Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 4-1] Utangulizi katika Kitabu cha Warumi Sura ya 4

Katika Warumi 4:6-8 Paulo anazungumzia juu ya watu walio barikiwa mbele ya Mungu. Mtu aliye barikiwa kwa hakika mbele ya Mungu ni yule ambaye matendo yake ya uovu yamesamehewa na dhambi zake kusitiriwa. Hivyo Paulo anatamka “Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi” (Warumi 4:8).
Ndipo Paulo anapomwelezea Abrahamu kama mtu aliye barikiwa. Akimtumia Abrahamu kama mtu halisi katika Biblia Paulo anaelezea nini maana ya kweli na baraka ya imani. Abrahamu angelikua na chakujisifu endapo matendo yake yangeliweza kumpatia haki, lakini ukweli ni kwamba haikua hivyo. Haki ya Mungu aliyo ipata iliwezekana kwa kuziamini kazi za Mungu tu.
Biblia inaonyesha kwamba imani ambayo yaweza kumfanya mtu awe mwenye haki na kubarikiwa ni imani ya unyenyekevu katika maneno ya Mungu kama ilivyo kwa Abrahamu. Katika Sura hii, Paulo Mtume anazungumzia juu ya namna mtu awezavyo kuamini maneno ya Mungu.
Hakuna yeyote asiyetenda dhambi kamwe katika maisha yake yote duniani. Zaidi ya yote, sisi watu tunatenda dhambi nyingi mfano wa wingu nene lifunikalo anga. Katika Isaya, imeandikwa kwamba dhambi zetu na uovu wetu ni mfano wa wingu nene (Isaye 44:22). Hiyvo hakuna kati yetu wanadamu awezaye kuikwepa hukumu ya Mungu pasipo kuamini haki ya Yesu Kristo.
Ubatizo wa Yesu alioupokea na damu yake msalabani vimeitimiza haki ya Mungu. Wote kati ya wale waliopokea ondoleo la dhambi na wale ambao bado wanatenda dhambi kwa miili yao, tunatenda dhambi ambazo wakati mwingine hatuzifahamu na hivyo, tume wekewa hatima ya hukumu ya dhambi hizo.
Mtu imempasa kuelewa kwamba ikiwa anadhambi hata kidogo itamlazimu kufa mbele ya sheria ya Mungu. Katika Biblia inasema kwamba “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23) na imetupasa kwa hiyo kuelewa na kuamini sheria ya Mungu. Lazima tulipe gharama ya dhambi tulizo tenda na baada ya kulipa ndipo basi tatizao la dhambi litakapo suluhishwa. Kwa upande mwingine haijalishi ni vipi tunaweza kujibidisha ikiwa tutaendelea kutokulipa gharama ya dhambi, hivyo kufanya swala la hukumu ya dhambi kutokwisha. Kile tunacho paswa kujua ni kwamba hata mtu mwenye kumwamini Yesu huku akiwa na dhambi atahukumiwa kwa dhambi zake.
Tunaishi katika dunia hii iliyo furika kila aina ya dhambi, kubwa na ndogo zielewekazo na zisizoeleweka, za hiyari na zisizo za hiyari. Hatuwezi kuacha kukubali ukweli kwamba imetupasa kuhukumiwa kifo kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na sheria ya Mungu. “Mshahara wa dhambi ni kifo.”
Ikiwa mtu anatamani dhambi zake zote zifutwe, basi inamlazimu kupokea ondoleo la dhambi kwa kuamini haki ya Mungu ambayo huja kwa maji, damu na Roho Mtakatifu. Mtu aliyekwisha kupokea ondoleo la dhambi kwa kuamini haki ya Mungu ana uwezo pia na hadhi iliyo sawa katika kutoa sadaka ya sifa kwa Mungu kila mara, kwa kuwa Mungu amekwisha kuzibeba dhambi zake zote kwa njia ya ubatizo na damu yake. Kwa kuwa Bwana wetu alikwisha kuzichukua dhambi zote za dunia zikiwemo zile zangu mfano wa wingu, kwa ubatizo wake, damu na ufufo wake, hivyo basi tuna kuja na shukrani mbele za Bwana aliyetupa uzima wa milele.
Ikiwa kama Yesu Kristo asingelibeba dhambi zote Yordani kwa kubatizwa na Yohana na kufa msalabani tungelipia mshahara wa kifo kwa kwenda jehanamu. Tutawezaje kumsifu yeye, ikiwa bado hajazifuta dhambi zetu zote? Je, itakuwa rahisi kwetu kulisifu jina la Mungu kila tunapo kuja mbele ya Mungu wetu Mtakatifu Mkuu, ikiwa mioyo yetu imejawa na dhambi? Je, tungeliweza kweli kutoa sadaka ya sifa kwa haki yake tukisema, “ametusamehe dhambi zetu zote” hali bado tukiwa na dhambi mioyoni mwetu? Hapana.
Lakini sasa tunaweza kumsifu Mungu kwa ajili ya haki yake. Yote haya yamewezekana kwa kuwa tunaamini karama ya haki ya Mungu, ambayo ndiyo tuliyo vikwa.
 

