Search

Mahubiri

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-8] Kupitia nani maji ya uzima ya Roho Mtakatifu hutiririka? (Yohana 7:37-38)

(Yohana 7:37-38)
“Hata siku ya mwisho siku ile kubwa ya sikukuu Yesu akasimama akapaza sauti yake akisema, mtu akiona kiu na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi kama vile maandiko yalivyonena mito ya maji yaliyo hai itatiririka ndani yake.”
 

Ni nani takaye kunywa maji 
ya uzima ya Roho Mtakatifu?
Ni wale wote wanao amini injili njema 
ya ubatizo wa Yesu na damu 
yake msalabani.

Maji ya uzima ya Roho Mtakatifu hutiririka toka mioyo ya wale wote wanao amini injili njema. Yohana 7:38 inasema “Aniaminiye mimi kama vile maandiko yalivyonena mito ya maji yaliyo hai itatiririka ndani yake.” Maana yake ni kwamba upo wokovu wa kweli na ondoleo la dhambi kwa wale wote wenye kuamini injili njema ambayo Mungu ametupatia.
Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani hutokea wakati gani? Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani utaweza kupatikana pale ambapo mtu atakapo sikia na kuamini injili ya kweli ambayo inasema kwamba, Yesu Kristo alibeba dhambi zetu zote ulimwenguni kwa njia ya ubatizo wake kwa Yohana. Kwanjia hii yeyote ataweza kunywa maji ya uzima ya Roho Mtakatifu. Wale wote wanao amini injili njema ndiyo walio na uwepo wa Roho Mtakatifu. Ndani yao wataweza kushuhudia matokeo ya maji ya uzima wa kiroho yakitiririka na kulowesha mioyo yao iliyokuwa mikavu pale kila mara wanapo hubiri au wanapo sikia neno la Mungu.
Maji ya uzima ya Roho Mtakatifu humiminika nje toka katika mioyo ya wale wanaoamini injili ya maji na Roho ambayo inasema Bwana alikuja ulimwenguni ili kuokoa wale wote wenye dhambi. Roho Mtakatifu ni mkweli asiye tenganishwa na injili ya maji na Roho na hukaa ndani ya watu wanao amini maneno ya Mungu.
Yeyote anayetaka kunywa maji ya uzima ya Roho Mtakatifu lazima apate ondoleo la dhambi zake zote kwa kuamini injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Maji haya ya uzima ya Roho Mtakatifu huwepo ndani ya mioyo ya wale wote wenyekuamini maneno ya Mungu. Watu wanao amini injili ya maji na Roho ndio walio na maji ya uzima ya Roho Mtakatifu ambayo hufananishwa na mto ufuatao mkondo kupitia mioyo. Hata sasa maji ya uzima ya Roho Mtakatifu hububujika kama maji ya chemchemi ndani ya mioyo ya wale wote walio pokea ondoleo la dhambi kwa kuamini injili njema ya ubatizo wa Yesu Kristo na damu yake msalabani.
Hata hivyo hakuna hata tone moja la maji ya uzima ya Roho Mtakatifu yatiririkayo toka moyoni mwa wale wote wasio amini injili njema ya kweli. Hapo mwanzo sikuwa hata na tone la maji ya uzima yamiminikayo toka moyoni mwangu hadi pale nilipomini na kuikubali injili ya maji na Roho. Kwa wakati huo ingawa nilimwaminiYesu Kristo kwa dhati, hata hivyo sikujua umuhimu wa maji ya uzima ya Roho Mtakatifu, kwa sababu sikuwa na Roho Mtakatifu ndani ya moyo wangu. Hata hivyo leo hii ninayo injili njema ya maji na Roho, na hivyo maji ya uzima ya Roho Mtakatifu humiminika moja kwa moja toka moyoni mwangu.
Kwa sasa maji ya uzima ya Roho Mtakatifu humiminika toka moyoni mwangu nahata pia kwa wale wote wenye kusikia na kuamini neno la Mungu. Kama vile Yesu alivyo sema “Yeyote aonaye kiu na aje kwangu nitamnywesha”. Maji haya ya uzima ya Roho Mtakatifu huwaburudisha watu kupitia wakristo wale walio zaliwa upya mara ya pili kwa kuamini injili njema ya maji na Roho. Kwangu mimi hububujika toka moyoni pamoja na imani yangu katika injili ya maji na Roho hata katika muda huu yakiruhusu wengine kuyanywa. Mungu amefanya maji ya uzima ya Roho Mtakatifu kutiririka toka mioyoni kama mto. Jambo hili ni lakueleweka kwa wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao.
Kama ilivyo andikwa katika Ufunuo kwamba hakuna ajuaye usipokuwa wale wote waliompokea Roho Mtakatifu na maji ya uzima, ambavyo ni siri ijulikanayo kwa wale wote tu waliokwisha iamini injili njema ya maji wa Roho. Hivyo yakupasa ujue kwanini Roho Mtakatifu huweka makazi ndani yao. Yakupasa ujue kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu ndani hutokea kwa wale tu wanao amini injili ya Yesu.
 

