Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 5-1] Utangulizi katika Kitabu cha Warumi Sura ya 5

Fundisho la Kanuni ya kuhesabiwa haki si la kweli.
 
Paulo alitamka kwa imani katika sura hii kwamba wale wote wenye kuamini haki ya Mungu “ndiyo walio na amami na Mungu” sababu ya hili ni kwamba Baba Mungu alimfanya Kristo abatizwe kwa ajili yetu na hata kumfanya pia amwage damu yake msalabani.
Hata hivyo, mara nyingi tunashuhudia Wakristo wa nyakati hizi kushindwa kuwa na amani na Mungu kwa sababu hawana hata chembe ya ufahamu wa haki ya Mungu. Huu ni ukweli kwa wale waumini wa Kikristo katika wakati tulio nao. Hivyo basi, fundisho la kanuni ya kuhesabiwa haki lililopo si sahihi mbele ya Mungu. 
Kupata haki ya Mungu kwa kuwa na imani ya haki yake ndiyo sahihi zaidi kuliko kuliamini fundisho la kuhesabiwa haki. Baba Mungu hakusema kwamba yeye atawaita wenye kumwamini Yesu kuwa watu wake ingawa wana dhambi mioyoni mwao. Mungu hawakubali wenye dhambi kuwa ni watoto kwake, kwani Mungu si wanamna hiyo. Yeye ni mwokozi asiye mchukulia mtu mwenye dhambi moyoni kuwa miongoni mwa watu wake. Mungu tunaye mwamini ni Mwenyezi. Je, Mungu huyu awezaye yote na afahamuye yote aweza kutambua ikiwa imani ya mtu ni bandia? —Ndiyo.— Yatupasa pia kujua ikiwa imani ya mtu ni bandia? Yatupasa pia kuja na kuamini kwamba yeye hawaiti Wakristo wenye dhambi wenye imani bandia kuwa ni moja wapo ya watu wake.
Kila mtu imempasa awe mkweli mbele ya Mungu. Fundisho la kanuni ya kuhesabiwa haki, ambalo watu wanalielewa visivyo na kuliamini ni jambo linalo mdhihaki Mungu kwa kweli. Kwa hiyo, yatupasa kumwamini Yesu kama mwokozi wetu baada ya kuelewa vyema ukweli wa haki ya Mungu. Baba Mungu hakubali ikiwa mtu anadhambi, bila kujali ukweli ikiwiwa mtu anamwamini Yesu au la. Yeye binafsi humhukumu mwenye dhambi kwa dhambi zake.
Kwa hiyo ili uweze kutatua tatizo lako la dhambi, unahitaji kufahamu na kuamini haki ya Mungu. Mungu akiona imani zetu katika ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani atatatua moja kwa moja swala la dhambi kwa sababu tunaamini haki ya Mungu, na hivyo kutuita kuwa watu wake. Atatukumbatia na hata kutubariki. Baba Mungu huthamini imani zetu katika haki yake ikiwa ni sawa na nisahihi.
 

Mungu si hakimu wa kidunia.
 
