Search

Mahubiri

Somo la 7: Udanganyifu katika nadharia ya Kuamua mapema na Uchaguzi wa Mungu

[7-1] Upotoshaji uliopo kwenye kanuni ya kujulikana na kuchaguliwa tangu asili (Warumi 8:28-30)

(Warumi 8:28-30)
“Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, nao akawaita; na wale aliowaita hao akawahesabia haki, na wale aliowahesabia haki hao akawatukuza.”
 

Je, ni kweli Mungu amewateua 
baadhi ya watu kati yetu?
Hapana. Ametuteua sisi sote 
katika Yesu Kristo.

Kanuni ya kitheolojia kuhusu kuchaguliwa toka asili na kuteuliwa, ambazo ni miongoni mwa misingi ya theolojia zinazounda misingi ya Kikristo, zimewapelekea wengi wenye kutaka kumwamini Yesu kushindwa kuelewa Neno la Mungu. Kanuni hizi potofu zimesababisha mkanganyiko mkubwa.
Kile theolojia hizi za uongo inachosema kuhusiana na kuchaguliwa toka asili ni kwamba, Mungu ameteua watu anaowapenda na kuwahukumu asiowapenda. Hii inamaana ya kwamba, kati ya watu, wapo walio teuliwa na kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho na kukubaliwa Mbinguni na wapo wengine ambao hawakuchaguliwa na hivyo hatima yao ni kuunguzwa motoni.
Ikiwa kweli Mungu amewateua watu kati yetu, hatutoweza kuvumilia taabu yetu juu ya swali “Je, kuchaguliwa huku ni kwa sababu ya wokovu?” Ikiwa hatukuchanguliwa, itakuwa kazi bure kwetu kumwamini Yesu. Kwa maana kanuni hii itawafanya watu wadhani kwamba wamechaguliwa na Mungu bila imani yenyewe.
Ikiwa tunaamini hili, je, tutawezaje kuwa huru kwa mashaka na kumwamini Mungu pekee? Tutathibitishaje kwamba Mungu ametuchagua kweli? Itakuwaje ni Mungu kwa hao walioteuliwa tu, ikiwa anasema “Au je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siyo Mungu wa mataifa pia? Naam, ni Mungu wa mataifa pia” (Warumi 3:29).
Kwa kuwa watu wengi wanaelewa visivyo maana ya kuchaguliwa toka asili na kuteuliwa, wanabaki na hofu ingawa wanamwamini Yesu.
Waefeso 1:3-5 inasema “Atukuzwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa Roho, ndani yake Kristo kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili tuwe watakatifu watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo sawa sawa na uradhi wa mapenzi yake.”
Kwahiyo yatupasa kuangalia upya dhumuni la theolojia ya kuchaguliwa toka asili na uteule. Yatupasa kwanza kuelewa nini Biblia inasema juu ya kuchaguliwa toka asili na uteule hivyo kuimarisha imani yetu katika wokovu kupitia maji na Roho.
Warumi inatueleza nini? Baadhi ya wanatheolojia walianzisha kanuni isiyo na msingi ya “uchaguzi usio wa sharti” Je, theologia ni Mungu? Theolojia yenyewe siyo Mungu. 
Hata baada ya kuumbwa kwa dunia Mungu alichagua wanadamu wote kupitia Yesu Kristo kwa kughairi ili kuweza kutuokoa sisi sote kwa kutufanya wenye haki. Yesu ametupenda pasipo sharti lolote. Usimfanye kuwa ni Mungu wa ubaguzi. Wasioamini wanayo imani katika mawazo yao lakini wenye kuamini huweka misingi ya imani zao katika maandiko ya neno la Mungu.
 

KUCHAGULIWA KATIKA AGANO LA KALE

Je, kanuni ya uchaguzi usio 
wa sharti ni ya kweli?
Hapana. Bwana wetu si mwenye 
akili finyu. Mungu amewachagua wenye 
dhambi wote kupitia Yesu na si 
katika kuwachagua wachache.

Mwanzo 25:21-26 tunasoma juu ya wana wawili wa Isaka, Esau na Yakobo. Mungu alimchagua Yakobo toka watoto hao wawili wa Isaka wakiwa tumboni mwa mama yao.
Wale wasioelewa neno la Mungu huchukulia jambo hili kuwa ndiyo msingi wa kanuni ya “kuchaguliwa pasipo sharti” na si kuchaguliwa kupitia Yesu Kristo, hivyo ni sawa kama kuabudu Mungu mfu na sanamu. Mungu si Mungu mfu. Ikiwa tungelimwamini Mungu mfu tungelikana mpango wa Mungu kwetu na kuangukia katika mtego wa shetani.
Ikiwa watu si watafiti wa mapenzi ya Mungu, basi si chochote bali ni sawa na hayawani ambao mwisho wake kuangamia. Hivyo basi kwa kuwa sisi wenye kuamini si kama hayawani, yatupasa tuwe waumini wa kweli wenye kusoma na kuamini ukweli wa maandiko ya biblia. Kabla ya kufikiri chochote juu ya ukweli wa maandiko katika biblia kwanza ni kumkomboa mtu kwa shetani.
Tukiwa na imani ya kweli yatupasa kwanza kuwaza juu ya maandiko ya kweli katika Biblia na kufuata imani ya wale waliozaliwa upya katika Kristo.
Ukalvini (Calvinism) husisitiza juu ya ukombozi wa mipaka. Hii ina maana kwamba upendo wa Mungu na ukombozi wa Bwana huwahusu baadhi ya watu. Je, hii yaweza kuwa kweli?
Biblia husema kwamba, Mungu mwokozi wetu…. “hutaka watu wote waokolewe” (1 Timotheo 2:4). Ikiwa baraka ya ukombozi ipo kwao wale tu wachache, wenye kuamini walio wengi wangekata tamaa kumwamini Yesu. Hata hivyo ni nani angependa kumwamini Mungu aliye na akili finyu namna hii?
Yatupasa kuwa na ujasiri kwamba Mungu wetu si mwenye akili finyu. Ni Mungu wa kweli, Upendo na Haki. Yatupasa kumwamini Yesu na injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho na hivyo kuweza kuokolewa kwa dhambi zetu zote. Yesu ni mwokozi wa wale wote waliozaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Kutokana na Ukalvini (Calvinism) ikiwa palikuwepo watu kumi, kati yao wataokolewa na Mungu hali wengine wataachwa na hivyo kuangamia motoni ahera. Hii si kweli, haileti maana yoyote kusema Mungu huwapenda baadhi ya watu na kuwachukia wengine. Hebu fikiria leo Mungu yupo nasi hapa. Ikiwa anaamua kuteua wale wote walio upande wa kulia na kuamua kuwatupa wale wote walio upande wa kushoto motoni. Je, tunge mthamini kuwa ni Mungu?
Je, wale wote ambao amewachukia wasingelitoa sauti kwa kulalamika? Hakika viumbe wote wangetoa sauti wakisema “Mungu gani huyu asiye tenda haki?” Uchaguzi usio wa sharti ni kanuni isiyo ya kweli kwa sababu Mungu amewachagua wanadamu wote kupitia Yesu Kristo.
Hivyo yeyote aliyeitwa na Mungu katika jina la Kristo amekwisha chaguliwa. Sasa basi Mungu amewaita watu wa aina gani kwake? Amewaita wale wote wenye dhambi, si wenye haki. Mungu hakuwaita wale wote wenye kujiona binafsi kama ni wenye haki.
Baraka ya ukombozi wa Mungu ni ya wale wote wenye dhambi na wale walio hukumiwa kwenda motoni. Uteuzi maana yake Mungu kuwaita wenye dhambi ili kuwafanya watoto wake wenye haki.
 

MUNGU NI MWENYE HAKI

Je, Mungu huwapenda 
wachache waliochaguliwa?
Hapana, Bwana si mwenye akili finyu, 
Mungu ni mwenye haki.

Mungu ni wa haki. Ni Mungu anayewapenda wale walio chaguliwa pasipo sharti. Amewaita wenye dhambi katika Kristo. Pasinge kuwepo wokovu kupitia ukombozi wa Yesu Kristo na msamaha wake wa dhambi, je, tungelifahamu vipi upendo wa Mungu na wokovu wake. Kamwe usimfanye kuwa ni Mungu asiye wa haki.
Hebu tazama katika mistari hii ya Waefeso 1:3-5 Bwana wetu Yesu Kristo alivyotubariki kwa baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa roho, kupitia Kristo ambaye ni msingi wa ulimwengu ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele yake katika pendo. “Kwa kuwa alitangulia kutuchagua ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo sawa sawa na uradhi wa mapenzi yake”-neno gani limekosekana katika sentensi hii? Neno “katika yeye” (Yesu). 
Uchaguzi usio sharti katika ukalvini (Calvinism) hauwiani na maneno ya Biblia. Biblia inasema “kama vile alivyotuchagua katika yeye (Yesu) kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.”
Mungu amewachagua wanadamu wote “katika yeye” Kristo ili tuweze kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na Roho. Wale wote wasio na jinsi zaidi ya kuzaliwa upya kwa sababu ni wenye dhambi ndiyo watakao kombolewa kwa dhambi zao na kuwa watoto wa Mungu. Amejumuisha wanadamu wote katika mlolongo wa wale watakao okolewa na kuchaguliwa katika Kristo Yesu.
Kwa kuwa wanatheolojia wengi wanatilia mkazo juu ya kuchaguliwa pasipo sharti kwa kusema kuwa ni wachache ndiyo waliochaguliwa, basi watu wengi wamenaswa katika imani ya kuchanganyikiwa katika mafundisho yasiyo na kichwa wala miguu. Wanatheolojia hawa waongo husema kwamba Mungu huwachagua baadhi na kuwachukia wengine kupitia fundisho la kuchaguliwa pasipo sharti, wakati ukweli juu ya neno lake ni kwamba Mungu kawachagua wenye dhambi wote kupitia Yesu. Watu wengi wameangamia kwa mafundisho yasiyo ya kweli kutokana na imani zao za kimazingaombwe.
Fahamu kuwa ikiwa utagundua kwamba Mungu aliamua kutuokoa wanadamu wote kupitia Yesu na hivyo basi ondoleo la dhambi lipo kwa kila mtu atakayemwamini Yesu. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kuokolewa kwa dhambi zetu zote, na kuwa wana wa Mungu, wenye haki, na hata kupata uzima wa milele na kuwa na uthibitisho kwamba Mungu ni haki!
 

