Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 4-2] Wale wapokeao Baraka za Mbinguni kwa Imani (Warumi 4:1-8)

 

(Warumi 4:1-8)
“Basi tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili? Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu. Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa haki lakini kwa mtu afanyaye kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema bali kuwa ni deni. Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki, kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo. Heri walio samehewa makosa yao na waliositiriwa dhambi zao. Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi.”
 

Heri kwao walio futiwa dhambi zao.
 
Nampa Bwana shukrani kwa kuokoa nafsi nyingi nyakati hizi. Biblia inazungumiza juu watu walio na heri katika Warumi sura ya 4, hivyo ningependa kuzungumiza juu ya wale walio na heri pia.
“Kama vile Daudi anenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo. Heri waliosamehewa makosa yao na waliositirika dhambi zao. Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi” (Warumi 4:6-8). Biblia inazungumzia juu ya wale wote walio barikiwa na Mungu. Wenye heri wa kweli ni wale ambao dhambi zao zimefutwa mbele ya Mungu na ambao Bwana hato wahesabia dhambi tena.
Kabla ya kwenda kwa kina katika maandiko, hebu tuchunguze hali zetu kwa sasa kama zilivyo. Biblia inazungumiza juu ya watu wenye haki walio pokea ondoleo la dhambi zao. Hebu tena tufikiri ikiwa kama nasi tunahadhi ya heri au la.
Hakuna hata mmoja duniani asiye tenda dhambi. Wanadamu hutenda dhambi nyingi na kubwa kama wingu nene kama ilivyo andikwa katika Isaya 44:22 Hakuna yeyote awezaye kukwepa hukumu ya haki itokayo kwa Mungu pasipo rehema ya Yesu Kristo.
Tumekombolewa kwa dhambi zetu na hukumu ya Mungu kwa njia ya ubatizo wa Yesu Kristo na damu yake msalabani. Zaidi ya yote, sasa tunaweza kuwa na uzima kwa kuwa Yesu Kristo amejitoa sadaka. Je ingewezekana kweli kwa yeyote kutotenda dhambi kweli katika dunia hii kwa maisha yake yote? Hata ikiwa kwa mtu ambaye tayari amekwisha kupokea ondoleo la dhambi au la bado ataendelea kutenda dhambi maishani mwake pote. Kwa kuwa basi tunaendelea kutenda dhambi pasipo hata kujielewa, hatima yetu ni kupokea hukumu kwa sababu ya dhambi hizo.
Naamini ukweli wa mtu mwenye dhambi hata ikiwa ni ndogo kiasi gani atakwenda jehanamu. Kwa nini? Kwa sababu Biblia inasema kwamba “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Mshahara wa dhambi, hata uwe vipi ni lazima ulipwe kwa dhambi kusamehewa pale tu mtu anapolipa gharama yake. Dhambi huleta hukumu tu.
Tunaishi katikati ya lindi la kila aina ya dhambi zote, kubwa na ndogo kwa aina yake, dhambi za kutokana na upumbavu, zitendwazo kwa kufahamu na zile zitokanazo na udhaifu. Kusema kweli hatuwezi kujizuia kutenda, bali kukiri mbele ya Mungu. Ijapokuwa tuna kuwa hodari kujitetea mbele zake. Je, una kubaliana na mtazamo huu? Si vyema kwetu kukataa kukiri dhambi zetu ingawa zote zime kwisha samehewa. Kila mmoja imempasa kukiri mambo ambayo yampasa kukubali kuwa kayatenda.
 

Ni wenye haki tu ndio wawezao kumsifu Bwana.
 
