudi na wale Wakristo wenye kufuata sheria. Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kwao wale wote wenye kuishi maisha ya kidini huku wakizigatia sheria wakati hawajazaliwa upya na hao wenye kuamini kuwa watakwenda mbinguni ikiwa watatenda yale Mungu anayo agiza katika torati. Mtu wa imani ni yule ambaye ni mwenye haki baada ya kumwamini Yesu Kristo. Yatupasa kuwajua wale wanaomwamini Mungu na kuishi maisha ya uadilifu pasipo kuzaliwa upya mara ya pili huku wakiwa hukumu wenye haki kwa kutegemea vigezo vyao vya kibinadamu.
Hata hivyo, Mungu kwa hakika atawahukumu. Wao hawajui kwa kuwahukumu wenye haki wanaji hukumu wao binafsi kwa vigezo vyao. Enyi mnao wahukumu wenye haki pasipo ninyi kuwa na msamaha wa dhambi mkiwa na imani batili bila ya kupokea neema ya Mungu, je, mnafikiri mtaweza hapo baadaye kuikimbia hukumu ya Mungu? Watu hawa watakuja kuhukumiwa na Mungu.
 

Hukumu ya Mungu ni ya kweli.
 
“Nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu ya wafanyao hayo” (Warumi 2:2). Tuna uhakika kwamba hukumu ya Mungu inatokana na ukweli dhidi ya wale wote wenye kuwahukumu wengine huku wao binafsi hawajazaliwa upya mara ya pili, ingawa wana mwamini Yesu. Yatupasa kuelewa kwamba Mungu huwatupa watu jehanamu na kuwa hukumu watu kulingana na ukweli wake.
Yeye huwatupa wote wenye dhambi jehanamu kwa sababu ukweli wake kuwa ni sahihi na hivyo hukumu hiyo imelenga mahala pake. Kwenda au kutokwenda kwa mtu jehanamu, hili halitegemei fundisho la Kanuni ya Kuchaguliwa kabla linalo hubiriwa kwamba “Mungu huwapenda baadhi, lakini pia huwa chukia wengine”. Ukweli ni kwamba, Mungu aliwachagua watu wote katika Yesu Kristo kabla ya misingi ya ulimwengu (Waefeso 1:4).
Yeyote aaminiye kwamba Yesu Kristo alifutilia mbali dhambi zake zote basi ndiye atakaye pokea msamaha wa dhambi. Hili Mungu alilichagua kabla. Hivyo wale wote ambao bado hawajazaliwa upya ingawa wana mwamini Yesu wata kwenda motoni. Watakwenda jehanamu kulingana na hukumu ya Mungu na hili ndilo kweli.
Hukumu ya Mungu inayo wapeleka wenye dhambi jehanamu ni ya kweli. Kwa nini? Kwa sababu wameukana upendo mkuu wa Mungu na hata kutopokea wokovu wake pasipo kumwamini. Ni sawa kwake kuwapeleka jehanamu wale wasio zaliwa upya kulingana na ukweli wake.
Wengine husema, “Kwa nini Mungu hukuni hubiria Injili mimi?” Je, hili ni kweli? Mungu ameihubiri Injili kwako mara nyingi. Pokea wokovu kwa kufungua macho yake. Yapo makanisa machache ambayo yana hubiri Injili ya kweli hapa duniani. Hata hivyo waweza kukutana na ukweli ikiwa unautafuta kwa moyo wako wote. Kwa upande wangu niliutafuta kweli! Mara nyingi nilipo maliza mahubiri wakati nilipo kuwa bado sijazaliwa upya mara ya pili, nilikuwa nikisali “Oh, Bwana mimi ni mwenye dhambi mbele zako, ingawa ni mimelihubiri neno lako kwa watu hawa. Niliyo waambia ndiyo niliyo iambia nafsi yangu pia. Mimi ni mwenye dhambi. Tafadhali ukutane nami. Tafadhali niokoe.”
Sijui ni mara ngapi nilijarbi kutafuta ukweli huu. Mungu anapenda kukutana na yeyote yule ambaye anamtafuta. Yeye anataka pia kuwakomboa hata wale wasio mtafuta, “Nitawaita watu wangu wale wasio kuwa watu wangu. Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu. Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu” (Warumi 9:25). Mungu anasema kwamba yeye ndiye Mwokozi wetu aliye kuja ulimwenguni kutuokoa. Watu wanao mtafuta Mungu kwa dhati hakika wataweza kukutana naye, Wapo baadhi ambao hawajamtafuta Mungu lakini wanapata fursa ya kukutana na Bwana pale wahubiri wa Injili wanapowajia na kuwahubiria. Baadhi hupendelea kuisikiliza na wengine hawapendelei. Watu watakao kwenda jehanamu wataishia huko kwa sababu waliikataa habari njema.
Nihaki kwa wale wenye kustahili jehanamu kutupwa huko kutokana na kipimo cha ukweli wa Mungu. Wale wenye kustahili kwenda Mbinguni hufika huko kwa kumwamini Yesu kwa kigezo kilicho sahihi ingawa hawana cha kujivunia nafsi ni mwao. Yote haya hutokea kwa hukumu ya kweli ya Mungu.
Mungu huwatupa watu jehanamu na wengine kuwapeleka Ufalme wa Mbinguni kwa namna ya uchaguzi usio zingatia upendeleo wowote kwa baadhi ya watu. Hivyo yeye huwahukumu kwa sheria ya haki katika ukweli. Hivyo yatupasa kuihubiri Injili. “Wewe mwenyewe je, wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?” (Warumi 2:3-4).
 

