Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 7-6] Tumsifu Bwana, Mwokozi wa Wenye Dhambi (Warumi 7:14-8:2)

(Warumi 7:14-8:2)
“Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi. Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”
 

Mwanadamu ni Mwenye Dhambi Aliyerithi Dhambi
 
Wanadamu wote walirithi dhambi toka kwa Adamu na Hawa na wakafanyika kuwa mbegu ya dhambi. Hivyo sisi ni viumbe wenye dhambi. Kwa asili tunazaliwa kama uzao wa dhambi na hivyo tunajikuta ni viumbe wenye dhambi. Watu wote duniani hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kuwa wenye dhambi kwa sababu ya baba yetu wa kwanza Adamu ingawa hakuna yeyote anayetaka kuwa mwenye dhambi. 
Je, asili ya dhambi ni nini? Inarithiwa toka kwa wazazi wetu. Tunazaliwa na dhambi katika mioyo yetu. Hii ndiyo asili ya kurithi dhambi kwa wenye dhambi. Tuna aina 12 za dhambi ambazo tunazirithi toka kwa Adamu na Hawa. Dhambi hizi ni —uzinifu, umalaya, uuaji, wizi, tamaa, ubaya, uovu, ufisadi, jicho ovu, machukizo, majivuno, na ujinga—dhambi hizi zimo ndani ya mioyo yetu tangu wakati tunapozaliwa. Asili ya msingi ya mwanadamu ni dhambi. 
Hivyo sisi tunazaliwa na aina kumi na mbili ya dhambi. Hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kukiri kuwa sisi ni wenye dhambi kwa sababu tunazaliwa na dhambi katika mioyo yetu. Mwanadamu anazaliwa akiwa na dhambi na hawezi kuikwepa dhambi kwa mtu huyo ana dhambi ndani yake hata kama mtu huyo hafanyi dhambi katika maisha yake yote. Mtu anakuwa mwenye dhambi kwa kuwa anazaliwa na dhambi katika moyo wake. Hata kama hatufanyi dhambi kwa miili yetu bado hatuwezi kukwepa kuwa wenye dhambi kwa kuwa Mungu anaangalia ndani ya moyo. Hivyo wanadamu wote ni wenye dhambi mbele za Mungu. 
 

Mwanadamu Anatenda Dhambi ya Uhalifu
 
Mwanadamu pia anatenda dhambi ya uhalifu. Mwanadamu anatenda dhambi kwa mwili hali akiichanusha ile dhambi ya asili toka ndani. Sisi tunaziita dhambi hizi “maovu” au “uhalifu.” Dhambi hizo ni makosa yaonekanayo katika tabia zetu za nje ambayo yanatokana na zile aina kumi na mbili za dhambi zilizo ndani ya mioyo yetu. Dhambi itokayo ndani inamfanya mwanadamu kutenda matendo maovu na hivyo inawafanya wanadamu wote kuwa wenye dhambi pasipo shaka. Mwanadamu haonekani kuwa ni mwenye dhambi hasa pale anapokuwa bado ni kijana mdogo. Kwa kawaida dhambi haionekani ndani ya mtu anapokuwa bado ni mdogo, ni kama ambavyo mti wa hiriki usivyoweza kuzaa matunda unapokuwa bado mdogo. Lakini dhambi inaanza kujitokeza zaidi na zaidi kadri tunavyozidi kuwa wakubwa na ndipo inapofikia hatua ya kufahamu kuwa sisi ni wenye dhambi. Dhambi hizi tunaziita maovu au uhalifu na ni dhambi ambazo zinatendwa kwa kupitia tabia zetu. 
Mungu anasema kuwa hizi zote ni dhambi. Dhambi katika mioyo na matendo maovu ya miili yetu yote ni dhambi. Mungu anamwita mwanadamu kuwa ni mwenye dhambi. Dhambi zote zinajumuishwa katika dhambi za moyo na katika dhambi za tabia. Hivyo, watu wote wanazaliwa wakiwa ni wenye dhambi mbele za macho ya Mungu bila kujalisha kuwa wanatenda dhambi katika tabia zao au la. 
Wasioamini wanasisitiza kuwa kwa asili mwanadamu anazaliwa akiwa mwema na kwamba hakuna mtu anayezaliwa akiwa mwovu. Lakini Daudi alikiri mbele za Mungu, “Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako, Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu. Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani” (Zaburi 51:4-5). Kifungu hiki kina maanisha kuwa, “Mimi siwezi kufanya lolote zaidi ya kutenda dhambi kama hivi, kwa kuwa kwa asili mimi ni mbegu ya dhambi. Mimi ni mwenye dhambi mkubwa. Hivyo, ikiwa utazichukulia mbali dhambi zangu basi ninaweza kukombolewa toka katika dhambi zangu zote na kuwa mwenye haki. Lakini ikiwa hutazichukulia mbali dhambi hizo nitapaswa kwenda kuzimu. Ukisema nina dhambi, nitakuwa na dhambi. Lakini kama ukisema sina dhambi, basi nitakuwa sina dhambi. Kila kitu kinakutegemea wewe Mungu na hukumu zako.” 
Tukiongea kwa mkazo, wanadamu wote hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuwa wenye dhambi mbele za Mungu kwa sababu wamerithi dhambi toka kwa wazazi wao. Wanadamu wanazaliwa wakiwa ni wenye dhambi bila ya kujalisha tabia zao. Njia pekee ya kuweza kuiepuka dhambi ni kuamini katika wokovu wa Yesu. Elimu ya jamii inawafundisha watoto wetu madai ya uongo ambayo yanaweza kuelezwa kwa ufupi kama ifuatavyo: “Kwa asili watu wote wanazaliwa wakiwa wazuri. Na hivyo wanaishi kwa uadilifu kulingana na mazingira mazuri ya wanadamu. Unaweza kutenda mazuri ikiwa utajaribu kufanya hivyo.” Wao wanazungumzia mambo mazuri tu. Wanadamu wanaishi chini ya mafundisho ya kanuni za kimaadili. Lakini kwa nini wanatenda dhambi katika mioyo yao au kwa miili yao katika jamii au nyumba wanazoishi? Wanatenda hivyo kwa sababu kwa asili wamezaliwa na dhambi. Wanadamu wanazaliwa kama mbegu ya dhambi. Mwanadamu hawezi kufanya lolote zaidi ya kutenda dhambi ingawa mwanadamu huyo anataka kutenda mema. Hii inathibitisha kuwa sisi tunazaliwa hali tukiwa na dhambi. 
 

Ni Lazima Ujifahamu Wewe Mwenyewe
 
Watu hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kutenda dhambi kwa mwili katika kipindi chote cha maisha yao kwa kuwa wamezaliwa wakiwa na dhambi. Hii ndiyo hali ya asili ya mwanadamu—ni lazima kwanza tujifahamu sisi wenyewe. Sokrato anasema, “Jifahamu Mwenyewe!” Na Yesu alisema, “Ninyi ni wenye dhambi kwa kuwa mlitungwa mimba katika dhambi na kisha mkalelewa katika maovu. Hivyo ni lazima upokee msamaha wa dhambi.” Jifahamu Mwenyewe. Watu walio wengi wanajielewa vibaya. Watu wengi sana wanaishi na kisha kufa pasipo kujifahamu wao wenyewe. Ni watu wenye busara tu ndio wanaojifahamu wao wenyewe. Wale wanaoufahamu na kuuelewa ukweli wa Yesu na wanaojitambua kuwa wao ni mbegu za watenda maovu hao ndio wenye busara. Watu hao wana haki ya kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. 
Wale wasiojifahamu wao wenyewe wanawafundisha watu kufanya unafiki na kutotenda dhambi tena. Wanawafundisha watu kutojielezea juu ya dhambi zilizo ndani yao. Wakufunzi wa dini wanawafundisha wao kutotenda dhambi na kuzifunika dhambi zao kila zinapojaribu kuwasukuma. Watu hao wapo katika safari ya kuelekea kuzimu. Watu hao ni akina nani? Ni watumishi wa shetani na wachungaji wa uongo. Kile wanachokifundisha si kile ambacho Bwana wetu alitufundisha. Kwa kweli Bwana wetu hakutufundisha sisi kutenda dhambi. Lakini anatueleza sisi kuwa, “Mna dhambi, ninyi ni wenye dhambi, na mshahara wa dhambi ni mauti. Mnaelekea katika maangamizi kwa sababu ya dhambi zenu. Hivyo ni lazima mkombolewe toka katika dhambi. Pokeeni karama ya wokovu itakayowaokoa ninyi toka katika dhambi zenu zote. Kisha dhambi zenu zote zitasamehewa na mtapokea uzima wa milele. Mtafanyika kuwa wenye haki, watakatifu wenye thamani na wana wa Mungu.” 
 

Kwa Nini Mungu Aliwapatia Wanadamu Sheria?
 