Wenye haki, ambao dhambi na uovu wao umesamehewa na kusitiriwa, ndiyo wasio na haki binafsi hivyo humpa Mungu shukrani. Hatuwezi kujizuia kumshukuru Mungu kila saa na dakika, kila tunapo kuja mbele zake, kwa kuwa Bwana ameondolea mbali dhambi zetu zote, ijapokuwa dhambi hizo ni kubwa kama wingu nene. Tunamshukuru Bwana aliye ondolea mbali dhambi zetu zote kwa kubatizwa kwake na Yohana Mbatizaji katika mto Yordani na kupata hukumu juu ya msalaba kwa ajili yetu.
Kama Bwana asingelichukua dhambi zetu zote juu yake kwa njia ya ubatizo au kama asingesulubiwa na kufa ili kulipia mshahara wa dhambi, je, kweli tungekosa heshima kwa kumwita yeye kuwa ni Baba? Tungewezaje kumsifu Bwana? Tungewezaje kulisifu jina la Mungu na kumshukuru kwa zawadi ya wokovu na kumtukuza? Yote haya ni kutokana na zawadi ya rehema za Mungu.
Sisi tukiwa watakatifu twaweza kumsifu Bwana na kumshukuru katika wakati huu kwa kuwa dhambi zetu tayari zimekwisha futiliwa mbali kwa njia ya sadaka ya Kristo na ule ukweli wa Bwana kubeba dhambi zetu zote, zikiwemo dhambi ndogo kama punje za shayiri twaweza kumsifu kumsifu Bwana.
Ingawa tumekwisha samehewa dhambi zetu, kamwe hatuwezi kuwa wakamilifu kwa matendo yetu huku tukiishi hapa duniani. Wote tu dhaifu lakini sisi tulio wenye haki, twamsifu Bwana aliye lipa mshahara ya dhambi zote za wasio watauwa kwa rehema zake Je, bado umo katika kiza? Haijalishi ni aina gani ya kiza lililo tanda ikiwa utakubali na kukiri hata dhambi iliyo ndogo mbele ya Mungu, ikiwa utakiri kwamba umetenda dhambi mbele ya Mungu, na ikiwa utaamini kwamba Bwana ndiye aliye zibeba dhambi zetu zote, ukweli wa Bwana uta kuruhusu kumsifu na kumshukuru yeye. Tunakuwa watakatikfu tusio weza kujizuia kumshukuru na kumsifu Yesu Kristo kwa sababu ya rehema zake na msamaha wa dhambi. Zaidi ya yote, tunakuwa wamwabuduo Mungu baada ya kupokea rehema ya ondoleo la dhambi mioyoni mwetu.
 

Ikiwa tumefanywa kuwa wenye haki pasipo matendo basi hiyo ndiyo zawadi ya Mungu.
 