Tayari Yesu alikwisha kuzifuta dhambi zote za ulimwengu kwa upendo wake.
 
Paulo Mtume anasema kwa wenye dhambi, Wayahudi na wale Wakristo wenye kufuata sheria za torati, ambao hawajaupokea upendo wa Yesu au hata kuzaliwa upya, kuwa ndiyo watakao hukumiwa siku ile ya mwisho na kwenda jehanamu. Lakini Injili ni nini? Katika Warumi 2:4, Mungu anasema “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake usijue ya kuwa wema Mungu wakuvuta upate kutubu?” Upendo wa Mungu umeonekana kwa watu wote na kudumu.
Hukuna aliye wekwa kando ya neema hii ya wokovu wa Mungu. Yesu ametutakasa kwa ukamilifu. Je, amefuta dhambi zile za asili tu na kutusamehe zile za kila siku pale tunapo fanya sala za toba na kusamehe wa? Hapana. Bwana amekwisha zifuata dhambi zote za ulimwenguni mara moja na kwa wakati wote. Wapo wale walio kinyume na Mungu, wanye kupuuzia wema wa upendo wa Mungu wakisema “Yesu alituokoa kwa njia gani? Nitawezaje kusesma sina dhambi ingawa bado ninaendelea kutenda dhambi kila siku? Ni upuuzi mtupu! Mungu atewezaje kufuta dhambizote hali bado ninaendelea kutenda dhambi, hata ikiwa yeye ni Mwokozi na Bwana Mungu?”
Watu hufikiria kulingana na mwili kama huu, lakini Mungu tayari ameosha dhambi zote za ulimwengu na upendo wake. Bwana alikuja ulimwenguni na akafuta dhambi zetu zote. Bwana anajua udhaifu na udhaifu wa wanadamu (Mwili hauwezi kutenda dhambi tena na tena). kwa hivyo, alifuta dhambi zote za ulimwengu mara moja na kwa Ubatizo wake na kumwaga damu yake msalabani. Bwana anajua udhaifu wa mwili vizuri. “Nimekuokoa kwa sababu nilijua utafanya dhambi tena na tena hadi utakapokufa.”
Bwana aliosha dhambi za ulimwengu. Bwana ametukubali sote kwa kutukomboa. Bwana alilipa mshahara wa dhambi kwa wadhambi na akawatakasa kwa nguvu na uadilifu wake (Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizi kwenye Mto Yordani). Bwana alituruhusu kubarikiwa, kuwa watoto wake na kutuwezesha kwenda kwenye Ufalme wa Mbingu kwa kulipa malipo ya dhambi zetu na uzima wake (damu). Bwana aliwageuza wenye dhambi kuwa watoto wake waadilifu.
 

Wasioamini lazima watubu na kugeuza mioyo yao kwa Bwana
 
“Au je! Unadharau utajiri wa wema wake, uvumilivu wake na uvumilivu wake, bila kujua kuwa wema wa Mungu unakuongoza kutubu?” Mungu awahukumu wale wanaodharau na kukataa wema, utajiri, uvumilivu na uvumilivu wa Mungu kwenda kuzimu. ni hakika kwamba Yesu Kristo aliosha dhambi zote za ulimwengu, na kwamba injili imeenea ulimwenguni kote. Walakini, watu bado huenda kuzimu kwa sababu hawaamini ndani. Yesu alituokoa kwa kuosha dhambi zetu zote kutuzuia kwenda kuzimu, hata ikiwa tunataka kwenda kuzimu kwa kudharau uvumilivu na utajiri wa wema wake. Hata kama tungetaka kwenda kuzimu, alituokoa.
Kwa hivyo lazima tuamini katika maji na damu ya Yesu Kristo ili kuokolewa. amini, na uokole. Wale wanaodharau upendo na wokovu wa Mungu wataenda kuzimu. Kuzimu ni mahali Mungu amewaandalia wale wanaodharau neema ya wokovu wake na utajiri wa wema wake. Makafiri tayari wamenunua tiketi zao kuzimu. watu wanaopangwa kwenda kuzimu lazima watubu na kugeuza mioyo yao kwa Bwana. Lazima pia uende kwa Ufalme wa Mbingu isipokuwa una imani katika injili ya kweli.
 