Paulo alisema, “Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi” (Warumi 5:20). Mungu alitupatia Sheria ili kwamba kwa kupitia Sheria hiyo dhambi zetu ziweze kufunuliwa jinsi zilivyo na dhambi zaidi (Warumi 7:13). Mungu aliwapatia wenye dhambi Sheria ili kwamba waweze kuzitambua dhambi zao kwa umakini. 
Mungu aliwapatia Waisraeli Sheria wakati wana wa Yakobo walipokuwa wakiishi jangwani baada ya kutoka Misri. Mungu aliwapatia aina 613 za amri. Kwa nini Mungu aliwapatia wanadamu Sheria? Kwanza, Mungu aliwapatia Sheria kwa sababu alitaka wazitambue dhambi zao, na pili ni kwa sababu wanadamu wanazaliwa wakiwa na dhambi. 
Amri kumi za Sheria zinaonyesha jinsi wanadamu walivyo na dhambi kubwa. “Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga..., Usilitaje bure jina la BWANA Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase... Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako. Usiue, Usizini, Usiibe, Usimshuhudie jirani yako uongo. Usitamani nyumba ya jirani yako... wala chochote alicho nacho jirani yako” (Kutoka 20:3-17).
Mungu alitupatia sisi sote Sheria na kwa kupitia sheria hiyo alitufundisha sisi sote kikamilifu juu ya dhambi tulizonazo katika mioyo yetu. Mungu alitufundisha kuwa sisi ni wenye dhambi wakamilifu mbele za Mungu na akatuangazia ule ukweli kuwa sisi ni wenye dhambi kwa sababu hatuwezi kuitunza na kuifuata Sheria. 
Je, inawezekana kwa mwanadamu kuitunza na kuishika Sheria ya Mungu? Wakati Mungu alipowaambia Waisraeli na Wamataifa mengine kutokuwa na miungu mingine mbele zake alitaka kuwaangazia jinsi walivyo wenye dhambi ambao tangu hapo mwanzo wasingeweza kuitunza na kuishika hata ile amri ya kwanza. Kwa kupitia amri wanadamu walikuja kutambua kuwa walikuwa wakivipenda viumbe vingine kuliko hata Muumba wao. Walitambua kuwa wamekuwa walitaja jina la Bwana bure na kwamba walikuwa wakiitumikia miungu na masanamu ambayo Mungu aliyachukia, na kwamba hawakupumzika hata pale ambapo Mungu aliwaambia wapumzike kwa faida yao wenyewe. Pia waligundua kuwa walikuwa hawawaheshimu wazazi wao, na kwamba walikuwa wakiua, wakifanya uzinifu, na kufanya matendo yote maovu ambayo Mungu aliwaambia wasitende. Kwa ufupi hawakuweza kuitunza na kuifuata Sheria ya Mungu. 
 

Sheria Inawatawala Wale Ambao Dhambi Zao Bado Hazijasamehewa
 
Je, unafahamu kwa nini Mungu alitupatia Sheria? Mungu aliwapatia sheria kwanza wale ambao hawajazaliwa tena upya. “Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?” (Warumi 7:1) Mungu aliwapatia Sheria wale ambao walikuwa wameirithi dhambi toka kwa wazazi wao na ambao hawajazaliwa tena upya ili kuwafanya waomboleze chini ya dhambi. Sheria inamtawala mtu anapokuwa bado angali hai. Kila uzao wa Adamu una zile aina kumi na mbili za dhambi katika moyo wake. Mungu aliwapatia Sheria wale ambao wana dhambi katika mioyo yao na akawaeleza kuwa wamejaliwa dhambi. Hivyo, kila wakati dhambi ya uuaji au uzinifu inapojitokeza ndani yetu na ikatufanya kutenda dhambi, Sheria inatueleza kuwa, “Mungu alikueleza kuwa usizini. Lakini umetenda uzinifu tena. Hivyo wewe ni mwenye dhambi. Mungu alikueleza kuwa usiue, lakini umeua kwa sababu ya chuki yako. Wewe ni mwenye dhambi ambaye unaua na kuzini. Mungu alikueleza kuwa usiibe lakini umeiba tena. Hivyo wewe ni mwizi.” Vivyo hivyo, dhambi inakuwepo mahali pale ambapo Sheria ipo. 
Hii ndiyo sababu Paulo anasema, “Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?” Sheria inawatawala wale ambao dhambi zao bado hazijasamehewa. Kwa wale wa mataifa ambao hawaifahamu Sheria ya Mungu, dhamiri zao zinakuwa ndio Sheria yao. Wanapofanya mabaya dhamiri zao zinawaeleza kuwa wametenda dhambi. Vivyo hivyo, dhamiri ya wasioamini inafanya kazi kama Sheria ndani yao na wanaweza kuitambua dhambi kwa kupitia dhamiri yao. (Warumi 2:15).
Kwa nini humtumikii Muumba hata pale ambapo dhamiri yako inakueleza wazi kuwa kuna Muumba? Kwa nini humtafuti Mungu? Kwa nini unaudanganya moyo wako? Unapaswa kuona aibu kwa sababu ya dhambi zako na kwamba watu wengine wanaweza kuzitambua dhambi zako. Lakini wenye dhambi hawamkiri Mungu na wale wanaoidanganya mioyo yao hawana aibu. 
Mara nyingi tunapokuwa na dhambi tunaona aibu tunapoliangalia anga, dunia, watu wengine, au viumbe vingine vyovyote. Mungu aliwapatia wanadamu dhamiri na sheria ya dhamiri inaionyesha dhambi. Lakini wengi wao wanaishi pasipokuwa na Mungu, wanacheza mchezo wa unafiki mbele ya uso wa Mungu na wanaishi kama wapendavyo. Wao wamefungwa ili kwenda kuzimu. Kama Paulo anavyowakumbusha wao kuizingatia Sheria, “Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?” Mwanadamu ni lazima azaliwe mara mbili—mara moja kama mwenye dhambi, na kisha azaliwe tena upya kwa neema ya ukombozi wa Mungu ili aishi kama mwenye haki. 
Paulo alielezea jinsi Bwana alivyotuokoa toka katika laana ya sheria ya dhambi katika namna ifuatayo: “Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume. Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi ajapoolewa na mume mwingine.” (Warumi 7:2-3). 
Ikiwa mwanamke aliyeolewa akiwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa basi mwanamke huyo huitwa mzinzi. Lakini ikiwa mume wake amekufa na kisha akaolewa na mwanamume mwingine hakuna ubaya katika jambo hilo. Ufahamu huo huo unahusika pia katika ukombozi wetu toka katika sheria ya dhambi. Sheria inawatawala wazao wote wa Adamu ambao dhambi zao bado hazijasamehewa. Sheria hiyo inawaeleza wao kuwa, “Ninyi ni wenye dhambi.” Hivyo wanalazimika kuzikiri dhambi zao chini ya Sheria wakisema “Ni lazima niende kuzimu. Mimi ni mwenye dhambi. Ni asili yangu kwenda kuzimu kwa sababu ya mshahara wa dhambi.” Lakini ikiwa tumeifia Sheria kwa kupitia mwili wa Kristo, basi Sheria haiwezi kututawala kamwe kwa sababu nafsi zetu za kale zilisulubishwa pamoja na Kristo kwa kubatizwa katika Kristo. 
 