“Basi tusemaje juu ya Ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili? Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia, lakini si mbele za Mungu maana maandiko ya semaje? Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa haki. Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa nideni. Lakini kwa mtu asiye fanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki” (Warumi 4:1-5).
Dhambi za wanadamu zinafutwa baada tu ya kulipa mshahara wake. Je, unahakika kwamba dhamira yako ni safi? Ukiachilia mbali ni aina gani ya dhambi, dhamira zetu zaweza kutakaswa ikiwa tu baada ya kulipa mshahara wa dhambi. Sisi wenye dhambi hatuna uchaguzi zaidi ya kufa, lakini Bwana alikufa kwa ajili ya dhambi hizo kwa hiyo wenye dhambi walifanywa kuwa wenye haki kwa kuokolewa.
Katika Warumi sura ya 4 Paulo alisema kwamba wenye dhambi waliokolewa na Yesu Kristo, aliyebeba dhambi zote za dunia juu yake katika Yordani na kusulubiwa kwa hukumu ya dhambi zao, akimtumia Ibrahimu, baba wa imani aliye amini maneno ya Mungu kama mfano. Biblia inasema kwamba Ibrahimu alikuwa mwenye haki kwa sababu alimwamini Mungu. Hakuokolewa kwa matendo yake, bali kwa imani ya neno la Mungu. Kwa hiyo Mungu alimhesabia haki. Ibrahimu alipata wokovu kwa kuyaamini maneno ya Mungu na hatimaye akawa baba wa wale wote wanao amini. Alifanywa kuwa mwenye haki kwa kuyaamini maagano ya Mungu.
Wokovu wa dhambi ni upi na rehema ya Mungu ni ipi iliyo juu yetu sisi wenye dhambi? Hebu basi tufikiri juu hili ili tuweze kuainisha kwa uwazi “Lakini kwa mtu afanyaye kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa nineema balikuwa ni deni” (Warumi 4:4). Mstari huu unazungumzia juu ya wokovu wa Mungu, wenye kutuokoa toka dhambini, unazungumiza juu ya ondoleo la dhambi. “Lakini kwa mtu afanyaye kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.” Ikiwa mtu anapokea mshahara kwa kazi yake je, atauchukulia mshahara huo kuwa ni neema au deni? Paulo Mtume anaelezea wokovu akimtumia Ibrahimu kama mfano. Ni halali kwa mtu aliyefanya kazi kupokea mshahara kwa kazi aliyo ifanya. Hata hivyo ikiwa tumefanywa kuwa wenye haki, watakatifu, ijapokuwa hatukuishi maisha yaliyo manyoofu, ni kwa njia ya kipawa cha Mungu na si kupitia juhudi zetu.
“Lakini kwa mtu afanyaye kazi ujira wake hauhesabiwi kawa ni neema bali kuwa ni deni” (Warumi 4:4). Wokovu kupita msamaha wa dhambi unatokana na ubatizo wa Bwana na kumwaga damu yake kwa sadaka. Wokovu uliwezekana kupitia rehema na karama ya ondoleo la dhambi. Mwanadamu hawezi kujizuia kutenda dhambi hivyo husukumwa kukiri kwamba ametenda dhambi. Mwanadamu hawezi kamwe kujitakasa binafsi dhambi alizo tenda. Haijalishi ni kwa kananu gani za mafundisho ya kiroho awezavyo kuamini au ni kwa jinsi gani awezavyo kuamini, au ni kwa jinsi gani awezavyo kuwa na juhudi ya kusali na kuomba kwa ajili ya dhambi hizo.
Njia ya pekee kwa mwenye dhambi kuweza kutakasa dhambi zake ni kuamini wokovu unenao kwamba, Bwana alizichukua dhambi za dunia juu yake kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani na alisulubiwa ili kupokea hukumu kwa ajili ya dhambi. Wenye dhambi hawana hadhi ya kuweza kulipia dhambi zao kwa njia ya aina yoyote ya sadaka waitoayo binafsi. Kile ambacho mwenye dhambi awezacho kukifanya ni kuamini wokovu kupitia kusamehewa dhambi. Kitu pekee wawezacho kutegemea ni rehama ya Mungu.
Kwa kupokea ubatizo katika Mto Yordani, Yesu alibeba dhambi zote kwa njia iliyo stahili na kwa kujitoa sadaka msalabani wenye dhambi waliokolewa toka dhambini mwao. Hii imejumuisha dhambi ndogo tutendazo kutokana na udhaifu wetu chini ya ulaghai wa shetani na dhambi kubwa mfano wa mlima mrefu. Hivyo basi, wenye dhambi walipokea wokovu kwa imani ya ubatizo na damu ya Yesu Kristo kupitia rehema bure ya wokovu, sisi tulio na dhambi sasa tu wenye haki.
 

Ondoleo la dhambi limetolewa kwa rehema na kipawa tu.
 
