Search

Mahubiri

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-10] Tembea katika Roho! (Wagalatia 5:16-26, 6:6-18)

(Wagalatia 5:16-26, 6:6-18)
“Basi nasema enendeni kwa Roho wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mnaongozwa na Roho hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo hayo nayo uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi uadui, ugomvi, wivu hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayo fanana na hayo katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wamesulubishwa mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho na tuenende kwa Roho tusijisifu bure tukichokozona na kuhusudiana.” 
“Mwanafunzi amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote. Msidanganyike Mungu hadhihakiwi kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho katika Roho atavuna uzima wa milele. Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake tusipo zimia roho. Kwa hiyo tupatapo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio. Tazameni ni kwa herufi gani kubwa nimewaandikia kwa mkono wangu mimi mwenyewe! Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili ndiyo wanao washurutisha kutahiriwa, kusudi wasiudhiwe kwa jili ya msalaba wa Kristo hilo tu. Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu. Lakini mimi hasha nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambao kwa huo ulimwengu umesulubishwa kwangu na mimi kwa ulimwengu. Kwa sababu kutahiriwa si kitu wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. Na wote watakao enenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naamu, kwa Israeli wa Mungu. Tangu sasa mtu asinitaabishe kwa maana nina chukua mwilini mwangu chapa zakeYesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Amina.”
 

Tufanye nini ili kutembea
katika Roho?
Yatupasa kuihubiri na kuifuata
injili njema.

Mtume Paulo aliandika juu ya Roho Mtakatifu katika Waraka kwa Wagalatia. Katika Wagalatia 5:13-14 alisema “Maana ninyi, ndugu mliitwa mpate uhuru lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili bali tumikianeni kwa upendo. Maana torati yote imetimilika katika neno moja nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako”. 
Kwa kifupi; ujumbe huu ni kwamba kwa kuwa tumeokolewa na kuwekwa huru toka dhambini kwa kuiamini injili njema tusichukulie uhuru huu kama fursa ya kujiingiza katika tamaa ya mwili bali kwa upendo ya tupasa kutumikiana wenyewe kwa wenyewe na kuifuata Injili hii njema kwa jinsi Mungu alivyotuokoa kutokana na dhambi zetu zote. Ni vyema kwetu kuihubiri Injili. Paulo alisema pia kwamba “Lakini mkiumana na kulana angelieni msije mkaangamizana” (Wagalatia 5:15).
 

Enenda katika Roho Ujazwe Roho Mtakatifu

Katika Wagalatia 5:16 Paulo alisema “Basi nasema enendeni kwa Roho wala hamtazitimiza kwamwe tamaa za mwili”. Na katika mistari ya 22-26 alisema “Lakini tunda la Roho ni upendo furaha amani, uvumilivu utu wema, fadhili uaminifu, upole, kiasi juu ya mambo kama hayo kakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wa wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.” Tukiishi kwa Roho Mtakatifu anatuhitaji kutembea katika Roho. Lakini tunaishi katika mwili.
Sisi wanadamu tumezaliwa tukiwa na mwili ambao kamwe hautoweza kuzaa tunda la Roho. Hata kama tukijaribu kutembea katika Roho, asili yetu haitoweza kubadilika. Na ndiyo maana ni wale tu watakao upokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao kwa kuamini Injili njema ndiyo watakao weza kutembea katika Roho na kuzaa tunda la Roho.
Biblia inapotuambia kutembea katika Roho inamaana kwamba yatupasa kuihubiri Injili njema ili wengine waweze kusamehewa dhambi zao. Tunapoishi katika Injili ndipo tutakapo zaa tunda la Roho kwa maneno mengine si swala la kubadilisha asili ya kuzaliwa. Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu upole, kiasi. Tunda la Roho hutusaidia kuwatumikia wangine kutoka katika dhambi zao kwa wokovu na kupata uzima wa milele.
 

Tamaa za mwili dhidi ya Matakwa ya Roho.