Nilizoea kuamini damu ya msalabani tu.

Ingawa niliamini damu ya Yesu na msalaba wake kwa muda wa miaka kumi bado dhambi ziliendelea kuwepo moyoni mwangu. Katika muda huo nilikuwa naamini kwamba dhambi zangu zilisamehewa kwa njia ya damu ya Yesu. Hata hivyo sikuweza kupokea msamaha wa dhambi ulio kamili, na hata pia uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yangu kwa imani ya aina hii. Hivyo nilichanganyikiwa nakuwa mtupu moyoni katika maisha yangu. Dalili pekee iliyojitokeza katika imani yangu kwa Yesu ni kuendelea kuhudhuria kanisani.
Hapa ndipo nilipoanza kuiangalia upya imani yangu, “Je, ni kweli nimempokea Roho Mtakatifu?” Mwanzo nilipoanza kuaminii juu ya Yesu, moyo wangu ulikuwa ukitamani upendo wa Yesu na hata nilifikia hatua ya yakuwa na karama ya kunena kwa lugha. Lakini nini kilicho tokea ndani yangu? Niligundua matokeo haya ya hisia kali hayakuwa nidalili ya uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yangu, na hivyo sikuwa kabisa nimempokea Roho Mtakatifu huyo. Nilimwamini Yesu, lakini Roho Mtakatifu na maji yake ya uzima haya kuwamo moyoni mwangu.
Haikuwa na umuhimu endapo moyo wangu ulikuwa moto au baridi, kwa kuwa imani yangu ilihusika na mafundisho ya theologia za 4 Kikelvini (calvinsm). Hakika maswali niliyo hitajika kuyajibu yalikuwa ya fuatayo:-
1) Je, Roho Mtakatifu yumo ndani yangu? - Hapana, sina uhakika kama kweli yumo ndani yangu.
2) Je, kunadhambi ndani yangu? -Ndiyo, ipo- Bila shaka ipo dhambi ndani yangu, ingawa ninamwamini Yesu na damu yake msalabani. Bado ninadhambi moyoni ingawa ninamwaniniYesu na kusali sala ya toba kilasiku. Dhambi moyoni mwangu haikufutika ingawa nilijaribu.

4 Theologia za Kikelvini (Calvinism) ni mpangilio wa tafsiri za kikristo uliotiliwa msukumo na John Calvin. Ulitilia mkazo kujuliwa tangu asili na wokovu. Vipengele vitano vya Ukelvini (Calvinism) vilitokana na kupinga nafasi ya Waarminia (Arminian). 
Ukelvini (calvinsim) ulifundisha: - 1) Uharibifu mkuu: ambapo mwanadamu ameharibiwa na dhambi kwa sehemu yote ya maisha katika mwili, roho, akili na hisia. 2) Upendeleo usio stahiki: ambapo upendaleo wa Mungu kwa mwanadamu uko wazi kabisa kwa uchaguzi wake binafsi na haumtegemei mwanadamu huyo. Haustahiki kwa mwanadamu. 3) Ondoleo la dhambi lililo na mipaka: ambapo Kristo hakubeba dhambi za kila mtu aliyeduniani, bali badala yake alibeba za wale tu waliochaguliwa kupata wokovu. 4) Neema isiyo zuilika: ambapo wito wa Mungu katika wokovu kwa baadhi ya watu hauwezi kupingika. 5) Uvumilivu wa watakatifu: ambapo haiwezekani wokovu wa mtu kupotea. Katika yote haya utaweza kutambua kwa uwazi tofauti zilizopo dhidi ya injili ya maji na Roho hasa kuhusiana na fundisho la ondoleo la dhambi lililo na mipaka.
 
