Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 3-2] Wokovu toka dhambini ni kwa njia ya imani tu! (Warumi 3:1-31)

(Warumi 3:1-31)
“Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiri kwa faa nini? Kwa faa sana kwa kila njia kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. Ni nini, basi ikiwa baadhi yao hawakuamini? Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo kama ilivyo andikwa, Ili ijulikane kuwa una haki katika maneno yake, ukashinde uingiapo katika hukumu lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je, Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu) Hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu? Lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali na hukumiwa kuwa ni mwenye dhambi? Kwa nini tusiseme (kama tulivyosingiziwa na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema, hivyo) Natufanye mabaya ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki.
Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo kwa maana tumekwisha kushitaki Wayahudi wa Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi kama ilivyo andikwa ya kwamba hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye, hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia. Hakuna mtenda mema, la! hata mmoja koo lao ni kaburi wazi. Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao inambio kumwaga damu. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. Wala njia ya amani hawakuijua. Kumcha Mungu hakupo machoni pao. Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanema kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu kwa sababu hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria, kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria, inashuhudia na torati na manabii, ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wana hesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho (kiti cha rehema) kwa njia ya imani katika damu yake ili aonyeshe haki yake kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa, apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu.
Ku wapi basi kujisifu? Kumefungiwa njee. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani. Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia; kama kwa kweli Mungu ni moja atakaye hesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo. Basi je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.”
 

Kutoamini kwa watu hakutobadilisha uaminifu wa Mungu
 
Mtume Paulo anasema kwamba kukamilishwa kwa sheria na ukombozi wa rehema ya Mungu havikuletwa kwetu kwa njia ya matendo yetu bali kwa imani. Tuliokolewa toka dhambini mwetu na hatimaye kuwa wenye haki kwa kupitia wokovu wa Mungu. “Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwa faa nini? Kwa faa sana kwa kila njia, kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausi ya Mungu. Ni nini basi ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo” (Warumi 3:1-4).
Wayahudi wamepata upendeleo kwa kuwa neno la Mungu lilikabidhiwa kwao. Waliishi huku wakisikiliza neno lake toka kwa mababu zao. Kwa sababu Mungu aliwakabidhi neno lake na kwa kupitia kwao walidhani basi wao walikuwa ni zaidi ya watu wa mataifa. Hata hivyo, biblia inasema kwamba Mungu aliwatelekeza Wayahudi kwasababu hawakumwamini Yesu aliye wakomboa kwa dhambi zao.
Paulo anasema “Ni nini, basi ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je, kutoamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha!” Kutoamini kwa watu hakutoweza kubadilisha wokovu wa Mungu. Na wokovu toka dhambini hautoweza kubadilika hata ikiwa Wayahudi hawaamini. Neno la ahadi ya Mungu ya kwamba, amekwisha tuokoa kwa kila anaye amini halitobatilika au kufutika hata ikiwa hawaliamini.
Watu wa Mataifa wataamini hata ikiwa Wayahudi hawaamini. Mungu anasema yeyote anayeamini ataokolewa toka dhambini. Kwa maana hiyo Mungu aliwatelekeza Wayahudi kwa sababu hawakuamini kwamba neno la kweli lilikamilishwa kulingana na ahadi ya Mungu ingawa yeye mwenyewe aliwakabidhi neno hili hapo awali.
Uthibitisho wa Mtume Paulo ni kama ifuatavyo:- Mungu alileta zawadi ya wokovu kwa wanadamu wote. Mungu anasema aliiahidi zawadi hii nyakati za Agano la Kale na kukamilisha ahadi hii kwa kumtuma Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee, kuja duniani. Baadhi ya watu wanaiamini Injili ya Mungu lakini wengine hawaiamini. Hivyo basi, yeyote anaye iamini amebarikiwa kuwa mwana wa Mungu kwa jinsi ili alivyo ahidi. Na baraka ya Mungu haibatilishwi hata ikiwa ni watu wangapi hawaiamini.
 

Yeyote anaye amini ukweli ataweza kupokea upendo wake mkuu.
 
Yeyote anaye sikiliza neno la kweli na kuliamini ataweza kupokea upendo mkuu wa Mungu, lakini wale wasio amini wamemfanya Mungu mwongo. Ukweli ni kwamba Mungu ameikamilisha ahadi yake lakini wasio iamini wametengwa na wokovu wa Mungu kwa kuwa hawaamini rehema ya ondoleo la dhambi.
Paulo anasema “Je, kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha!” Mungu aliahidi hapo mwanzo na kutimiza kwa uaminifu ahadi ya wokovu na utukufu kwa watu wote.
Biblia inasemaje juu ya zawadi ya Mungu? Biblia inasema kwamba Mungu Baba alimtuma mwana wake wa pekee na kuleta rehema ya kuwafanya kuwa watoto wake wale wote wanye kuamini ondoleo la dhambi kwa njia ya mwanae. Hata kabla ya misingi ya dunia alikwisha kupanga kwamba atawapatia wanadamu wote utukufu wa kuwa watoto kwake na wokovu toka dhambini kwa njia ya haki yake. Na alitimiza hili kwa uaminifu mkuu.
Kwa hiyo wenye kuamini wamebarikiwa kwa kulingana na neno la Mungu, lakini wale wasio amini watahukumiwa kwa sababu ya hilo. Asiye amini anastahili kwenda jehanamu. Mungu aliweka sheria ili kwamba tuweze kuokolewa kwa imani ya Neno lake. Pia anasema kwamba uaminifu wa Mungu kamwe hautobatilika hata ikiwa watu hawato amini. Tumebarikiwa kwa kukubali uaminifu wa wokovu wa Mungu. Mungu anasema “Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo, kama ilivyo andikwa ili ijulikane kuwa una haki katika maneno yako, ikashinde uingiapo katika hukumu” (Warumi 3:4).
Kila mtu ni mwongo. Mungu ni amini. Kwa nini? Kwa sababu Mungu anasema “kama ilivyo andikwa ili ijulikane kuwa una haki katika maneno yako, akashinde uingiapo katika hukumu.” Mungu anasema kwamba anatoa ahadi mapema kabla na kuwabariki wale wote ambao watabarikiwa na kulaani wale wote watakao laaniwa. Ni haki ya sheria ya Mungu kuwabariki wanaoamini na kuwalaani wasio amini. Mungu anasema “Mungu aonekanie kuwa amini na kila mtu mwongo.”
“Ijulikane kuwa una haki katika maneno yake, ukashinde uingiapo katika hukumu.” Mungu anasema kwamba ataokoa watu kulingana na neno lake. Neno lili fanyika kuwa mwili, kuishi kati yetu na kutuokoa. Hivyo Bwana anahukumu kwa neno lake.
Bwana alimshinda shetani kwa maandiko ya neno la Mungu. Bwana ni wa haki na mkweli kwa nafsi yake na mbele ya shetani na wote walio viumbe wa kiroho kwa sababu alikamilisha kile alicho ahidi. Hata hivyo, wanadamu si waaminifu. Tabia zao hubadilika punde wanapo kuwa katika hali ya kuathirika. Kinyume na hili Mungu hajawahi kwamwe kuvunja ahadi. Hivyo Mtume Paulo anasema kwamba imani zetu yapaswa kuwa katika msingi wa neno la Mungu.
 

Udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu
 
Warumi 3:5 inatamka kwamba “Lakini ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu tuseme nini? Je, Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu).” Wanadamu wote ni dhalimu lakini tusemeje ikiwa udhalimu wao waithibitisha haki ya Mungu katika wokovu? Tutasemaje ikiwa dhambi zetu zinathibisha haki ya Mungu? 
Haki ya Mungu inathibitishwa zaidi kwasababu ya dhambi zetu na udhalimu wetu. Mungu ni mkweli hakika. Yeye ni Bwana wa wokovu, Mwokozi na Mungu wa kweli anaye ahidi kutuokoa sisi kwa neno lake na kutimiza kile alicho agana. Tusemeje basi ikiwa haki ya Mungu imethibitishwa kwa sababu ya udhalimu wetu? Udhaifu wetu ume dhihirishwa kwa haki ya Mungu zaidi kwa sababu tutaendelea kutenda dhambi hata mwisho wa kifo chetu.
Tunajua kwamba Mungu ni Bwana wa upendo? Twaweza kujua hili kutokana na udhaifu wetu. Upendo wa Mungu unadhihirishwa kwetu kwa sababu tunatenda dhambi na kuendelea hata siku ya mwisho wa uhai. Bwana anasema kwamba amefuta dhambi za dunia mara moja na kwa wakati wote. Upendo wa Mungu usengelikamilika ikiwa kama angewapenda watu wema tu wasio tenda dhambi. Ni kutokana na upendo wake wa kweli ndiko kumemsukuma kuhusika na sisi wenye dhambi ambao kamwe tusingeliweza kukubaliwa.
Sisi wanadamu ni dhalimu na tumemuasi Mungu. Hatumwamini na hatuna sehemu ya kupendeza mbele yake. Wenye dhambi ni wale watendao uovu tu, lakini Yesu aliyetuokoa toka dhambini na katika makosa yote tayari alikwisha timiza upendo wa Mungu kwetu.
Mungu anasema kwamba ilikuwa kwa njia ya haki yake na upendo ndipo alipo mtuma mwana wake wa pekee kutuokoa toka kiza cha shetani na laana pale wanadamu walipo tenda dhambi na kuhukumiwa hatima ya jehanamu kwa sababu ya ulaghai wa shetani. Ni upendo na rehema ya Mungu.
“Lakini ikiwa udhalimu wetu unaonyesha haki ya Mungu, tutasema nini?” anasema Mtume Paulo. Mawazo ya waumini na yale ya wasioamini yamegawanywa katika kifungu hiki. Waumini wasioamini hujaribu kuwa wazuri ili kuingia katika Ufalme wa Mbingu na kubarikiwe na Mungu. lakini Paulo anatoa maoni tofauti, akisema, “Lakini ikiwa udhalimu wetu unaonyesha haki ya Mungu, tutasema nini?” Paulo anasema kwamba sisi wanadamu hatuwezi kufanya uadilifu wa Mungu lakini tu kutenda dhambi mbele zake, na kwamba uovu wetu unakuja kuonyesha upendo wa kweli wa Mungu. Ndio ni kweli. wanadamu wote ni waovu na hawawezi kuwa waadilifu, lakini Bwana aliwaokoa kutoka kwa dhambi zao zote.
 

Tumeokolewa kwa haki ya Mungu.
 
Mtume Paulo anasema kwamba wandamu hawatoweza kuwa wenye haki na hivyo wamenaswa katika mtego wa dhambi. Bwana amewaokoa wenye dhambi hawa toka dhambini mwao na hivyo, kuwapenda. Tunahitaji pendo lake kamili kwa sababu hatutoweza kujizuia kutenda dhambi kila siku. Tuliokolewa kwa kujizuia kutenda dhambi kila siku. Tuliokolewa kwa upendo halisi wa Yesu, rehema ya bure, na zawadi ya wokovu kwa njia ya Yesu Kristo.
Mtume Paulo anasema, yeye ameokolewa kutokana na haki ya Mungu. Kile Mungu alicho fanya ili kuokoa wenye dhambi kutokana na dhambi zao ndicho kionyeshacho juu ya haki yake. Haki ya Mungu inadhihirishwa katika Injili ya maji na Roho. Wokovu wetu unataegemea haki ya Mungu aliyoitekeleza kwa ajili yetu. Hivyo basi wenye dhambi waliokolewa toka dhambini kwa imani zao. Wale ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili hudhani kwamba imewapasa kuwa wema ili kwamba waweze hatimaye kuingia Ufalme wa Mbinguni.
Paulo hakumaanisha kwamba twaweza basi kutenda maovu kwa makusudi lakini bado watu huishia kwenda jehanamu kwa kujaribu kutenda matendo mema ya kiuadilifu pasipo kuipokea ile haki ya Mungu. Imewapasa kutubu kwa kugeuka na kuamini wokovu Mungu alio wapa ili kukwepa kuingia motoni.
Ni nani awezaye kutenda mema mbele za Mungu? Hakuna yeyote. Sasa basi inawezekanaje mwenye haki kuokolewa kwa dhambi zake zote? Imempasa kubadilika kifikra. Mtume Paulo anasema kwamba, yeye binafsi aliokolewa kwa imani. Lakini watu hudhani nini? Watu hudhani kwamba wataweza kuokolewa kwa kutenda mambo mema. Ndiyo maana kamwe hawato kombolewa.Wale ambao wameokolewa toka dhambini kwa kumwamini Yesu na kuwa na ondoleo kamili la dhambi zao, hujisifu kwa haki ya Mungu tu nakuishangilia.
Hata hivyo, wale ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili, ingawa wana mwamini Yesu. Hudhani kwamba wataweza kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa kutenda mema, na kinyume cha hilo watakwenda jehanamu ikiwa imani zao si sahihi. Imani ya Mutume Paulo inafanana na ile ya wale walio zaliwa upya. Wale wasio zaliwa upya mara ya pili ingawa wao hudhani wanamwamini Yesu, wana imani isiyo sahihi kwa sababu hujaribu kujumuisha matendo yao katika imani zao. Hatujaokolewa kwa kuongezea matendo ya uadilifu katika imani zetu bali kwa kuamini haki ya Mungu; ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani.
 

Wenye haki hawawezi kutenda dhambi kwa makusudi.
 