Paulo alisema “Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho na Roho kushindana na mwili kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka” (Wagalatia 5:17). Kwa kuwa sisi tuliokwisha kukombolewa tuna tamaa za mwili na za Roho kwa wakati mmoja vitu vyote hivi viwili wakati wote huvutana. Matokeo yake ni kwamba kipo kimoja kisicho weza kutosheleza mioyo yetu.
Roho hutufanya kutamani ndani ya kina cha moyo kuihubiri Injili njema na kumtumikia Bwana. Hutufanya kuwa wakereketwa katika kujihusisha na kazi za kiroho. Hutusaidia katika kuwatumikia wengine tokana na dhambi zao katika wokovu kwa kuwahubiria Injili njema ya Mungu.
Lakini kwa upande mwingine matakwa yetu huamsha tamaa za mwili hivi tusiweze kutembea katika Roho. Hii ni vita ya milele kati ya Roho na tamaa za mwili katika kuutumikia mwili. Mwili huweka matakwa yake kinyume na Roho. Vyote hivi kupingana hatakufikia hali ya kutotenda tusiyo penda.
Sasa basi, nini kinachohusika katika kutembea katika Roho? Na ni vitu gani vinavyo mridhisha Mungu? Mungu alisema kwamba kuihubiri na kuifuata Injili njema ndiyo maisha ya kutembea katika Roho. Huwatia moyo wale wote wanao tembea katika Roho na walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao, ili waweze kuzaa tunda la Roho. Kwa Paulo kutuambia kutembea katika Roho ilikuwa ni kutuasa na kutuamuru kutumikia wengine katika wokovu wa dhambi zao kwa kuwahubiri Injili njema. Kutembea katika Roho maana yake ni kuishi maisha ya kumridhisha Mungu.
Ili tuweze kutembea katika Roho tunahitaji kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu. Kabla ya yote yatupasa awali kuiamini Injili njema ambayo Mungu alitupatia ikiwa tunataka kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yetu. Kama hatutoamini Injili njema miayoni mwetu kwa ndani, hatutoweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu wala kupata wokovu kwa dhambi zetu, ambapo inamaana hatutoweza kutembea katika Roho.
Roho hutuelekeza kuhubiri Injili njema kumtumikia Mungu na kumletea Mungu utukufu. Matakwa hayo huja toka katika moyo ulio jitolea kwa Mungu na kuihubiri Injili njema duniani pote. Pia huja toka katika moyo ulio na hiyari kutenda chochote kinacho hitajika katika kuihubiri Injili njema. Wale wote wanaoiamini Injili njema na kumpokea Roho Mtakatifu baada ya kusamehewa dhambi zao ndio watakao weza kutembea katika Roho na kujitolea nafsi zao kuihubiri Injili. Huu ndio urithi wao toka juu.
Wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao ndiyo watakao mtii Roho Mtakatifu na kutembea katika Roho, ingawa bado wangali na tamaa za mwili kwa sababu Roho Mtakatifu kaweka makazi ndani yao. Paulo alisema “Enendeni katika Roho” Anacho maanisha hapa ni kwamba ni lazima tuihubiri Injili njema ya maji na Roho Mtakatifu ambayo Yesu alitupatia ili tuweze kuwasaidia wengine katika kusamehewa dhambi zao.
Wakati mwingine tunapokuwa tukitembea katika Roho kwa wakati huo pia tunakuwa tukitembea katika mwili. Tamaa ya mwili na matakwa ya Roho huwa katika vita katika maisha yetu, lakini tunacho paswa kuelewa hapa na kugundua kwa uwazi ni kwamba, wale wote walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao lazima waenende katika Roho. Kwa njia hii pekee ndipo tutakapo weza kujazwa na baraka za Mungu. Ikiwa wale walio na uwepo na Roho Mtakatifu watakataa kuzaa tunda la Roho basi wataishia kuangamia. Hivyo basi matunda yao ni rahisi kuharibika na ya siyofaa, na hapo ndipo ilipo sababu ya kuishi na kutembea katika Roho.
Tumekwisha sikia “Kutemea katika Roho” lakini baadhi yetu tunaweza kudhani, “Nitawezaje kufanya hivyo wakati sihisi uwepo wa Roho wa Mtakatifu ndani yangu.” Baadhi yetu tunadhani kwamba tunaweza kugundua uwepo wa Roho Mtakatifu pale tu Mungu anapoonekana na kuzungumza moja kwa moja nasi. Lakini huku ni kuelewa vibaya. Roho hutupa hamu ya kuishi katika Injili njema ya maji na Roho.
Upo muda mwingine tunapokuwa na uhakika ndani yetu lakini hatuwezi kumhisi kwa sababu tunatembea katika mwili, wengi baadhi wanaweza kumhisi Roho Mtakatifu huku wangalia wakitembea katika mwili. 
Watu hawa wanafariji miili yao wenyewe na hufanya kama inavyoamuru lakini wanateseka mwishoni kwa sababu ya mahitaji ya mwili ya kuongezeka. hata wale ambao wanaishi ndani ya Roho Mtakatifu huwa wanaishi kulingana na tamaa za miili yao, kwa sababu wanafikiri ni kawaida kufanya hivyo. Lakini wale ambao hujitiisha kwa mwili hatimaye huwa watumwa wa mwili.
Bwana anatuambia tuishi katika Roho maana yake ni kuitumikia Injili njema. Maana yake pia ni lazima tujitolee nafsi zetu kwa dhati katika Injili njema ya maji na Roho. Yatupasa kuishi namna hiyo kwa kujifunza maana ya kuenenda katika Roho. Je, wewe una enenda katika Roho?
 