Paulo alisema kwamba tumepata haki ya Mungu kwa kuamini kile Mungu alicho kifanya.
 
“Basi tusemaje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili? Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake analo la kujisifia, lakini si mbele za Mungu. Maana maandiki yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa haki. Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema bali kuwa nideni. Lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiye kuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa” (Warumi 4:1-5).
Hapa Paulo anaelezea namna ya kuhesabiwa haki kwa kumchukulia Abrahamu kuwa mfano. Ipo sababu kwa mtu kupokea ujira anaostahili kwa kazi yake. Hata hivyo ni kwa karama halisi za Mungu na si mshahara kwa matendo yetu pale tunapo fanywa kuwa wenye haki kwa kuzaliwa upya mara ya pili pasipo kutenda chochote au kuishi maisha yaliyo makamilifu mbele ya Mungu.
Paulo Mtume alisema “Lakini kwa mtu afanyaye kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema bali kuwa ni deni.” Hii inazungumiza namna vile mwenye dhambi apatavyo wokovu wa dhambi kupitia ubatizo wa Yesu Kristo na damu yake ya dhabihu. Wokovu huu ulitolewa kwetu kama baraka ya ondoleo la dhambi kwa wote wenye kuamini haki ya Mungu.
Wakovu wa wenye dhambi ni kipawa au zawadi isiyo na sharti toka haki ya Mungu. Aliyezaliwa akiwa mwenye dhambi hana uchaguzi zaidi ya kutenda dhambi na pia hana uchaguzi zaidi ya kukiri kwa Mungu kwamba yeye ni mwenye dhambi bila hiyari au kujizuia. Dhambi za watu aina hii kamwe haziwezi kutoweka kwa sababu tu ya kuamini aina fulani ya kanuni na mafundisho ya Kristo yaliyopo.
Mwenye dhambi hawezi kujisifia haki yake mbele ya Mungu “kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi” (Isaya 64:6). Hivyo, mwenye dhambi hana uchaguzi zaidi ya kuiamini haki ya Mungu, ambayo ilitimizwa kwa ubatizo wa Bwana katika Mto Yordani na kifo chake cha upatanisho msalabani. Ndipo hapo basi tutakapo samehewa dhambi zetu zote kwa imani katika haki ya Mungu. Hakuna la ziada au zaidi mwenye dhambi aweza kulifanya ili kupokea haki ya Mungu. Ondoleo lako la dhambi laweza kupatikana kwa kuamini haki ya Mungu.
Wenye dhambi wote wanaweza kupata haki yake kupitia ubatizo wa Yesu Kristo na damu ya upatanisho msalabani. Kwa hiyo ni imani katika haki ya Mungu ndiyo inayomwezesha mwenye dhambi kupokea wokovu wa dhambi. Hili ni kweli. Hii ndiyo zawadi ya haki ya Mungu.
 

Mtume Paulo anazungumzia juu ya mwenye dhambi awezavyo kupokea wokovu wa dhambi zake zote.
 