Imani katika Haki ya Mungu iko katika msingi wa imani ya Ibrahimu, ambaye kwa uwazi aliamini maneno ya Mungu. Wakristo wengi hawaelewi vyema juu ya “Fundisho la kanuni ya kuhesabiwa haki” na hivyo yatupasa kuwa na ufahamu ulio safi juu ya swala hili. Hakika unaelewa kwamba hakuna kitu kama usawa kamili au hukumu iliyo sawa na kamili yenye kufanywa na mahakama za dunia hii. Yakupasa uelewe kwamba hakimu ya dunia hii aweze kufanya kosa katika uamuzi wake.
Sababu ya hili ni kwamba, wanadamu wote walio mahakimu hawana ukamilifu na hato weza kulewa haki ya Mungu amboko ndicho kipimo cha mazuri na mabaya. Wakristo wengi ni rahisi kwao kutoelewa haki ya Mungu na hatimaye kutuhukumu sisi “wenye haki kwa imani” (Warumi sura ya 5) kwa sababu wao hudhani kwamba Mungu hutoa hukumu akitumia njia ifananayo na hakimu wa dunia hii.
Fundisho la kanuni ya kuhesabiwa haki ni fundisho lisilo na hukumu iliyo sawa. Ni kwa sababu fundisho hili liliwekwa katika msingi wa fikra za kibinadamu. Watu huwa ni rahisi na wepesi kuhukumu isivyo kwa sababu wao si wenye enzi. Kwa hiyo humwamini Mungu visivyo, kwa kuchukulia kuwa Mungu huwafanya kuwa na haki kwa mawazo yao yaliyo katika msingi wa Fundisho la kanuni ya kuhesabiwa haki. Hii hupelekea kwao kuamini kwamba Mungu anasema “Nakuchukulia wewe kuwa si mwenye dhambi kwa sababu kwa kiasi una niamini.”
Hata hivyo Mungu kamwe hawezi kufanya hivi. Watu mara nyingi huamini kwamba ingawa bado wana dhambi mioyoni mwao, Mungu bado anawakubali kuwa miongoni mwa watu wake kwa sababu wanamwamini Yesu kwa namna yeyote. Hili ni jambo lililo katika msingi wa fikra zao na hakuna la zaidi bali ni imani bandia, ambayo ni matukio ya kudanganywa na pepo wachafu.
Kwa hiyo imewapasa kujenga nyumba zao za kiimani katika imani ya haki ya Mungu. Ingewezekanaje kwa Mungu aliye mtakatifu na Mwenyezi kumchukulia yule mwenye dhambi moyoni kama si mwenye dhambi? Je, Mungu huamua kwamba wale wenye dhambi mioyoni mwao si wenye hatia na wasio na dhambi? Kwa kudhani na kuamini hivyo kwamba jambo kama hili laweza kuwa la kweli si chochote zaidi ya fikra za kibinadamu. Mungu ni Mungu wa kweli na hatoi hukumu iliyobatili. Je, itawezekanaje Mungu yeye aliye kweli binafsi, kufanya makosa katika hukumu yake kama walivyo wanadamu? Hili kamwe halito weza kutokea. Mungu ni mwenye haki, mwenye kutoa hukumu juu ya wale wanao iamini haki yake kama watu wasio na dhambi kwa kigezo na msingi wa haki yake.
Je, unaifahamu haki ya Mungu? Je, unaiamini na kuielewa haki yake? Haki hii kwa ukamilifu yaweza kupatikana katika maneno ya Injili ya maji na Roho. Ili uweze kuielewa vyema haki ya Mungu iliyozungumziwa katika kitabu cha Warumi, yakupasa kufahamu na kuamini juu ya Injili ya Maji na Roho. Kamwe hauto elewa juu ya haki ya Mungu pasipo kufanya hivyo. Kila mmoja imempasa kujua ukweli huu. Yule anaye elewa juu ya haki ya Mungu ndiye mwenye ufahamu ulio sahihi wenye kumfanya awe mwenye haki.
Yatupasa sote kuiamini haki hii ya Mungu iliyo funuliwa katika Biblia, bila hivyo kwa njia nyingine imani yako itakuwa ni bure iliyo na msingi wa maamuzi ya kibinadamu na mawazo yake. Ikiwa ulikwisha wahi kuwa na imani ya aina hii isiyo ya kweli, yakupasa sasa uamini kulingana na maneno ya Mungu yaliyo na haki yake kuanzia leo.
Wakristo wengi walijifunza juu ya kanuni hii potofu ya kuhesabiwa haki toka kwa wanatheologia na kudhani kuwa ni kweli hata sasa. Hata hivyo yakupasa urudi katika kweli kwa kuamini haki ya Mungu. Haki ya Mungu imedhihirika kwa uwazi kupitia imani katika ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji na damu yake msalabani.
 

Biblia inasema kuwa, dhiki huleta Saburi.
 
Imeandikwa katika Warumi 5:3-4 kwamba, “Na sio hiyo tu, lakini pia tunajivunia dhiki, tukijua ya kuwa dhiki inazalisha uvumilivu; na uvumilivu, tabia; na tabia, tumaini.” Wakristo wote waliozaliwa mara ya pili wana tumaini kwamba hakika Mungu atawaokoa kutoka kwa kila aina ya dhiki. tumaini hili hutoa uvumilivu na uvumilivu hutoa tabia. Kwa hivyo, waadilifu, ambao wanaamini katika haki ya Mungu, hufurahiya nyakati za dhiki.
Paulo alisema kwamba imani katika haki ya Mungu inatarajia Ufalme wa Mungu na haidumuni tumaini. wenye haki wana tumaini gani? Wana tumaini ambalo wanaweza kuingia na kuishi katika Ufalme wa Mungu. Je! Imani ya aina hii inatoka wapi? Inatokana na kuamini katika haki ya Yesu Kristo kupitia upendo wa Baba wa Mungu.
 

Bwana asema, sisi tulikua si watauwa.
 
“Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu wakati ulipo timia, Kristo alikufa kwa ajili ya uovu” (Warumi 5:6). 
Tokea wakati ule kabla hatuja tungwa mimba, au wakati tukiwa katika matumbo ya mama zetu au tulipo zaliwa punde, hatukumfahamu Bwana, hatukuwa na uchaguzi zaidi ya kutenda dhambi wakati wote wa maisha yetu hadi kifoni na hatimaye kuishia jehanamu.
Wakati wazazi wetu wa kale Adamu na Hawa walipo tenda dhambi Mungu aliahidi kumtuma Mwokozi akisema “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake, huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino” (Mwanzo 3:15). Kutokana na ahadi hii, Yesu Kristo alikuja duniani hapa, hata kabla hatuja tenda dhambi na kutuokoa kwa dhambi zetu zote. Alibatizwa na Yohana ili kubeba dhambi za dunia hatimaye kuzifuta kwa kumwaga damu yeke msalabani. Bwana alibeba dhambi zote za wanadamu na hata za wale wasio watauwa kama mimi na wewe, kwa njia ya ubatizo wake, na kutuokoa sisi tunao amini, kwa kufa msalabani.
Je, wewe ni mtauwa? Mtu aliye mtauwa ni yule mwenye kusimama mbele ya utukufu wa Mungu na kuwa mbali na dhambi. Ni haki kamili ya Mungu ndiyo iliyo wezesha Yesu kubatizwa kwa ajili yako na yangu, sisi tusio watauwa, alisulubiwa na hatimaye kufufuka. Pia ilikuwa ni upendo wa Mungu ulio tuokoa hali tukiwa hatuna nguvu.
Jinsi ile kwa mfano wa Waisraeli walivyoli weza kutwika juu ya sadaka ya dhambi kisasi cha dhambi za mwaka mzima juu ya mnyama kwa kuwekewa mikono na kuhani Mkuu katika Agano la kale, (Walawi 16:20-21) Yesu Kristo katika Agano Jipya, naye pia hakubeba dhambi za wanadamu tu mara moja na kwa wakati wote, akibatizwa na Yohana Mbatizaji, bali pia alikwenda msalabani kusulubiwa kwa kuwa alikuwa amebeba dhambi za dunia. Haki ya Mungu inamaana ya ule ukweli kwamba Yesu Kristo alisafisha dhambi zote za wanadamu kwa kubatizwa na kumwaga damu yake.
Je, wewe ni Mtauwa? Je, Bwana hakuja kutuokoa sisi tulio wenye dhambi kwa kuwa hatukuwa watauwa hapo awali? Mungu anajua vyema kuwa sisi si watauwa kwa kuwa hatuwezi kujizuia kutenda dhambi toka siku tuliyo zaliwa hadi tutakayo kufa. Hata hivyo kwa kubatizwa na Yohana na kumwaga damu yake msalabani, Kristo alidhihirisha upendo wake kwetu wakati tukiwa bado wenye dhambi.
 

Yesu alibadilisha hatima yetu.
 
