Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 2-2] Wale wenye kuidharau Neema ya Mungu (Warumi 2:1-16)

(Warumi 2:1-16)
“Kwa hiyo wewe mtu uweye yote uhukumuye, huna udhuru, kwa maana katika hayo umhukumuyo mwinginie wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia, kwa maana hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. Wewe binadamu uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda hayo mwenyewe Je, wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimiliwa wake na uvumilivu wake usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? Bali kwa kadiri ya ugumu wako na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu atakaye mlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake, wale ambao kwa sabubu ya kutenda mema wakatafuta utukufu na wale wenye fitina, wasioitii kweli bali wa kubalio dhuluma watapata hasira na ghadhabu, dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia, bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Myunani pia kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu. Kwa kuwa wote walio kosa, wenye sheira watahukumiwa kwa sheria. Kwa sababu sio wale wasikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakao hesabiwa haki. Kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Hao waionyeshe kazi ya torati iliyoandikwa mioyono mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao yenyewe kwa yenywe yakiwashitaki au kuwatetea, katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu sawa sawa na Injili yangu kwa Kristo Yesu.”
 

Watu wa matendo ya sheria huwahukumu wengine huku wao hawawezi kuifuata sheria hiyo.
 
Hebu tuzungumzie juu ya sheria. Paulo Mtumie aliwaambia Wayahudi walio ifuata sheria “kwa hiyo wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru, kwa maana katika hayo umhukumuye unafanya yale yale: Nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. Wewe binadamu uhukumuye je, wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu?” (Warumi 2:1-3). Waifuatao sheria hudhani kwamba wao ndio wanao mheshimu Mungu zaidi. Aina hii ya watu hawamwamini Mungu kwa mioyo yao yote, bali kwa majivuno yao bandia yaliyo katika msingi wa matendo yao. Watu hawa hupenda kuwahukumu wengine na ni wepesi kwa hilo sana. Hata hivyo wakiwa wana wahukumu wengine kwa maneno ya Mungu hawagundui ya kwamba wao nao wanafanana na hao wanao wahukumu na pia kufanya makosa hayo hayo.
Kwa mfano, hawaifuati Sabato takatikfu, ingawa wao huwaeleza wengine kuitimiza kwa kulingana na Amri za Mungu. Huwaambia wengine kuitii na kuifuata sheria lakini wao hawatendi hivyo. Paulo Mtume alisema kwa watu wa aina hii “Wewe binadamu uhukumuye wale wafanyao hayo na kutenda hayo hayo mwenyewe je, wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu?” (Warumi 2:3).
Wafuatao sheria hawatoweza kuokolewa na Mungu. Sheria kamwe haitoweza kutuokoa, hivyo Mungu atatuhukumu ikiwa maisha yetu ya kidini yamo katika msingi wa sheria. Wafuatao sheria huleta hasira ya Mungu. Wale ambao bado hawajaokoka bado wana imani za kufuata sheria. Huwaelekeza wengine kuishi kwa namna fulani, kulingana na sheria lakini wao hawakupaswa kusema mambo ya aina hiyo nyakati hizi.
Hapo zamani Wakristo wengi katika nchi yetu walizoea kuwa namna hii. Watumishi waliofuata sheria walizoea sana kuwakemea wanawake walio na nywele ndefu za mtindo, wakisema kwamba watatupwa jehanamu. Ikiwa tungelikuwa chini ya uongozi wa mtumishi mwenye kufundisha wafuasi wa kanisa kwa matendo ya sheria kwa njia hii bila shaka tungeliamini kwamba wale wote walio na mitindo ya nywele ndefu moja kwa moja wataingia jehanamu. Hili ni jambo lilitokea takribani miaka 15-20 iliyopita. Ikitokea mwanamke akijipaka rangi ya mdomo tafsiri yake ni kwamba atapelekwa toharani (mahali au hali ya kuteseka kwa ajili ya kutenda kosa au makosa na hatimaye kuweza kurejeshwa au kutakaswa upya) chini ya maelekezo ya mtumishi wa aina hii.
Watu hawa walikuwa ni wafuatao sheria. Kwa mtazamo wa nje kimwili walionekana kuwa ni watakatifu, wakiwafundisha watu kutopaka rangi za midomo au mitindo ya nywele ndefu, kutembea kwa upole na kutouza au kununua dhidhaa yoyote. Washika sheria hawa huwaeleza waumini yaliyo mema na siyo mema kwa mtazamo wa maneno ya Mungu, huku wao binafsi ni wanafiki.
 

