Search

Mahubiri

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-2] Je, inawezekana mtu kumnunua Roho Mtakatifu kwa uwezo wake? (Metendo 8:14–24)

(Metendo 8:14–24)
“Na Mitume waliokuwako Yesuramu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu wakawaombea wampokee Roho Makatifu kwa maana bado hawajawashukia hata mmoja wao ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya Mitume akataka kuwapa fedha akisema, nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakaye mwekea mikono yangu apokee Roho Mtakatifu. Lakini Petro akamwambia fedha na ipotelee mbali pamoja nawe kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. Basi, tubia uovu wako huu ukamwombe Bwana ili kama yamkini usamehewe fikira hii ya moyo wako. Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu. Simon akajibu akasema, niombeeni ninyi kwa Bwana yasinifike mambo haya mliosema hata moja.”
 

Je, mtu aweze kumpokea 
Roho Mtakatifu kwa
kuwekewa mikono?
Hapana. Imempasa kuamini Injili 
ya maji na Roho.

Husika na somo kuu katika kifungu hiki, napenda kuleta ujumbe huu iwapo “mtu anaweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani yake kwa kupitia juhudi binafsi”. Mitume katika nyakati hizo za Kanisa la kwanza waliweza kupokea nguvu toka kwa Mungu na kutumwa sehemu kadhaa naye. Yapo matendo ya miujiza kadhaa katika Kitabu cha Matendo, mojawapo likiwa kushuka kwa Roho Mtakatifu juu ya waumini pale Mitume walipowawekea mikono. Biblia inasema “Mitume walipowawekea mikono wale ambao hawakuwa wamempokea Roho Mtakatifu ingawa walikwisha mwamini Yesu, walipokea Roho Mtakatifu.”
Sasa basi, ni kwa namna gani walimpokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono? Kwa wakati huo maneno ya Mungu bado yalikuwa yakiendelea kuandikwa na hivyo basi kazi ilikuwa bado haijakamilika hivyo Mungu aliwapa Mitume nguvu za pekee kuweza kufanya kazi zake. Alikuwa pamoja na Mitume na kuweza kuleta miujiza mingi na maajabu kupitia kwao. Kilikuwa ni kipindi pekee, wakati Mungu alipofanya maajabu na miujiza ambayo iliweza kuonekana kwa macho ya wanadamu ili kuweza kuwafanya watu waweze kumwamini Yesu Kristo kuwa kweli ni mwana wa Mungu na ndiye mwokozi. Palikuwepo na umuhimu kwa Mungu pamoja na Mitume kwa nguvu za ajabu kuweza kuonyesha kazi ya Roho Mtakatifu ili kuthibitisha kwamba Yesu Kristo ndiye Mungu na kwamba ndiye Mwana wa Mungu Mwokozi. Ikiwa Roho Mtakatifu asingefanya kazi kupitia miujiza na maajabu kwa nyakati hizo za kanisa la kwanza hakika pasingekuwepo na yeyote awezaye kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi.
Hata hivyo hakuna umuhimu tena kwetu sisi leo hii kumpokea Roho Mtakatifu kupitia miujiza na maajabu ya kuonekana kwa macho ya kawaida kwa sababu Biblia imekamilika. Badala yake sasa, kuwa na Roho Mtakatifu ndani yetu kunategemea imani zetu zaidi. Kwa maneno mengine ni kuamini Injili ya kweli. Mungu ametupatia Roho Mtakatifu awe ndani yetu kwa wale tu watakao kuwa na imani ya Injili ya kweli mbele ya Mungu. Kuwa na Roho Mtakatifu ndani hutokea kwa wale tu wanao amini maneno ya Mungu kama ilivyo timia kwa kuja kwake Yesu hapa ulimwenguni na kwa ubatizo wake na damu yake.
Nyakati hizi wachungaji wengi hufundisha waumini wao kwamba matendo yasiyo ya kawaida yawezayo kuonekana kwa macho ndiyo ishara tosha ya kuwa na Roho Mtakatifu. Hivyo kuwaongoza waumini kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia hiyo. Huwapotosha watu kwa kuwapa mafundisho ya uongo kama yale ya kunena kwa lugha kuwa ndiyo ishara ya kushukiwa na Roho Mtakatifu. Wachungaji hawa hujiona kuwa wao ndiyo mitume watendao miujiza na maajabu makuu na hivyo kuvutia washabiki wa kidini ambao hutaka kumjua Mungu kwa hisia zao.
Ushabiki huu umeenea kwa Wakristo walio wengi duniani pote na wengi wao hufuata imani hizo na hatimaye kupatwa na roho za kishetani kwa kupitia njia za nguvu za giza. Hata leo, watu hao waliokumbwa na ushabiki wa aina hii hudhani kuwa nao wataweza kuwafanya wenzao kuweza kumpokea Roho Mtakatifu kupitia kuwekewa mikono.
Hata hivyo kwa jinsi Simoni alivyo potoka, nao huwa kama wachawi wanaonekana katika kifungu hicho. Wameharibiwa kwa kujikonga nafsi zao na tamaa ya mwili lakini matendo yao yote huleta tafrani katikati ya watu. Aina hii ya mafundisho ya uongo hupindisha njia ya kweli katika kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu mbele ya Mungu.
Hata leo, wengi wa mitume waongo hufanya kazi za ibilisi kupitia mambo yasiyo sahihi ya kidini, wakijifanya kutenda kazi za Roho Mtakatifu. Wakristo walio wa kweli ni lazima walishike neno la Mungu ambalo ndiyo ufahamu pekee wa kuweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani. Wale wote wanaojifanya kuwa ni Wapentekoste, ambao husisitizia mwonekano wa nje kimwili nilazima waache imani hizi potofu wayarejee maneno ya Mungu na kuamini ukweli ambao kwa hakika utawaongoza katika kumpokea Roho Mtakatifu ndani yao.
Simoni alikuwa mchawi maarufu Samaria katika nyakati hizo. Baada ya kuwaona mitume wa Yesu wakisababisha watu kumpokea Roho Mtakatifu, alitamani kumnunua Roho Mtakatifu kwa fedha. Watu wa imani ya aina hii bila shaka huishia kuwa watumwa wa ibilisi wakitumiwa kutenda kazi zake. Simoni alitaka kumpokea Roho Mtakatifu lakini tamaa zake zilikuwa si nyingine bali ni kujipatia kipato binafsi. Tunaweza kuona aina hii ya imani siyo yakupelekea kumpokea Roho.
Simoni alijaribu kumnunua Roho Mtakatifu kwa fedha kwasababu ya uchoyo ulio tokana na kutamani nguvu za Roho Mtakatifu. Alikemewa vikali na mtumishi wa Mungu Petro. Ingawa ilisemekana kwamba Simoni alikuwa akimwamini Yesu hakuwa ni mtu kamwe aliyekuwa amempokea Roho Mtakatifu kupitia ondoleo la dhambi. Kwa maneno mengine yeye alidhani ya kwamba angeweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake kwa kutoa mali za kidunia kwa Mungu.
Ingawa muonekano wake wa nje ulionyesha kwamba alikuwa akimwamini Yesu, mawazo yake halisi ndani yalikuwa hayawiani na maneno ya Yesu. Badala yake alijawa na tamaa za kimwili. Petro aliye yagundua mawazo ya Simoni alimkemea kwa kuwa alijaribu kutaka kumpokea Roho Mtakatifu ambaye ni zawadi ya Mungu kwa fedha. Alimtaadharisha Simoni kwamba angeweza kuangamia na fedha zake.
Nyakati hizi mitume waongo walio tawaliwa na roho za ibilisi hunena kwa kuwalaghai watu kwa kuwafanya kudhani kwamba miujiza na maajabu yote ni kazi za Roho Mtakatifu. Tunaweza kuona mara nyingi watu wakifurahia aina hizi za nguvu na kuomba kwa dhati nao waweze kumpokea Roho Mtakatifu. Hata hivyo mtu imempasa kuwa makini kwamba hapana yeyote atakaye mpokea Roho Mtaktifu ndani yake kupitia maombi yaliyo na tamaa za kidunia.
Je, wapo pia watu wa uamsho wa vipawa (karismatiki) kati yako kwa nafasi yoyote? Imekupasa uwe mwangalifu dhidi ya watu wa aina hii. Huwafata watu kwa imani hizi za mashamshamu na kishabiki. Husema kwamba wanaweza kukemea mapepo na hata kuweza kuwafanya watu kumpokea Roho Mtakatifu kupitia kuwawekea mikono. Hata hivyo watu hawa huwa na nguvu ambazo si za Roho Mtakatifu bali ni nguvu za pepo wachafu. Wale wanaodai kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia ya kuwekewa mikono hujiongoza wao binafsi na wengie katika kupokea roho chafu.
Kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu huja kwa sisi wote tu naoamini maneno ya maji na Roho (1 Yohana 5:3-7). Ingawa injili ya majina Roho imeandikwa kwa uwazi katika Biblia, bado watu walio wengi hudhani mioyoni mwao kwamba wataweza jaribu kumfikia Mungu kwa kupitia nguvu za miujiza na kwa hali za kupumbaza, kunena kwa lugha, maono na kukemea pepo. Na ndiyo maana manabii waongo wameweza kuwadanganya watu wengi katika kuamini mazingaombwe ya Kikristo yatokanayo na ibilisi mwovu.
Petro alimkemea Simoni kwa kumwambia, “Fedha yako na ipotee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili. Basi tubia uovu wako huu ukamwombe Bwana ili kama yamkini usamehewe fikra hii ya moyo wako. Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo na tena u katika kifungo cha uovu.” Yatupasa kujawa na simanzi kwa sababu leo hii wapo watumishi wa aina hii. Wengi wao ni wale wajiitao wenye vipawa au wakarismatiki. Hudai fedha kwa makundi yao. Tuwe mbali sana nao na watu wa imani hizi na tumpokee Roho Mtakatifu ndani yetu kwa Injili ya kweli katika maji na Roho (Mathayo 3:15, 1 Petro 3:21, Yohana 1:29, Yohana 19:21-23).
 