Paulo anazungumza hili kwa kumtumia Ibrahimu kama mfano halisi “Lakini kwa mtu afanyaye kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa nineema bali kuwa ni deni.” Paulo Mtume anasema kwamba mtu hatoweza kupata haki ya Mungu kwa kufanya aina fulani ya matendo ya sheria. Njia pekee tuwezayo kupata haki ya Mungu ni kwa kuamini maneno yake ya haki juu ya tohara ya kiroho.
Haki ya Mungu ni ukweli ambao kamwe hautoweza kupatikana kwa juhudi za kibinadamu au matendo. Zawadi hii ya haki ya Mungu ni kama ifuatayo:— Wewe na mimi tulikuwa ni watu tulio kuwa na hatima ya kuingia adhabu ya milele, lakini Mwokozi Yesu Kristo alibeba dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo wake toka kwa Yohana katika Mto Yordani. Kwanjia hiyo alibeba dhambi zetu zote juu yake na kwenda msalabani ambapo alilipa mshahara wa dhambi hizo kwa gharama ya damu yake. Ndipo hapo basi Yesu alipo itimiza haki ya Mungu. Matendo yote ya haki yalitimizwa kwa haki ya Mungu yenye kuokoa wenye dhambi kwa kifo cha milele.
 

Wale wote wenye kuamini maneno ya Mungu wataweza kupata haki ya Mungu.
 
Mstari wa 5 unatamka “Lanini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.”
Katika sehemu hii Paulo Mtume anaelezea njia ya kuelekea katika haki ya Mungu kwa kutumia neno “asiyekuwa mtawa” kama mfano. “Wasio watawa” ni wale wote ambao pamoja na kwamba hawamwogopi Mungu pia hutenda kufuru kwa maisha yao yote. Maneno ya Mungu yasemayo kwamba watu wote wamezaliwa wakiwa na wingi wa dhambi bila shaka ni ya kweli. Zaidi ya yote, pia ni sawa na kusema kwamba siri ya kweli ya wanadamu ni ile kwao kutokuwa na uchaguzi zaidi ya kutenda dhambi mpaka pale watakapo pokea hukumu ya kutisha toka kwa Mungu. Hata hivyo ikiwa Mungu anatuita sisi tusio watauwa kuwa tusio na dhambi na hata kutuhesabia imani zetu kuwa haki, sasa basi ni lipi la ziada liwezeshalo hili zaidi ya haki ya Mungu?
Bwana wetu ananena nasi tusio watawa. Bwana mwenyewe ili mlazimu apokee ubatizo katika Mto Yordani toka kwa Yohana Mbatizaji, Kuhani Mkuu wa Agano la kale aliye wa mwisho, ili kubeba dhambi zote za dunia. Pia ilimpasa alipe mshahara wa dhambi kwa kumwaga damu ya upatanisho msalabani ili kutimiza sheria ya maneno yake ya “mshahara wa dhambi ni mauti”. Je, unaamini kwamba Yesu Kristo alilipa mshahara wote wa dhambi kwa haki ya Mungu kwa njia ya ubatizo alio upokea na damu yake msalabani? Mungu huihesabu imani ya wale wote wanao amini haki ya Mungu kuwa ndiyo yenye haki. Hili halikuwa ni tukio la kujaribu kupingana bali ni ukweli uliotokana na usawa wa haki ya Mungu.
Kwa hiyo kwa mtu anaye iamini haki ya Mungu, Mungu Baba anasema, “Sawa ninyi ni watu wangu. Mnaamini haki yangu. Sasa ninyi ni watoto wangu. Ninyi hamna dhambi tena, kwa nini? Kwa sababu nimewafanya kuwa msio na dhambi kwa kuzibeba dhambi zenu zote kupitia ubatizo wa Mwana wangu wa pekee na damu yake! Pia alilipa gharama ya dhambi zenu kwa damu yake aliyo mwaga kutokana na sheria ya “mshahara wa dhambi ni mauti”. Akafufuka tena toka kifoni kwa ajili yenu. Hivyo yeye ndiye Mwokozi wenu na ni Mungu, Je, mnaamini hili?”
“Ndiyo ni mimi” Nakuendelea kusema “Nimewapa haki yangu iliyo kamilishwa na tendo la haki la Mwana wangu. Sasa mmekuwa watoto kwangu, nimewarithi kwa maji na damu ya Mwana wangu.”
Wanadamu wote si wataua mbele za Mungu. Hata hivyo, Bwana wetu Yesu alibeba dhambi zao zote hao wasio watauwa, zote mbili, za kale na zijazo mbeleni—zaidi Mungu amewavika wale wote wenye kuiamini haki ya Mungu kwa vazi la haki yake na hivyo kuwaokoa kwa dhmbi zao zote “kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu” (Wagalatia 3:26-27). Sasa swali ni juu ya ama kweli tunaamini neno la Mungu kwa mioyo yetu au la!. Tunakuwa wenye haki ikiwa tunaamini, lakini kinyume cha hili basi tuna ipoteza haki ya Mungu.
 