Wayahudi nao wanafana hivyo.
 
Wayahudi nao hufanana hivyo. Wao huwahukumu watu wa Mataifa kwa sheria wakisema mambo kama vile “Hawamjui Mungu na wanaabudu sanamu, Wameangamia jehanamu na ni wa katili sana.” Hata hivyo wao binafsi hupenda mali na utajiri wa dunia hivi vikiwa ni miungu ya ugenini zaidi kuliko Mungu.
“Wewe binadamu uhukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je, wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu?” Wayahudi waliwahukumu wengine kwa sheria, lakini kamwe hawakufuata walicho fundisha. Zaidi ya yote, wale ambao hawakuamini haki ya Mungu au kuwa na wokovu wa Yesu mioyoni mwao hudhani wao kuwa wako sambamba na neno la Mungu lakini wao nao wanafanana na Wayahudi.
 

Wafuatao sheria watahukumiwa.
 
Watu wa kizazi kipya leo hii labda hawajawahi kabisa kuishi maishi yenye tabia za kidini. Hata hivyo wale wa kizazi kilicho pita wao bila shaka waliwahi kusikia mahubiri yaliyo katika misingi ya sheria. Watumishi walizoea kuwashutumu na kuwakemea wale walio na mitindo ya nywele ndefu kwa sababu tu inaonekana ni kutamanisha kimwili. Nyakati hizi mtumishi hatoweza kufanya hivi tena. Ilikuwa ni moja kwa moja shutuma kusema maneno kama “wenye haki” au “kutakaswa kabisa” hapo kale. Siku hizi ingawa wati wengi kwa ujumla hutumia maneno kama “wenye haki” hii inamaanisha kwamba kwa sasa mwelekeo wa Ukristo umebadilika. Walimu waongo kwa sasa hawana tena fursa katika kuzungumza uongo watakavyo kwa sababu washirika wao tayari wamekwisha kukombolewa kwa Injili ya kweli kupitia vitabu vyetu na kanda za redio. Hivyo hawawezi tena kunena mbele za wanao wasikiliza pasipo sababu.
Jambo muhimu kujua ni kwamba wafuatao sheria ambao hudharau wokovu wa Yesi Kristo na ambao kuishi kwa kufuata dini huenenda kwa sheria na hivyo watahukumiwa mbele ya Mungu.
Mstari wa 4 unazungumzia juu ya hukumu ya Mungu. Hebu tuisome “Au wadharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilvi wake usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?” Mungu atawahukumu watu wafuatao sheria. Wapendwa imani ya wafuatao sheria inapingana na Mungu. Wafuatao sheria hupinga upendo wa Mungu kwa vigezo vilivyo katika msingi wa matendao yao. Wafuatao sheri huidharau Injili ya wokovu itamkayo kwamba Mungu alikwisha samehe dhambi zote na uovu wote kwa kupitia utajiri wa wema wake, ustahimili na uvumivu wake.
Wale wote waishio maisha ya kidini huenda kwa kulingana na sheria na watahukumiwa mbele ya Mungu. Hata hivyo watu wengi kufuata dini zao wakiishi kwa sheria mbele ya Mungu. Tusiwe na mawazo kama vile “Tumeepushwa na hukumu ya Mungu kwa sababu tayari tumeokoka.” Paulo Mtume alisema kwamba wafuatao sheria wasingeliweza kuokoka, badala yake wataangamia kwa hukumu. Yatupasa kufahamu kwamba ni watu wa aina gani wenye kuishi maisha ya kufuata dini kwa kufuata sheria ili kwamba tuweze kuja na mpango wa kuwasaidia kukombolewa kwa kuwapatia Injili.
 

Wapo wafuatao sheria pamoja na Wayahudi hapa ulimwenguni.
 