Watu huenda jehanamu kwa kuukataa upendo wa Mungu.
 
“Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ili ya haisra na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu” (Warumi 2:5). Wenye mioyo ya huzuni na watu wasio tubu watakwenda jehanamu. Baadhi ya watu watakwenda jehanamu kwa sababu wamekataa upendo mkuu wa Mungu. Wenye dhambi wenye kukataa ukweli kwa kuifanya mioyo kuwa migumu huku wakifuata mawazo yao watakwenda motoni, kutokana na mshahara wa dhambi ni mauti. Wale wenye kukataa kupokea upendo wa Mungu na kuendelea kufanya sala za toba ilikufikia hatua ya utakaso wata kwenda jehanamu. Ghadhabu ya Mungu kushikiliwa hadi siku ya ufunuo na hukumu ya Mungu ni kutokana na upendo wa Mungu kukataliwa kwa sasa.
Katika mpango wake wa ukombozi, Mungu aliamua kuokoa wenye dhambi. Mungu alimtuma mwana wake ili kutuokoa na kututakasa. Hata hivyo wenye dhambi hawaja lipokea hili wameifanya hasira ya Mungu kufikia kipimo cha juu na wata hukumiwa siku ya hukumu na ufunuo wa hukumu ya haki. Hukumu ya haki ya Mungu ni kuwapeleka wale wote wenye dhambi mioyoni mwao jehanamu.
Kwa nini? Kwa sababu Mungu alitakasa dhambi zote za ulimwenguni na kumfanya kila mtu kuokolewa kwa imani. Wasio amini hakika watakwenda jehanamu. Ni wenye mioyo migumu na wenye kujitolea kwenda jehanamu na wengine hupenda kwenda Ufalme wa Mbinguni pasipo kufuata taratibu za Mungu na mamlaka yake. 
Hata hivyo haipaswi kamwe kuwa hivi. Mungu ameweka jehanamu kwa ajili ya wale wote walio wagumu mioyoni wakikataa upendo wake na ukweli wake ili kwamba kuwe na sehemu wanayo stahili kwenda.
Biblia inasema kwamba, jehanamu ni mfano wa moto uwakao au ziwa la moto. Wamo funza watokao waandama wale wote wenye dhambi. Watu hawa wataweza kulia. “Hapana, Hapana sipapendi mahala hapa”, lakini Mungu atasema “Nilikwisha takasa dhambi zenu zote za duniani, lakini wewe ulisema kwamba hukujali ikiwa kama ulikuwa ni mwenye dhambi. Hivyo sasa ninakupa hawa funza kama zawadi kwako na rafiki kwako kwa sababu hukupenda msamaha wa dhambi” watajibu, “hapa Bwana, sipendi namna hii.”
“Wewe ndiwe uliye taka hivi ingawa sasa hupendi, Mimi ni Bwana wa haki. Nakupa kile ulicho hitaji Ninawapa jehanamu kwa wale wote wenye kupenda kuwa na dhambi mioyoni mwao.” Hii ndiyo hukumu ya haki kwa Mungu. Ingawa wanadamu hutenda dhambi hali wakiishi katika ulimwengu huu, lakini bado hawawezi kudharau wokovu wa Mungu ambaye ameutakasa ulimwengu kwa dhambi zote.
Watu huenda jehanamu kwa sababu ya mioyo yao migumu. Imetupasa tusiwe na mioyo migumu mbele ya Mungu. Yatupasa kuamini kwamba tayari yeye amekwisha takasa dhambi zote za duniani. Yakupasa uamini hivyo hata ikiwa ni vigumu.
 

Mungu anatuambia kuwa tayari amekwisha tupenda.
 