Nitawezaje kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yangu? Nitawezaje kutakaswa dhambi zangu moyoni? Haya yalikuwa ni maswali yangu mawili yaliyo leta matatizo yaliyo kuwa katika fikra zangu hata baada ya kumwamini Yesu. Nilikuwa nikinena kwa lugha baada ya kumwamini Yesu na pia niliamini kwamba dhambi zangu zilitakaswa baada ya kuisifu imani katika damu ya Yesu.
Hata hivyo kadiri muda ulipo zidi kwenda dhambi juu ya dhambi ziliendelea kurundikana moyoni mwangu. Nilikuwa ni mwenye dhambi. Sala za toba na kufunga kula hakukuweza kutakasa dhambi zangu moyoni pamoja na kwamba nilitegemea damu ya Yesu tu. Nilipatwa na hofu kwa muda mrefu juu ya dhambi za kila siku. Kila nilipozidi kuhofu ndipo nilipo zidi kuhubiri ujumbe wa Yesu kwa kushutumu mbele za watu. Pia nilikuwa nikihudhuria kanisani mara kwa mara na kujitolea nafsi yangu kumtumikia Yesu huku nikiitegemea damu ya Yesu.
Ingawa muda ulivyozidi kwenda dhambi zangu za kila siku ziliweka kizuizi moyoni kuweza kuwa na imani ya kweli. Ilikuwa ni vigumu kumwamini Yesu kuliko hapo mwanzo. Nilijaribu kuitegemea damu ya Yesu na kuweka mbele juhudi zangu na kuweka mbele zaidi kujitoa kwangu kwa Mungu. Hata hivyo hali ya utupu moyoni mwangu ilizidi kuwa kubwa. Imani ya aina hii ilinifanya ni hisi hali ya utupu na kunyong’onyea, hivyo kunifanya niwe mkristo mnafiki aliye jali zaidi kuonekana kwa nje. Nilijisemea “kumwamini Yesu kwa njia hii, ndivyo ilivyo hata kwa wengine na sikuwa pike yangu!” Sikuamini kuwa imani yangu ilikuwa ni potofu. Ingawa damu ya Yesu na sala za toba bado hazikuweza kutakasa dhambi zangu za kila siku.
Sasa basi, kwa imani gani dhambi zangu za kila siku zitaweza kutakaswa? Dhambi zangu za kila siku zitaweza kusafishwa kupitia imani yangu ya kwamba, dhambi zangu zote zilitwikwa juu yake Yesu pale alipo batizwa katika mto Yordani. Hivi ndivyo ilivyoandikwa katika Mathayo 3:13-17. Sasa basi, kwanini dhambi nilizokuwa nikitenda kila siku hazikuweza kutakaswa kwa damu ya Yesu? Sikua nimeifahamu na kuiamini injili ile njema iliyojumuisha maana ya ubatizo wa Yesu.
Je, hii inamaana kuwa dhambi zote za ulimwengu zilisafishwa kwa njia ya ubatizo wa Yesu? Ndivyo ilivyo. Biblia imeshuhudia hilo kwa kusema, “mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia Ufalme wa Mungu” (Yohana 3:3-5). Yesu alikuja hapa ulimwenguni na kukubali kubeba dhambi za ulimwengu kwa njia ya ubatizo wake kwa Yohana.
