Search

Mahubiri

Somo la 5: Ukiri Sawa wa Dhambi

[5-1] Ni Namna Ipi Ya Kufanya Toba Ya Kweli Na  Sahihi Kwa Dhambi (1 Yohana 1:9)

(1 Yohana 1:9)
“Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.”
 

INJILI YA DAMU NI INJILI ILIYO NUSU

Je, tutaweza kuingia 
ufalme wa mbinguni kwa 
injili ya damu pekee?
Kamwe. Ni lazima kamini injili 
yote kiukamilifu.
(injili ya maji na Roho)

1Yohana 1:9 ipo kwa wenye haki tu. Ikiwa mwenye dhambi hakuwa amekombolewa na kujaribu kupatanishwa na dhambi za kila siku kulingana na maneno yaliyo katika kifungu hicho kwa kutubu makosa yake, dhambi zake hazitofutika. Je, unaelewa ninachojaribu kuelezea? Kifungu hicho katika 1Yohana 1:9 hakiwi kigezo kwa wenye dhambi ambao hawajazaliwa upya mara ya pili.
Wapo wengi duniani hapa ambao hawajazaliwa upya mara ya pili, lakini angali wanadhani kwa kutumia maandiko katika 1Yohana sura ya 1 na kwa kusali na kutubu dhambi zao hudhani watasamehewa.
Lakini je, mtu ambaye hajazaliwa upya mara ya pili ataweza kweli kukombolewa kikamilifu kwa dhambi zake kupitia sala ya toba? Hili ni jambo muhimu kulichukulia na kulibadilisha kabla hatuja endelea.
Kabla ya kusoma 1Yohana, unapaswa kuamua ikiwa Mtume Yohana alikuwa ni mwenye haki au ni mwenye dhambi. Hebu nikuulize swali hili. Je, mtume Yohana alikuwa ni mwenye haki aliyezaliwa upya mara ya pili kwa kuamini injili ya maji na Roho au alikuwa mwenye dhambi?
Ikiwa utasema Mtume Yohana alikuwa ni mwenye dhambi kibiblia umekosea imani yako. Ikiwa Mtume Yohana alikuwa mwenye haki aliyezaliwa mara ya pili alipomwamini Yesu inakuwa wazi kwamba imani yake ilikuwa ni tofauti na yako. Yakupasa uwe na imani sawa na ya Mtume Yohana.
Hebu nikuulize swali jingine. Je, Mtume Yohana likuwa akiandika waraka huu kwa wenye haki au wenye dhambi? Mtume Yohana alikuwa akiandika waraka huu kwa wenye haki.
Hivyo basi ikiwa wenye dhambi ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili wataona maneno ya 1Yohana 1:8-9 na kuyatumia kwao itakuwa batili. Ikiwa unahitaji kuwa mwenye haki, kiri dhambi zako mbele ya Mungu na amini injili ya maji na Roho. Bwana atakutakasa kwa dhambi zako zote kwa injili ambayo tayari imeshasafisha dhambi ya ulimwengu.
Imani ya Mtume Yohana ni kama hii. Katika 1Yohana sura ya 5 anasema kwamba anaimani katika “maji, damu na Roho” Je, unamwamini Yesu Kristo aliyekuja kwa maji, damu na kwa Roho? Je, unamwamini Yesu aliyekuja kwa msalaba, au ubatizo, damu na kwa Roho?
Je,utaweza kuingia ufalme wa mbinguni kwa kuamini injili ya damu tu? Ikiwa imani yako ipo katika injili ya damu ya msalaba pekee, umeelewa nusu ya injili. Ikiwa unaamini damu msalabani pekee bila shaka utajikuta ukisali sala za toba kila siku. Swala ni kwamba unaamini kuwa dhambi zako zitaweza kutakaswa kwa kuomba toba?
