Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 3-1] Utangulizi katika Kitabu cha Warumi Sura ya 3

Paulo alisema, kutokuamini kwa watu hakubadili uaminifu wa Mungu. Akindelea kutoka sura ya 2, Mtume Paulo alitaja katika sura hii kwamba Wayahudi hawana upendeleo zaidi ya watu wa Mataifa. Katika sura hii, Paulo alilinganisha sheria na ile kanuni ya haki ya Mungu kabla ya kuzungumzia sheria ya haki ya Mungu inayo mruhusu mwenye dhambi kupokea haki yake na hatimaye uzima wa kweli. Pia alifafanua katika sura hiyo juu ya wokovu toka dhambini kuwa si kupitia matendo yetu bali kupitia imani katika haki ya Mungu.
Mtume Paulo alisema kwamba ingawa, Wayahudi na watu wengine hawaiamini haki ya Mungu, kutoamini kwao bado hakubatilishi haki yake. Mungu hawezi kudanganya uaminifu wa haki yake. Kamwe hauto toweka. Matokeo yake kamwe hayato potea kwa sababu tu eti Wayahudi hawamwamini yeye na haki yake.
Haki ya Mungu ambayo Paulo alihubiri juu yake haiwezi kubatilishwa kwa sababu tu ya watu kutoiamini. Yeyote aaminiye wokovu Mungu aliowapa wenye dhambi atapokea haki ya Mungu na haki hii ni sahihi zaidi na imepita akili za kibinadamu.
Paulo aliwashutumu wale wote wasio iamini haki ya Mungu kwa kumfanya Mungu kuwa mwongo. Mungu alisema kwamba kwa ukamilifu aliwaokoa watu toka dhambini mwao kwa njia ya haki yake, lakini hawakuiamini, hivyo basi wakamfanya kuwa mwongo. Hata hivyo haki ya Mungu haijaathirika kwa kutoamini kwao.
 

Haki ya Mungu imedhihirika Vipi?
 
Wale wote wasio iamini haki ya Mungu watahukumiwa kwa dhambi zao. Sote twaweza kuidhihirisha haki ya Mungu kwa wokovu aliotupatia. Wale wote wenye kuiamini haki yake hupokea msamaha wa dhambi na kupata uzima wa milele. Hivyo kila mmoja aweza kubarikiwa kwa kuiamini haki ya Mungu.
Haki ya Mungu si batili bali ni kweli. Kila mmoja si mkweli mbele ya Mungu. Lakini Mungu hutenda vile alivyo ahidi na hata kutimiza ahadi zake. Hivyo uaminifu wake huushinda uongo wa wanadamu. Wanadamu yawapasa kuiamini haki yake. Mungu haendi kinyume au kubadili kile alichosema, bali wanadamu mara nyingi hubadilika fikra kulingana na mazingira wanayo tathimini. Siku zote Mungu hushika uaminifu katika kile alicho waambia wanadamu.
Warumi 3:5 inatamka kwamba “Lakini ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu tuseme nini?” Udhalimu wa mwanadamu waithibitisha haki ya Mungu.
Haki ya Mungu inathibitishwa zaidi kwa udhaifu wetu. Hii ni kutokana na vile ilivyo andikwa, Yesu binafsi alitenda haki ili kuokoa wenye dhambi tokana na dhambi zote. Hivyo haki ya Mungu hung’ara zaidi na zaidi hata katika udhaifu wa wanadamu. Ukweli huu waweza kupatikana katika Injili ya maji na Roho ambayo imejaa haki ya Mungu. Sababu ya hili ni kwamba, watu wote huendelea kutenda dhambi hadi mwisho wa mauti yao, na upendo wa Mungu huokoa wenye dhambi zaidi.
Bwana wetu alishinda dhambi zote za ulimwengu na kukamilisha wokovu wake kwa njia ya msamaha wa dhambi. Hakuna yeyote awezayo kuishi pasipo kutenda dhambi. Kwa kuwa hatima ya watu ni motoni, Mungu amekwisha suluhisha juu ya hilo kwa upendo wake ambao ndiyo haki yake.
Sisi tulikuwa ni walaghai toka tulipo zaliwa na kuikataa haki ya Mungu kwa kutoamini maneno yake. Mwanadamu mwisho wake alikua ni kuangamia mbele za Mungu, kwa sababu hakuna hata tendo moja lao lilokubalika mbele zake. Lakini Mungu alituokoa kutokana na dhambi zetu kwa upendo wake kwa kutuonea huruma. Watu wote walikuwa watupwe motoni kwa sababu walikuwa ni dhalimu kwa udanganyifu wa shetani na hivyo wote kutenda dhambi. Hata hivyo Mungu alimtuma mwana wake wa pekee ili kutuokoa tokana na mikono ya shetani na nguvu za giza.
Mtume Paulo alisema kwamba mwandamu aweze kuwa na tabia njema kila siku, lakini mwishowe hawezi kujizuia kutenda dhambi maishani mwake pote. Hata hivyo udhalimu huo wake hatimaye unadhihirisha haki ya Mungu na upendo wake. Kusema kweli, wanadamu hawana haki binafsi na hivyo kupelekea kumhitaji mjumbe kama Mtume Paulo. Yeye aliijua na kuipokea haki ya Mungu na hatimaye kuweza kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake. Na hii ndiyo sababu aliweza kuihubiri haki ya Mungu.
 

Injili Paulo aliyohubiri ilihusika na haki ya Mungu.
 