Je, mtu asiye na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake ataweza kuenenda katika Roho?

Wale wote ambao hawajazaliwa upya mara ya pili hawawezi kuelewa nini maana ya kuenenda katika Roho. Hivyo watu wengi hujaribu kumpokea Roho Mtakatifu na kumtamani kwa kupitia njia zao binafsi. Hudhani kwamba tendo la kumtamani ni sawa na kujazwa naye.
Kwa mfano, wakati watu wanapokusanyika katika ushirika fulani kwa ibada, mtumishi kiongozi husali kwa sauti na ndipo kila mtu huanza kulia kwa sauti wakiliitia jina la Bwana. Baadhi yao husikika wakinena kwa lugha utadhani wamejazwa na Roho Mtakatifu lakini hakuna lolote katika hayo kuwa ni kweli, kwani hata wenyewe hawaelewi wanalofanya au kusema. Wakati huo pia baadhi yao huanguka chini hovyo na miili yao kuanza kutetemeka kwa furaha. Hakika watu hawa huwa wamekumbwa na pepo lakini wao hudhani kwamba ndio wamempokea Roho Mtakatifu. Hapo ndipo hujaa kelele zaidi pale watu wanapo paza sauti ama kulia kwa sauti “Bwana Bwana!” Huita Bwana machozi yakiwatiririka na kupiga makofi. Hali hii isiyo ya kawaida mara nyingi wao husema kuwa ndiyo “kujazwa Roho Mtakatifu”.
Huku mtumishi huyo akinena kwa lugha naye, watu hupiga kelele na kuita “Bwana Bwana!” watu ainia hii hupendelea aina hii ya hali na hata baadhi huanza kushuhudia kuwa wamepata maono juu ya mti wa matunda ya kujua mema na mabaya katika bustani ya Edeni na maono ya uso wa Yesu wakati wa mfadhaiko huo wa aibu. Hukosea katika mambo haya pale wanapo dhani ndiyo kumpokea Roho Mtakatifu au kujazwa naye na kuenenda naye. Matunda haya potofu husababishwa na kutokujua juu neno la Mungu na Roho Mtakatifu. 
Kuenenda katika Roho hivi ndivyo Mungu asemavyo kwa wale tu walio zaliwa upya mara ya pili. Maana yake ni kufanya mambo yampendezayo yeye. Paulo alifananisha matendo ya mwili na lile tunda la Roho Mtakatifu akisema “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi” (Wagalatia 5:22-23).
“Kuenenda katika Roho” maana yake ni kuihubiri Injili njema na kuwatumikia wengine kwa wokovu wa dhambi zao. “Tunda la Roho ni upendo, furaha amani, uvumilivu, utu, wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi” na tutaweza kuzaa tunda hili ikiwa tutaishi katika Injili njema. Mtu akiihubiri na kuitumikia Injili, akijitoa nafsi yake kwa ajili ya Injili ndipo atakapo weza kuenenda na kuishi maisha ya kujazwa Roho Mtakatifu.
“Utu wema” Maana yake matendo mema. Pia maana yake ni mkazo katika kazi njema ya Injili na kufanya jambo kwa faida ya wengine ndiyo utu wema. Jambo kuu lililo jema mbele ya Mungu kati ya yote ni kuihubiri Injili kwa faida ya wengine.
Na “fadhili” ni kuona huruma kwa watu. Aliye na rehema kwa wengine ndiyo hutumikia Injili kwa uvumilivu na kwa fadhili na kupata amani. Anayetembea katika Roho ni mwenye furaha kila anapoona kazi ya Bwana ikikamilishwa. Hupenda kufanya kazi yake, kuwapenda wengine na kuwa mwanimifu kwa yote. Ingawa hakuna yeyote ambaye amempa jukumu la lazima katika kufanya hilo, aliye na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake ni mwaminifu kwa kazi yake hadi pale anapokamilisha. Ni muungwana na hujizuia au ni mtu wa kiasi. Mtu huyu ndiye aliye na tunda la Roho. Aliye na Roho Mtakatifu ndani yake imempasa kutembea katika Roho. Anapotenda haya ndipo atakapoweza kuzaa tunda la Roho.
Nawe pia utaweza kuzaa tunda la Roho ikiwa utaenenda katika Roho. Lakini kama hutoenenda hivyo matokeo yake utaishia kutembea katika tamaa ya mwili. Maandiko yanasema katika Wagalatia 5:19-21 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya uasherati, uchafu, ufisadi ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayo fanana na hayo katika hayo nawaambia mapema kama nilivyo kwisha kuwaambia ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawata urithi ufalme wa Mungu”.
 