SWALA LA KUCHAGULIWA KWA HABARI YA YAKOBO NA ESAU.

Ni nani aliyeteuliwa na Mungu? 
Je, ni wale waliochaguliwa?
Hapana. Mungu aliwachagua wanadamu wote 
kupitia Kristo. Hivyo yeyote anayemwamini 
Kristo, hana tena dhambi kupitia 
ubatizo wa Yesu na huko ndiko 
kuchaguliwa.

Katika Mwanzo 25:19-28, Esau na Yakobo walikuwa wakishindana ndani ya tumbo la mama yao Rebeka. Mungu alisema katika Mwanzo 25:23 “Bwana akamwambia, mataifa mawili yako tumboni mwako na kabilia mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili na mkubwa atamtumikia mdogo.”
Hapa wenye dhambi hugeuza maneno haya kuwa kanuni ya kitheolojia na uteule wa kimungu wa kuwaacha wengine wenye kumwamini Yesu kuwa katika hali ya kuchanganyikiwa ikiwa nao wamechaguliwa au hapana! Wanapotafakari juu yao kwamba wamechaguliwa basi hudhani wamekwisha okolewa na hivyo kuondoa hitaji lao katika kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Swala la kuchaguliwa pasipo sharti limewageuza wengi wanaomwamini Yesu kuwa mbali na ukombozi na hivyo kuhukumiwa motoni. Pia limemfanya Mungu aonekane asiye wa haki.
Kwa kuwa wanatheolojia wengi hufundisha mafundisho yasiyo ya kweli yatokayo ndani ya mawazo yao, wengi wanaomwamini Yesu hukosa tumaini na hivyo kuhangaika kwa kutaka kujua ikiwa kama nao wamechaguliwa au labda ukombozi wao ulikwisha kuwepo kabla ya misingi.
Kati ya Yakobo na Esau ni yupi aliyechaguliwa na Mungu? Alimchagua Yakobo kupitia Yesu Kristo. Katika Warumi 9:10-11 inasema kwamba Mungu alimchangua Yakobo badala ya kaka yake ingawa wote walikuwa tumbo moja kabla ya kuzaliwa na hawakuwa wamekwisha fanya jambo lolote kati ya baya au jema.
Nia ya Mungu ilikuwa kumteua Yakobo si kwa sababu ya matendo yake bali kwa sababu ya uchaguzi wake. Biblia pia inatueleza kuwa Yesu amekuja kuwaita wale wote wenye dhambi, si wale walioishi maisha mema.
Watu wote wakiwa ni uzao wa Adamu ni wenye dhambi. Daudi alisema kuwa alikuwa ni mwenye dhambi toka siku ile aliyokuwa tumboni mwa mama yake na ya kwamba alizaliwa akiwa na hali ya uovu. “Tazama mimi naliumbwa katika hali ya uovu, mama yangu alinichukua mimba hatiani” (Zaburi 51:5).
Watu wote wanazaliwa wakiwa ni wenye dhambi kwa sababu ya dhambi ya wazazi wao wa kwanza. Hivyo kila mtu anayezaliwa hapa duniani pasipo matarajio anakuwa ni mwenye dhambi, kutenda mambo ya dhambi na kubeba matunda ya dhambi.
Mtoto ambaye hajatenda bado dhambi ya aina yoyote tayari amekwisha kuwa ni mwenye dhambi kwa sababu amezaliwa kwa mbegu ya dhambi. Anamawazo ya uovu, uzinzi, uasherati na uuaji ndani ya moyo wake. Amezaliwa na dhambi za wazazi wake wa kwanza. Hivyo watu wote ni wenye dhambi hata punde tu wanapozaliwa.
Sababu Mungu ya kutufanya kuwa dhaifu ni kama ifuatavyo. Wanadamu ni viumbe wa Mungu lakini Bwana alikwisha kupanga kutufanya kuwa watoto kwake kwa kutuokoa na dhambi. Na ndiyo maana aliruhusu Adamu kutenda dhambi.
Tulipokuwa wenye dhambi matokeo yake Mungu alimtuma Yesu kuja ulimwenguni, alikubali mwana wake wa Pekee kuchukua dhambi zote za wanadamu kupitia ubatizo wake.
Nia ya Mungu ilikuwa ni kutukomboa wanadamu kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani na kutupatia nguvu ya kuwa wana wake kwa kumwamini Yesu. Aliruhusu Adamu kutenda dhambi kwa ahadi ya kusafisha dhambi zote kupitia Kristo.
Wenye dhambi wanao amini fundisho lenye kusema “mtazame Yakobo na Esau. Mungu alimchagua mmoja na kumchukia mwingine pasipo sharti” Mungu hakutuchagua pasipo sharti, bali ametuchagua kupitia Yesu Kristo. Ni vyema tukaangalia maandiko ya neno katika Biblia tu. Warumi 9:10-12 inasema “Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja naye Isaka, baba yetu (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto wala hawajatenda neno jema au wala baya ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo bali kwa sababu ya nia yake aitaje) aliambiwa hivi mkubwa atamtumikia mdogo.”
Mungu alimchagua Yakobo kupitia Yesu. Yakobo alikuwa ni aina ya wenye dhambi wasio faa na wasio na chochote cha haki. Waefeso 1:4 inasema Mungu alimchagua.
Kwa nini basi Mungu alimchagua? Alimchagua Yakobo kwa sababu alikwisha jua kwamba alikuwa ni mwenye dhambi nyingi na asiye na haki mbele ya Mungu na ni mwenye kumtegemea Mungu. Alimwita Yakobo katika jina la Mwana wake Yesu Kristo na kumkomboa kupitia injili ya maji na damu kumfanya kuwa mwana wake. Hivyo Mungu alimwita Yakobo kisha kumbariki kwa ukombozi.
Mungu huita wenye dhambi na kuwafanya wenye haki kupitia ukombozi katika Yesu. Huu ni mpango wa Mungu.
 

FUNDISHO LA UONGO JUU YA KUCHAGULIWA PASIPO SHARTI. 

Kwa nini Mungu 
alimpenda Yakobo?
Kwa sababu Yakobo alikwishajua 
juu ya yeye kutokuwa 
mwenye haki.

Hivi karibuni nilisoma kitabu kinacho husu hadithi ya kuchaguliwa pasipo sharti. Kijana mmoja aliota ndoto. Bibi kizee alimtokea ndotoni na kumwambia kijana huyo kuja sehemu fulani, na akaenda. Ndipo bibi kizee huyo alipomwambia kuwa amechaguliwa na Mungu.
Kijana alimuuliza Bi Kizee huyo kwamba ni kwa vipi amechaguliwa na Mungu hali yeye hajawahi hata kumwamini Mungu? Bi Kizee akamwambia kwamba Mungu amemchagua pasipo sharti yeye ingawa hana imani.
Hii si kweli. Ni kwa vipi Mungu kwa makusudi ahukumu watu motoni na kuwachagua wengine kwa wokovu? Mungu ameteua kila mtu kupitia Yesu.
Mafundisho ya kitheolojia kuhusu kuchaguliwa yanayomtenga Yesu si ya kweli. Ni ya uongo. Lakini wanatheolojia wengi husisitiza kwamba Mungu amechagua baadhi yetu tu. Hili si kweli. Mungu anataka kutuokoa sisi wote kupitia Yesu. Ni wale tu wasio amini ukombozi katika maji na Roho kupitia Yesu ndiyo ambao hawatakolewa.
Mungu amekwisha chagua toka asili wanadamu wote kwa wokovu kupitia Mwana wake Yesu na kudhamiria kutufanya kuwa wana wake hata kabla ya kuumba ulimwengu. Alipanga kuokoa wanadamu kwa dhambi zao zote ulimwenguni kupitia ukombozi wa Yesu Kristo. Huu ni ukweli kama ilivyoandikwa katika biblia.
Wenye haki waliozaliwa upya mara ya pili katika Kristo ndiyo waliochaguliwa. Lakini wanatheolojia husisitiza kwamba Mungu huchagua baadhi yetu. Husema kwa mfano, kasisi wa Kibudha ni kati ya hao ambao hawakuchaguliwa na Mungu. Lakini Mungu amewachagua hawa kupitia Yesu.
Ikiwa Mungu amewachagua pasipo sharti bila Yesu, pasinge kuwepo na haja ya kuhubiri injili. Ikiwa Mungu alikwisha kupanga kuchagua baadhi pasipo Yesu, wenye dhambi wasinge hitaji kumwamini Yesu. Kwa namna gani basi maneno ya upendo wake wa kweli na ukombozi vingetimia?
Sababu Mungu kumchagua Yakobo kupitia Yesu, sababu ya kumpenda Yakobo na kumchukia Esau ni kwamba alikwisha kujua kabla kuwa Yakobo angemwamini Yesu kabla ya kuumbwa kwake na Esau asinge mwamini.
Wapo wenye dhambi wengi hapa duniani wenye kumwamini Yesu. Baadhi yao wako kama Esau na wengine ni kama Yakobo.
Kwa nini Mungu alimpenda Yakobo? Yakobo hakuwa mwenye haki na kufahamu juu ya kutofaa kwake. Kwa hivyo alikubali kuwa yeye ni mwenye dhambi mbele ya Mungu na kuomba neema yake. Na ndiyo maana Mungu alimwokoa Yakobo.
Lakini Esau alitegemea zaidi nafsi yake kuliko Bwana na hakuwa na kiu ya neema ya Mungu. Hivyo Mungu alimpenda Yakobo na kumchukia Esau. Hili ni neno la kweli.
Mungu ametuchagua pasipo sharti kupitia wokovu katika Yesu. Wenye dhambi wote wanacho hitaji kufanya ni kumwamini Yesu. Ndipo ukweli na haki ya Mungu vitaingia ndani ya mioyo yao. Wenye dhambi hawana haja ya kutenda lolote bali kuamini kwa moyo wote namna ya kuokolewa kupitia Yesu. Linalo hitajika kufanyika ni kuamini ukombozi kupitia Yesu.
 