Bado nilikuwa na wasiwasi juu ya hili nahivyo kuchukua hatua ya kuoanisha Agano la Kale na lile Jipya ili kubainisha jambo hili. Matokeo yake nilipata jibu kuwa nilikuwa sahihi. Dhambi zote za ulimwengu zilitwikwa juu ya Yesu pale alipobatizwa. Hivyo hata dhambi zangu zote nazo pia zilitwikwa kwake katika muda huo. Nita takaswa kwa kupitia imani ya maneno haya. Nikagundua kwamba hilo ndilo neno la kweli kama ilivyo andikwa katika Biblia, na ndiyo injili halisi kwa dunia hii.
Kwa kuongezea niligundua pia kwanini dhambi zangu hazikuweza kufutika kupitia imani katika damu ya Yesu peke yake. Sababu ilikuwa kwamba, sikuwa nimemtwika Yesu dhambi zangu za kila siku pale ambapo sikuwa najua ukweli unaohusu ubatizo wake katika mto Yordani. Mwisho wake nilipata ukweli na kujifunza kwamba Yesu alikuja katika ulimwengu huu kwa ajili yangu, na hivyo alibeba dhambi zote za dunia kwa ubatizo wake, na ndipo baadaye alisulubiwa ili kutukomboa kwa dhambi zetu zote ulimwenguni. Pia nilijifunza na kuamini ukweli kwamba sababu ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ilikuwa ni kuondoa dhambi zote ulimwenguni. Leo hii mimi ni mwenye haki nikishukru kwa imani yangu ya injili njema ya Yesu aliyo tupatia na kwakuwa dhambi zangu zote zimesamehewa.
Hili halikuwa ni fundisho la kanisa ambalo lilifuta dhambi zangu, bali ni ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ndiyo iliyofanya yote haya. Ukweli huu ulikuwa katika injili njema. Niliokolewa na dhambi zangu zote na kuwa mwenye haki si kwa njia ya imani katika damu ya Yesu pekee, bali kwa njia ya imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani, ambavyo ndiyo wokovu wangu.
Jambo moja jingine ninalohitaji kumshukuru ni hili la Roho wa Mungu kuja juu yangu baada tu ya kuanza kuamini injili njema. Hii leo Roho Mtakatifu ameweka makazi ndani yangu, yu pamoja nami akiwa na maneno ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani.
Namshukuru Bwana aliye nipatia injili njema na aliyeniruhusu kuhubiri imani hii waliyo kuwa nayo mitume wa Yesu. Mungu amenipa kipawa cha Roho Mtakatifu ambapo kitu pekee nilichoweza kufanya ni kuamini injili njema. Leo hii nimepata fursa ya kuleta ujumbe kwa heshima kubwa na ushahidi kwa watu wote ulimwenguni. Hakika ninachoweza kuwaambia ni kwamba, kuamini damu ya Yesu pekee hakutoweza kufuta dhambi zenu zote kamwe!
Ila ninacho waeleza ni kwamba dhamba, zenu zote hakika zitatakaswa ikiwa tu watu wataamini injili njema ambayo inaongelea juu ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana na na damu yake msalabani. Sina aibu hata kidogo mbele ya Mungu ninapo hubiri injili hii njema ya kuzaliwa upya kwa maji na kwa Roho kwa watu wote ulimwenguni. Namshukuru Bwana. Namshukuru yeye kwa kuniruhusu kunywa maji ya uzima ya Roho Mtakatifu kwa kupitia injili ya maji na Roho.
 