Paulo Mtume hakuzungumiza ukweli wa Yesu kutakasa dhambi zote za ulimwengu tu, pia alizungumzia namna ile watu wanavyo ishi kiudini kwa kufata sheria kama vile Wayahudi wanompinga Mungu watakavyo hukumiwa. Wanadharau upendo wa Mungu ambao kwa kupitia huo, alidhihirisha huruma yake kwetu. Wanadharau Injili ya ondoleo la dhambi za dunia. 
Je hawapo washikao sheria karibu yako ambao hufuata udini kama hivi? Wapo wengi wenye kuamini kwamba Mungu hana huruma na dunia na kwamba hakusafisha dhambi zetu zote. Hata hivyo wapo baadhi wenye kuukubali upendo wa Mungu na kuweka kando mawazo binafsi na kuitwa wenye haki mbele ya yake. Wapo pia wale washikao sheria wenye kuidharau haki ya Mungu na kuweka kando wokovu wa Mungu kwa mawazo binafsi hata sasa hivi. Hawa ni wengi zaidi na huwadharau wale wenye haki walio okoka.
Nataka uelewe ya kwamba wapo watu wengi wakuzungukao ambao wao wameudharau wingi wa wema wa Mungu, uvumilivu na subira kama walivyo Wayahudi. Je, hili ni kweli au si kweli? Ndiyo wapo wengi washio namna hii. Wafuatao sheria huwadharau wengine mbele ya Mungu. Ni nini wanacho kidharau? Wokuvu kamili wa Mungu.
Watu wengi wanao ishi duniani hudharau ukweli wa Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu wakiwemo Wayahudi. Wayahudi ni watu wa Israeli wao husema “itakuwaje awe ni Mwana wa Mungu? Yeye ni moja tu ya manabii.” Wao wanamtambua kama ni nabii tu. Waisraeli walimdharu Mwana wa Mungu na kumpiga makofi wakisema “amekufuru” (Mathayo 26:65). Walimdharau. Hawa mwamini Mwana wa Mungu. Inaeleweka kwamba Waisraeli walimdharau Yesu kwa sababu hawakumwamini. Hata hivyo wafuatao sheira huwadharu watu wa mataifa kwa lipi? Hudharau wingi wa upendo wa Mungu na haki.
 

Wafuatao sheria kuishi kwa msingi wa matendo yao binafsi.
 
Katika dhehebu la wafuata sheria hufundisha wafuasi kugeuza shavu la upande wa kushoto wanapo pigwa la kulia. Wasiwe wenye hasira. Pia wanaelekeza namna ya kuhubiri kanuni za mafundisho ya upole, namna ya kutabasamu na mambo mengine. Hudhani kwamba wao wanajua juu ya maandiko yote. Na kusisitiza kwamba dhambi yao ya asili ilisamehewa lakini wanaweza kupokea msamaha wa dhambi za kila siku kwa kufanya kitubio katika sala za kila siku.
Jambo kama hili ni imani iliyo katika msingi wa sheria. Mambo haya pia huwafanya watu wadharau wingi wa upendo wa Mungu na wokovu wake. Husema, “wewe ni mwenye majivuno unapo sema kwamba huna dhambi, nimwenye haki na kwamba tayari umekwisha pata msamaha wa dhambi zote kwa kuamini kwamba Yesu alikwisha zitakasa!” Wao hudhani kwamba, Mungu huwaita wao kuwa ni wenye haki ingawa ukweli ni kuwa wao bado si wenye haki kamili.Wafuatao sheria wote huamini mafundisho haya potofu ya Kikristo. Hivyo yatupasa kuwa mbali na wafuatao sheria hawa.
Baada ya kumwamini Yesu, je, kupokea msamaha wa dhambi za kila siku kwa njia ya kufanya sala za toba si kufuata sheria? Je, sivyo? —Ndivyo.— Je, haitokani na sheria ya matendo au la? —Ndiyo inatokana.— Hii si imani sahihi. Watu wenye kutamka kwamba wao huishi kwa kufuata maandiko ya sheria hawa ni wafuatao sheria. Wapo wengi watu wa aina hii kati yetu.
Paulo Mtume alipokea ondoleao kamili la dhambi kwa kumwamini Yesu Kristo. Hata hivyo, Waisraeli walio kuwa na imani katika Agano la Kale kwa kufuata sheria waliamini Uzayuni. Je, wote hawa waliokua kati ya watu hawa nao walikuwa wafuata sheria au la? Walikuwa ni kati ya wafuata sheria, wakifundisha mambo ya mwilini kama vile namna ya kuenenda, kile kilicho marufuku, kilicho najisi au usicho paswa kufanya.
Hivyo Paulo Mtume aliwashutumi watu hawa kwa sauti ya ukali. Alifanya hivi kwa njia ya busara. Wakristo wa leo hufuata maisha ya kushika sheria pia. Wao huamini kwamba ingawa wametakaswa kwa imani, dhambi zao husamehewa kila siku pale wanapo fanya sala za kitubio. Hawa ni washika sheria na imani zao ni za kisheria.
Wachungaji wengi ni wepesi kuhubiri huku wakisema “tumeokolewa kwa imani” ingawa hatimaye humalizia wakisema “lakini inatupasa kukiri yale tuliyo tenda kama ni dhambi kwa kutubu.” Wachungaji hawa ni washika sheria. Hutegemea matendo yao kwa wokovu, huku wakiacha kuamini au kutegemea katika Yesu.
Je, nasi tulikuwa ni washikasheria kabla ya kuokoka?     —Ndiyo— Kabla ya kuzaliwa upa mara ya pili tulidhani kwamba kutenda mema kungelituokoa. Wapo wengi duniani wenye kudhani hivyo. Mungu anawaasa kutububu. “Tubuni basi mrejee ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana” (Matendo 3:19). Hata hivyo watu hawa hawataki kutubu. Hakika ni wakaidi! Hivyo Paulo Mtume kwa mara nyingine anazungumza na watu hawa wakaidi.
 