KANUNI YA UONGO KATIKA UTAKASO WA HATUA KWA HATUA

Je, ni kweli mwenye dhambi 
ataweza kutakasika hatua hadi hatua 
kufikia kuwa mwenye haki?
Hapana. Haiwezekani. Mara moja na kwa 
wakati wote, Mungu amewafanya wenye dhambi 
kuwa wenye haki na wasio na doa kupitia 
ukombozi wa ubatizo na kifo 
chake pale msalabani.

Shetani huwalaghai wenye dhambi kwa kanuni ya utakaso wa hatua kwa hatua ili wasiweze kuokolewa kwa dhambi zao. Utakaso wa hatua kwa hatua maana yake wenye dhambi kuwa watakatifu kutoka hatua moja kwenda nyingine baada ya kumwamini Yesu.
Kanuni hii ipo kama ifuatavyo. Mwenye dhambi hawezi kuwa mwenye haki mara moja kwa wakati wote bali huokolewa kwa dhambi zake za asili tu kwanza pale anapomwamini Yesu. Dhambi halisi, yaani zile azitendazo siku hadi siku hutakaswa kwa kupitia sala za toba na hivyo kumfanya mtu atakaswe hatua moja kwenda nyingine.
Ulaghai wa kanuni hii ni ule utakaso wa viwango. Hii inaweza kuonekana kuwa ni vyema hivyo kumfanya mtu amwamini Yesu na hivyo kwa kupitia viwango ataweza kuwa mkristo aliye mtakatifu. Kanuni hii imewadanganya wakristo wengi kwa miongo mingi kwa kuwafanya wajihisi ni salama salimini. Ndiyo maana sababu kwa nini wapo wakristo wenye viwango vya juu vya utakatifu kuliko wengine katika ukristo. 
Hudhani kuwa siku moja kirahisi watakuja kubadilika na kutotenda dhambi tena. Lakini matokeo yake huishi maisha yao wakiwa wenye dhambi na watahukumiwa kama wenye dhambi mbele ya Mungu baada ya kifo. 
Hebu soma neno la kweli la Biblia. Katika Warumi 8:30 “Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita na wake aliowaita hao akawahesabia haki na wale aliowahesabia haki hao akawatukuza.”
Na katika mstari wa 29 “maana wale aliowajua tangu asili aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.” Mwanzo ukiangalia utadhani kuwa zipo hatua za kuweza kuwa mwenye haki. Lakini neno linatueleza kwamba haki imetolewa mara moja kwa wakati wote.
“Na wale aliowaita hao akawahesabia haki” Yesu aliwaita wenye dhambi na kuwafanya kuwa haki kupitia ubatizo wakekatika mto Yordani na kifo chake msalabani.
Hivyo mtu anayeamini ukombozi katika Yesu anakuwa mtoto mtukufu kwa Mungu. Ni kwa neema ya Mungu kukomboa wenye dhambi na kuwatukuza katika jina hili.
Hivi ndivyo Mungu anatueleza. Lakini baadhi ya wakristo hutuambia kuangalia katika Warumi 8:30 “Zipo hatua za utakaso. Je, haina maana tunabadilika hatua kwa hatua?” Hivi ndivyo wanavyodanganya. Huwaeleza watu kwa wakati ujao kwamba wenye dhambi wataweza kuwa wenye haki kwa wakati. 
Lakini biblia inatuambia si katika wakati ujao bali wakati uliopita mkamiliu kwamba tumekwisha fanywa wenye haki mara moja na kwa wakati wote. Ipo tofauti ya wazi kati ya swala la wakati ujao na ule wakati uliopita mkamilifu.
Yatupasa kuamini Biblia kikamilifu. Kutokana na vile ilivyoandikwa, tutaweza kuwa watoto wa Mungu mara moja na kwa wakati wote. Hii ni tofauti na fundisho la utakaso wa hatua kwa hatua.
Utakaso wa hatua kwa hatua fundisho lake husema kwamba dhambi za asili ndizo zenye kusamehewa pale tunapomwamini Yesu. Hii hupelekea kwamba yatupasa kuishi maisha ya kidini na kutubu dhambi kila siku hivyo tunaposimama kutubu dhambi kila siku, hivyo tunaposimama mbele ya Mungu ndipo tunapo kuwa wenye haki.
Kwa sababu watu wengi huamini kanuni hii hivyo huendelea kubaki kuwa wenye dhambi hata baada ya mumwamini Yesu. Ndiyo maana utakaso wa hatua kwa hatua si kanuni iliyo ya kweli.
Biblia inatueleza wazi kwamba tunakuwa wenye haki na wana wa Mungu kwa imani. Kama ilivyo watoto wanavyozaliwa duniani, wana wa Mungu pia hutakaswa punde wanapogundua na kuamini ukombozi wa Yesu. Kanuni hii ya uongo, utakaso wa hatua imechipuka kutokana na ulaghai.
 

UKOMBOZI WA DHAMBI ULIO KAMILI

Yatupasa kufanya nini ili 
tuweze kutakaswa kabisa?
Yatupasa kuamini ukombozi 
kwa maji na kwa Roho.

Warumi 8:1-2 inasema “sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule uliokatika Kristo Yesu imeniacha huru mbali na sheria ya dhambi na mauti” Hii inatuambia kwamba Mungu aliwafanya wenye dhambi wote kuwa wenye haki na kuwakomboa wale wote walio kuja kwa Yesu toka sheria ya dhambi na mauti.
Biblia inatueleza juu ya ukombozi uliokamili katika Waebrania 9:12. “Wala si kwa damu ya mbuzi na ndama bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika patakatifu akiisha kupata ukombozi wa milele.” Hii inamaana kwamba sisi wenye kumuamini Yesu tumekombolewa na kukubalika mbinguni.
Tuliisikia na kuiamini injili ya aukombozi wa maji na kwa Roho katika Kristo Yesu na kusamehewa dhambi zetu zote. Lakini wenye dhambi wanao amini kwamba walisamehewa dhambi zao za asili tu hawatoweza kuokolewa kabisa. Ili waweze kutakaswa kwa dhambi walizotenda baada ya kumwamini Yesu, hudhani kuwa imewapasa kutubu kila siku.
Imani hii potofu huwapeleka motoni. Kuamini kwao kwa kimakosa husababisha waingie kwenye sala za toba kila siku ili waweze kuwa huru kwa makosa yao yote. Hii si imani ya kweli ambayo inatuokoa toka motoni.
Kama wangeli mwamini Yesu na kukombolewa mara moja na kwa wakati wote, wangeliweza kuwa wenye haki na wana wa Mungu. Ukombozi wa kweli huwafanya wanao amini kuwa wenye haki na kuwageuza kuwa wana wa Mungu mara moja na kwa wakati wote.
Ingawa wenye kuamini hukombolewa kwa dhambi zote za ulimwengu, miili yao haibadiliki hadi siku ya kufa kwao. Lakini mioyo yao hufurika haki ya Mungu. Kamwe tusielewe vibaya juu ya ukweli huu. Biblia inatueleza ya kwamba tunatakaswa na kuwa wenye haki pale tunapo amini injili.
Hebu tuangalie Waebrania 10:9-14 ili tuone injili ya kweli “ndipo aliposema tazama nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza ili kusudi alisimamishe la pili. Katika mapenzi hayo mmepata utakaso kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu. Na kila kuhani husimama kila siku na kufanya ibada kutoa dhabihu zile zile mara nyingi ambazo haziwezi kabisakuondoa dhambi. Lakini huyu alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi mkono wa kuume wa Mungu tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.”
“Katika mapenzi hayo mmepata utakaso kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu” Gundua ya kuwa hapa imeandikwa kwa wakati uliopita na si wakati ujao.
Ili kuweza kutakaswa kikamilifu, sisi sote yatupasa kuamini ukombozi wa maji na Roho ambao Yesu ametupatia.

YESU AMETUPATIA UKOMBOZI MARA MOJA NA KWA WAKATI WOTE.

Kwa nini mtu imepasa kufurahi 
siku zote? (1 Thesalonike 5:16)
Kwa sababu Yesu alibeba dhambi zote, 
hivyo mtu hawezi kujizuia zaidi ya 
kushukuru kwa unyenyekevu kwa 
Rehema za Mungu.

Ikiwa tunaamini juu ya ukombozi wa milele kwake Yesu basi tunakuwa wenye haki mara moja na kwa wakati wote. Biblia inasema “Furahini siku zote, ombeni bila kukoma shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu” (1 Wathesalonike 5:16-18).
Furahini siku zote. Je, tutawezaje kufurahi muda wote? Wale wote waliopokea ukombozi wa milele mara moja na kwa wakati wote ndiyo watakaoweza kufurahi pasipo kikomo. Kwa sababu wamewekwa huru toka dhambini, wapo salama katika kujua kwamba Yesu alizichukua dhambi zote katika Yordani. Wamekuwa wanyenyekevu mbele za Mungu na kushukuru kwa Rehema zake na hivyo watakuwa wenye furaha bila kikomo. 
“Heri waliosamehewa makosa yao, na waliositiriwa dhambi zao” (Warumi 4:7). Hii haina maana kwamba dhambi zetu zimesitiriwa kiasi kwamba bado zinendelea kuwepo katika mioyo yetu. Mioyo yetu imetakaswa, Yesu amekwisha safisha dhambi zote na kutuokoa mara moja na kwa wakati wote.
Ukombozi huu wa milele ndiyo unaozungumziwa katika Agano Jipya. Yesu alipo batizwa alisema “Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15).
Kama ilivyo mbuzi au mwanakondoo alivyobeba dhambi za watu kupitia kuwekewa mikono katika Agano la Kale, Yesu alibeba dhambi zetu zote ulimwenguni na kutakasa wanadamu kwa njia inayo stahili na muafaka.
“Kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” alisema Yesu. Yesu alibatizwa kwa njia inayostahili na kubeba juu yake dhambi za dunia. 
Haki ya Mungu ilikamilishwa. Tusijaribu kuchukulia kwa kuelewa juu ya swala hili la ukombozi wa milele. Bali yatupasa kulichukulia likiwa ni neno la ukombozi wa Mungu. “Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake” (Zaburi 32:1).
Dhambi zote za mwilini na moyoni, Yesu alikwisha zibeba pale alipo batizwa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani. Alihukumiwa kwa dhambi tuzitendazo katika ulimwengu huu ulio haribika na kupotea. Baada ya kuzibeba, alikufa msalabani.
Yeyote anaye amini juu ya ukombozi wa dhambi atakuwa mwenye haki na asiye na doa mara moja na kwa wakati wote. Kwa kuwa Yesu yu hai milele, basi yeyote yule aaminiye ukombozi wa Kristo ataendelea kuwa mwenye haki.
Tutaweza sasa kusimama mbele ya Mungu kifua mbele na kusema “Salam Bwana! Naamini kuwa wewe ni mwana wa pekee, Yesu Kristo nami pia ni mwana kwako. Nashukuru Baba. Nashukuru kwa kunikubali kuwa mwana wako. Hii si kwa sababu ya matendo yangu, bali tu kwa imani ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho kupitia kwake Yesu. Umeniokoa toka dhambi zote za ulimwengu. Naamini yote unayosema “kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15). Kupitia ubatizo wa Yesu na msalaba wake, nimekuwa mwana kwako. Kwa hilo ninakushukuru.”
Je, umekwisha mtwika dhambi zako zote Yesu? Je, dhambi zako zote zimekwisha kubebwa naye? Biblia inatueleza kwamba, shukrani kwa ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani, kwa wenye dhambi hutakaswa kwa kuamini hayo.
 