Watu wa vipawa hutenda kazi kwa kuwekea mikono!

Yatupasa kuwa mbali na imani ya aina hii. Baadhi ya watu siku hizi wanaimani potofu kwamba wataweza kumpokea Roho Mtakatifu ikiwa watawekewa mikono na wale waliokwisha kupokea nguvu hizo. Wao hudhani kwamba kwakuwa maandiko yanasema kuwa watu wengi walimpokea Roho Mtakatifu waliposhuhudia kuwekewa mikono na Mitume, hivyo nao wataweza kufanya namna hiyo pia. Baadhi yao wanajisingizia kwa imani potofu za aina hii, wanadhani kuwa wataweza kuwapa wengine Roho Mtakatifu kwa kupitia kuwawekea mikono juu yao. Yatupasa kuwa makini na kuwepo kwa watu wa aina hii.
Hata hivyo yatupasa kuweka akilini kwamba imani za watu hawa zinautofauti mkubwa na zile za Mitume wakati wa kipindi cha Kanisa la mwanzo. Siku hizi jambo kuu lenye kuleta ubishani mkali katika imani za baadhi ya Wakristo ni kwasababu hawana imani katika Injili ya kweli ya maji na Roho kati yao. Wengi husema kwamba wanamwamini Mungu lakini hawakumweshimu na hivyo badala yake hujidanga nafsi zao na zawenzao. Hata hivyo wenye dhambi kamwe hawatoweza kudanganya swala la kumpokea Roho Mtakatifu au hata kufanya wengine wadanganyike. Ikiwa mtu fulani atasema kwamba Roho amekuja juu yake yeye mwenye dhambi basi roho huyo hakuwa ni yule Roho Matakatifu kweli, bali badala yake ni roho wa shetani ajifanyaye kuwa Roho wa kweli.
Mitume wakati wa Kanisa la mwanzo walikuwa ni watu waliomjua na kumuamini Yesu Kristo kuwa ndiye mwokozi aliyechukua dhambi zote za wanadamu kupitia ubatizo wake alioupokea kwa Yohana na kifo chake msalabani. Waliweza kupokea Roho Mtakatifu kwa sababu waliamini ukweli juu ya ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani. Pia walihubiri Injili ya maji na Roho kwa wengine hivyo kuweza kuwasaidia katika kuwaongoza kumpokea Roho Mtakatifu.
Lakini siku hizi Wakristo wengi wamempokea katika imani za kishabiki. Je ni kweli mwenye dhambi katika nyakati hizi ataweza kumpokea Roho Mtakatifu kupitia kuwekewa mikono toka kwa mhudumu mwingine aliye na dhambi? Hakika hili halifikiriki. Wapo watu wanaosema kwamba ingawa wanadhambi moyoni, wamempokea Roho Mtakatifu ndani yao. Hata ikiwa mtu anaonekana ni mchungaji mzuri machoni pa kundi lake kamwe hawawezi kumsababisha yeyote kumpokea Roho Mtakatifu ndani ikiwa yeye mwenyewe anadhambi moyoni. 
Hii ndiyo sababu Manabii wengi wa uongo wameweza kuwaongoza watu kuelekea motoni. Yakupasa uelewe ukweli kwamba wale wote wenye kufundisha aina hii ya imani ni manabii wa uongo. Hawa ni watu ambao tayari wameshikiliwa na mapepo.
Ikiwa mtu anadhambi moyoni, je, Roho Mtakatifu ataweza kukaa ndani yake? Jibu ni hapana. Jingine, je, itawezekana kwa mtu aliye na dhambi kuweza kusababisha mtu mwingine aweze kupokea Roho Mtakatifu? Kwa mara nyingine jibu ni hapana. Sasa basi nini kinacho sababisha watu wanao semekana kuwa na vipawa (karismatiki) katika nyakati hizi kuweza kufanya miujiza na maajabu katika ukristo huku wakiwa bado wanadhambi mioyoni mwao? Mapepo au roho chafu hufanya hivyo. Roho Mtakatifu kamwe hawezi kuishi ndani ya mwenye dhambi. Yeye hukaa ndani ya wale tu walio na imani katika Injili ya maji na Roho. Je? wewe nawe unauhakika roho aliye ndani yako ni Roho Mtakatifu?
Katika Yohana 3:5 Yesu alisema “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu.” Kwa namna hii basi Roho Mtakatifu kuweka makazi ndani kutawezekana kwa wale tu watakao amini injili ya maji na Roho. Kosa ambalo wakristo wengi wafanyalo nyakati hizi nikwamba, huamini kwamba mtu ataweza pia kumpokea Roho Mtakatifu ndani yake kwa kuwekewa mikono na mtumishi mwenye dhambi. Hili nikosa kubwa na la hatari. Nyakati hizi, wakristo wengi na watumishi wao wanaimani na dhamiri zao kwamba, kuwa na Roho Mtakatifu ndani ya mtu huja kwa kupitia kuwekewa mikono.
 

