Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 2-3] Tohara ni ya Moyo (Warumi 2:17-29)

(Warumi 2:17-29)
“Lakini wewe, ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea torati na kujisifu katika Mungu na kuyajua mapenzi yake na kuyakubali mambo yaliyo bora, nawe umeelimishwa katika torati na kujua hakika ya kuwa wewe mwenyewe u kiongozi wa vipofu mwanga wa walio gizani mkufunzi wa wajinga walimu wa watoto wachanga, mwenye namna ya maarifa na ya kweli katika torati basi wewe umfundishaye mwingine je, hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubirie kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe? Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe ujisifuye katika torati mnamvunjia Mungu heshima kwa kuasi torati? Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyo andikwa. Kwa maana kutahiriwa kwa faa kama ikiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutotahiriwa. Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa kuyashika maagizo ya torati je, kutokutahiriwa kwake hakutohesabiwa kuwa kutahiriwa ukaihalifu torati? Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu wale torati siyo ile ya nje tu katika mwili bali yeye ni Myahudi aliye myahudi kwa ndani na tohara ni ya moyo, katika roho si katika andiko ambayo sifa yeke haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.”
 

Yatupasa kutahiriwa moyoni.
 
“Tohara ni ya moyo.” Tunaokolewa pale tunapo amini kwa moyo. Yatupasa kuokolewa moyoni. Mungu anasema “tohara ni ya moyo katika roho si katika andiko ambayo sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu” (Warumi 2:29). Yatupasa kuwa na ondoleo la dhambi. Ikiwa hatutokuwa nalo mioyoni mwetu basi ni bure tu. Mwanadamu ana “utu wa ndani” “na utu wa nje” na kila mtu inamlazimu kupokea ondoleo la dhambi ndani ya utu wake.
Mtume Paulo anawaambia Wayahudi “tohara ni moyo.” Sasa basi Wayahudi walikuwa wakitahiriwa sehemu gani? Wao walikuwa wakitahiriwa sehemu ya mwili. Hata hivyo Mtume Paulo alisema “tohara ni ya moyo.” Wayahudi walikuwa wakitahiriwa “utu wa nje” lakini Paulo aliwaambia kwamba tohara ni ya moyo. Leo hii Mungu anatuambia nasi kwamba tohara ni ya moyo pale tunapokuwa watoto wake.
Paulo hakua akizungumzia tohara ya nje bali tohara na ondeleo la dhambi katika moyo. Hivyo basi aliposema kwamba “ni ni basi ikiwa baadhi yao hawakuamini?” (Warumi 3:3) alimaanisha kwamba “ni nini ikiwa basi baadhi hawatoamini moyoni?” hakuwa akizungumzia juu ya kuamini kwa nje, bali alisema “amini ndani ya moyo.” Yatupasa kujua kile Paulo Mtume alichokua akimaanisha na ni nini maana ya ondoleo la dhambi. Yatupasa pia kujifunza namna ya kupata ondoleo la dhambi moyoni mwetu kupitia neno la Mungu.
“Ni nini basi ikiwa baadhi yao hawakuamini?” Maana yake “Ni kwa vipi basi ikiwa Wayahudi hawakuamini juu ya Yesu Kristo kama Mwokozi, je, kutokuamini kwao kutafanya uaminifu wa Mungu kutokuwa na maana?” Je, ukweli wa Mungu kufuta dhambi zote pamoja na dhambi za kizazi cha Abrahamu utakuwa ni bure? Kamwe Paulo anasema kwamba hata Wayahudi ambao nao ni uzao wa Abrahamu kwa mwili wataweza kuokolewa pale watakapo amini kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi, Mwana wa Mungu aliye beba dhambi zote za dunia kwa njia ya ubatizo na kusulubiwa. Pia anasema kwamba wokovu na neema ya Mungu kupitia Yesu Kristo hautoweza kamwe kubatilika.
Warumi 3:3-4 inatamka. “Ni nini, basi ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je, kutokuamini kwao kuta ubatili uaminifu wa Mungu? Hasha. Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo, kama ailivyo andikwa, ili ujulikane kuwa una haki katika maneno yako, ukashinde uingiapo katika hukumu.” Bwana alikwisha toa ahadi kwa neno lake na kutakasa wale wote waaminio kwa kuhitimisha ahadi hiyo mwenyewe. Mungu anataka kuonyesha haki yake na kuwapatia haki hiyo wale wote wenye imani katika Yesu kwa njia ya neno lake, na kwa kukamilisha kile alichao ahidi pale anapo taka kuja kuhukumu. Hata sisi tulio na ondoleo la dhambi mioyoni mwetu, pia tunapaswa kuhukumiwa na neno lake na kuishinda hukumu hiyo kwa neno hilo hilo katika siku hiyo ya hukumu.
 