Injili ambayo Paulo aliihubiri ilikuwa katika msingi wa haki ya Mungu. Ilimlazimu Paulo kuihubiri Injili hii kwa sababu Mungu aliwapenda wenye dhamba na hivyo kuwaokoa kwa dhambi zao. Upendo wa Mungu wa ukombozi umo katika Injili ya maji na Roho. Hivyo, msamaha wa dhambi hutegemea imani zetu katika haki ya Mungu. Hata hivyo, tatizo ni watu kudhani kiujumla kwamba imewapasa kuishi maisha ya uadilifu ili waweze kuokolewa au kuendelea na wokovu wa Mungu. Wanadamu kamwe hawatoweza kuwa wema kwa msingi wa tabia. Hiki ndicho kizingiti cha kuikubali haki ya Mungu. Watu imewapasa kuvunjilia mbali mawazo yao au fikra zao katika kuishi maisha ya uadilifu ili kuweza kuikubali Injili ya tohara ya kiroho ndani ya mioyo yao ambayo Mungu aliileta.
Ukweli ni kwamba, hakuna hata mmoja awezaye kuwa mwema. Sasa basi, mwenye dhambi atawezaje kuokolewa kwa dhambi zake zote? Yampasa kuachilia mbali fikra ya kwamba imempasa kuishi maisha ya uadilifu ili aweze kuokolewa. Wengine hukataa kuacha fikra zao na viwango vyao, na hivyo hawato weza kuokolewa kikamilifu kwa dhambi zao. Haki ya Mungu, ambayo imefunuliwa katika Injili ya tohara ya kiroho ndiyo ituwezeshayo kubaini vile namna ambavyo udhalimu wetu ulivyo hifadhiwa, ili kwamba tu upendo wa Mungu ubainishe vile haki yake ilivyo. Kwa sababu hiyo basi wale wote wenye kuamini haki ya Mungu wanajivunia haki yake na si ile haki yao binafsi. Haki yenye kujivunia haki ya Mungu na kuitukuza zaidi huja toka kwa Mungu.
Mtume Paulo hudhihirisha hadhi ya washika sheria wenye kuamini kwamba wataingia Mbinguni ikiwa watatenda matendo ya uadilifu, lakini wasipo tenda na kuishi kwa uadilifu baada ya kumwamini Yesu, kamwe hawatoweza kufikia haki ya Mungu. Sheria inafanana na kioo kinacho bainisha na kuweka wazi dhambi za wanadamu. Paulo anafundisha kwamba watu wanaimani zenye mwonekano wa kupendeza kwa nje ambazo si sahihi. Hivi ndivyo Paulo afundishavyo na kuelekeza vile haki ya Mungu ilivyo.
Paulo huzungumza na wale wote wenye kufuata walimu waongo wasio fikiri kwamba wataweza kuwa wenye haki na wasio na dhambi baada ya kumwamini Yesu. Hufundisha wasioamini kuweza kuiamini haki ya Mungu na hata kuwa huru toka hukumuni. Paulo husema kwamba wale wasio amini wokovu wa maji na damu ya Yesu, wamo chini ya hukumu na kwa kuwa hawamwamini Mungu ni halali kwao kuhukumiwa. Husema kwamba wenye dhambi imewapasa kuirudia haki ya Mungu na hatimaye kuipokea haki yake ili waweze kukombolewa toka hukumu ya kutisha.
 

Je twaweza kutenda dhambi zaidi kwa kuwa tu, twaiamini haki ya Mungu?
 
Mstari wa 7 unatamka “Lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu mbona mimi ni ngali na hukumiwa kuwa ni mwenye dhambi?” Kwa hiyo ikiwa tunaitwa wasio na dhambi je, twaweza kutenda dhambi kwa uhuru? Paulo alifafanua kipengele hiki. Kwa kuwa Mungu alikuokoa kwa haki yake, sasa basi je, umeruhusiwa kusema uongo kwa uhuru? Ikiwa unaamini hivyo, basi yakupasa ujue kwamba bado hujaifahamu haki ya Mungu na hivyo unaipuuza haki hiyo.
Hata nyakati hizi, wapo watu wengi wenye kuipuuza haki ya Mungu mioyoni mwao; na hii hainatofauti na hapo wakati wa nyuma. Paulo aliandika hili takribani miak 2000 iliyopita na hata hapo nyuma palikuwepo watu walio waza kwa fikra zao.
Hata leo hii, Wakristo wengi ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili, huelewa visivyo kwa kudhani basi wataweza kutenda tena dhambi kwa makusudi. Watoe ambao bado hawajazaliwa upya hudhihaki wenye haki ambao wamezaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho kwa kupitia fikra zao za kimwili na kuwasengenya kwa mawazo yao yasioyo na imani. Imani ya kweli haitoweza kueleweka kwa mwili wa mwanadamu. Dhambi ni kitu unachoendelea kutenda maishani pote. Wote wenye haki na wasio na haki hawatoweza kujizuia kwa dhambi. Hata hivyo wale wote wenye kuipinga na kuidharau haki ya Mungu ndio wenye dhambi huku wale wenye kuiamini ndiyo wasio na dhambi.
Paulo alisema kwa wale wasio amini “Ni nini basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je, kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha!” (Warumi 3:3-4). Kwa kuwa wanadamu hawaiamini haki ya Mungu, kutoamini kwao hakutoweza kuifanya haki yake iwe ni bure. Ikiwa mtu ataiamini haki ya Mungu basi ataokolewa. Hata hivyo ikiwa mtu hatoiamini basi hatoweza kuipokea haki hiyo. Hivi ndivyo ilivyo. Haki ya Mungu itasimama imara daima. Wale waendao jehanamu ndiyo wasio amini ubatizo na damu ya Yesu na kamwe hawato weza kutakaswa kwa dhambi zao. Haki ya Mungu yenye kuwaelekeza wanao amini katika kuzaliwa upya kamwe haito potea kwa sababu tu watu hawaiamini.
 

Kuipata haki ya Mungu hakuhitaji juhudi ya kibinadamu.
 