“Lakini ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu tusemeje.” Biblia inasema kwamba udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu pekee na upendo wake. Pia inasema “Lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu mbona mimi ningali na hukumiwa kuwa ni mwenye dhambi? Kwa nini tusiseme (kama tulivyosingiziwa na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo) Na tufanye mabaya ili yaje mema, ambao kuhukumiwa kwao kuna haki” (Warumi 3:7-8). Majina ya wale wote wasio amini yameandikwa katika kitabu cha Hukumu na watatupwa jehanamu katika ziwa la moto. Kwa hivyo imewapasa kutubu ili wageuke na kuamini wokovu uliokamilishwa kwa maji na damu.
Mtume Paulo anasema “Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu.” (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu) Watu hukosea pale wanapo sema “Je, Mungu si haki kwake kuleta ghadhabu kwa wasio amini na kuwatupa jehanamu kwa kuwa tu hawamwamini Yesu kuwa amekwisha waokoa kwa dhambi zao?” Lakini Paulo anasema “Je, Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu?” Kwa wasio amini imewastahili kwenda jehanamu kwa kuwa hawaiamini ile kweli. “Mungu si dhalimu”.
Warumi 3:7 “Lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu mbona mimi ningali na hukumiwa kuwa ni mwenye dhambi?” Ndipo watu husema “Je, tutende dhambi kwa makusudi kwa sababu tayari tunaondoleo la dhambi? Tudanganye zaidi kwa kuwa tumekwisha okolewa kwa haki ya Mungu. Je tutenda dhambi zaidi kwa makusudi?” “Je, tutenda dhambi zaidi kwa makusudi?” Lakini biblia inasema kwamba walitenda hayo yote kwasababu ya mioyo miovu, huku wasijue wokovu wa Mungu wala kuamini upendo wake.
Hivyo basi, Paulo anasema kwamba ukweli wa Mungu umejawa na utukufu wake, ukizidi udhalimu na ulaghi wetu. Lakini watu hupingana na Paulo kwa fikra zao wakisema, “Waweza kutenda dhambi zaidi ikiwa utaamini kwamba umekwisha okolewa kwa imani pasipo matendo”. Si kweli kwamba watu hutenda dhambi kwa kupenda tu. Hawawezi kujizuia kutenda dhambi kwa sababu walizaliwa wakiwa ni wenye dhambi. Ni asili kwa mti wa mtufaa kuzaa tunda la mtufaa. Biblia inasema kwamba pia ni asili kwa mwanadamu aliye zaliwa akiwa na asili ya dhambi kuendelea kutenda dhambi. Bwana alituokoa sisi wenye dhambi kwa haki yake; na twaweza kukombolewa kwa kukubali wokovu wa Bwana tu.
“Kwa nini tusisemae (kama tulivyosingiziwa na kama wengine wanavyo kaza kusema ya kwamba twasema hivyo) Natufanye mabaya ili yaje mema? Ambao kuhumiwa kwao kuna haki.” (Warumi 3:8) Wale wote walio katika udanganyifu wa walimu waongo huku wakidhani wanamwaminiYesu, hufikiri kwa jinsi hii. Waraka wa Warumi uliandikwa na Mtume Paulo takribani miaka 2,000 iliyo pita. Watu wengi, katika nyakati hizo walifikiri namna hii, kama ilivyo hata kwa wasio amini katika wakati huu. Waumini waongo hufikiri kwa namna ile ya wasio amini. Wakati ule Paulo alisema, Je, tutatenda dhambi kwa makusudi ikiwa unaondoleo la dhambi, na unafahamu kwamba pia dhambi zako zijazo zilikwisha samehewa?
Wasio amini hutenda kulingaa na fikra zisizo za kiimani. Hawatoweza kuingia katika wokovu wa kweli wa Mungu kwa sababu ya fikra zao potofu za kimwili. Bila shaka hata wenye haki bado hutenda dhambi baada ya kupokea ondoleo la dhambi lakini kuna kikomo. Biblia inasema kwamba wenye dhambi huendelea kutenda dhambi kwa sababu hawafahamu kwamba wanatenda dhambi na pia hawaelewi nini maana ya kuwa mtenda dhambi na kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho. Hata hivyo, Biblia inasema kwamba wenye haki hawatoweza kutenda dhambi bila kujali kwa sababu wapo chini ya uongozi wa Mungu.
Baadhi ya watu walimweleza Mtume Paulo, “Je, hautendi mambo ya uovu ili kwamba mema yaje kwa sababu tu Mungu alikwisha kukuokoa tokana na dhambi zako zote? Ingekuwa ni vyema zaidi ukitenda mambo maovu mengi ili basi haki ya Mungu iweze kudhihirika zaidi.” Paulo anasema kwamba watu hawa hatima yao ni hukumu. Anamaanisha kwamba ni haki yao kuhukumiwa na hatimaye kutupwa jehanamu. Kwa nini? Kwa sababu hawategemei imani, bali matendo yao.
 

Haki ya Mungu kamwe haitobadilika.
 
Mtume Paulo anasema “Ni nini basi ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je, kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?” Je, kutokuamini kwao kutaubadili wokovu wa Mungu? Watu wanokolewa ikiwa wataamini, lakini wanapoteza rehema ya ondoleo la dhambi ikiwa hawatoamini. Haki ya Mungu husimama imara. Je,unaelewa hili? Wale waendao jehanamu wamejitolea kwenda huko kwa sababu wanachagua kutoamini. Kazi ya Mungu na rehema ya wokovu toka dhambini haibadiliki. Husimama imara.
Wokovu wa Bwana hauna uhusiano na juhudi zozote za kibinadamu zitokanazo na msingi wa matendo ya sheria bali unauhusiano na wanao amini tu. Wenye kuamini huokolewa kwa kupitia ukweli wa Mungu lakini kwa wale wote wasio amini wata kwenda motoni kwa sababu hawajaokolewa kutokana na kuukana ukweli wa Mungu. Mungu ameweka “jiwe la kujikwaa na mwamba wa kuangusha” (Isaya 8:14) Yeyote anaye mwamini Yesu hufanywa kuwa mwenye haki na kupata uzima wa milele, ingawa aweza kuwa dhaifu kimwili. Asiye mwamini Yesu atakwenda jehanamu kwa sababu ya mshahara wa dhambi, ingawa aweza kuwa ni mwema. Yesu ni jiwe la kujikwaa na mwamba wa kuangusha kwao wote wasio amini msamaha wa dhambi.
 

Hakuna mwenye haki asiye tenda dhambi.
 
Mtume Paulo anazungumzia juu ya imani ya wokovu kwao wale wajifanyao kuwa wema, hivyo watu huchukulia Warumi kama ni neno la Mungu lenye kuelezea juu ya imani. Baadhi ya watu huwashangaa wale wenye kujitambulisha kama wo ni wenye haki. Ukweli ni kwamba, wale ambao dhambi zao zimekwisha samehewa na Yesu ni wenye haki kwa sababu dhambi zao zote zilisamehewa. “Yesu ni mwaminifu” maana yake “Kwa uaminifu aliokoa wenye dhambi.” Baadhi husema kwamba wao ni “wenye dhambi walio kombolewa”, lakini hakuna watu wa aina hii mbele za Mungu. Mtu atawezaje kuwa mwenye dhambi baada ya kukombolewa dhambini? Tumeokolewa ikiwa Yesu alituokoa na niwenye dhambi ikiwa Yesu hakutuokoa. Hakuna mizani ya kati katika wokovu.
Je, yupo mwenye haki ambaye anadhambi? Hakuna mwenye haki aliye na dhambi. Mtu ni mwenye dhambi ikiwa anadhambi, lakini ni mwenye haki na asiye na dhambi ikiwa anamwamini Yesu. Tutawezaje kusuluhisha tatizo la dhambi la kila siku na zile za mbeleni? Watu hudhani kwamba wao ni wenye dhambi kwa kuwa hutenda dhambi kila siku na wataendelea kutenda dhambi hadi mwisho wa maisha yao. Hata hivyo, tumefanywa kuwa wenye haki kwa kuamini Injili isemayo Yesu alibeba dhambi za dunia zikiwemo hata zile za mbeleni katika mto Yordani nakusulubiwa.
“Mtu mwenye haki aliye na dhambi”, hii haiingii akilini! Je, ipo sababu kweli ya kufikiri kwamba mtu aweza kuendelea kuwa na deni ingawa tayari amekwisha lipa deni hilo. Kwa mfano, mtu fulani aliwahi kuwa na fedha nyingi. Mtoto wake akaangukia kuwa na tabia mbaya ya kununua vitu vitamu vya kutafunwa kwa mikopo katika kila duka sehemu aliyokuwa akiishi, kila siku. Hata hivyo baba yake aliyetajiri akalipa fedha kiwango zaidi ya deni lake maishani pote katika kila duka kwa ziada na hakuweza kuwa mdaiwa ingawa aliendelea kula vitu hivyo pasipo kulipa fedha hadi mwisho wa maisha yake.
Bwana alituokoa kwa haki pale alipochukua dhambi zetu juu yake mara moja na zote katika Mto Yordani. Alituokoa kwa ukamilifu. Hivyo, kwamwe hatutoweza kuwa wenye dhambi tena, ingawa tu dhaifu. Mungu anasema kwamba tumefanywa kuwa wenye haki ikiwa anasema kwamba tumefanywa kuwa wenye haki ikiwa hatutoweza kukana kile alicho weza kukifanya.
 