Njia ya Majaribio ambayo huonyesha injili ya kweli ndiyo iliyo ya maji na Roho.

Je, umekwisha pokea kweli ondoleo la dhambi na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako? Utawezaje kugundua injili iliyo yakweli? Hapo awali nilifanya uchunguzi kwa watu walio taka kuamini injili njema aliyotupatia Yesu. Mmoja wapo nilimhubiria ujumbe wa damu ya Yesu msalabani. Pia nilimwambia kuwa hatokuwa na dhambi kwa kumwamini Yesu. Yule mwingine nilimhubiria injili njema ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani. Matokeo yake ni kwamba yule aliye pokea ondoleo la dhambi kwa kuamini damu ya Yesu, alisema kwamba ilimbidi kundelea kutubu kila mara kwa dhambi zake za kila siku. Lakini yule mwingine aliye amini injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake, kwa upande mwingine alisema kwamba kwa sasa amekuwa mtu kamili asiye na dhambi.
Alisema kwamba hana tena dhambi moyoni mwake kwasababu ameamini ukweli ambao Yesu alizichukua dhambi zake zote na kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi hizo. Na hivyo aliweza kumpokea Roho Mtakatifu toka kwa Mungu kwa sababu aliamini injili njema ambayo inasema, ubatizo wa Yesu kwa Yohana ulisafisha dhambi zote ulimwenguni. 
Kwa ndugu huyu kusema kwamba hakuna tena dhambi moyoni, ilikuwa ni kwasababu amepokea Roho Mtakatifu moyoni mwake kwa kupitia imani yake katika injili njema. Roho Mtakatifu alimpa ushuhuda wa wakusema hana tena dhambi moyoni. Mungu hutoa kipawa cha Roho Mtakatifu ndani ya moyo kwa wale wote wanao amini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Roho Mtakatifu huweka makazi kwa watu gani? Roho Mtakatifu hutolewa kama kipawa au zawadi kwa wale wote wanaoiamini injili njema ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana, na damu yake msalabani. 
Kwa kuangalia lile tendo la ajabu katika siku ile ya pentekoste, kumesababisha watu wengi kutoelewa ukweli juu ya namna ya kumpokea Roho Mtakatifu huku wakiweka kando injili njema. Watu hudhani kwamba, ikiwa wataomba kwa dhati na kumtafuta Roho Mtakatifu ndivyo watakavyoweza kumpokea na kuweka makazi ndani yao. Takribani muda mrefu wakristo ulimwenguni hawakuwahi kuwa na wazo ambalo linasema kwamba, mtu ataweza kumpokea Roho Mtakatifu ikiwa tu ataamini injili njema ya ubatizo na damu ya Yesu Kristo. Hata hivyo leo hii watumishi wengi wa Mungu waliopokea kipawa cha Roho Mtakatifu ndani yao kwa njia ya imani katika injili ya maji na Roho ndiyo wanao ihubiri injili kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Matokeo yake ulimwenguni pote wamejifunza injili hiyo na hivyo kupokea Roho Mtakatifu.
Mungu amewezesha watu wale wanao amini injili njema kuweza kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu. Katika biblia inasema “itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto” (Matendo 2:17). Hata hivyo mtu imempasa aelewe kwamba kujaribu kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu pasipo kujua na kuiamini injili njema ni kosa. Hakuna njia nyingine ya kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu zaidi ya kuamini ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake msalabani.
Kwa kuwa Mungu anasema kwamba mtu ataweza kuingia ufalme wa mbinguni ikiwa tu atazaliwa upya mara ya pili kwa maji na Roho, napia niwale tu waliozaliwa upya ndiyo watakao weza kuhodhi karama ya Roho Mtakatifu. Hakuna shaka kwamba kila mtu anahitaji uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake ili aweze kuingia Ufalme wa Mbinguni. Utaweza vipi kumpokea Roho Mtakatifu au kuingia katika Ufalme wa Mbinguni ikiwa hautoamini injili njema ya Maji na Roho? Hakuna njia ya kwenda mbinguni bila ya kuiamini injili njema. Utaweza kumpokea Roho Mtakatifu ikiwa tu utaamini injili njema ya ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani. Kama vile tunapolipa fedha tunaponunua bidhaa, ndivyo hivyo pia tunavyo weza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu pale tu tunapoamini injili njema.
Nataka kukuambia kwamba ikiwa kweli utahitaji kumpokea Roho Mtakatifu ndani yako ni lazima kwanza uijue na kuiamini injili njema ya maji na Roho na hivyo kuwa na uwepo wake ndani yako.
Naamini injili njema na kadiri muda unavyosogea nahisi kuimarika zaidi na kwamba injili hii njema ambayo Mungu ametupatia ndiyo njema zaidi na yathamani kupita chochote ulimwenguni. Ningependa tushukuru kwakuwa sisi tuliokwisha kupokea Roho Mtakatifu ndani yetu ndiyo tuliobarikiwa zaidi.
Nawapa ujumbe wa namna ya kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yenu kwa njia ya kuamini injili njema. Watu wataweza kuhitimu wenyewe katika kuupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao, ikiwa tu watakubali baraka itakayo tokana na injili njema na kuzaliwa upya kwa mara ya pili katika maji na Roho. 
Katika Yohana 7:38 Yesu anasema, “Aniaminiye mimi kama vile maandiko yalivyonena mito ya maji iliyo hai itatoka ndani yake”. Maana yake ni kwamba, wale wote waliopokea ondoleo la dhambi kwa kuamini injili njema ya Yesu Kristo ndiyo walio na uwepo wa Roho Mtakatifu. Ndani yao. Maji yaliyo hai ya Roho Mtakatifu yata miminika kama mto toka mioyoni mwao. Wale wote wanao amini injili njema watashuhudia kumiminika kwa maji haya ya kiroho toka ndani yao.
Ingawa mwanzoni nilijitolea katika kumwamini Yesu kabla sijazaliwa upya kupitia injili ya maji na Roho, bado sikuona maji yaliyo hai yakitiririka moyoni mwangu. Lakini baada ya kuamini injili njema ndipo maji haya yalipo anza kutiririka moja kwa moja toka moyoni mwangu kama ilivyo andikwa katika Biblia. Hata hivi sasa yanatiririka pamoja na injili ya maji na Roho ambayo Mungu ametupatia. Maji haya hutiririka wakati wote. Uinjilisti wangu ulianza pale punde nilipo pokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yangu.
 