Yatupasa kufikiri kuhusiana na hatima gani sisi tukiwa wanadamu ingetukabili tokea mwanzo tulipo zaliwa. Hatima yetu ni kwenda jehanamu. Sasa basi, nini kilifanyika kwako na kwangu kuweza kuokolewa mbali na hatima hii ya jehanamu? Hatima yetu ilibadilika kwa sababu tulimwamini Mungu na haki yake. Ukweli ubadilishao hatima yetu ni Injili ya maji na Roho. Hatima yetu ikawa baraka kwa sababu tulimwamini Yesu Kristo aliye dhihirisha haki ya Mungu.
Unaweza ukawa unafahamu mistari ifuatayo ya wimbo huu wa tenzi za rohoni usemao “♪Rehema ya ajabu! ♫Ni kwa namna gani ilivyo sauti nzuri, ambayo iliyoniokoa mwenye dhambi mimi! ♫Nilipotea lakini sasa nimepatikana, ♫Nili kua kipofu sasa nimefunguliwa♪” Rehema ya Mungu na haki yake ni ukweli uthibitishao wokovu wetu. Yeyote aweza kusamehewa dhambi zake zote moyoni na kufurahiya amani ya mbinguni pale anapo fahamu na kuamini haki ya Mungu. Kwa sasa kila mmoja duniani hapa mwenye kuwa na dhambi moyoni mwake, ingawa anamwamini Yesu imempasa kuirudia Injili ya maji na Roho ili aweze kuifahamu haki ya Mungu.
Ukweli ni kuwa Wakristo wasio ifahamu Injili ya maji na Roho na pia wasiofahamu kwamba dhambi zao zilikwisha twikwa juu ya Yesu, hawana uwezao wa kupata haki ya Mungu. Ingawa wanamwamini Yesu aliyekuja duniani na kuwaokoa kwa dhambi zao kwa kufa msalabani, watu hawa hawawezi kuwa na uhakika wa wokovu wao. Kwa jinsi hii basi wao hujisikia unafuu wa kihisia kwamba Mungu labda tayari amekwisha wachagua kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Kwa maneno mengine, wana amini Ukristo kama vile ilivyo moja wapo ya dini na madhehebu mengine ya duniani.
Mstari wa 11 unatamka “Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa yeye sasa tumepokea huo upatanisho.” Ni nani aliye tupatanisha sisi wenye dhambi kwa Mungu? Yesu Kristo ndiye aliyetupatanisha na Baba. Kwa vipi? Kwa kuja kwake ulimwenguni binafsi akabatizwa na Yohana Mbatizaji akiwa na umri wa miaka 30, akasulubiwa na hatimaye kufufuka toka kifoni kwa njia hii akakamilisha kazi ambayo ndiyo iliyo dhihirisha na kuhitimisha haki ya Mungu. Yesu amekwisha kuwa Mwokozi wetu sisi tunao amini haki ya Mungu, kwakuja kwake duniani akiwa kuhani Mkuu wa Mbinguni na kubeba dhambi zote za wanadamu, kwa kubatizwa kwake na Yohana Mbatizaji na kuwa Kuhani Mkuu wa daima.
Kwa kuwa Yesu Kristo aliondolea mbali dhambi zetu zote tumeweza kupokea haki ya Mungu kupitia imani zetu. Yeyote anayeamini kwamba Yesu alituokoa kwa ukamilifu kutokana na dhambi zetu zote atafurahi katika Mungu. Yeye mwenye dhambi hata chembe kidogo ndani moyo wake, si mwana wa Mungu.
Ninyi ndugu zangu, labda nanyi pia mnawajua watu wa aina hii duniani wenye kudhani Mafundisho ya kanuni ya kuhesabiwa haki na utakaso wa awamu kwa awamu ndiyo ya kweli. Je, ni vyema Mungu kutoa hukumu ikiwa hatuna dhambi huku tukisema kuwa tunamwamini Yesu ingawa tuna dhambi mioyoni mwetu? Au ni sahihi pia kuchukuliwa kuwa ni watu wa Mungu kwa kuwa tu tumejitambulisha kuwa ni Wakristo?
Twasema “Baba yetu uliye mbinguni Jina lako litukuzwe” katika sala ya Bwana. Usemi huu maana yake ni kuwa wale wenye dhambi mioyoni mwao bila shaka hawawezi kumwita Mungu “Baba Yetu”. Je, tuendelee kuamini Fundisho la kanuni ya kuhesabiwa haki? Je, inawezakana kwa mtu aliye na dhambi kwa sasa kumwita Bwana kuwa Mwokozi wake? Anaweza kumwita Bwana kwa miaka kadhaa lakini hatimaye atamwacha kwa sababu ataona aibu ndani ya dhamira yake kuweza kuwa Mkristo. Kwa hiyo yakupasa uelewe kwamba Fundisho la Kanuni ya kuhesabiwa haki litaweza kukutenga na haki ya Mungu.
Fundisho la Kanuni ya kuhesabiwa haki ni batili. Fundisho hili hutamka kwamba, twaweza kupitia mabadiliko hatua kwa hatua hadi kufikia kuwa watakatifu kamili kwa siku za mwisho kabla ya kufa na hiyvo tutaweza kukutana na Mungu tukiwa watu watakatifu. Je, unadhani utaweza kuwa mtu mtakatifu ili kukidhi kiwango cha Mungu pasipo dhambi? Hakuna jinsi. Ukweli unatuambia kwamba mtu aweza kuingia Ufalme wa Mungu kwa kujua na kuamini kwa dhati haki ya Mungu tu.
 

Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni.
 
Hebu sasa tusome mstari wa 12 “kwa hiyo kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti, na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” Kupitia nani dhambi iliingia katika mioyo ya watu wote na kupitia nani na kwa kupitia watu wangapi dhambi ili ingia duniani? Maandiko yanasema “kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwengu”.
Kwa maneno mengine ilisemekana kwamba dhambi ilikuja kwa sababu ya mtu mmoja, Adamu. Na sisi sote ni uzao wake. Kwa hiyo kupitia nani dhambi za dunia zilifutwa? Yaweza kusemekana kwamba ilitokea kwa jinsi hiyo pia ya kuingia duniani.
Dhambi za wanadamu zilikuja kwa sababu ya mtu ambaye hakuiamini sheria ya Mungu aliyo iweka. Hata sasa, mtu asiye amini maneno ya Mungu atabaki kuwa mwenye dhambi na hatimaye kuishia jehanamu.
Kwa hiyo yatupasa kujua yafuatavyo. Sisi si wenye dhambi kwa sababu tu ya dhambi zetu binafsi, bali ni kutokana na wazazi wetu wa kwanza walio turithisha. Yatupasa kujua kwamba sababu ya watu kutenda dhambi ni kutokana na kuwa dhaifu na kuwa na dhambi mioyoni mwao. Dhambi wazitendazo watu huitwa maovu. Sababu ya kutenda maovu ni kwa kuwa walizaliwa duniani huku wakiwa na dhambi mioyoni mwao hata kabla ya kuzitenda. Kwa kuwa basi kila mtu nidhaifu na kuzaliwa duniani akiwa nadhambi, basi hatutoweza kujizuia kutotenda dhambi hizo daima.
Kiasili tumekuwa wenye dhambi, mbegu ya uovu, kwa sababau tumeirithi dhambi hiyo kwa wazazi wetu wa kwanza. Hata hivyo yakupasa kuelewa kuwa yeyote aweza kuwa mtakatifu na mwenye haki mara moja na kwa wakati wote ikiwa ataiamini haki ya Mungu tu.
 