Kamwe watu hawawezai kuiamini Injili au hata kuzaliwa upa mara ya pili kwa njia ya fikra za kimwili.
 
Wakristo wenye kujitambulisha kuwa wao ni “wenye dhambi walio kombolewa” huwa na fikra za kimwili. Kuwa na fikra za kiroho ni kuamini maneno ya Mungu. Akili ya kimwili ni akili ya kibinadamu. Ni hekima ya kibinadamu. Mwili hauwezi kuacha kutenda dhambi lakini twaweza kuwa wenye haki kwa kuamini ubatizo na msalaba wa Yesu. Biblia inasema kwamba kamwe hatutoweza kuwa wenye haki na kutakaswa kwa kujaribu kuacha kutenda dhambi.
Je, mtu aweza kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa kuwa mtu mtakatifu asiye tenda dhambi kamwe baada ya kumwamini Yesu? Au je, inaweazekana kwa wokovu wa mara moja na kwa wakati wote? Je, wenye dhambi wanafanywa kuwa wenye haki kwa rehema ya ondoleo la dhambi? Haiwezekani kwako kuwa mwenye haki kwa akili ya kimwili. Mwili kamwe hautoweza kuwa wenye haki. Mwili wakati wote hutaka na kutamini kula kitu fulani kila unaposikia njaa.
Haito wezekana kwa mwili kutakasika kwa sababu mwili huo unatamaa na mahitaji binafsi. Kwa sababu ya hilo tunaweza kufanywa kuwa wenye haki kwa kuamini maji na damu ya Yesu tu. Je, tutaweza kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa kutotenda dhambi na kujitakasa hata kuwa safi kama theluji? Hiki ni kiburi na majigambo ya kibinadamu, ambao ni wenye tamaa na upenzi wa kimwili kuweza kutakaswa kwa kujizuia kutenda dhambi. Haiwezekani kamwe.
Watu hatoweza kuiamini Injili au hata kuzaliwa upya mara ya pili kwa sababu wao hufikiri juu ya imani kwa akili za kimwili. Yesu alisema “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa kwa Roho ni roho” (Yohana 3:6).
Haiwezekani kuwa mwenye haki kwa akili za kimwili. Waweza kudhani kwamba haiwezekani kwa sababu kesho utatenda dhambi, ingawa ni kwa kiasi gani unatubu mara kwa mara nakumwamini Yesu hadi leo. Unaweza kuwaza, “Nitasemaje kuwa sina dhambi hali ninaendelea kutenda dhambi kila leo?” Je, ni vigumu kwako kuwa mwenye haki ikiwa unafikra za kimwili, kama mwili ufanyavyo? Haiwezekani kuwa mwenye haki kwa utakaso wa mwili.
 

Hata hivyo Mungu ametufanya kuwa wenye haki.
 
Hata hivyo Mungu anaweza kutuokoa kwa ukamilifu ikiwa mwanadamu ameshindwa. Mungu aweza kututakasa dhamira zetu na hatimaye kutuwezesha kukiri kwamba sisi ni wenye haki na kwamba yeye ni Baba yetu na Mwokozi. Yakupasa ufahamu kwamba imani huanzia katika kulikubali na kuliamini neno la kweli kwa moyo wako. Linaanza na neno la kweli. Tumefanywa kuwa wenye haki katika neno la kweli mioyoni mwetu. Kamwe hatutoweza kuwa wenye haki kwa matendo ya sheria.
Hata hivyo, wale wote ambao hawajazaliwa upya mara ya pili hawatoweza kujiweka huru binafsi kutokana na mawazo au fikra zao. Kamwe hawatoweza kujiita wenye haki kwa sababu hudhani na kuwaza kimwili. Kinyume cha hili, imani ambayo twaweza kusema ni wenye haki huanza kwa kuijua kweli ya neno la Mungu. Ikiwa kweli unahitaji kuzaliwa upya mara ya pili, basi unaweza kwa hakika, na endapo tu kwa kusikia neno la kweli kupitia kwa yule aliye zaliwa upya mara ya pili, kwa kuwa Roho aliye ndani ya mtakatifu huyo inampandeza kuitenda kazi kwa ukweli na “huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu” (1 Wakorintho 2:10). Watu waweza kuzaliwa upya mara ya pili endapo watasikia neno la Mungu kupitia wenye haki kwa sababu Roho huweka makazi ndani ya watu hao wenye haki ambao ndiyo walio zaliwa upya kwa hakika. Napenda uelewe hilo zaidi. Yakupasa basi ukutane na mwenye haki ambaye amezaliwa upa mara ya pili ikiwa kweli unataka kupokea rehema ya kuzaliwa upya mara ya pili.
Abrahamu alimzaa Ishimaeli na Isaka. Ismaelie alizaliwa toka kwa kijakazi mtumwa. Ishimaeli alikuwa amefikisha umri wa miaka 14 wakati Isaka anazaliwa. Ishimaeli alimnyanyasa Isaka, aliyezaliwa toka kwa mke huru. Ni nani haswa aliye na haki ya urithi? Isaka aliye zaliwa toka kwa mke huru Sara, ndiye aliye kuwa na haki ya urithi.
Isaka alikuwa na haki ya urithi na alikubaliwa ingawa Ishimaeli alikuwa ni mkubwa na mwenye nguvu kimwili kuliko Isaka. Kwa nini? Isaka alizaliwa kwa neno la Mungu. Imani iliyo katika msingi wa fikra za kibinadamu ni sawa na nyumba ya udongo. Watu wanaweza kuzaliwa upya mara ya pili ikiwa tu watajifunza ukweli wa neno la Mungu na kuuamini. 
“Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? Hasha! Hata kidogo kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi kama ilivyo andikwa ya kwamba hakuna mwenye haki hata mmoja” (Warumi 3:9-10). Je, kifungu hiki kina maana gani? Je, kinaashiria hali ya wanadamu kabla ya kuzaliwa upya mara ya pili? Sisi sote tulikuwa wenye dhambi kabla ya kuzaliwa upya mara ya pili, “Hakuna mwenye haki.” Hii ndiyo hali ya wanadamu kabla ya Yesu kufuta dhambi zote za ulimwengu. Mtu kamwe hatoweza kutakaswa pasipo kumwamini Yesu.
Usemi wa “Utakaso wa hatua kwa hatua katika viwango” ulikuja kutoka waabuduo sanamu katika dini za kipagani. Biblia inasema “hakuna mwenye haki hata mmoja.” Je, inawezekanaje mtu kutakaswa kwa kujizoesha nafsi yake? Mwanadamu hawezi kuwa mwenye haki kupitia nafsi yake mwenyewe. Hakuna yeyote aliyewahi kuwa mwenye haki au kutokea kuwa mwenye haki kwa matakwa yake binafsi. Hii inawezekana ikiwa tu ni kwa imani ya neno la Mungu. Biblia inasema “hakuna afahamuye; hakuna amtafutaye Mungu” (Warumi 3:11).
 