Ushuhuda wangu baada ya kuamini injili njema na kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yangu.

Ilikuwa punde tu baada ya mwisho wa majira ya kipupwe katika umri wangu wa miaka ishirini ya mwanzo. Kipupwe hicho hicho hasa ndicho kilichonifanya kuwaza uwezekano wa kifo changu. Maisha yangu katika mwaka huo yaliandamwa na kupagawa; utupu ndani ya moyo na giza kutokana na dhambi ndani ya moyo wangu. Nilielekea pahala pabaya pasipo kuelewa ni njia gani hasa ya kurudia. Mwili wangu ulikumbwa na maradhi pamoja na utupu moyoni uliendelea kukua.
Kwasababu ya dhambi zangu nilikuwa katika hali ya kukata tamaa na sikuwa na uhakika wa chanzo chake. Sikuwa na uchaguzi bali nikusubiri hukumu ya Mungu katika kiama kitakacho kuja ghafla maishani mwangu. Nilianza kuomba toba kwaajili ya dhambi zangu. “Oh Bwana nahitaji kupata ondoleo la dhambi zangu kupitia imani yangu kwako kabla ya kufa. Pia nakusihi niponye maradhi yaliyo mwilini mwangu!” Niliomba na kuomba.
Ndipo hapo tumaini jipya lilianza kumiminika toka kina cha moyo wangu ulio kata tamaa. Moyo wangu ulijawa na hamu ya Mungu na uliungua kwa joto kali. Hii haikuwa ni kwa kukata tamaa bali ni tumaini jipya ndilo lililo kuwa likiniunguza kwa joto hilo kama kaa la moto moyoni. Tokea siku hiyo nilianza maisha mapya ya kidini kwa kumwamini Yesu kwamba alikufa msalabani kwaajili ya kuniokoa mimi kwa dhambi zangu.
Haikupita muda baadaye nikapatwa na hali ya kunena kwa lugha. Baadaye niliendelea na hali ya kutokwa na machozi kila nilipoifikiria damu ya Yesu aliyo itoa pale msalabani kwaajili yangu. Nilijawa na shukrani kwakuwa ilikuwa ni kwaajili yangu.
Baada ya tukio hili niliyaacha maisha yangu ya awali na kupata kazi mpya ambayo iliniwezesha kuikumbuka siku takatifu ya Jumapili. Katika kipindi hicho moyo wangu ulijawa na upendo kwa Yesu na kujawa na shukrani zisizo na mwisho kila nikifikiria vile Yesu alivyo mwaga damu yake msalabani katika kuniokoa. Maisha haya ya kidini yalianza kukua ndani yangu huku yakiwa katika msingi wa neno la damu ya Yesu msalabani.
Hata hivyo kadiri muda ulivyo zidi kwenda maisha haya ya kidini yalianza kukumbwa na matatizo kutokana na udhaifu na dhambi za kila siku. Dhambi zangu za kila siku hazikuweza kutakaswa moja kwa moja kwa sababu imani yangu ilikuwa ni katika damu ya Yesu msalabani pekee. Nilijaribu mara kwa mara kujitakasa kila siku kwa kutubu. Hata hivyo sala nilizokuwa nikiomba huku nikitegemea kupata msamaha wa Mungu hazikuweza kabisa kunitakasa. Yote yalikuwa ni kwasababu sikuweza kuifuata sheria ya Mungu. Sasa basi dhambi hizo za kila siku zilianza kurundikana.
Ingawa sikuweza kujitakasa kwa sala hizo, bado niliendelea kufanya sala za toba. Niliamini kwamba kila wakati nilipotenda dhambi nilikuwa nafursa ya kujitakasa kwa dhambi hizo kwa njia ya kuomba toba na kuvuta hisia kwa kile damu ya Yesu ilicho fanya pale msalabani. Kadiri nilivyo rudia rudia tendo hili kila siku ndivyo dhambi zangu zilivyo zidi kurundikana tokana na udhaifu wangu. Mateso yalizidi kutokana na dhambi hizi.
Nilielekea katika Ukristo wa “kifarisayo”, na hata kufikia kuteuliwa kuwa shemasi na baadaye kuwa mwinjilisti ingawa nilikuwa na mzigo wa dhambi moyoni. Nilikwenda huku na huko nikihubiri injili kila nilipo hisi maumivu ya dhambi zangu za kila siku moyoni huku nikidhani kwamba hii ndiyo iliyo kuwa njia pekee ya kujitakasa. Dhambi zangu za kila siku ambazo ni halisi hazikuweza kutakaswa kwa njia ya imani hii ambayo msingi wake ni fundisho la kutoa nafsi.
Wakati fulani niliwahi kuingia katika mtego wa shetani. Nilihisi kuhukumiwa kutokana na dhambi zangu halisi na hata kudhani kuwa nilistahili kufa kwa uovu wangu. “Umetenda dhambi, kweli?” Hivi ndivyo shetani alivyo endelea kunihukumu na kunitesa kwa dhambi zangu.
Imani yangu ilikuwa njia panda kuporomoka. Niligundua kwamba nisingeliweza kamwe kutakasa dhambi zangu halisi kupitia njia ya imani ya damu ya Yesu na sala za toba pekee na matokeo yake nilipatwa na mfadhaiko wa kiakili.
Kwa kujifunza theologia za Ukelvini katika seminari, nikawa na hamu ya kujifunza sababu ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana. Niliwauliza maprofesa wengi juu ya sababu ya kubatizwa kwa Yesu na Yohana katika mto Yordani. Lakini majibu yao yalikuwa ni yakunikatisha tamaa na kufedhehesha, pengine huku wakisema alibatizwa ili kuonyesha mfano au kujitangaza kuwa yeye ni mwana wa Mungu. Hata hivyo majibu haya na mengine hayakunitosheleza kiu yangu ya kutafiti. 
 

