Search

Mahubiri

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-9] Injili ya ubatizo wake iliyo tutakasa (Waefeso 2:14-22)

(Waefeso 2:14-22)
“Kwa maana yeye ndiye amani yetu aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja, akabomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuondoka ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapa njia ya msalaba akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. Akaja akahubiri amani kusema ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Basi tangu sasa ninyi si wageni wale wapitaji bali ninyi ni wanyeji pamoja na watakatifu watu wa nyumbani mwake Mungu Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni katika yeye jengo lote linaunganishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.”
 
 
Nini kilicho
mtenganisha mwanadamu
na Mungu?
Dhambi zake ndizo zilizo
Mtenganisha
 

Mtoto aliye rithiwa kutokana na ufukara

Nusu ya karne imekwisha pita tangu toka kuisha kwa vita ya Wakorea, lakini imeacha majeraha makubwa kati ya watu wa nchi ya Korea. Baada ya tukio hili la kivita watoto wengi wadogo walirithiwa kwa mataifa ya ughaibuni, kutokana na jeshi la umoja wa Mataifa lililokuja Korea na kutusaidia kwa juhudi wakati huo, kuzaa na wanawake wa Korea, na hivyo watoto wengi walibaki hawana baba baada ya wao kurudi makwao.
Baadhi ya wengi wa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa walikuwa na wanawake na watoto katika Korea, hivyo waliporudi makwao waliwatelekeza nyuma. Wengi wa watoto hawa nao waliachwa na kutelekezwa na mama zao katika nyumba za mayatima na hatimaye ilibidi wapelekwe nchi za ughaibuni kwa nia ya kurithiwa. Hakika ilikuwa ni bahati njema kwa vijana hawa kuweza kupata wazazi walezi na hivyo kulelewa vyema.
Watoto hawa walio rithiwa waligundua ya kwamba walikuwa na utofauti dhidi ya wazazi walio kuwa wakiwalea na hata majirani zao kila walipokuwa wakikuwa kiumri na hivyo kung’amua kwamba walikuwa wamerithiwa toka nchi ya mbali, Korea. “Kwa nini wazazi wangu walinitelekeza?” kwa uchanga wa akili zao watoto hawa hawakuweza kuelewa nini kilicho wapata.
Utundu wao wa kutafiti na chuki dhidi ya wazazi wao wa kweli ulianza kuchipua mioyoni mwao na kutamani kukutana nao. “Nashangaa sijui wazazi wangu wanafananaje? Waliwezaje kunitelekeza? Hivi walitenda hili kwa sababu walikuwa wakinichukia? La hasha labda palikuwepo na sababu ya hili” Labda walikuwa na mengi wasiyo yaelewa na wakati mwingine ilipelekea wewe na chuki kubwa. Na nyakati zingine walipendelea zaidi kuachana kabisa na mambo haya katika fikra zao. Kabla ya hata kuwa na ufahamu juu ya haya muda ulipita na watoto hawa walikuwa kiumri hata kuwa watu wazima, waliingia katika ndoa na kupata watoto na kuunda familia zao.