Mungu anatuambia tayari amekwisha tupenda “Nimekwisha takasa dhambi zenu zote”. Imewapasa kuamini ukweli huu. Mungu anaposema kwamba aliumba mbingu na nchi, yatupasa kuamini hili kwa sababu ya neno la Mungu lililo la kweli. Imani huanzia pale unapo amini neno la Mungu. Watu huamini jambo fulani pale tu wanapo lielewa jambo hilo kwa akili zao ndogo, na kutoamini ikiwa hawatoweza kulielewa. Wasioamini ambao hawamwamini Mungu katika wokovu wa wenye dhambi wata kwenda jehanamu. Ni wao ndio walio dhamiria kwenda jehanamu.
Yupo Mkristo fulani maarufu aliye tamba hadharani akisema, “Nakiri mbele ya Mungu kwamba mimi ni mwenye dhambi mapaka siku ya mwisho wa uhai.” Alikufa na kwa hakika alikwenda jehanamu. Yeye alimwambia Mungu “Natamka rasmi kwamba mimi ni mwenye dhambi mbele ya Mungu na kamwe sintoweza kuwa mwenye haki mbele yako” nakuendelea kuwa mwenye dhambi hadi mwisho wa muda katika kifo chake. Alikataa upendo wa Mungu na ukweli wake hata siku ya mwisho. Ndipo Bwana alipomwambia “Wewe ni mwaminifu kwa imani yako binafsi, ni haki kwako kwenda jehanamu kulingana na imani yako. Nakupeleka huko kwa sababu kamwe wenye dhambi hawatoweza kuingia ufalme wa Mbinguni.”
 

Kama ningeliamini.
 
Yule mtu aliyesema “Nina kiri kwakamba mimi ni mwenye dhambi hadi mwisho wa uhai wangu”, hatimaye alikwenda jehanamu. Hata Mungu hawezi kuwasaidia watu wa ina yake. Si kwamba alitamka kwamba yeye ni wenye dhambi tu ijapokuwa alikua hatarini kuishia jehamamu siku za usoni, bali pia waliwafundisha hili na wengine walio mwamini “Sisi ni wenye dhambi hadi siku ya mwisho wa uhai wetu na tutakapo simama mbele ya Mungu.” Hivyo waumini wengi nao pia hufuta njia hizi za kidini. Mungu alisema kwamba wenye dhambi watakwenda jehanamu. Kwa sasa Wakristo wasio na idadi hufuata mafundisho haya kwa wakati huu katika Ukristo. Mungu alisema kwamba wale wenye dhambi watajutia milele, wakisagameno katika moto wa jehanamu, wakisema “kama ningeliamini, hakika kama tu ningeliamini hilo.”
“Kama ningeliamini ukweli wa kwamba Yesu alikwisha safisha dhambi zangu zote kwa kuachana na fikra zanga, ningeliweza kuingia ufalme wa Mbinguni.” “Kama ningeli amini, tu!” Wapo watu wengi watakao sema maneno ya namna hii huko jehanamu. Watasema “Kama ningeli amini, kama ningelipokea ukweli huu, ningeliweza kuwa mwana wake. Kwa nini niliufanya moyo wangu kuwa mgumu?”
Sisi wenye haki tutamuuliza Mungu kwa wakati huo, “Bwana, tafadhali hebu tuonyeshe vile wenye dhambi walivyo kwa sasa. Kwa maana alituhukumu sisi wenye haki”. Ndipo atakapo jibu “Hapana si vyema kwenu watoto wangu kwa sababu mioyo yenu itasononeka baada ya kuona mateso yaliyomo kwao. Lakini je, mngependa kweli kuona watu muwajuao wakiteseka?” “tafadhali japo kidogo tu” Bwana ataweza kutuonyesha wakati huo ujao kwa sababu ya ukarimu wake. Hivyo hebu tusema kwamba tutaona. Patakuwemo na vilio vingi vikisikika “Kama ningeliamini, kama ningeliamini”. Ndipo tutakapo baki na mshangao na kusema “Kelele hizi zote ni za nini?” Wanaume na Wanawake katika moto huo wakiimba wimbo kujutia “Kama ningelijua hakika, kama ningeliamini”.
Wenye mioyo migumu watakwenda jehanamu endapo hawato simamia yaliyo ya kweli. Kwa hakika tunahitaji moyo wa kusimamia imara kwa mambo ya kweli. Mtu asiwe mwenye kushindwa kutoa uamuzi. Yatupasa kuwa wenye kusimamia mambo katika njia iliyo sahihi na kuondolea mbali msimamo huo pale inapo hitajika.
 

