Search

Mahubiri

Somo la 3: Injili ya Maji na Roho

[3-9] Hebu Natutende Mapenzi ya Baba Kwa Imani (Mathayo 7:21-23)

(Mathayo 7:21-23)
“Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; Bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Watu wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako na kwa jina lako kutoa pepo na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu.”
 

LABDA NAMI NI MMOJA WAO….
Je, kila mtu asemaye “Bwana, Bwana” 
ataingia ufalme wa mbinguni?
Hapana. Wale tu watendao 
mapenzi ya Mungu.
 
Yesu Kristo alisema “Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; Bali yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Maneno haya yameleta woga katika mioyo ya wakristo wengi, hata kuwafanya wahangaike kwa bidii kutenda mapenzi ya Mungu.
Wakristo wengi hudhani kitu cha pekee wanachohitaji kufanya ni kumwamini Yesu ili waweze kuingia Ufalme wa Mbinguni, Lakini katika Mathayo 7:21 inatueleza kuwa si kila mtu amwambiaye Yesu “Bwana, Bwana” ataweza kuingia ufalme wa Mbinguni.
Wengi wasomao kifungu hiki hupelekea kushangaa “labda nami ni mmoja wao” Hujaribu kujishawishi, “Hapana Yesu, hapa anamaana ya wasio amini” Lakini wazo hubaki akilini na kuendelea kuwagonga ndani.
Hivyo wanabaki na sehemu inayofuata katika kifungu hiki kinachosomeka “bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” Hapo hushikilia neno, “afanyaye mapenzi ya Baba” na kudhani kwamba wataweza kufanya hivyo kwa kutoa zaka (kikumi) kwa uaminifu mkubwa, maombi ya kila siku jioni, kuhubiri matendo ya kiadilifu na kutotenda dhambi…. na hujaribu kwa bidii sana. Kwa kweli nawasikitikia sana.
Watu wengi hufanya makosa kwa sababu hawaelewi juu ya mistari hiyo katika maandiko. Hivyo ningependa kufafanua juu ya kifungu hiki kwa uwazi zaidi ili ninyi nyote muelewe mapenzi ya Mungu na kuyafuata.
Kwanza yatupasa kuelewa kwamba mapenzi ya Mungu ni kwa Mwana wake kubeba dhambi za wanadamu wote na kutuweka huru sisi kwa dhambi.
Katika Waefeso 1:5 imeandikwa “kwa kuwa alitangulia kutuchagua ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.”
Kwa maneno mengine, dhumuni lake ni kutufanya tujue injili ya kweli kwamba Yesu Kristo alisafisha dhambi zetu zote, hivyo kutuwezesha kuzaliwa upya mara ya pili. Anataka tuzaliwe upya mara ya pili kwa maji na kwa roho kwa kutwika dhambi zote juu ya mwana wake Yesu. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu.
 

NI KWA KUSEMA “BWANA BWANA”
 
Tunapaswa kuelewa nini pale 
tunapomwamini Yesu?
Mapenzi ya Baba.
 
“Si kila mtu aniambiaye, Bwana Bwana atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21).
Imetupasa kuelewa mapenzi ya Baba katika njia mbili. Kwanza yatupasa kujua kwamba ni mapenzi yake kwamba tunapata msamaha wa dhambi zetu na kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho. Pili kuishi kwa msingi wa imani.
Ni mapenzi yake kufuta dhambi zote za watu hapa duniani. Shetani ndiye aliyesababisha kuanguka kwa mzazi wetu wa kwanza Adamu kupitia dhambi. Lakini mapenzi ya Baba yetu ni kufuta dhambi zote za watu. Yatupasa kuelewa kwamba si mapenzi ya Baba yetu kwetu kutoa zaka kwa uaminifu na kufanya maombi ya jioni, bali ni kutuokoa kwa dhambi zetu zote. Ni mapenzi yake kutuokoa sisi sote toka bahari ya dhambi.
Biblia inasema kwamba si kila mtu aitaye “Bwana Bwana” ataingia katika ufalme wa Mbinguni. Maana yake ni kwamba hatupaswi kumuamini Yesu tu, bali pia kujua kile Baba yetu anachohitaji kwetu. Ni mapenzi yake kutuokoa toka dhambini na hukumu ya motoni, kwa kujua kwamba kwa kuwa sisi ni uzao wa Adamu na Hawa hatuna jinsi bali ni kuishi kwa kutenda dhambi tu.
 