Kuipata haki ya Mungu hakuna uhusiano na juhudi zetu binafsi. Ina husiana na imani zetu za kweli ambazo haki ya Mungu ndiyo ondoleo la dhambi zetu. Mtu anaye amini kweli wa maji na Roho ndiye apokeaye haki na hukumu kulingana na maneno ya kweli ya Mungu.
Hivyo Mungu alimtuma Yesu ulimwenguni na kumfanya awe ni jiwe la kizingiti na mwamba wa mkosaji kwa wale wote wasiotii haki ya Mungu. Wapo watu wengi ambao kwa hiyari hupenda jehanamu kwa sababu hawataki kuiamini haki ya Mungu. Hata hivyo Yesu jiwe la kizingiti na mwamba wa mkosaji, amewapa haki ya Mungu kwa njia ya kuwa Mwokozi. Hata yule aliye mwovu zaidi aweze kuipata njia ya kuwa mwenye haki na hatimaye uzima wa milele. Hata mtu atendaye matendo mema hatoweza kukombolewa toka katika uaribifu ikiwa hatoiamini haki ya Mungu ambayo ndiyo imwezeshayo kupokea ondoleo la dhambi na hatimaye kuzaliwa upya mara ya pili.
Kwa kuwa basi mshahara wa dhambi ni mauti yeyote yule mwenye dhambi atapitia hukumu. Yesu amekuwa ni jiwe la kizingiti na mwamba wa mkosaji kwa wale wote wanao jaribu kuanzisha haki binafsi na kutaka kuingia Mbinguni pasipo kuiamini haki ya Mungu. Hivyo sababu ya watu kuangamia ni kuto amini haki yake.
Baadhi husema kwamba wao ni wenye dhambi walio okoka, lakini hakuna kitu kama hicho, “mwenye dhambi aliye okoka.” Yawezekanaje mtu awe mwenye dhambi tena baada ya kuokolea kwa dhambi zake zote? Mtu si mwenye dhambi ikiwa ameokolewa toka dhambini na pia atakuwa ni mwenye dhambi ikiwa bado kupokea wokovu wa dhambi. Dhambi ikiwa bado imo ndani yake basi hawezi kupokea wokovu. Hapatakuwepo hata mtu mmoja mwenye dhambi katika Ufalme wa Mbinguni. Mungu asema “Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni wala wakosaji katika kusanyika la wenye haki” (Zaburi 1:5).
Watu hubaki bumbuwazi wakiwa na swali la namna ya kuweza kuwa wenye haki huku kila siku wakitenda dhambi. Hata hivyo hakuna haja kwao kutaharuki juu ya hilo. Kuwa mwenye haki kwa kuamini haki ya Mungu inawezekana kwa kuwa tu tayari Bwana alikwisha zibeba dhambi za ulimwengu pamoja, hata na zile zijazo juu yake kwa kupokea kwake ubatizo katika Mto Yordani, na hatimaye kufa msalabani hivyo basi kuitimiza haki ya Mungu. Wenye dhambi wataweza kuwa wenye haki kwa kuamini haki ya Mungu. Je, bado ni mdaiwa hata baada ya deni lako lote kulipwa?
Bwana wetu aliondoshea mbali dhambi zote kwa haki yake. Bwana aliokoa wale wote wenye imani thabiti katika Injili ya maji na Roho. Hivyo kwamba hakuna tena hukumu kwao hata ikiwa ni wenye udhaifu kwa namna yeyote. Sote twaweza kuwa wenye haki kwa kuamini haki ya Mungu.
 

Fikra za kibinadamu hupelekea mauti.
 
Fikra za kibinadamu hutupeleka mautini na chanzo chake ni akili ya kimwili. Akili ya kiroho imetokana na imani katika haki ya Mungu. Ni rahisi mno kwa shetani kutawala akili au fikra za wanadamu. Wanadamu hawana jinsi zaidi ya kutenda dhambi kwa kupitia miili yao. Hata hivyo mtu mwenye imani ya haki ya Mungu aweza kuwa mwenye haki kwa imani katika ubatizo na damu ya Yesu. Mtu hatoweza kuwa mkamilifu asiye na dhambi kwa mabadiliko ya umbile, tabia au utu wa nje ili aweze kuingia Mbinguni, kwa kuwa hakuna mtu mtakatifu asiye tenda kamwe makosa au dhambi mbele za Mungu.
Twaweza kuokolewa toka dhambini mara moja kwa kuamini haki ya Mungu. Zaidi ya yote kila mwenye dhambi huamini rehema uliyomo katika Injili ya maji na Roho, ambayo ndiyo iongozayo wenye kuiamini kuelekea kuzaliwa upya mara ya pili. Yawezekana, kuonekana ni vigumu kwa mtu kuweza kuwa asiye na dhambi kwa mtazamo wa kibinadamu. Hata hivyo inawezekana kwa imani katika neno la Mungu. Mtu hawezi kuishi pasipo kutenda dhambi kupitia mwili. Lakini moyo wake waweza kuwa usio na dhambi ikiwa kweli anaimini haki ya Mungu. Miili ya wanadamu huitaji kujitosheleza na haja zake kirahisi na hivyo kuangukia dhambini kwa kuwa wakati wote hutamini mazuri. Mungu hunena kweli, mtu aweza kuwa mwenye haki ikiwa tu atakuwa na imani katika Injili ya maji na Roho, ambayo Bwana wetu alitupatia. Hatutoweza kuingia Mbinguni kupitia miili yetu bali kwa kuiamini haki ya Mungu.
 

Ipo tofauti kati ya akili ya kimwili na ile akili ya kiroho.
 
Akili ya kimwili kamwe haiwezi kuelewa ukweli kwamba waweza kutokuwa mwenye dhambi kwa imani na hatimaye kuwa mwenye haki, Mkristo aliyezaliwa upya mara ya pili. Kwa sababu hudhani kwamba ingawa mtu atatubu makosa yake bado ataendelea kutenda dhambi siku inayofuata.
Hata hivyo ingawa si rahisi kwa mtu kuwa mwenye haki kwa njia ya matendo mema ya kibinadamu, kwa upande mwingine inawezekana kabisa kupitia haki ya Mungu. Hii ni kutokana na mtu aweza kuipokea haki ya Mungu kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu. Haki ya Mungu inauweza wa kufutilia mbali dhambi zote za wanadamu. Inawezesha sisi kuwa wenye haki na hatimaye kumwita Mungu kuwa ni Baba. Hivyo inakupasa kufahamu kwamba imani ya kweli huanzia katika imani ya haki ya Mungu. Imani ya kweli haianzi kwa fikra au mawazo ya kimwili bali ni kwa imani ya maneno ya kweli.
Watu wengi ambao bado hawajazaliwa upya hawawezi kukwepa fikra zao kwa sababu wakati wote wamefungwa ndani yake. Watu hawa kamwe hawawezi kusema kwamba wamekuwa wenye haki kwa sababu hufikiri kimwili tu, ingawa husema wanamwamini Yesu. Mtu aweza kusema kwamba yeye hana dhambi mbele ya Yesu pale tu atakapo amini maneno ya tohara ya kiroho ambayo huleta haki ya Mungu.
Hivyo basi, ikiwa mtu atahitaji kupokea haki ya Mungu, inampasa ayasikilize maneno ya kweli toka kwa mtu aliye zaliwa upya mara ya pili ndipo basi ayaamini kwa moyo wake wote. Roho Mtakatifu huweka makazi kwa kila mtakatifu anaye amini haki ya Mungu. Natumaini ninyi ndugu zangu mnaendelea na ukweli huu akilini mwenye. Ikiwa unatamani kweli kupokea baraka ya kuzaliwa upya, Mungu ataruhusu na kuwezesha wewe ukutane na mtu anaye amini haki ya Mungu.
 