Uhusiano kati ya ondoleo la dhambi la kweli na tendo la kuwekea mikono.

“Kuwekea mikono” ni namna ambayo mtu huweza kutwika au kutoa kitu alicho nacho juu ya kitu kingine. Kwa mfano, ikiwa tutazungumza katika kipaza sauti, sauti hiyo husafiri kupitia waya toka kipaza sauti na kutokea upande wa pili kwa sauti kubwa zaidi katika spika ili kila mtu aweze kusikia. Ndivyo pia katika Agano la kale pale mwenye dhambi alipoweka mikono yake juu kichwa cha mnyama wa sadaka na hivyo kusamehewa. Kwanjia hiyo pia, nguvu ya Mungu huwekwa juu ya mtu kwa mtu kwa tendo la kuwekewa mikono toka kwa mtumishi wake. Hivyo tendo la kuwekea mikono limechukua maana ya “kuhamisha, kutwika”.
Watu wanaojiita ni wenye vipawa (wanakarismatiki) hawawezi kamwe kusababisha mtu kuweza kuwa na Roho Mtakatifu ndani yake kwa njia ya kuwekea mikono, badala yake kusababisha watu hao kupokea roho chafu. Lazima ukumbuke kwamba mtu aliye na nguvu za roho chafu huamisha roho hizo kwa wengine kupitia tendo la kuwekea mikono. Mtu aliye tawaliwa na mapepo anapoweka mikono juu ya kichwa cha mwingine, pepo lililomo ndani yake huingia ndani ya mtu huyo kwa sababu shetani hutenda kazi kupitia wenye dhambi. Kwasababu hiyo basi kila mtu imemlazimu kuamini injili ya maji na Roho ikiwa anataka kupokea Roho Mtakatifu ndani yake. Shetani hutawala wale wote walio na dhambi hata ikiwa wanamwamini Yesu, huku wakiwa wameshindwa kupokea ondoleo la dhambi.
Ikiwa mtu atapokea tendo la kuwekewa mikono toka kwa mtu aliye na mapepo, mapepo hayo yatahamia juu yake mtu huyo, hivyo naye pia moja kwa moja ataweza kufanya miujiza ya uongo. Yatupasa kujua kwamba mapepo huja na kufanya makazi ndani ya mtu kwa kupitia tendo la kuwekewa mikono. Na kumpokea Roho Mtakatifu ndani huwezakana tu kwa imani katika injili ya maji na Roho.
Tendo la kuwekea mikono ni njia mahususi iliyo wekwa na Mungu katika kutwika kitu juu ya kingine. Lakini shetani husababisha watu wengi kupokea roho chafu kwa kupitia tendo hilo. Ukweli ni kwamba watu wengi nyakati hizi hujaribu kununua nguvu za Roho Mtakatifu kwa fedha na hivyo kufanya tatizo hili kuwa kubwa zaidi.
 

Wakristo wengi wanaufahamu wa kimakosa juu ya ukweli wa kuwa na Roho Mtakatifu ndani. 

Tulipouliza kwa namna gani wataweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani yao, wengi wa watu hujibu kwamba inawezekana kwa kupitia sala za toba na kufunga. Hili si kweli kabisa. Je, nikweli Roho Mtakatifu huja juu yako pale unapo fanya maombi maalumu kwa Mungu? Hapana kuweza kuwa na Roho Mtakatifu ndani yako huja kwa wale tu wanao amini injili ya maji na Roho.
Kwa kuwa Mungu ni kweli ameweka sheria kwa ajili ya kuweza kupokea Roho Mtakatifu ndani. Je, Roho Mtakatifu ataweza kuwa ndani ya mtu aliye na dhambi moyoni? Jibu bila shaka hapana. Mtu hawezi kumpokea Roho Mtakatifu kupitia tendo la kuwekewa mikono. Hata ikiwa mtu atahudhuria mikutano ya uamsho na maombi ya uchungu kwa Mungu ili aweze kupokea nguvu ya Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu atabaki kuwa mbali naye. Wenye dhambi hakika hawatoweza kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ndani yao. Wenye dhambi wataweza kupokea kipawa hicho cha Roho Mtakatifu ikiwa tu watapokea ondoleo la dhambi kwa kuamini Injili ya maji na Roho.
Yeyote asiyefahamu injili ya maji na Roho, kamwe hatoweza kumpokea Roho Mtakatifu. Siku hizi injili ya maji na Roho imeenea kwa kasi kupitia vitabu, mikutano ya makanisa, tovuti na hata vitabu vya kielectronikali ulimwenguni pote. Hivyo, yeyote anayetafuta ukweli wa injili, ataweza kuamini hili na kuweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani yake. Ikiwa bado hujampokea, yakupasa uelewe kwamba ili uweze kumpokea ni lazima uamini injili ya maji na Roho.
 

Mfano muhimu wa imani potofu.

Wakati tunapo pima dalili za watu wale wote waliompokea roho potofu tunaweza kuona kuwepo kwa mapepo dhahiri ndani yao. “Mikutano ya Uamisho wa Roho Mtakatifu” ni mojawapo ya mikusanyiko ambayo ni watu wanao taka kumpokea Roho Mtakatifu kwa kiu kubwa. Katika mikutano hii tunaona watu wakipiga makofi na kufanya maombi ya toba huku wakilia na kufunga. Mhubiri huwaelekeza kufanya maombi ya kishabiki kwa kuwaambia kwamba Roho Mtakatifu hatoweza kuja juu yao hadi pale watakapo piga makelele. Ndipo watu huita kwa kelele za ajabu “Bwana” na kuanza kuomba kwa jazba.
Je, watu wa aina hii wataweza kweli kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia hii? Hapana. Utaweza kuona watu wakiangua kilio na kelele huku wakianguka kifudifudi na kuanza kutetemeka, huku wakifanya kelele za ajabu katika mikutano ya aina hii. Wengine huangukia mgongo na kuanza kutetemeka wakiwa chini hapa na pale na tunaweza kuwaona wakipiga kelele na kuanza kunena kwa lugha. Wengine wataweza kulia kwa sauti wakati wote na ndipo umati wote unaingiwa na hisia. Wengine hupatwa na mfadhaiko wa kimawazo wakitetemeka mwili mzima huku wakinena kwa lugha. Watu husema mambo haya yasiyo ya kawaida ndiyo ushaidi kwamba Roho Mtakatifu amewashukia na kuwa ndani yao. Lakini hebu fikiri nini kinacho tokea pale pepo anapo fanya haya?
 