Paulo Mtume anazungumzia namna mwenye dhambi alivyo okolewa kwa dhambi zake zote “Lakini kwa mtu afanyaye kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema bali kuwa ni deni.” Anaelezea rehema ya wokovu kwa kulinganisha na juhudi za kimwili. Ikiwa mwenye dhambi baada ya kufanya kazi mbele ya Mungu, akisema amepata wokovu toka dhambini, basi hapa hii sizawadi au karama ya Mungu, bali ni kutokana na kiasi cha kazi alicho tenda. Ondoleo la dhambi linalotolewa kwa rehema ni kama karama au zawadi tu. Hakuna hata matendo yetu yaliyo jumuishwa katika rehema hiyo ya Mungu. Wokovu toka dhambini ni zawadi ya Mungu kwetu ambayo tunaipokeao. Je, ndiyo au sivyo? Ndivyo ilivyo. Hatuna la kuchagua bali kuangamia kwa sababu ya dhambi zetu. Hata hivyo, Yesu Kristo Mwokozi wetu alibeba dhambi zetu zote juu yake kwa kubatizwa na Yohona Mbatizaji katika Mto Yordani.
Tunaokolewa toka dhambini kwa kuamini ukweli wa Yesu Kristo kulipa mshahara wa dhambi na kufa kwa ajili yetu. Alitutakasa kwa kuzichukua dhambi zetu zote kwa ubatizo wake na kwenda msalabani kusulubiwa, hivyo kutuokoa. Yote haya yametokana na rehema za wokovu wa Yesu. Kukombolewa kwetu kuliwezekana kwa kupitia rehema ya Mungu. Ni zawadi. Ni bure kwa wenye dhambi waliokolewa kwa upendo wa Mungu dhidi yao. Yesu alizichukua dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo wake na kuwaokoa wenye dhambi kwa dhambi zote za dunia kwa njia ya hukumu kwa kusulubiwa kwake.
“Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki” (Warumi 4:5). Kabla ya kuzungumzia juu ya mtu afanyaye kazi, usemi wa “Lakini kwa mtu asiyefanya kazi” unamaanisha kwa wale ambao wasio tenda uadilifu kwa nia ya kuwa wenye haki. Paulo anaendelea na kusema “bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.”
Hapa anamtumia asiyekuwa mtauwa kama mfano katika kuelezea haki ya Mungu. Nini maana ya “asiye kuwa mtauwa?” Ni yule asiye weza kusimama mbele ya utakatikfu wa Mungu, ambaye anaye ishi maisha yasiyo manyoofu hata mwisho wa pumzi yake. Ambapo ni kinyume na mtauwa. Neno hili linaashiria mtu atendaye dhambi mbele ya Mungu mpaka siku ya mwihso wa kifo chake. Ni kweli kwamba watu wamezaliwa wakiwa na wingi wa dhambi. Zaidi ya yote ilikuwa ni asili ya kweli ya wanadamu kwa hatima yao kupokea hukumu ya Mungu kutokana na dhambi zao.
Hata hivyo imeandikwa “Lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabiwa kuwa haki” Hapa usemi “Lakini kwa mtu asiyefanya kazi” maana yake “ingawa si mtauwa.” Je, sisi ni watauwa? —Hapana.—
Bwana anasema kwetu, tusiowatauwa “Wewe huna tena dhambi na ni mwenye haki”. Bwana alibeba mshahara wa dhambi zetu zote na kuulipa. Je unamwamini Yesu kwamba alikwisha lipa mshahara wote? Kwa wanaoamini, imani yake wahesabiwe haki “Ni kweli Unaamini hivyo. Ninyi ni watu wenye haki. Hamna tena dhambi kwa kuwa nilikwisha zifuta pale nilipo batizwa na Yohana Mbatizaji na kuhukumiwa kwa ajili yenu msalabani!”
Mungu alibeba dhambi za wasio watauwa katika dunia hii kwa njia ya ubatizo wa Yesu ijapokuwa wanadamu wote si watauwa. Mungu alimtuma Mwana wake wa pekee na kubeba dhambi zote kwa ubatizo na kusulubiwa badala ya watu hao. Mungu alikamilisha yote mawili, sheria isemayo mshahara wa dhambi ni mauti na sheria ya upendo wa Mungu kwa wakati mmoja. Aliokoa wenye dhambi wote kwa dhambi zao.
Mungu anasema “Ndiyo wewe huna tena dhambi. Mwana wangu wa pekee ndiye alikuokoa. Ulikwisha kuokolewa” kwa wale wote wenye kuamini kwamba Yesu alibeba dhambi za dunia katika Mto Yordani kupitia tendo lake la haki kwa niaba ya wenye dhambi. Kwa hiyo wamefanywa kuwa haki ingawa si watauwa. Mungu anasema kwamba wao ni watu wake wasio na dhambi ingawa si watauwa, kila anapo ziangalia imani zao katika wokovu wa Bwana. Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi.
Mungu anatuhitaji sisi tusio watawa akisema “Lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiye kuwa mtauwa imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.” Je, tunatenda mema? Hatuwezi, ila tuna udhaifu wa kutenda dhambi, ingawa Mungu bila kujali alituokoa kwa karama ya wokovu. Tunaamini wokovu wa Bwana, ujulikanao kama ubatizo na damu ya Yesu.
 

Yatupasa kuishi kwa imani katika wokovu wa Bwana.
 