Je, wewe wasema kwamba hakuna mwenye haki?
 
Mstari wa 9 na 10 unatamka! “Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi kama ilivyo andikwa ya kwamba hakuna mwenye haki hata mmoja.”
Maana yake ni nini? Je, maneno haya yanazungumzia hali yetu kabla au baada ya kuzaliwa upya mara ya pili? Sote tulikkuwa wenye dhambi mbele ya Mungu kabla ya kuokolewa. Maneno “hakuna mwenye haki hata mmoja” yanabainisha na kuelezea kipindi kabla Yesu kuitimiza huduma ya kuondolea mbali na kufuta kabisa dhambi ya ulimwengu. Mtu hatoweza kuwa mwenye haki pasipo kumwamini Yesu.
Hivyo maneno “utakaso wa awamu hatua kwa hatua” yalikuja na kuwepo kupitia wale wote walio kuwa wakitumikia dini na madhehebu au miungu ya sanamu. “Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Je, unadhani kwamba mwenye dhambi aweza bila shaka kuwa mwenye haki kwa kupitia kuifunza nafsi yake na kupanda mema? Kamwe mtu hatoweza kuwa mwenye haki hata mmoja. 
“Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Hakuna hata mmoja atakaye weza kuwa mwenye haki au amekwisha kuwa mwenye haki kwa kupitia maisha binafsi ya uadilifu. Hakuna hata mmoja aliye kwisha kuwa mtu asiye na dhambi kwa njia binafsi. Inawezeka pale tu kupitia imani katika tohara ya kiroho yenye haki ya Mungu ndani yake.
Mstari wa 11 pia unatamka kwamba “Hakuna afahamuye hakuna amtafutaye Mungu” hakuna hata mmoja anaye elewa juu ya uovu wake. Kwa maneno mengine, hakuna anaye elewa kwamba yeye ndiye utakaye kwenda jehanamu. Mwenye dhambi haelewi hata kidogo kwamba yeye ni mwovu. Mwenye dhambi huishi huku haelewi kabisa na bayana kwamba atakwenda motoni kwa sababu ya dhambi zake. Mtu hujaribu kupokea wokovu toka dhambini kwa kuelewa kwamba anastahili kwenda jehanamu kwa sababu ya dhambi zake. Hata hivyo hakuna hata mmoja anaye elewa asili ya nafsi yake yenye dhambi mbele ya Mungu au hatima yake kwenda jehanamu.
Je, sisi ni viumbe tulio wa thamani au la, mbele ya Mungu? Wanadamu wote hawana thamani hadi pale watakapo zaliwa upya mara ya pili. Ingawa sote kwa fadhila zake tume kuwa wenye haki, je, hapo mwanzo hatukuwa tukimpinga Mungu huku tukikataa kuamini ukweli na hata kufikia kumtwika lawama?
Sasa ni kwa vipi mwenye dhambi aweza kumtukuza Mungu? Ni kwa jinsi gani mwenye dhambi ambaye hajaweza kusuluhisha tatizo lake la dhambi atakavyoweza kumtukuza na kumsifu Mungu? Kumtolea shangwe Mungu katika hali ya dhambi hakuwezi kuwa ni sifa ya kweli. Kwa uwezekano gani mwenye dhambi aweza kumsifu Mungu? Mwenye dhambi kamwe hatoweza kumtukuza Mungu na pia Mungu hakubali chochote toka kwa mtu aina hii.
Siku hizi huduma za kusifu zimetapakaa mahala pote ulimwenguni. Hata hivyo ni kwa wale tu wanaoamini haki ya Mungu ndiyo watakao weza kumsifu Mungu. Je, unadhani kwamba Mungu aweza kuridhika na wenye dhambi kumsifu? Sifa za wenye dhambi ni sawa na sadaka ya Kaini. Kwa nini Mungu hakubali sifa isiyo na maana toka mioyo ya wenye dhambi?
Mstari wa 12 unatamka kwamba “Wote wamepotoka wameoza wote pia, hakuna mtenda wema, la! Hata mmoja.” Wote wamepotoka hawaijui kazi kuu Mungu aliyo wafanyia na hawamwamini yeye au Neno la kweli. Zaidi ya yote, wenye dhambi hawalikubali neno la Mungu au kuliamini bali wamejikita zaidi na mambo ya mwili katika fikra zao. Hivyo hawawezi kutofautisha kati aya jema na baya mbele ya Mungu.
Hukumu sahihi inawezekana kwa maneno ya kweli yenye haki ya Mungu. Uamuzi mzuri na sahihi wa hukumu waweza kufanyika ndani ya haki ya Mungu. Yakupasa ujue kwamba hukumu zote za kisheria hazitokani na wanadamu bali na ndani ya haki ya Mungu. Fikra za kibinadamu zimepotoka na kuweka kando haki ya Mungu. Watu husema “Nafikiri hivi na kuamini kwa kulingana na mawazo yangu bila kujali Biblia ina zungumziaje juu ya hilo.” Lakini natumainai utagundua kwamba yule asiye achana na fikra zake kwa namna hii ndiye hasa anaye kataa haki ya Mungu kwa sababu ya fikra za kikaidi zenye ubinafsi. Kwahiyo, kuwaza kwa jinsi hii hakutomwezesha kuirudia haki ya Mungu.
 

Akili ya kimwili hupelekea roho ya mtu mautini.
 