Shetani ana wadanganya Wakristo wengi

Shetani huwalaghai wakristo wengi nyakati hizi. Wakristo wengi huishi maisha ya aina hii ya kidini, ambayo ndiyo shetani apendayo. Shetani hudanganya watu kwa kuwambia kwamba imewapasa kupokea tendo la kuwekewa mikono toka kwa mtumishi mwenye nguvu ili waweze kumpokea Roho Mtakatifu, na hapo ndipo wakristo wengi huingia katika kuamini hili kama fundisho la msingi. Naye shetani hupandikiza wazo hili akilini mwa watu kwamba watapokea Roho Mtakatifu ikiwa watafanya maombi zaidi. Shetani amekuwa akijaribu kuzidisha mara mbili na zaidi, hata mara tatu idadi ya watu walio na imani ya aina hii.
Hivyo watu wengi hawajui, na hata hawajaribu kujifunza juu ya injili ya maji na Roho. Lazima tujishughulishe ili kuzuia mawazo ya shetani anayo weka katika vichwa vyetu na kuweza kufahamu na kuamini injili ya maji na Roho. Kuwa na Roho Mtakatifu ndani yako huja pale tu kwa wale wote watakao amini injili ya maji na Roho. Lazima uamini hili.
 

Upotofu wa wakristo juu ya kuwa na Roho Mtakatifu.

Kwanza kabisa, upo upotofu mkubwa katika imani ya wafuasi wa vipawa vya Kikristo (Wanakarismatiki). Wao hujaribu kumpokea Roho Mtakatifu wakiwa na dhambi moyoni mwao. Huamini kimakosa kwamba japokuwa wanadhambi mioyoni wataweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani yao. Hata hivyo mtu asiye na imani ya injili ya maji na Roho hatoweza kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu.
Pili, inasemekana kwamba upumbavu wa watu ndiyo unaowazuia kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Sasa basi je, hii inamaana kwamba mtu ataweza kumpokea Roho Mtakatifu ikiwa hato onyesha tabia ya kiburi? Je hakuna yeyote ulimwenguni asiye onyesha tabia ya kuburi hata kidogo? Mwenye kiburi asiyeweza kusamehewa na Mungu ni yule aongezaye mawazo binafsi katika neno la Mungu. Watu wengi wanao jaribu kumpokea Roho Mtakatifu ndani yao kwa kupitia njia zao binafsi, hudharau ukweli au Injili ya maji na Roho. Ingawa kuwa na Roho Mtakatifu ndani huja kwa wale tu wanao amini injili ya maji na Roho.
Tatu, inasemekana kwamba, kuwana Roho Mtakatifu ndani huja wakati mtu anapokiri dhambi zake zote kwa uaminifu mbele ya Mungu. Lakini kumbuka kwamba kuwa na Roho Mtakatifu ndani hakuji pale mtu anapo kiri dhambi tu. Wakristo wengi nyakati hizi, hutamani kuwa na Roho Mtakatifu ndani yao na kujazwa tele lakini inashindikana kwasababu bado wanadhambi mioyoni mwao. Hivyo basi mtu aliye na matamanio haya ya haraka huishia kutekwa nyara na mapepo.
Nne, baadhi husema kwamba, kuwa na Roho Mtakatifu ndani kutawezekana pale Mungu anapo shawishiwa kwa dhati ili kutupatia baraka hiyo. Lakini kipawa hiki hakiwezi kamwe kupatikana kwa kuomba, hii ni makosa.
Tano, baadhi hudhihirisha kuwa na Roho Mtakatifu ndani kwa nguvu za kiroho. Kunena kwa lugha huchukuliwa kuwa ni udhihirisho wa kumpokea Roho Mtakatifu. Lakini Roho Mtakatifu hakai ndani ya mioyo ya watu kwasababu tu ameweza kukemea pepo katika jina la Yesu au kunena kwa lugha. Dhambi ni ya shetani. Je, itawezekana kweli mtu aliye na dhambi moyoni kuweza kusema kuwa amempokea Roho Mtakatifu ndani yake kwasababu tu ameweza kuwa na nguvu za maajabu? Kwa maana nyingine, tabia hii ya ufedhuli hufanywa na mapepo.
Injili ya majina na Roho ambayo Yesu ametupatia ndiyo ukweli pekee ambao utakao tuongoza katika kumpokea Roho Mtakatifu ndani yetu. Ikiwa bado unadhani kwamba ataweza kumpokea Roho Mtakatifu na ondoleo la dhambi kwa kupitia njia nyingine basi hakika utakuwa umepotoka. Upo uwezekano kwako kujiweka huru toka imani potofu na hivyo basi uweze kuwa na mawazo ya kiroho na imani halisi.
Si jambo la uzushi pale inaposemekana kwamba wengi wa Wakristo katika nyakati hizi wametawaliwa na pepo. Wakristo wengi ulimwenguni hujikuta wakiwa chini ya pepo kwasababu hujaribu kuwa na Roho Mtakatifu ndani yao kwa kupitia mikutano maalumu ya uamsho au kwa kuwekewa mikono. Huwafuata watu fulani maalumu kama vile wasimamizi wa nyumba za maombi, mashemasi wakuu, wanauamsho au wachungaji wanaosemekana kuwa na nguvu za upako wa Roho Mtakatifu ndani kupitia aina hii ya imani huku wakiwa wana mwamini Yesu kwa dhati. Kwa maneno mengine hakuna yeyote zaidi ya Mungu awezavyo kusababisha mtu kupokea Roho Mtakatifu ndani.
Kama ilivyo kuwa kwa Simoni, watu wengi nyakati hizi hujaribu kumnunua Roho Mtakatifu. Hujaribu kumpokea Roho Mtakatifu ndani yao kwa kuamini mafundisho ya kidunia na siyo injili. Wakristo wengi duniani pote wamekwama katika mtazamo huu. Roho Mtakatifu huja kwa wale tu walio na viwango muhimu katika kumpokea. Njia pekee ya kumpokea Roho Mtakatifu ni kwa kuamini Injili ya maji na Roho, na hili ndilo jibu la ukweli (Matendo 2:38).
Kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia ya kuwekewa mikono kuliwezekana kwa muda mfupi na maalumu wakati wa kanisa la mwanzo. Baada ya hapo kumpokea Roho Mtakatifu ndani, huja juu ya watu katika muda huo huo pale mtu anapo jua na kuanini Injili ya maji na Roho. Hivyo, zaidi ya kazi ya Roho Mtakatifu itokanayo na imani ya neno la Mungu kazi nyingine ni za shetani. Mungu alisema kwamba mapepo ni watumishi wa shetani, naye anafanya ujanja kwa namna ya kwamba watu hawatoweza kupokea ondoleo la dhambi hata ikiwa wanamwamini Yesu. Shetani hulaghai watu kwa kuwaambia kwamba atawapatia Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono. Shetani hupanua ufalme wake duniani pote kwa njia ya ujanja.
Tuangalie dalili za wale wote waliokumbwa na pepo. Kwanza, tunapo chunguza dalili za kupagawa na mapepo kwa wapiga bao au “shama” tunaona kwamba huwa na tabia za kutetemeka, kuzimia na hata kuanguka. Pia ndimi zao huanza kucheza cheza na huku maneno yasiyo ya kawaida huwatoka kinywani pasipo kujielewa. Hunena kwa lugha ngeni.
Wote, wachawi na wanaojiita Wakristo walio pagawa na mapepo kupitia kuwekewa mikono wote kwa pamoja hupatwa na mambo haya. Wale watu wa uamsho walio na vile viitwavyo vipawa utawakuta wakishika vipaza sauti na kupiga kelele, “Kwa moto, kwa moto, kwa moto” ndipo waumini huanza kupanda mori na kupoteza fahamu. Wale wote wenye kupenda kuwekewa mikono na watu wa aina hii hukimbilia haraka sana mbele. Hukumbwa na hali ya kutetemeka na kunena kwa lugha. Dalili hizi ni kazi ya pepo ajifanyaye kuwa ndiye Roho Mtakatifu akifanya kazi.
Watu walio kumbwa na roho za shetani ambazo zinaweza kuaguliwa na “shama” au wapiga ramli toka katika kila aina za dini za kifukara, huonyesha dalili kama zile za Wakristo walio na mapepo kupitia tendo la kuwekewa mikono. Hata hivyo watu hawaelewi juu ya hili ingawa upo ushahidi kama huu. Wakristo hawa wamejipachika katika lindi la kuchanganyikiwa kwasababu wao hudhani kuwa wamempokea Roho Mtakatifu pale walipo patwa na aina fulani ya dalili za hisia na matendo ya nje.
 