Mtume Paulo anazungumzia juu ya utu wa nje na wandani.
 
Paulo anazungumzia juu ya “utu wake wa nje na ndani”. Sisi nasi tuna utu wa nje na ndani ambapo ni mwili na roho. Tunafanana naye. Hivyo Paulo anashughlika na mambo haya.
Warumi 3:5 inasema, “lakini ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu tuseme nini?” Hapa Paulo hamaanishi kwamba “utu wa ndani” ni safi. Mwili wake ni mchafu na kuendelea kutenda dhambi hadi siku ile ya kifo chake. Pamoja na watu wote duniani hili ndivyo ilivyo. Hata hivyo ikiwa Mungu alikwisha kuokoa watu wote, je, haitothibitisha haki ya Mungu? Je, Mungu si wa haki ikiwa amekwisha okoa wanadamu wote, ingawa utu wao wa nje ni dhaifu? Hivyo Paulo alisema “Lakini ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu tuseme nini? Je Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu) Hasha kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu?” (Warumi 3:5-6). Paulo anafafanua kwamba hatujaokolewa kwa sababu tu utu wetu wa nje ni safi.
Tuna utu wa nje na ndani. Hata hivyo Paulo anashughulika na eneo la moyo, akisema, “nini basi ikiwa baadhi yao hawakuamini?” Tohara ni ya moyo. Si imani ya kweli ikiwa tutaweza kuwa watu wa haki mara moja na baadaye kuwa watu wenye dhambi siku inayofuata kwa kuanzisha imani yetu katika msingi wa utu wa nje ambao hutenda dhambi na wenye udhaifu mwingi kila mara.
 

Utu wa nje hutenda dhambi hadi siku ya mwisho kifoni.
 
Mtume Paulo hukuweka matumaini yake katika utu wake wa nje. Wale ambao dhambi zao zimekwisha futwa wana utu wa ndani na wa nje. Wanajisikiaje pale wanapo uona utu wao wa nje? Hawawezi kuacha kukata tamaa. Hebu tuangalie utu wetu wa nje. Wakati mwingine tu wema lakini wakati mwingine tunakuwa wapotofu. Lakini biblia inasema kwamba, utu wetu wa nje ulikufa na Yesu Kristo, yeye alisamehe dhambi zetu zote katika utu wa nje.
Sisi tulio okolewa mara kwa mara tunakata tamaa kwa utu wetu wa nje pale tunapo angalia jinsi tulivyo kwa nje. Tunakuwa na matumaini pale utu wa nje unapofanya mema, lakini mara tunakata tamaa pale tunapo shindwa kukidhi matarajio ya utu wa nje. Tunajaribu kudhani kwamba imani zetu ni mbovu pale tunapo kata tamaa na hali zetu za nje. Hata hivyo hivi sivyo ilivyo. Utu wetu wa nje tayari ulikwisha sulubiwa na Yesu Kristo. Wale wote walio na ondoleo la dhambi nao pia huendelea kutenda dhambi kwa miili yao huku wakiwa na ondoleo la dhambi. Lakini je, hizi si dhambi? Ndiyo ni dhambi, lakini ni dhambi zilizo kufa (matendo mafu) Zimekufa kwa sababu dhambi zote zilibebwa hadi msalabani na Bwana. Dhambi ambazo utu wa nje hutenda si tatizo kubwa sana, ingawa ni jambo la hatari zaidi pale mioyo yetu isipokuwa sawa mbele ya Bwana.
 