MAPENZI YA MUNGU
 
Mapenzi ya Mungu ni yapi?
Ni kutufanya kuwa watoto wake kwa 
kutuweka huru toka dhambi.
 
Mathayo 3:15 inasema “kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” kwa hivyo ilikuwa ni kutimiza mpango wa Mungu na ndiyo maana Yesu alikuja ulimwenguni kutuokoa sisi sote kwa dhambi zetu. Mapenzi ya Mungu yalitimia pale Yesu alipobatizwa na Yohana Mbatizaji.
Alitaka kutuokoa na kutufanya tuwe watoto kwake. Na ili kutimiza hilo, Mwana wake Yesu, ilimpasa abebe dhambi zetu zote. Ilikuwa ni mapenzi yake kuwafanya watu wote kuwa watoto kwake. Hivyo alimtuma mwana wake ili kubeba dhambi zote za watu walioanguka katika mtego wa shetani. Ilikuwa ni mapenzi yake kuutoa uhai wa mwana wake kwa ajili ya watu wote ili kwamba waweze kuwa watoto kwake.
Yesu alipobatizwa na kufa msalabani, mapenzi ya Mungu yalitimizwa. Pia mapenzi yake kwetu kuamini kwamba dhambi zetu zote zilitwikwa juu ya Yesu pale alipobatizwa na hivyo kupokea hukumu kwa niaba ya uovu wetu kupitia kifo chake msalabani.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae pekee” (Yohana 3:16). Mungu aliokoa watu wake toka dhambi zao. Kwa kufanya hivyo kitu cha kwanza Yesu alichofanya katika huduma yake ya wazi ilikuwa ni kubatizwa na Yohana Mbatizaji.
“Yesu akajibu akawaambia kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akakubali” (Mathayo 3:15). Ilikuwa ni mapenzi ya Mungu kwamba Yesu aje ulimwenguni, abebe dhambi zote za ulimwengu kupitia ubatizo wake, afe msalabani na kufufuka.
Yatupasa kuelewa hili bayana. Watu wengi husoma Mathayo 7:21 na kudhani kwamba mapenzi yake kwetu ni kumtumikia Bwana, hata katika hatua ya kifo, kwa kutoa mali zetu zote kujenga makanisa.
Wapendwa Wakristo, sisi wenye kumwamini Yesu yatupasa kwanza kujua mapenzi ya Mungu na ndipo basi kuyatenda. Ni kosa kwako kujitolea kwa nafsi yako kwa kanisa pasipo kujua mapenzi ya Mungu.
Watu hujiuliza wenyewe nini kingine zaidi ya kuishi kwa imani katika makanisa yetu yaliyo halisi. Lakini mimi binafsi niliyewahi kujifunza mafundisho na kanuni za Ukalvini (Calvinism) katika kanisa la Presbyterian na kukuzwa chini ya mama wa kambo ambaye alikuwa ni mshika dini akiwa mchungaji mstaafu. Nilijifunza juu ya kanisa la “asili” (Orthodox).
Mtume Paulo alisema kwamba angeweza pia kujivunia kwamba alitokea katika kabila la Benjamini na kujifunza sheria chini ya Gamalieli ambaye alikuwa rabi maarufu kwa wakati huo. Kabla Paulo hajazaliwa upya alikuwa njiani akielekea kuwakamata wale wote wanao mwamini Yesu. Lakini akakutana na imani katika Yesu barabarani akielekea Dameski na akawa mwenye haki kupita baraka ya kuzaliwa upya mara ya pili katika maji na Roho.
 