Ni lini dhambi ilitokea na kuwepo?
 
“Maana kabla ya sheria dhambi ilikuwemo ulimwenguni lakini dhambi haihesabiwi isipokuwa sheria” (Warumi 5:13). Je, dhambi ilikuwepo kabla ya kujua sheria ya Mungu? Kabla ya kujua sheria ya Mungu hatukuwa tunakifahamu kile kilicho tuhukumu kuwa ni wenye dhambi mbele ya Mungu. Mungu anatuambia “Usiwe na Miungu mingine zaidi yangu au kujifanyia chochote kwa mfano wa vilivyo mbinguni au hata duniani chini, au kilichomo majini, chini ya ardhi, usivisujudie au kuvinyenyekea, usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako na ikumbuke siku ya sabato uitakase.” Kabla ya kujua sheria kama hizi na vipengele vyake 613 vya sheria vinavyo tuelezea juu ya “kufanya” na “kutofanya” hakika hatukuwa tunaifanhamu dhambi ni nini na ni ipi.
Kwa hiyo “kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwe isipokuwapo sheria” kwa kuwa sisi watu wa mataifa hatukuwa na sheria na hivyo hatukujua juu ya hilo, tulitenda dhambi pasipo kujielewa. Wakorea wengi wamekuwa wakifanya ibada katika miamba wakidhani ni Buddha, lakini bado hawajafahamu kwamba wana abudu sanamu. Hawakujua kwamba kuabudu miungu wengine ni dhambi mbele ya Mungu.
Hata hivyo, kabla ya sheria kuja dhambi ilikuwa tayari imekwisha kuwepo duniani. Mungu ametupatia sheria takribani miaka 2,500 iliyo pita baada ya kumuumba Adamu. Ingawa Mungu aliwapa sheria wana wa Israeli kupitia Musa karibia miaka 1,450 KB, (Kabla ya Kristo) dhambi ilikuwepo tayari duniani kupitia mwanadamu Adamu na hatimaye ikawa ndani ya mioyo ya watu tokea mwanzo hata kabla ya kuja kwa sheria.
 

Yesu ni Mwokozi wa watu wake.
 
Je, Yesu Kristo alifuta dhambi zote za ulimwengu yeye mwenyewe? Ndiyo. Hapa mstari wa 14 unasema kwamba, mauti ilitawala hata wao wasio fanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu. Kwa hiyo Adamu alikuwa ni mfano wa Mungu aliye paswa kuja baadanye. Mwanadamu alikuja kuwa mwenye dhambi kupitia mtu mmoja kwa jinsi hiyo pia, Yesu Kristo alikuja duniani kutuokoa sisi toka dhambini kupitia Injili ya maji na Roho.
Yesu amekuwa Mwokozi aliyewaokoa watu wake kutokana na dhambi zao. Yupo mwokozi mmoja tu anaye tuokoa sisi tulio uzao wa Adamu toka dhambini, “wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbinguni walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwako” (Warumi 4:12). Jina lake ni Yesu Kristo Mwokozi wetu wa milele.
Yatupasa kuelewa kwamba tunakuwa wenye dhambi moja kwa moja kupitia mtu mmoja Adamu. Je, unajua kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi aliyefuta dhambi zote za ulimwenguni mara moja na kwa wakati wote? Je, unaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi aliye futa dhambi zote duniani kwa njia ya ubatizo wake na damu yake aliyo mwaga msalabani mara moja? Je, unaamini kwamba Yesu amekuwa Mwokozi wa kweli kwa wanadamu wote kwa kuondolea mbali dhambi za dunia, kama ilivyo mfano wa Adamu kuwa chanzo cha dhambi zote kwa kutenda kosa moja?
Yesu alikuja hapa duniani kuokoa wale wote waliokuwa wenye dhambi kutokana na mtu mmoja, Adamu, na kubeba dhambi zote za wanadamu kwa kupokea ubatizo toka kwa Yohana, akapokea hukumu ya dhambi msalabani kwa kumwaga damu yake na hatimaye kuitimiza haki ya Mungu yenye kufuta dhambi zetu zote. Ndipo akawa Mwokozi wetu kamili.
Hatukupata wokovu kwa kuamini Fundisho la Kanuni ya kuhesabiwa haki au utakaso baada ya kumwamini Yesu. Yesu ametupatia wokovu wa milele mara moja na kwa wakati wote. Yesu alisema kwamba, wale tu walio zaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho wataweza kuingia Ufalme wa Mungu.
Ni mawazo gani yanayo nasa na kukaa katika kina cha dhamira za wanadamu? Ni kanuni ya uungwana na ustaarabu. Wao hudhani ndani ya kina cha fikra zao kuwa, juhudi na nguvu zao zitawezesha kuupata wokovu au hata kuendelea nao. Hata hivyo, kila mtu anapokea wokovu wa kweli toka dhambini kwa kuweza kuwa na imani mara moja tu na kwa wakati wote, ikiwa ataamini Injiliya maji na Roho. Zaidi ya yote, Yesu alikuja duniani na kusulubiwa ili kutuokoa sisi toka dhambini. Akawa Mwokozi wa wote wale wenye kuamini Injili ya kweli.
Jiweke huru toka katika fikra zisizo na maana ambazo husema kwamba mtu aweza kufikia kiwango cha kutosheka na hatimaye kuwa mwenye haki kupitia sala za toba. Katika Biblia mtu mmoja, Yesu Kristo alikuja duniani akabatizwa ili kubeba dhambi zetu zote na kutimiza wokovu wote, kupitia upatanisho wake wa dhambi msalabani.
 

