Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 3-3] Je, unamshukuru Mungu kwa ajili ya Bwana? (Warumi 3:10-31)

(Warumi 3:10-31)
“Kama ilivyo andikwa ya kwamba hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye! Hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia, Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja, Koo lao ni kaburi wazi. Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao ina mbio kumwaga damu, uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. Wala njia ya amani hawa kuijua. Kumcha Mungu hakupo machoni pao. Basi twajua kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini na torati, ili kila kinywa kufumbwe na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu kwa sababu haku na mwenye mwili atakaye hesababiwa haki mbele zake kwa katendo ya sheria, kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria. Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria, inashudiwa na torati na manabii ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti, kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake ili aonyeshe, haki yake kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizo tangulia kufanywa, apata kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu. Ku wapi basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani. Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imanai pasipo matendo ya sheria. Au Je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam ni Mungu wa Mataifa pia, kama kwa kweli Mungu ni mmoja atakaye wahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasio tahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imna iyo hiyo. Basi je, twaibitili sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.”
 

Wanadamu hawana chochote cha kujisifu kwa miili yao.
 
Warumi 3:10-12 inatamka “Kakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye, hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia, hakuna mtenda mema la! hata mmoja.” Sisi sote ni wenye dhambi mbele ya Mungu kwa sababu ya miili. Je, mtu aweza kuwa mwenye haki kwa mwili wake binafsi? Je, kuna mwenye haki kwa asili mbele ya Mungu? Mwanadamu kamwe hawezi kuwa mwenye haki kwa kutegemia mwili. Mwili hautoweza kuwa wenye haki pasipo kukombelewa toka dhambini kupitia Yesu Kristo.
Wale ambao dhambi zao zimefutwa hawana la kujisifu katika miili yao, sisi ambao dhambi zetu zilifutwa pia hatuna la zaidi ila kuachana na miili yetu na kuona kwamba hatuna uwezo wa kutenda jema. Hatuwezi kusema kwamba tumeishi kwa udilifu kama siyo pale tunapomtumikia Bwana na kufanya kazi za kiroho, kama vile Yesu alivyosema “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho” (Yohana 3:6) mwili hupendelea zaidi kufuata tamaa zake na roho kumfuata Roho. Kamwe mwili hautoweza kubadilika na kuwa roho.
Wanadamu wote wamezaliwa wakiwa na dhambi, wa kiishi chini ya dhambi, kufa wakiwa njia panda na hatimaye kutupwa katika moto wa jehanamu. Wasingeliweza kuwa na tumaini ikiwa kama Mungu asinge mtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni kuokoa wenye dhambi wote. Ikiwa kama kunatumaini kwetu, ni kwa sababau tu Mungu ndiye aliye tupati tumaini la kweli. Kama isingelikuwa ni Mungu, basi tusingelikuwa wenye haki au tumaini. Hii ni kweli pale tunapo chunguza hatima ya kila nafsi ikiwemo yako na yangu hapa ulimwenguni.
Ingawa tunaitwa “mabwana wa uumbaji” bado hatima yetu ni kuzaliwa tukiwa wenye dhambi, bila kujali utashi wetu, tukiishi katika njia panda na hatimaye jehanamu. Ni kwa jinsi gani basi tulivyo wa muda mfupi! Mara kadhaa maisha ya mwanadamu yanatafsiriwa kama maisha ni ya muda mfupi kama yale ya nzi anayezaliwa na kuishi maisha yake yote kwa masaa au siku chache hatimaye kurudi mavumbini bure. Hatuna tumaini pasipo Yesu. Jambo ambalo ni muhimu zaidi analoweza kulifanya mwanadamu katika uahi wake maishani ni kuzaliwa kula kunywa kufa na kwenda jehanamu ingawa aweza kuwa maarufu au tajiri. Tunaishi pasipo faida na kutoweka pasipo faida na hatimaye kupokea hukumu ya milele.
Hata hivyo, Mungu alitupatia sheria ili kutuwezesha kutambua dhambi na kutupatia haki bure kwa rehema zake kupitia ondoleo la dhambi katika Yesu Kristo. Alimtuma mwana wake wa pekee Yesu, aliyezichukua dhambi zetu zote na kusulubiwa ili awe kipatanisho kwa wale wote watakao amini ubatizo na damu ya Yesu. Mungu alimfanya Yesu awe kipatanisho kwa ajili yetu na kutufanya tuwe wenye haki.
Itawezekanaje kwa wale walio na ondoleo la dhambi kuweza kuwa wenye haki? Je, sisi wenye ondoleo la dhambi tuna haki ya kimwili? Je, kuna sehemu tunayo weza kujisifia mbele za Mungu? Hatuna cha kujisifia katika mwili kwa sababu ya Bwana Mungu, tunafanyika na kumpa shukrani yeye, kwa kuwa tunalo ondoleo la dhambi, uhakika wa wokovu na uzima wa milele.
Sisi tulio na ondoleo la dhambi hatuna chochote pasipo Mungu. Je, mwili wa mwanadamu unachochote cha kujisifu? Je, mwili unayo haki hata kidogo? Je, tunachochote cha kujisifia katika umri wa miaka 70-80 ya maisha yetu? Mwanadamu hana haki. Je, nini tulicho nacho cha kujisifia? Mwili hauna chochote cha kujisifu, hata kwa 0.1%.
 