UHUSIANO KATI YA UBATIZO WA YESU NA UKOMBOZI

Ni upi uhusiano kati ya ubatizo 
wa Yesu na ukombozi?
Ubatizo wa Yesu ni mfano wa ukombozi 
uliobarikiwa kwa njia ya kuwekewa mikono 
katika kipindi cha Agano la Kale.

Fikiria mtu mwenye kuishi akiwa na dhambi ingawa anamwamini Yesu na kuomba kanisani kwa kusema “Mungu wangu tafadhali nisamehe dhambi zangu nilizo tenda juma lililopita. Nisamehe kwa dhambi zilizopita katika siku tatu; Oh Bwana nisamehe kwa dhambi za leo. Namwamini Yesu.”
Hebu tuseme kwamba mtu huyu atasamehewa dhambi zake za kila siku kwa sala hii. Lakini hata hivyo, akaendelea tena na maisha ya dhambi. Hivyo atakuwa mwenye dhambi tena.
Yesu alikuwa Mwana kondoo wa Mungu na kubeba dhambi za wale wote wenye dhambi kupitia ubatizo na kuwakomboa kwa kusulubiwa msalabani. Ili kuweza kukombolewa wenye dhambi imewapasa kuamini yafuatayo.
Dhambi zote alibeba Yesu pale alipobatizwa na Yohana Mbatizaji, hivyo kuitimiza haki yote ya Mungu. Dhambi zote za ulimwengu zilisafishwa. Yeyote anayeamini ukweli huu amekombolewa. Kama ilivyo andikwa katika Mathayo 3:13-17 “hivi ndivyo” Yesu alivyobatizwa na Yohana Mbatizaji na kuwa mwokozi wa wote wenye kuamini.
Injili ya kweli hutueleza kwamba Yesu alibeba dhambi ya dunia mara moja na kwa wakati wote. Lakini wanatheolojia waongo hutueleza kwamba tunakombolewa kila siku. Tunamwamini nani? Je, tumekombolewa mara moja na kwa wakati wote, au tunakombolewa kila siku? 
Bila shaka Yesu alitukomboa mara moja na kwa wakati wote. Imani ya kweli ni kuamini juu ya ukombozi wa maji na Roho ulio mara moja na kwa wakati wote. Wale wote wenye kuamini kwamba yatupasa kukombolewa kila siku hakika hawata kombolewa milele.
Imewapasa kujua kwamba ukombozi wa kweli huja kwa kumwamini Yesu kuwa ametukomboa mara moja na kwa wakati wote kupitia ubatizo wake na kifo chake mslabani. Kile kitupasacho kufanya ni kumshukuru Mungu na kuamini injili ya kweli.
Ila wale wote wanaopotoka katika imani zao kwa kusema kwamba wamekombolewa kwa dhambi zao za asili tu hivyo imetupasa kuwa wenye haki hatua kwa hatua, hili ni kosa.
Ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani vyote vimekamilisha msamaha wa dhambi mara moja na kwa wakati wote. Hii ndiyo kweli. Dhambi zetu zilipaswa kutwikwa juu yake Yesu kupitia ubatizo wa Yohana Mbatizaji na hivyo Yesu ilimpasa afe msalabani ili sisi tuweze kuokolewa.
Kutamka “nisamehe” baada ya kutenda dhambi hakuitimizi haki ya Mungu. Sheria ya Mungu inasema kwamba mshahara wa dhambi ni mauti. Yatupasa kuelewa hili kuwa Mungu ni wa Haki na Mtakatifu.
Wale wenye kuomba mbele ya Mungu “Nasikitika tafadhali nisamehe” baada ya kutenda dhambi hakika hawa hawaifahamu haki ya Mungu. Huomba msamaha lakini hujaribu kupooza dhamira zao tu. Je, ni haki kweli mtu kutenda dhambi kila siku na kujipa moyo ndani ya dhamira yake kwa kurudia rudia kutubu kwa ajili ya makosa yake? Njia pekee ya kuweza kukombolewa ni kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Inatubidi kuamini kwa mioyo yetu yote. Ni njia pekee ya kuweza kukwepa hukumu ya Mungu.
Hebu tufikiri zaidi juu ya ukombozi wa dhambi Waebrania 9:22 inasema “na katika torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.”
Kulingana na sheria ya haki ya Mungu, dhambi huitajika kufutwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo la dhambi. Hii ni sheria ya haki ya Mungu pasipo kulipa mshahara wa dhambi, hapatoweza kamwe kuwepo na ondoleo.
Sheria ya Mungu ni ya haki. Yesu alibatizwa na Yohana Mbatizaji na kumwaga damu yake msalabani kutukomboa wenye dhambi. Alibeba makosa yetu yote kupitia ubatizo na kumwaga damu yake msalabani kwa ajili ya dhambi zetu zote. Alilipa mshahara wa dhambi zetu.

Je ukombozi hutolewa mara moja 
kwa wakati wote au kila siku?
Mara moja kwa wakati wote. Yesu alibeba 
dhambi zote za wenye dhambi 
kupitia ubatizo wake.

Katika Mathayo 3:15 wakati Yesu alipobatizwa kwa njia ipasavyo, alisafisha dhambi zote kupitia ubatizo na kufa juu ya msalaba kutuokoa na dhambi zote za dunia.
Kuomba kusamehewa kila siku kutakuwa sawa na kumhitaji Yesu kubeba dhambi zetu na kufa kwa mara nyingine. Yatupasa kuielewa vyema sheria ya Mungu. Haipasi tena Yesu kufa kwa mara nyingine ili kutuokoa kwa dhambi zetu.
Mungu huchukulia hili kuwa ni ubaradhuli kwa wale wote wenye kumwamini Yesu kuendelea kuomba msamaha kila mara kwa dhambi za kila siku. “Hawa ni wapumbavu! Wana hitaji mwana wangu wa pekee, Yesu, kubatizwa kwa mara nyingine tena ya pili na kufa msalabani! Wanaamini ukombozi katika Yesu na bado wanajuta wenye dhambi! Nitawahukumu kwa sheria yangu na kuwatupa katika kina cha moto. Je, mpo radhi kumwua mwana wangu wa pekee kwa mara ya pili tena? Mnanihitaji kumwua kwa sababu ya dhambi zenu za kila siku. Tayari nilikwisha kumwua ili kuwaokoa mara moja na kwa wakati wote kwa dhambi zenu zote ulimwenguni. Hivyo msipandishe ghadhabu yangu kwa kutaka niwasamehe dhambi zenu za kila siku, mnachopaswa kufanya ni kuamini injili ya ukombozi katika maji na Roho.”
Yesu huwaambia wale wenye kubaki wakiwa na dhambi kwamba yawapasa waende kanisani ambamo injili ya kweli huubiriwa hivyo kuachana na imani potofu na kupokea ukombozi kwa kupinga imani ya uwongo.
Sasa ni wakati wako wa kuokolewa kwa kuamini kwa moyo wako wote. Je. Unaamini?
 

MATOKEO YA IMANI ISIYO YA KWELI ITOKAYO KATIKA MATENDO

Kwa nini wakristo walio 
wengi hushindwa kuishi maisha ya 
kiimani moja kwa moja?
Kwa sababu huishi kwa kutegemea 
matendo yao.

Hata wenye dhambi wenye kumwamini Yesu lakini wangali bado hawajakombolewa wataweza kung’ara kwa muda wa miaka 3 hadi 5. Hupata hamasa mwanzoni, lakini imani yao huanza kuyeyuka siku hadi siku. Ikiwa unamwamini Yesu kupitia matendo yako, hamasa yako hupote pia.
Kipofu hawezi kuona. Hivyo hutegemea viungo vingine vya hisia kwa ajili ya kukusanya ufahamu kwa njia hii. Hivyo wanapohisi machozi kutoka hukosea kwa kudhani ndiyo ishara ya ondoleo la dhambi. Ondoleo la dhambi lililo la kweli si habari ya hisia.
Kipofu wa kiroho hutafuta kurudi katika upendo wao wa mwanzo kwa kuhudhuria mikutano ya uamsho katika hali isiyo na mwelekeo, lakini hawawezi kurudisha hisia. Ondoleo la dhambi vile vile ni jambo lisilo rahisi kupata. Ikiwa watu wa aina hii wangeliamini vile ipasavyo toka mwanzo ondoleo la dhambi na Rehema ya Mungu ingeng’ara zaidi kama vile nuru ilivyo nyakati za mchana.
Lakini ondoleo la dhambi lisilo la kweli hung’ara katika siku za mwanzo tu na kuanza kutoweka kadri muda unavyokwenda. Nuru ya hamasa punde hutoweka kwa sababu kipofu wa roho alishindwa kusikiliza injili ya kweli toka mwanzo.
Waandishi na Mafarisayo wanafiki hubeba Biblia mikononi, hushika kwa kumbukumbu sala ya Bwana na kanuni ya mitume na kuomba muda wote. Hupandishwa vyeo makanisani na kupandwa hamasa huku dhambi zao zikiongezeka na mwishowe kukataliwa na Mungu. Kwa nje wamefunikwa na ganda la udini, lakini ndani fikra zao zimeoza kwa dhambi. Na hii ndiyo matokeo ya imani isiyo ya kweli yenye kutegemea dini na matendo mema.
 