Matendo ya kimwili ni bayana

Matendo ya kimwili ni bayana. Moja wapo ya kwanza katika matendo ya kimwili ni “uasherati.” Maana yake ni kujiingiza katika mahusiano ya kimwili na jinsia tofauti. La pili ni “uzinzi”, Tatu “uchafu”, Nne “tamaa mbaya”, maana yake tamaa ya mwili, Tano “ibada ya sanamu” ambapo maana yake ni kutumikia sanamu kuliko Mungu, Sita ni “uchawi”, Saba ni “uadui”. Ikiwa mtu hana Roho Mtakatifu hutembea katika mwili, hivyo hatoweza kujizuia kuwa na uadui na wengine kutokana na asili yake. Nane ni “ugomvi.” Hii maana yake kuzusha tafrani na marafiki au familia. Mengine ni “wivu, hasira, husuda na ulafi.” Yote haya ni dalili ya mtu atembeaye katika mwili.
Kumi ni “faraka.” Mtu anapo enenda katika mwili wakati wote si rahisi kwake kufanya kazi katika kanisa na hatimaye ataishia kulihama kwa sababu ya ugomvi. Kumi na moja ni “uzushi.” Anaye tembea katika mwili hufanya hivyo ili kuiridhisha nafsi yake na mapenzi yake. Lakini maisha hayo ni tofuati na Injili njema. Uzushi maana yake ni kuugeuzia kisogo ukweli wa biblia. Hapana yeyote aliye na imani katika neno la Mungu na kutembea katika Roho awezaye kugeuzia kisogo mapenzi ya Mungu. “Husuda, ulevi, uuaji, na mambo yafananayo na hayo katika mwili, mtu hutenda, na ndiyo maana Bwana anasema “enenda katika Roho.” Sisi tulio zaliwa upya yatupasa kuenenda katika Roho.
Wale amabao hawajazaliwa upya mara ya pili hawana lolote zaidi ya tamaa ya mwili mioyoni mwao. Ndiyo maana hujihusisa na “uasherati, uchafu ufisadi na ibada ya sanamu.” Watumishi wasio zaliwa upya mara ya pili kujihusisha na “uchawi” kwa wafuasi wake ili kuwashawishi kuchangia fedha nyingi. Hugawa madaraka na nafasi kubwa za kanisa kwa wale wote wenye kuchangia zaidi. Wale wote wenye kuishi katika mwili kuchukia wengine. Hugawa makanisa katika madhehebu mengi, kujigamba na madhehebu yao na kushutumu wengine kuwa ni wazushi. Uadui, ugomvi vimo ndani ya mioyo ya wale ambao hawajazaliwa upya mara ya pili. Na hii itawezekana kwetu pia ikiwa tutatembea katika mwili.
 