Nilitamani kujua juu ya watoto hawa kupitia kipindi maalumu katika mtandao wa hapa wa TV. Katika kipindi hicho, mtoa habari wa TV hiyo alikuwa akimhoji mwanamke mmoja ambaye kwa wakati huo alikuwa akiishi Ujerumani na ambaye aliwahi kurithiwa. Mwanamke huyu alikuwa na umri kati ya miaka ishirini kwa wakati huo na alikuwa akijifunza theologia. Mwanzoni alianza kujizuia kukutana na watoa habari kwa sababu hakupenda mtu yeyote kujua ya kuwa yeye aliwahi kurithiwa. Mtoa habari huyo alimshawishi ya kwamba kukubali kwake ahojiwe kungesadia kuchochea wimbi la waliorithiwa mataifa ya ughaibuni kujua hatima na asili zao. Hatimaye mwanamke huyo alikubali.
Moja ya swali la mwana habari huyo lilikuwa “Utasema nini ikiwa utakutana na wazazi wako halisi?” Mwanamke huyo alijibu “Sielewi kwanini waliniacha nirithiwe. Ningelipenda kuwauliza ikiwa walinichukia. Mama yake mzazi aliyaona mahojiano hayo katika TV. Na hivyo kuwasiliana na kituo hicho cha kurusha matangazo huku akisema angelipenda kukutana na mtoto wake. Na hivi ndivyo alivyo kutana naye tena.
Mama huyo alidamka mapema kuelekea uwanja wa ndege na kusubiri kuwasili kwa binti yake, Binti alipowasili katika sehemu ya kutokea, mama yake alisimama wima na kuanza kulia.
Watu hawa wawili hawakuwahi kukutana uso kwa uso, mara ya kwanza mama alipo mwona binti yake huyo aliye kuwa kiumri ni katika kipindi cha TV. Ingawa walikuwa wakionge lugha tofauti, waliweza kuongea kupitia mioyo yao, na kupitia hisia nyusoni mwao kwa mawasiliano, Walifanana sana nyuso zao huku mama akiomba msamaha kwa aliyoyafanya. Alichoweza ni kulia tu na kurudia kuomba msamaha.
Mama alimpeleka binti yake huyo nyumbani kwake na kushiriki karamu pamoja ingawa binti aliweza kuongea kijerumani tu na huku mama naye kikorea waliweza angalau kuwasiliana ingawa si kwa maneno. Kwa sehemu fulani kwa kuwa walikuwa ni mama na binti yake hii iliwezesha kwao kuelewana zaidi. Walikuwa na mawasiliano ya kibubu na kujionyesha zaidi kwa nyuso, kushikana na kupapasana nyuso zao na kuzungumza kwa kupitia macho na mioyo yao.
Ulipofika wakati wa binti kurudi Ujerumani, tayari alikwisha kungundua ya kwamba mama yake alikuwa akimpenda. Mwanahabari yule aliyekuwa akiongoza kipindi hicho pia alimuuliza kwa mara nyingi tena swali lile la awali kabla ya kurudi, binti alijibu “Sina haja tena ya kumuuliza mama yangu sababu ya yeye kunitelekeza hadi kufikia kurithiwa. Mama yangu nifukara hata sasa. Matajiri katika nchi hii wanauwezo hata kufikia kumiliki magari ya nje, lakini mama yangu mzazi bado angali akiishi katika ufukara wa kupindukia”. Aliendelea kusema, “Ingawa si kumuuliza mama yangu mzazi juu ya swali hili na sikupata jibu toka kwake, japo nimeweza kung’amua sababu ya yeye kunitelekeza hata kurithiwa ili niweze kuokolewa na ufukara. Na hivyo sikuhisi hitaji la kumuuliza juu ya swali hilo, na hivyo wasiwasi wangu na chuki kwasasa vimetoweka moyoni mwangu.”
 