Hatimaye tunamsifu Bwana na kumshukuru kwa zawadi yake ya upendo na rehema ya wokovu toka dhambini, tukijua vile kwa hiyari yake alivyo lipa mshahara wote wa dhambi zetu, sisi tusio watauwa. Hatuwezi kumshukuru ipasavyo kwa kulipa kwake mshahara wa dhambi zetu kupitia ubatizo na msalaba pale tunapo hisi kuwa si watauwa mbele za Mungu. Hata hivyo hatuwezi kutoa shukrani zetu vile ipasavyo kwa rehema hiyo ya Mungu ikiwa bado tuna dhani sisi ni watauwa.
Mtu anaye mwamini Yesu Kristo, anaye wafanya wale wasio watauwa kuwa na haki, imani yake inahesabiwa kuwa ya haki. Wale wote wanao amini ukombozi na hukumu ya Yesu ambayo inawafanya kuwa na haki, hupokea zawadi ya Mungu. Hakuna yeyote aliye mtauwa mbele ya Mungu kwa kuwa watu wote hutenda makosa mengi wakijaribu kuishi maisha ya utauwa.
Ukweli wa kamba wanadamu hawawezi kujizuia kutenda dhambi kuthibitisha kutokuwa watauwa. Hivyo basi, mimi ninaishi kwa imani katika wokovu wa Mungu, ijapokuwa si mtauwa. Kuishi kwa imani hakuna maana ya kuishi vile upendavyo. Ipo njia fulani ya kuishi kwa imani kwa mtu aliye mwenye haki kwa imani.
Kila siku, Injili ya wokovu wa Yesu inahitajika kwa walio zaliwa upya mara ya pili. Kwa nini? Kwa kuwa matendo yao si yakiutauwa hapa duniani na hivyo hawawezi kujizuia kutenda dhambi maishani mwao pote. Kila mtu imempasa kuisikiliza habari njema isemayo, Yesu alizibeba dhambi zetu zote duniani kwa njia ya ubatizo wake. Wenye haki ni lazima waisikie na kuitafakari Injili hii kila siku, ndipo basi roho zao zitaweza kuishi na mara kwa mara kuimarishwa kama chemchemi. “Lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.” Ni kwa watu gani ujumbe huu upo? Ujumbe huu umelengwa hasa kwa wale wote tuliopo duniani hapa, tukiwemao mimi na wewe.
Biblia inatueleza kwa undani namna Adamu alivyo fanywa kuwa mwenye haki. Lakini kwa mtu afanyaye kazi, wokovu wa Mungu haumstahili na wala haukubali na badala yake huukataa. Mtu huyu hawezi kuishukuru Injili. Kwanza kabisa kile mstari huu wa 4 inachoelezea ni mtu afanyaye kazi ambapo hujaribu kutenda mema ili aingie Ufalme wa Mbinguni. Aina hii ya mtu hawezi kamwe kushukuru sadaka ya Yesu. Kwa nini? Kwa sababu kutenda kazi nyingi za kimaadili huku akifanya sala za toba ili asamehewe kwa dhambi zake za kila siku, na kwa jinsi hiyo yeye hudhani kwamba, hapaswi kuwa na shukrani kwa rehema za Mungu, ambayo ndiyo Injili kutokana na juhudi zake kwa kiasi fulani katika kupokea msamaha wa dhambi zake. Kwa hiyo mtu huyo hawezi kupokea zawadi ya wokovu wa Mungu.
Biblia inasema “Lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiye kuwa mtauwa imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki” (Warumi 4:5). Maana yake ni kwamba Bwana alituokoa kikamirifu sisi wale tusio watauwa ambao dhambi zetu zisingeweza kusamehewa kwa matendo yetu mema. Pia inaonyesha rehema ya Mungu iliyo thibitishwa kwa wenye haki, waliookolewa kwa kupokea ondoleo la dhambi.
 

Lakini kwa mtu asiyefanya kazi huchukulia rehema ya Mungu kuwa ndiyo rehema hasa.
 