Ukweli wa ubatizo wa Yesu kwa Yohana kulisababisha niigundue injili njema

Baada ya kipindi changu katika seminari, dhambi zangu zilikuwa bado hazija safishwa, na niliteseka kwa uzito wake kuliko wakati wote. Ndipo siku moja nikaja kuelewa sababu ya Yesu kubatizwa na nikwasababu gani alisema haki yote itakamilishwa kwa tendo hilo. Hii ilikuwa ni injili njema kwangu kuwa dhambi zote zilitwikwa kwake kwa njia ya ubatizo pale mto Yordani. Mungu aliniwezesha kugundua hili kwa njia ya maneno yake.
Baada ya kusoma zaidi maneno ya Mungu, ambamo imo injili njema iliandikwa, mwishowe niligundua ukweli juu ya dhambi zetu zilivyo twikwa juu yake Yesu kwa njia ya ubatizo ule wa Yohana na kuhukumiwa kwake msalabani.
Hapa ndipo nilipo gundua pia kwamba uwepo wa Roho Mtakatifu hakika umenijia. Dhambi zote moyoni mwangu zilisamehewa moja kwa moja baada ya kuigundua na kuiamini injili hii. Zile dhambi zilizokuwa ziki nichanganya na kunikatisha tamaa hakika zote zilisafishwa kwa nguvu ya injili hii njema. Dhambi zile zilizokuwa bado hazija ondolewa ingawa nilijitolea nafsi yangu na kufanya sala za toba nazo zote zilitoweka mara moja. Nampa Bwana shukrani zangu za dhati.
Nasema kweli ninapo shuhudia kuwa dhambi zote za ulimwenguni zisinge weza kutakaswa kwa damu ya Yesu msalabani pekee. Ubatizo wa Yesu kwa Yohana nao pi ulipelekea ondoleo la dhambi. Sasa kila mtu anapaswa kuelewa na kuamini kwamba dhambi zake zote zilitakaswa kwa msaada wa injili njema ya maji na Roho. Ninauwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya kina cha moyo wangu kwasababu niliamini injili hii njema, na neno la Mungu ndilo linishuhudialo juu ya Mwana wa Mungu. Ushuhuda huu ulitosha kabisa kuondoa dhambi zote moyoni mwangu. Nilimpokea Roha Mtakatifu kama hua kutokana na imani yangu katika injili jnema.
Tokea siku hiyo, Roho Mtakatifu amekuwa akifanya kazi ndani ya moyo wangu akiniwezesha kutenda kazi za kiroho, kwa maneno mengine, kuihubiri injili njema. Sasa hakuna tena dhambi moyoni mwangu Ubatizo wa Yesu kwa Yohana na damu yake pale msalabani vyote vinabeba ushahidi wa msamaha wa dhambi zangu na kupelekea uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yangu. Haleluya! Namsifu Bwana. Roho Mtakatifu kwa upole alijaa ndani yangu kama hua na kuweka makazi toka siku ile nilipo amini injili ya maji na Roho. Alianza kufanya kazi ndani ya moyo wakati mwingine kama hua, hata wakati mwingine kama mlipuko wa moto mkali.
Sasa nawe utaweza kupoke uwepo wa Roho Mtakatifu ikiwa tu utaamini injili hii njema ya maji na Roho. Je, hutaki kumpokea Roho Mtakatifu na kumsifu Mungu kwa kuiamini injili ya maji na Roho pamoja nami? Je, hutaki kushirikiana nami katika kuihubiri injili ya maji na Roho ulimwenguni pote? Injili njema ya maji na Roho itakutosheleza na kukupa uwepo wa Roho Mtakatifu. Haki ya Mungu imefunuliwa katika injili toka imani hadi imani. Na hii ndiyo maana uwepo wa Roho Mtakatifu upo kwa njia ya imani katika injili njema ya maji na Roho.
 

Mambo mema Roho Mtakatifu aliyo nifanyia.

Baada ya kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu, nilianza kufanya kazi katika kanisa jipya nikiihubiri njili njema. Roho Mtakatifu aliniwezesha kwa nguvu kuihubiri injili hii njema.
Na ndipo muda huo likatokea jambo lifuatalo. Katika mjini nilio kuwa nikiishi, palikuwepo na fundi wa kushona nguo aliye kuwa akifanya biashara na watu toka nje ya nchi. Bwana huyu alikuwa ni shemasi wa kanisa. Siku moja alisimamishwa karibu na hoteli moja jirani kwaajili ya biashara na ndipo alipo ona tangazo letu lililokuwepo karibu na hapo. Alivutiwa kwa mwaliko, na hivyo akajaribu kuwasiliana nami. Alikutana na mimi na kusema kuwa alikuwa akiishi na dhambi kwa muda mrefu. Baada ya takribani muda wa saa tano ya ushauri juu ya injili ya maji na Roho naye, hatimaye akagundua ukweli wa ondoleo la dhambi. Hatimaye akazaliwa upya na pia kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu katika muda huo.
Ipo habari nyingine tena iliyo tokea nilipo kwenda kutafuta jengo la kanisa. Nilipata jengo zuri na lakupendeza sana. Lakini katika muda huo sikuwa na fedha ya kutosha kukodi jengo hilo kutokana na ufinyu wa bajeti niliyo ipanga hapo awali. Hata hivyo Roho Mtakatifu alinieleza ndani yangu akisema, “Uwe imara na mwenye kujiamini”. Kwa mshangao niliweza kupata jengo hilo na hivyo kuweza kufanya kazi ya Mungu kwa masaa wa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu aliniwezesha kuihubiri injili ya maji na Roho tokea hapo. Roho huyu ndiye aliyepo ndani yangu hata hivi sasa akinipa uwezo katika kuihubiri injili njema kwa wote. Na nina shuhudia wale wote wenye kuisikiliza na kuiamini injili hii nao watapokea uwepo wa Roho Mtakatifu.
Namshukuru Roho Mtakatifu aliye nipatia uwezo wa kuihubiri injili njema. Najua kuwa hata maishani mwangu pote haitoshi kuandika juu ya yote aliyo yafanya Roho Mtakatifu juu yangu. Roho Mtakatifu ndiye aniwezeshaye kuishi huku maji ya uzima yakimiminika bila kikwazo toka moyoni mwangu. Nampa shukrani huyu Roha akaaye ndani yangu.
 