Yule ambaye hajazaliwa upya mara ya pili ndiye ahukumuye. Aina hii ya watu hakika hawajali juu ya kilichoandikwa katika maneno ya Mungu, badala yeke ikitokea jambo kwenda kinyume na fikra zao, husema kuwa si sahihi na hivyo kukubali yale yaliyo nje ya maneno ya Mungu yenye kuendana na fikra zao na ubinafsi wao. Ikiwa mtu anatumaini kukombolewa toka dhambini kwa njia iliyo sahihi basi anahitaji haki na sheria ya Mungu. Sasa basi ni ipi sheria ya Mungu?
Sheria ya Mungu ni haki yake na inakupasa kujua kwamba neno la Mungu ni kipimio cha sheria ya haki ya Mungu. “Hapo mwanzo kulikuwako Neno naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1). Nafsi hii ni nani iliyoitwa “Neno?” Nafsi hii ni nani aliye kuwako kwa Mungu Baba na Roho Mtakatifu? Ni Mwokozi wetu Yesu Kristo. Yesu Kriso alikuwa ni Mwokozi na Mfalme wa wafalme. Yesu ni Mungu.
Inanenwa katika Yohana kwamba palikuwako na Neno hapo mwanzo naye, Neno alikuwako kwa Mungu ni chapa ya nafsi yake (Waebrania 1:3). Mwokozi ndiye Mungu kwa hiyo, kwa sababu Neno ndiye Mungu mwenyewe. Maneno yake ya haki ni tofauti na fikra za wanadamu. Yakupasa ugundue kwamba wenye dhambi huthubutu kuielewa haki ya Mungu kwa njia ya mtazamo wao huku wakiwa hawaijui haki ya Mungu. Yule asimamaye kidete kwa imani katika haki ya Mungu anafaidika na kutumiwa vyema na Mungu. Yule anaye simama imara na kuyashika maneno ya Mungu ndiye mtu wa imani na ni mwenye faida mbele ya Mungu. Aina hii ya mtu huwa amebarikiwa pia.
Watu wote kila mara hukinzana na Mungu kwa fikra zao. Yakupasa ujue kwamba anayejitia kuwa ni mtakatifu na mwema, au kujifanya mkarimu na mwenye rehema kwa wengine, yote haya ni matendo ya kinafiki yenye kutokana na mawazo na fikra zenye kumlaghai Mungu. Kujifanya kuwa mwema ni kinyume na Mungu hakuna aliye mwema zaidi ya Mungu. Ikiwa Mkristo hakubali upendo wa Mungu alio ukamilisha na haki ya wokovu wake pasipo kuzaliwa upya mara ya pili, ni kinyume na Mungu na ukaidi katika kweli.
Je, unadhani kwamba ni wale tu wanao tenda dhambi kubwa ulimwenguni ndiyo watakao pokea adhabu ya Mungu? Wale wote wasio iamini haki ya Mungu hawato salimika na hasira ya Mungu.
Mtu asiye mwamini Yesu kwa usahihi amejawa na mtazamo wa haraka akidhani ataweza kuishi maisha mazuri. Ni nani aliye wafundisha mawazo haya? Ni shetani ndiye aliyewafundisha. Hata hivyo wanadamu hawana uwezo wa kuishi maisha ya uadilifu toka kuzaliwa. Hivyo, neno la Mungu latuambia kwamba yatupasa kupokea ondoleo la dhambi. Je, hii inamaana kwamba yatupasaa tutende maovu kwa nia ya rehema iongezeke? Bila shaka sivyo. Kwa kuwa wanadamu wameambukizwa dhambi toka siku waliyo zaliwa hatima yao ni jehanamu kutokana na majeraha ya dhambi ya kuambukizwa. Kwa hiyo Mungu amewaambia wapokee ondoleo la dhambi ambalo Yesu alikwisha litayarisha kwa ajili yao. Yeye ndiye Mungu wa wokovu na kutushauri sisi sote kupokea wokovu kwa kulikubali neno la haki yeke, ambalo ni kweli, mioyoni mwetu.
 

Mwanadamu ni nani kwa asili?
 