Warumi 4:5 inamhusu yule anaye mkubali Mungu na kuamini maneno yake kama ilivyo kwa Abrahamu. Tunamwamini Bwana aliyeokoa wasio watauwa. Wapo aina mbili za watu kati ya Wakristo. Wale ambao bado wafanyao kazi ili waweze kusamehe dhambi zao na wale ambao walio kombolewa ipasavyo kutokana na dhambi zao. Kama ilivyo andikwa katika mistari ya 4 na 5 “Mtu afanyaye kazi” na “Ujira wake hausheabiwi kuwa neema bali kuwa ni deni” hukataa rehema ya ondoleo la dhambi kwa sababu yeye huja mbele za Mungu akiwa na matendo yake baada ya kumwamini Yesu.
Watu hawato weza kujizuia kuwa wenye dhambi kwa kuwa wana weka mbele matendo yao kwa Mungu. Fundisho la kanuni ya kuhesabiwa haki, nifundisho la Kikristo lenye kutamka kwamba muumini aweza na imempasa kujitakasa hatua kwa hatua kwa viwango hadi siku ya mwisho kifoni, ina pelekea wanao iamini kuikana zawadi ya ondoleo la dhambi na hatimaye kupingana na Mungu. Biblia haisemi kwamba mtu aweza kuwa mwenye haki hatua kwa hatua kupitia viwango. Wale wote wenye kujaribu kujitakasa hatua kwa hatua kupitia viwango kwa kusali sala za toba, kwa kutenda mema na kwa kujisafisha uchafu wao ni wale wafanyao kazi. Hawa ndio watu wanao stahili kwenda jehanamu wakiwa ni watumishi wa shetani. Hawatoweza kuhesabiwa haki kwa sababu wamekataa rehema ya Bwana.
Hakuna kati yetu aliye mtauwa. Hata hivyo wapo watu wengi wanafuata na kuamini mwelekeo usio wa kweli katika nyakati hizi. Wao huamini kwamba dhambi zao halisi husamehewa pale wanapo tubu kila siku, wakijua kwamba Yesu alitakasa dhambi zote za asili na zile za nyuma. Hufanya hivi kwa kuwa hudhani kwamba wao kwa kiasi fulani ni watauwa. Hujionyesha hadharani juu ya uzuri na usafi wa matendo yao mbele za Yesu. Hatimaye hukosa ondoleo la dhambi ambalo ni zawadi ya Mungu.
 

Ni yupi aliye na heri?
 
Watakatifu walio kombolea kutokana na dhambi zao wamekuwa wenye haki kwa kuwa na imani katika Yesu. Jibu la swali ni aina gani ya watu wenye kuwa na haki ni kama ifuatavyo. —Mtu anaye tambua na kukubali juu ya udhaifu wake ana nafasi ya kuwa mwenye haki kwa imani kati ya wengine. Ni wale tu wasi na uwezo wa kuwa watu wema kwa kutenda mema, kufanya maombi, kufuata utauwa na wale wote walio masikini wa roho ndiyo watakao pokea ondoleo la dhambi toka kwa Yesu. Watafanywa kuwa wenye haki. Watu hawa hawakufanya chochote kilicho chema mbele ya Mungu.
Kitu pekee walicho fanya kwa uwazi ni kukiri kwa kusema “Nimetenda dhambi. Mimi ni mwenye dhambi nisiyeweza kujizuia au kuchagu bali kwenda jehanamu nitakapo kufa” Ndipo Yesu Kristo atakapo mpa zawadi ya wokovu kamili alio ukamilisha. Amini ule ukweli wa Bwana kubatizwa na Yohana Mbatizaji mto Yordani ili kubeba dhambi zote za dunia na kusulubiwa kwake, ambako kwa hakika ndiko kunako wezesha wenye dhambi kuokolewa kutokana na dhambi zao zote mioyoni mwao. Wanao amini huvikwa baraka za kuwa watoto wa Mungu. Ni zawadi ya Mungu kwa wote wenye dhambi kuokolewa toka dhambini mbele za Mungu. Namshukuru Bwana, Yesu Kristo kwa kutukomboa tokana na kuangamia.
Katika mstari wa 6, Paulo Mtume anaelezea juu ya mtu aliye barikiwa na Mungu “Pasipo matendo”. Anafafanua sehemu tatu zifuatazo juu ya kwanza “Mtu afanyaye kazi” na pia “mtu asiye fanya kazi”. Biblia inasema, “Kama vile Daudi aunenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa haki pasipo matendo. Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi” (Warumi 4:6-8). “Kutohesabiwa dhambi na Bwana” hakumaanishi kwamba Mungu humhesabia mtu kuwa asiye na dhambi ingawa bado anadhambi, bali maana kamili ya kweli ni kwamba mtu huyo ni kweli hana dhambi.
Mungu anatuambia juu ya baraka za wanadamu. Watu ambao wamesamehewa dhambi zao zote ni wenye furaha. Je, hivi sivyo? Hakuna mwenye furaha kama sisi. Hakuna mwenye furaha kama mtu aliye pokea ondoleo la dhambi. Maana yake ni kwamba, yeyote yule mwenye dhambi, hata ikiwa ndogo kama punje ya shayiri bado atahukumiwa na Mungu, na kamwe hawezu kuwa na furaha hata kidogo. Hata hivyo wenye haki ni wenye furaha kwa sababau wanalo ondoleo la dhambi, Mungu anasema “Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi” (Warumi 4:8).
“Walio sitiriwa dhambi zao” maana yake ni kwamba Bwana alifuta dhambi zote za wanadamu. Daudi pia alisema “Heri waliosamehewa makosa yao” Heri wale ambao makosa yao yamesamehewa, ingawa bado wanaendelea kutenda dhambi siku hata siku hapa duniani bado ni wenye haki, waliopokea ondoleo la dhambi, wameokolewa kutoka na dhambi zao za maisha kupitia Yesu Kristo. Ni wenye haki na hakika ni wenye furaha.
 