YATUPASA KUFAHAMU MAPENZI YA MUNGU KABLA YA KUYATENDA
 
Ni kitu gani kilicho muhimu kabla 
ya kumuamini Yesu?
Yatupasa kwanza kuelewa 
mapenzi yake.
 
Utakaso wetu ndiyo mapenzi yake “maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kutakaswa kwenu mwepukane na uasherati” (1Wathesalonike 4:3). Twajua kwamba ni mapenzi ya Mungu kwamba tunatakasika kupitia maji na Roho na kuishi kwa imani maisha yetu yote.
Ikiwa kuna yeyote anayemwamini Yesu lakini bado ana dhambi moyoni, basi haishi kulingana na mapenzi ya Mungu. Kufuata mapenzi yake kunahitaji kuweza kutakaswa kupitia wokovu upatikanao katika Yesu. Kwa kujua hili ndipo utatenda mapenzi ya Mungu.
Nikikuuliza, “Je, bado ungali na dhambi moyoni hata ukiwa unamwamini Yesu?” na ukajibu ndiyo, basi hakika bado huelewi mapenzi ya Mungu. Ni mapenzi ya Mungu tuweze kutakaswa na kuokolewa toka dhambi zetu zote kupitia imani yetu katika maji na Roho.
Hapo kale palikuwa na mtu aliyekuwa na watoto walio watiifu. Siku moja alimwita yule wa kwanza ambaye naye alikuwa mtiifu zaidi na kumwambia “mwanangu nenda kijiji kile kupitia shambani….” kabla ya kumaliza kuongea yule mtoto akasema “ndiyo, Baba” na kutoweka. Hakusubiri kujua alichokuwa akielekezwa. Alikwenda tu. Baba yake akamwita “mwanangu, ni vyema na ni vizuri kwamba wewe ni mtiifu lakini yakupasa kujua ni nini nilichotaka ufanye.”
Lakini yule mtoto akasema “ni sawa baba nitakutii, ni nani awezaye kukutii zaidi yangu?”
Lakini matokeo yake alirudi mikono mitupu. Hakuwa na njia ya kutenda mapenzi ya Baba yake pasipo kujua nini alicho hitaji. Yeye alitii kama kipofu.
Nasi twaweza kuwa namna hii ikiwa hatutoweza kumwelewa Yesu Kristo. Wengi hujitolea nafsi zao kwa kufuata mafundisho ya theolojia, kutoa zaka kwa uaminifu, kusali usiku kucha, kufunga….yote pasipo kujua mapenzi ya Mungu.
Pale wanapo kufa na dhambi mioyoni mwao, hurudishwa mlangoni mwa mbinguni. Walikuwa na bidii ya kutenda mapenzi ya Mungu lakini hawakufahamu ni yapi Mungu alihitaji wayafanye.
 
Nini maana ya kutenda uovu?
Kumwamini Yesu ukiwa bado hujaielewa 
injili ya maji na Roho.
 