Hata asiyekuwa mtauwa mbele ya Mungu…
 
Hata kwa wale wasio watauwa mbele ya Mungu, yeye aliahidi kwamba haki yake itakuwa ni yao ikiwa tu wataamini kwamba Yesu alibeba dhambi za dunia mara moja kwa kubatizwa mto Yordani. Kwa hakika Mungu alitoa haki yake kwa kila aiaminiye. Yeyote anaye amini haki ya Mungu hupokea wokovu kutokana na dhambi zake zote. Baba yetu anawaeleza wale wenye kuiamini haki yake kwamba wao ni watoto wake. “Ndiyo, sasa ninyi hamna tena dhambi. Mwana wangu Yesu aliwaokoa kutokana na dhambi zenu zote. Ninyi ni wenye haki. Mmekwisha okolewa kwa dhambi zenu zote.”
Ingawa sisi si watauwa, Mungu ametuweka mhuri wa haki juu yetu ili kudhihirisha kwamba tu wa haki. Haki ya Mungu ni ya milele. Bwana Yesu ametenda kazi njema hakika kwa wanadamu wote. Watu wa dunia hii waliokolewa kwa dhambi zao zote duniani kwa haki ya Mungu. Mungu huzihesabia nafsi za wasio watauwa kama wasio na dhambi kwa kuangalia imani zao katika haki yake. “Heri mtu yule ambeye Bwana hamhesabii dhambi” kwa kuwa ameipata baraka ya haki ya Mungu kwa imani.
Mungu anatuuliza, “Je, weweni mtauwa?” Ndipo tunapo kiri ukweli kwamba si watauwa mbele zake Mungu. Tunapo ukubali ukweli huu ndipo tunapo ridhika kwamba Yesu aliupokea ubatizo kwa ajili ya wenye dhambi, akamwaga damu yake msalabani na kwamba hiyo ndiyo haki ya Mungu yenye kuichukua dhambi za dunia na si juhudi zetu. Hata hivyo ikiwa tutadhani kwamba sisi ni watu ambo tunaweza kuitii sheria vyema, basi hatutoweza kuridhika au hata kuwa na imani katika haki yake.
Anayeamini haki ya Mungu “yenye humhesabia haki asiyekuwa mtaua” apata haki yake Mungu kama zawadi. Haki ya Mungu itatolewa kama zawadi kwao wale wenye kuamini ukombozi na hukumu ya Yesu Kristo, lakini kwao wasio amini haki ya Mungu baraka zote za Mungu na rehema zake zitabaki kufungwa.
Hata kwa aliyezaliwa upya mara ya pili haki ya Mungu iliyo dhihirishwa na Yesu ni muhimu siku hata siku, kwa kuwa hata sisi tunao amini haki ya Mungu ni watu tusioweza kujizuia kutenda dhambi huku tukiishi duniani. Hivyo, tunahitaji kujikumbusha nafsi zetu juu ya habari ya furaha ya haki ya Mungu kila siku ambapo Yesu alizichukua dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo wake na damu yake msalabani. Kila wakati tunapo sikia habari za furaha zinatukonga nafsi zetu na kututia nguvu mioyo yetu kwa wingi wa nguvu. Je, sasa unaelewa maana ya kifungu kisemacho “Lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabiaye haki asiyekuwa mtaua?” (Warumi 4:5). Maandiko haya huzungumzia juu ya watu wote duniani.
Biblia inazungumzia kwa undani namna ya mtu awezavyo kupata haki ya Mungu kupitia mfano wa Ibrahimu. Hata hivyo inaseme kwamba mtu “afanyaye kazi” anapingana na Mungu badala ya kuridhika na wokovu wake. “Anaye fanya kazi” haiamini haki ya Mungu na hivyo haridhiki nayo. Kile mstari wa 4 inacho sema ni kwamba mtu anaye jaribu kwenda Mbinguni kwa kutenda matendo mema basi kwake haihitaji haki ya Mungu.
Kwa nini? Kwa sababu hakuna haki ya Mungu inayowezekana kupatikana kwa kujaribu kutakasa dhambi kwa njia ya kutenda mema na kusali sala za toba kila siku. Mtu aina hii hataki kuikubali haki ya Mungu moja kwa moja, kwa kuwa kwa hiyari hataki kutupilia mbali yale yanayo onekana kuwa ni mema kwake, kwani kwa njia ya sala za toba yeye hujaribu kupata wokovu wa nafsi yake huku akilia na kufunga kula. Kwa hiyo haki ya Mungi inatolewa kwao wale tu wanao amini maneno ya haki ya Mungu kwa dhati.
 