Je, ni kweli itawezekana kwa dhambi kutakaswa pale tunapoamini damu ya Yesu msalabani tu, kutubu na kuomba msamaha kwa dhambi za kila siku? Ikiwa wewe ni mmoja wao kati ya watu wa aina hii, basi dhambi zako zitabaki kuwa ndani ya moyo wako, kwa kuwa hakuna yeyote atakaye takaswa kwa dhambi zake kwa kupitia damu ya Yesu msalabani peke yake, au sala za kila siku za toba. Ikiwa wewe ni mmoja wao, basi bado huifahamu injili ya maji na Roho na hakika imani yako haijakamilika.
Mtume Yohana alizaliwa upya mara ya pili kwa kuwa aliiamini injili ya maji na damu na Roho. Lakini wewe unaamini damu ya msalabani pekee. Unapokuwa huna ufahamu wa kweli wa injili ni kwa namna gani basi utaweza kuongoza wengine kuelekea katika wokovu? Hujazaliwa upya wewe binafsi lakini unajaribu kujipatanisha kwa dhambi kupitia sala za toba. Njia hii kamwe haito kupeleka popote.
Haijalishi ni kwa namna gani mtu atafanya sala ya toba dhambi zake hazitoweza kutakaswa moyoni. Ikiwa unahisi wakati mwingine kuwa dhambi zako zimetakaswa moyoni, huu ni mtazamo wako tu ukichanganya na nguvu ya hisia iliyomo akilini mwako. Ikiwa utasali na kutubu unaweza kuhisi kupata nguvu mpya kwa siku au zaidi. Lakini kamwe hutoweza kuwa huru na dhambi kwa njia hiyo.
Wenye dhambi husali na kutubu wakitumaini kuokolewa kwa dhambi zao. Na hii ndiyo maana bado wanaendelea kubaki na dhambi hata baada ya kumwamini Yesu kwa muda mrefu. Hawaifahamu injili ya maji na Roho. Ikiwa unamwamini Yesu huku ukiwa bado hujazaliwa upya utaweza kuwa moja wapo ya watu wa aina hii. Ikiwa unajaribu kujiletea upatanisho wa dhambi zako kwa kusali na kutubu kila siku huu ni ushuhuda tosha kwamba hujazaliwa upya. Lazima uchague ama kuamini injili ya maji na Roho kama Mtume Yohana alivyo au kuwa na imani kulingana na mawazo yako pamoja na hisia zako. Moja kati ya haya ni sahihi na jingine si sahihi.
Injili ya kweli kulingana na biblia ni kwamba Yesu alibatizwa na kubeba dhambi zote za ulimwengu mara moja na kwa wakati wote na kupokea hukumu kwa dhambi hizo kwa niaba ya wenye dhambi pale msalabani. Ikiwa mtu ataamini ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani ataokolewa mara moja na kwa wakati wote.Kwa upande mwingine, ikiwa mtu atajaribu kutakasa dhambi na makosa yake kwa sala za toba, hakika kamwe hatoweza kuwa huru na dhambi. Je, unafikiri kuwa utaweza kukumbuka dhambi zako za kila siku? Je, unadhani Mungu hazifuatilii dhambi ambazo hukutubu? Je, sala za toba ni suluhisho wazi kwa tatizo la dhambi za kila siku? Jibu pekee ni “siyo”.
 