“Wengi wataniambia siku ile Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri. Sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu” (Mathayo 7:22-23).
Yapo mambo Mungu anayotuhitaji kuyafanya na ipo imani anayoihitaji kwetu. Anatuhitaji kumwamini Yesu kwamba ndiye aliyechukua dhambi zetu zote. Manabii wengi, hukemea pepo na kufanya miujiza kwa jina lake pasipo kuufahamu ukweli wa maji na Roho.
Kufanya miujiza maana yake ni kujenga majengo mengi ya kanisa, kuuza mali zako zote ili kuchangia kanisa, kutoa maisha yako kwa Bwana kati ya hivi.
Kutoa unabii kwa jina la Yesu maana yake ni kuwa kiongozi. Watu wa aina hii wanafanana na Mafarisayo wanaojigamba kuishi kulingana na sheria huku wakipingana na Yesu. Hii pia humaanisha kuwa Mkristo wa kanisa halisi.
Kukemea pepo ni kutumia nguvu. Wote hawa ni washabiki katika imani zao, lakini Bwana atawaambia siku ile ya mwisho kuwa hakuwajua. Atawauliza kwamba watawezaje kumjua yeye hali yeye hawafahamu?
Bwana amesema “ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe, ondokeni kwangu mtendao maovu” siku hiyo, umati wa watu utapiga kelele kwake “Bwana nakuamini. Nakuamini wewe ni mwokozi” Watasema kuwa wanampenda Yesu lakini bado wana dhambi mioyoni. Mungu atawaita kuwa ni watendao uovu (wenye dhambi wasio kombolewa) na atawaambia waondoke mbele yake.
Siku hiyo, wale waliokufa pasipo kuzaliwa upya mara ya pili watapaza sauti mbele ya Yesu “Nilitoa unabii nilijenga makanisa na kuwatuma wamisionari 50 kwa jina lako.”
Lakini Yesu atawatamkia hawa wenye dhambi “sikuwajua ninyi kamwe. Ondokeni kwangu ninyi mtendao maouvu.”
“Una maana gani? Hujui kuwa nilitoa unabii kwa jina lako? Nilitumikia kanisa kwa miaka mimgi…… nilifundisha wengine kukuamini wewe. Inakuwaje leo hunitambui mimi?”
Ndipo atakapojibu “sikutambui. Wewe unayedai kunitambua mimi hali unadhambi moyoni, ondoka mbele yangu!”
Ni uovu mbele ya Mungu kumwamini yeye huku ukiwa na dhambi moyoni au kutomwamini kulingana na sheria yake ya wokovu. Ni uovu kutojua mapenzi yake. Ni uovu kujaribu kufanya mapenzi yake pasipo kuyafahamu au pasipo kujua baraka ya kuzaliwa upya katika maji na katika Roho. Ni uovu pia kumfuata yeye pasipo kutii mapenzi yake. Uovu ni dhambi.
 

MAPENZI YA MUNGU KATIKA BIBLIA
 
Watoto wa Mungu ni akina nani?
Ni wenye haki wasio na dhambi.
 
Nimapenzi ya Mungu kwetu kuamini injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Injili ya kweli hulea makuzi yetu. Pia ni mapenzi ya Mungu kwamba tuifuate injili tukiwa ni watoto wake. Yatupasa kufahamu mapenzi ya Mungu lakini wengi hawaifahamu injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Ninapowauliza watu kwa nini wanamwamini Yesu wengi husema wanamwamini Yesu ili waokolewe toka dhambi zao.
Nauliza “sasa je, una dhambi moyoni mwako?”
Hujibu “Bila shaka, ninazo.”
“Sasa je, umeokoka au hapana?”
“Bila shaka nimeokoka.”
“Je, mwenye dhambi moyoni aweza kuingia ufalme wa mbinguni?”
“Hapana hawezi.”
“Sasa je, wewe utakwenda katika ufalme wa mbinguni au utakwenda motoni?”
Husema watakwenda ufalme wa mbinguni, lakini kweli wataweza? Watakwenda motoni.
Wengi hudhani kwamba kwa kuwa wanamwamini Yesu, wataweza kuingia ufalme wa mbinguni, hata kama wana dhambi mioyoni mwao na haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwao kuwa hivyo. Lakini Mungu hakubali wenye dhambi kuingia ufalme wa Mbinguni.
Mapenzi ya Mungu ni nini? Imeelezwa katika biblia kwamba mapenzi ya Mungu ni kwamba sisi tumwamini mwana wake, kuamini baraka ya kukombolewa kupitia ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Wale wenye kuamini baraka ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho huwa wana wa Mungu. Ni utukufu wetu kuwa watoto wake. Watoto wake ni wenye haki.
Mungu anapotuita wenye haki, je humchukulia mkristo mwenye dhambi kuwa ni mwenye haki? Mungu hawezi kudanganya. Hivyo mbele yake, wewe ni mwenye dhambi au mwenye haki. Hapawezi kuwepo kamwe “kuchukuliwa kutokuwa mwenye dhambi” Huita wale tu wanaoamini injili ya maji na Roho kuweza kutakaswa.
 