Lakini kwa mtu afanyaye kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema!
 
“Lakini kwa mtu asiyefanya kazi anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki” (Warumi 4:5). 
Ndugu, andiko hii linahusiana na mtu mwenye kumkubali Mungu na ambaye mwenye kuyaamini maneno ya Mungu kama ilivyo Ibrahimu.Tuna mwamini Bwana wa wokovu aliyetuokoa sisi tusio watauwa. Wapo aina mbili za waumini Wakristo duniani. Katika mstari wa 4 hapo, wapo wale “wafanyao kazi” na aina hii ya watu hawauchukulii wokovu wa Mungu kama zawadi bali ni deni. Kwa sababu aina hii ya watu hupenda wajulikane kwa matendo yao mema mbele ya Mungu baada ya kumwamini Yesu, hivyo hujikuta wakikataa wokovu wa haki ya Mungu. Aina gani ya sadaka unadhani hakika katika kupokea haki ya Mungu inahitajika?
Ikiwa unatembea mbele ya Mungu kwa kushikilia matendo yako mema, basi umekuwa ni mwenye dhambi tu kwa kutopokea haki ya Mungu. Je, unajua kwamba “Fundisho la Kanuni ya Utakaso”, ambalo Wakristo wengi hulikubali huwashawishi zaidi katika kufanya matendo mema, na kuwafanya wawe adui kwa kupingana na haki ya Mungu? Biblia haitamki kwamba tunaweza kupata haki ya Mungu hatua kwa hatua. Au hata kusema kwamba tunaweza kupata haki ya Mungu kwa matendo yetu mema.
Wanao kubaliana na “matendo mema ya kibinadamu” hufundisha kwamba, waweza kutakaswa kupitia sala za toba. Husema kwamba waweza kuwa mwenye haki zaidi ikiwa utaishi maisha safi na ya uadilifu na hivyo kuokoka ikiwa utaishi hata mwisho wa kifo ijapokuwa tayari Yesu Kristo amefuta dhambi zako.
Hata hivyo, haki ya Mungu haichanganyiki na matendo ya mwanadamu. Wale wenye kukabiliana na haki ya Mungu hujikuta wakiwa washirika na pepo wachafu kwa sababau aina hii ya watu hukataa haki ya Mungu. Wakishindwa kupokea ondoleo la dhambi mbele ya Bwana.
Ndugu sisi ni 100% tusio watauwa. Hata hivyo ukweli ni kwamba watu wengi hawaielewi vyema haki ya Mungu na kwa maana hiyo hutembea katika njia ya imani isiyo kweli. Basi kwa kuwa watu hudhani kwamba kwa kiasi fulani wao ni watauwa, hawaamini haki ya Mungu. Huamini kwamba wataweza kusamehewa dhambi zao za kila siku na zile za mbeleni kwa kuomba toba. Watu hawa huamni kwamba upo utauwa kwa kiasi fulani ndani yao, hivyo basi huweka mbele matendo yao mema pasipo kuitafuta na kuiamini haki ya Mungu.
Aina gani ya Mtu aweza kuwa mwenye haki? Wale ambao hawawezi kufanya sala za toba wataweza kuwa wenye haki. Hii haina maana kwamba mtu haitaji kukiri dhambi zake. Natumaini hauto elewa vibaya ninacho elezea katika sehemu hii. Baadaye ni takuja kuelezea somo la “maisha ya mwenye haki”. Wale wapingao haki ya Mungu huwaza kutenda matendo mema wakifanya maombi ya kufunga chakula au kuishi kwa uadilifu mkubwa.
Hata hivyo, ni wale tu wenye kujua kwamba matendo yao hayajitoshelezi ndio watakao weza kuwa wenye haki wakitoka katika hali ya dhambi mioyoni mwao. Kitu pekee tunachopaswa kufanya ni kuamini haki ya Mungu na kujua kwamba hakuna cha kujisifia kati ya haki zetu. Kile tunacho paswa kukikubali mbele ya Mungi ni kusema “O, Mungu! Tumetenda dhambi hizi. Sisi ni wenye dhambi ambao tutaendelea kutenda dhambi hata mwisho wa uhai wetu” Hicho ndicho kitu pekee tuwezacho kukiri kwa uwazi. Na kitu kingine pekee tunacho paswa kufanya ni kuamini kuwa Yesu Kristo ameitimiza haki yake yote.
Kwa kuiamini haki ya Mungu, kila mwenye dhambi ataweza kupokea wokovu kwa dhambi zake zote moja kwa moja. Tuna sifu kwa imani katika haki ya Yesu Kristo kwa kuwa ilitubidi kuangamia katika dhambi, hivyo badala yake tumepata wokovu wa dhambi zetu zote.
 