Yatupasa kumwamini Mungu kwa Moyo wetu wote.
 
Uovu zaidi unajitokeza ndani ya mwenye haki punde tu anapo pokea ondoleo la dhambi. Hivyo wokovu wa Mungu utakuwa batili ikiwa tutaweka msingi wa wokovu huo katika utu wa nje ambao hauwezi kuacha kutenda dhambi wakati wote. Imani zetu zitaweza kwenda mbali na imani katika Mungu, ambayo Abrahamu alikuwa nayo ikiwa tutaweka imani zetu katika msingi wa matendo ya utu wa nje.
Mtume Paulo anasema “tohara ni ya moyo.” Tunatakaswa na kuwa wenye haki kwa kuamini moyoni. Hili halitegemei ikiwa kama utu wa nje unaweza kutenda Mungu atakayo au la. Je, unaelewa hili? Tatizo ni kwamba, tuna vyote viwili utu wa nje na ndani vinavyo pingana mara kwa mara.Hivyo wakati mwingine tunajaribu kutegemea zaidi ule wa nje. Tunakuwa wenye uhakika pale utu wetu wa nje unapo kuwa safi, lakini tunakata tamaa ukiwa kinyume. Paulo anasema kwamba hii si imani sahihi.
“Tohara ni ya moyo” Ukweli hasa ni upi? Tunajuaje na kuamini kwa moyo? Katika Mathayo 16 Yesu alimuuliza Petro “Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?” Ndipo Petro alipo kiri imani yake kwa kujibu, “Wewe ndiwe Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.” Petro aliamini kwa namna hiyo ndani ya moyo wake. Yesu akamjibu “heri wewe Simoni Bar-yona, kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.” Yesu alitamka kwamba imani ya Petro ilikuwa ni sahihi.
Abrahamu hakuwa na mtoto. Mungu alimwamuru kwa neno lake na kutoa ahadi kwake kwamba atampatia mwana na atakuwa ni baba wa mataika mengi. Pia akasema kwamba Mungu atakuwa ni Mungu kwake na kizazi chake hata baada yake. Mungu alimwagiza Abrahamu, familia yake na kizazi chake kitahiriwe kama ishara ya Agano kati ya Mungu na Abrahamu. “Kovu la kukatwa kwa sehemu ya mwili ni agano la kwamba mimi ni Mungu kwako, asema Mungu.” Abrahamu aliamini Agano hili kwa moyo wake wote. Aliamini kwamba Mungu atakuwa ni Mungu kwake na kumbariki moyo wake. Pi aliamini kwamba Mungu atakuwa ni Mungu kwa kizazi chake hata baada yake. Alimwamini Mungu pekee.
 

Tunafanywa kuwa wenye haki kwa kuamini Injili ya maji na Roho kwa Moyo.
 