TOBA YA KWELI NA SABABU YA KUKIRI

Ni ipi mipaka ya kukiri 
na matendo mema?
Ingawa imetupasa kukiri dhambi zetu 
maishani pote, kamwe hatuokolewi 
kwa kukiri makosa na 
kutenda mema.

Kutubu katika Biblia maana yake ni kugeuka toka imani potofu na kuelekea imani ya kweli, na kuwa mwenye haki, maana yake kutambua uovu binafsi na kuirudia nuru ya injili.
Ikiwa wewe ni mwenye dhambi yakupasa kutubu kama ifuatavyo “Mungu wangu, nimetenda dhambi na kustahili kwenda motoni. Lakini ninatamani kuokolewa kwa dhambi zangu. Tafadhali niokoe kwa dhambi zangu zote. Sijazaliwa upya mara ya pili na nafahamu nimehukumiwa motoni” Hii ndiyo toba sahihi.
Pia aina gani ya toba kwa mtu aliyezaliwa mara ya pili anayopaswa kufanya? “Mungu wangu nimetenda dhambi ya kuufuata mwili wangu. Ninaamini kwamba Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kuniokoa kwa dhambi zote, hata dhambi hii niliyotenda sasa amabapo ilinipasa nife kwa ajili hiyo. Namshukuru Bwana aliyeniokoa kwa maji na damu” Toba ya aliyezaliwa upya na asiyezaliwa upya ni tofauti.
Yatupasa sote tuwe na imani sawa na mtume Yohana. Ikiwa utajaribu kuficha dhambi zako kwa kutumia toba ya mwenye haki, kamwe hautookolewa kwa kifo amabacho ndiyo mshahara wa dhambi.
Wenye dhambi wote ambao bado hawajazaliwa upya waache mara moja kuficha dhambi zao kwa kigezo cha sala ya toba na kuanza kwanza kuamini kweli ya injili ya maji na damu na Roho. Wanapaswa wajifunze juu ya imani ya mtume Yohana kwanza na ndipo wapate wokovu.
Wenye dhambi hawajafahamu vile ilivyo hukumu kali ya dhambi zao itakavyo kuwa. Dhambi iliyo hatari kupita zote mbele ya Mungu ni kutoamini injili ya kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho.
Wale wote wanao mwamini Yesu lakini bado hawajazaliwa upya imewapasa kutubu mbele ya Mungu hivi, “Bwana, mimi ni mwenye dhambi anayepaswa kutupwa motoni” badala ya kurudiarudia kwa kusema “Bwana, tafadhali nitakase dhambi zangu” Mwenye dhambi anapoichukua injili moyoni mwake kuwa Yesu amemwokoa kupitia ubatizo wake Yordani na damu yake mslabani, atakuwa huru kwa dhambi zake zote.Hii ndiyo namna ya toba ambayo mwenye dhambi hufanya ili aweze kuokolewa kwa dhambi zake zote mbele ya Mungu.
Mwenye dhambi imempasa kutubu kuwa hajazaliwa upya tu na kuamini injili ya maji na Roho. Na ndipo ataokolewa mara moja. Kwa injili ya maji na Roho, wokovu wa wenye dhambi wote ulikamilika. “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12). Mungu ameokoa wenye dhambi wote kwa dhambi zao kwa kuruhusu mwana wake Yesu Kristo abatizwe na Yohana Mbatizaji na kufa msalabani.
Bwana ametakasa dhambi zote wazitendazo watu kwa miili yao na mioyo yao toka kuzaliwa hadi kufa kwao. Yatupasa kuamini ukweli wa injili hii ili tuokolewe. Ni kwa injili hii pekee ndiyo tutakayoweza kuwa huru kwa dhambi zetu zote na kutakaswa kwa hakika. Tutaweza kuwa wenye haki mara moja na kwa wakati wote tutakapoamini injili ya maji na Roho.
Yesu alibatizwa, kubeba dhambi za dunia, kulipia dhambi hizo msalabani kwa uhai wake, alifufuka baada ya siku tatu na leo ameketi kuume kwa Mungu. Huu ndiyo ukweli pekee.
Yatupasa sote kukiri. “Bwana, siwezi kujizuia kutenda dhambi hadi siku ya kifo. Nilizaliwa nikiwa na dhambi toka tumboni mwa mama yangu, nakubali dhambi zote nilizotenda imenipasa kutupwa motoni niangamie. Kwa sababu hiyo, nataka nimwamini Yesu, aliyekuja kwa maji, damu na Roho na kuwa mwokozi.”
Kama ilivyoandikwa katika Mathayo sura ya 3 Yesu aliichukua dhambi ya ulimwengu, pamoja na dhambi zote tutakazotenda hadi mwisho wa maisha yetu duniani, pale alipo batizwa mto Yordani “Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32).
Ikiwa Yesu alituokoa kwa dhambi zetu za asili tu na kutuambia kutafuta suluhusho la tatizo la dhambi zetu za kila siku hakika tungekuwa kwenye mateso yasiyo kwisha. Lakini Yesu ametuweka huru kwa dhambi zetu zote kwa ubatizo na damu yake. Sasa kwa nini tuwe na wasiwasi? Tunapoamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani na kumshukuru Bwana, Roho hukaa ndani ya mioyo yetu.
Je, unamwamini Yesu? Je, unaamini Roho akaaye ndani yako? Dhambi zote alitwikwa Yesu alipobatizwa na kubeba dhambi ya ulimwengu. Baadaye alihukumiwa kwa dhambi hizo msalabani kutuweka huru kwa adhabu ya milele. Hii ni injili ya kweli. 
 