Watu hutengwa na Mungu kutokana na dhambi mioyoni mwao.

Kwanini tunatengwa na Mungu, na ni kwasababu gani hatuwezi kumjongelea kwa karibu? Yule mwanake aliye rithiwa alikuja kugundua yakwamba mama yake mzazi alimtelekeza hata kufikia kurithiwa ili aweze kumkomboa tokana na ufukara. Nini kingeliweza kututenganisha na Mungu? Jibu ni kwamba, shetani alipo mjaribu mwanadamu kutenda dhambi ndipo hapo dhambi hiyo ilipotutenga na Mungu.
Hapo mwanzo, Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake na kumpenda sana kiumbe huyo. Watu waliumbwa wakiwa ni uthibitisho wa pendo lake na hivyo kumiliki uweza mkubwa zaidi ya viumbe wangine. Hata hivyo malaika mpotofu aitwaye shetani aliadhimia kumtenga mwanadamu na Mungu. Shetani alimshawishi mwanadamu ili asiyaamini maneno ya Mungu na hivyo kumfanya ale tunda la ujuzi wa mema na mabaya.
Hivyo mwanadamu akatengwa na Mungu tokana na dhambi zake. Mwanadamu huyu hakumtii Mungu. Hakula tunda la mti wa uzima ambalo huleta uzima wa milele ambalo ndilo Mungu alilomruhusu, badala yake akala tunda lililokataliwa, ambalo lilimpa ujuzi wa mema na mabaya. Matokeo yake akatengwa na Mungu.
Mwanzoni nia ya upendo wa Mungu kwa mwanadamu ilikuwa ni njema. Aliacha utii na hivyo kutengwa naye kutokana na kiburi. Kutokana na dhambi hiyo kukaa ndani ya moyo, hatimaye mwanadamu alitengwa na Mungu. Baadaye mwanadamu alikaa mbali na Mungu kwa muda mrefu na kuanza kulalamika “kwanini Mungu ametutelekeza baada ya kutuumba? Kwa nini alituachia tutende dhambi? Kwa nini anatupeleka motoni hasa baada ya kutufanya dhaifu? Ingelikuwa ni bora zaidi kama angeliacha kabisa kutuumba hapo mwanzoni.” Nasi pia tunaishi tukiwa na maswali mengi ya aina hii pamoja na utafiti, mashaka na chuki kabla ya kuzaliwa upya mara ya pili.
Nilipo mwona yule mwanamke aliye rithiwa katika kile kipindi cha TV, niligundua ya kwamba, mahusiano kati ya mwanadamu na Mungu nayo ni yaaina hii pia, kati ya yule binti na mamaye. Hakuna dhiki kuu, vurugu, laana au dhambi ya aina yoyote itakayoweza kumtenganisha Mungu na mwanadamu katika mazingira ya aina yoyote. Pia niliweza kugundua pia ingawa uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu umewekwa kwa msingi wa upendo, ilikuwa bado si rahisi kutoelewana kutokea kama vile ilivyo kwa yule mama asingeliweza kumtelekeza bintiye kwa chuki. 
Hivyo ndivyo nasi Mungu pia hakuweza kututenga kwa sababu ya chuki binafsi bali kwa sababu ya dhambi. Hakuna hata sababu ya Mungu kumchukia mwanadamu na pia mwanadamu kumchukia Mungu. Sote tunapendana. Sababu ya mwanadamu kuendelea kutengwa na Mungu ni kutokana nakuwa ni mwenye dhambi na hasa baada ya kuanguka katika mtego wa shetani.
 