Nafsi Zetu Za Kale Zimekufa
 
Bwana wetu alimshughulikia mume wetu wa zamani na akatuwezesha kuolewa na Yeye. “Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda” (Warumi 7:4). Mungu aliwapatia Sheria wanadamu wote ambao walikuwa wamezaliwa na dhambi toka kwa wazazi wao wa kale Adamu na Hawa ili kwamba kwa kupitia zile amri dhambi iweze kufunuliwa zaidi. Mungu aliwafanya hao wenye dhambi kudumu chini ya hukumu ya Mungu, lakini Mungu aliwaokoa kwa kupitia mwili wa Kristo. Yesu Kristo alikufa kwa niaba yetu. Je, si haki kwetu kwenda kuzimu kwa sababu ya Sheria ya Mungu? Ni haki kabisa. Hata hivyo, Bwana alitumwa kuja hapa ulimwenguni akazichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa ubatizo wake katika Mto Yordani, alisulubiwa, alihukumiwa na akasulubiwa kwa laana ya Sheria kwa niaba yetu. Ni kwa kupitia tendo hili pekee ndipo tunapoweza kuokolewa na kuzaliwa tena upya kwa kuliamini tendo hili. 
Wale ambao hawajazaliwa tena upya ni lazima waende kuzimu. Ni lazima wamwamini Yesu na kuokolewa. Ni lazima tufe mara moja pamoja na Yesu Kristo. Ikiwa nafsi zetu za kale hazifi, basi hatuwezi kufanyika viumbe vipya na kisha kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Ikiwa nafsi zetu za kale hazijahukumiwa kwa mujibu wa Sheria kwa kupitia imani yetu iliyoungana na Yesu, basi kwa hakika ni lazima tuhukumiwe na kwenda kuzimu. Wale wote ambao hawajazaliwa tena upya ni lazima waende kuzimu. 
Wale wasioamini wanaishi vizuri hali wakifurahia kila kitu ambacho maisha mazuri yanaweza kutoa, lakini hawazingatii kuhusu adhabu yao ya milele. Wanadamu wote ni lazima wapokee msamaha wa dhambi toka kwa Bwana Yesu wanapokuwa wangali wanaishi hapa duniani. Kila nafsi ya kale ni lazima ife mara moja na kisha iungane na Yesu katika imani, hii ni kwa sababu hatuwezi kuzaliwa tena upya mara baada ya kuondoka katika ulimwengu huu. Ni lazima tuuawe mara moja na kisha kukombolewa toka katika dhambi zetu kwa kupitia imani yetu katika Yesu Kristo. Kwa kupitia nani? Ni kwa kupitia mwili wa Yesu Kristo. Kivipi? Ni kwa kuamini kuwa Yesu alikuja hapa ulimwenguni na akazichukulia mbali dhambi zetu zote. Je, umekufa? Je, kuna yeyote yule ambaye bado hajafa? Bila shaka unaweza kushangaa, “Ninawezaje kufa? Ninaishije sasa ikiwa nimekufa?” Hii ni siri; ni fumbo ambalo hakuna dini inayoweza kulitatua. 
Ni wale tu waliozaliwa tena upya ndio wanaoweza kusema kuwa wamekwisha kufa katika muungano na Yesu. Wenye dhambi wanaweza kuzaliwa tena upya na nafsi zao za kale zinaweza kufa pale wanapolisikia Neno la Mungu toka kwa waliozaliwa tena upya. Na kwa kupitia jambo hili wanaweza kufanyika watumishi wa Mungu. Wanadamu wote ni lazima walisikilize Neno la Mungu toka kwa watakatifu waliozaliwa tena upya. Huwezi kuzaliwa tena upya ikiwa utayadharau mafundisho yao. Pamoja na kuwa Paulo alikuwa amejifunza Neno la Mungu toka kwa Gamaliel ambaye alikuwa ni mwalimu mashuhuri wa Sheria wa wakati huo bado hakuweza kuzaliwa tena upya pasipo Kristo. Tunamshukuru Mungu sana!. Tunaweza kuyaleta matunda ya haki kwa Mungu kwa kuamini katika Yesu Kristo ambaye alifufuka tena toka kwa wafu pale tunapokuwa wafu kwa kupitia mwili wa Yesu Kristo kwa imani. Hivyo tunaweza kumletea Mungu aina tisa za matunda ya Roho Mtakatifu. 
 

Tamaa ya Dhambi Katika Viungo Vyetu Zilifanya Kazi Ili Kuizalia Matunda Mauti
 
“Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilikuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao” (Warumi 7:5). “Tulipokuwa katika hali ya mwili” maana yake ni kuwa “kabla hatujazaliwa tena upya.” Tamaa za dhambi katika viungo vyetu zilikuwa zikitenda kazi ili kuizalia mauti matunda wakati tulipokuwa hatuna imani kwa kupitia mwili wa Yesu Kristo. Kwa wakati huo tamaa ya dhambi ilikuwa ikifanya dhambi wakati wote katika viungo vyetu. Kuna aina kumi na mbili za dhambi katika moyo. Ukisema kwa namna nyingine, kuna ina kumi na mbili za milango ya dhambi katika mioyo yetu. Kwa mfano, leo hii, dhambi ya uzinzi inaweza toka katika mlango wake na kisha ikauamsha moyo. Kisha moyo unakiamrisha kichwa, “uzinifu unatoka katika shimo lake na unanieleza mimi kufanya uzinifu.” Kisha kichwa kinajibu, “Sawa, nitaiamrisha mikono na miguu kutekeleza jambo hilo. Sikilizeni, enyi mikono namiguu, fanyeni kama mpendavyo. Fanya haraka!” Kichwa kinaviamuru viungo vyake kwenda katika mahali ambapo mwili utafanya uzinifu. Kisha, mwili unakwenda na unafanya kama kichwa kinavyoamuru. Vivyo hivyo, wakati dhambi ya uuaji inapotoka katika shimo lake, inaufanya moyo kuwa na hasira na kisha moyo unakifanya kichwa kuwa na hasira juu ya mtu fulani. Kisha kichwa kinauamuru mwili kujiandaa kwa ajili ya mauaji. Hivyo dhambi inatenda kazi katika viungo vyetu kwa jinsi hii. 
Hii ndiyo sababu inayotufanya tupokee msamaha wa dhambi zetu. Ikiwa hatuna msamaha wa dhambi basi hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kutenda kama ambavyo moyo unaamuru hata kama hatupendi kufanya hivyo. Kila mtu ni lazima azaliwe tena upya kwa injili ya kweli. Mtu anaweza kuwa mkamilifu pale anapozaliwa tena upya kama ambavyo buu anafanyika kuwa kereng’ende. Wachungaji wanaweza kumtumikia Mungu kwa kweli baada ya kuwa wamezaliwa tena upya. Kabla ya kuzaliwa tena upya wanachoweza kukisema ni kuwa “Wapendwa watakatifu, ni lazima mtende mema.” Hii ni sawa na kumwambia mgonjwa ajiponye yeye mwenyewe. Wachungaji wa jinsi hiyo wanawasisitiza waumini wao kuisafisha mioyo yao ingawa wao wenyewe hawajui namna ya kuisafisha mioyo yao yenye dhambi. 
Tamaa za dhambi katika viungo vyetu zilikuwa zikifanya kazi ili kuizalia mauti matunda. Je, mtu anatenda dhambi kwa kuwa anataka kufanya hivyo? Sisi tunatenda dhambi kama watumishi wa dhambi kwa kuwa tulizaliwa na dhambi na kwa sababu dhambi zetu zilikuwa bado hazijatoweshewa mbali, na kwa sababu tulikuwa bado hatujafa kwa kupitia mwili wa Yesu Kristo. Tunatenda dhambi ingawa tunachukia kufanya hivyo. Hivyo kila mtu ni lazima apokee msamaha wa dhambi. 
Ni vema kwa wachungaji ambao dhambi zao bado hazijachukuliwa bado waache kumtumikia Bwana. Itakuwa ni vema kwao ikiwa wataanza kuuza kabichi za kichina. Ninawashauri wafanye hivyo. Itakuwa ni jambo jema kwa wao kufanya hivyo kuliko kuwadanganya watu kwa kuwaeleza uongo ili kupata fedha nyingi na kujichukulia sadaka kuwa mali yao na kisha kuwa wanene kama nguruwe. 
Ikiwa mtu hajaokolewa toka katika dhambi zake zote, basi dhambi na tamaa zake katika mwili wake zinaendelea kufanya kazi ili kuizalia mauti matunda. Tunaweza kumtumikia Bwana chini ya neema yake kwa kupokea Roho Mtakatifu baada ya kuwa dhambi zetu zote zimechukuliwa mbali nasi. Lakini hatuwezi kumtumikia Bwana chini ya Sheria. Hivyo Bwana wetu anatueleza sisi kuwa, “Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho si katika hali ya zamani, ya andiko” (Warumi 7:6).
 