Tutawezaje kuwa 
watoto wa Mungu?
Kwa kuikubali injili ya 
maji na damu.
 
Kwa kuwa Mungu alimtwika dhambi zote za ulimwengu Mwana wake, hata kuhukumiwa msalabani. Hivyo basi Mungu kamwe hawezi kudanganya. Mungu anasema “Mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Mwana wake alipokufa kiza kilitanda duniani kwa saa tatu.
“Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema Eloi, Eloi lama sabakthani! Yaani Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?” (Mathayo 27:46).
Yesu alibeba dhambi zetu zote duniani kupitia ubatizo ili tuokolewe watu wote kwa dhambi zetu. Alichukua dhambi za wanadamu, kwa kujua kwamba itampasa kusulubiwa na kuachwa na Mungu, Baba yake. Hivyo Mungu alimhukumu Mwana wake kwa dhambi alizobeba Yordani na kumgeuzia kisogo kwa saa tatu.
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12).
Je, nanyi ni watoto wa Mungu? Tumezaliwa upya mara ya pili kwa sababu tumeikubali injili ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Wale wote waliozaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho ndiyo wenye haki. Sasa sisi wote tumekuwa wenye haki. 
“Mungu akiwepo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?” (Warumi 8:31) Mwenye haki anapojiita hivyo mbele ya Mungu na watu wale wasiokombolewa hujaribu kumtuhumu. Hivyo Mtume Paulo anasema, “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki” (Warumi 8:33). Mungu alifuta dhambi zetu zote kupitia Yesu na kutuita watakatifu walio na haki na wana kwake. Ametupa haki ya kuwa watoto watukufu wa Mungu.
Wale waliozaliwa upya kwa maji na kwa Roho ni watoto wa Mungu. Huishi naye milele. Wao sio kama viumbe wa dunia tena bali watoto wa Mungu walio mali ya mbinguni.
Sasa ni watoto wa Mungu wenye haki, hapana yeyote awezaye kuleta tuhuma dhidi yao, kuwa hukumu au kuwatenganisha na Mungu.
Yatupasa kuielewa injili ya maji na Roho ili tuweze kumwamini Yesu. Yatupasa kuielewa Biblia. Ni muhumu kwamba tujue na tuamini mapenzi ya Mungu ili tuweze kuyatekeleza kulingana na mapenzi yake.
 

NIMAPENZI YA MUNGU KWAMBA WENYE DHAMBI WAZALIWE UPYA MARA YA PILI KWA MAJI NA KWA ROHO
 
Kwa nini Mungu alimtuma 
mwana wake kwa mfano wa mtu 
mwenye dhambi?
Ili aweze kubeba dhambi zote 
za wanadamu.
 
Ni mapenzi ya Mungu kwamba tukombolewe na kuzaliwa mara ya pili kwa maji na Roho. Kwa maana hii ndiyo mapenzi ya Mungu, utakaso wake (1 Wathesalonike 4: 3).
Ilikuwa mapenzi ya Mungu kumtuma Mwanae ili dhambi zote zipitishwe kwake na tuweze kuokolewa. hii ndio sheria ya Roho inayoruhusu kuzaliwa upya kwa maji na Roho. Ilituokoa kutoka kwa dhambi zote.
Tumeokolewa. Sasa je! Nyinyi nyote mnaweza kutambua mapenzi ya Mungu? Ni mapenzi yake kutukomboa sisi sote. hataki tuongoze ulimwengu na badala yake tuamini maneno yake tu na tumwabudu yeye tu.
Ni mapenzi ya Mungu pia kwamba wale ambao wamezaliwa mara ya pili washuhudie Injili na wanaishi kanisani, wakijitoa katika kazi ya kurudisha mioyo mingine kwa Mungu.
Sisi hatutendi kwa sababu tunataka, lakini kwa sababu sisi ni dhaifu. Lakini Yesu aliondoa dhambi hizo. mungu alipitisha dhambi zote za ulimwengu kwa Yesu kupitia Yohana Mbatizaji. Alimtuma Mwanawe mwenyewe kwa sababu hiyo na akamfanya abatizwe na Yohana. Tumeokolewa kwa kuamini katika hii. Hi ni mapenzi ya Mungu
 