Mungu ametukumbatia kupitia Yesu

“Lakini sasa, katika Kristo Yesu ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga naye akiisha kuondoa ule uadui kwa mwili wake ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya moja ndani ya nafsi yake; akafanya amani” (Waefeso 2:13-15). Bwana alibatizwa na Yohana na kubeba dhambi zote za ulimwengu ili kuitimiza amri na sheria ya Mungu. Hapo ndipo alipo mwaga damu yake msalabani ili kuokoa wanadamu kwa dhambi zao na kuruhusu kuweza kukumbatiwa na Mungu. Kwa sasa Mungu anewakumbatia wale wote walio pokea utakaso wake.
Je umekwisha wahi kufikiri jinsi ile ulimwengu ungekuwa bila maji? Siku chache zilizo pita niliwahi kuhudhuria mkutano wa biblia katika mji wa Inchon, moja ya bandari kubwa katika Korea ambamo maji ya bomba yalikuwa yamekatika katika muda huo kwa muda wa siku chache na hivyo nikawaza kuwa, ama kwa hakika watu hawawezi kuishi pasipo maji.
Ikiwa Mungu angeliumba ulimwengu huu pasipo maji kwa mwezi tu, basi ingekuwa vigumu kuishi mijini kutokana na harufu mbaya, uchafu na kiu. Hapa yatupasa kuelewa thamani ya maji Mungu aliyotupatia kama ilivyo maji na umuhimu wake kwa wanadamu, yaani ubatizo wa Yesu aliupokea kwa Yohana pale Mto Yordani ambao hauwezi kuwekwa kando.
Kama Yesu asingelikuja duniani na kubatizwa na Yohana ni kwa namna gani basi wale wote wenye kumwamini Yesu wangeliweza kupokea msamaha wa dhambi? Vile jinsi watu wasivyo weza kuishi pasipo maji, kila mtu ulimwenguni angelikufa kwa dhambi kama Yohana asingelimbatiza Yesu.
Hata hivyo tokea ubatizo wa Yesu kubeba dhambi zetu tunaweza kujionea wenyewe uhakika katika kufahamu kwamba mioyo yetu imetakaswa na kuweza kubarikiwa kwa wokovu, ubatizo wa Yesu ni muhimu kwa imani yetu. Zaidi ya yote ubatizo wake hakika ni muhimu kwetu kuweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu.
Petro moja kati ya mitume wa Yesu alisema “mfano wa mambo haya ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili basi jibu la dhamira safi mbele za Mungu) kwa kufufuka kwake Yesu Kristo” (1 Petro 3:21). Kauli hii ya Petro inayosema kwamba ubatizo wa Yesu kwa Yohana mbatizaji na kumwaga damu yake ili kutuokoa sisi sote ulimwenguni ndiyo injili ya kweli.
Hebu sasa na tutazame kifungu cha biblia juu ya lile birika la shaba katika Kutoka 30:17-21 “Bwana akanena na Musa na kumwambia. Fanya na birika la shaba na tako lake la shaba ili kuogea, nawe utaliweka kati ya hema ya kukutania na madhabahu nawe utalitia maji. Na Haruni na wanawe wataosha mikono yao na miguu yao humo hapo waingiapo ndani ya boma ya kukutania; watajiosha majini ili wasife. Au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike kumteketezea Bwana sadaka ya moto, basi wataosha mikono yao na miguu yao ili kwamba wasife; na neno hili litakuwa amri kwao milele kwake yeye na kwa wazao wake katika vizazi vyao vyote”.
Ndani ya Hema palikuwepo na birika la shaba, ambalo lilikuwa limewekwa kati ya mahala pa kukutania na madhabahu ambalo ndani mwake lilijazwa maji ya kujikosha. Endapo maji haya yasingelikuwemo Hemani hapo, namnagani basi wale makuhani waliokuwa wakifanya shughuli za utoaji wa sadaka za wanyama wangekuwa wachafu kila mara na kwa wakati wote.
Kiasi gani cha madoa ya damu na uchafu ungeligandamana katika nguo za makuhani hao walio kuwa wakitoa sadaka za wanyama kila siku kwa niaba ya watu, huku wakiwekea mikono yao juu ya sadaka za dhambi na hatimaye kuwauwa kwa kuwa chinja shingo? Ikiwa pasingelikuwemo birika hiko la shaba lenye maji katika hema makuhani wangelichafuka sana.
Na hii ndiyo maana Mungu alitayarisha birika hili la shaba lenye kuwekewa maji ndani yake ili waweze kuja tena mbele ya Mungu wakiwa na mikono safi. Wenye dhambi hutwika dhambi zao kupitia kuwekea mikono juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi na ndipo makuhani humtoa kafara mnyama huyo kwa Mungu kwa niaba yao. Mungu alitayarisha birika la shaba ili makuhani waweze kuingia pahala patakatifu na hivyo basi wakiwa wamejisafisha kwa maji wasiweze kufa. Hata kuhani asingeliweza kuingia katika patakatifu akiwa na madoa ya uchafu na damu za wanyama mwilini. Na ndiyo maana makuhani walijisafisha na kujitakasa uchafu walionao kwa maji yaliyomo katika birika lile la shaba ili waweze tena kujongea mbele ya Bwana baada ya kutoa sadaka kwa niaba ya watu wao.
 