Sheria Inazifanya Dhambi Zetu Kuwa Mbaya Zaidi 
 
“Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani. Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa. Nami nilikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa. Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti. Kwa maana dhambi, kwa kupata nafasi kwa ile amri, ilinidanganya, na kwa hiyo ikaniua. Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki na njema. Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.” (Warumi 7:7-13).
Paulo alisema kuwa Mungu alitupatia Sheria ili kuzifanya dhambi zetu kuwa mbaya zaidi. Pia alisema kuwa, “Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria” (Warumi 3:20). Hata hivyo, Wakristo wanajaribu kuishi kwa kufuata Sheria hali wakiitafuta haki ya Sheria. Hivyo wachungaji wengi ambao hawajazaliwa tena upya wanahakika kuwa watu wengi wanaugua kutokana na kutoitii Sheria na kwamba watu hao wanaweza kupona toka katika kuugua huko ikiwa wataishi kwa kuifauta Sheria. 
Je, tunaweza kweli kuhitimisha kuwa magonjwa yetu yanatokana na kutoitii Sheria? Wakristo wengi, wahudumu pamoja na wafuasi wao wanafikiri kuwa mambo hayaendi vizuri ati kwa kuwa wameshindwa kuishi kwa kulifuata Neno la Mungu. Wanafikiri kuwa wanaugua kwa sababu ya dhambi zao. Hivyo wanaiogopa sana dhambi. Wanalia kila siku. Bila shaka wanaweza kuongeza kifungu katika Biblia wakisema, “Lia zaidi na zaidi. Lia bila kukoma. Katika kila kitu lia,” lakini Biblia inatueleza sisi kuwa “Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu” (1 Wathesalonike 5:16-18). Lakini wachungaji wa uongo wanawafundisha watu kulia zaidi na zaidi, kulia bila kukoma, kana kwamba machozi mengi ndiyo ishara ya imani yao. 
Wale walio na imani ya kisheria wanadai kuwa waliaji wana imani nzuri. Wachungaji wa uongo ambao hawajazaliwa tena upya wanamchagua mwanamke anayelia sana kuwa ndiye Shemasi wa kike na mwanamume Mkristo mwenye machozi mengi kuwa mzee wa Kanisa. Ikiwa kweli unataka kulia usilie ukiwa Kanisani lia ukiwa nyumbani kwako. Kwa nini Yesu alisulubiwa? Je, alisulubiwa ili kutufanya sisi kuwa watoto waliaji? Kwa kweli hapana! Yesu aliichukulia mbali huzuni yetu, laana, magonjwa na maumivu mara moja na kwa ajili ya wote ili kwamba kusulubiwa kwake kutufanye sisi kutolia tena na badala yake tuishi kwa furaha. Sasa kwa nini wanalia? Ikiwa watajaribu kulia katika kanisa la waliozaliwa mara ya pili basi watu hao wanapaswa warudishwe nyumbani kwao.
 

Kuna Tofauti Gani Kati ya Waliozaliwa Tena Upya na Wale Ambao Hawajazaliwa Tena Upya? 
 
Sheria haikosei kamwe. Sheria ni takatifu. Sheria ni ya haki wakati sisi si wenye haki kabisa. Sisi tupo kinyume na Sheria kwa sababu tunazaliwa tukiwa na dhambi kama wana wa Adamu. Tunafanya yale ambayo hatukupaswa kuyatenda hali hatutendi yale ambayo tulipaswa kuyatenda. Hivyo Sheria inazifanya dhambi zetu kuwa mbaya zaidi. 
“Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?” (Warumi 7:14-24).
Kabla ya kifungu hiki, Paulo anasema kuwa sisi sote akiwemo yeye mwenyewe tunapaswa kuhukumiwa na Sheria. Paulo anasema kuwa ni wale tu waliokwisha pokea hasira na hukumu ya Sheria kwa kupitia mwili wa Yesu Kristo ndio wanaoweza kumzalia Mungu matunda ya haki. Pia anasema kuwa hakuna kitu kizuri kinachokaa ndani yake na kwamba mtu ambaye hajazaliwa tena upya hawezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kutenda dhambi. Pia hata yule aliyezaliwa tena upya atatenda dhambi pia. Lakini kuna tofauti kubwa kati ya watu hao wawili. Wale waliozaliwa tena upya wana mwili pamoja na Roho, hivyo kuna aina mbili ya matamanio ndani yao. Lakini wale ambao hawajazaliwa tena upya wao wana ile tamaa ya mwili tu, na wanapenda kutenda dhambi tu. Hivyo wanachokijali ni uzuri wa kule kutenda dhambi. Hili ndilo lengo ambalo linapatikana sana kwa wale ambao hawajazaliwa tena upya. 
Dhambi inawafanya watu kutenda dhambi. Warumi 7:20 inasema, “Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.” Je, kuna dhambi katika moyo wa yule aliyezaliwa tena upya? Hapana. Je, kuna dhambi ndani ya mioyo ya wale ambao hawajazaliwa tena upya? Ndiyo! Ikiwa una dhambi katika moyo wako basi dhambi hiyo itakufanya wewe utende dhambi zaidi. “Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.” Wanadamu hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kutenda dhambi katika maisha yao yote kwa kuwa wanazaliwa hali wakiwa na dhambi. 
Waliozaliwa tena upya wanaweza kuzaa matunda ya Roho yanayoonekana. Lakini wale ambao hawajazaliwa tena upya hawawezi kuyaleta matunda kama hayo. Hawana huruma kwa watu wengine. Baadhi yao wanadiriki hata kuwaua watoto wao wenyewe pale wanaposhindwa kuwatii. Ukatili unatoka katika mioyo yao na wanaua watoto wao wanaposhindwa kuwatii. Ingawa wengine hawawaui watoto wao kimwili bali katika mioyo yao wanawaua watoto wao mara nyingi. 
Je, unaelewa kile ninachojaribu kukisema hapa? Lakini wenye haki hawawezi kufanya jambo kama hilo. Wenye haki wanaweza kuingia katika mdahalo lakini hawawezi kutamani na kuwa na mioyo mikatili kiasi hicho ikiwa imejazwa na uchungu mwingi na hasira dhidi ya watu wengine kama ilivyo kwa wengine. 
Badala yake, wenye haki wanapenda kuwaonea huruma watu wengine katika mioyo yao hata wale ambao wanaweza kuwa wameshindania hoja fulani katika mdahalo. “Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya.” Wanadamu wanapenda kutenda mema kwa kuwa waliumbwa katika sura na mfano wa Mungu. Lakini kwa kuwa dhambi bado ipo ndani ya mioyo yao basi ni dhahiri kuwa ni maovu tu ndiyo yatakayotoka ndani yao. 
Wakristo ambao hawajazaliwa tena upya wanazungumza kwa pamoja hali wakiomboleza, “kwa kweli ninapenda kutenda mema, lakini nashindwa.” Ni lazima wafahamu kuwa hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa wao ni wenye dhambi ambao bado hawajaokolewa. Ni lazima watambue kuwa hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa wao ni wenye dhambi ambao bado hawajokolewa. Hawawezi kufanya mema kwa kuwa wana dhambi katika mioyo yao. Wale waliozaliwa tena upya wanatamani mambo ya Roho pamoja na tamaa za mwili, lakini wale ambao hawajazaliwa tena upya bado hawana Roho Mtakatifu. Hii ndiyo tofauti kubwa inayotofautisha kati ya waliozaliwa tena upya na wale ambao hawajazaliwa tena upya. 
Katika sura ya 7 Paulo anazungumzia juu ya hali yake ya kutozaliwa tena upya. Hali akiielezea Sheria katika Warumi sura ya 7:1 na kuendelea, Paulo anasema kuwa alikuwa hawezi kufanya mema ambayo alitaka kuyafanya bali alitenda mabaya ambayo hakutaka kuyatenda. Kwa maneno mengine, yeye hakuwa na nia ya kufanya dhambi na alipenda kufanya mema tu, lakini bado alitenda yale ambayo hakutaka kuyatenda huku yale aliyokuwa akitaka kuyafanya toka ndani ya moyo wake yakishindikana kufanyika. “Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?” Paulo aliilalamikia hali yake hii ya kuhuzunisha lakini mara akamsifu Bwana akisema, “Namshukuru Mungu—kwa Yesu Kristo Bwana wetu!” 
Je, unaelewa maana ya maneno hayo hapo juu? Sisi, ambao tumezaliwa mara ya pili tunaweza kuulewa msemo huo hapo juu lakini wale ambao hawajazaliwa tena upya hawawezi kuulewa msemo huu kamwe. Buu ambalo halijawa kereng’ende haliwezi kutambua kile ambacho kereng’ende anakisema. “Wawaa! Ninaimba nyimbo kwa masaa mengi kila siku juu ya mti. Kwa kweli upepo umetulia sana!” Buu anaweza kujibu toka ardhini, “Ni kweli? Upepo ni kitu gani?” Buu hawezi kutambua kile ambacho kereng’ende anakisema lakini kereng’ende anajua upepo ni kitu gani. 
Kwa kuwa Paulo alikuwa amezaliwa tena upya basi aliweza kuelezea vizuri tofauti kati ya wale waliozaliwa tena upya na wale ambao hawajazaliwa tena upya. Paulo anasema kuwa Mwokozi aliyemwokoa yeye ni Yesu Kristo. Je, Yesu Kristo alituokoa? Kwa kweli alituokoa! “Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.” 
Wale wanaotenda dhambi wamenyang’anywa kule kuitumikia sheria ya Mungu kwa mioyo yao. Je, wanatumikia nini basi kwa miili yao? Wanaitumikia sheria ya dhambi kwa miili yao. Mwili unapenda kutenda dhambi kwa kuwa bado haujabadilika kabisa. Mwili unapenda mambo ya mwili na Roho inapenda mambo ya Roho. Hivyo wale ambao dhambi zao zimeshachukuliwa mbali wanaweza na wanapenda kumfuata Bwana kwa kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yao sasa. Lakini wale ambao dhambi hazijachukuliwa mbali hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuifuata dhambi kwa akili na miili yao. Wale waliozaliwa tena upya ambao dhambi zao zimechukuliwa mbali wanaweza kumfuata Mungu kwa akili zao hata pale miili yao inapokuwa ikiifuata dhambi. 
 