Tunafanywa kuwa wenye haki kwa kuamini kwa mioyo yetu kwamba Mungu wetu ndiye Mwokozi wetu. Tunaokolewa kwa kuamini kwa mioyo yetu. Hatuokolewi kwa namna nyingine yeyote. Tunakuwa wenye haki kwa kuamini kwa mioyo yetu kwamba Mungu ndiye Mungu wetu na alifuta dhambi zetu zote kwa ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani. Kwa kuamini kwa mioyo yetu ndiko kunako tuokoa sisi. Hivyo biblia inasema, “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa kukiri hata kupata wokovu” (Warumi 10:10). Mtume Paulo katika hili alikuwa akitenganisha utu wa nje na utu wa ndani.
Tunachopaswa kuweka wazi wakati huu ni kwamba tumefanywa waadilifu kwa kuamini kwa mioyo yetu, na sio kwa matendo mema ya miili yetu. Hatungekuwa waadilifu ikiwa Yesu angeunganisha masharti kwa nafsi zetu za nje, akisema, “Nitaifuta dhambi zako zote, lakini kwa sharti moja. unaweza kuwa mtoto wangu ikiwa utaepuka kufanya dhambi. Huwezi kuwa mtoto wangu ikiwa utashindwa kufanya hivyo.”
Tumefanywa wenye haki kwa kuamini na mioyo yetu. Je! Tungeweza kufanywa waadilifu kama Mungu angeweka masharti kwa mwanadamu wetu wa nje? Je! unaamini ya kuwa Mungu alikuokoa kwa kuondoa dhambi zako kupitia Ubatizo wake katika Mto Yordani, akasulubiwa na kuhukumiwa mahali pako? Je! Unaaminije hii? Je! Huamini na moyo wako? ungekuwa umeokolewa kikamilifu ikiwa Mungu angesema, “nitasamehe udhaifu wako mdogo lakini sitasamehe zile kubwa. Nitafanya uokoaji wako kuwa halali ikiwa utashindwa kutunza hali hii”?
 

Lazima tutenganishe mtu wa nje na mtu wa ndani
 
miili yetu, mtu wa nje, ni dhaifu kila wakati na haiwezi kufikia haki ya Mungu peke yake. Tumefanywa wenye haki kwa kuamini na mioyo mbele za Mungu kwa sababu Aliahidi kuwaokoa wale wanaoamini kwa mioyo yao. Kuona imani yetu kwamba tunakubali yale Mungu alifanya na kwamba Yesu aliondoa na kufuta dhambi zetu zote kwa moyo, Mungu anatufanya tuwe watoto wake waadilifu. Ni agano la Mungu, na alituokoa kwa kutimiza ahadi yake.
Mungu anasema kwamba wakati anaona imani mioyoni mwetu, sisi ni watu wake. lazima tutengane na mtu wetu wa nje na mtu wetu wa ndani. Hakuna mtu ulimwenguni angepokea ondoleo la dhambi ikiwa tutaweka alama yetu ya wokovu kwenye matendo yetu ya mwili wa nje. “Kutahiriwa ni ile ya moyo.” Tumeokolewa kwa kumwamini Yesu Kristo na mioyo yetu. Je! Unaelewa hii? “Kwa maana kwa moyo mtu huamini kwa haki, na kwa kukiri kwa kinywa hufanywa wokovu” (Warumi 10:10). Kwa kawaida mtume Paulo anamtenganisha mtu wa nje na mtu wa ndani.
Utu wa nje ni mchafu kuliko hata kinyesi cha mbwa. Hauna thamani. Twahitaji kumtumia Abrahamu kama mfano. Jiangalie mwenyewe. Angalia mwili wako usivyo na thamani. Mwili hupendelea ujanja wa kujipatia nafasi ya juu katika jamii na kuishi kwa sifa. Je, mwili haufanyi chochote isipokuwa kutafuta yaliyo yake? Mwili utahukumiwa zaidi ya mara kumi na mbili kwa siku kama ingelikuwa kuhukumiwa kwa jinsi ufikiriavyo na utendavyo. Mwili huenda kinyume na Mungu wakati wote.
Kwa bahati mbaya Mungu hajali sana kuhusiana na utu wa nje bali yeye huwa makini kwa utu wa ndani tu. Anatuokoa pale anapo tuona kwamba hakika tunamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wetu kwa mioyo yetu. Anatuambia kwamba alituokoa kwa dhambi zetu zote.
 

Hatuto weza kuokolewa kwa kupitia mawazo yetu.
 