Kitu pekee cha kujisifu ni haki ya Mungu.
 
Kile tunacho jisifu ni kwamba, Bwana alituokoka toka dhambini, kama ilivyo andikwa “Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria, inashuhudiwa na torati na mababii.” Bwana ndiye uzima wetu wa milele na Mwokozi. Ametufanya kuwa haki. Sisi ni wenye haki kwa sababu Yesu ametuokoa vile ipasavyo. Hatuna cha kujisifu kwa mwili au kwa matendo ya sheria. Tunamshukuru na kumsifu Bwna kwa kubatizwa na kusafisha dhambi zote za dunia ili kuitimiza haki yote.
Tunakuwa na haki ya imani. Bwana aliokoa watu wote ulimwenguni kwa dhambi zao pasipo kumwacha hata mmoja. Wokovu wa Mungu unatufanya kuwa wenye furaha na kutupa tumaini, unatupa nguvu mpya. Hatuna cha kujisifia bali Bwana. Zaidi tukijisifia juu ya haki zetu mbele ya Mungu tutaona aibu. Watu wengi hujaribu kujitolea juhudi zao kwa Mungu kwa majivuno ya matendo yao na haki zao binafsi lakini haki hizo binafsi ni sawa na nguo chafu. Wanaweza wakawa na kitu cha kujisifu baina yao au kwao binafsi lakini si mbele ya Mungu.
Bwana ni Mwokozi kamili kwetu. “Yesu maana yaki ni Mwokozi” na pia ameitwa ni Kristo, Maana yake ni kwamba Mwokozi aliyekuja kwa mfano wa mtu ndiye Mungu. Tunamwita “Yesu Kristo.” Yesu ndiye mwokozi wetu na ni Mungu. Tunampa shukrani Bwana tukimsifu yeye, tukizifanya kazi za haki mbele yake na kuwa na maisha ya uaminifu kwa kuwa Mungu alituokoa kikamilifu. Ni wale tu wenye kumwamini Mungu ndiyo watakao weza kutenda kazi za haki.
Tunaweza kufanya kazi kwa haki pasipo na dhambi kwa kuwa Bwana amekwisha kuzibeba dhambi zetu zote. Hatutoweza kusuluhisha tatizo la dhambi binafsi. Mwanadamu hawezi kufuta dhambi zake au hata kufuata haki ya Mungu kwa kutenda mambo mema kwa mwili.
Mungu alizifuta dhambi zote na tunapokea haki toka kwa Mungu. Sisi ni wenye haki. Je, tunaweza kubaki na haki zetu kwa njia ya kujitakasa miili yetu kwa matendo ya uadilifu kwa upande wetu? Ikiwa yupo ambaye angeweza kufanya hivyo basi angelikuwani kaka au dada mkuu kwa Yesu. Yesu asingeliweza tena kuwa Mwokozi kwa mtu huyo. Tunakasumba yakufuata haki zetu kwa uwezo wa miili yetu na hisia zetu pasio kuelewa hili. Mwili hufuata kasumba. Tuna kasumba ya kukwepa hatari pale tunapo kumbana nayo, kupenda kula sana pale tunapo ona chakula kitamu na kutaka kucheza pale tunapo ona jambo la kufurahisha.
Tunakasumba ya kufuata sheria ya Mungu kwa miili kwa sababu miili hufuata kasumba. Hata hivyo kuokolewa kwetu si kwa njia ya haki zetu binafsi. Hatuto weza kuokolewa kwa kufuata sheria za Mungu (torati) kwa nafsi zetu. Juhudi zetu hazijumuishwi katika haki ya Mungu, hata kwa 0.1%. Tumefanywa wenye haki kwa kuamini kwamba Mungu alikuja ulimwenguni kwa mfano wa mwanadamu na kupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji kabla ya kusulubiwa ili kuikamilisha haki yote, ambayo kwa uhakika na kwa ukamili ndiyo iliyo tuokoa kutokana na dhambi zetu.
 