Heri yao waliositiriwa dhambi zao.
 
Pili, Ni mtu gani aliye na furaha? “Heri walio samehewa makosa yao na waliositiriwa dhambi zao.” Mara zote sisi hutenda dhambi, lakini nini maana ya mtu kusitiriwa dhambi zake ambazo ndizo Yesu alizibeba kwa ubatizo wake na kusulubiwa kwake. Hivyo basi je, Mungu atatuhukumu? Je, dhambi za wenye dhambi zimesitiriwa? Hatuto hukumiwa kwa kuwa Yesu alibeba dhambi zetu zote, kumwaga damu yake msalabani na kufa kwa ajili yetu kwa kuwa tu ndani yake.
Heri yao wale ambao dhambi zao zimesitirika. Kifo ambacho ni mshahara wa dhambi, hakiwi juu yetu kwa kuwa Yesu alikwisha zibeba dhambi zetu zote kwa ubatizo wake. Haleluya! Tunafurahi! Je tuna dhambi? Hapana. Wale wasio mjua Yesu Kristo, aliyekuja kwa maji na damu, wala hawafahamu kuwa dhambi zote za dunia zilitwikwa juu yake alipo pokea ubatizo katika mto Yordani, kila mara ndio watakao kuwa na dhambi, ingawa wao hujiona wana mwamini Yesu kikamilifu.
Hata hivyo, wale wenye kufahamu juu ya ukweli wa wokovu na kuuamini hawana tena dhambi. Heri yao wale ambao wamemtwika dhambi zao zote Yesu Kristo katika ubatizo wake kwa Yohana Mbatizaji. Ni nani aliye na furaha zaidi katika ulimwengu huu? Heri yao wale walio na mwokozi kwao ingawa wana udhaifu. Heri yao wale wenye kumwamini Yesu, Mwokozi aliyebeba dhambi zao zote, zikiwemo hata ndogo na aliyesulubiwa kuhukumiwa kwa niaba yao.
 

Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi.
 
Heri yao wale wenye kuamini ukweli wa wokovu na kuwa na Mchungaji mwema kwao. Tatu, Daudi alisema “Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi” (Warimi 4:8).
Sisi tulio na ondoleo la dhambi ni wenye haki, ingawa tu dhaifu kimwili. Miili yetu bado huendelea kuwa dhaifu ingawa tu wenye haki kwa imani. Je, Bwana alizichukua dhambi zako zote kupitia ubatizo wake? Je, Bwana anatuchukulia kama watu wa kuhukumiwa? Hapana Bwana hakubaliani na kuwa sisi tuhukumiwe ingawa si wakamilifu na dhaifu. Kwa nini bwana hatuhesabii dhambi? Kwa sababu tayari amekwisha lipa mshahara wa dhambi na kuhukumiwa kwa niaba yetu. Bwana hakumbuki dhambi zetu sisi tulio wenye haki kwa imami au hata kutu hesabia hukumu.
Heri yake mtu yule aliye fanywa haki kwa imani. Heri yake yule mtu aliye zaliwa upya kwa maja na kwa Roho (Yohana 3:5). Mara nyingi tunashughulika zaidi na mambo ya dunia na kupoteza baraka za Mungu, huku tukisahau ukweli kwamba Mungu alituokoa na kutubariki. Tutaweza kwenda kinyume ikiwa tutaipoteza rehema yake. Yatupasa kuwa na rehema ya Mungu katika fikra zetu kila wakati. Wokovu wa Mungu utaendelea kuwemo ndani ya wale wote wenye kuuamini.
Roho Mtakatifu wa Mungu huweka makazi ndani ya wale wote ambao dhambi zao zimefutwa. Ni wenye haki pekee ndiyo wasio hukumiwa na Mungu. Heri yao wale wasio hukumiwa na Mungu katika dunia hii na hata katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa nini? Kwa kuwa watahesabiwa haki na kuwa wenye haki kwa Mungu wakipokea upendo wake na hatimaye kuwa watoto kwake.
 