Ni mtu gani aliye barikiwa haswa?
 
Ni mtu gani haswa aliye barikiwa mbele ya Mungu? Biblia ina mwelezea mtu aliye barikiwa kama ifuatavyo, “Heri waliosamehewa makosa yao, na waliositirika dhambi zao.” Hata ikiwa mtu hana uwezo wa kutenda matendo mema au hakuweza kufuata sehemu fualani ya sheria za Mungu, yeye bado hutoa baraka ya ondoleo la dhambi kwa uzima wa wale wanye imani katika haki ya Mungu yenye kufuta dhambi zetu zote kwa ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Watu aina hii huiamini haki ya Mungu na ndiyo walio barikiwa hasa mbele ya Mungu, kwa kuwa wamepokea baraka ya pekee mbele yake dhidi ya umati wote. Tumepokea wokovu kutokana na dhambi zetu zote kwa kuiamini haki ya Mungu. Tunaamini hivyo Mungu alivyo nena. Je, tunachochote zaidi kuongeza katika maneno yake ingawa tariyai Mungu amekwisha nena hivyo? La hasha hatuna.
Wapo watu wengi duniani ambao bado wanajaribu kupata wokovu kwa matendo yao mema, ingawa wao hukiri kwamba Yesu ni Mwokozi wao.
Je, kunachochote cha ziada kuongezea ukweli wa wokovu toka dhambini, ambao unatamka kwamba Yesu alibatizwa na Yohana akamwaga damu msalabani na kufufuka baada ya kifo? La hasha, hakuna.
Hata hivyo, Wakristo wa nyakati hizi wamechanganyikiwa juu ya sehemu ile ya kuamini haki ya Mungu. Watu hudhani kwamba wangeweza kupata wokovu kwa kumwamini Yesu tu. Lakini kwa upande mwingine bado wanaendelea kudhani ni muhimu kwa wokovu wao kwamba, inawalazimu kujitakasa hatua kwa hatua, wakiishi kwa uadilifu, na kufuata sheria ya maneno ya Mungu punde wanapo anza kumwamini Yesu. Kwa njia hii basi watu hao huishia kuchanganyikiwa.
Ingawa kile wanacho sema kinaonekana kufanana na lile la kuwa mwenye haki, lakini ni mbali na imani ambayo hutambua na kuiamini haki ya Mungu. Itawezakana vipi mtu kumwamini Bwana vile ipasavyo? Inaweza kana pale tu tunapokuwa na imani isiyo na maswali katika maneno ya maji na Roho Mtakatifu, yaliyo na haki ya Mungu na kwa hiyo kuweza kupokea wokovu wa dhambi zetu zote. Ukweli wa Mungu unatuwezesha kupokea wokovu tokana dhambi zote kwa imani zetu katika ubatizo na damu ya msalabani, ambamo ndimo dhahiri kulimo na haki ya Mungu.
Yatupasa kutupilia mbali mafundisho batili ya kanuni za Kikristo yanayo husu utakaso wa viwango hatua kwa hatua, kuchaguliwa pasipo sharti na kufanya haki kusiko zingatia sheria ya Mungu, au imani isiyo ya kweli itamkayo kwamba mtu aweza kupata wokovu hapo mbeleni kwa kuto kula nguruwe au kufuata sabato. Yatupasa kujiepusha na hao wazungumzao upuuzi wa aina hii. Watu wa aina hii hawana hitimisho au jibu sahihi kwa mazungumzo yao.