Bwana aliye tuokoa hakika ndiye Mwokozi.
 
Bwana aliitimiza haki yote kwa kuzichukua dhambi zote za wanadamu wazitendazo kabla ya kufa, kwa kuwa hakika yeye ndiye Mwokozi kwao na hatimaye kuwafanya kuwa wenye haki. Mungu ametufanya kuwa kamili kwa kutimiza haki yote. Mungu andiye atuwezeshaye kiroho kutende kazi. Tuna hadhi ya kufanya kazi za kiroho mbele ya Mungu kwa kuwa tumekwisha pokea haki yake tukiwa watu wasio na dhambi, ingawa miili yetu huendelea kufanya ya kimwili. Hata hivyo, wale ambao bado dhambi zao hazija futwa hawatoweza kuenenda kiroho. Hawana hadhi.
Tumepewa hadhi ya kufanya kazi za kiroho na Mungu. Sasa tunaweza kufanya mambo ya kiroho. Tunaweza kutenda kazi ya haki ya Mungu ukiachilia mambo ya kimwili. Ni kwa namna gani ilivyo vyema, Mungu kuwa Mwokozi wetu! Mungu aliye umba vitu vyote, wakiwemo wanadamu, amedhihirishwa kwetu kama Bwana wa wokovu kwa sababu alikuja duniani na kuitimiza haki yote. Kwa uhusiano nasi, Mungu akawa Bwana na Mwokozi aliye tuokoa.
Wakovu hautokamilika ikiwa mtu aliye dhaifu na asiye na uwezo atakuokoa. Kutakuwa na uwezekano wa kushindwa wakati mwingine. Kinyume cha huyu wa jinsi hii, aliye tuokoa sisi. Yeye ndiye Mungu na Muumba aliye umba vitu vyote. Yohana 1:3 inatamka “Vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.” Yesu ni nani? Yeye ndiye Mwokozi. Mwokozi ni nani? Ndiye Mungu Muumba. Mungu alituokoa vyema. Wokovu wetu ni kamili kwa sababu yeye ndiye aliye tuokoa. Ni wa milele. Hata hivyo ungeweza kubatilika ikiwa kama yeye asingelikuwa ni Muumba, au kuwa ni mtu kati ya viumbe. Usinge kuwa ni wamilele na haki yake ingekuwa kama matambara mabovu, ikwa mtu atavaa nguo zilizo safi na ngumu, hazitoweza kuchakaa kwa urahisi kamwe, hata ikiwa atacheza soka au kujigaragaza. Lakini ikiwa nguo hizo si madhubuti, mara moja zitachakaa.
Bwana aliye tuokoa toka dhambini yeye si dhaifu. Bwana aliyetuokoa ndiye Mungu aliye mkamilifu. Wokovu wa Yesu aliyebatizwa ili kubeba dhambi zetu zote, akasulubiwa akafufuka toka kifoni na ameketi kuume kwa Mungu Baba kamwe hautobatilika, ingawa miili ya wanaoamini ni dhaifu. Huu ndio wokovu Mungu alio tupatia.
 