Shetani hutenda kazi kwa kupitia Wakristo kama mpiga ramli. 

Shetani humwezesha mtu aliye kumbwa na pepo kufanya maombi ya kinabii. Watu hawa hutoa unabii wakati mwingine kwa kusema “utakuwa Kiongozi mzuri maelfu ya kondoo watachungwa nawe Mungu utakufundisha hapo mbeleni na kukufanya kuwa kiongozi mzuri”. Kwa wengine huwaeleza maneno ya kilaghai “Utakuwa mtumishi mzuri wa Mungu utaheshimika sana na Mungu” yote haya ni kumpa moyo mtu kuweza kuyafuatilia na kuishi akiwa kama mtumishi wa mapepo maishani mwote.
Watabiri pia hutoa unabii juu ya siku za mbeleni katika maisha ya watu “Inakubidi uwe mwangalifu sana na maji”, au “siku zijazo utapata fedha nyingi” “Mtu wa heshima ata kujia akitoka mashariki ili kukusaidia” Hii ni mifano ya mambo ambayo watabiri husema. Dalili zinazo jitokeza kwa mtu aliye kumbwa au kutawaliwa na mapepo ni kutoa unabii wa uongo.
Ndipo hunena kwa lugha kiasi cha kushindwa hata wao wenyewe kujitambua. Hupatwa na hali ya kutetemeka ambayo ni dalili ya kukosa kujitawala. Ukimwona mtu aliye wa “shama” au mpiga ramli (mtabiri), je ataweza kung’amua juu yao kuwa na utu? Mara nyingine huwa na maneno ya hasira kwa watu walio wakubwa kiumri zaidi yao.
Hata hivyo, watu walio na Roho Mtakatifu ndani yao ndiyo ambao wamempokea kwa kuamini ukweli wa Kibiblia unaosema kwamba Yesu amesafisha dhambi kwa kupitia ubatizo wake na kifo chake msalabani. Watu hawa pia husaidia wengine kujua na kuamini Injili ya maji na Roho ambayo huwasaidia kupokea ondoleo la dhambi na kipawa cha Roho Mtakatifu. Wao binafsi hujaribu kuishi katika njia za haki na utu wao ni wa kuridhisha na kuonekana. Huwaongoza wengine katika baraka ya imani ya Mungu na katika aina ya maisha Mungu anayo waitaji. Hata sasa au baadaye Mungu huwarudisha kwa upole ili wawe wateule pale akili zao zinapojaribu kurudi ulemwenguni.
Wenye haki ambao wamepokea ondoleo la dhambi kwa hakika huwa ni tofauti na watu ambao utu wao umeharibiwa na roho za shetani. Utu wa kweli hujitokeza kwa mara nyingine, ikiwa mtu atapokea ondoleo la dhambi na hivyo kumpokea Roho Mtakatifu ndani yake. Kwa nyongeza wenye haki hupatwa na wasi wasi mkubwa juu ya wengine wasio na mazingira mazuri ya kile wanacho hitaji katika neno la Mungu, kuwaombea na hata kujitoa nafsi zao kwa kuwasaidia.
Kwa upande mwingine, tunaweza kuona kwamba utu wa yule aliye kumbwa na mapepo unakuwa umeharibiwa vibaya. Shetani hushika hatamu na hata kuwalazimisha watu wa aina hii kufuata mapenzi yake kwa sababu hudhani mambo kama kutetemeka na kunena kwa lugha ni vipawa vya Roho Mtakatifu. Hata hivyo hali ya kupatwa na mambo kama haya na mengine ama kwa hakika si vipawa vya Roho Mtakatifu.
Wapo watumishi wengi wanao jivunia juu nguvu au upako kama vile kutoa unabii kwa jina la Mungu, kuwa na uwezo wa kufanya miujiza na kunena kwa lugha. Lakini haya yote ni bure ikiwa ndani yao wanaendelea kuwa na dhambi moyoni, ni ushuhuda wa ulaghai wao na uhakika kuwa wanapepo ndani yao. Hivyo basi kamwe hawawezi kumwongoza yeyote kuweza kumpokea Roho Mtakatifu bali zaidi atawezesha kuwapa pepo wachafu ndani yao. Pia kwa kuwa shetani ni mlaghai miujiza wanayofanya huisha mara moja katika muda mfupi.
Ipo tafauti ya wazi kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na pepo. Ingawa inaweza kuonekana kwamba kazi ya Roho Mtakatifu haina aina fulani ya mwonekana wa nje au karama ya ajabu kwa awali, kwa kadiri muda unavyo kwenda nguvu ya Mungu hukua ndani ya moyo wa mwenye haki kama machweo ya jua wakati wa asubuhi.
 