Mstari wa 13-18 unatamka, “Koo lao ni kaburi wazi kwa ndimi zao wametumi kila sumu ya fira chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao ina mbio kumwaga damu. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao wala njia ya amani hawa kuijua. Kumcha Mungu hakupo machoni pao.”
“Kwa ndimi zao wametumia hila.” Ni kwa kiasi gani wametumia hila! Katika Yohana iliandikwa “asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe” (Yohana 8:44). Utasikia mtu akisema, “nakwambia kweli, huu ni ukweli. Unanielewa?” Maneno yote ya mtu asiye zaliwa upya mara ya pili husisitiza kuwa ni ya kweli mara zote huwa ni ya uongo.
Mtu ambaye hajazaliwa upya mara ya pili hawezi kujizuia kusema uongo kila anapo zungumza na watu. Husisitiza yale yote anayoongea kuwa ni kweli, lakii si ukweli halishi, kwani hulaghai watu kila anapo sema kuwa ni kweli. Kila mambo anayoyasema mtu ambaye hajazaliwa upya mara ya pili ni ya ulaghai kwa sababu haiamini haki ya Mungu.
Walaghai hawakosei baada ya kuwaeleza watu kuwa kile wafanyacho ni hujuma. Huzungumza kama vile ni halisi. Huzungumza na watu kwa namna ya uhakika na ukweli ili aweze kuwafanya wamwamini “Nawaeleza ukweli, halisi na bayana. Ukiwa utawekeza fedha hapa utavuna kiasi kikubwa. Jaribu kuwekeza kiasi cha milioni na kwa mwaka tu utapata kiasi cha milioni mbili zaidi ya ulicho wekaza. Na kwa miaka miwili ifuatayo, utavuna fedha nyingi sana. Hii ni biashara mpya kabisa na hakika ni salama. Njoo fanya haraka, fikiri na uamue kwa sababu wapo wengi wasubirio nao”. Hivi ndiyo matapeli waongeavyo. Yakupasa ukumbuke kwamba mtu huyu ambaye bado hajapokea msamaha wa dhambi zake anatenda ulaghai kwa ulimi wake.
Biblia yasema kwamba shetani hunena uongo toka kwa yaliyo yake. Kila anacho nena mtu asiye okoka, ni uongo. Si ajabu kwa mhudumu wa kiroho ambaye hajaokoka kulaghai wafuasi wa kanisa kwa kusema wataweza kuwa matajiri ikiwa watashika wadhifa wa kuwa mzee wa kanisa kwa “baraka zisizo zuilika za Mungu. Hivyo watu hujibidisha na kuitafuta uzee wa kanisa na nafasi zake? Ni kwa sababu ya ulaghi wa watumishi wao wa kiroho wenye kudai kwamba Mungu atamjaza mtu na utajiri wa mali pale atakapo shika wadhifa wa nafasi ya uzee wa kanisa. Wapo Wakristo wengi waliopoteza mali zao baada ya kujaribu kutaka nafasi ya uzee wa kanisa. Wamejitolea gharama kubwa kwa watumishi wao walaghai kwa sababu walitamani nafasi hizo katika kanisa.
Hebu natuangalie kwa undani Waruni 3:10 tena Mstari wenye maneno “Kama ilivyoandikwa” unatuashiria kwamba, mstari unaofuatia umenukuliwa toka Agano la Kale. Badala ya kutoa maelezo ya ziada Paulo alinukuu vile vya mstari ulivyo toka chanzoni mwa maandiko. “Maana vinywani mwao hamna uaminifu. Mtima wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, ulimi wao hujipendekeza” (Zaburi 5:9). “Miuguu yao hukimbilia maovu nao hufanya harak kumwaga damu isiyo na hatia, mawazo yao ni mawazo ya uovu, ukiwa na uharibufu zaonekana katika njia kuu zao” (Isaya 59:7). Watu wanao ishia jehanamu kwa kuto jua haki ya Mungu wanasikitisha.
Mstari wa 19 unatamka, “Basi twajua ya kuwa mambo yote inanayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati ili kila kinywa kifumbwe na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu.”
Sheria huleta hukumu (Warumi 4:15). Mungu ameleta sheria kwa wale ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili ili awawezeshe kufahamu kwamba wao ni wenye dhambi. Sheria hufundisha kila mwenye dhambi kwamba hanauwezo wa kuishi kulingana na sheria ya Mungu. Kwa uwazi imeandikwa kwamba Mungu hakutupa sheria ili tuifuate lakini hii haifanyi sheria kubatilika? Hapana, yeye hafanyi hilo. Mungu alisema kwamba aliileta sheria kupitia Musa ili aweze kutufundisha kwamba sisi ni wenye dhambi. Anataka tugundue asili ya dhambi kwa njia ya sheria na hivyo haikuletwa ili kwamba tuifuate. Kazi ya sheria ni kutaja na kubainisha udhaifu na upungufu wa wanadamu.
Hivyo mstari wa 20 unatamka kwamba “Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria kwa maana kutambua dhimbi huja kwa njia ya sheria.” Hakuna mwili utakao hesabiwa haki mbele yake kwa matendo ya sheria. Hakuna aliye wahi kuweza kufuata sheria yote na hakuna atakaye weza kuifuata. Hivyo hitimisho ni kuwa, mtu hatoweza kuwa mwenye haki kwa matendo ya sheria.
Je, twaweza kugeuzwa kuwa watu wenye haki kwa kuifuata sheria? Tunapo tazama vifungu hivi vya maandiko twaweza kiurahisi kudhani kwamba utakatifu kwetu huja hatua kwa hatua hadi kufikia utakaso kamali kwa kuishi maisha mema kupitia matendo yetu baada ya kuwa waumini wa Yesu. Hata hivyo hili si kweli kabisa. Kusema kwamba mtu aweza kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa kutakaswa kupitia awamu kwa awamu hakika hili si kweli.
Wale wote ambao hawajazaliwa upya bado wamo chini ya sheria ya Mungu, yaani “sheria ya dhambi na mauti” (Warumi 8:2). Ni kwa sababu, punde mtu anapo kuwa Mkristo hudhani kwamba imemlazimu kuishi kwa kufuata mandiko ya Mungu katika torati. Wakristo hudhani ni wajibu kufuata sheria kwa matendo yao, lakini kiuhalisi, hawawezi kamwe kufuata sheria zote. Ndiyo maana hujikuta wakifanya sala za toba kila siku. Hawagundui kwamba wanaangukia katika mtego wa kidini usio na matumaini uitwao “dini ya Kikristo”. Hii inathibitisha kwamba kuishi katika aina hii ya maisha ya kidini ni makosa tokea awali. Kujaribu kufuata sheria za Mungu baada ya kutoelewa sheria inayo pelekea Ukristo wa kidini ni makosa makubwa. Wale wenye kushindania na haki kwa sheria, ingawa sheria hiyo ipo kwa ajili ya kutuelekeza kwamba sisi ni wenye dhambi hutenda makosa.
Fundisho la utakaso wa viwango katika awamu ndani ya Ukristo linafanana na fundisho la dini za kipagani katika ulimwengu huu. Fundisho hili ni sawa na lile la dini ya kibudha liitwalo “Nirvana”, (hali ya kuwa na amani na furaha ambayo mtu huifikia baada ya kuachana na tamaa binafsi) ambamo katika Ukristo fundisho la utakaso wa viwango katika awamu hutamka kwamba mwili wa mtu na roho yake hufikia utakatifu zaidi baada ya mtu huyo kumwamini Yesu na hatimaye mtu huyo kuwa mtakatifu vya kutosha kuingia Mbinguni.
Mtu aliyezaliwa na maambukizo ya dhambi aweza kutenda kazi ya kueneza dhambi hiyo maishani mwake pote. Sababu ya hili ni kwa kuwa mtu huyo amekwisha ambukizwa dhambi. Virusi vya dhambi hutoka ndani ya mwili wa mtu huyo hata ikiwa hakudhamiria kueneza dhambi. Ipo tiba moja tu ya ugonjwa huu. Ni kusikiliza na kuamini neno la Injili ya kweli iliyo na haki ya Mungu. Mtu aweza kuokolewa kutokana na dhambi zake zote na hata kupokea uzima wa milele ikiwa atasikia na kuamini maneno ya ondoleo la dhambi, ambalo linatuwezesha kupokea tohara ya kiroho.
Kutawezekana vipi kuwepo mtu katika dunia hii anayeishi maisha yaliyo makamilifu kwa kufuata sheria hata baada ya kuzaliwa upya mara ya pili? La hasha! Hakuna. Biblia inatamka “kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria” (Warumi 3:20). Je, ukweli huu si bayana na rahisi kueleweka? Adamu na Hawa waliacha neno la Mungu kwa kutoamini kwao na hivyo kuanguka dhambini kwa kurubuniwa na shetani katika kipindi kile cha “Nyakati za kutokuwa na hatia” na hatimaye kuirithisha dhambi hiyo kwa kizazi chao baada ya tukio hili. Hata hivyo ingawa wanadamu wote wamerithi dhambi toka kwa wazazi wa kwanza, hawakufahamu kwamba walikuwa wamezaliwa wakiwa wenye dhambi.
Tokea sasa pale kipindi cha Abrahamu, Mungu aliwapa wanadamu ufahamu mkubwa wa juu ya haki yake ili kuwawezesha watu kupokea ondoleo la dhambi kwa kuamini neno la Mungu.
 

Paulo hushuhudia juu ya haki ya Mungu pasipo sheria.
 