TUNAKUWA WENYE HAKI KWA IMANI

Je, ukombozi wa dhambi zote 
hapa duniani ulikwisha timia?
Ndiyo. Ulikwisha timia kupitia ubatizo 
wa Yesu na kifo chake msalabani.

Hebu tusome Waebrania 10:16-18 “hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana. Nitatia sheria zangu mioyoni mwao. Na katika nia zao nitaziandika ndipo anenapo. Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi ondoleo la hayo likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.”
Hivyo sasa tumekombolewa kupitia maji ya ubatizo wa Yesu na damu ya msalaba wake, hatuhitaji tena upatanisho wa dhambi. Hili linaweza kuonekana ni jipya kuweza kusikia, lakini ni kulingana na maneno ya Biblia. Je, haya ni maneno ya mwanadamu? Biblia ni dawati la kupimia na ni biriji ya kupimia kila kitu.
“Na baada ya siku zile anena Bwana. Nitatia sheria zangu mioyoni mwao. Na katika nia zao nitaziandika” (Waebrania 10:16) Unajisikiaje pale baada ya kukombolewa? Sasa moyo wako upo huru kwa dhambi na unajisikia vyema. Umekuwa mtu mwenye haki na utakuwa nuruni.
Na Bwana anasema katika Waebrania 10:17 “Dhambi zao na uasi wao sita ukumbuka tena kabisa” Anatuambia kuwa hatokumbuka dhambi tena na yale matendo ya uovu ya yule aliyekombolewa. Kwa nini? Kwa sababu Yesu alibatizwa kwa njia iliyo stahili, “hivi ndivyo”. Baada ya kuzichukua dhambi zote, Yesu alihukumiwa kwa niaba ya wale wote wenye kumwamini.
Sasa leo hii alikwisha lipa dhambi zetu zote, ingawa tutaweza kuzikumbuka lakini hatuhitaji kujisikia hukumu juu yake. Hatuwezi tena kufa kwa dhambi zetu kwa sababu Yesu alitakasa dhambi zote na kutoa damu yake pale msalabani kwa ajili yetu.
Waebrania 10:8 inasema “Basi ondoleo la hayo likiwapo hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” Hii maana yake ni kwamba, Yesu amefutilia mbali dhambi zote za ulimwengu. Na pia kwa wale waliozaliwa upya katika Yesu hawahitajiki tena kutoa sadaka (kafara) kwa ajili ya dhambi zao.
“Oh Mungu, tafadhali nisamehe. Sababu ya kumwamini Yesu na bado kuishi kombo ni kwamba bado sijakombolewa. Mimi ni mkristo, lakini mawazo yangu yameoza kwa dhambi kabisa.” Hatuhitaji kusali namna hii!
Wenye dhambi hutenda dhambi pasipo kuelewa juu ya hili. Hawajui nini maana ya dhambi kwa sababu hawajui sheria ya kweli ya Mungu, wanachojua ni kupitia hisia zao kwamba wasitende makosa lakini hawajui nini maana yake kutenda dhambi mbele ya Mungu. Mungu ametuelekeza bayana kwamba ni dhambi kutomwamini Yesu.
Katika Yohana 16:9 Mungu anasema nini maana ya kutenda dhambi mbele ya Mungu. “Kwa habari ya dhambi kwa sababu hawaniamini mimi” Ni dhambi mbele ya Mungu kutomwamini yeye. Yohana 16:10 inasema huu ya haki. “Kwa habari ya haki kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba wala hamnioni tena.” Kwa maneno mengine Yesu tayari alikwisha kukomboa dunia tokana na dhambi zote na hivyo haitaji tena kukomboa kwa mara nyingine kwa ubatizo na kifo chake msalabani.
Huwaita wale wote wenye kuamini ukombozi, kwa ajili ya kuwatakasa na kuwafanya wenye haki. Ukombozi katika dunia ulikwisha timizwa kupitia ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani. Hakuna tena ukombozi unaohitajika kwa ajili ya kuokoa wenye dhambi.
“Kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12). Yesu alishuka duniani, alibatizwa na Yohana Mbatizaji, na kutoa damu yake msalabani ili kuwakomboa wenye dhambi wote. Amini hili kwa moyo wako wote na uokolewe. Yesu amekutakasa kwa maji na Roho.
Yesu alisafisha dhambi zetu zote katika miili kupitia maji na Roho. Tumeokolewa kwa imani. Ikiwa tutaamini ukweli huu, ikiwa tutaamini injili kupitia Yesu Kristo, tutakuwa wenye haki mara moja na kwa wakati wote. Ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani; haya mambo mawili yameunda msingi wa ukweli.
 

MAANDIKO AMBAYO WENYE DHAMBI HUTUMIA KAMA NGAO YAO.

Je, kweli tutaweza 
kuokolewa kupitia toba ya 
dhambi zetu kila siku au tayari 
tumekwisha kukombolewa?
Mungu alikwishatupatia ukombozi kwa 
dhambi zetu zote mara moja 
na kwa wakati wote.

1 Yohana 1:9 inasema “tukiziungama dhambi zetu yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.”
Itakuwa vizuri ikiwa tutahitajika kuungama dhambi zetu tu ili tusamehewe. Kwa wazo hili, baadhi ya wanatheolojia walikuja na wazo kuu la fundisho jipya. Wao husisitiza kwamba kila wakati mtu anapoungama dhambi zake ataweza kusamehewa. Je, ndivyo ilivyo rahisi kama hivi? Lakini Yesu kamwe hakusema kwamba tutaweza kusamehewa kila wakati tunapoungama mbele ya Mungu.
Je, ni kweli tutaweza kusamehewa kwa kuungama dhambi zetu tu au je, tayari tumekwisha kombolewa? Lipi kati ya haya unaamini? Watu wenye kupigia debe mafundisho ya uongo huamini kwamba husamehewa kila wakati wanapo ungama dhambi zao, lakini ukweli ni kwamba, dhambi hubaki mioyoni mwao kwa sababu hawajui maneno ya kweli ya ukombozi. Haina maana kusamehewa kila wanapoomba kusamehewa dhambi za kila siku.
Kwa sababu hii, yatupasa kuchukulia maneno ya Mungu kuhusiana na ukombozi kwa dhati hivyo kuweza kutofautisha kati ya kweli na ulaghai, ukitupilia mbali nini ulichokwisha ambiwa hapo mwanzo.
Wenye dhambi wameelewa visivyo 1 Yohana 1:9. Kwa makosa hudhani swala la kusamehewa dhambi za kila siku ni sawa. Hebu tusome mafundisho kwa uangalifu mkubwa. “Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote” Je, unadhani tunaokolewa kwa dhambi ya asili hivyo yatupasa kuungama zile za kila siku kwa kuwa yeye ni mwaminifu na wa haki hata kutuondolea dhambi? Haya ni mawazo potofu tu yatokanayo na udhaifu wa miili yetu.
Tunagundua kuwa hili si kweli pale tunapoamini ubatizo na damu ya Yesu. Dhambi zote zilikwisha safishwa kwa ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani siku nyingi, siku nyingi zilizopita.
Kuamini kutokana na roho na kuamini kutokana na mawazo potofu ni mambo mawili tofauti kabisa. Wale wanaoamini kutokana na mawazo yao binafsi huhisi hitaji la kusafisha dhambi zao kila siku, lakini wale wote wenye kuamini ukombozi kwa njia ya maji na damu huelewa kwamba wao tayari wamekwisha kukombolewa mara moja na kwa wakati wote kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake Kristo.
Wale wote wenye kuamini kwamba iliwapasa kuungama kila siku ili kukombolewa upya ukweli ni kwamba wanatenda dhambi ya kutoamini ukombozi utokanao na ubatizo na damu ya Yesu.
Je, umekwisha kukombolewa mara moja na kwa wakati wote kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake? Wale ambao hawajakombolewa bado hujaribu kutafuta wokovu kwa kuungama dhambi zao kila siku. Hii huwaacha wangali na tatizo la kutojua wafanye nini juu ya dhambi zao za kila siku watakazotenda hapo mbeleni.
Wanaweza kujaribu kuungama hata kabla ya kutenda. Lakini kwa kufanya hivyo huonyesha kukosa imani kwa Yesu. Watu hawa ni vipofu kwa injili ya ukombozi. Yesu ametukomboa kwa dhambi mara moja na kwa wakati wote kupitia ubatizo wake na damu kwa kuibeba hukumu yeye mwenyewe. Tumekombolewa kwa kumwamini yeye tu. 
Ikiwa unadhani imekupasa kuungama hata zile dhambi utakazotenda hapo mbeleni ili uokolewe, basi wewe huna tofauti na asiyeamini, yule asiye jua juu ya kuzaliwa upya kwa maji na Roho. Wenye dhambi hawawezi kukombolewa kupitia toba.
Hivyo ikiwa utaungama dhambi zako kwa uaminifu “mimi ni mwenye dhambi ambaye sijakombolewa” na pia ikiwa utasikiliza na kuamini injili ya ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani; Mungu atakukomboa tokana na dhambi zako zote.
Lakini ikiwa hutoamini injili ya ukombozi na kujificha chini ya sala ya toba tu, utakumbana na hukumu kali pale Yesu atakapo rudi mara ya pili duniani akiwa Hakimu wa Haki.
Wale wasioamini injili ya ukombozi wa maji na Roho watahukumiwa. Ikiwa watajificha nyuma ya toba watakutana na hukumu. Hivyo usisubiri siku ya Hukumu. Amini sasa katika baraka ya injili ya maji na Roho.
 

TOBA NJEMA NA IMANI YA KWELI

Toba ipi iliyo njema kwa 
wote wenye dhambi?
Kutubu kwamba bado wana dhambi 
na watakwenda motoni ikiwa
hawatoiamini injili ya kweli.