Haki zetu binafsi ni lazima zivunjike ili tuweze kuenenda kwa Imani.
 
Katika Biblia wale walio jawa na haki zao walipitia magumu mengi kwa sababu Mungu aliwahitaji kuzivunja haki zao kwanza kwa kupitia taabu. Vipo vifungu vingi mfano “hata hivyo mahala pa juu hapakutwaliwa” katika matukio ya wafalme. Maana yake ni kwamba mwanadamu kwa kuwa yeye si mkamilifu lakini alifanywa kuwa mwenye haki kwa kumwamini Bwana.
Wapendwa watakatifu, Mungu wetu ndiye Mwokozi hakika na kweli, haijalishi vile tulivyo wadhifu kimwili, tatakufa ikiwa tutaishi kwa haki zetu tu. Lakini Bwana Mungu alituokoa ipasavyo kutokana na dhambi zetu. Atafurahi pamoja nasi ikiwa tutaishi kwa kuifuata haki ya Bwana ingawa tutakuwa wadhaifu. Isaya 53:5 inatamka “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu.” Mungu alichukua uovu wetu mara moja na kwa wakati wote. Hatuhitaji tena kuwa waoga kwamba haki aliyo tupatia itavunjika.
Baadhi ya watu wanahadhi zifananazo na vyombo vya vioo. Kuna dada fulani ninaye mfahamu aliye kwenda Marekani. Alikuwa ni waheshima akizungumza kwa uangalifu hukuwahi kamwe kuongea mambo machafu kila nilipo kutana naye. Alikuwa na mazoea yakusema “Oh! Huyu ndugu ni mwovu sana” kwa kumshutumu mtu dhaifu ingawa yeye binafsi alikua amepokea ondoleo la dhambi kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabini. Ingawa kwa upande mwingine alijawa na haki binafsi. Hata hivyo kwake yeye baada ya kupokea ondoleo la dhambi bado alikuwa akijitafutia na kujiwekea haki binafsi hata kuwa mwangalifu sana akijaribu kutojionyesha nafsi yake kwa kuogopa kwamba haki hiyo ingevunjika. Wapo wengi wa aina yake. Je, lakini haki hizi zao hudumu? Zitavunjika punde.
Je, mwili wako bado unaudhaifu ingawa umeokolewa? Ndiyo. Je, unaishi maisha yaliyo nyofu na kamili? Tunaweza kuishi maisha nyoofu yaliyo kamili baada tu ya ondoleo la dhambi ikiwa tutaenenda katika Roho. Kazi za wenye haki ndizo tu zenye kukidhi viwango vya juu mbele ya Mungu. Tunathamini ikiwa tuna tenda na kuenenda katika Roho. Hatuna tuwezacho kujivunia katika mwili. Baadhi ya watu kati ya watakatifu wenye ondoleo la dhambi hujaribu kutunza haki zao kwa hofu ya kuvunjika.
Hata hivyo, Bwana hapendezwi nao. Haki ya kibinadamu huvunjika. Ingelikuwa vyema zaidi ivunjike mapema. Lakini itaweza kuvunjika baada ya miaka 10 au 20. kwa hiyo utu wa nje utakuwa na unafuu zaidi pale utakapo vunjika mapema ili kwamba utu wa ndani uweze kuenenda kwa imani. Watu hujaribu kutuza haki zao ingawa zitavunjika bila shaka.
Bwana alikuwa Mwokozi wetu. Ni kwa namba gani alivyo kwetu! Bwana Mungu amekuwa Mwokozi wetu. Ametuokoa wewe na mimi. Je, unakuwa mwenye dhambi tena kwa sababu ya udhaifu wa mwili wako? Hapana Mungu aliitimiza haki yote. Haki yetu ilivunjika baada ya kuokoka. Uovu wetu sasa unajidhihirisha mara kwa mara kila tumfuatapo Bwana. Hujitokeza pamoja na kujaribu kujificha, hasa ubinafsi na kujitokeza pia mbele za watu wakati tunapo jihusisha na wengine. Haki zetu zinapo jidhihirisha, ni pale tu inapotaka kuvunjika huku ile haki ya Mungu husimama imara.
 

Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
 
Ningependa uamini kwamba Bwana Mungu ndiye Mwokozi wetu hakika. Hivyo kwamba yatupasa kuenenda kwa imani. Mungu anataka haki zetu binafsi ziweze kuvunjika na aweze kuridhika kwa hilo. Yohana 3:6 inatamka kwamba “kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” Mwili kamwe hautoweza kugeuka na kuwa roho. Katika dini ya Budha lipo “fundisho la kujikomboa toka uwepo wa kidunia.” Fundisho hili hutilia mkazo kwamba mwili waweza kugeuka na kuwa roho. Kamwe haitowezekana. Ni nani awezaye hili? Bila shaka hakuna!
Sung-chul, kasisi maarufu wa Korea katika dini ya Kibudha alifariki miaka iliyo pita kidogo. Alitafuta ukweli huku akitafakari kwa kina huku uso wake akiugeuzia ukuta kwa miongo 2. Hakulala kwa miongo kadhaa ili kuweza kupata ueleo wa Kiroho. Alilala akiwa amekaa kwa wakati mwingine kwa takribani miaka 10 na huku akijaribu kuwa na mawazo mema akishindana na mawazo ya uovu, uzinzi, tamaa mabaya, uuaji, wizi, udhaifu, majivuno na ujinga utakavyo ndani yake. Wengi walidhani kwamba yeye ndiye Mungu wa kibudha aliye hai. Hata hivyo, yeye binafsi alifahamu kwamba asingeweza kuzima tamaa za mwili wake hata, kidogo hivyo hatimaye aliacha nyuma kipande cha shairi kiitwacho “Nirvan” alipo karibia kufa baada ya kuitosa akili yake kwa miongo 2 akiishi katikati ya milima. Shairi hilo ni kama ifuatavyo:—
“Ama nimewalaghai watu wengi, wanaume na wanawake wakati wa uhai wangu, Dhambi zangu ni kubwa kuliko mlima ulio mrefu zaidi,Nitadondokea ndani ya Jehanamu isiyo na kina. Sononeko langu litagawanyika katika njia elfu kumi, Kipande cha jua chenye rangi nyekundu kinazama nyuma ya milima ya rangi ya samawati.”
Watu wote washika dini waliusifu utu wake na mafundisho yake yenye umadhubuti. Ingawa binafsi kwake alitamka ukweli kwamba angelikwenda jehanamu.
Kamwe mwili hautoweza kuwa roho, lakini nafsi zetu hugeuka na kuwa watoto wa Mungu pale tunapo zaliwa upya mara ya pili kwa kuamini wokovu wake. Tunakuwa viumbe wapya kwa rehema ya Mungu aliyetufufua katika haki yake. Wanadamu hawatoweza kufanywa upya kupita juhudi zao binafsi.
Wahudumu wa Kiroho, Makasisi na mapadre wa Kikatoliki, wote hawa hujihusisha na huduma za wafungwa wakiwashauri kuishi kwa uadilifu maisha yao yote. Hata hivyo, mwili kamwe haubadiliki. Mungu anatuhitaji kuachana na haki binafsi na kwa dhati tuamini kwamba Bwana ndiye Mwokozi. Amini ubatizo na Msalaba wa Yesu. Ndipo basi utaweza kuwa na imani kuu katika wokovu.
 

Sasa Mungu anatafuta wenye Kuamini.
 