NI MAPENZI MUNGU KWETU KUMWANI YESU, ALIYEMTUMA
 
Kwa nini Yesu alikuja
kwa mfano wa mwanadamu 
mwenye dhambi?
Kuondoa dhambi zote
za wanadamu
 
Biblia inasema kufanya mapenzi ya Mungu ni kumuamini yeye aliye mtuma mwana wake “Basi wakamwambia tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu akawaambia. Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye. Wakamwambia unafanya ishara gani ili tuione tukuamini? Unatenda kazi gani. Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, aliwapa chakula cha mbinguni ili wale” (Yohana 6:28-31).
Watu walimwambia Yesu kwamba Mungu alimpa Musa alama alipokuwa njiani kuelekea Kanani, kwa kuwapa Waisraeli mana toka mbinguni, na matokeo yake walimwamini Mungu (Yohana 6:32-39). Watu walimuuliza Yesu “Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?”
Yesu aliwajibu kwamba imewapasa kumwaminini yeye ili kutenda kazi ya Mungu. Ikiwa imetupasa kutenda kazi ya Mungu, imetupasa basi kumwamini Yesu na kazi zake. Ni mapenzi ya Mungu kwetu si kuamini tu na kuhubiri injili bali kuifuata.
Mungu anaamuru “Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na roho Mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari” (Mathayo 28:19-20).
Yesu kwa uwazi anatuelekeza kuwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kila kitu alichofanya kwa Baba na Roho kimejumuishwa katika ubatizo wake. Tunapoelewa hili tutaweza kumwamini Mungu na kuona kila kitu Yesu alichofanya ulimwenguni na kwa namna gani Roho ashuhudiavyo juu yake.
 

KUTENDA KAZI YA MUNGU
 
Dhumuni la maisha yetu ni nini?
Kufanya mapenzi ya Mungu kwa kueneza 
injili ulimwenguni pote.
 
Ikiwa imetupasa kutenda kazi ya Mungu, yatupasa kwanza kuamnini injili ya ubatizo wa Yesu na kifo chake msalabani. Ni kazi ya Mungu kumwamini yeye (Yesu) aliyetumwa na Mungu. Ili tuweze kumwamini Yesu yatupasa kwanza kuamini kwamba ametuokoa kwa maji na kwa damu yake.
Mapenzi ya Mungu yamekamilika ndani yetu pale tunapomwamini Yesu na kuihubri injili. Kwa njia hii ndipo tunapotenda kazi ya Mungu. Ametueleza kwamba wale tu wanao amini baraka ya kuzaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho ndiyo watakaoingia ufalme wa Mbinguni.
Hebu sasa sisi sote tuchukue nafasi katika Ufalme wa Mbinguni kwa kuelewa ukweli ulio muhimu ufuatao. Kuelewa mapenzi ya kweli ya Mungu kwa kufahamu na kuamini kwamba dhambi zetu zote zilitwikwa juu ya Yesu kwa ubatizo wake. Kuishi kwa kueneza ufalme wake. Mwisho kuhubiri injili hadi mwisho wa maisha yako.
Wapendwa Wakristo! Wale wote wanaoamini injili ya maji na Roho ni wale watendao kazi ya Mungu. Ni kazi ya Mungu kumwamini yeye (Yesu) aliyetumwa na Mungu. Ndiko kufanya mapenzi yake katika kuamini kwamba dhambi zote zilitwikwa juu yake (Yesu) ambaye Mungu alimtuma na hivyo Yesu Kristo ni Mwokozi wetu.
Kazi ya kumkomboa mtu toka dhambini ilikamilika pale Yesu alipobatizwa Yordani na kufa kwa ajili yetu msalabani. Sehemu ya pili ya kazi ya Mungu kwetu ni kumwamini Yesu aliyetumwa na Mungu. Kumwamini Mwokozi aliyebeba dhambi zote za ulimwengu na kuihubiri injili duniani pote.
Sasa sisi tuliozaliwa upya mara ya pili yatupasa kuishi na kuihubiri injili hadi mwisho wa dunia.
 