Roho ndiye imwezeshaye Mkristo aliye zaliwa upya mara ya pili kuzaa tunda la Roho Mtakatifu

Wale wote waliozaliwa upya mara ya pili emewapasa kuishi huku wakihubiri Injili njema. Kama ilivyo vigumu kumfuata Bwana tukiwa peke yetu, nilazima tuifanye kazi ya kuitumikia Injili njema kwa kujiunga na kanisa la Mungu. Imetupasa kusali na kuomba kwa pamoja na kujitolea nguvu zetu, kuwa watu tunao tembea katika Injili njema ya Roho. Watu wenye kutembea katika Roho huishi huku wakiihubiri injili ya maji na Roho. Kwa maneno mengine, kutembea kwa kuufuata mwili maana yake ni kuishi maisha binafsi, hali kuenenda katika Roho maana yake ni kutumika katika wokovu wa nafsi nyingine. Wengi wa Wakristo walio zaliwa upya, huishi maisha mema. Huishi kwa kuwatendea mema wengine.
Ipo idadi kubwa ya watu duniani ambao bado kabisa hawajapata kuisikia Injili njema. Tunawapenda watu wa Afrika na Asia. Tunampenda kila mmoja katika Ulaya na Amerika pamoja na visiwa vyake. Yatupasa kuonyesha upendo kwa kuitambulisha Injili ya maji na Roho kwao.
Yatupasa kuenenda katika Roho. Hapana sheria katika hili “Tunda la Roho ni upendo furaha, amani, uvumilivu, utu wema fadhili, uaminifu, upole, kiasi, juu ya mambo kama hayo hakuna sheria” (Wagalatia 5:22-23). Je, kuna sheria yeyote iliyo kinyume na hili? Hapana hii ni sheria ya Roho ambayo imetupasa kuitii. Paulo anatueleza kuenenda katika Roho. Kama vile Bwana wetu alivyo toa uhai wake kwa ajili ya wenye dhambi yatupasa pia nasi kuihubiri Injili yake kwa wengine. Kutumikia wengine katika wokovu wa dhambi zao ndiyo kuenenda katika Roho.
Paulo alisema katika Wagalatia 5:24-26 “Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa Roho na tuenende kwa Roho. Tusijisifu bure tukichokozana na kuhusudiana”. Yatupasa kuishi kwa kutumikia nafsi zilizo potea katika wokovu na ndiyo kuenenda katika roho. Roho Mtakatifu amabaye Mungu alitupatia hutuongoza katika kuishi na Yesu Kristo moyoni.
Paulo alisema “Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake” (Wagalatia 5:24). Pia alisema kwamba wale walio zaliwa mara ya pili wamekufa pamoja na Yesu Kristo. Wale walio zaliwa mara ya pili ni kweli tayari wamekwisha kufa na Yesu. Hatuelewi hili kwa wakati mwingine, lakini ukweli ni kwamba tumekufa na Yesu Kristo. Kusulubiwa maana yake ni wewe na mimi kufa naye msalabani. Kifo chake ni kifo chetu na ufufuo wake ni alama ya uhakika wa kufufuka kwetu pia. Wewe na mimi tunaishi na kufa katika Yesu Kristo kwa njia ya Imani. Yatupasa kuwa na Imani. Imani yetu hutuongoza katika kuenenda katika Roho.
Mungu ametupa nguvu katika kuenenda katika Roho. Hivyo sisi tuliokwisha samehewa dhambi zetu zote imetupasa kushukuru kwamba dhambi zetu zote zilisamehewa na hivyo kujitolea katika kuihubiri Injili njema kwaajili ya wokovu wa walio potea. Ingawa mtu amesamehewa dhambi zake na kuzaliwa upya mara ya pili, ataweza kuwa mbali na kanisa la Bwana na kushindwa kumtumikia yeye ikiwa ataishi kwa kuifuata tamaa ya mwili. Mimi na wewe imetupasa kuishi kwa Injili ya maji na Roho hadi mwisho wa ile siku ya Bwana Yesu Kristo.
 