Wote wamepotoka.
 
“Wote wamepotoka, wameoza wote pia” (Warumi 3:12). Je, mwanadamu anafaida yoyote mbele za Mungu? Mwanadamu hana faida mbele ya Mungu. Wale wote ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili hawana faida yoyote mbele ya Mungu. Je, hawaelekezi vidole vyao mbinguni huku wakigombana na kumlaani Mungu wakimshutumu kwa kuto leta mvua wakidhani kwamba wanamdai?
“Wote wamepotoka, wameoza wote pia” asema Mungu. Ni kwa namna gani mtu mwenye dhambi moyoni aweza kumtukuza Mungu? Kwa namna gani mwenye dhambi ambaye hawezi kusuluhisha tatizo lake la dhambi aweza kumsifu Mungu? Mwenye dhambi awezaje kumwimbia sifa Mungu? Mwenye dhambi kamwe hatoweza kumtukuza Mungu.
Huduma za kusifu kwa nyimbo zimeenea nyakati hizi sana. Watu wenye dhambi hutunga nyimbo za Injili huku wakinukuu Maandiko katika kitabu cha Ufunuo “Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketimye juu ya kiti cha enzi na yeye Mwana—Kondoo hata milele na milele”    (Ufunuo 5:13). Bwana ndiye anastahili kusifiwa bila shaka ni kwa wale wenye haki tu ndio wawezao kumsifu Mungu. Je, unadhani kwamba Mungu anakubali sifa za wenye dhambi kwa furaha? Sifa za wenye dhambi ni sawa na sadaka ya Kaini. Sifa zao ni bure waimbapo mbele ya anga tupu ingawa wao hudhani wanamsifu Bwana. Kwa nini? Kwa sababu Bwana hawafurahii. Mungu kamwe hawasililizi wenye dhambi na sala zao (Isaya 59:1-2).
Biblia inasema kwamba wote wanaopotoka, wameoza wote pia. Maneno “wote wamepotoka,” maana yake ni kwamba wameamini fikra na mawazo yao binafisi waki kataa neno la Mungu. Hukumu ya kweli imo katika neno la Mungu. Ni Mungu pekee anaye hukumu. Wanadamu hawawezi kuhukumu. Maneno “wote wamepotoka” maana yake ni kwamba wamefuata mawazo yao. Husema mambo kama vile “Dadhani kwa njia hii na kuamini hivi” Wale wote wasio achana na mawazo yao hawato weza kuyarudia maneno ya Mungu.
Wale ambao hawajazaliwa upya hufikiri kwamba wanaweza kujihukumu wenyewe. Kile kilichoa andikwa katika neno la Mungu kwao hakina umuhimu. Wao hung’ang’ana katika fikra zao na kuhukumu kile wanachoona kuwa ni sawa au si sawa huku wakisema “Nafikiri hivi na kuamini kwa njia hii. Hivi sivyo vile ninavyo fikiri mimi”. Watawezaje watu wa aina hii kupata ukweli? Mungu anasema wanadamu wote wamepotoka kimawazo. Yatupasa tusipotoke kimawazo. Badala yake tumrudie Bwana Yatupasa kuokolewa kwa njia iliyo sahihi. Yatupasa pia kuhukumiwa mbele ya neno la kweli. Hivyo basi, nini maana haki?
 

Yatupasa kuzaliwa upya mara ya pili kwa neno la Mungu.
 
Haki ni neno la Mungu ambalo ni la kweli. Neno la Mungu ni chombo ambacho hupimia viwango vya haki. Yatupasa kujua kwamba neno la Mungu ni mizani “Hapo mwanzo kulikuwa Neno” (Yohana 1:1). Ni nani alikuwa na Mungu Baba na Roho Mtakatifu? Ni Mungu Neno. Neno ni Mungu Yesu Kristo, Mwokozi wetu na Mfalme wa wafalme ndiye Neno, Mungu wetu.
Imeandikwa kwamba Neno alikuwa na Mungu hapo mwanzo. Ni nani alikuwa na Mungu? Neno. Kwa hiyo Neno ndiye Yesu au Mwokozi na Mungu. Mwokozi ni Mungu. Kiwakilishi cha asili yake ni Neno. Hivyo neno la Mungu ni tofauti na mawazo na fikra zetu kwa sababu Neno ndiye Mungu. Ni upumbavu kwa mwanadamu kujaribu kuelewa neno la Mungu kwa mawazo na fikra za kimwili.
Kwa hivyo, Mungu anaweza kumtumia mtu mwenye kusimama imara katika neno lake na katika imani. Mtu asimamaye imara katika neno la Mungu ni mwaminifu na mwenye faida mbele za Mungu, hivyo Mungu humbariki mtu wa aina hii.
Je, mtu aweza kutenda kile kilicho chema? Neno ambaye ndiye Mungu anasema hakuna mwenye haki hata kidogo. Hata hivyo, baadhi hudhani “Inaonekana yupo mtu anaye tenda mema.” Ukweli ni kwamba watu hufanya unafiki mbele ya Mungu. Yatupasa kujua kwamba hatukuwa na sura ya haki kabla ya kuzaliwa upya mara ya pili.
Wanadamu wote wamemwasi Mungu. Hudanganyana na hata kumdanganya Mungu huku wakijifanya kuwa watakatifu, wema na wenye rehema. Ni sawa na kumdhihaki Mungu kwa kujifanya kuwa mwema. Ni Mungu tu ndiye mwema. Hii ni sawa na kwenda kinyume na Mungu na kuasi ukweli wake kwa kujifanya mwema pasipo kuzaliwa upya mara ya pili na kuamini upendo wake na haki yake.
Je, unadhani kwamba wale tu wenye dhambi kubwa ndiyo watakao hukumiwa na Mungu? Yeyote ambaye hajazaliwa upya mara ya pili, hatoweza kuikwepa hasira ya Mungu. Hivyo achana na unafiki wako katika maisha na usikilize neno la Mungu. Uzaliwe upya mara ya pili. Ndipo hapo basi utaweza kuikwepa ile hukumu ya Mungu.
Je, umekwisha muona mtu dhalimu asiye na tamaa ya kupenda kuwa mwema kati ya wale ambao hawajazaliwa upya mara ya pili? Kwa asili watu hutamini sana kuonekana kuwa wao ni wema. Ni nani aliye fundisha hivi? Shetani. Mwanadamu kwa asili hatoweza kuwa mwema. Mwanadamu aweza kuwa na maisha mema endapo tu dhambi itafutwa moyoni mwake mbele ya Mungu. Hivyo basi, je, Mungu anatuelekeza kutenda mambo maovu kwa makusudi? Hapana Mungu anatuambia tupokee ondoleo la dhambi zetu kwa kuwa tayari tumekwisha athirika kwa dhambi hata kabla ya kuzaliwa na hatima yetu ni jehanamu. Mungu anatuhitaji sisi sote kupokea neno lake la kweli ili kwamba tuweze kuokolewa.
 

Shetani Mara zote husema uongo kupitia wasio amini.
 