Wakristo walio na mapepo

Kwa nini watu wengi hujikuta 
wakipatwa na mapepo ingawa wanajaribu 
kumpokea Roho Mtakatifu?
Kwa sababu hupokea mapepo kupitia tendo 
la kuwekewa mikono toka kwa 
manabii wa uongo.

Cha ajabu, tunaweza kuona wengi wa wanao mwamini Yesu ambao miili yao na roho zao huangamia kwasababu hupokea mapepo kwa kupitia tendo la kuwekewa mikono toka kwa manabii wa uongo. Watu wa aina hii hawana maana mbele za Mungu kwani imani zao haziendi sambamba na maneneo ya biblia. Hujishughulisha na kutumia nguvu zao bila ya kujua kwamba huduma yao inasababisha watu wengi kuwa watumishi wa shetani. Kwanini basi watu hawa hujishughulisha sana kuonyesha nguvu zao katika Ukristo? Kwasababu hiki kinachoitwa nguvu baada ya muda kitakwisha ikiwa wataacha kutumia. Na ndiyo maana huwa katika hali ya kushughulika sana.
Huendelea kufanya maombi na kufanya miujiza na ishara kwa jina la Yesu. Watu wanaosema “nimepokea karama ya kuhubiri injili” ndipo inapo walazimu kuendelea kuhuburi injili kwasababu kwa kutofanya hivyo, furaha yao bandia itaweza kuyeyuka. Ikiwa watu wa aina hii hawawezi kuwa waaminifu kwa karama hizo za pepo za kunena kwa lugha na uponyaji au unabii kwa maneno mengine siyo waaminifu kwa kazi za shetani na hivyo wakati mwingine huwafanya kuwa wadhaifu kwa maradhi pale wanapo acha utumishi wa shetani. Ndiyo maana inawasababisha kutumia vipawa wanavyo pokea kwa shetani kwa dhati kabisa ili wasije kukumbwa na balaa baada ya kuzoea kutumikia nguvu hizo.
Zamani nilimfahamu mtu fulani aliyekuwa muumini mzuri tu wa Yesu na alikuwa kama mwenye nguvu nyingi za Mungu. Aliwaasa watu kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu na aliongoza mikutano ya uamsho ambamo alikemea mapepo kwa kuwekea mikono watu na pia kufanya miujiza kama vile kunena kwa lugha na uponyaji. Alionewa wivu sana na kuheshimiwa kwa kazi zake za miujiza. Maelfu ya umati wa waumini walimfuata. Hata hivyo punde alipo anza kumkana Yesu kwa kusema “Yesu Kristo ameshindwa si Mwana wa Mungu.” Alimtusi Yesu Kristo hata kudai kuwa yeye binafsi ni Mungu. Mwishowe alimuua Yesu Kristo moyoni mwake na katika mioyo ya Wakristo wengi.
Watu kama hawa hupinga Injili ya maji na Roho kwa sababu, shetani huwaongoza. Hutokea kwamba wamekuwa na imani potofu toka mwanzo kwa kuwa wana maono potofu kwa kujiona kuwa wana nguvu sawa na Mitume kwa kujiona uwezo wao wa kufanya watu kunena kwa lugha, kukemea pepo kwa kuwawekea mikono, basi wanaamini kwa dhati kuwa Roho Mtakatifu yupo juu yao.
Huwafundisha watu juu ya kanuni na njia za kuweza kumpokea Roho Mtakatifu wakidhani kuwa inawezekana kumpokea kwa kufanya sala za toba. Hata hivyo njia hii za kumpokea Roho Mtakatifu haziko katika msingi wa neno la Mungu. Badala yake husema kwamba ikiwa wanao mwamini Yesu wakinena kwa lugha na kufanya unabii basi huo ndiyo ushahidi wa kumpokea Roho Mtakatifu katikati yao. Kwa sababu hiyo watu wengi hawaelewi ile kweli juu ya kumpokea Roho Mtakatifu ndani, hivyo kupelekea kuamini kwamba wataweza kumpokea kwa tendo la kuwekewa mikono na kufuata mafundisho ya manabii waongo. Hivyo ndivyo shetani ameweza kuwajaza Wakristo wengi na roho za pepo na hata kuwatawala watu hao. Njia hizi zote ni mitego ya shetani.
Idadi ya watu wengi wanaweza kupatwa na pepo kwa kupitia mafundisho ya mitume hawa waongo. Waumini wa kawaida huishi maisha ya kupumbaa kidini nahivyo kutumia nguvu za roho za shetani hata kuonekana kuwa na upenzi wa maisha ya kidini. Je huonyesha uwezo gani? Wanauwezo wa kuponya, kunena kwa lugha na hata kuongoza wengine katika kupokea mapepo ndani yao kwa kuwawekea mikono. Yatupasa kuelewa kuwa tendo la kuwekea mikono ni njia mahususi katika kugawia au kuwekea kitu juu ya kingine, na katika mamlaka za kipepo njia hii imekuwa ndiyo pekee katika kupanua mamlaka yao.
 

Roho za shetani hutenda kazi kwa kupitia tamaa za watu!

Shetani hutenda kazi ndani ya watu kama Simoni katika kurasa iliyopita. Watu hawa husema kuwa wamempokea Roho Mtakatifu kwa kupitia tendo la kuwekewa mikono wakiachilia mbali imani katika Injili ya majina Roho. Nyakati hizi watu wengi wamedanganyika na shetani na kujaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa kupitia sala za toba kufunga, kujitolea nafsi au kuwekewa mikono. Hata hivyo wanakuwa wamekumbwa na mapepo na hata kuishi maisha ya kivita wakati wote.
Yatupasa kuelewa vyema viunganishi hivi kama vile tendo la kuwekewa mikono ambalo Wakristo hupokea duniani pote hufanikisha kazi za shetani. Watu hawa walio na mwelekeo sawa na Simoni ni manabii waongo mbele ya Mungu. Hata wale waumini wa Yesu ikiwa nao watakuwa na dhambi moyoni ni rahisi kwao kukumbwa na mapepo. Watu hawa wataweza pia nao kutenda miujiza kupitia kazi za shetani kwa kuwafanya watu wengine kupokea roho za pepo kwa tendo la kuwekea mikono na hivyo kupanua ufalme washetani duniani pote. Nyakati hizi Makanisa ya Vuguvugu la Karama za Kipentekoste 2 pentecostal –Charismaatic Movement ya metambulika rasmi kama ni moja wapo ya madhehebu ya Kikristo duniani pote.
 