Tusijisifu bure kamwe bali tuenende kwa ukamilifu wa Roho Mtakatifu

Paulo alisema nini maana ya neno “kujisifu bure?” Ni kuenenda kwa tamaa ya mwili. Wapo watu wengi duniani wanao enenda wakijisifu bure nafsi zao. Watu wengi kujilimbikizia fedha, kutamani ukuu, kupenda mambo mazuri ya dunia na kuishi kwa mtazamo wa mahala alipo kwa wakati uliopo tu. Hakuna uaminifu katika hili hivyo wataoza na kuangamia kadiri siku zinavyo kwenda. Na ndiyo maana watu wanaoenenda katika mwili huitwa wapenda sifa za bure. Hata kama watu wanautajiri, je, ipo amani na kutosheka mioyoni mwao? Tunda la mwili hatimaye ni kuoza. Vitu vya dunia havina faida kwa roho za wengine bali kwa yule aliye navyo tu. Vinafaida kwa yule tu anaye enenda kwa mwili.
Biblia inasema “Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi kuna azuiaye isivyo haki lakini huelekea uhitaji” (Methali 11:24). Wale ambao bado hawajazaliwa upya mara ya pili hujaribu kujilimbikizia fedha kupita kiasi. Kwa kuwa vitu vya dunia ni kipaumbele kwao, hawana nafasi kabisa katika kuwajali wengine. Na ndiyo maana hutaka na kujali zaidi maisha yao. Lakini Biblia inasema kwamba kuna azuiaye isivyo haki lakini kuelekeza uhitaji na hivyo kumfanya fukara. Watu huenenda kwa tamaa ya mwili, lakini matokeo yake ni sawa na kukumbana uso kwa uso kwa kujibamiza katika mlango wa chuma na kufa. Mwisho wa yote haya ni matokeo ya kujisifu bure.
 

Wale wanaopenda kufuata matamanio ya Roho.