Ndugu, je, si imani sahihi au la, kwetu kupata wokovu toka dhambinbi kwa kuamini haki ya Mungu pasipo kutenda chochote chema? —Ndiyo ni kweli hiindiyo imani halisi.— Aina gani ya matendo tuliyofanya katika kupokea haki ya Mungu? Je, tumetenda chochote mbele ya Mungu?                 —Hapana.— Je, sisi ni wakamilifu kwa uwezo wetu au hata kimawazo? —Hapana.— Sasa basi, je, hii inamaana kwamba imetupasa kuishi namna vile tutakavyo? —Hapana.— Je, imetupasa kuishi kwa ustaarabu na kufuata sheria ili tuwe watoto wa Mungu? —Hapana.— Ina maana sasa imetupasa kuwa watoto wa Mungu kweli kwa kuamini haki yake tu, kwa kupata ondoleo la dhambi, na kumpokea Roho Mtakatifu kama zawadi kupitia imani sahihi.
Haiwezekani kabisa kwa mtu kuishi maisha ya udilifu kwa sheria. Hata hivyo ingawa mtu hawezi kutenda mema ikiwa bado anaiamini haki iliyo tolewa na Yesu, basi mtu huyo anaheri na ameokolewa kwa dhambi zake zote. Kila mtu ametoka katika asili ya kushindwa kuishi maisha yaliyo nyooka kiudilifu. Kwa hiyo Mungu alisikitishwa kwa hili hata kumtuma Yesu kuja katika ulimwengu huu na kumfanya abatizwe na Yohana Mbatizaji ili kwamba abebe dhami za dunia. Na ndipo Yesu alipopelekwa nazo msalabani na kusuluhisha tatizo la dhambi.
Katika mithali za Mashariki ya Mbali, upo usemi usemao “Mtu imempasa kutoa uhai wake kuwa kafara kwa ajili ya mazuri ya wengine.” Mtu anapojitosa na kuangamia kwa ajili ya uhai wa mwingine anaye angamia kwa mafuriko, husifiwa kwa hatua ya kujitoa mhanga. Ndugu wapendwa, hii inamaana kwamba kujitoa mhanga kumwokoa mtu aliye hatarini ni kawaida kujisifia na kujiona kuwa wa zaidi juu ya hili.
Upo usemi mwingine wa kale kwa lugha ya Kikorea unaosema, “Ingwa-eungbo” Maana yake, ikiwa mtu ataishi maisha ya uadilifu basi atabarikiwa mbeleni, lakini aweza kuadhibiwa ikiwa hatokuwa na tabia njema ya udilifu. Ndugu wapendwa, je, hivi kweli yupo mtu awezaye kujitoa mhanga maisha yake kwa ajili ya mtu mwingine? Hata kama ni kwa swala la mapenzi ya jinsia za tofauti, wanaume na wanawake hupendana kwa sababu kwa wakati huo inakidhi haja zao. Kwa mifano hii, watu wote kwa msingi ni wenye tabia ya ubinafsi.
Kwa hiyo, Mungu anasema kwamba hakuna uadilifu ndani ya mwanadamu na imetupasa kujichunguza kwa uangalifu ikiwa kweli tunategemea na kuiamini haki ya Mungu au la, ambayo ndiyo iliyo ondoa hata ule udhaifu wetu mkuu, ingawa bado hatuja wahi kutenda matendo mema kamwe. Yatupasa kupokea wokovu kwa dhambi zetu zote kwa kuamini haki ya Mungu aliyo tupatia.
 

Yatupasa kupokea ondoleo la dhambi zote za matendo maovu.
 