Ni sehemu gani watu wale wanao 
mwamini Yesu pasipo kuyajua mapenzi 
ya Mungu watakapo ishia?
Wataishia Motoni.
 
“Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako na kwa jina lako kutoa pepo na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri. Sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu” (Mathayo 7:22-23).
Kifungu hiki kinatueleza wazi kuwa ni watu gani walio na dhambi mbele ya Mungu na ni akina nani watendao uovu.
Wapo wengi ambao hawajazaliwa upya mara ya pili kati ya hao wamwitao “Bwana, Bwana”. Wanaugulia kwa sababu bado wana dhambi mioyoni mwao. Hivyo hulia mbele za Mungu wakimwita “Bwana, Bwana” upande mmoja walikilalamika, kwa sala za uchungu wakiabudu.
Huamini dhamiri zao zitaweza kutakasika ikiwa watalia katika maombi, lakini si rahisi kwa sababu dhambi hubaki mioyoni mwao. Huomba milimani kulia kwa uchungu, utafikiri Mungu yupo mbali sana. Ikiwa hatuna imani kamili, ndipo tunapoanza kulia “Bwana, Bwana” mara kwa mara.
Katika makanisa kadhaa ambayo waumini hawajazaliwa upya mara ya pili husali kwa jazba na hisia nyingi hata kufikia madhabahu kuvunjika.Lakini tunaweza kuona katika Biblia kwamba si wale wamwitao “Bwana, Bwana” ndiyo watakaoingia ufalme wa Mbinguni. Ni wale tu wanaoamini injili ya maji na Roho ndiyo walio na imani itakayo waongoza kutenda kazi ya Mungu.
Biblia inatueleza kuwa ni uovu kuliitia jina lake ukiwa na dhambi moyoni. Je, umekwisha kuwepo katika maombi ya mlimani? Baadhi ya mashemasi wa kike walio wazee hulia na kulia, wakiitia jina lake (Yesu) kwa sababu hawajakutana naye katika kweli au hata kupokea Roho ndani ya mioyo yao na bado hawajazaliwa upya mara ya pili kwa maji na kwa Roho. Huliitia jina la Yesu haraka kwa sababu wanaishi katika hofu ya kudumu na kuwa watakwenda motoni.
Hebu fikiri mtu fulani aliyejitoa maishani mwake kutumikia kanisa kama mmisionari au mchungaji akikataliwa na Bwana moja kwa moja. Kutelekezwa na wazazi au mwenza katika ndoa kunatosha kabisa kuvunjika moyo, lakini kutelekezwa na Mungu, Mfalme wa Wafalme, Hakimu wa Roho, utakwenda wapi?
Natumaini hili kamwe halitokutokea wewe. Tafadhali sikiliza na uamini injili ya maji na Roho. Ni mapenzi ya Mungu kwetu kuzaliwa upya mara ya pili na kumamini injili ya maji na Roho.
Sisi wakristo yatupasa kwa kweli kuiamini injili ya maji na Roho na tupate nguvu toka katika kweli ya Biblia. Ndipo basi tutakapo okolewa na hukumu ya Mungu.