Mungu ndiye atakaye mlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
 
Mungu ndiye “atakaye mlipa mtu kwa kadiri ya matendo yake, wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele” (Warumi 2:6-7). Mungu humlipa kila mtu kulingana na matendo yake na kumhukumu pia. “Kulipa” maana yake “kipato/mshahara kulingana na matendo.” Ni mtu wa aina gani asimamaye imara akiendelea kutenda mema akitazamia kuupata utukufu, heshima na uzima wa milele? Ni yule anaye amini wokovu kamili wa Yesu.
Wapo watu wengi ulimwenguni, lakini Mungu amewapa uzima wa milele kwao wale wasimamao imara katika haki na kuamaini ukweli wake bila kujali kile watu wasemacho. Mungu hutoa utukufu wa Ufalme wa milele kwa wale watakao penda kuwa wenye haki na kutamani kuishi maisha ya furaha milele. Huendelea kutenda mema na kutafuta utukufu, heshima na uzima wa milele; wakitaka kuwa wana wa Mungu. Wataendelea kuvumilia na kutenda mema na kuyafuata na kuyatekeleza yaliyo ya haki kwa Mungu. Mungu amewapa watu hao uzima wa milele. Yeye ndiye aliye wawezesha kuishi milele huku akiwafanywa kuwa wana kwake. Wana wa Mungu ni miungu katika Ufalme wake.
“Na wale wenye fitina, wasiotii kweli bali wakubalio dhuluma wata pata hasira na ghadhabu” (Warumi 2:8). Maneno, “Na wale” linamaanaisha jumuia ya watu walio kinyume na barak. Hasira na ghadhabu ya Mungu huwapata wale wote wasio tii ukweli. Mungu huwatosa jehanamu wale wote wasio zaliwa upya mara ya pili na wasio tii kweli, wakaidi na wapenda ukorofi. 
Katika historia yote ya Korea mababu zetu walifanyiana ukaidi na ukorofi baina yao katika maswala ya kisiasa. Jamii iliyo ongoza ndiyo iliyo amua ni nani atakaye kuwa mfalme. Ilipotokea mwana familia wa ukoo wa Lee kuwa mfalme basi watu wote wa ukoo huo watawekwa katika daraja la juu katika jamii huku wengine wakifukuzwa au hata kuteswa. Lakini ikiwa utawala utabadilika na kuwa kwa familia ya Kim, ndipo kila jambo litabadilika kabisa. Watu hufanya magombano na ukorofi kwa ajili ya faida zao na si kutafuta haki kwa ajili ya faida zao.
Ukristo wa nyakati hizi nao unafanana kwa jinsi hii. Hufanya madhehebu na makundi. Kwa ajili gani? Ili kutotii ukweli wakiwa kwa pamoja. Husema vile isivyo, kwamba wao ni wenye dhambi, ingawa Yesu alikwisha safisha dhambi zote za duniani. Hujifanya kuwa ni wenye haki na walio okoka, lakini hawaitii ile kweli. Huwashutumu wenye haki kuwa ndiyo wazushi, wakisema kwamba imewastahili wao kuwa wenye dhambi. Bwana anasema kwamba wenye dhambi ambao ndiyo faraka dhidi ya wenye haki ndiyo wakosaji na hivyo imewapasa wote kwenda jehanamu.
Wale wenye kuishika ile kweli na kumtii, Mungu ndiyo wenye kulikubali neno la Bwana. Sisi wenye haki tunaamini hukumu ya Mungu kuwa ni ya kuendana na ukweli.
 

Je Madhehebu ya Kikristo yataweza kutupeleka Mbinguni?
 
Madhehebu kamwe hayatoweza kutupeleka Ufalme wa Mbinguni. Mke wangu aliwahi kumkemea mama mkwe wake kwa ukali pale alipomwambia “Dhehebu lako halitoweza kukupeleka Ufalme wa Mbinguni”. Kusema kweli sijui kwa nini mama yangu alichukia sana hata mpaka leo. Je, unadhani taasisi za kidini zitaweza kuwapeleka watu Ufalme wa Mbinguni? Kwa binafsi tunaokolewa na kuingia Ufame wa Mbinguni kwa kuamini neno la Mungu. Je, dhehebu la kanisa la Presbeteriani litaweza kumfikisha mtu Ufalme wa Mbinguni? Je, Kanisa la Utakatifu nalo? Je, Kanisa la Wasabato nalo? Hapana. Tunaingia Ufalme wa Mbinguni pale tu ikiwa tutaamini msamaha wa dhambi ambao Yesu aliutayarisha kwetu.
 

Yatupasa kushikamana na Kanisa la Mungu.
 