Ni matendo gani maovu mbele za Mungu? Makosa yote tuliyo kwisha tenda mbele ya Mungi ni matendo ya uovu.
Kwa jinsi gani basi mimi na wewe dhambi zetu zaweza kusitiriwa mbele ya Mungu? Je, vazi nene la kuzuia risasi laweza kusitiri dhambi zetu? Au je mita 1 ya unene wa chuma cha pua chaweza kusitiri dhambi zetu mbele ya Mungu? Ndugu zangu kila tunapofanya matendo mema, je, matendo haya yanaweza kufunika makosa na uovu tunao tenda mbele ya Mungu? Hapana. Matendo mema ya mwanadamu si chochote zaidi ni namna ya kujiliwaza tu. Mtu kamwe hawezi kukwepa hukumu ya haki ya Mungu kwa kujiliwaza nafsi yake kwa kutenda mema. 
“Heri walio samehewa makosa yao na waliositiriwa dhambi zao.” Hivi ndivyo ilivyo nenwa katika Biblia. Ndugu wapendwa ikiwa tunahitaji kusitiriwa dhambi zetu mbele ya Mungu, njia pekee ya kufanya hilo ni kuiamini haki ya Mungu ambayo ndiyo iliyotuokoa sote. Haki hii ya Mungu ikijumuisha kuja kwa Yesu Kristo hapa duniani, kupokea ubatizo, kubeba dhambi zetu na kujitoa mhanga kwa kifo cha msalabani. Kwakuwa Yesu alibeba dhambi za dunia kwa kubatizwa na kwa sababu alipokea hukumu ya kifo msalabani, hii ndiyo haki ya Mungu. Dhambi zote husitirika pale mtu anapo amini haki hii ya Mungu.
Hata ikiwa mtu atajaribu kusitiri dhambi zake kwa matendo mema, hakuto kuwa na maana mbele za Mungu. Ni tendo pekee la haki ya Yesu katika ubatizo na damu yake ambalo ndilo liwezalo kusitiri dhambi zako na zangu. Ilitupasa kuhukumiwa, kuangamizwa na kwenda jehanamu kutokana na hasira ya Mungu juu ya dhambi zetu, lakini Yesu alikuja duniani na kuitimiza haki ya Mungu kwa ajili yetu kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji na kufa msalabani. Yakupasa uamini hili. Dhambi zetu zaweza kusitiriwa kwa imani katika haki ya Mungu. Kwa nini? Kwa sababu haki ya Mungu tayari imekwisha fanya fidia ya haki kwa dhambi za dunia kupitia ubatizo na damu iliyo mwagika. Mimi na wewe dhambi zetu zaweza kusitirika kwa kuamini ukweli huu tu.
Ni aina gani ya mtu aliye mwenye heri? Ni yule mwenye imani aina hii ndiye mwenye heri “Heri walio samehewa makosa yao, na waliositirika dhambi zao.” Mtu aliye na aina hii ya imani ndiye mwenye furaha na mwenye heri. Je mimi na wewe tuna aina hii ya imani? Mtu yule ambaye ni mwenye heri hakika huya chukulia maneno ya Mungu ndani ya moyo wake, ambayo Yesu Kristo alituokoa kwa maji na Roho Mtakatifu. Ampokeaye Yesu Kristo pamoja na maji na damu yake kwa pamoja moyoni mwake na kufanya makazi ndani ya Yesu Kristo hakika ni mwenye heri. 
Kwa imani, sisi tunao iamini ya haki ya Mungu tumepokea wokovu wa ajabu usio jumuisha wazo au tendo jema la mwanadamu hata kidogo. Mtu pekee aliye na heri niyule anaye amini katika hili na kuhubiri Injili ya kweli.
Ndugu zangu usithubutu kamwe kuwa mtoto wa Mungu au kuokolewa toka dhambini kwa kujumuisha matendo yako mema na ya udilifu katika rehema zake! Je, wewe ni mwadilifu! Ni majivuno ikiwa mtu atajaribu kuwa mwadilifu ingawa kwa hakika sivyo alivyo akidhani kuwa ataweza. Ikiwa mtu fukara atapokea kipande kikubwa cha almasi toka kwa tajiri bilionea kama zawadi, kitu pekee fukara hiyo atakacho fanya ni kusema “Ahsante”. Mfano huu ni sawa na kupokea haki ya Mungu.
Warumi sura ya 4 ilizungumza juu ya watu waliobarikiwa na Mungu. watu kama hao wameokolewa kutoka kwa dhambi zote kwa kuamini maneno ya injili ambayo yana haki ya Mungu.
Natumaini baraka hizi zitakuwa ni zako.