2 Ukristo wa Magharibi ulianza kuyumba kwa kutumaini mafanikio ya kimali na matumizi yake mwanzoni mwa nusu ya karne ya 20. Kwa wakati huo pia, matokeo haya, Wakristo wengi waliokuwa wakitafuta njia ya kutembea karibu na Yesu hawakuridhika na ukame uliomo ndani ya Makanisa yao ya awali, Wengine waliteseka kwa kukosa au kuwa na amani ya Kiroho inayokuwa kwa taratibu, na pia wengine walichanganyikiwa kwa kushindwa kutafsiri Imani yao katika upendo kibinafsi na Yesu. Vuguvugu lijulikanalo kama Karama za Kipentekoste – Pentecostal – Christimatic Movement, lilichipuka katika mazingira haya. Wale wote waliojihusisha na vuguvugu hili walitafuta kuwa na tabia ya ushabiki na kufanya mambo kama vile kunena kwa lugha, kutoa unabii, kufanya miujiza na maajabu wakitamani tukio lile la Pentekoste ya kwanza. Kwa ushabiki huo wao walikuwa radhi kujitoa katika mamlaka iliyodhaniwa kuwa ni ya Roho Mtakatifu, lakini kwa kusema kweli mafundisho yao mengi na nyendo zao hazikuhusika katika biblia.
Katika nchi za mataifa yalioendelea, vuguvugu hili lilikuwa kwa kasi kulingana na mahitaji ya watu. Viongozi wa watu hawa aliwavutia Wakristo katika nchi zinazoendelea kwa baraka za utajiri wa mali na afya pamoja na ushabiki wa kidini. Vuguvugu nyingine zilizojitenga kama vile Upentekoste wa Kisasa (Neo-Pentecoste) imesikika kuwa wana uhusiano wa mafundisho na Vuguvugu la Nyakati za Kisasa (New Age Movement).
 
Ulimwengu huu unafikia kikomo taratibu. Ikiwa tunataka kuzaliwa upya mara ya pili katika nyakati hizi za mwisho, yatupasa kuelewa ni kwa namna gani shetani anafanya kazi na kusimama kidete dhidi ya mbinu zake. Pia yatupasa kuokolewa toka dhambini mara moja na kwa wakati wote hata kuweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani ikiwa ni zawadi kwa kuamini Injili ya maji na Roho. Lazima turudi katika ile kweli kwa maarifa yaliyo kamili namna Roho wa Mungu anavyoweza kuwa ndani yetu.
Kama Mungu alivyosema “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” (Hosea 4:6) siku hizi wanaotafuta ukweli huangamia kutokana na upumbavu wao, ambapo watu wenye kujiita wanavipawa (Charistmatic) huwapotosha. Watu husema kwamba hata Makanisa yanayoitwa ya kiroho - ya karama za Kipentekoste yakianzishwa jangwani bado watu watakusanyika. Kwa nini iwe hivyo? Watu wanaojiita wenye karama hutumia makanisa yao kwa kuwachanganya wengine kwa nguvu au upako wao wa bandia hata kuwafanya wapatwe na mapepo kwa kuwawekea mikono. Moja ya karama zao mahususi ni kwamba, punde mtu anapopatwa na mapepo kwa kuwawekea mikono, huishia kuwa na ushabiki wa kupenda kuishi maisha ya kidini.
Dalili nyingine za watu wanaojiita wenye vipawa na upako ni kwamba huchangia kiasi kikubwa cha fedha katika makanisa yao na bila sababu hata hufikia hatua ya kuwa muumini mkereketwa. Hata baadhi ya wakristo ni wakereketwa katika Uinjilisti kwa nguvu za mapepo, lakini bila shaka nao watakwenda motoni pasipo kuelewa mwisho wao. Watu hawa, kwa dhati huamini nguvu za shetani kama ushuhuda wa wokovu wao, na hutarajia kwenda mbinguni, pasipo shaka hata kidogo. Hata hivyo wanadhambi mioyoni mwao na wataangamia.
Ikiwa wataulizwa swali lifuatalo “Je, bado unadhambi moyoni mwako, ingawa unamwamini Mungu?” kwa uhakika watajibu kwamba ni kawaida kwao kuwa na dhambi. Hudhani kwamba haiwezekani kwa mtu kutokuwa na dhambi moyoni, hata ikiwa unamwamini Yesu.
Watu hudhani kwamba wanastahili kuingia Ufalme wa Mbinguni hata kama bado wana dhambi mioyoni mwao, kwa sababu huwa na hisia ya amani katika kumwamini Yesu kwa kuwa wana ushuhuda wa nguvu ambazo ni za bandia.
Ama kweli tumaini hili ni la kipuuzi kabisa! Sababu ya msimamo wa imani yao ni kwamba wana aina fulani ya nguvu za miujiza ndani yao. Wamekwisha jiona kuwa wanauwezo wa kunena kwa lugha, kuwa na maono na kuponya wagonjwa na hivyo kudhani na kuamini kwa msimamo juu ya mambo haya kuwa ni kazi ya Roho Mtakatifu. Hivyo hujiambia nafsini mwao kwamba bila shaka wamempokea Roho Mtakatifu pamoja na Mkombozi.
Kutokana na kupatwa na mambo hayo kwa watu hawa wana maarifa yasiyo kamili juu ya maneno ya wokovu, hawana uhakika katika wokovu wao endapo hawaoni uwezo wowote kwa macho ndani yao. Hivyo watu wa aina hii hujaribu kwa bidii hatimaye huishia kutumiwa na shetani katika kazi zake. Kwa sababu watu hawa huangaika kutafuta majibu ya Mungu kupitia sala za toba au kujitolea nafsi zao badala ya kuamini Injili ya maji na Roho, ghafla kuishia kupokea roho za shetani badala ya Roho Mtakatifu.
Shetani hushitaki watu kwa kuwanongoneza katika masikio yao “umetenda dhambi, je si kweli?” na kuwafanya waanguke katika kujihukumu. Yupo mtu fulani niliye mfahamu ambaye kwa sasa amepokea ondoleo la dhambi na Roho Mtakatifu. Hili ni jambo lililomtokea kabla ya kuzaliwa upya mara ya pili alipo kuwa muumini wa dhati kwa Yesu lakini alikuwa si mwangalifu. Mtu huyu alifikia hata kunena kwa lugha na kufanya miujiza. Ingawa alipaza sauti huku akifanya sala za toba usiku kucha. Ingawa alimwamini Yesu dhambi zilizomo moyoni mwake ziliendelea kumtesa. “Hapa umetenda dhambi hivyo ni vyema ufe kuliko kuishi”. Shetani mara nyingine alimjia na kumhukumu, kumtesa na hata kumkumbushia dhambi zake za nyuma. Shetani alimwingiza katika hali ya kujishutumu na kujihukumu. Hata hivyo alichoweza kukifanya ni kukiri dhambi moyoni mwake. Hakuweza kujiweka huru tokana na hukumu hizo za shetani hadi pale alipokuja kusikia na kuamini injili njema.
Yakupasa ujue kwamba wale wasiyo amini injili ya maji na Roho huwa mara zote ni mawindo ya shetani. Je unadhani yeyote ambaye hajapokea ondoleo la dhambi anaweza kuwa na nguvu ya kumkataa shetani? Yeyote asiye kumbatia ukweli wa injili ya maji na Roho ataweza kukamatwa na kuteswa na shetani. Injili ya maji na Roho ambayo ni ya Mungu hakika ndiyo muhimu kuweza kumkemea na kumwondoa shetani. Hivyo yeyote anayeamini juu ya Yesu ni lazima aweze kuamini Injili hii ya maji na Roho na pia kuihubiri kwa watu wote ulimwengu. Wale wote wanao sikia hili imewapasa kutii na kuamini.
 