Sheria ya Roho wa Uzima Ulio Katika Kristo Yesu Imetuweka Huru Mbali na Sheria ya Dhambi na Kifo 
 
Kwa sasa hebu tuhamie katika Warumi 8:1. Wale ambao dhambi zao zimechukuliwa mbali kwa kuamini katika wokovu wa Yesu hawahukumiwi tena na Sheria ya Mungu pamoja na kuwa walizaliwa wenye dhambi. “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeaniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti” (Warumi 8:1-2). 
Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Hakuna hukumu ya adhabu! Wale waliozaliwa tena upya hawana dhambi na hakuna hukumu ya adhabu juu yao. Hakuna dhambi iliyobakia katika mioyo yao kwa kuwa Sheria ya uzima katika Kristo Yesu imewaweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti. Bwana wetu ndiye asili ya uzima. Yeye alifanyika kuwa Mwanakondoo wa Mungu, aliyetungwa mimba kwa Roho Mtakatifu na kisha akazichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake katika Mto Yordani kwa kupitia ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana. Akahukumikiwa kwa niaba yetu, alisulubiwa kwa ajili yetu. Kwa kupitia mambo haya Yesu alizichukua dhambi zetu zote kikamilifu. 
Je, tunapaswa kufa tena kwa ajili ya dhambi zetu? Je, tuna kitu chochote ambacho kwa hicho tunapaswa kuhukumiwa? Ikiwa dhambi zetu zote zilipitishwa na kuchukuliwa na Yesu Kristo kwa kupitia ubatizo wake, Je, bado tuna dhambi ndani yetu? Kwa kweli hapana! Hatupaswi kuhukumiwa kwa kuwa Bwana alibatizwa katika Mto Yordani, alibatizwa kwa ajili yetu na kisha akafufuka tena toka kwa wafu katika siku ya tatu ili kuwaokoa wenye dhambi wote. 
Wokovu wa Mungu unatuweka huru mbali na hukumu yake wakati Sheria inatuletea ghadhabu. “Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.” Ghadhabu ya Mungu inafunuliwa kwa wale walio na dhambi. Mungu atawapeleka hao kwenda kuzimu. Lakini Bwana ametuweka huru mbali na sheria ya dhambi na kifo kwa kuzichukulia mbali dhambi zote toka katika mioyo yetu. Mungu aliwafanya waamini walio katika Kristo Yesu kuwa huru toka katika dhambi. Je, dhambi zako zimechukuliwa mbali? 
“Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya Roho” (Warumi 8:3-4). 
Bwana wetu anatueleza wazi kuwa mwili ni dhaifu na hauwezi kuyatii maagizo ya haki ya Sheria. Kwa hakika Sheria ya Bwana ni njema na nzuri, lakini hatuwezi kuishi kwa kuifuata kwa sababu mili yetu ni midhaifu mno. Sheria ya Mungu inatuhitaji sisi tuwe wakamilifu. Inatutaka sisi tuufikie ule utii mkamilifu kwa Sheria ya Mungu, lakini miili yetu haiwezi kuishi kwa kuyafuata maagizo yote ya Sheria kwa sababu ya udhaifu wa miili hiyo. Hivyo Sheria inatuletea ghadhabu yake kwetu sisi. Lakini ikiwa tutakwenda kuhukumiwa Yesu yupo kwa ajili gani? 
Mungu alimtuma Mwanawe pekee ili kutuokoa. Mungu alitupatia sisi haki yake kwa kumtuma Mwanawe pekee katika mfano wa mwili ulio wa dhambi kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu alitumwa ulimwenguni katika mfano wa mwili. “Akaihukumu dhambi katika mwili.” Mungu alizipitisha dhambi zetu zote juu ya Yesu ili kwamba maagizo ya haki ya Sheria yatimizwe ndani yetu sisi tusioenenda kwa kuufuata mwili bali tuifuatao Roho. Dhambi zetu zinachukuliwa mbali na imani yetu katika Yesu Kristo kwa mioyo yetu. Dhambi zetu zinatoweshewa mbali wakati tunapokiri yale ambayo Yesu Kristo ameyafanya kwa ajili yetu. 
 

Wale Wanaoishi Kwa Jinsi ya Roho na Wale Wanaoishi Kwa Jinsi ya Mwili 
 
Kuna aina mbili za Wakristo: wale ambao wanayafuata mawazo yao binafsi na wale ambao wanalifuata Neno la kweli. Hawa walifuatao Neno la kweli wanaweza kuokolewa na kufanyika wenye haki wakati hilo kundi jingine litaangamia. 
“Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifutao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.” (Warumi 8:5-6). Wale wanaofikiri kuwa kumwamini Mungu ni kuishi kwa mujibu wa Sheria hawawezi kuwa wakamilifu. “Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili.” 
Mambo ya mwili ni kule kuisafisha nafsi kwa nje. Wale wanaofanya hivyo wanaitupa Biblia na kisha kwenda kanisani hali wakiwa kwenye mwendo mtakatifu ingawa watu hao wanapigana na wake zao na kutenda maovu wawapo nyumbani. Siku ya Jumapili wanakuwa ni malaika. 
“Hallo, umeshindaje?” 
“Ni furaha sana kuonana nawe tena.” 
Wanasema “Amina” mara nyingi kila wakati mchungaji wao anapohubiri kwa sauti takatifu na namna ya heshima na huruma. Baada ya ibada ya kuabudu wanatoka kanisani taratibu na ghafla wanageuka na kuwa wenye tabia nyingine mara wanapoona kuwa kanisa halionekani katika macho yao. 
“Je, Neno la Mungu lilisema nini kwangu? Sikumbuki vizuri; hebu twende tukanywe pombe?” 
Watu hao wanakuwa ni malaika wawapo kanisani lakini wanakuwa ni viumbe waovu wanapokuwa mbali na kanisa. 
Hivyo, wenye dhambi ni lazima wamwombe Mungu kama ifuatavyo: “Mungu tafadhali niokoe, mimi niliye maskini. Siwezi kuuingia Ufalme wa Mbinguni na nitaenda kuzimu ikiwa hautaniokoa. Lakini ikiwa utazioshelea mbali dhambi zangu zote ambazo ninazitenda hadi nitakapokufa, basi ninaweza kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa imani.” Ni lazima wamtegemee Mungu kikamilifu. 
Kila mwamini anaweza kupokea ukombozi wa dhambi zake na kisha kuishi maisha ya kiroho pale anapolifuata Neno la Mungu. “Wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.” Ikiwa tunafikiri na kuamini kwa mujibu wa ukweli wa Mungu basi amani itakuja kwetu. “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.” (Warumi 8:7-8). Wale ambao dhambi zao hazijachukuliwa na ambao bado wapo katika mwili hawawezi kumpendeza Mungu. 
“Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.” (Warumi 8:9). Watu wengi wanachanganywa na vifungu hivi kwa kuwa Paulo anazungumza katika lugha ya ndani ya kiroho. Wale ambao hawajazaliwa tena upya wanasumbuliwa na kuchanganywa na Warumi sura ya 7 na ya 8. Hawawezi kuielewa sehemu hii ya Biblia. Lakini sisi tuliozaliwa tena upya hatumo katika mwili na wala hatuishi kwa ajili ya mwili tu. 
Hebu soma vizuri kile ambacho Paulo anakisema katika kifungu cha juu yake. Je, Roho Mtakatifu anakaa ndani yako? Ikiwa mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo basi mtu huyo si wa Kristo. Na kama mtu huyo si wake basi ina maanisha kuwa mtu huyu ni wa Shetani na ni mwenye dhambi ambaye amefungwa kwenda kuzimu. 
“Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Lakini ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.” (Warumi 8:10-11). Amina. 
Bwana wetu alitungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, alitumwa kuja ulimwenguni katika mwili na akazichukua dhambi zetu zote. Bwana amekuja katika mioyo ya waamini wanaoamini katika ukombozi wa dhambi na anakaa katika moyo wa kila mwamini. Roho Mtakatifu anakuja ndani ya moyo na anathibitisha kuwa Bwana wetu Yesu amezioshelea mbali dhambi zetu na kuzifanya kuwa nyeupe kama theluji. Pia Mungu ataipatia uhai miili yetu wakati Yesu atakapokuja tena ulimwenguni kwa mara nyingine. “Yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.”
 