Mungu alitukomboa mara moja na kwa wakati wote. Hapa upo mfano wa kweli wa maisha katika kuelezea kile ninachosema. Hebu tufanye mfano, mpelelezi wa Korea ya Kaskazini amekuja Korea ya Kusini. Akaona vile tulivyofanikiwa na kujua amedanganywa na kuamua kujisalimisha.
Baada ya kwenda kituo cha polisi kilichokaribu naye, ataweza kukiri kama ifuatavyo “mimi ni mpelelezi toka Kaskazini” au “Nimekuja hapa Kusini kutaka kuwaua watu kadha wa kadha na kulipua hiki na kile, nimekwisha lipua hiki, lakini sasa najisalimisha. Hivyo mimi si mpelelezi tena kuanzia sasa.”
Je, toba hii ni njema? Ikiwa kweli alipenda kutubu (kukiri), kile alichopaswa kusema ni “mimi ni mpelelezi” Hivi ni kauli rahisi inayomaanisha kila kitu; ya kwamba yeye si mtu mzuri na imempasa kuhukumiwa. Kwa kauli hiyo rahisi, ukiachilia mbali mpango wake aliotumwa ataweza kusamehewa.
Kama hivi, ikiwa mwenye dhambi atatubu mbele ya Mungu “mimi ni mwenye dhambi bado sijakombolewa. Hatima yangu ni kutupwa motoni na kuhukumiwa. Tafadhali niokoe” na baadaye kumwamini Yesu, basi mtu huyo atakombolewa. Yesu alibatizwa na kumwaga damu yake kwa ajili yetu na kile tunachopaswa kukifanya ni kuamini wokovu kupitia Yesu ili tuokolewe.
Ufunuo 2:17 inasema “nami nitampa jiwe jeupe na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.” Biblia inasema kwamba kwa wale tu watakaoipokea injili ya kweli ndiyo watakao lifahamu jina la Yesu. Wale tu waliokombolewa mara moja na kwa wakati wote ndiyo wenye kufahamu siri ya kuwa mwenye haki.
Wale wasiojua hili wataendelea kuwa wenye dhambi ingawa watafanya sala za toba kila siku. Hata ikiwa mtu amekuwa Mkristo kwa miaka 10, bado ataendeea kuwa mwenye dhambi ikiwa ataendelea kuomba msamaha kila siku. Atakuwa bado si mtoto wa Mungu.
Ili waokolewe itawapasa kutubu kuwa wao ni wenye dhambi na kuamini ukombozi wa Yesu. Hii ni imani ya kweli.
 

KUTAJA ORODHA YA DHAMBI TU SIVYO 1 YOHANA 1:9 INAVYOTUELEZEA JUU YA KUTUBU

Je, imetupasa kutubu 
dhambi zetu kila siku au mara 
moja tu na kuokolewa?
Mara moja tu.

Je, yawezekana mwizi na muuaji kutubu matendo yao na kuweza kukombolewa? Wenye dhambi hawakombolewi kwa kutubu dhambi zao tu. Wataweza kukombolewa tu kupitia baraka ya injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho kupitia Yesu. Baadhi ya wakristo walio potoka hutubu namna hii.
“Mungu wangu nimegombana na mtu fulani tena leo. Nimetenda dhambi. Nimemlaghai mtu fulani. Nimeiba kitu fulani.” 
Ikiwa watu wa namna hii wataendelea namna hii Mungu atawaambia, “nyamaza wewe mwenye dhambi! Kwa hayo yote sasa unataka iweje?”
“Tafadhali endelea kunisikiliza. Mungu, umetueleza kuwa tutubu dhambi zetu. Naomba rehema yako.”
Aina hii ya sala siyo ile Mungu anayoihitaji kusikia. Yeye anachohitaji kusikia ni sala ya wale wote wenye kuamini ukombozi wa maji na Roho. Wale wote waliokiri dhambi zao na kuamini injili ya kweli na kuzaliwa upya mara ya pili.
Agustino alisema kwamba alitubu hata kwa kunyonya ziwa la mama yake. Alidhani aina hii ya toba itaweza kumuongoza katika ufalme wa mbinguni. Jambo hili ni la kutuchekesha sana. Kutubu dhambi hakutotusaidia.
Mungu anasema, Nyamaza na niambie tu ikiwa umetenda dhambi. Ikiwa unayo, basi acha kuizungumzia. Umeamini vibaya hadi sasa, kwa hivyo nenda kwenye kanisa ambalo ukweli hufundishwa. Amini injili ya ukombozi kwa njia sahihi na ukombolewa. Ikiwa sivyo, nitakuja kukuhukumu.
Kurudia rudia sala za toba na namna yoyote ya kujaribu kuokoka kupitia toba huonyesha upotofu na imani isiyo ya kweli.
Imeandikwa katika 1 Yohana 1:9 kwamba tunapokiri dhambi zetu zote injili ya maji na damu ndiyo itakayo tukomboa kwa dhambi zetu.
 

“ONDOKENI KWANGU”

Nini maana ya kutenda maovu?
Maana yake ni kumwamini Yesu huku 
ukiwa na dhambi moyoni.

Wakristo wenye dhambi wanaimani potofu, watendao maovu mbele ya Yesu. “Wengi wataniambia siku ile Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu” (Mathayo 7:22-23).
Fikiria yule anayeamini uongo atakapokufa anaposimama mbele za Mungu na kusema “Salamu Bwana? Unaonekana kuwa mzuri vile nilivyokuwa nikikuwaza nilipokuwa duniani. Lakini unaonekana mzuri zaidi hapa sasa. Nakushukuru Bwana uliniokoa. Naamini kwamba hunichukulii mimi kuwa ni mwenye dhambi ingawa ninazo moyoni. Nimekuja kwako kutokana na ahadi yako kwangu kuwa utakuja kunipeleka mbinguni. Nitakwenda huko ambapo maua mengi yamechanua. Kwa heri natumaini nitakuona huko.”
Anapoanza kuingia bustanini, lakini Yesu anamsimamisha “subiri! Hebu tuone mtu huyu kama anazo dhambi moyoni. Je, wewe ni mwenye dhambi?” 
“Bila shaka ninadhambi Bwana. Lakini je, sijakuamini wewe?”
“Je, unazodhambi hata unaponiamini mimi?” 
“Kweli ninadhambi.” 
“Nini? Unadhambi? Niletewe kitabu cha uzima. Na pia niletewe kitabu cha matendo. Tazama jina lake. Tazama ni katika kitabu kipi ameandikwa.”
Kwa uhakika jina lako limo katika kitabu cha matendo.
“Sasa taja dhambi zote ulizotenda duniani.” 
Ndipo mtu huyu atakapojaribu kukataa, lakini Mungu atamlazimisha kufungua kinywa chake ili kukiri dhambi hizo.
“Ndiyo, nimetenda dhambi kadhaa wa kadhaa.”
Huchanganyikiwa wakati wote na kushindwa kufunga mdomo wake.
“Sawa, inatosha! Uliyoyafanya yanatosha kuweza kupelekwa motoni. Inatosha na zaidi! Mpelekeni sehemu kunakowaka moto wa kiberiti.”
Hatopelekwa mahala palio na maua ya kuchanua bali sehemu iliyojaa moto na makaa. Atasaga meno huku akipelekwa motoni.
“Nilikuamini wewe Bwana, nilifanya unabii kwa jina lako, nilihubiri kwa jina lako, niliuza nyumba yangu kwa jina lako, nilifanya maombi usiku kucha, kuwatunza wagonjwa……. kweli ninastahili kwenda motoni?” 
Atasaga meno sana hata yachakae na kuisha bure. Atakapowasili motoni, atawaona wakristo wote ambao hawakuelewa mana ya ukombozi. Wale wote ambao hawakuielewa injili ya ukombozi watakataliwa na Mungu.
 

DHAMBI ZA WASIO AMINI ZIMEANDIKWA KATIKA KITABU CHA MATENDO

Ni wapi dhambi za 
wasioamini huandikwa?
Zimeandikwa katika mioyo 
yao na katika kitabu 
cha matendo.

Ikiwa tunamwamini Yesu au hapana, Mungu huwaangamiza wale wote wenye dhambi moyoni. Ikiwa atakuta tone la dhambi katika moyo wa mtu hakika mtu huyo atahukumiwa kwenda motoni katika siku ile ya hukumu. Mungu anawaasa wenye dhambi ambao bado hawaja kombolewa kukiri kwamba hawajakombolewa ikiwa wanataka kupata ukombozi.
Makosa ya mwenye dhambi huandikwa katika moyoi wake. Wale ambao tayari wamezaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho, wataweza kukumbuka dhambi zao, lakini tayari zimekwisha kusafishwa mioyoni mwao na ni wenye haki.
Lakini wale ambao hawajazaliwa upya mara ya pili bado dhambi zao zimo mioyoni mwao. Hivyo ni wenye dhambi mbele ya Mungu. Kila wanapopiga magoti na kusali, dhambi hizo huwatenganisha na Mungu na kuzuia yeye kutowasikia sala zao. Huishia kutubu tu, kuungama kwa makosa yao waliyotenda miaka 10 iliyopita, miaka 11 ilioyopita na hata 20 iliyopita.
Je, ni kweli watahitajika kutubu na kutubu katika sala zao? Kwa nini wanafanya hivyo? Hawapendi kufanya hivyo lakini pale tu wanapoanza kusali, hujikuta wakikumbuka kuwa wanadhamira isiyo njema mbele ya Mungu. Hivyo wanahisi wanahitaji upatanisho wa dhambi zao kwanza kabla ya kuomba kwa dhati.
Mungu anaandika dhambi za wanadamu kwa kalamu ya chuma yenye ncha ya almasi katika mbao za mioyo yao, hivyo kwamba dhambi zao haziwezi kufutika. Matokeo yake huhisi kwamba wanahitaji kuungama dhambi zao kila mara wanapokuja mbele ya Mungu. Hivyo wale wenye kuamini injili nusu isiyo kamili ya Yesu imewapasa kuishi maisha ya taabu wakiwa ni wenye dhambi na kuishia motoni.
Yeremia 17:1 imeandikwa. “Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao na katika pembe za madhabahu zenu.”
Yuda ni jina la kifalme la kabila la watu wa Israel. Biblia inachukulia Yuda kama uakilishi wa wanadamu wote hivyo Yuda maana yake ni watu wote ulimwenguni.
Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma na kuchorwa kwa ncha ya almasi ambayo inayoweza kuchimba chuma. Almasi ni moja ya vitu vigumu duniani. Kwa kalamu ya chuma na ncha ya almasi ndivyo huandikwa. Dhambi hizo zinapochorwa kamwe haziwezi kufutika. Hazitoweza kufutika ikiwa hatutoamini ukweli wa maji na Roho.
Kama dhambi zisivyoweza kufutika pasipo ubatizo wa Yesu, wenye dhambi wataendelea kuzikumbuka kwa kusema “Bwana, mimi ni mwenye dhambi,” kila wanaposali. Bado wanadhambi mioyoni mwao ingawa kwa kiasi kikubwa hujaribu kuwa na usharika na Mungu kwa kubeba majukumu mengi kanisani na kujifunza theologia na kanuni.
Hivyo hudiriki kupanda milimani kujaribu pasipo mwelekeo kwa kunena kwa lugha na kutafuta maono ya miali ya moto, lakini haina maana. Ikiwa dhambi zitaendelea kuwa moyoni, kamwe hautokuwa na amani.
Kama ilivyoandikwa katika Yeremia 17:1, dhambi zetu zimechorwa katika pembe za madhabahu. Mbinguni kuna vitabu vya uzima na matendo. Dhambi zote za waovu zimeandikwa katika kitabu cha matendo na watu hawawezi kukwepa makosa yao. Mungu huandika katika kitabu cha Matendo na mbao za dhamira zetu, dhambi zetu na kutuonyesha kupitia sheria yake.
Inatubidi kufuta kumbukumbu hizo kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu aliyomwaga kwa ajili yetu na kutuokoa. Na ndipo tutakuwa tayari kwa uzima wa milele na majina yetu yataandikwa katika kitabu cha uzima.
 