TOBA YA MWENYE HAKI

Ni toba ipi iliyo ya kweli 
kwa mwenye haki?
Kukiri kwamba anatenda dhambi kila siku 
lakini kuwa na imani ya ukweli kwamba 
Yesu alikwisha zitakasa dhambi hizo 
za kila siku miaka 2000 iliyopita 
kwa mara moja.

1Yohana 1:9 inasema,“tukiziungama dhambi zetu yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.” Maana yake ni kwamba mtu atakayeamua kuamini injili ya maji na Roho inampasa kukiri dhambi kwa kusema “Bwana siwezi kujizuia kutenda dhambi maishani mwangu, lakini nafahamu siwezi kuokolewa kwa dhambi zangu zote kwa sala ya toba. Naamini kuwa mshahara wa dhambi ni mauti na hakuna jingine zaidi ya ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kwake kutakakonitakasa kwa dhambi zangu zote. Ninakiri kutenda dhambi leo lakini namwamini Yesu kuwa alikwisha takasa dhambi hii niliyotenda leo tangu miaka 2000 iliyopita”Ikiwa mtu huyu ataomba namna hii, tatizo la dhambi katika dhamira yake litakwisha mara moja.
Andiko tulilosoma leo linawafaa sana wenye haki. Lakini mwenye dhambi akilichukua na kulitumia katika tafsiri potofu, ataishia motoni. Hata hivyo ni moja kati ya vifungu vyenye kutumika vibaya katika biblia. Kwa muda mrefu kumetokea kutokuelewana kati ya wakristo juu ya hili.
Upo msemo usemao “tabibu mjinga huua wagonjwa.” Wakati tabibu mjinga anapojaribu kufanya zaidi ya uwezo wake, ataweza kuishia kumuua mgonjwa wake.
Ni kanuni ya maisha ambapo mtu yampasa awe na ujuzi wa kutosha na mazoea ili kufanya kazi yake vyema. Ni sawa na neno la imani. Wale wenye kufundisha kama ilivyo andikwa sawia na kwa uwazi na wale wanaojifunza toka kwao yawapasa kuwa na imani kwa kile walichojifunza.
Ikiwa mhubiri atawafundisha wafuasi wake mafundisho potofu au ikiwa waumini watajifunza Biblia kimakosa itasababisha hukumu ya motoni kwa wote. Ni wale waliozaliwa upya tu ndiyo watakaoweza kufundisha biblia kwa sahihi. Hata dawa nzuri yaweza kuuwa mgonjwa ikiwa maagizo yake hayatakuwa sahihi na ndivyo ilivyo katika kufundisha na kujifunza neno la Mungu. Ni muhimu kama ilivyo moto katika maisha yetu. Kama vile utakavyoleta janga la moto utakapoachwa katika mikono ya watoto, neno la Mungu pia litaweza kuleta janga kuu likiwa katika mikono isiyofaa.
Yatupasa tuwe na ufahamu juu ya tofauti kati ya toba ya mwenye haki na mwenye dhambi. 1Yohana 1:9 ni kwaajili ya wenye haki tu. Wakati mwenye haki anapokiri juu ya dhambi zake mbele ya Bwana kwa imani, huwekwa huru kwa dhambi hizo kwa sababu Yesu tayari alikwisha takasa dhambi zote miaka 2000 iliyopita.
Ni kosa kwa mwenye dhambi kuamini kuwa dhambi zake hutakaswa kila mara anaposali sala ya toba. Mtu anapokuwa hajazaliwa upya mara ya pili je, dhambi zake zitatakaswa kwa toba?
Mungu ni wa haki. Alimtuma mwana wake wa pekee duniani na alimfanya achukue dhambi za dunia kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Hivyo mwenye haki anapokiri dhambi, Mungu humwambia kuwa tayari Yesu alikwishazichukua dhambi zake miaka 2000 iliyopita.Mtu wa aina hii kwa hiyo huthibitisha kwamba hana tena dhambi moyoni ingawa mwili utaendelea kutenda dhambi.