Paulo Mtume bila shaka aliwatenganisha wenye dhambi ambao wengelielekea jehanamu na wale wenye haki ambao wataingia Ufalme wa Mbinguni kati ya Wakristo wote. Injili iko sawa kwa yeyote, Myahudi, na Myunani kwa pamoja. Hapa Wayunani husimama badala ya watu wa Mataifua na Wayahudi ndiyo Waisraeli. Mungu huangalia mtu mwenye kuamini neno lake kwa moyo wake. Je, unaamini kwamba Yesu ni Mungu? Je, unaamini kwamba Yesu ndiyo Mwokozi? Twaweza kwenda Ufalme wa Mbinguni pale tu tutakapo mwamini Yesu ndiye aliye zibeba dhambi za ulimwengu kwa ubatizo wake. Yatupasa kuamini hivyo na si kwenda kinyume. Roho Mtakatifu aliye ndani yetu hutukinga katika kuikana imani yetu na kutusaidia katika kuwashinda maadui zetu pale hatari inapo tukabili. Yatupasa tuwe waangalifu.
Katika biblia upo mfano wa aina nne za mashamba, kati ya mashamba hayo yapo yale yanayowakilisha wale masio weza kuokolewa. Mbegu zilizo pandwa katika mashamba hayo zilikufa punde zilipochipua. Tukio kama hili ni sawa na kuwa mbegu iliyo kufa. Ndipo sasa je, tutaweza kuendelea kuwa na imani pale Bwana atakapo tupa nguvu ya kuvumilia magumu yoyote na kutupa tatizo kwa kila ugonjwa wa kiroho tukishikamana katika mzabibu wa kweli.
Kanisa la Mungu ndiyo mzabibu. Bwana hutupatia baraka, uponyaji na imani katika kuvumilia mateso pale tunapo shikamana na Kanisa la Mungu. Lakini nini kitakacho tokea kwetu ikiwa hatushikamani katika mzabibu? Tutakufa haraka. Moyo wa mwenye haki hautoweza kusimama dhidi ya mashambulizi ya shetani na waweza kuugua ikiwa bila ridhaa yao hawatoungana na kanisa ingawa wataweza kuwa na uwezo na nguvu binafsi. Je, unaona hili? Hatua kwa hatua wataanguka na kuwa wasio faa siku hadi siku. Biblia inasema “Ninyi ni chumvi ya dunia lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu” (Mathayo 5:13).
Hata wenye haki hawato kuwa na maana ikiwa wataishi mbali na kanisa. Wataweza kutia nuru na kubarikiwa pale wanapo shikamana na Kanisa. Ila wataweza kuangamia ikiwa wataachana na kanisa na kushindwa kusimama dhidi ya dunia pale wanapo potea kutokana na kuliacha Kanisa. Mpaka lini utaendelea kukumbatia imani yako? Mpaka lini utaendelea kusimama kinyume na kanisa la Mungu? Hata watumishi wa Mungu hawato endelea kukuvumilia. Hata hivyo ikiwa tutashikamana na mzabibu wa kweli, watu wa nyumba yetu nao wataokolewa, na hivyo wengi kuweza kuwa na msamaha wa dhambi kwa kupitia kwetu. Je, Ruthu aliishia wapi baada ya kufuata mapenzi ya mwili? Alikwenda Sodoma. Aliishi kwa raha katika mji huo. Nini matokeo yake? Aliangamia. Biblia inasema kwamba kizazi chake chote Ruthu kiliangamia. Wamoabi na Waamori walitokana na uzao wa mabinti zake.
Kwa nini walikuwa ni kizazi kilicho kuwa Kinyume na Mungu huku wakiwa wanazaliwa na mtu mwenye haki, Ruthu? Ni kwa sababu yeye Ruthu alijitenga na kanisa. Sababu yangu kutojali pale nyakati ngumu zinapojitokeza ni kwamba Mungu amelijenga kanisa lake. Mungu hulibariki kanisa pale wenye haki wanapo shikamana kwa pamoja na kuchungwa na Bwana wa kanisa kwa kila moja. Hii ndiyo ahadi na uhakika kwetu.
“Kwa kuwa wote walio kosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria na wote waliokosa, wenye sheria watahukumiwa kwa sheria. Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu bali ni wale waitendao sheria watakao hesabiwa haki kwa maana watu wa mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Hao waionyesha kazi ya torati iliyo andikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudi na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, wakiwa shitaki au kuwatetea” (Warumi 2:12-15).
Mtu asiye kwenda kanisani haifahamu sheria katika nyakati hizi. Ndipo dhamira yake hugeukia maovu; ingawa anajua lililo jema au baya katika dhamira yake. Ndipo basi, ni dhambi na hivyo kuanza kumtafuta Bwana ili aweze kumwokoa kwa dhambi zake. Mungu hukutana na wale wote wenye kumtafuta yeye.
Yatupasa kuitafuta rehema yake na kumwamini. Yatupasa tumwamini huku tukiachana na majivuno yetu. Yatupasa kuishi kwa imani. Tusitengane na Kanisa la Mungu, yatupasa kutafuta, kuamini na kushikamana na kanisa lake. Mungu hatufukuzi pale tunapo shikamana na kanisa, hata ikiwa sisi ni dhaifu na tusio madhubuti.
 