Paulo alipenda kuishi maisha katika Roho. Na alifanya hivyo. Alitufundisha kuishi vyema kwa njia ya neno la Mungu. Alisema katika Wagalatia 6:6-10 “Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake, msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwakuwa chochote apandacho mtu ndicho atakacho vuna, maana yeye apandaye kwa mwili, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa roho katika roho atavuna uzima wa milele. Tena tusichoke katika kutenda mema maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwetendee watu wote mema, na hasa jamaa ya waaminio.”
Paulo aliwashauri wale wote walijualo neno la Mungu wawashirikishe mambo mema waalimu wao. Hapa “mema” alimaanisha kumfurahisha Bwana kwa kutumikia Injili kwa nafsi zilizo potea kwa njia ya kuenenda katika Roho kwa kuihubiri Injili njema. 
Wale wote waliozaliwa upya mara ya pili imewapasa kuwaunga mkono wanao fundisha na kuenenda katika Roho huku wakiwa na lengo moja, upendo na hukumu moja. “Amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote”. Mambo haya “mema” ni katika kutumikia Injili kwa ajili wengine waweze kuokoka kwa njia ya kanisa. Paulo ametuambia tufanye kila jambo kwa nia moja katika sala moja na katika kujitolea pamoja. Yatupasa kufanya kazi ya Bwana pamoja.
Paulo alisema “Msidanganyike Mungu hadhihakiwi kwa kuwa cho chote apandacho mtu ndicho atakachovuna” hapa neno “dhihaka” maana yake kungo’ng’a au “kuzomea kwa ishara ya dharau na kejeli.” Hivyo “Msidanganyike Mungu hadhihakiwi” maana yake ni kusema usimngo’ng’e au kumzomea au kumdhihaki Mungu. Kwa mfano mtu asilichukulie neno la Mungu kijuu juu kutafsiri kwa maneno yake na hata kushindwa kuamini. Paulo alisema “kwa kuwa chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna” Maana yake ni kwamba apandaye mwili atavuna uharibifu lakini apandaye Roho atavuna uzima wa milele na wokovu wa dhambi zake. Tutavuna tunda la Roho kwa kuongoza nafsi za wengine kuelekea katika ukombozi kwa dhambi zao na uzima wa milele kupitia baraka za Mungu.
Lakini vipi kuhusu wale wanaoenenda katika mwili? Huvuna uharibifu na hatimaye hakuna jingine zaidi ya kifo. Hakuna la zaidi kwao baada ya kifo. Mwanadamu amezaliwa mikono mitupu na hufa akiwa mikono mitupu.
Akifanya kazi kwa ajili ya wokuvu wa wengine basi ataweza kuvuna tunda la Roho na uzima wa milele. Lakini akiendelea kuenenda katika tamaa za mwili ataishia kuvuna uharibifu. Atavuna laana na moja kwa moja kuirithisha laana hiyo kwa wengine.
Hivyo Paulo ambaye alifahamu mengi juu ya kuenenda kwa imani alishauri kwetu tusienende kulingana na mwili. “Tena tusichoke katika kutenda mema maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia roho” Paulo alikuwa mtumishi wa Mungu aliyeeneda katika Roho.
Pindi watu wanapoona katika Biblia swala la kuenenda katika Roho, baadhi wanaweza kudhani Roho Mtakatifu atawaagiza moja kwa moja kufanya mambo kama vile “Paulo nenda kulia na ukutane na mtu fulani” au “imekupasa umwepuke mtu huyu” lakini hivi sivyo kweli.
Alienenda katika Roho kwa kuihibiri Injili ya wokuvu kwa wengine na kusaidia katika wokovu wa nafsi zao. Paulo pia alimtumikia Bwana kwa kujiunga na wengine ambao nao walienenda katika Roho. Kati ya wakristo, wapo watu wasio enenda katika Roho bali kulingana na tamaa za miili yao. Hawakumkaribisha Paulo bali walimpinga na kumsingizia uongo. Paulo alisema hakuhitaji chochote kutoka kwao hao walio mpiga vita na kuwasingizia uongo wafuasi wa Yesu Kristo.
Ikiwa unataka kuenenda katika Roho yakupasa uifuate Injili siku zote. Walimuudhi Paulo. Katika Wagalatia 5:11 inasema “Nami ndugu zangu ikiwa na hubiri habari ya kutahiriwa kwa nini ningali nina udhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika!” Waliotahiriwa walikuwa ni wale walioshindania desturi ya tohara wakisema “Ingawa mtu atazaliwa upya mara ya pili kwa Imani katika Yesu inampasa atahiriwe. Ikiwa hatotahiriwa govi lake kamwe si mwana wa Mungu” Kwa nini walimuudhi? Ni kwasababu Paulo aliamini kwamba ukombozi na baraka ya uzima wa milele ilikuja kwa imani tu ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, na hili ndilo basi alilokuwa akilihubiri siku zote.
Imani ifanyayo watu waweze kuwa wenye haki huja toka kwa kujifunaza ukweli na kuuhuhubiri ukweli huo. Paulo alichukulia ukweli juu ya maji na Roho kuwa ndiyo muhimu zaidi ya yote. Aliamini kwamba wale wote walio kwisha elewa ukweli waliweza kuenenda katika Roho na hivyo hapakuhitajika kwao kutahiriwa na hivi ndivyo alivyo hubiri.