Maajabu ya mtenda uovu tayari yapo ulimwenguni yakitenda kazi!

Ulimwengu wote leo hii umegubikwa na shughuli za mapepo. Ikiwa tunataka kuhubiri Injili ambayo itawaongoza watu kumpokea Roho Mtakatifu yatupasa kuondoa kabisa kina cha upotofu juu ya kumpokea Roho Mtakatifu ndani.
Kabla ya yote yatupasa kuweka bayana kwamba ni uongo mkubwa kusema kwamba Roho Mtakatifu huja kwa kupitia tendo la kuwekewa mikono, yatupasa kuthibisha kwa awali kwamba matukio kama yale ya “kunena kwa lugha baada ya kuwekewa mikono, kuhisi joto kwa kupitia kutubu na kufunga na kusikia ujumbe wa moja kwa moja toka kwa Yesu” ni kazi za shetani. Ni kwa imani tu katika Injili ya maji na Roho ndipo watu wataweza kukombolewa toka katika mitego ya shetani. Ni kwa imani tu ndipo tutakapo okolewa kwa dhambi zetu kupitia Injili ya maji na Roho.
Ni lazima tumshinde shetani “baba wa uongo” kwa Injili ya maji na Roho. Shetani amewafunga watu wengi ulimwenguni kwa kongwa la kujihukumu, hivyo inatupasa kuwarudisha watu hawa kwenye ukweli kwa kuwafanya wagundue na kuelewa kwamba matukio ya udanganyifu pamoja na hisia zao ni mojawapo ya uongo wa shetani.
Nyakati hizi watu walio kama Simoni Msamaria aliyetamani kumnunua Roho Mtakatifu kwa fedha ndiyo hao wanahudumia makanisani. Ni vipofu wanaongoza vipofu. Kamwe hawawezi kuwaonyesha watu juu ya wokovu wa kweli na ulio kamili kwa sababu hawaifahamu Injili ya maji na Roho na bado ndani ya mioyo yao wana dhambi. Hivyo wanachofanya ni kusababisha shetani kuweka makazi ndani ya mioyo ya wafuasi wao kwa kushikilia maombi ya usiku kucha kuitisha sala za kutubu na kutumia tendo la kuweka mikono watu. Watu hawa kusema kweli wamekuwa na mapepo ndani yao, na ikiwa tunahitaji wao warudi katika neno la Mungu yatubidi tuziharibu kazi za shetani kwa kuwahubiria habari ya kweli juu ya maji na Roho. Ikiwa watu hawaelewi juu ya mikakati ya shetani hapatokuwa na jinsi zaidi ya kuteseka pasipo msaada wowote.
Kama nilivyosema hapo awali, kufanya miujiza kama vile kunena kwa lugha na kutumia unabii baada ya kuwekewa mikono hizi zote ni kazi za shetani. Kwa maneno mengine, nguvu walizonazo watu anaojiona ni wenye vipawa (Karismatiki) hujionyesha kwa kupitia kazi za shetani. Yatupasa kuwaelekeza kwa upole “Ni shetani ndiye atendaye kazi yako ikiwa bado unadhambi moyoni. Kama unadhani Roho Mtakatifu yumo ndani yako, hata kama unadhambi ndani ya moyo wako, basi umedanganyika ndugu”.
Imani za Mitume na za watu wale wote waliopokea tendo la kuwekewa mikono katika ujumbe mkuu wa Matendo 8 imewekwa katika tabaka moja, kwa kuwa wote hawa walikuwa wamekwishajuwa Injili ya Yesu Kristo, Injili ya maji na Roho. Lakini Imani ya Mitume ilikuwa ni tofauti kabisa na hii ya Wakristo wengi wa nyakati hizi ambao wao huamini tendo la kuwekewa mikono ndilo linalowasabisha kuweza kumpoke Roho Mtakatifu.
Je, mtu humpokea Roho Mtakatifu, kwa kupitia tendo la kuwekewa mikono na mtu ambaye amepokea ondoleo la dhambi? Kamwe Biblia inasema kwamba “Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji” (Mwanzo 1:2). Hii ina maana kwamba ili mtu aweze kupata ondoleo la dhambi na Roho Mtakatifu, ni lazima aisikie na kuiami Injili ya Maji na Roho. Mungu amemtuma Roho Mtakatifu kama kipawa kwa Wakristo walio zaliwa upya mara ya pili, ambao wanaamini Injili ya Maji na Roho.
Yatupasa kukumbuka kwamba itakuwa nisawa na kupinga Injili ya maji Roho, ambayo Mungu aliikusudia katika kutuokoa sote toka dhambini ikiwa tutawafundisha watu juu ya kutafuta kuwekewa mikono ili kupokea Roho Mtakatifu. Kwa kudhani kwamba mtu ataweza kumpa mwingine karama hii ni sawa na kumpinga Mungu, na watu walio na aina hii ya imani ni rahisi kwao kunaswa na mtego wa shetani. Jambo hili lisiruhusiwe kabisa.
Dhambi zetu zote husamehewa pale tunapoiamini Injili ya maji na Roho, na ndipo basi Roho Mtakatifu hushuhudia juu ya hili kwa wale ambao wanaoamini Injili ya maji na Roho kuwa hawana tena dhambi mioyoni mwao. Hii haina maana kwamba hatotenda dhambi tena, lakini badala yake ni kwa sababu anaamini nguvu iliyo katika Injili ya maji na Roho. Injili ya maji na Roho hushuhudia kwamba yeye hana tena dhambi moyoni, naye Roho Mtakatifu hushuhudia hili pia. Mtu hawezi kumwita Yesu kuwa ni mwokozi wake pasipo kuwa na Roho wa Mungu ndani yake.
Watu walio na mapepo hawajui lolote juu ya Injili ya maji na Roho, na kamwe hawawezi kuiweka Injili kuwa ndiyo mazungumzo yao rasmi. Hawajui kamwe juu ya Injili ya maji na Roho, na cha zaidi hawawezi kuwa na utambuzi wa ukweli. Husema kwamba Roho Mtakatifu huja juu yao pale tu wanapofanya na kupokea tendo la kuwekewa mikono. Hata hivyo Roho Mtakatifu kamwe haji kwa kupitia tendo la kuwekea mikono. Yakupasa uelewe kwamba kazi za shetani nyakati hizi hufanyika kwa ushawishi mkubwa juu ya watu makanisani ulimwenguni pote kupitia mafundisho ya uongo kama haya. Kwa sababu hiyo, ni muhimu kumpokea Roho Mtakatifu ndani kwa kuamini Injili ya maji na Rohotu.