Wafuatao sheria hutamka kwamba wao ni wenye dhambi mpaka siki ya kufa.
 
Tuangalie Warumi 2:5 “Basi kwa kudiri ya ugumu wako, na kuwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu.” Hasira ya Mugu imeshikiliwa kama kisu cha kuchinja koo zao. 
Wanapo patwa na hatari, bado watakiri kwamba wao ni wenye dhambi mbele za Mungu daima hata mpaka kifo. Hakika ni wakaidi! Husema kwamba wao ni wenye dhambi kwa sababau kamwe hawatoweza kuishi kwa kufuata maneno ya Mungu ingawa wanamwamini Yesu Kristo.
Je, Mungu anasemaje? Anasema “Kwa kuwa hamwezi kuishi kwa kufuata maneno yangu nimekwisha kuwaokoa. Nimefuta dhambi zenu zote na kuwakomboa daima.” Watu hawa hawana imani katika Yesu Kristo au hata katika kujaribu kuikubali haki ya Mungu ili wakombolewe kwa dhambi zao. Badala yake husisitiza kwamba wao ni wenye dhambi hata mwisho wa kifo hivyo hujaribu kuokolewa kwa matendo ya sheria wakichanganya na imani katika Yesu Kristo. Nilazima wajue ya kwamba wakati utakuja pale watakapo hukumiwa kwa imani zao na matendo.
“Basi kwa kadiri ya ugumu wako na kwa moyo wako usio na toba wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu” (Warumi 2:5). Paulo Mtume anamaana “Kwa jinsi gani mlivyo wakaidi. Imewapasa kuhukumiwa kwa ajili ya mioyo iliyo migumu na isiyo na haya.Mnajiwekea akiba ya hasiri yake.” Yesu Kristo alifuta dhambi zetu zote, bila kujali kama mtu anaamini hili au la. Kwa njia hii kila mtu ataweza kuokolewa kwa dhambi zake zote kwa njia ya Yesu Kristo. Tuliokolewa kwa imani ya ule ukweli wa kwamba, Yesu Kristo alisafisha dhambi zetu zote. Tusingeliweza kuishi kwa kuifuata sheria huku tukiomba sala za toba kila siku ili kupokea msamaha wake, hivyo basi tulirudi kwa Yesu Kristo toka katika dini za Mataifa. Hatima yetu siku zote ni kutenda dhambi hadi kifo, hivyo hatutoweza kuwa wenye haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani katika Bwana.
Je, unatamka kwamba wewe ni mwenye haki hata mwisho wa kifo mbele ya Mungu? Au unatamka kwamba utaendelea kuwa mwenye dhambi hata mwisho wa kifo? —Tunatamka kwamba sisi ni wenye haki.— Baadhi watasema labda hili ni shinikizo tu. Bila shaka ni nani atafuata aina hii ya fundisho la kushinikiza? Hakuna.
Tuseme kwa mfano, atokee mtu fulani aweke kwenu fundisho la kushinikiza kila siku. Bila shaka mtalalamika vikali mkisema “Kwa nini iwe hivyo? Kwa hiyo?” Je, wengi hawatong’aka kwa maneno makali namna hii? Je twaweza kuamini jambo lolote ambalo haliko katika msingi wa kibiblia kwa maneno mazuri ikiwa tu mtu atajaribu kutulaghai ili kuamini jambo hilo? Haito wezekana. Hata kwa kiasi kidogo. Twajua kwamba watu ni wakaidi lakini tuna nyenyekea na kuamnini ukweli ikiwa kama unatokana na neno la Mungu.
 