Tumebarikiwa kwa imani.
 
Heri yao wale watakao kuwa wenye haki kwa imani. Je, walio zaliwa upya mara ya pili ni wenye heri mbele ya Mungu? —Ndiyo.— Paulo Mtume alisema “Furahini siku zote, ombeni bila kukoma, mshukuruni kwa kila jambo, maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu” (1 Wathesalonike 5:16-18) kwa kuwa alibarikiwa kwa imani akiwa ni wa uzao wa Ibrahimu Baba wa imani. Sisi nasi ni uzao wa Ibrahimu. Ibrahimu, aliokolewa kwa imani katika neno la Mungu kama tufanyavyo sisi leo hii. Mungu alizungumza na Ibraahimu “Usiogope Abramu, mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana” (Mwokozi 15:1).
Lakini Abramu akasema “Bwana Mungu, utanipa nini nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakaye miliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?” Ikaendelea kusema “Tazama, hukunipa uzao na mtu aliye zaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu. Ndipo neno la Bwana likamjia likinena, huyu hata kurithi. Akamleta nje akasema Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyo kuwa uzao wako. Aka mwamini Bwana naye akamhesabia jambo hili kuwa haki Kwa njia hii Abramu aliamini maneno ya Mungu.”
Je, wewe nawe waweza kuamini neno la Mungu kama ilivyo Abramu katika ulimwengu huu? Je, haionekani kuwa ni ngumu kwa wanadamu? Mke wa Abramu alikuwa ni mzee sana kushindwa kuzaa mtoto. Hata hivyo Abramu aliamini neno la Mungu na kwa wakati ule neno hili lilikuwa ni tumaini hafifu kwake. Hivyo Abramu akahesabiwa haki mbele ya Mungu.
Yesu alifuta dhambi zetu zote. Yesu alibeba dhambi zetu zote juu yake kwa ubatizo wake na kuhukumiwa kwa kumwaga damu yake. Tunakuwa uzao wa Ibrahimu kwa kupokea ondoleo la dhambi na wokovu wa Mungu kwa sababu tulikuwa si watauwa. Wapo wengine wasioamini katika hili. Biblia inasema “kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu” (1 Wakorintho 1:25). Mungu amewafanya wale wenye kuamini Injili ya Mungu kuwa watoto wake kupitia imani zao katika ubatizo wa Yesu (maji) na msalaba wake (damu). Hili lawezekana kuonekana kama ni upumbavu kwa wanadamu lakini wokovu wa Mungu na hekima yake katika ondoleo la dhambi ndivyo ulivyo. Yawezekana pia kuonekana kuwa ni upumbavu kwa mtazamo wa kibinadamu lakini Mungu amekwisha okoa wenye dhambi wote kwa karama hii ya bure.
Yesu alimwita mmoja mmoja kati ya maelfu toka pande nne za dunia na kuwa bariki hivyo kupokea sifa kupitia kwao. Je, tumebarikiwa au la? —Ndiyo, tumebarikiwa.— Usije sahau haikua kwa sababu ya kazi yako. Ni kwa kuwa tumeamini baraka ya Mungu aliyotupatia na kwa kuwa ametupatia imani kupitia maneno yake Mungu, kutufanya kuwa watoto wake kwa kuja kwake kwa maji, damu na Roho, (1 Yohana 5:4-8) na kwa kuwa ametupatia upendo wake.
Tumebarikiwa ingawa tunaishi tukiwa na madhaifu mengi duniani. Kwa kweli na mshukuru Mungu. Ametupatia baraka zenye thamani, hakutuesabia dhambi, akatusamehe dhambi zetu zote na kutusitiri ingawa sisi tusio watauwa, hatuna uwezo wa kutenda mema kwa ajili ya utakaso wetu. Tumebarikiwa kwa wokovu kupitia imani zetu tu.