JE, JINA LAKO LIMO KATIKA KITABU CHA UZIMA?

Majina ya nani yameandikwa 
katika kitabu cha uzima?
Majina ya wale wote wasio na dhambi 
katika mioyo yao ndiyo yaliyo 
orodheshwa humo.

Ni muhimu sana jina lako kuandikwa katika kitabu cha uzima. Ikiwa jina lako halijaorodheshwa humo, kuna maana gani kumwamini Yesu? Ili uweza kukombolewa kwa hakika yakupasa kuamini juu ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Yesu alishuka duniani alibatizwa alipotimiza miaka 30, alitakasa dhambi zote za ulimwengu na kufa msalabani kutukomboa. Kama ilivyoandikwa katika Mathayo 3:15 “hivi ndivyo” Yesu alivyobatizwa na kusulubiwa msalabani. Yatupasa kuamini hivi ili majina yetu yaweze kuandikwa katika kitabu cha uzima.
Watu wanapokufa na kusimama mbele ya Mungu, Mungu atasema “Angalia mtu huyu ikiwa jina lake limeandikwa katika kitabu cha Uzima.”
“Limo Bwana.”
“Ndiyo, umeteseka na kutoa machozi ukiwa duniani kwa ajili yangu, sasa nitafanya hivyo ili usijeukateseka tena.”
Mungu humpa taji la haki likiwa ni malipo yake mtu huyo.
“Nakushukuru Bwana. Nafurahia daima.”
“Malaika, weka taji juu ya mtu huyu.”
“Bwana, inatosha na zaidi kwa kuwa umeniokoa. Taji litakuwa ni zaidi kwangu. Nakushukuru. Nafurahia daima kwamba uliniokoa. Nimeridhika na zaidi kwa kuwa katika uwepo wako.”
“Malaika pigeni magoti na mumpokee mtoto huyu wa 10,000 katika orodha yangu, mpakieni mgongoni.”
Ndipo malaika watajibu “Ndiyo Bwana!”
“Tafadhali panda mgongoni mwetu.”
“Ni raha iliyoje. Kweli ni mimi mwenye kufanyiwa haya? Twendeni.”
Malaika watatembea kwa uangalifu.
“Je, utapenda kutembea mwenyewe?”
“Loo! Hapa ni pazuri sana. Je, ni pakubwa kiasi gani?”
“Nimekwisha tembea sehemu yote hapa takribani mara bilioni katika miaka, lakini sijaona mwisho.”
“Je ni kweli? Sasa nitakuwa mzito kwako. Utaweza kuniweka chini tu.”
“Hatupungukiwi nguvu hapa.”
“Nashukuru, lakini ningependa kusimama katika ardhi ya ufalme wa mbinguni. Sasa, wako wapi wale wote wenye haki na ambao wapo hapa kabla yangu?”
“Wapo pale.”
“Hebu na tuende.”
Haleluya! Wanakumbatiana na kuchekeana na kuishi kwa furaha kuanzia hapo.
Sasa, hebu fikiria juu ya yule anayemwamini Yesu lakini bado anaendela kuwa na dhambi anapokufa na kwenda mbele ya Mungu. Yeye pia atasema kwamba anamwamini Yesu na kukubali kuwa ni mwenye dhambi.
Mungu atasema “angalia ikiwa jina lako limeandikwa katika kitabu cha Uzima.”
“Halipo katika kitabu cha Uzima.”
“Hebu tazama katika kitabu cha matendo.”
“Jina lake na dhambi zake zimo humo.”
“Sasa basi mpeleke mtu huyu sehemu ambayo kamwe hatoweza kuwa na wasiwasi juu ya gharama ya mafuta ya kuunguzia na akae hapo milele.”
“Lo! Mungu, hivi si halali….”
Atasema si halali. Kwa nini atupwe motoni hali alikuwa akimwamini Yesu kwa bidii?
Sababu ni kwamba alidanganywa na shetani na hivyo kusikiliza nusu ya kweli katika injili. Ikiwa tutaelewa vibaya maana halisi ya ukombozi wa Yesu, hakika nasi tutaishia motoni.
Mtu huyu alimwamini Yesu lakini alidanganywa na shetani na kudhani kuwa hakuwa mwenye dhambi. Kama angelisikia injili ya kweli, angeligundua kwamba imani yake ilikuwa si sahihi. Lakini alishindwa kuamini kutokana na kushikilia ubinafsi kwa imani zake potofu.
Ikiwa unataka kwenda katika ufalme wa mbinguni yakupasa uamini katika kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Kama ilivyoandikwa katika Mathayo 3:15, “hivi ndivyo” Yesu alivyobeba dhambi zote za ulimwengu. Yakupasa kuamini wokovu katika maji na damu.

Majina ya nani yameandikwa 
katika kitabu cha Matendo?
Majina ya wale wote walio na dhambi 
moyoni mwao ndiyo 
yaliyoorodheshwa humo.

Ikiwa umechagua kuamini chochote kama vile mtu mwadilifu asiye penda kuingilia uhuru wa mtu mwingine kamwe, utaweza kuishia motoni. Wapo watu waadilifu wengi motoni, lakini kule mbinguni wapo wapiganaji wa kweli waliopigania walichokiamini.
Wale walio mbinguni walijua kwamba wao ni wenye dhambi waendao motoni na kwa furaha waliamini yakuwa dhambi zao zilitakaswa kwa njia ya ubatizo na damu ya Yesu.
Inasemekana kwamba yapo marundo ya masikio na midomo kule mbinguni. Kwa kuwa watu wengi wanaamini ukombozi wa Yesu kwa midomo na masikio yao, basi Mungu hutupa viungo vya mwili vilivyobaki katika moto wa kiberiti uwakao.
Hebu fikiria yule anayemwamini Yesu lakini bado ni mwenye dhambi moyoni anaposimama mbele ya Mungu na kusema “Bwana watu waliniita mimi ni mwenye haki kwa sababu nilimwamini Yesu, ingawa ninadhambi moyoni. Naamini kwamba hata wewe pia utaniona kuwa sina dhambi. Hivi ndivyo nilivyojifunza na kuamini. Niliamini kile tu watu wengi walichoamini. Ilikubalika kwa wote imani hii katika sehemu niliyokuwepo.”
Ndipo Bwana atakapo jibu “siwezi kamwe kuwasamehe wale wote walio na dhambi mioyoni mwao. Nilisafisha dhambi zenu zote kwa baraka ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Lakini umeshindwa kuamini hili. Malaika! Mtupilie mbali huyu mtu baradhuli katika moto wa milele!”
Yeyote anayemwamini Yesu huku akidhani kuwa bado anadhambi moyoni ataishia motoni. Isikilize injili ya ukombozi na ukombolewe kwa dhambi zako zote. Ama sivyo utakwenda motoni.
Kusema kuwa huna dhambi huku ukiwa na dhambi moyoni ni kumlaghai Mungu. Tunaweza kuona namna ilivyotofauti kati ya wenye dhambi na wenye haki katika siku ile ya mwisho. Utagundua ni kwa nini ninawasisitizia kukombolewa.
Utaona tofauti kati ya wale wanaoamini ukombozi uliokamilika (Ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani) na wale wasioamini huku wakisimama njia panda kati ya Mbinguni na motoni.
Je, bado unamwamini Yesu lakini bado umebaki kuwa ni mwenye dhambi? Sasa basi unapaswa kuelewa kwamba imekupasa kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Mungu huwatupa wale wote wenye dhambi mioyoni motoni. Ni wale tu wanaoamini msamaha kamili wa dhambi ndiyo watakaoingia mbinguni.
Kubali sasa. Ukidharau yaweza kuwa utachelewa. Uwe tayari kabla. Kabla hujaishia motoni, amini ukombozi wa maji na Roho na utakaswe.
Utukufu ni kwa Bwana Yesu! Tunashukuru kwa fadhila zake za kutufanya sisi wenye dhambi kuwa wenye haki. Haleluya!
 

YESU: KIELELEZO CHA HAKI

Je, dhambi zetu zitaweza 
kufutwa kwa sala ya toba?
Hapana. Hakika haitowezekana kabisa. 
Hii ni mojawapo ya njia za 
shetani katika kutulaghai.