Ni kwa jinsi gani wafuatao sheria walivyo wakaidi.
 
Ni kwa jinsi gani walivyo wakaidi. Wao hutamka kwamba ni wenye dhambi mpaka siku ya mwisho wa uhai wao. Wapo watu wengi wanao amini Uzayuni (Zionism). Je, wapo watu wengi katika nyakati hizi za Wakristo wenye kuamini Uzayuni? Au hawapo? —Wapo Husema.— “Bwana ninakuja mimi mwenye dhambi. Tafadhali nisamehe dhambi zangu.” Wapo wengi watamkao kwamba wao ni wenye dhambi mbele ya Mungu kwa sababu wao huangalia udhaifu wao na dhambi zao za kila siku kwa mtazamo binafsi. Ingawa wapo Wakristo zaidi ya bilioni duniani na milioni kumi katika Korea wengi wa hawa ni wafuatao sheria
 

Washika sheria wanafananishwa na Mafarisayo.
 
Nami nilikuwa ni miongoni mwa washika sheria kabla ya kuamini Injili ya maji na Roho. Nilizoea kufikiri kuwa, “Nitawezaje kuwa mwenye haki hali bado ninaendelea kutenda dhambi kila siku?” Lakini kwa sasa sivyo hivyo tena. Watu wengi wanatabia ya ukaidi. Je, watu hawa watakwenda wapi kulingana na Biblia? Wataishia jehanamu kwa kuwa wamejiwekea akiba ya hasira ya Mungu kwa sababu ya ugumu wa mioyo isiyo na subira. Wafuatao sheria nao pia imewapasa kutubu mara moja wakibadilika huku wakiwa bado wanashi hapo duniani kwa kushukuru na kuamini kwa hakika kwamba Yesu Kristo alikwisha kuondoa dhambi zao zote.
Hata hivyo wao ni wakaidi kuweza kutubu. Watu hawa wanasikitisha sana. Hawatubu ingawa imewapasa kufanya hivyo. Wapo watu wengi wanao shika tabia za Kifarisayo. Husalimu watu kwa unyenyekevu wanapokuwa makanisani wakisema “mpendwa hujambo? Unahali gani mpendwa?” huku wakishikilia biblia mikononi mwao kwa unyenyekevu wote na upole. Macho yao hufumba nusu kwa tabia ya majivuno wanapo kutana na wengine katika siku za Jumapili. Hujaribu kuonekana wenye tabia ya Uungu kuliko hata Yesu mwenyewe. Ingependeza vipi ikiwa kama wangeliweza kuwa namna hii kila siku?
Je, unajua wake za wachungaji washikao sheria husema nini? Husema kuwa wao ni wenye furaha siku zote pale waume zao wanapo toa mahubiri katika madhabahu kwa sababu waume hao huongea kwa sauti za upole na maneno muruwa ya upole kama vile maneno ya utakatifu na rehema. Lakini hubadilika punde wanaporudi majumbani mwao. Siku moja mke wa mchungaji ashikaye sheria aliamua kuleta vifaa vya shughuli zake za jikoni karibu na madhabahu ya mumewe. Mume alipomuuliza sababu ya kufanya hivyo, mkwewe akajibu kuwa, anapokuwa katika madhabahu huwa ni mtu mpole sana na mnyenyekevu lakini akirudi nyumbani hugeuka na kuwa mkali na mkorofi kama mbogo na kumbugudhi sana.
 