Yesu ametupatia ondoleo la dhambi milele lisilo lingana na makosa yetu.
 
Mstari wa 15 unatamka, “Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa, kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya walio wengi.”
Je, dhambi zangu na zako zilitwikwa juu yake Yesu pale alipo batizwa? Ndiyo, zilitwikwa. Yesu alikwenda msalabani akiwa tayari amebeba dhambi za dunia na kupokea hukumu ya dhambi hizo kwa niaba yetu. 
Wokovu wa Mungu ni zawadi bure na ni zaidi hata ya makosa yetu.
Yesu alituokoa, sisi tusio weza kujizuia kutenda dhambi maishani mwetu pote, kupitia ubatizo na damu yake msalabani akiwa na umri wa miaka 33. Hata baada ya kupata wokovu huo kwa kuamini ondoleo la dhambi lililo kamilishwa mara moja bado miili itaendelea kutenda dhambi kwa sababu si mikamilifu na ni dhaifu sana. Ingawa kwa hili tunaweza kupata ondoleo la dhambi la milele mara moja na kwa wakati wote ikiwa tutaamini ule ukweli wa Yesu kubeba dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote kwa njia ya ubatizo, na hivyo kuitimiza haki ya Mungu. 
Ondoleo la dhambi halikutolewa kila siku kama ilivyo dhambi za watu kila siku. Ukweli wa ondoleo la dhambi unasema kwamba, Bwana alikwisha tuokoa kutokana na dhambi zetu zote mara moja na kwa wakati wote kwa kubatizwa na kumwaga damu yake takribani miaka 2000 iliyo pita.
Karama ya wokovu yenye kutuokoa kutokana na dhambi zetu zote ni haki yenye kutimizwa mara moja kwa ubatizo na damu msalabani. Ondoleo la dhambi la milele si sawa na msamaha wa kila siku kupitia sala za toba ambapo Wakristo wengi hufanya siku hizi. Ukweli huu husema kwamba Bwana alikwisha tangulia kuona kwamba tutaendelea kutenda dhambi na hivyo alikwisha zichukua dhambi hizo za dunia mara moja pale alipobatizwa. Kwa hiyo, Baba Mungu alitimiza haki yake yote kwa ubatizo wa mwana wake na kusulubiwa kwake. Haki yote ya Mungu imekwisha kutimizwa kwa sababu Yesu alibatizwa, kumwaga damu yake msalabani na kufufuka.
Siku hizi Wakristo wengi huamini kwamba dhambi zao huweza kufutwa pale wanapo fanya sala za toba. Je, hili ni kweli? Hakika sivyo. Mtu anayedhani kwamba anaweza kupatanishwa kwa dhambi zake baada ya kuuvua utu wa nje huku akifanya sala ya toba ni mokosa. Kufikiri kwa namna hii si chochote bali ni fikra za kibinadamu. Ili kuondolewa dhambi kwa upande wa Mungu, mtu imepasa kila mara kulipa mshahara wa dhambi. Na ili kufanya hivyo, Mungu alimfanya Mwana wake Yesu kubatizwa na Yohana na kufuta dhambi zote kwa kumwaga damu yake msalabani dhambi za wanadamu zaweza kusafishwa na kuondolewa mbali kwa kuamini ubatizo na damu ya msalabani na si kufanya sala za toba.
Kwa hiyo Biblia inasema “kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa zaidi sana neema ya Mungu na kipawa kilichokatika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kumezidi kwa ajili ya wale wengi.” Zawadi ya Mungu ya wokovu imejaa na kupita kiasi. Kama ilivyo kwa maji kujaa na kupita kiasi hata kumwagika pale bomba linapo achwa wazi na kutiririka usiku kucha, haijalishi ni dhambi kiasi gani tulizo tenda, wokovu wa Mungu umefurika katika kuokoa dhambi zetu zote.
Yesu amechukua dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa. Pia, kwa sababu wokovu wa Mungu ni mkubwa zaidi kuliko maovu ambayo tumetenda, wokovu wake ni mwingi hata baada ya kuokolewa. Je! Hii ni wazi?
 