Bwana alifanywa kuwa kipatanisho kwa ajili yetu. Yeye alibatizwa ili abebe dhambi zetu zote zenye kututenganisha na Mungu Baba. Alisulubiwa ili alipe mshahara wa dhambi zetu alihukumiwa badala yetu na kutuokoa toka dhambini. Mungu alikuwa upatanisho kwetu.
Anasema “Ambaye Mungu amekwisha kumweka upatanisho (kiticha rehema) kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, na kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa apate kuonyesha haki yake wakati huu ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu” (Warumi 3:25-26).
Mungu alikuja dunaiani na kutimiza haki yote. Kila mtu duniani hana tena dhambi. Hakuna aendye jehanamu kwa kuamini wokovu halisi na kweli wa Mungu. Mtu yeyote ataweza kwenda jehanamu kutokana na kutoamini kweke. Aweza kuokolewa ikiwa ataachana na haki binafsi na unafiki akimwamini Mungu kama Mwokozi kwa njia ya imani katika ubatizo wa Yesu na kifo cha msalabani. Tunaishi katika kipindi ambacho hakuna dhambi kwa mtazomo wa Mungu kwa kuwa yeye mwenyewe ndiye aliye zibeba dhambi hizo za dunia juu yake na hatimaye kuziondolea mbali kwa kifo cha msalabani kwa kumwaga damu.
Mimi na mwamini Mungu. Je, wewe nawe? Yeye ndiye Mwokozi. Hatuna tena dhambi. Bwana Mungu alituokoa kikamilifu. Tatizo pekee lililo baki kwetu ni namna ya kuishi maisha yaliyo salia. Tutaishije? Yatupasa kuenenda katika Roho. Hatuna sababu ya kuhofu juu ya kufuta dhambi zetu. Maneno yasemayo “Kuziachilia kufanywa” maana yake ni kwamba, Mungu hatuhukumu kwa sababu ya dhambi tena. Hatuna dhambi na hatuna la kuhukumiwa kwa sababu tayari Mungu alikwisha tuokoa toka dhambini kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji ili abebe dhambi hizo na hatimaye kusulubiwa. Hivyo basi Mungu hatuhukumu kwa dhambi zetu. Yeye huwatazama wale wote wanaoamini ukweli kwa mioyo yao yote.
Bibilia inasema kwamba hakuna mtu mwadilifu, lakini sisi tumefanywa wenye haki kwa imani katika Mungu. mungu anasema, “Hakuna mwadilifu, hapana, hapana; Hakuna anayeelewa; Hakuna mtu anayemtafuta Mungu. Wote wamepotea; Wote kwa pamoja wamekuwa wasio na faida; Hakuna anayefanya mema, hapana, hapana. koo zao ni kaburi wazi; Kwa lugha zao wamefanya udanganyifu; Sumu ya mianzi iko chini ya midomo yao; Ambaye mdomo wake umejaa laana na uchungu. Miguu yao ni wepesi kumwaga damu; Uharibifu na shida ziko katika njia zao; Na njia ya amani hawaijui. hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yao” (Warumi 3:10-18).
Mungu alikuja duniani na kubeba dhambi zote za wale watendao kila aina ya uovu wakiwa duniani, wasio na haki wala faida, katika mto Yordani. Je, unaamini hili?
Kwa sasa, Mungu anawatafuta wale wenye kuamini kwamba aliwaokoa toka dhambini. Jicho la Bwana lipo juu ya wale wote wenye haki. Yeye hutupa moyo sisi wenye haki. Anatuchunga, yuko nasi wakati wote akitutazama na kufanya kazi nasi. Yeye ndiye aliye tupa dhamana ya kazi yake ya haki. Yesu atasikitika zaidi ya vile tusikitikavyo kutokana na uovu utokanao na miili yetu Husema “Kwa nini unasikitika kwa dhambi zako huku tayari nimekwisha kukuokoa kwa dhambi zote?” 
Kile tuwezachoweza kukifanya ni kumwamini Mungu tukitembea katika Roho na kuihubiri Injili kwania ya kuzivuna nafsi zilizo potea. Haya ndiyo mambo ambayo yatupasayo kutenda kwa sasa. Je, unaamini hili? Usijionyeshe vile ulivyo mwenye haki binafsi au kujaribu kuimarisha na kuiweka haki binafsi kwa kujilinganisha na wengine kwa kujionyesha. Kamwe usiwadharau wale wasio na haki kwa nafsi zao ukweli ni kwamba hakuna mwenye haki binafsi kwa asili yake.
 