Yatupasa kuihubiri Injili.
 
Nasema bila unafiki, mimi nilikwisha wahi kutoa maneno makali kwa mke wangu. Hii ni kwa kuwa mke wangu husema “Unacho jali wewe ni Injili tu!” Ukweli ni kwamba mimi siwezi kufanya kila jambo vile ipasavyo kwa sababu si mtu makamilifu. Hivyo basi jambo la kwanza ninalopaswa kufanya ni kazi ya Mungu kwanza. Pili ni angalie nyumba yangu. Tatu ni shughuli nyingine za hapa na pale. Huu ndiyo mtiririko wa majukumu yangu. Na hii si kwa kuwa mimi ni mchungaji. Nafanya haya kwa sababu nasimamia zaidi katika kutumikia Injili baada ya kufanya mambo yangu binafsi. Sidhani kama nitaweza kuihubiri Injili baada ya kumaliza maswala yanayo nihusu kibinafsi kwa namna yoyote.
Wafuatao sheria hujifanya kuwa kama malaika wanapo simama madhabauni. Huwafundisha waumini namna ya kulia kwa ajili ya dhambi zao. Kila mshika sheria imempasa kupokea msamaha wa dhambi punde anapomwamini Yesu kwakuwa ndipo hapo atakapo weza kuwa na amani na furaha kwa kutokuwa na dhambi moyoni. Hii ni njia pekee kwa nafsi ya mtu kuweza kuwa na furaha. Watu hutenda dhambi na kufanya yasiyo na ustaarabu huku wakiendelea na maisha yao, na hivyo ikiwa mtu atakuwa na dhambi moyoni itakuwa ni tabu zaidi ya jehanamu kwake. Mungu huwahukumu watu wa aina hii.
Siwezi kuacha kusema kwamba watu wengi wanajiwekea akiba ya hasira mbele ya Mungu. Wale wasio tubu, wasio badilika na hata kumwamini Yesu Kristo, huku wakijisingizia kumwamini, hakika watahukumiwa na hasira ya Mungu. Hawawezi kuendelea kumdhihaki Mungu. Hatutoweza kumdhihaki Mungu ikiwa kama tuna imani za kweli mbele yake. Tunapokea hukumu tusipo mwamini. Hasira yake itafunuliwa kwa wale wasio na imani. wataunguzwa na moto usio zimika. Wapo wengi watakao unguzwa kwa moto huu kutokana na kutoamini kwao.
Hivyo basi, inatupasa kuihubiri Injili. Yatupasa kuendelea kueneza neno la Mungu kila mara tukutanapo pamoja. Yatupasa kutafakari Injili hii na si kujifikiria nafsi zetu tu, bali pia kuchukua wakati katika kuwajali wengine kwa Injili. Sababu ya lazima katika kuihubiri Injili ni kuwasaidia watu wote kuepuka hasira ya Mungu, ingawa watu hawa hutuhukumu na kuudharau upendo wa Mungu.
Yatupasa kuelewa yafuatayo. Wapo watu wengi miongoni mwetu watakao pokea hasira hii. Yatupasa tufikirie upya juu ya kutoshuhudia au kushuhudia kwa jambo hili. Kwa nini tusifanye vile tuwezavyo katika kuihubiri Unjili zaidi kuliko kukusanya sadaka toka kwa watu. Je, Mungu ataridhika ikiwa tutaachiliwa hukumu yake juu yao? Hatuwezi kuwaacha vile walivyo. Kwa kujua hili vyema, ni lazima tuihubiri Injili ulimwenguni pote.
Ikiwa kama yupo mshika sheria katika familia yako, basi familia yote, itahukumiwa kwa hasira ya Mungu. Nini maana ya ghadhabu? Pale watoto wanapo acha kutii wazazi wao tunasema “usipo tii utakoma!”. Hapo ndipo wazazi wanapo waadhibu watoto wao kwa kuwacharaza fimbo ikifikia hushindwa kuwavumilia. Ndipo baadaye watoto hukiri makosa yao na kuomba msamaha. Wazazi huwasamehe kwa sababau ni watoto wao. Katika mstari wa 4 imeandikwa “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?” Mungu hustahimili kwa miaka 70-80 na zaidi hapa duniani, lakini watu huwaadhibu watoto wao kwa fimbo baada ya kustahimili mara moja au mbili tu. Mungu hustahimili hadi mwisho wa uhai
 

Mungu alitayarisha moto wa jehanamu kwa wale wote wafuatao sheria.
 