“Koo lao ni kaburi wazi kwa ndimi zao wametumia hila, sumu ya fira i chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao ina mbio kumwaga damu. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. Wala njia ya amani hawakuijua, kumcha Mungu hakupo machoni pao” (Warumi 3:13-18).
“Kwa ndimi zao wametumia hila” Watu wote ni wepesi sana kusema hila au uongo, Mungu anasema juu ya Shetani “Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe kwa sababu yeye ni mwongo na baba wa huo” (Yohana 8:44). Wale wote ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili utasikia wakiapa “Hakika na kueleza ukweli, Ni kweli tupu” lakini maneno yote haya ni uongo. 
Wale wenye kusisitiza kwamba maneno yao ni ya kweli ndiyo waongo. Je, umekwisha wahi kumwona tapeli akisema “mimi ni mwongo na tapeli” anapo jaribu kudanganya watu? Huongea kama vile kila asemalo ni ukweli mtupu. Wanaweza kushawishi wakisema “ni kweli tupu”. Wanaweza kushawishi wakisema “Hebu ni kwambie jambo: ukiwekeza fedha hapa utaweza kunufaika kwa fedha nyingi. Ukiwekeza shilingi milioni, utaweza kupata faida mara moja haraka. Ni mradi mzuri sana. Je, ungependa kuwekeza sasa? “Wale ambao hawajazaliwa upya mara zote hudanganya kwa ndimi zao.”
Shetani anenapo uongo, hunena kwa yaliyo yake. Mhubiri ambaye hajazaliwa upya hudai kwamba mtu atakuwa tajiri ikiwa atatoa zaka ya kiwango kikubwa. Je, kuna kifungu chochote katika Biblia kisemacho mtu ataweza kutajirika ikiwa atakuwa katika nafasi ya uzee wa kanisa? Kwa nini basi watu hugombania nafasi hii? Jibu, hupendelea nafasi ya uzee wa kanisa kwa sababu wameelezwa kwamba ikiwa watakuwa katika bafasi hiyo Mungu atawapa baraka za kidunia. Wamedanganywa kwa sababu wanaamini kwamba wataweza kuwa na rehema za utajiri ikiwa wata kuwa katika nafasi za uzee wa kanisa. Wamenaswa katika mtego wa ulaghai.
Je, umewahi kuwa katika nafasi kama hii na kudanganywa? Watu wengi wameishi wakiwa kama omba omba baada ya kuwa wazee wa kanisa. Na wafahamu wengi. Manabii wa uongo ambao hawajazaliwa upya mara ya pili huteua matajiri katika nafasi za uzee wa kanisa. Kwa nini? Kwa sababu wana hitaji wazee hao watoe michango mikubwa katika makanisa yao, wakati mwingine huchagua watu wasio na kipato kwa sababu wanapenda kuwageuza kuwa wafuasi vipofu.
Usemi ulio kawaida kwamba “Mtu atabarikiwa kwa mali ikiwa ata kuwa mzee wa kanisa” ni wa kilaghai. Biblia haikutamka hivyo popote. Biblia inasema watumishi wa Mungu imewafaa kuteswa kuliko kupata rehema za utajiri. Bwana anasema “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa” (Mathayo 6:33).
“Sumu ya fira i chini ya midomo yao” ndivyo isemavyo Biblia. Wanadamu wana sumu ya fira katika midomo yao. Nini wasemacho wale wote ambao hawajazaliwa upya mara ya pili dhidi ya wenye haki? Huwatusi wenye haki na kunena sumu ya fira. Biblia inasema “Miguu yao ina mbio kumwaga damu. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao wala njia ya amami hawakuijua. Kumcha Mungu hakupo machoni pao.”
 

Nini kusudi la sheria?
 
Maneno “Kama ilivyoandikwa” maana yake ni kuwa imenukuliwa kutoka Agano la Kale. Mtume Paulo alinukuu Agano la Kale mara nyingi. Alisema “Miguu yao inambio kumwaga damu. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. Wala njia ya amani hawakuijua. Kumcha Mungu hakupo machoni pao.” Nawasikitikia wale wote watakao kwenda jehanamu pasipo kujua njia ya kuzaliwa upya mara ya pili.
Warumi 3:19 inatamka “Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe na uliwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu.” Mungu huleta gadhabu kutokana na sheria kwa wale ambao bado hawajazaliwa upya. wasiojua dhambi na wasiojali dhambi kuwa ni dhambi, ili kuwaweka wazi wenye dhambi wasio weza kufuata sheria katika mazingira yao halisi. Mungu hakutupatia sheria ili kuifuata. Sasa basi, Je, Mungu anasema kwamba ameiharibu sheria? Hapana. Ametupatia sheria kupitia Musa ili kutupatia ufahamu wa dhambi zetu. Hakutupa ili tuweze kuifuata. Sheria ya Mungu ina kazi ya kutufundisha vile tulivyo wenye dhambi.
 

Hakuna awezaye kuwa mwenye haki kwa matendo ya sheria.
 