Hebu tuyaone mawazo yetu yalivyo. Tunadhani kwamba tunaweza kuamini kwa fikra zetu. Tunaweza kuamini kwa fikra zetu za kimwili tukisema “niliokolewa kwa sababu Mungu ndiye aliye fanya hivyo.” Hata hivyo bado hatutoweza kuokolewa kwa fikra zetu. Fikra za kimwili hubadilika mara zote na kila mara hupelekea uovu. Je, hii si kweli? Mawazo ya kimwili hupendelea kutenda hili na lile kutokana na tamaa zake.
Mfano pale mtu anapoweka imani yake katika msingi wa fikra zake, anaweza kuwa na uhakika na wokovu wake pale fikra hizo zinapoendana na zile za hapo nyuma ambazo ni, “Yesu alizichukua dhambi zangu zote katika mto Yordani.” Ingawa kwa sababu ya fikra za kimwili hujitokeza, si imara zote mtu huyo ataweza kuwa na uhakika na wokovu wake pindi panapo jitokeza wasi wasi kidogo katika wokovu. Imani iliyo jengwa katika msingi usio sahihi wa mawazo ya mwili huanguka kwa kipigo cha wasiwasi huo.
Hakika hatutoweza kumwamini Mungu na ukweli ikiwa tutaweka msingi wa imani zetu katika mawazo yetu. Imani hii ni mfano wa nyumba iliyo jengwa juu ya mchanga “Mvua ikanyesha mafuriko yakaja pepo zikavuma zikaipiga nyumba ile ikaanguka, nalo anguko lake likawa kubwa”          (Mathoyo 7:27).
Hivyo basi imani ya mtu anayeamini kwa kupitia fikra zake ni mbali na imani iliyo katika msingi wa neno la Mungu. Mungu alisema “Ili ujulikane kuwa una una haki katika maneno yako ukashinde uingiapo katika hukumu” (Warumi 3:4). Wokovu wetu uwe katika msingi wa neno lake. Neno likawa mwili na kuishi kati yetu na Mungu ndiye neno. Neno lilikuja duniani kati yetu kwa mfano wa mwanadamu. Yesu alibatizwa na alituokoa baada ya kutimiza umri wa miaka 33 duniani, na kuwaelekeza Mitume wake kuandika neno la ahadi ambalo ni utimilifu wa Agano la Kale, ambalo alikwisha waeleza watumishi wake hapo awali. Mungu aliandika kile alicho sema na kutekeleza katika Biblia. Mungu alijitokeza ndani yake na kwa Neno akinena kwa Neno na kutuokoa kwa Neno hili.
Hatuto weza kuwa na ondoleo sahihi la dhambi kwa kupitia mawazo yetu, huku tukicha kuamini neno la Mungu na kusema “nadhani nimeokoka lakini wakati mwingine ninashaka na wokovu huu.” Hatutoweza kuokolewa kwa fikra kwa sababu mara zote hubadilika na wakati mwingine si za kweli.
Hivyo Mtume Paulo anasema kwamba tohara ni ile ya moyo. Hivyo tunaamini haki ya Mungu kwa moyo. Mioyo yetu inapoamini neno lake, basi moja kwa moja tutashuhudia ahadi Mungu aliyo iweka katika Agano la Kale na kulikamilisha katika Agano Jipya. Mungu alituokoa kwa namna hii katika Agano Jipya, yaani kwa Neno lake. Tumeokolewa na kuwa watoto wa Mungu kwa kuamini maneno yake kwa mioyo yetu.
 

Tuliokolewa toka dhambini kwa kuamini Injili ya maji na Roho kwa moyo.
 