Hapo ndipo mwisho pale Mungu atakaposhika kiboko mkononi mwake. Mungu alitayarisha moto mkali kwa wale wote wafuatao sheria, ambo moto huo huyeyusha miamba na kiberiti. Mungu atawafufua wafu katika miili yao kwa hasira yake. Ataifanya miili hiyo isife tena ili kwamba waweze kuhisi machungu milele na kuwatupa katika ziwa la moto wa kiberiti lisilo zimika milele. Hasira ya Mungu itawafufua katika miili ya milele na kuwafanya wateseke milele. Hawatokufa kwa kuungua, ingawa wata waka moto sana na kusema “nihurumie umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini auburudishe ulimi wangu, kwa sababu ninateswa katika moto huu” (Luka 16:24).
Yatupasa kuihubiri Injili hii kwao kwa kuwa ni kitambo kidogo tu watahukumiwa. Sababu ya kuihubiri Injili hii kwa washikao sheria baina yetu, ingawa twaweza kudharauliwa na kuhukumiwa nao, ni ili kuweza kuwasaidia waokoke kutokana na hasira na kuangamia. Je, unaelewa ni kwa nini tunafanya kila tuwezalo katika hili, kwa nini tunahamu ya kuwatumikia wengine na ni kwa nini tunatumia kiasi kikubwa cha fedha za kanisa katika huduma ya vitabu? Tungeliweza kuwa matajiri kama tungelitumia fedha hizo kwa ajili ya kanisa pekee. Tunge kula na kuishi vizuri sana.
Hata hivyo vitendea kazi vinahitajika zaidi katika kuieneza Injini duniani pote.Unaelewa ni kwa nini? Kwa sababu kwa njia hii ndipo watu watakapo weza kuokolewa. Sasa basi tunajitolea katika kuihubiri Injili duniani pote. Tusipo fanya hivyo, je, watu wata weza kweli kwa hakika kupokea msamaha wa dhambi zao?
Kama tusinge ihubiri Injili kwenu, je, mngeweza kuokolewa, hata kama Mungu alikwisha kuwaokoa? La hasha! Msingeokolewa. Sisi nasi kwa nyakati fulani tulikua wafuata sheria kabla yakuokolewa. Tulikuwa ni wenye dhambi ingawa tulimwamini Yesu. Tungeliweza kuangamia hapa duniani ikiwa kama tusinge sikia habari hii njema.
Je, tutathubutu kweli kuacha watu waangamie jehanamu? La hasha! Hatutoweza kamwe. Hatutoweza kuwaacha watu waende jehanamu kwa sababu sisi tuna fahamu juu ya Injili ya Bwana na wokovu wake. Twajua ni yupi atakaye kwenda jehanamu na ni yupi atakaye ingia Ufalme wa Mbinguni kwa kigezo cha maandiko ya Mungu. Hivyo basi, tuna hofu juu yao na kuwaombea huku tukiwahubiria habari njema. Sababu ya kutafuta fedha na kuzitumia kwa kiwango kikubwa katika huduma hii ni kwa sababu ya mambo yafuatayo:—Kuokoa nafsi ni kipaumbele na muhimu sana kuliko kujipatia na kujilimbikizia chochote cha dunia hii. 
Sababu ya kuihubiri Injili tukiwa na uvumilivu na subira licha ya kudharauliwa na kuhukumiwa na wafuatao sheria, ni kusaidia wokovu wa nafsi zielekeazo katika hukumu na ghadhabu ya Mungu.
Waweza kudhani kuwa “Ninyi mna vitabu vizuri zaidi visomekavyo kirahisi katika Injili ya kweli na kuvisambaza dunia nzima kama vipeperushi” Tumefanya hivyo kwakuwa ni njia bora zaidi katika kuhubiri Injili ya kweli. Lakini kwa kuwa bado haitoshi, tunalazimika pia mara kwa maara kujaribu kila liwezakanalo na kuendelea kusali zaidi.
Sisi wahubiri wa Injili ya kweli hatujaribu kuhubiri Injili ili tu tuweze kunufaika kwa kipato. Tunahubiri Injili ili kusaidia kuokoa nafsi kwa kuwa inajulikana kwamba wahubiri wale washika sheria, wao huangaikia tamaa za duniani huku wakijivunia kujitolea kwao katika Ukristo. Yatupasa kuelewa sababu ya mafundisho ya Injili za washikao sheria.
Yatupasa pia kujua kwa nini Bwana ametuamuru kuitunza siku ya Sabato kuwa ni takatifu katika Amri Kumi, na ni kwa nini wale wote wasio ishika na kuitunza kwa wakati ule wa Agano la Kale waliadhibiwa kwa kupigwa mawe hata kufa. Siku ya Sabato inamaanisha Injili ya Yesu katika kutakasa dhambi zetu zote. Yatupasa kuweka akilini kwamba Yesu alitakasa dhambi zetu zote. Yatupasa pia kuihubiri Injili hii kwa imani katika Bwana, ambayo inajumuisha ule ukweli wake katika kufuta dhambi zote za dunia.
Nadhani kwamba hasira yangu dhidi ya washika sheria imenishuka hasa baada ya mahubiri haya. Lakini yatupasa kusamehe na kuwa na mtazamo mzuri dhidi yao. Hatima yao ni jehanamu ikiwa sisi tutafunga midomo. Sisi wahubiri wa Injili hatuwezi kuruhusu wafuata sheria kutudharau kwa fedha zao au kujigamba kwa vigezo vya mambo ya kimwili.
 