Warumi 3:20 inatamka, “hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” Wakristo walio zaliwa upya wanafahamu kwamba hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa haki kwa matendo ya sheria. Mtume Paulo na watumishi wengine wote wa Mungu husema “hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa haki kwa matendo ya sheria.” Hakuna yeyote anaye fuata sheria au atakaye fuata sheria hapo mbeleni. Hivyo basi yatupasa kukiri kwamba kamwe hatuto hesabiwa haki kwa matendo ya sheria. Matendo yetu hayawezi kutufanya kuwa wenye haki.
Mtume Paulo alijua na kuamini hili. Je, twaweza kuhesabiwa haki kwa kufuata sheria? Je, sheria yaweza kutuhesabia haki? Unapo soma maandiko je, unadhni ni vyema kuamini kwamba miili yetu hubaadilika ili kuhesabiwa haki na hatimaye kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa kutenda mambo mema baadya ya kumwamini Yesu? Hapana hili si kweli. Ni uongo. Ukweli wa kwamba mtu huingia Ufalme wa Mungu kwa kubadilishwa hatua kwa hatua katika viwango vya kuwa mwenye haki na utakaso ni uongo na kejeli mbele za Mungu. Watu wote ambao bado hawaja zaliwa upya mara ya pili ndiyo alio chini ya sheria kwasababu inawalazimu kufuata sheria ya neno la Mungu kwa matendo yao. Ndivyo sheria iwalazimishavyo katika kuifuata huku wakisali sala za toba kila leo. Na hii hutokana na kufunga kifungo cha kwanza katika vazi. Sheria ndiyo itupayo ufahamu wa kuwa ni wenye dhambi. Juhudi ya wenye dhambi kufuata sheria ni kutokana upumbavu wao na mawazo yao yaliyo kinyume na wokovu wa kweli na pia kutokana na miili yao. Hii ni imani iliyo batili.
Fundisho la utakaso, lisemalo kwamba tuna hesabiwa haki kwa kubadilika toka viwango hata viwango, pia laweza kupatikana katika dini za duniani. Ubudha (Buddhism) nao una fundisho kama hili, ambalo huitwa “Nirvana”, ambalo lafanana na hili la Kikristo. Watu wengi husema kwamba miili yao yaweza kutakasika zaidi na zaidi na wataweza hatimaye kuingia Ufalme wa Mbinguni. Lakini ukweli ni kwamba, Bwana alitakasa roho zetu mara moja na kwa wakati wote.
Hata mwenye haki hawezi kutakaswa mwili. Wale wote wasio na Roho kamwe hawato takaswa. Kila watakapo jaribu kutenda mema, ndivyo watakavyo zidi kuwa wenye dhambi zaidi na zaidi. Hii ni kutokana na kwamba bado wanadhambi mioyoni mwao. Kila jambo chafu hutoka mioyoni mwao na hatimaye kuwachafua ingawa kwa nje wanaweza kuonekana wakijaribu kwa dhati kujitakasa kwa sababu ndani yao wamejaa dhambi. Huu ndio ukweli halisi wa wenye dhambi mioyoni.
Hali hii ya kibinadamu ni kinyume kwa wale ambao tayari wanaondoleo la dhambi. Wanaweza kuishi maisha safi ingawa hawawezi kujizuia kutenda dhambi kwa miili yao. Wenye dhambi walio zaliwa wakiwa waathirika wa dhambi husambaza dhambi hizo maishani mwao pote kwa sababu dhambi hutoka nje ya mapenzi yao. Hawana uchaguzi zaidi ya kupata tiba ya mara moja ambayo itaweza kuondolea mbali dhambi zao moja kwa moja na kwa wakati wote. Tiba hiyo ya mara moja ni Injili ya neno la Mungu, wataweza kukombolewa kutokana na dhambi zao kwa kusikiliza neno la ondoleo la dhambi. Napenda nanyi msikilize neno la kuzaliwa upya mara ya pili na hatimaye kupokea ondoleo la dhambi.
Ni nani awezaye kuishi kwa kuifuata sheria bara bara? Ni nani awezaye kuishi maisha ya kiukamilifu kwa kulingana na sheria ingawa amezaliwa upya mara ya pili? Hakuna. Katika Warumi imeandikwa “Kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” Ni rahisi kabisa kueleweka. Adamu na Hawa walidanganywa na shetani nyakati za hutotuhumiwa na wakajikuta chini ya dhambi. Na dhambi hii ikarithiwa kwa vizazi vyao ambavyo hawakufahamu neno la Mungu. Hawakujua kwamba wao wamezaliwa wakiwa ni wenye dhambi ingawa walikuwa wamerithi.
Baada ya kipindi cha Abrahamu na Yakobo, Waisraeli walisahau juu ya imani na hali ya dhambi zao, ingawa mzee wao Abrahamu alifanywa kuwa mwenye haki kwa imani. Hivyo basi Mungu akawapa sheria yake ili kwamba waweze kuja dhambi zao na kuwahitaji kupokea ondoleo la dhambi kwa kuamini agano lake. Je, wewe nawe unaamini hili?
 

Lakini sasa haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria.
 
Warumi 3:21 inatamka kwamba “Lakini sasa haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria inashuhudiwa na torati na manabii.” Mtume Paulo anasema kwamba haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria. Maneno “Inashuhudiwa na torati na manabii” yanaashiria Agano la Kale. Injili ya maji na Roho ni haki ya Mungu iliyo dhihirishwa kupitia mpagnilio wa utoaji wa sadaka katika Agano la Kale. Injili inadhirisha haki ile yenye kutuongoza katika kupokea ondoleo la dhambi kupitia sadaka ya dhambi.
Warumi 3:22 inatamka “Ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio maana hakuna tofauti.” Imani zetu zimo mioyoni. Yesu ni mwanzilishi na mwenye kutimiza imani yetu. Waebrania 12:2 inatamka kwamba “tukimtazama Yesu mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu.” Mwanzilishi na mtimizaji wa imami ni Yesu na tunaona Neno la kweli, ambalo ndiye Mungu. Yatupasa kujifunza na kuamini ukweli na maneno ya biblia toka kwa wale walio zaliwa upya mara ya pili, watumishi wa Mungu, ili kwamba tuokolewe kutokana na dhambi zetu zote na hatimaye tuishi kwa imani. Yatupasa kumwamini Yesu kwa mioyo yetu yote.
Mungu anasema “Ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti.” Kwahiyo, tumefanywa kuwa wenye haki kwa kuamini neno la kweli kwa mioyo yetu na hatimaye kuwa na uhakika wa wokuvu kamili kwa kukiri kwa vinywa vyetu. Hatutoweza kuokolewa kwa matendo yetu bali kwa imani. Tunampa Bwana shukrani yeye pekee na kanisa la Mungu.
Je, unafungwa na matendo yako ingawa dhambi zako zote zimekwisha kufutwa? Wewe ni mwenye haki ikiwa unamwamini Mungu kwa moyo wako wote ukiachilia kwamba mwili wako kuwa dhaifu. Roho Mtakatifu hushuhudia neno la Mungu mioyoni mwetu akisema “Wewe ni mwenye haki” kwa sababu anatuongoza katika kuelewa neno la kweli pale tunapo sikia neno. Je, uliokolewa kwa imani baada ya kusikia neno la Mungu?
“Ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti.” Yeyote anaye jifunza na kuamini neno la Mungu ambalo ndilo kweli, ataweza kuokolewa toka dhambini mwake.
 

Yesu alitakasa dhambi zote toka mwanzo hata mwisho na dunia.
 
Warumi 3:23-25 inatamka kwamba “Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu ambaye Mungu amekweisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake ili aonyeshe haki yake kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa.”
Biblia inasema kwamba wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Tunapokea msamaha wa dhambi na kufanywa wenye haki bure kwa rehema zake na upendo wake huku wale walio na dhakmbi hutupwa jehanamu. Tunafikia utukufu wa Mungu na kufanywa wenye haki. Mungu amemleta Yesu ili awe kipatinisho kwa damu yake kupitia imani.
Mstari wa 25 na 26 unatamka kwamba “Ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake ili aonyeshe haki yake kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kuhesabiwa haki yeye amwaminiye Yesu.” Hapa maneno “amekwisha kumweka” maana yake Mungu alimtuma Mwana wake Yesu ili awe upatanisho wa dhambi kwa ulimwengu wote.
Yesu alizichukua dhambi zote za dunia kwa ubatizo wake. Yesu ni Alfa na Omega. Hebu tufikiri juu ya mwanzo na mwisho wa dunia. Mungu alitukomboa kwa imani ambayo itakasayo dhambi zetu zote toka mwanzo hadi mwisho wa dunia. Mungu alimweka Yesu awe upatanisho kupitia imani ya kweli. Mstari usemao “Ili aonyshe haki yake kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimi wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa” sikuweza kuuelewa hadi pale nilipo amini Injili ya kweli.
Dhambi zetu zote zimeondolewa pale tunapo amini neno lisemao Yesu alikwisha futa dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo wake na damu yake. Tunapokea ondoleo la dhambi mara moja na kwa wakati wote, lakini miili yetu bado inaelendela kutenda dhambi. Mwili hutenda dhambi kutokana na udhaifu wetu. Hata hivyo Biblia inatamka kwamba “Kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilitangulia kufanywa.” Dhambi amabazo mwili hutenda hata sasa na mbeleni ni dhambi zilizotangulia kufanywa mbele ya mtazamo wa Mungu.
Kwa nini? Mungu aliufanya ubatizo wa Yesu kuwa ndiyo kitovu cha dira ya wokovu. Hivyo dhambi za mwili katika wakati uliopo ni dhambi zilizokwisha kufanywa kwa mtazamo wa Mungu, kwa sababu ondoleo la dhambi lilihitimishwa na Yesu Kristo mara moja na kwa wakati wote. Dhambi za wakati ulipo ni dhambi ambazo tayari zilikwisha futwa. Maneno yasemayo, “Kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa” yana maana kwamba “tayari Mungu amekwisha lipa mshahara wa dhambi za dunia” Dhambi zote za dunia zimekwisha samehewa kwa kupitia ubatizo wa Yesu na msalaba wake.
Kwa hiyo Mungu amekwisha futa dhambi zote zitendwazo toka mwanzo hadi mwisho wa dunia. Hivyo basi dhambi zote zilikwisha tendwa siku za nyuma kwa mtazamo wa Mungu. Watu duniani hutenda dhambi ambazo tayari zimekwisha futwa na Mwana wa Mungu. Yesu amekwisha takasa dhambi zote ambazo zitatendwa mwaka 2002 tokea miaka 2,000 iliyo pita. Je, unaona maana yake? 
Unaweza ukachanganyikiwa na kutoelewa ikiwa utahubiri Injili kwa watu kama hujaelewa hili. Maneno “dhambi zilizo kwisha kufanywa” yanamaana kwamba Mungu hazitazami tena dhambi zilizo kwisha pita kwa sababu alikwisha zifuta takribani miaka 2,000 iliyo pita. Dhambi za wanadamu wote zimekwisha hukumiwa kwa sababu Yesu alibatizwa katika mto Yordani na kusulubiwa. Mungu alimtwika dhambi zote Yesu kwa sababu alimleta duniani na kwa njia iliyo stahiki aliwafanya wanadamu kuwa wenye haki mara moja na kwa wakati wote. Kwa hiyo Mungu hadai dhambi zilizotendwa na watu duniani ambazo zimekwisha kufutwa naye bali kwa sasa yeye hudai lile la kutoamini ubatizo na msalaba wa Yesu ambako ndiko anako wahukumu.
Je, unaelewa kile Mtume Paulo anacho maanisha? Ni muhimu sana. kwetu sisi tulio okolewa. Wale ambao bado hawajaokoka wata ishi jehanamu kwa sababu wanadharau hili. Yatupasa kusikia na kuwa na imani sahihi katika kufahamu neno. Itakuwa na msaada mkubwa kwa imani yako na kwa kuihubiri Injili kwa watu wengine.
 