Mstari wa 21-22 unatamka “Lakini sasa haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria, inashuhudiwa na torati na manabii ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio maana hakuna tofatu.”
Inasema kwamba haki ya Mungu imedhihirisha yaani “inashuhudiwa na torati na manabii”. Hapa “torati na manabii” ina maanisha Agano la Kale. Sasa, Paulo alizungumzia juu ya Injili ya haki ya Mungu ambayo ilidhihirishwa kwa kupitia mpangilio wa utoaji wa sadaka katika hema ya madhabahu ambapo mtu aliweza kupokea ondoleo la dhambi kupitia sadaka ya dhambi, na imani ya Paulo pia ili husika na imani katika haki ya Mungu ambaye ilidhihirishwa katika maandiko yote.
Paulo aliazimia kwamba yeyote mwenye imani katika Yesu Kristo bila upendeleo ataweza kupokea haki ya Mungu. Kuokolewa au kutookolewa kwa mtu hakika hutegemea imani au kutoamini kwake. Kwa hiyo anasema kwamba, “haki ya Mungu imedhihirishwa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti”.
Imani ya kweli ni ipi? Nani aliye kiini cha imani? Ni yesu Kristo. Waebrani 12:2 inatamka “Tukimtazania Yesu mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu.” Yatupasa kujifunza juu ya ukweli wa Mungu toka kwa wale walio zaliwa upya mara ya pili na kupokea wokovu katika Yesu Kristo kwa kuamini ukweli huo na hatimaye kuishi kwa imani ya maneno ya Mungu. Kuamini haki ya Bwana kwa moyo ni kuwa na imani ya kweli.
Warumi 10:10 inatamka “kwa maana kwa kwamoyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Twaweza kuwa wenye haki kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu kwa mioyo yetu na kuthibitisha wokovu kwa kukiri imani zetu kwa kinywa. Ondoleo la dhambi halitoweza kupatikana kwa matendo yetu, bali kwa imnai zetu katika haki ya Mungu.
Mistari ya 23-25 inatamka “Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupongukiwa na utufkufu wa Mungu wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyesha haki yake kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa”.
Biblia inatamka kwamba “wote wametenda dhambi na kupungukiwa utukufu wa Mungu.” Wenye dhambi hawana uchaguzi zaidi ya jehanamu, hata hivyo kupitia ukombozi ambao ndiye Kristo Yesu na haki Mungu, watu wamepokea ondoleo la dhambi bure. Watu hawana dhambi tena kwa sababu wanaiamini haki ya Mungu. Yesu kawa kipatanisho kwa damu yake kupitia imani.
Tunapo tazama mistari ya 25-26 imeandikwa “ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyesha haki yake kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa”.
Hapa usemi “ili aonyeshe haki yake” una maanisha haki ya Mungu iliyo kamilishwa kwa tendo la ustahimili alilotenda Yesu Kristo. Sababu ya Yesu kumwaga damu msalabani ilikuwa kwamba, kabla ya kifo chake ilimpasa kuitimiza haki yote ya Mungu kwa kubatizwa na Yohana katika Mto Yordani (Mathoyo 3:13-17). Mungu baba alimfanya Yesu awe sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi za dunia hii ili kwamba alete amani kati ya wanadamu naye. Yesu Kristo aligeuzwa kuwa haki ya Mungu.
Yesu alibeba dhambi zote za dunia kwa kupokea ubatizo wa Yohana. Yesu alikuwa ni alfa na omega. Hii maana yake kwamba kila mmoja atawezakupokea wokovu toka dhambini ikiwa ataamini maneno yenye kutamka kwamba, Bwana alifuta dhambi zote za dunia tokea mwanzo hadi mwisho wa dunia.
Haki ya Mungu amabayo Yesu aliyoitimiza inatuwezesha kuwa na amani na Mungu. Ilifanyika ili kwamba ni kwa mtu yule atakaye kuwa na amani na Mungu ndiye pekee atakaye ingia Mbinguni. Binafsi, ni pale nilipo anza kuamini Injili ya kweli ndipo nilipo elewa maandiko yasemayo “Mungu amekwisha kumwekea awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa” hivyo kuamini haki ya Mungu kupitia Yesu.
Haki ya Mungu ilikamilishwa wakati ulio pita ambapo huonyesha kwamba tayari imekwisha kamilishwa. Twapokea ondoleo la dhmbi kwa imani ya neno la kweli lisemalo kwamba, Yesu aliondolea mbali dhambi zote kwa ubatizo wake na damu yake. Ingawa roho zetu zimekwisha samehewa dhambi mara moja zote, miili yetu bado haito jizuia kutenda dhambi. Mungu anamaana dhambi iliyo tendwa wakati uliopo hapa ulimwenguni kuwa hizi “ni dhambi zote zilizo tangulia kufanywa”.
Kwa nini? Mungu aliuweka ubatizo wa Yesu kuwa ndiyo sehemu ya kwanza ya wokovu. Hivyo ndivyo ambavyo ondoleo la dhambi lilivyo kamilishwa mara moja kwa njia ya haki ya Mungu, ambapo Yesu Kristo ndiye aliye alikamilisha. Dhambi tuzitendazo kwa miili katika wakati huu ni dhambi zilizo ondolewa kupitia ubatizo wa Yesu kwa mtazomo wa Mungu. Dhambi zote za dunia zimekwisha semehewa mbeli ya Mungu. “Kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa” maana yake ni “kuchukulia kwamba mshahara wa dhmbi umekwisha lipwa.” Dhambi zote za dunia ni dhambi zote za wanadamu toka mwazo wa ulimwengu hadi mwisho wake, toka Adamu hadi siku ya mwisho wa dunia. 
Pia ni dhambi za watu wazitendazo sasa na dhambi zilizotangulia kutendwa”, ambazo Yesu alikwisha ziondoa hapo nyuma. Wale waaminio haki ya Mungu hawana tena dhambi. Ukweli huu ni kwamba, dhambi zilizokwisha tendwa tayari zimekwisha twikwa kwake. Hata dhambi tuzitendazo katika muda huu nazo pia ni mojawapo za dhambi zlizokwishatangulia kufanywa na kusamehewa mbele ya Mungu. Watu wa dunia hii hutenda dhambi ambazo tayari zilikwisha kuondolewa na Mwana wa Mungu aliye letwa ulimwenguni ni ili kubeba dhambi za dunia. Dhambi tuzitendazo sasa hivi ni zile zilizo kwisha futwa. Je, unaelewa maana ya hili?
Yesu alisema, tayari amekwisha ondoa dhambi za dunia kwa njia ya haki ya Mungu. Mtu anaweza asielewe vyema juu ya hili ikiwa hataelewa kwa undani maana ya kifungu hiki. Kwa mtazamo wa Bwana, dhambi tuzitendazo sisi wanadamu ni zile zilizo kwisha kuhukumiwa toka pale yeye alipo batizwa mto Yordani na kuhukumiwa msalabani. Sababu Mungu kutuambia tusiwe na wasi wasi juu ya dhambi ni kwa kuwa Yesu alikuja ulimwenguni na kuwafanya watu kuwa wenye utakaso kamili mara moja na kwa wakati wote.
Ukweli huu ambao Paulo anauzungumiza katika kifungu hiki ni muhimu sana kwa yule aliye okolewa kwa kuamini haki ya Mungu. Hata hivyo, watu ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili huidharau haki ya Mungu na hatimaye watakwenda jehanamu. Ndugu zangu yakupasa usikilize na kuelewa vyema neno la Mungu. Ndipo hapo itakapo kuwa vyema katika kustawi kwa imani yako na katika kuihubiri Injili kwa wengine. Je, wajua kwamba Mungu huuhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu yake? (Yohana 16:8). 
Mungu alimfanya Yesu kuwa kipatanisho kwa njia ya damu yake kwa imani, ili kuonyesha haki yake kwa sababu ya uvumilivu wake. Mungu alimtwika Yesu dhambi zilizokwisha tendwa. Kwa kuwa Mungu alimweka Yesu kuwa kipatanisho, anatufundisha kwamba dhambi zote zimekwisha kuondolewa. Hivyo basi tunakuwa wenye haki kwa kuamini haki ya Mungu.
Katika mstari wa 26 imeandikwa, “apate kuonyesha haki yake wakati huu ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminie Yesu”. Wakati huu Mungu ametuwezesha kuwa na uzima wa milele, na haitaji kuuhukumu ulimwengu. “Wakati huu” alipo mtuma Yesu Kristo “apate kuonyesha haki yake.” Bwana alionyesha haki ya Mungu kwa ubatizo na damu yake. Mungu alimfanya Mwana wake wa pekee kubatizwa na kusulubiwa na hatimaye kuonyesha kwetu upendo wake na haki yake.
Mungu aliitimiza haki yake kwa njia ya Yesu. Kila anaye amini haki ya Mungu ni mwenye haki. Mungu wetu alitimiza kitendo cha haki katika kufuta dhambi zote za dunia mara moja na kwa wakati wote. Je, twaweza sasa kuiamini haki ya Mungu kwa mioyo yetu? Mungu anasema kwamba sisi ni wenye haki na tusio na dhambi pale tunapo amini haki yake. Kwa nini? Je, wanao mwamini Yesu hawana dhambi kwa kuwa amekwisha tenda tendo la haki katika kutakasa dhambi zao? Anaye amini haki ya Mungu ni mwenye haki, Bwana amekwisha futa dhambi zote tutendazo maishani mwetu pote, hivyo tuna uwezo wa kuamini haki ya Mungu. Kwa njia nyingine tusingeweza kamwe kupokea haki ya Mungu.
 