Roho Hushuhudia Pamoja na roho Zetu Kwamba Sisi Tu Watoto wa Mungu
 
Baada ya kuzaliwa mara ya pili ni lazima tuishi kwa imani katika Mungu na kwa Roho Mtakatifu. “Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia Aba, yaani Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye” (Warumi 8:12-17). Tunalia, “Abba, Baba,” kwa sababu tumepokea Roho wa urithi na sio roho ya utumwa na hofu. 
“Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu.” Kwanza kabisa, Roho Mtakatifu hushuhudia kwamba tumepokea ondoleo la dhambi kwa kupitia Neno la Mungu lililo imara. Ushuhuda wa pili ni kuwa sisi hatuna dhambi. Roho ameshuhudia kuwa sisi tumeokolewa. Roho Mtakatifu amefanya hivyo katika mioyo ya wale ambao dhambi zao zimekwisha chukuliwa mbali. “Hakuna mwenye haki hata mmoja” (Warumi 3:10). Ni kweli, lakini hali hii ilikuwa ni wakati Mungu hajatukomboa. Chini ya kifungu hicho, imeandikwa kuwa tunaokolewa bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu (Warumi 3:24). Pia imeandikwa kuwa Roho mwenyewe hushuhudia kuwa sisi tu watoto wa Mungu. Roho huja kwetu pale tunapokiri katika mioyo yetu yale ambayo Mungu ameyafanya kwa ajili yetu, lakini ikiwa hatuamini basi Roho hawezi kupatikana popote ndani yetu. Ikiwa tutayapokea yale ambayo Mungu ameyafanya kwa ajili yetu katika mioyo yetu, basi Roho atashuhudia, “Ninyi ni wenye haki. Ninyi ni watoto wangu. Ninyi ni wenye haki. Ninyi ni watu wangu.” “Basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.” Kwa hiyo ni sahihi kabisa kwa watoto wa Mungu kuteseka pamoja na Bwana na kisha kutukuzwa pamoja naye. Wale walio na Roho Mtakatifu, wanaoongozwa na Roho, wanaweka matumaini yao katika lengo zima la kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. 
 

Pamoja na Mateso Tunayoyapata Sasa Hivi Bado Tunaishi Katika Matumaini ya Utawala wa Milenia na Ufalme wa Mbinguni
 
Hebu tuangalie Warumi 8:18-25. “Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu. Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha katika tumaini; kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja navyo vina utungu pamoja hata sasa. Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu tukikutazamia kufanywa wana, yaani ukombozi wa mwili wetu. Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho? Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi.”
Sisi ni malimbuko ya Roho. Sisi tuliozaliwa tena upya ni malimbuko ya ufufuo. Tutashiriki katika ufufuo wa kwanza. Yesu Kristo ndiye limbuko la kwanza la ufufuo na sisi ndio wale ambao tutakuwa tumekamatana naye. Wale walio wa Kristo watashiriki katika ufufuo wa kwanza na ndipo mwisho utakuja. Wale wasio wa kimungu watashiriki katika ufufuo wa pili ili waweze kuhukumiwa. Hii ndiyo sababu Paulo anasema, “Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.” Kule kusema kwa utukufu anazungumzia juu ya ule Utawala wa Milenia na Ufalme wa Mbinguni. Sisi sote tutabadilishwa wakati kipindi cha baraka kitakapokuja. Watoto wa Mungu watafufuka wote kikamilifu toka kwa wafu na kila mmoja wao atapokea uzima wa milele toka kwa Bwana. Kwa hakika mwili utafufuka tena toka kwa wafu (maana nafsi zetu zimekwisha fufuka tena toka kwa wafu). Mungu atavifanya vitu vyote kuwa vipya na wenye haki wataishi kwa furaha kama wafalme kwa miaka elfu moja.
Viumbe vyote ulimwenguni vinasubiria kudhihirishwa kwa watoto wa Mungu. Uumbaji utabadilishwa kama ambavyo sisi tutakavyobadilishwa. Katika kipindi hicho cha Ufalme wa Milenia hakutakuwa na vitu kama maumivu, mateso, au vifo. Lakini sasa tunaugua. Kwa nini? Kwa sababu mwili bado ni dhaifu. Nafsi zetu zinaugua kwa ajili ya jambo gani? Zinaugua kwa ajili ya ukombozi wa miili yetu. 
“Sisi pia tunaugua katika nafsi zetu tukikutazamia kufanywa wana, yaani ukombozi wa mwili wetu. Kwa maana tuliokolewa kwa taraja; lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho? Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi” (Warumi 8:23-25). 
Sisi tunatarajia kwa hamu kufanywa warithi kwa kuwa tuliokolewa katika tumaini au taraja. Sisi ambao dhambi zetu zimekwishachukuliwa mbali tutaingia katika Ufalme wa Milenia na katika Ufalme wa Mbinguni. Sisi hatutaangamia hata kama ulimwengu utafikia katika ukomo wake. Katika mwisho wa dunia Bwana wetu atakuja tena katika ulimwengu huu. Atavifanya vitu vyote kuwa vipya na kisha ataiinua miili mipya kwa ajili ya wenye haki. Kisha atawafanya wenye haki kutawala kwa miaka elfu moja. 
Mwisho wa ulimwengu huu ni mbaya sana kwa wenye dhambi bali ni tumaini jipya kwa wenye haki. Paulo alikuwa akiutarajia mwisho huo. Je, unaugua? Je, unasubiria ukombozi wa mwili wako? Je, Roho inasubiria pia? Sisi tutabadilishwa kwenda katika miili ya kiroho kama ule mwili wa Yesu Kristo baada ya ufufuo mwili ambao hauoni maumivu wala udhaifu. 
 

Roho Mtakatifu Anawasaidia Wenye Haki Kuwa na Imani
 
Roho Mtakatifu anatusaidia sisi kuwa na imani. Je, tunatumaini yale tunayoyaona? Hapana, tunatumainia yale ambayo hatuwezi kuyaona. “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu” (Warumi 8:26-27). 
Je, Roho Mtakatifu anataka nini ndani yetu? Je, anatusaidia sisi kufanya mambo gani? Je, unatumaini au unatarajia nini? Sisi tunatarajia mbingu na nchi mpya (2 Petro 3:13), ambayo ni Ufalme wa Mbinguni. Hatupendi kuishi katika ulimwengu huu unaoangamia kwa mara nyingine. Tumechoka, na kwa hiyo tunaitarajia Siku ya Bwana. Tunapenda kuishi milele pasipo na dhambi, pasipo magonjwa, pasipo roho mbaya; tunataka kuishi katika nchi hiyo mpya kwa furaha, amani, upendo na unyenyekevu hali tukiwa na ushirika kamilifu na Bwana Yesu na kila mmoja wetu. 
Hivyo, Roho anaugua hali akituombea sisi hali akiwa anasubiria nchi na mbingu mpya. Kusema kweli, sisi wenye haki, hatuna raha katika ulimwengu huu labda mara chache tunapokuwa tukicheza mpira pamoja na wapendwa watumishi wa Mungu wenzetu. Tunaishi katika ulimwengu huu kwa sababu tunapendezewa katika kuihubiri injili. Lakini kama ingekuwa si Utume huu Mkuu, basi wenye haki wasingekuwa na sababu ya kuwepo katika ulimwengu huu. 
 

Mungu Anaviruhusu Vitu Vyote Vifanye Kazi Pamoja Kwa Ajili ya Mema ya Wale Waliozaliwa mara ya pili na Wanaompenda Yeye
 