Ku wapi basi kujisifu?
 
Biblia inasema “Ili aonyeshe haki yake kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zlizotangulia kufanywa.” Mungu anatufundisha kwamba dhambi zilizopita tayari zimekwisha futwa kwa sababu Mungu alimfanya Yesu kuwa upatanisho. Kwa hiyo tumefanywa kuwa wenye haki kwa imani.
Mstari wa 26 unatamka “apate kuonyesha haki yake wakati huu ili awe mwenye ahaki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu.” “Kwa wakati huu” ameupa ulimwengu upendo wa milele ili kwamba usiangamie, “kwa wakati huu.” Mungu alimtuma Yesu Kristo ili kudhihirisha haki yake na kukamilisha kile alicho ahidi. Bwana alidhihirisha haki yake. Mungu alimtuma mwana wake wa pekee na kumfanya abatizwe na kusulubiwa ili kutuonyesha upendo wake kupitia wokovu wa kweli.
Bwana alikuja kwa wenye dhambi akiwa ni Mwokozi “Apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kuhesabiwa haki yeye amwaminiye Yesu.” Mungu ni mwenye haki na afutaye dhambi za dunia mara moja na kwa wakati wote. Tunamwamini Yesu kwa mioyo yetu, hivyo hatuna dhambi. Wale wote wamwaminio Yesu kwa hakika, ndiyo wasio na dhambi kwa sababu alizitakasa na hata kutuokoa kwa zile za mbeleni. Kuamini kile Yesu alichofanya kwa mioyo yetu hutuokoa. Matendo yetu hayamo hata kwa 0.1% katika imani ya wokovu wake.
Warumi 3:27-31 inatamka kwamba “Ku wapi, basi kujisifu? Kumefungiwa nje, kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! bali kwa sheria ya imani. Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. Au Je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia; kama kwa kweli Mungi ni mmoja atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo. Basi je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.”
Maneno ya “twaithibitisha sheria” maana yake hatutoweza kuokolewa kwa kupitia matendo yetu. Sisi si wakamilifu na nidhaifu na inatupasa kwenda jehanamu mbele ya sheria. Hata hivyo neno la Mungu limetufanya kuwa wenye haki na kamili kwa sababu tumeokolewa kwa neno la Mungu. Bwana anatuambia kwamba miili yetu bado si kamilifu hata baada ya kuokolewa kwa dhambi zetu zote. Twaweza kuwa karibu na Mungu kwa kuamini kwamba Yesu alituokoa.
“Ku wapi basi, kujisifu? Kumefungiwa nje kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani.” Yatupasa kujua sheria ambayo Mungu aliyoidhihirisha na kwamba sheria hiyo ni ya Ufalme wake wa milele “Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani” asema Mungu. Je, unaelewa hili? Mungu alituokoa kwa dhambi zetu zote duniani. Tumeokolewa pale tulipoamini kulingana na ukweli. Yatupasa kukumbuka kwamba matendo ya sheria hayatoweza kutuokoa.
Mungu anazungumzia juu ya sheria ya imani kupita Mtume Paulo katika Warumi sura ya 3 Mungu anasema “Je, kutoamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?” (Warumi 3:3). Wenye kuamini husimama imara kwa imani lakini wasio amini huanguka. Wale wasio na imani iliyo kamilika katika Injili ya kweli wata kwenda jehanamu, ingawa wao wanadhani kuwa wana mwamini Yesu.
 

Mungu alituokoa sote kiukamilfu kutokana na dhambi zetu zote.
 
Mungu aliidhihirisha sheria yake ili kwamba wale wote wenye kuamini kulingana na mawazo yao waweze kujikwaa kwa sheria ya imani. Mungu alituokoa vyema sisi sote kwa dhambi zetu zote. Warumi sura ya 3 inazungumzia juu ya sheria ya imani. Tumeokolewa kwa kuamini neno la kweli. Tuna urithi Ufalme wa Mbinguni na hata kuwa na amani kwa imani. Wasio amini kamwe hawawezi kuwa na amani. Badala yake watakwenda jehanamu kulingana na sheria ya kweli ya Mungu kwa kuwa hawakulipokea neno la kweli la Mungu. Wokovu huja kutoka katika upendo wa Mungu na tunaokolewa kwa kuifahamu kweli na kuamini kile Bwana alicho tenda kwa mioyo yetu Je, unaelewa hili?
Namsifu Bwana aliyetupatia imani hii na kanisa lake hapa duniani. Nampa Bwana shukrani aliyetupa ukweli, imani na neno, ambalo alikua nalo Mtume Paulo, na ndiye aliye funua siri ya ondoleo la dhambi kwa kanisa la Bwana. Namsifu toka katika kina cha moyo wangu.
Tunamshukuru Bwana kwa kuwa ametuokoa kupitia ubatizo na kifo chake msalabani. Hakuna uchaguzi bali kwenda jehanamu pasipo kuwa na imani hii na kanisa lake. Tulikuwa ni wenye dhambi ambao kamwe tusinge okolewa kutokana na asili yetu, lakini tunaamini haki ya Mungu kwa mioyo yetu yote. Tunakuwa watoto wake wenye kuamini haki kwa moyo na kuokolewa kwa kukiri kwa kinywa (Warumi 10:10).