Tumeololewa kwa imani kwa sababu twaweza kukubali juu ya Mungu, lakini fikra zetu za kimwili haziwezi kamwe kumkubali Mungu. Tunakuwa watoto wa Mungu kwa kuamini kwa mioyo yetu, si kwa matendo au fikra za utu wa nje. Ni dhahiri kwamba tunakuwa watoto wa Mungu kwa kuamini neno lake kwa mioyo yetu. Je, wewe nawe unaamini kwa moyo wako? Je, umetahiriwa moyoni mwako? Je, unaamini moyoni mwako kwamba Yesi ni Mwokozi kwako? Yule anayeamini juu ya Mwana wa Mungu anao ushuhuda huo ndani yake. Je, unao ushuhuda na neno ambalo Yesu alituokoa kwa usahihi na si ushuhuda wa kile kilichomtokea mtu mwingine? Je, unaneno la ushuhuda linye kukuletea ondoleo la dhambi? Kuwa na imani ya kweli ndiko kuokolewa kwa imani.
Tunapokea ondoleo la dhambi kwa kuamini neno la Mungu mioyoni mwetu. Hata hivyo mara kwa mara tunakatishwa tamaa pale tunapoiacha imani katika Mungu.Yule asiye elewa kikamilifu ukweli huu, yupo katika hatari ya fikra potofu. Wakristo wengi huweka kipimo cha imani zao katika matendo yao kimwili. Hili ni kosa kubwa. Kamwe tusipime imani zetu katika mwili kwa sababu mwili hauna cho chote. Katika Agano la Kale na Agano Jipya tunaelezwa kamba mtu anafanywa kuwa mwenye haki pale anapo amini neno la Mungu moyoni. Hatuokolewi kwa matendo ya mwili. Hata kama tunatenda mema au la haihusiani na Mungu pamoja na utukufu wake.
Hivyo imani ya kweli maana yake ni kuokolewa kwa kuamini ukweli wa wokovu wa neno la Mungu kwa moyo. Imani zetu ni batili pale mioyo inapo kuwa si sahihi, na pia imani inakuwa sahihi ikiwa mioyo ni sahihi. Tabia mbaya yaweza kuja kwa sababu tu moyo ni dhaifu. Lakini lililomuhimu ni lile la Mungu kuangalia moyo. Mungu huangalia moyo na kuuchunguza. Mungu huangalia endapo moyo ni sahihi au la. Mungu huangalia endapo hakika tunaamini kwa moyo au la. Je, unaelewa hili? Je, wajua kwamba Mungu huangalia mioyo? 
Mungu huchunguza ikiwa kama kweli tuna mwamini Yesu Kristo kwa mioyo yetu, kwa kuangalia mioyoni. Je, unaamini kwa moyo wako? Mungu huchunguza ikiwa kama tunaamini kwa moyo au la. Yeye huangalia mioyoni mwetu. Yatupasa kujichunguza mioyoni mwetu mbele za Mungu.Tohara ni ile ya moyo. Je, unaamini kwa moyo? Mungu huangalia mioyo yetu endapo tunamfuata yeye na kuamini neno lake.
 

Yapo madhehebu ya kidini yawekayo mkazo juu ya muda sahihi wa kuzaliwa upya mara ya pili.
 
Ni muhimu kuwa na ufahamu sahihi wa kile Yesu Kristo alichofanya na kuamini kwa moyo. Yapo madhehebu ya kidini yanayo waambia kaka na dada zetu katika kanisa letu kwamba hawaja okoka. Nasikitikia nafsi zilizoko katika madhehebu hayo ya kidini. Napenda kuwaelewesha na kuwafundisha juu ya Injili ya maji na Roho. Je, dhambi zetu zilifutwa?               —Amina.— Je, unaamini kwa moyo?
Lakini wapo baadhi ya watu wanaosema kwamba imani zetu si sahihi. Husema kwamba yatulazimu kutoamni neno vile lilivyo andikwa na kuamini kile tu kilicho thibitika kisayansi. Husema kwamba wokovu huu ndiyo sahihi na ndiyo imani iliyo sahihi kwa mtu kukumbuka (kwa saa, tarehe, mwezi) ni lini alizaliwa upya mara ya pili. Pale ndugu yetu Hwang alipo kutana na moja kati yao na kumuuliza kaka eti ni siku gani aliyo okoka, hivyo naye akamjibu kwamba hakumbuki kwa uhakika tarehe na saa. Lakini swala muhimu nikuwa ameokoka kwa kuamni Injili ya maji na Roho hapo nyuma. Ndipo akasema kwamba kaka Hwangi hukuwa ameokoka.
Bila shaka tunaweza kujua na kutaja kwa muda, tarehe mwezi shahihi na hata mwaka ikiwa tutajaribu kutafuta katika kumbukumbu zetu. Tunaweza hata kutaja ikiwa niasubuhi au mchana. Hata hivyo wokovu hutegemea kuamini kwa moyo. Haijalishi ikiwa tutaweza kukumbuka muda sahihi au la!
 