Hebu tusome Warumi 8:28-30. “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.” 
Katika Warumi 8:28 Paulo anasema, “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.” Kifungu hiki ni cha muhimu sana. Watu wengi wanafikiri kuwa, “Kwa nini nilizaliwa? Mungu alipaswa kuniweka mahali ambapo Shetani hayupo, na angelipaswa kuniruhusu kuishi katika Ufalme wa Mbinguni tangu hapo mwanzo. Kwa nini Mungu alinifanya mimi kuwa kama hivi?” Baadhi ya watu waliozaliwa katika hali mbaya wanakuwa na kinyongo kwanza na wazazi wao na kisha wanakuwa na kinyongo na Mungu. “Kwa nini mlinifanya nizaliwe katika hali ya mateso kama hii?”
Kifungu hiki kinatupatia sisi jibu sahihi kwa maswali kama hayo. Tulizaliwa kama viumbe wa Mungu. Je, si kweli? Sisi ni sehemu ya uumbaji wake. Mungu alituumba sisi katika sura na mfano wake lakini bado sisi ni viumbe wake. Mungu ana makusudi ya kutuweka sisi katika ulimwengu wa jinsi hii. Maandiko yanasema, “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.” Sisi tulizaliwa kama wenye dhambi na tunateseka kwa sababu ya dhambi ya asili iliyorithiwa toka kwa Adamu na Hawa ambao walidanganywa na Mwovu. Lakini Mungu alimtuma Yesu Kristo kwa ajili yetu ili kutufanya sisi kuwa watoto wake kwa imani. Na hilo ndilo kusudi la Mungu la kutuumba. Pia Mungu anataka kutupatia sisi maisha ya furaha na milele ya kimungu pamoja na Yesu Kristo na Mungu Baba katika Ufalme wa Milenia na katika Ufalme wa Mbinguni. 
“Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.” Mapenzi ya Mungu kwetu yalitimizwa yote wakati dhambi zetu zilipochukuliwa mbali. Je, hii si kweli? Je, hatupaswi kufurahia kuwa tulizaliwa katika ulimwengu huu? Tunapofikiria juu ya utukufu kwa hakika tutafurahia hapo baadaye na hatuwezi kufanya lolote zaidi ya kufurahia kuzaliwa kwetu hapa ulimwenguni. Lakini watu wengi hawana furaha na hii ni kwa sababu wanaukataa upendo wa Mungu. 
Je, unafahamu ni kwa nini kuna magonjwa na dhambi? Na kwamba ni kwa nini kila kitu kinaonekana kuwa kinaenda vizuri kwa watenda maovu hali wale wanaojaribu kutenda mema wakiendelea kuteseka? Ni kwa sababu ni hadi tutakapoteseka tu ndipo tutafikia hatua ya kumtafuta Mungu, kukutana na Mungu na kufanyika watoto wa Mungu kwa kupokea ondoleo la dhambi zetu. Mungu anawaruhusu watu waovu waendelee kuishi katika ulimwengu huu ili kuyafanya mambo yote kwa ajili ya mema ya wale wampendao. 
Je, unafikiri kwa namna hii: “Sifahamu ni kwa nini Mungu aliniumba hivyo. Kwa nini Mungu alinifanya nizaliwe katika famili ya kimaskini ili niteseke?” Mungu anatufanya sisi tuzaliwe katika ulimwengu huu chini ya uongozi wa Shetani na Sheria ili kutufanya sisi kuwa watoto wake na kutufanya sisi kuishi milele kama wafalme pamoja na Bwana wetu katika Ufalme wake unaokuja. Mambo yote yalifanya kazi pamoja kwa ajili ya mema ya watu wake na Mungu ametufanya sisi kuwa watoto wake. Hili ndilo kusudi la Mungu la kutuumba kwa namna hii. Hatuna sababu ya msingi ya kutufanya kulaumu na kunung’unika dhidi ya Mungu. “Kwa nini niliumbwa hivi? Kwa nini niko hivi?” Mapenzi mema ya Mungu yanatimizwa kwa kupitia magumu haya. 
Usilalamikie kuhusu mateso yako. Usiimbe nyimbo za huzuni kuhusu maisha yako tena. “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Waebrania 9:27). Kuna neema ya wokovu wa Mungu kati ya kuzaliwa kwa mtu na hukumu. Tunamwamini Yesu Kristo, dhambi zetu zote zimechukuliwa mbali kwa neema ya Mungu na kisha tutatawala katika Ufalme wa Milenia na Ufalme wa Mbinguni. Sisi tutaitwa “bwana wa uumbaji wote.” Je, unafahamu sasa kuwa ni kwa nini Mungu anakufanya uteseke? Mungu ametupatia mateso na magumu ili aweze kutubariki sisi kuwa watoto wake kwa kutufanya sisi kurudi kwa Mungu. 
 

Mungu Alikwishatupangia Sisi ili Tufanane kwa Sura na Mfano wa Mwanawe
 
Haichukui muda mrefu kwa sisi kupokea ondoleo la dhambi, pia haituchukui muda mrefu kuokolewa toka katika hukumu ya Mungu na kufanyika wenye haki. Sisi tulifanywa wenye haki mara moja na daima, na tunaweza kufanyika watoto wa Mungu mara moja kwa imani. Wokovu wa Mungu si matokeo ya mchakato wa muda mrefu wa kujitakasa sisi wenyewe. Mungu alituokoa sisi mara moja na kwa ajili ya wote na akatufanya sisi kuwa wenye haki. 
“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza” (Warumi 8:29-30). 
Watu wengi wanayaweka yale “mafundisho matano ya kidini ya Kalvin” katika vifungu hivi. Lakini watu hao wamekosea. Katika vifungu hivi Paulo anasema kuwa, “Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake.” Mungu alituchagua tangu asili ili tuwe watoto wake katika Kristo Yesu. Mungu alituchagua asili ili tuzaliwe katika ulimwengu huu chini ya mpango wake. Mungu alituumba ili tufananishwe na mfano wa nani? Ni ili tufananishwe na mfano wa Mwana wake. 
Mungu alituruhusu sisi kuzaliwa na kisha kuturithi ili tuwe kama watoto wake kwa kupitia Yesu Kristo kwa mujibu wa mapenzi yake. Mungu aliahidi kumtuma Mwanawe ili kutufanya sisi kuwa wana wake. Mungu alituita sisi kwa kupitia Yesu Kristo wakati tulipokuwa tungali wenye dhambi kama uzao wa Adamu. “Njooni kwangu ninyi nyote mnaosumbuka na kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha” (Mathayo 11:28). Mungu alituita sisi baada ya kuwa amekwishazichukua dhambi zetu zote. Mungu alituita ili atufanye sisi kuwa wenye haki kwa imani. 
 

Mungu Alitufanya Sisi Kuwa Wenye Haki na Alitutukuza 
 
Mungu aliwaita wenye dhambi na aliwafanya kuwa wenye haki mara moja na kwa ajili ya wote. Sisi sote tumeumbwa ili tuwe wenye haki mara moja na milele kwa kuamini katika Yesu Kristo Mwokozi wetu na si kwa kutakaswa kunakoendelea kama wanatheolojia wanavyosema. Mungu anawaita wenye dhambi na anawafanya kuwa wenye haki—hii ndiyo sababu inayomfanya Mungu kuwaita wenye dhambi. 
“Wale aliowaita, hao akawahesabia haki.” Wale walioitwa na Mungu na wanaoamini katika yale ambayo Yesu Kristo ameyafanya wanafanyika kuwa wenye haki. Hapo kabla sisi kama wazawa wa Adamu kwa hakika tulikuwa na dhambi, lakini dhambi zetu zote zilichukuliwa mbali wakati tulipoamini katika ukweli kuwa Yesu kwa hakika amezichukulia mbali dhambi zetu. Je, una dhambi katika moyo wako au la? Kwa kweli hapana! Hatuna dhambi tena iliyobakia ndani yetu. “Wale aliowaita, hao akawahesabia haki.”
Wenye haki ni wale ambao wamefanyika kuwa watoto wa Mungu. Si kweli kuwa tunafanyika kuwa watoto wake kwa hatua, yaani hatua kwa hatua. Badala yake, tunatukuzwa mara moja kama watoto wa Mungu kwa ukombozi wake. 
“Na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.” Mungu alitufanya sisi kuwa watoto wake. Ninashindwa kufahamu jinsi watu wanavyoamini juu ya “hatua tano za wokovu.” Wokovu na kufanyika watoto wa Mungu vinafanyika mara moja na kwa wote. Inatuchukua muda kushiriki katika ufufuo wa miili yetu kwa kuwa inatupasa kusubiri kuja kwa Bwana wetu mara ya pili lakini ukombozi wa dhambi unapatikana mara moja kama vile kope ya jicho inavyocheza. Tunaweza kuupata ukombozi mara moja wakati tunapolikubali Neno la ondoleo la dhambi zetu ambalo Mungu anayetuita ametupatia na pia tunapoyakubali yale ambayo ameyafanya ili kutuokoa. “Asante Sana, Bwana. Halleluya! Amen! Nimeokolewa kwa sababu uliniokoa. Nisingeweza kukombolewa ikiwa usingekuwa hujazioshea mbali dhambi zangu zote. Asante Sana, Bwana wangu! Halleluya!” Dhambi zetu zimetoweshewa mbali kwa njia hii. 
Ukombozi hauhitaji matendo yetu wala muda wetu. Matendo yetu hayana la kufanya hata kwa asilimia 0.1% katika ukombozi wetu. Wakalvin wanasema kuwa mtu anaweza kuhesabiwa haki hatua kwa hatua ili aweze kukombolewa na kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Kama vile mnyoo usivyoweza kukimbia kwa urefu wa mita 100 kwa sekunde hata kama ukijaribu kiasi gani, basi ukweli ni kuwa watu hawawezi kuwa wenye haki kwa kutegemea juhudi zao binafsi hata kama wangekuwa ni wazuri kiasi gani na hata kama wangejitahidi kuishika Sheria kwa kiwango cha juu. Mnyoo unabakia kuwa ni mnyoo hata kama utajiosha sana na kujipamba kwa vipodozi vya gharama kubwa. Vivyo hivyo, kwa kuwa wanadamu wana dhambi katika mioyo yao, basi watu hao wanabakia kuwa ni wenye dhambi hata kama wanaweza kuonekana kuwa ni watu wazuri kiasi gani. 
Inawezekanaje kwa mwenye dhambi kuwa mwenye haki mkamilifu kwa kutakaswa hatua kwa hatua? Je, mwili unafanyika kuwa bora kadri muda unavyozidi kwenda? Hapana, mwili unazidi kuwa na dhambi na mwovu zaidi kadri unavyozidi kukomaa na kuzeeka. Lakini Biblia inasema, “Na wale aliowachagua tangu asili hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.” Kifungu hiki kinapangilia kwa mfuatano yale yaliyotokea mara moja kwa neema ya Mungu; wala hakisemi kuwa ukombozi na kuhesabiwa haki vinatekelezwa kwa hatua. Mtu anaweza kufanywa mwenye haki mara moja na milele kwa kuwa na imani katika Bwana na si kwa imani ya utakaso unaozidi. 
Watheolojia wengi hali wakiwa hawajui kile wanachokifanya wamekuwa wakikazia nadharia mbovu wasizozifahamu na kwa sababu hiyo wamekuwa wakiwapeleka watu kuzimu. Mungu alituahidi sisi kupata ukombozi na akatuita sisi kwa kupitia Yesu Kristo, akatufanya kuwa wenye haki na kisha akawatukuza wale walioitika. “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. Ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12). Je, Mungu ametutukuza sisi? Ndiyo! Je, tunaweza kutukuzwa kwa kufanya matendo mema? Je, tunaweza kujaribu kwa juhudi ili kuwa wenye haki? Kwa kweli hapana. Sisi tumekwishafanyika wenye haki. 
 