Yatupasa kuhubiri Injili kwa familia zetu na kwa nafsi nyinginezo.
 
Lazima tuihubiri Injili kwa kila mtu, pamoja na wengineo. Twajua ya kwamba nafsi zote ni zenye thamani kama za familia zetu. Yatupasa kuwajali watu wengine kuwa ni wenye thamani kwa sababau wote ni sawa mbele za Mungu.
Siwezi kujizuia kusema ukweli wa wokovu kila ninapo hubiri kwa sababu nafsi nyingi zinaangamia jehanamu. Yatupasa kuwaokoa ili wasiende motoni. Lazima tuihubiri Injili kwa wana ndugu wetu na marafiki kwa kutumia hata vitabu ikiwa vitaweza kuleta mvuto kwao napia kufanya maombi kwa yale tutakayo juu yao. Yatupasa kuihubiri kwa kila namna na njia mbali mbali. Tuwaandalie hata karamu pale nafsi hizo zinapo mrudia Mungu. Tunaongoza nafsi katika kuokoka pale tunapokuwa na mikutano ya uamsho katika kuihubiri Injili. Wakati mwingine watu huirudia dunia ingawa tulikwisha fanikiwa kuwahubiria Injili. Hapo sasa tunajawa na hasira. Lakini hatimaye tunarudi tena kuwahubiria tukiweka kando hisia zetu za kuudhika juu yao.
Nataka uelewe jambo moja leo. Kumbuka ukweli kwamba, wapo Wakristo wafuata sheria wengi kati yetu na hivyo inatulazimu kuwahubiria Injili. Wao hujisingizia kufuata sheria ingawa hawawezi kamwe kujizuia kutenda dhambi kila siku, na hudhani kwamba wataweza kupokea msamaha wa dhambi zao za kila siku kwa kufanya sala za toba kila mara na kufuata yale yaliyo katika torati.
Huikataa Injili isemayo kwamba Yesu alikwisha zifuta dhambi zetu zote. Wao hufikiri kwamba Yesu alichukua dhambi zile za asili tu, akiachilia zile za kila siku, na hii ni kwa sababu hawafahamu ukweli wa ondole la dhambi. Wale wasio jua ukweli wa wokovu ndiyo washikao sheria na torati. Yatupasa kuwasaidia katika kuokoka kutokana na dhambi zao kwa kuwahubiri Injili ya haki ya Mungu.