Ni hakiya Mungu pekee ndiyo yakujisifia.
 
Mstari wa 27-31 unatamka, “Ku wapi, basi, kujisifu kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani. Basi twaona ya kuwa mwanadamu kuhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. Au je! Mungu ni Mungu kwa Wayahudi tu? Siye Mungu ya Mataifa pia? Mungu ni mmoja atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani nao wale wasio tahiriwa watahesabiwa haki kwa njia ya imani iyo hiyo. Basi je? twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.”
Kuithibitisha sheria maana yake ni kwamba hatutoweza kuokolewa toka dhambini kwa matendo yetu. Sisi ni dhaifu na tusio viumbe wakamilifu, lakini haki ya Mungu ndiyo iliyotufanya kuwa wakamilifu kwa neno lake. Kwa kuamini neno la haki ya Mungu ndiko kuliko tuokoa. Hata baada ya kuokolewa toka dhambini, Bwana wetu anaendelea kunena nasi akisema “Wewe si mkamilifu lakini nimekutakasa. Hivyo yakupasa uwe karibu na Mungu kwa haki yake”.
Katika mstari wa 27 imeandikwa “Ku wapi basi kujisifu? La! Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! bali kwa sheria ya imani.” Mtu imempasa kuelewa sheria ya haki ya Mungu ambayo Mungu ameiweka na hivyo kuamini sheria ya haki yake. “Kwa sheria ya namba gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani.”
Yakupasa ujuwe ya kwamba tulikombolewa toka dhambini pale tu tulipo amini haki ya Mungu, hivyo hatuto weza kukombolewa kwa matendo yetu. Paulo Mtume amnasema, “Je, kutoamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Hasha!” Anaye amini haki ya Mungu atasimama imara, lakini yule asiye amini ataanguka.
Warumi sura ya 3 inadhihirisha haki ya Mungu kwa uwazi. Yakupasa uelewe kwamba, Mungu amedhihirisha sheria ya haki yake ili kuwawezesha wale wanaoazimini fikra zao binafsi kuanguka. Mungu ametuokoa kikamilifu kutokana na dhambi zetu zote. Hivyo twaweza kuokolewa toka dhambini kwa kuamini Neno lake linalo dhihirisha haki yake. Twaweza kuurithi ule Ufalme wa Mungu na kuwa na amani naye kwa kuamini haki yake.
Wale wote wasio amini haki ya Mungu hawatoweza kuwa na amani moyoni mwao. Swala la mtu kubarikiwa au kulaaniwa hutegemea ikiwa anaiamini haki ya Mungu au la. Ikiwa mtu hachukulii maneno ya haki ya Mungu, basi atahukumiwa kulingana na sheria ya hukumu ya maneno ya Mungu. Wokovu asili yake ni upendo wa Mungu, na hivyo tunaupokea kwa ajili ya dhambi zetu kwa kuamini haki ya Mungu. Tumshukuru Bwana aliyetupatia imani hii ya haki ya Mungu. Tumshukuru kwa kuwa tunaimani sawa na ile ya Paulo Mtume! Tumsifu Bwana.
Pia tunamsifu na kumpa shukrani na kumpa shukrani yeye kwa kuwa tumekombolewa toka dhambini kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Kama isingekuwa wokovu huu, imani na kanisa la Mungu, tusingeliweza kamwe kupokea ondoleo la dhambi. Kwa hakika tuna iamini haki ya Mungu kwa moyo, na kukiri wokovu kwa kinywa. Tunampa shukrani Mungu aliyetuokoa kutokana na dhambi zetu zote kwa njia ya Haki yake.