Hakuna Anayeweza Kututenganisha na Upendo wa Mungu 
 
Ikiwa Mungu yupo upande wetu, ni nani anayeweza kuwa kinyume nasi? Hakuna. “Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajii yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. Ni nani atakaye tutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala mwenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Warumi 8:31-39).
Hakuna anayeweza kututenga na upendo wa Mungu. Hakuna anayeweza kutufanya sisi wenye haki kuwa wenye dhambi tena. Hakuna anayeweza kuwazuia wale waliokwishafanyika watoto wa Mungu ambao wataishi katika Ufalme wa Milenia na katika Ufalme wa Mbinguni. Je, mapigo yanaweza kutufanya sisi kuwa wenye dhambi? Je, mateso kwa ajili ya imani yanaweza kutufanya sisi kuwa wenye dhambi? Je, njaa, uchi, adha, au upanga vinaweza kutufanya sisi kuwa wenye dhambi? “Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?” Mungu anatupatia Ufalme wa Mbinguni. Anatupatia mambo yote bure kwa kuwa hakumzuilia Mwanawe pekee ili kutuokoa sisi. Ikiwa Mungu alihiari kufanya sadaka kuu ya kuteketezwa kwa ajili yetu inawezekanaje basi asitufanye sisi kuwa watoto wake? 
 

Ukombozi Ambao Mungu Anatupatia Ni...
 
Mungu anasema kuwa ili kukombolewa toka katika dhambi zetu kwanza kabisa ni lazima tukiri kuwa Yesu Kristo alitumwa kuja hapa ulimwenguni kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu Baba. Pili, ni lazima tukiri kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa kupitia ubatizo wake katika Mto Yordani. Tatu, ni lazima tukiri kuwa Yesu alisulubiwa kwa ajili yetu, na kisha akafufuka. Kwa kweli hatuwezi kuokolewa ikiwa hatuamini katika mambo hayo matatu hapo juu. 
Wale wasioamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu au kwamba Yesu ni Mungu na Muumbaji basi watu hao wametengwa toka katika wokovu wa Mungu. Ikiwa mtu anakana uungu wa Yesu Kristo, basi mtu huyo anakuwa ni mtoto wa Shetani. Wale wanaoukana ukweli kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake wakati alipobatizwa na Yohana Mbatizaji hawawezi kuokolewa pia. Yesu hawezi kuwa Mwokozi wao. Hawawezi kuokolewa katika mioyo yao hata kama wanamwamini Yesu kwa akili zao. Watu hao watakwenda kuzimu pamoja na kuwa wanamfahamu Yesu. Yesu Kristo alikufa kwa ajili yetu kwa kuwa alikuwa amezichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa ubatizo wake. Yesu alikufa kwa sababu ya dhambi zetu, na si kwa sababu ya dhambi zake. Kisha Yesu akafufuka tena toka kwa wafu ili kuwahesabia haki wale wote wanaoamini na kuwafufua katika ufufuo. 
 

Tunaokolewa Kwa Imani Katika Ubatizo Wake
 
Hadi sasa nimekwisha hubiri katika sura ya 7 nikiiunganisha na sura ya 8. Sura ya 7 inasema kuwa yeye aliye na dhambi hawezi kutenda mema. Lakini sura ya 8 inasema kuwa sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu na kwamba imani yetu katika Yesu Kristo inatufanya sisi kutokuwa na dhambi. Sisi ni wadhaifu na hatuwezi kuishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu, hivyo Mungu Baba alimtuma Yesu Kristo ili kuwa Mwokozi wetu, kisha Yesu akazichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa ubatizo wake wakati sisi tulipokuwa bado ni wenye dhambi. Sasa tumeokolewa toka katika dhambi zetu zote na ametufanya kuwa wenye haki kwa kupitia Yesu Kristo. Huu ndio ukweli ambao Paulo anaufundisha katika sura ya 7 na ya 8. 
“Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya Roho.” Sasa hatuna dhambi. Je, wewe umo ndani ya Yesu Kristo? Je, unakiri kile ambacho Yesu Kristo alikifanya kwa ajili yako? Kama ambavyo Paulo alivyokombolewa toka katika dhambi zake, basi dhambi zetu zote zimechukuliwa mbali pia kwa kupitia imani katika Ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. Tumekombolewa kwa kuamini katika ubatizo, damu na ufufuo wa Yesu. Ikiwa mtu anakataa kwa ujeuri kuamini katika ubatizo wa Yesu Kristo, na ikiwa mtu huyo anakazia kuwa Yesu alibatizwa ili kutuonyesha sisi unyenyekevu wake, basi Mungu atampeleka mtu huyo kuzimu. Usiwe na ujeuri mbele ya Neno la Mungu. Inawezekanaje kwa wachungaji na wahudumu kuudharau ubatizo wa Yesu wakati Paulo mwenyewe ameuzungumzia sana? Inawezekanaje wakaidharau imani hata ile ya Paulo ambaye ni mmoja kati ya mababa wakubwa wa imani? Wanawezaje kuyadharau mafundisho ya mtumishi wa Mungu ambaye Mungu mwenyewe alimfanya kuwa mtume? 
Ikiwa tunapenda kuhubiri kuhusu Yesu Kristo, basi ni lazima tuhubiri kama ilivyoandikwa katika Biblia, na ni lazima tuamini kwa mujibu wa Biblia. Bwana anatueleza sisi kuwa, “Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kwelil; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:31-32). Wewe na mimi tulifikia hatua ya kuuamini ubatizo wa Yesu kama alivyofanya Paulo. 
Ni lini dhambi zako zilipopitishwa katika mwili wa Yesu Kristo? Dhambi zako zote zilipitishwa katika mwili wa Yesu Kristo wakati alipobatizwa na Yohana Mbatizaji. Yesu alimwambia Yohana, “Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” Kwa lugha ya kiyunani kule kusema “kwa maana” “hoo’-tos gar”, kuna maanisha “kwa namna hii au kwa njia hii,” au “itupasavyo,” au “hakuna njia nyingine zaidi ya hii.” Neno hili linaonyesha kuwa kwa hakika Yesu alizichukua dhambi za wanadamu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo alioupokea toka kwa Yohana. Ubatizo maana yake ni “kuoshwa.” Ili dhambi zetu zote zilizo katika mioyo yetu ziweze kuoshwa basi ilipasa dhambi hizo kupitishwa kwenda katika mwili wa Yesu Kristo. 
Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu katika mwili wake, alisulubiwa badala yetu, na kisha alizikwa pamoja nasi. Hivyo Paulo alitangaza kuwa, “Nimesulubiwa pamoja na Kristo” (Wagalatia 2:20). Tunawezaje kusulubiwa wakati ukweli ni kuwa Yesu ndiye aliyeuawa Msalabani? Sisi tulisulubiwa pamoja na Kristo kwa sababu tunaamini kuwa Yesu alizichukua dhambi zetu katika mwili wake na kwamba alisulubiwa kwa sababu ya dhambi hizi. 
Ninamsifu Bwana ambaye ameniokoa toka katika dhambi zangu zote. Tunaweza kuihubiri injili kwa ujasiri kwa kuwa Yesu ametufanya sisi kuwa wenye haki. Ninamshukuru sana Bwana wetu kwa kutuokoa sisi ambao miili yetu ni midhaifu sana na ambao tumepungukiwa na utukufu wa Mungu kwa sababu ya dhambi zetu.