Dhambi ya Wayahudi.
 
Sasa Paulo Mtume anaanza kuibubiri Injili katika viwango vya juu kwa Wayahudi baada ya kuwa tofautisha kati yao na wale watakao ingia Ufalme wa Mbinguni.
“Lakini wewe, ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati na kujisifu katika Mungu na kuyajua mapenzi yake, na kuyakubali mambo yaliyo bora nawe umeelimishwa katika torati na kujua hakika ya kuwa wewe mwenyewe u kiongozi wa vipofu, mwanga wao walio gizani, mkufunzi wa wajinga walimu wa watoto wachanga mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati basi wewe umfundishaye mwingine, Je! Hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asizini wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu wateka mahekalu?” (Warumi 2:17-22).
Yatupasa kuelewa ifuatavyo. Mwanzoni Mungu aliongea na Wayahudi, hivyo wakawa na neno la Mungu na mpangiliowa utoaji wa sadaka. Aliahidi kuja kwa Masia kupitia Wayahudi na kuwaonyesha mpango wake wale walio kua watumishi wake wa Kiyahudi. Hivyo Musa na mitume wote walikuwa ni Wayahudi. Hata hivyo walidhani kuwa wanaelewa kile kimpendezacho Mungu na jinsi ilivyo sheria yake huku wakiifuata kwa uangalifu na kuitunza katika kumbukumbu za vichwa vyao neno moja hadi jingine la Mungu. Hata hivyo, Paulo Mtume alisema “Lakini wewe ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati na kujisifu katika Mungu”. Wayahudi hawakuwa wameokolewa, ingawa walijisifu katika Mungu na hata kuhudumia katika utoaji wa sadaka kwa uadilifu. Wale wote wasio mwamini Yesu kwa ujumla, kwamba yeye ndiye Mwokozi ni sawa na wasio mwamini. Maana yake hawamwamini Mungu au hata ahadi zake ambazo atawaokoa kwa jinsi ile ya mpangilio wa sadaka, pia kutomwamini Yesu kuwa ndiyo Mwokozi.
Wayahudi watakwenda jehanamu kwa sababau hawa mwamini Yesu kuwa ni Mwokozi. Haiukuwa na maana kwao kuwekea mikono juu ya kichwa cha kondoo kila mara.Hawakuamini kwamba tendo la kuwekewa mikono linafanana na kutwika dhambi katika nyakati za Malaki wakati ule wa Agano la Kale. Waliamini vile ipasavyo hadi kipindi cha Daudi, lakini imani zao zilianza kutetereka muda hata muda wakati wa Sulemani. Wakati wa kipindi cha kugawanyika kwa ufalme, ndipo walipo anza kuabudu miungu kama vile Baali na Ashera huku wakiendeleza utaratibu wa utoaji wa sadaka katika Hekalu la Mungu. Kuendeleza utaratibu wa utoaji wa sadaka ni sawa na kutomwamini Mungu. Mungu huridhika pale tunapo amini na kulishika neno lake.
Katika mpangilio wa utoaji wa sadaka kwenye hema dhambi za mtu zilitwikwa juu ya kichwa cha mnyama wa kutolewa kafara wakati mikono ilipo wekwa juu ya kichwa chake. Lakini wao hawakuendelea kuliamini hili, au kuwafundisha wengine, ingawa walifahamu lililo sawa na lisilo sawa. Hii ndiyo iliyokuwa dhambi ya Wayahudi. Kutoamini ukweli wa neno la Mungu, kulijua neno lake baadaye na kuhubiri neno la mtu mwingine ndiyo iliyokuwa dhambi ya Wayahudi.
Ni sawa na kutomwamini Mungu. Ni dhambi ya hatari sana. “Lakini wewe, ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati, na kujisifu katika Mungu na kuyajua mapenzi yake na kuyakubali mambo yaliyo bora, nawe umeelimishwa katika torati na kujua hakika ya kuwa wewe mwenyewe ni kiongozi wa vipofu, mwanga wao walio gizani mkufunzi wa wajinga, walimu wa watoto wachanga mwenye namna ya maarifa n
a ya kweli katika torati.” Paulo alilenga ile dhambi ya kutoamini iliyokuwepo kwa Wayahudi.
 

Ni kumtia najisi Mungu kwa kumwamini Yesu huku ungali na dhambi moyoni.
 