Lakini wale waliotahiriwa waliamini tohara kuwa ni sehemu muhimu katika imani binafsi ya wokovu. Hata hivyo hakuna Injili zaidi ya ile iliyoshushwa na Mungu na hivyo imetupasa tusiongeze chochote au hata kuondoa chochote katika hiyo.
Wakati Paulo alipoenenda katika Roho, alidharauliwa na kuudhiwa na Wayahudi wenzake. “Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo; hilo tu kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari juu ya miili yenu. Lakini mimi, hasha nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambao kwa huo ulimwengu umesulubishwa kwangu na mimi kwa ulimwengu kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa bali kiumbe kipya” (Wagalatia 6:12-15). Na Paulo alisema kwa waliotahiriwa. “Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa; makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo.”
Paulo aliwakemea wale waliokuwa wakienenda katika tamaa ya mwili. Katika nyakati za Matendo ya Mitume na palikuwepo na watu wengi kama hao. Lakini Paulo alikataa mahusiano nao. Paulo alisema “Lakini mimi hasha nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo”. Yesu Kristo alibatizwa na Yohana ili kubeba dhambi zote za ulimwengu na kufa msalabani katika kumwokoa Paulo na watu wote kwa jinsi Mungu atakavyo waita. Paulo alisema “Ulimwengu umesulubishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu, kwa sababu kutahiriwa si kitu wala kutotahiriwa bali kiumbe kipya” Paulo alikuwa amekufa kwa ulimwengu na kuishi kupitia Yesu Kristo tena.
Ukweli ni kwamba, nasi pia tunakufa katika Yesu Kristo. Lakini wakati mwingine tunasahau juu ya ukweli huu. Yatupasa kuamini hili kama hatuna imani ya ukweli huu. Tutakuwa tumefungwa kwa tamaa za mwili na familia zetu na hata kutuzuia kuenenda na Bwana. Miili yetu ni dhaifu kiasi kwamba hata familia zetu haziwezi kutusaidia katika kumfuata. Ni yeye Bwana tu ndiye awezaye kutusaidia. Lakini sasa tumesulubiwa na ulimwengu. Watu walio kufa watawezaje kusaidia watu wa ulimwengu kwa mambo ya ulimwengu? Watu waliokufa katika dunia hii hawawezi kamwe kuhodhi vitu vya duniani.
Yesu alifufuka, na ufufuo wake ndio uliotuwezesha kuzaliwa upya mara ya pili katika maisha mapya kiroho. Sasa leo hii unayo kazi mpya, familia mpya na tumaini jipya. Sisi ni watu tulio zaliwa upya mara ya pili. Tukiwa kama askari wa mbinguni tunajukumu la kulihubiri neno la Mungu. Paulo alikiri kwamba alikuja akiwa mtu wa kusaidia wengine katika kuupata wokovu si kwa njia za kimwili bali kwa kupitia njia za kiroho. Alisema kwamba yeye yu tayari amwekwisha kufa na kuzaliwa upya kwa njia ya Yesu Kristo. Tujibidishe ili tuwe watu tutakao thubutu kutoa tamko la imani zetu kama yeye.
Paulo alisema katika Wagalatia 6:17-18 “Tangu sasa mtu asinitaabishe kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu. Ndugu zangu neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu Amina.” Paulo alichukua mwilini alama za Bwana Yesu. Kutojali juu ya afya yake kwa ajili ya Bwana ndiko kuenenda katika Roho. Hakuweza hata kuandika pale alipoanza kuingiwa na upofu hatua kwa hatua. Hivyo baadhi ya nyaraka zake nyingi ziliandikwa na washirika wake kama vile Tito pale alipokuwa akiongea maneno ya Mungu. Ingawa kimwili alidhoofika bado alikuwa ni mwenye furaha hata kuweza kuenenda katika Roho na kusema “Kwa hiyo hatulegei bali ijapokuwa utu wetu wa nje anachoka, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku” (2 Wakoritho 4:16).
Paulo anatushauri tuwe wema kwa watu ambao nao huenenda kwa Roho. Pia anasema “Kuenenda katika Roho maana yake ni kuishi maisha ya kuieneza Injili” mimi na wewe ni lazima tuelewe kwamba, nini maana ya kuenenda katika Roho. Tusihangaikie katika kutafuta mambo yasiyo na maana na badala yake tuitumikie na kuishi katika Injili. Hebu na tuenende katika Roho kwa imani maishani mwetu pote.
Sasa basi kwa kuamini Injili ya maji na Roho, Roho wa kweli yumo ndani ya mioyo yetu kwa furaha Mungu atajibu punde tunapo omba kulingana na Injili. Kuzaa tunda la Roho maana yake ni kuenenda katika Roho na kusaidia katika ukombozi wa nafsi nyingine. Utaweza kuzaa tunda la Roho ambamo kuna upendo, furaha amani, uvumilivu, utu wema, fadhili uaminifu, upole kisasi, pale unapo enenda katika Roho na kuishi katika Injili. Kuihubiri Injili ya maji na Roho lazima utaabike, uvumilie, ufanye mema na kutenda mazuri kwa nafsi zinazopotea.
Tunda la Roho huzaliwa kwa wale wote wanaojishughulisha katika kazi ya kuokoa nafsi zipoteazo kwa kuwatendea mema na kuwahubiria Injili ambayo huwawezesha kumpokea Roho Mtakatifu. Haya yote hutokea katika kuzaa tunda la Roho na kuenenda katika Roho.