Ubatizo wa Yesu ulisafisha dhambi zote za ulimwengu.

Kupitia ubatizo wa Yesu kwa yohana pale Mto Yordani dhambi zote za ulimwengu zilihamishiwa juu yake. Na kwa kuzamishwa kwake katika maji kunaashiria juu ya kifo chake na kuibuka kwake toka katika maji kuna wakilisha ufufuko wake. Kwa maneno mengine, Yesu alibatizwa na Yohana ili aweze kubeba dhambi zote za ulimwenguni, kulipia gharama ya dhambi hizo kwa kufa juu ya msalaba. Kifo chake kilikuwa ni kulipa mshahara wa dhambi na ufufuko wake ndiyo utupao uzima wa milele.
Ikiwa hatukuamini ya kwamba Yesu alibeba dhambi zetu zote kwa njia ya ubatizo wake, mioyo yetu itaendelea kujawa na dhambi. Kwa jinsi hiyo basi, tungeliwezaje kujongea mbele ya Mungu? Injili ya ondoleo la dhambi si fundisho la mojawapo ya mafundisha ya madhehebu bali huu ndiyo ukweli halisi wa Mungu.
Hatuwezi kuiongoza imani yetu pasipo ufahamu sahihi, kwa maneno mengine, hatuwezi kuushinda ulimwengu ikiwa hatujali kuwa Yesu alibatizwa na Yohana. Kama jinsi ambavyo viumbe hai vinahitaji maji ili viweze kuishi, sisi nasi tunahitaji ondoleo la dhambi na maji ya ubatizo wa Yesu ili tuweze kuishi kwa imani na kisha kuuingia Ufalme wa Mbinguni. Ilibidi Yesu abatizwe, afe Msalabani, na kufufuka ili kutuokoa toka katika dhambi zetu. Hii ni injili ya maji na ya Roho ambayo ni sharti tuiamini kwa mioyo yetu yote. 
Pamoja na kuwa Yesu alisulibiwa hadi kifo pale Msalabani, hakuwa amefanya lolote baya lililomfanya astahili adhabu hiyo. Yesu alikuja hapa ulimwenguni ili kuziosha dhambi zetu, alibatizwa alipokuwa na umri wa miaka 30, na akawa Mwokozi wetu kupitia kifo chake katika Msalabala alipokuwa na umri wa miaka 33. Mungu alihitaji kuwafanya wanadamu kuwa watoto wake bila ya kujali jinsi tulivyokuwa wenye dhambi. Hii ndiyo maana Yesu alibatizwa. Mungu alitupatia ondoleo la dhambi na karama ya Roho Mtakatifu kwa wakati mmoja. 
“Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kwamwe kuuingia Ufalme wa Mungu” (Yohana 3:3-5). Unapaswa kufahamu na kuamini kuwa Yesu alibatizwa ili aweze kuziosha dhambi zetu zote. Hata kama mtu fulani ni Mkristo aliyezaliwa upya, kama hatafakari juu ya ukweli kuwa Yesu Kristo alizichukua dhambi zote za ulimwengu kupitia ubatizo wake, moyo wake utachafuka kwa haraka. Kwa sababu sisi ni viumbe wenye mwili, tunajikuta tukichafuliwa na dhambi katika maisha ya kila siku. Ndio maana tunatakiwa kuishi kwa imani kila wakati hali tukitafakari juu ya ubatizo wa Yesu, damu yake, na ufufuko wake. Imani hii inatutegemeza hadi siku ile tutakapoingia katika Ufalme wa Mungu. 
Yesu hakuwa na chaguo bali kubatizwa na kufa kwa ajili ya dhambi zetu, hivyo ni lazima tuamini kuwa kwa kufanya hivyo alituletea Wokovu. Hakuna tunachoweza kukifanya zaidi ya kuamini katika injili hii nzuri ili tuweze kukombolewa toka katika dhambi zote za ulimwengu. 
Tunamshukuru sana Bwana, aliyetupatia injili ya maji na ya Roho. Zawadi kuu ambayo Mungu alitupatia ilikuwa ni kumtuma Mwana wake pekee kutuokoa toka katika dhambi zetu zote kupitia ubatizo na damu yake. 
Sababu iliyotufanya tusiweze kumkaribia Mungu kiasi kwamba tukalazimika kuishi mbali na Mungu ni kuwa tulikuwa na dhambi katika mioyo yetu. Yesu alibatizwa na Yohana ili kuzichukua dhambi zote za ulimwengu na kufa juu ya Msalaba ili kuuvunja ukuta uliokuwa ukimtenganisha Mungu na mwanadamu. Uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu ulirudishwa kupitia ubatizo na damu ya Yesu. Tunamshukuru Mungu kwa karama hizi. Upendo wa wazazi wa kimwili kwa watoto wao ni mkubwa, lakini hauwezi kulinganishwa na upendo wa Mungu ambao kwa huo Yesu alituokoa sisi wenye dhambi. 
Ubatizo wa Yesu na damu, vyote ni muhimu. Ikiwa pasinge kuwepo na maji katika ulimwengu huu je viumbe wangeliweza kushi? Pasipo ubatizo wa Yesu pasingekuwepo na yeyote asiye na dhambi moyoni. Ikiwa Yesu asingelibatizwa na ikiwa asingeli kufa msalabani hakuna yeyote angeliweza kupokea ondoleo la dhambi. Kwa bahati Yesu alibatizwa na kuweka sadaka ya kiwango cha mwisho kwa ajili yetu. Ingawa tuna mapungufu ya udhaifu bado tunaweza kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuamini ubatizo na damu yake pale msalabani.
Watu wenye kuamini ubatizo wa Yesu Kristo na kifo chake msalabani wataweza kujongea mbele ya Mungu wakisali na kusifu. Tunaweza kumsifu Bwana na hata kumwabudu yeye kwasababu tumefanywa kuwa wana kwake. Hii ndiyo neema ya Mungu na baraka. Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake pale msalabani hakika ni ya ajabu. Sote tunaweza kupokea wokovu na uwepo wa Roho Mtakatifu kwa kuamini injili hii njema.