Kwa yule mmoja, Yesu Kristo.
 
Mstari wa 16 na 17 unatamka “Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu, bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya kukosa mtu moja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema na kile kipawa cha haki watatawala katika uzima kwa yule mmoja Yesu Kristo.”
Mauti imetawala wanadamu wote kupita kosa la mtu mmoja. Hii inaonyesha kwamba dhambi ya mtu mmoja Adamu ilisababisha watu wote kuwa wenye dhambi na kwa sababu ya dhambi hiyo, kila mtu anahitajika kukabiliana na laana ya Mungu. Yeyote aliyetenda dhambi imempasa kufa na kwenda jehanamu. Kwa mfano wa mtazamo huo, pia haki ya Mungu inatawala kwa uzima kutokana na mtu mmoja, Yesu Kristo. Wale walio kwisha pokea utele wa rehema na haki ni wale walio pata karama ya wokovu kwa imna zao katika Injili ya maji na Roho. Hupokea rehema zaidi toka kwa Mungu na kutawala katika uzima wa milele.
Mstari wa 18 unatamka “Basi tena kama kwa kosa moja watu wote wali hukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima”.
Hapa tunahitaji kujiuliza na kulijibu swali, Je, ni kweli kudhani kwamba kwa dhambi ya mtu mmoja basi wote tumekuwa wenye dhambi? Je umekuwa mwenye kutokana na dhambi zako binafsi au kutokana na kosa la mzazi wa kwanza Adamu dhidi ya Mungu? Ikiwa tumekuwa wenye dhambi kutokana na kosa la Adamu, basi wale wote wanao amini tendo la haki la Yesu Kristo alilofanya katika kutuokoa kutokana na dhambi zetu watakuwa ni sawa na wako sahihi. Ikiwa mtu anaamini haki ya Mungu je, hakika dhambi zake zitafutwa?  —Ndiyo.— Atakuwa si mwenye dhambi tena.
“Kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.” Kupokea zawadi bure ya haki ya Mungu haina maana kwamba mtu imempasa kufanya sala za toba kila siku ili kufikia kiwango cha utakaso baada ya kuokolewa kwa kumwamini Yesu. Kamwe! Wala si maana mojawapo ya fundisho fulani la kanuni za Kikristo lijulikanalo kama “Kuhesabiwa haki kwa imani.” Wakati Paulo Mtume alipozungumzia juu ya hili alisema, “baada ya kuhesabiwa haki kwa imani.”
Wakristo wengi wanazo dhambi mioyoni mwao kwa sababu wao huiamini damu ya Yesu pekee. Hivyo hukubaliana na kuunga mkono Fundisho hilo la kanuni ili kwamba waweze kuzificha dhambi zao mioyoni mwao, huku wakijiliwaza nafsi zao; wakisema “ingawa ninadhambi moyoni bado Mungu ananichukulia kuwa si mwenye dahmbi” Hata hivyo fundisho hili la kanuni ni la kugadhabisha na kutia kichefuchefu na hakika, litalaaniwa.
Mstari wa 19 unatamka “Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wa wameingizwa katika hali ya wenye haki”.
Hapa anaonekana mtu mmoja asiyetii na mwingine anayetii, mmoja ni Adamu na mwingine ni Mwokozi wa wanadamu, Yesu Kristo. Katotii kwa Adamu kumefanya wanadamu wote kuwa wenye dhambi, na hivyo Yesu alitii mapenzi ya Baba yake ili kuwapatanisha watu na Mungu kwa kupokea ubatizo toka kwa Yohana, kufa msalabani kwa dhambi za dunia na kufufuka ili kutuokoa toka dhambini. Mungu Baba aliwafanya wote wamwaminio Yesu kuwa wenye haki kamili kupitia haki yake.
Mstari wa 20 unatamka, “Lakini sheria iliingia ili kosa, lile kubwa sana, na dhambi ilipo zidi neema ilikuwa nyingi zaidi”.