Tunaweza kulitumia kosa hili la Wayahudi kwa wengi wa Wakristo wa nyakati hizi. Wayahudi nao ni sawa na wale wasio amini ya kwmaba tayari Yesu alikwishafuta dhambi zao zote. “Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati? Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa kwa ajili yenu” (Warumi 21:23-24). Ni kulitia jina la Mungu najisi ikiwa tutamwamini Yesu kwa njia isiyo sahihi. Ni kulitia najisi jina la Mungu ikiwa hatuto mwamini Mungu namna ile ilivyo sahihi, yaani namna ile Yesu alivyo tenda na pia ikiwa hatuto zaliwa upya mara ya pili.
Ni kumkufuru Mungu kwa kumwamini Yesu pasipo kuzaliwa upya mara ya pili. “Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kuto kutahiriwa. Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je, kutokutahirwa kwake hakutohesabiwa kuwa kutahiriwa? Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je, hata hukumiwa. Wewe uliye na kutahiriwa ukaihalifu? Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo katika roho si katika andiko ambayo sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu” (Warumi 2:25-29). Yatupasa sisi sote kupokea neno la Yesu kwa mioyo yetu yote.
 

Lipi lililokuja kabla, tohara au sheri?
 
Lipi lililotangulia, kati ya tohara au sheria? Lipi kati ya moja ya haya Mungu aliwapa Waisraeli kwanza? Tohara. Mungu alimwamuru Abrahamu atahiriwe. Abrahamu hakua na mtoto wa kumzaa ingawa alikuwa na umri wa miaka 99. hata hivyo, Mungu alimpa ahadi Abrahamu ya kumpa, mtoto alipokuwa na umri wa miaka 75, Mungu alimwambia “Toka nje, nitakupa wazao mfano wa nyota angani.” Abrahamu aliamini neno la Mungu na kusubiri takribani miaka 25. Ahadi mwishowe ilitimia baada ya miaka 25. Hivyo mtoto wake alipatikana huku yeye akiwa na umri wa miaka 100. alisubiri miaka 25, ingawa kidogo akate tamaa na hata kupelekea kufanya makosa pale alipo kuwa akisubiri. Mungu pia aliahidi pia pamoja na mtoto kumpa nchi ya ahadi, Kanani ambayo inamaanisha kuwa ni Ufalme wa Mbinguni kwa tafsiri ya kiroho.
Baada ya ahadi ya Ufalme wa Mungu, Mungu alimwambia Abrahamu na kila mume kati ya wanaume wa nyumba zake kutahiriwa. Mungu alisema kwamba tohara hiyo ni alama ya agano la Mungu na wao. Hivyo Abrahamu alitahiriwa govi lake. Wanaume wote katika nyumba yake walifuata tendo hili. Tohara inafanana na imani ambayo tunayoiamini na kupokea Injili yakweli.
 

Waisraeli waliikataa tohara ya moyo.
 
Hata hivyo, Waisraeli walijivunia kwa kuwa ni uzao wa Abrahamu, nakutahiriwa huku wakijigamba mbele ya watu wa Mataifa, “Je, ninyi mmekwisha tahiriwa?” Yatupasa kutahiriwa mioyo yetu. Tumeokolewa pale tunapo pokea neno la Yesu katika ondoleo la dhambi za dunia na kuamini kwa moyo wetu wote.
Hakuna nchi yoyote iliyo wahi kuvamiwa kama Israeli. Walikuwa na masononeko makuu wakiwa yatima na wasio na makazi kwa takribani miaka 2000. Mungu aliwapa kibano Waisraeli. Kwa nini? Kwa sababu hawakumwamini yeye.
Walitia najisi jina la Mungu kwa sababu hawakuamini, ingawa Mungu aliwapenda na kuwataka waamini kwamba yeye alikwisha safisha dhambi zao zote. Mungu anataka kuwa shinda adui zake akiwa ni mchungaji wa Israeli na kutaka kuwabariki, kuwapenda na kuwapa utukufu.
Mungu aliahidi kuwapa utukufu watu wote na kuwafanya kuwa watoto kwake ikiwa tu watamwamini yeye kwa mioyo yao yote na kuwa na ondoleo la dhambi kwa mfano wa Waisraeli, Mungu ana watahadharisha watu wote wa ulimwengu kwamba atawatupa jehanamu ikiwa hawato pokea ahadi yake.
Mungu ameahidi ya kwamba yeyote anaye amini Injili yake ya kweli ataweza kupokea baraka zake zote ambazo Yesu aliziahidi, ingawa aweza kuwa dhaifu kwa matendo yake. Njia pekee ya kukwepa hukumu ya Mungu ni kuiamini Injili na ndipo utakapo okolewa na hata kukwepa jehanamu.
Nawatakia rehema ya Bwana iwe juu ya nafsi zote.