Tunampa Bwana shukrani aliyetuokoa kupitia ubatizo wake na msalaba.
 
Hakika hakuna la kujisifu mbele ya Mungu zaidi ya ule upendo wake alio tuokoa nao. Kile tuwezacho kukifanya ni kujisifia wokovu wa Mungu tukiuimbia shangwe, kumtukuza na kuihubiri Injili ya maji na Roho. Hatuhitaji kuwa na hofu juu ya dhambi na kwenda jehanau tena “Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (Warumi 8:1) kamwe. Je, unaona hilo? Mtu anakwenda jehanamu ikiwa haungani na ukweli usemao, Bwana alituokoa kwa tendo lake la haki. Hata hivyo mtu haitaji kuwa na hofu ya kutupwa motoni ikiwa anaamini hili.
Bwana Mungu alituokoa kwa dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo na damu ya Yesu. Kwa jinsi gani tumshukuru! “Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam ni Mungu wa Mataifa pia” (Warumi 3:28-29).
Mungu si Mungu wa Wayahudi bali pia ni Mungu wa Mataifa. Ni Mungu wa wanadamu wote Bwana Mungu alituokoa kutokana na dhambi zetu. Ili kufanya hivyo alikuja ulimwenguni akabatizwa ili kubeba dhambi zetu zote, na kusulubiwa ili kupokea hukumu ya dhambi zote. Hili ndilo hitimisho la Warumi sura ya 3. Mtume Paulo aliamini hili. Nasi pia tunaamini hivyo.
Mtume Paulo hazungumzia juu ya udhaifu wa kimwili tu bali pia haki ya Mungu pasipo sheria. Hatutoweza kuokolewa kwa matendo ya sheria. Sasa basi tunaweza kukombolewe kwa njia gani? Kwa imana ya wokovu na Mungu. Lakini Bwana Mungu alikuwa ni upatanisho kwa ajili yetu na kujitwika dhambi zote zilizo kwisha kutendwa. Kwa hiyo, wasioamini watahukumiwa kwa dhambi ya kumpinga (kumkufuru) Roho Mtakatifu. Yeye haukumu dhambi ambazo zilizo kwisha kutendwa kwa udhaifu wa mwili kwa kuwa hakuna tena dhambi duniani.
Kwa hiyo yatupasa kumwamini Bwana Mungu. Hakuna hukumu au adhabu kwa wanao amini Mungu. Wanao amini hivyo yatubidi kutumia muda wetu ulio salia katika maisha yetu kwa kuenenda katika Roho. Wakati wote tunaweza kutenda mambo ya kiroho kwa sababu dhambi zetu zote zilikwisha samehewa tayari, ingawa miili yetu inaendelea kutamani kuishi kwa tamaa. Bwana Mungu ni Mungu wa wote, Wayahudi na Mataifa. Yeye pia ni Mungu wa wote wanao amini na wasio amini. Hii maana yake kwamba, Mungu anataka wanadamu wote waokolewe toka dhambini mwao. Yeye aweza kuwa Mwokozi wa wasio mwamini. Tayari amekweisha kuwa Mungu wa wanao mwamini.
Namshukuru Bwana Mungu kwa kina cha moyo wangu. Ninge angamia kwa kiasi gani kama Bwana Mungu asingelikuwepo, kama asingelikuja duniani kwa mfano wa mwanadamu, na kama asingelibatizwa mto Yordani kubeba dhambi zetu zote. Kama asingelikuwa Mwokozi wa kweli, tungelikuwa wenye dhambi tena baada ya kupokea ondoleo la dhambi kwa sababu sisi tu dhaifu hadi siku ya mwisho kifoni. Namshukuru Bwana Mungu.