Inasema kuwa sheria ilikuja kuongeza uovu wetu. Wakiwa ni uzao wa Adamu, watu kwa asili wamezaliwa na dhambi, lakini hawakuitambua dhambi ingawa waliitenda. Pasipo sheria mtu, hawezi kuelewa kuwa anatenda dhambi na ni kwa sheria ya Mungu tu ndipo, tunapo kuja kuelewa sheria basi ndipo hapo tunagundua juu ya dhambi zetu zaidi na zaidi. Ingawa watu kwa asili wamefurika dhambi, bado hawaelewi juu ya hali yao ya dhambi hadi hapo wanapokuja kuelewa hatua kwa hatua matendo yao ya dhambi baada ya kuipokea sheria. Hivyo basi, Biblia inatamka kwamba “Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana”.
“Nadhambi ilipozidi neema ili kuwa nyingi zaidi.” Hii inamaanisha kwamba, kupitia sheria ya Mungu ndipo mtu anagundua juu ya dhambi zake na hatimaye kuwa mtoto wa Mungu kwa kuiamini haki ya Mungu. Mwanadamu aweza kugundua rehema ya Mungu tu pale anapo elewa na kufahamu udhaifu wake na hali yake ya dhambi kupitia sheria ya Mungu. Wale ambao wanaelewa vyema juu ya dhambi zao mbele ya sheria ya Mungu, kukiri kwamba ilikuwa ni halali kwao kwenda jehanamu, na kwa sababu hiyo wakiwa na shukrani kubwa, humwamini Yesu aliye waokoa kwa njia ya ubatizo wake na kifo chake msalabani. Kiasi tunacho gundua zaidi juu ya hali ye tu ya dhambi kupitia sheria ya Mungu ndicho kiasi zaidi tunaweza kuimarishwa kwa wokovu huo wa haki ya Mungu.
Mstari wa 21 unatamka “Ili kwamba kama vile dhambi ilivyowatawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.”
Imesemwa katika Biblia kwamba, dhambi ilitawala katika mauti. Hata hivyo rehema ya Mungu iliyo ya maji na damu ya Yesu ni haki ya Mungu kwa sababu haki yake imekamilisha kutuokoa toka dhambini, na hivyo tumekuwa watoto wa Mungu.
Fundisho la kanuni ya utakaso na kuhesabiwa haki ni upuuzi wa kufikirika uliotokana na mtazamo wa kibinadamu na hatimaye kuundwa na wale wenye kulidharau neno la Mungu. Si jambo la kutia chumvi inapo semekana kuwa mafundisho hayo si chochote bali ni utapeli wa wanafilosofia wa kitheologia, yasiyo leta utatuzi kamwe. Ukweli wa Mungu u wazi na thabiti.
Tumeokolewa toka dhambini katika dunia kwa kuamini ule ukweli wa Yesu aliye Mungu mfano wa umbo la mwanadamu kutuokoa kwa dhambi zetu zote. Wale walio na imani kwake ndiyo walio okolewa. Je, unaamini hili? -Ndiyo.-
Ikiwa unaamini haki ya Mungu, basi umekwisha okolewa. Bila shaka utaokombolewa na kuokolewa kwa dhambi zako zote. Ikiwa bado unashikilia kufanya sala za toba na kujifanya kuishi maisha yasiyo ya lawama ili kufikia kiwango cha utakaso ukidhani utaokolewa, basi wewe ni mkaidi unayeshikilia wazo la kuokolewa pasipo Yesu. Yesu ndiye lango pekee kuelekea wokovu, haijalishi ni aina gani ya udanganyifu uliomo katika mafundisho ya kanuni za utakaso yafundishiyo namna ya kuweza kuokolewa kwa matendo binafsi na juhudi kwa kutupilia mbali ukweli.
Kushindwa kufuata hata 0.1% ya sheria ni sawa na kushindwa 100% zote. Mungu anatuambia kwamba hatuwezi kutii hata 0.1% ya sheria zake. Wale wenye kudhani kuwa wanafuata hata 5% kwa kipindi cha muda fulani hakika hawa ni wapumbavu wasio elewe juu ya uwezo wao na wanashindana na haki ya Mungu. Usijaribu kamwe kutafuta kuielewa haki ya Mungu kwa mtazamo na maoni binafsi. Haki yake ndiyo iliyo tuokoa toka dhambini mwetu na kutusubiri sisi ilituweze kuwa watoto wa Mungu.
Mungu ni Mwenye enzi na rehema hivyo alituokoa kwa haki yake mara moja na kwa wakati wote. Tunamshukuru Mungu kwa ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ambavyo kwa hakika vilituokoa kwa dhambi zetu tu.