Tohara ni ile ya Moyo.
 
Bwana alibeba dhambi zetu zote juu yake pale Mto Yordani na hatimaye kusulubiwa kwa niaba yetu ili kupokea hukumu ya dhambi hizo. Alijeruhiwa kwa uovu wetu na kusulubiwa kwa makosa yetu. Alibeba dhambi zetu zote za utu wa nje na ndani. Roho zetu zilifufuka upya toka kifoni na sasa tunaweza kumfuata Bwana vile atakavyo, ingawa baadhi ya watu wanaweza kutuzushia kwamba hatuja okoka. 
Biblia inasemaje juu ya utu wa nje? Udhaifu mwingi zaidi hujitokeza na kugundulika baada ya kupokea ondoleo la dhambi. Udhaifu wetu wote hauja jitokeza bado. Hata hivyo bado tumeokolewa mioyoni mwetu ikiwa tutaendelea kuamini kwamba Mungu ndiye Mungu wetu na kwamba Yesu alizibeba dhambi zetu zote katika mto Yordani kwa njia ya ubatizo wake na kusulubiwa.
Hatuwezi kulinganishwa na watu wenye kuwekea mkazo juu ya tarehe waliyo okoka na kuamini tu kile kinacho weza kuthibitika kisayansi. Kwa uwazi watu hao ndio ombao hawaja okoka. Tunaamini kwa mioyo yetu ili kuweza kuwa wenye haki. Je, unaamini kwamba Yesu Kristo ndiye Mwokozi wetu? Amina. Imani huanzia mahali hapo na ndipo Bwana anapoongoza mioyo yetu tokea muda huo. Bwana anasema kwamba sisi ndiyo watoto wake wenye haki na imani zetu ni sahahi. Hubariki mioyo yetu na kutuhitaji kumfuata yeye kwa moyo wetu kiimani. Mungu hutuongoza na kutubariki pale tunapo tembea naye kwa imani mioyoni mwetu.
“Tohara ni ya moyoni.” Tumeokolewa kwa kuamini kwa mioyo. Watu wengi duniani husema kwamba kuiamini Injili kwa mioyo yao kuliwaokoa. Hata hivyo bado wanongezea matendo yao katika imani. Huchukulia kwamba matendo ya utu wa nje ni kigezo muhimu katika imani zao. Husema kwamba kuwa na imani katika Injili ya maji na Roho kamwe hakutoweza kuwaongoza katika wokovu, kwa sababu huchanganya imani ya moyoni na matendo yao mema. 
Matokeo yake wanajikuta wakishughulika zaidi na vile utu wa nje ulivyo stawi, kuangalia mara ngapi zaidi wanafanya sala za toba au kfanya maombi mara kwa mara. Watu hawa wako mbali na wokovu ingawa wao hudhani kuwa wameokoka toka dhambini.
 

Mungu huchunguza na kuangalia Moyoni.
 
Tunaamini kuwa wenye haki katika mioyo yetu. Kwa uwazi utu wetu wa ndani umewekwa mbali na hauna uhusiano kabisa na matendo yetu. Wokovu wenyewe hauna uhusiano na matendo yetu. Je, umejengeka na kuburudishwa baada ya kujifunza kwamba dhambi zako zote zilifutwa? Je, ungependa kumtumikia Bwana kwa furaha? Je, wewe nawe unaihubiri Injili kwa furaha? Je, ungependa kujishughulisha na kazi yake njema? Moyo unapata amani na furaha kwa kuwa Mungu amezithibitisha imani zetu na kuzitambua pale tunapo amini kwa mioyo yetu. Hivyo, moyo ni muhimu mbele ya Mungu.