Hebu tusome 1 Yohana 2:1-2, “watoto wangu wadogo nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye mwombezi kwa Baba Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.”
Je, unaona kilikichoandikwa hapa? Sasa yupo yeyote anayeamini hali akiwa na dhambi moyoni? Ikiwa unadhambi moyoni na huku ukimwambia Mungu kwamba huna, unamdanganya Mungu. Na pia unajidanganya mwenyewe.
Laini ikiwa unamwelewa Yesu vyema na kuamini kile alichokifanya katika kutakasa dhambi pale Yordani, utaweza kuwa huru kwa dhambi na kwa hakika unaweza kusema “Bwana, nilikwisha zaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho kupitia kwako. Sina dhambi. Nitaweza kusimama mbele yako pasipo aibu.”
Ndipo Bwana atakapokujibu “ndiyo, unasema kweli kama vile Abrahamu alivyoniamini na kujiamini yeye binafsi ili kuwa mwenye haki, nawe pia ni mwenye haki kwa sababu nilikwisha takasa dhambi zako zote.”
Lakini hebu chukulia yule mwenye dhambi moyoni hali ikiwa anamwamini Yesu. Husema “Kwa kuwa namwamini Yesu, nitakwenda mbinguni hata ikiwa ninadhambi chache moyoni.”
Mtu huyu hutamani sana kuingia mbinguni kiasi kwamba atakaposimama katika kile kiti cha hukumu atakuwa mbishi kukubali hukumu atakayopewa hata hivyo bado atakwenda motoni. Kwa nini? Hakuitambua baraka ya injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Kila mtu imempasa kukiri kuwa ni mwenye dhambi katika kipindi cha maisha ya hapa duniani. “Mimi ni mwenye dhambi. Nitakwenda motoni. Tafadhali niokoe Bwana” Mwenye dhambi haokolewi kwa sala ya toba. Bali, inapasa akiri kuwa yeye ni mwenye dhambi na kukubali ukombozi wa maji na Roho ili aweze kukombolewa. Ataweza tu kuwa mwenye haki kupitia ukombozi wa maji na Roho.
Ni injili iliyojaa uongo kusisitiza kuwa ni dhambi ya asili tu ndiyo isamehewayo kupitia Yesu na imetupasa kuungama dhambi zetu za kila siku ili tuweze kupata wokovu. Hii hupelekea wengi kwenda moja kwa moja motoni. Hivyo waumini wengi hujiangamiza wenyewe motoni kwa kuamini injili isiyo ya kweli na tabia hii imeenea sana nyakati hizi.
Je, unaelewa ikiwa kama umeangukia katika injili hii ya uongo? Kweli utaweza kuwa mdaiwa baada ya kulipa madeni yako yote? Hebu fikiria juu ya jambo hili. Ikiwa bado unajichukulia kuwa ni mwenye dhambi hali ukimwamini Yesu, utaweza kweli kusema kuwa umemwamini kwa njia iliyosahihi? Je, unamwamini huku ukiendelea kuwa na dhambi au unamwamini na kuwa mwenye haki?
Utaweza kuchagua mwenyewe. Ama utaweza kuamini kuwa dhambi zako zote zimesamehewa, au utaweza kuamini kuwa imekupasa kuendelea kutubu kila siku kwa sababu ya makosa yako. Chaguo lako ndiyo litakalotoa uamuzi kama utakwenda mbinguni au motoni. Inakupasa kuwasikiliza wainjilisti wale wenye kukuhubiria injili ya kweli.
Wale wenye kuamini injili ya uongo bado wangali wakiendelea kusali sala za toba kwa ajili ya dhambi zao kila siku katika mikutano ya maombi na mikesha, kila ibada za Jumatano, mikesha ya Ijumaa kwa nia ya kujitakasa kwa dhambi zao.
“Bwana nimetenda dhambi. Nimetenda dhambi juma hili.” Ndivyo husema. Baadaye hukumbuka pia dhambi za miaka iliyopita na kuomba tena msamaha. Ama kwahakika huku ndiko kupuuzia injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Dhambi zetu lazima zilipiwe kwa damu. Waebrania 9:22 inasema “pasipo kumwagika damu hakuna ondoleo”. Ikiwa unadhani unazo dhambi, ni sawa na kumwambia Yesu amwage damu yake tena kwa ajili yako? Wale wote wasioamini ukombozi kamili wanahukumu ya kugeuza ukombozi wa Yesu kuwa uongo. Ukweli ni kwamba wanasisitiza kuwa Yesu hakutukomboa mara moja na kwa wakati wote na hivyo Yesu ni mwongo.
Ili kuweza kukombolewa katika Yesu yakupasa kuamini ukweli wa ukombozi wa maji na Roho. Je, itawezekana kweli kusamehewa dhambi, kwa idadi ya sala mara mia au mara elfu au milioni? Injili ya kweli hutukomboa mara moja na kwa wakati wote. Utaweza kuwa mwenye haki na kuingia ufalme wa mbinguni na kuishi milele muda wote.
Wimbo “♪Naishi maisha mapya katika Yesu. Ya kale yamepita na nimekuwa kiumbe kipya. Muda uliopotea umekwisha. Oh Yesu ndiye uzima wangu kweli. Ninauzima mpya katika yesu.”
Unaishi maisha mapya katika Yesu. Achilia mbali ikiwa huonekani kuwa ni mzuri kwa jinsi ungependa iwe, hata ikiwa ni mfupi sana, mnene kidogo kiunoni, wale waliobarikiwa kwa injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho ndiyo wenye maisha ya furaha. Inajalisha nini ikiwa kama pua yako haijakaa vyema au mfupi kidogo? Kwa sababu hatupo kamili ndiyo maana tunaamini katika kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho kupitia Yesu. Lakini wale wote wenye kujiona bora wataishia motoni.
Nakushukuru Bwana. Mara zote ninamshukuru Bwana. Kwa kuwa tunaamini katika kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho hakika tutakiribishwa Mbinguni.
 

UDANGANYIFU UTATUPELEKA MOTONI

Ni nani atapokea taji ya 
haki siku ya mwisho?
Yule atakaye upinga udanganyifu.

Wadanganyifu hutuambia kwamba yatupasa kutubu kila siku ili tuweze kusamehewa, lakini injili ya maji na Roho inatuambia kwamba tayari tumekwisha samehewa tunachopaswa kufanya ni kuamini tu.
Upi ni uongo? Yatupasa kutubu kila siku? Au ni sahihi kuamini kwamba Yesu ametukomboa pale alipobatizwa kwa njia ile ipasavyo kubeba dhambi zetu zote? Ukweli ni ule ambao Yesu alizichukua dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote na kwa njia ile ipasavyo kwa wokovu wetu.
Yatupasa kuushinda udanganyifu kwa njia ya vita ya kiroho. Watu wengi wanafuata udanganyifu. “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika: Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali mwenye makali kuwili. Napajua ukaapo ndipo penye kiti cha enzi cha shetani nawe walishika sana jina langu wala hukuikana imani yangu, hata katika siku ya Antipa shahidi wangu mwaminifu wangu aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo shetani” (Ufunuo 2:12-13).
“Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea” (Ufunuo 2:17).
Palipo na pepo waovu na udanganyifu huwepo hapo ukijifanya kuwa ukweli, shetani huonekana kama malaika wa nuru. Mungu, kamwe hawezi kumsaidia yeyote anaye sikiliza na kufahamu ukweli wa wokovu katika maji na Roho lakini hataki kuuamini. Mtu wa aina hii hakika huishia motoni tu.
Kila moja imempasa kuamua binafsi ikiwa kama ataamini wokovu wa Yesu. Hakuna atakaye kupigia magoti akikuomba uamini ili uokolewe. 
Ikiwa unahitaji kuokolewa toka dhambi zako inakupasa uamini wokovu utokanao kwa maji na Roho. Ikiwa utajisikia kushukuru kwa upendo wa wokovu wa Yesu na neema yake ya kutuokoa basi amini tu. Ikiwa wewe ni mwenye dhambi unayekwenda motoni, basi amini katika maji na Roho, ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani. Ndipo utakapokuwa mwenye haki.
Ikiwa unadhani kuwa wewe si mwenye dhambi, basi huitaji kukombolewa kwa kumwamini Yesu. Ni wenye dhambi tu ndiyo wanaokombolewa kwa dhambi zao zote kwa maji na kwa Roho. Yesu ni mwokozi wa wenye dhambi na mfariji wa wenye taabu, ni muumba, na Bwana wa upendo.
Kwa uaminifu nawasihi kuamini injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Amini hivyo. Utaweza kupata uhakika kwamba Yesu atakuwa Mwokozi, Mchungaji na Mungu kwako. Ikiwa hutaki kuishia motoni yakupasa uamini hivyo. Mungu habembelezi uamini injili ya wokovu.
Unataka kuingia mbinguni? Sasa basi amini injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Yesu anasema “Mimi ni njia kweli na uzima. Niamini mimi.” Je, unasema kwamba ungependa kutupwa motoni? Basi usiamini. Yesu asema amekwisha tayarisha makao motoni kwa ajili yako.
Mungu hakubembelezi. Mchuuzi hukaribisha wateja bila ubaguzi ili auze bidhaa zake, lakini Mungu ametupa ufalme wa Mbinguni bure kwa wale tu waliokombolewa. Mungu ni mwenye haki.
Watu husema mwisho wa dunia u karibu. Ndiyo hata mimi nadhani hivyo. Na ni upumbavu sasa kutoamini injili ya kweli katika kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Amini wokovu wa baraka ya injili katika kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Twendeni pamoja katika Ufalme wa Mbinguni. Hutaki kwenda nami alipo Yesu?

Je, wewe ni mwnye 
dhambi au mwenye haki?
Mwenye haki asiye na 
dhambi moyoni.

Hebu na tusome toka Warumi 8:1-2 “sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”
Yesu alizichukua dhambi zetu zote kupitia ubatizo wake na kifo chake msalabani. Aliokoa wote wenye dhambi ambao walipaswa kuhukumiwa kwa dhambi zao.
Wokovu wa Mungu umejumuisha mambo mawili. Moja, sheria na lingine upendo wake. Sheria hutuelekeza kuwa sisi ni wenye dhambi. Kulingana na sheria mshahara wa dhambi ni mauti. Hatuwezi kuokolewa kwa sheria. Sheria hutufundisha juu ya asili yetu ya uovu na matokeo yake tu. Hutufanya tuelewe kuwa sisi ni wenye dhambi.
Ili kulipia mshahara wa dhambi Yesu alishuka duniani, alibeba dhambi zote na kuzilipia zote kwa uhai wake ili atuokoe na hukumu. Ni upendo wa Mungu uliotuokoa kwa dhambi.
Ni lazima tuushinde udanganyifu. Mungu ametupa baraka ya wokovu wa maji na Roho kwa wale watakao upinga udanganyifu.
Tumeokolewa kwa kumwamini Yesu. Kwa kuamini maneno yake, tunapokea haki na kuelewa kweli. Amini ukweli wa wokovu huu kwa moyo wako wote na utaokolewa.