Roho Mtakatifu alipandikiza kanisa lenye kuendana naye kwa njia ya injili ya maji na Roho

Siku moja nilitoka kwenda nyikani kuihubiri injili njema. Katika muda huo, Mungu aliniongoza katika mji mmoja mdoga na nilikutana na kikundi kidogo cha watu walio kuwa wakimtafuta Mungu. Mungu aliniongoza niwahubirie habari ya injili njema, ambayo hatimaye iliwawezesha kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa kuisikia na kuamini kwao. Hatimaye Roho Mtakatifu aliwaongoza ili wawe watenda kazi nami huku tukishirikiana, na hivyo kusababisha niweze kuihubiri injili hii njema ulimwenguni pote toka wakati huo hadi hivi leo.
Mwanzoni walikuwa ni kundi dogo la watu, wasiomilikiwa na dhehebu lolote la kidini. Walipenda kuishi kwa kuyafuata maneno ya Mungu, lakini bila mafanikio wali omboleza huku wakiomba toba kwa dhambi zao kwasababu walikuwa ni watumwa wa dhambi hizo. Roho Mtakatifu aliniongoza katika kundi hilo la watu katika kuihubiri injili njema. Niliona vile Roho Mtakatifu alivyo weza kututayarisha sisi sote ili kuweza kukutana kwa pamoja. Mungu aliniongoza kuihubiri injili njema kwa kuanzia na somo la mpangilio wa utoaji wa sadaka kama ulivyo andikwa katika kitabu cha Walawi, hivyo waliweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa maneno ya injili njema.
Mungu aliwezesha kuwepo kwa kanisa la Roho Mtakatifu tukiwa pamoja nao wale walio iamini injili njema. Mungu aliwateua kuwa wafuasi wa Yesu kwa njia ya injili njema. Kwasasa kondoo wengi wameweza kumpokea Roho Mtakatifu na kujumuishwa katika kanisa hilo.
Shetani amekuwa akiwalaghai watu toka muda mrefu na ataendelea kufanya hivyo. Yeye huwaambia watu kwamba wataweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia ya sala za toba, kufunga na kuwekewa mikono. Hakika hili si kweli kabisa. Watu hawato weza kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia hii. Njia pekee kwao ni pale watakapo samehewa dhambi zao zote kwa kuiamini injili njema ya maji na Roho, ambayo Mungu alitupatia. Na hii ndiyo maana kamili ya kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu amekuwa akiwaongeza mara kwa mara wafuasi wa Yesu Kristo katika kuihubiri injili njema ili nao wengine waweze kumpokea Roha Mtakatifu.
 

Roho Mtakatifu ametuwezesha kufanya huduma ya uandishi wa vitabu ulimwenguni pote. 

Kwajinsi ile Mtume Paulo alivyo weka kumbukumbu ya injili njema katika nyaraka zake, Roho Mtakatifu aliye ndani ya moyo amekua ni kichocheo kwangu katika kuihubiri na kuieneza injili ya maji na Roho kwa kupitia vitabu. Hii ndiyo sababu ya kuihibiri injili kwa kupitia vitabu vyenye injili njema, ambavyo vinawaongoza wenye kuamini kuweza kumpokea Roho Mtakatifu. Mwanzoni tulianza na vipeperushi vyenye kurasa chache, lakini baadaye punde vitabu vilivyo na injili njema vilianza kutapakaa duniani kote.
Roho Mtakatifu aliye ndani yangu husababisha watu wengi kuweza kujiunga na kanisa baada ya kupaokea msamaha wa dhambi baada ya kusoma vitabu hivyo na kuamini injili njema. Zaidi ya hapo, hutuongoza katika kuihubiri injili hii katika lugha mbali mabali. Hutuongoza kuihubiri injili hii kwa takribani katika nchi zipatazo 150 duniani kote ikiwa pamoja na Marekani.
Roho Mtakatifu ameliwezesha kanisa kuomba kwaajili ya huduma ya umisionari kwa dunia na kutuwezesha kutafsiri injili njema katika lugha mbalimabali na kutuongoza katika huduma ya vitabu ili mataifa yote yaweze kuisikia na kuiamini injili hii. Roho Mtakatifu ameniongoza katika kufanya kazi na wafuasi wapya toka mataifa mengine na kuihubiri pamoja nao injili hii. Nampa shukrani Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu amenijaza hamasa katika kuihubiri injili hii kule Urusi. Alituongoza katika sala na kutupatia nafasi ya kukutana na wainjilisti wa Kirusi na kuihubiri kwao. Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwao kuisikia injili hii njema. Nao pia waliweza kumpokea Roho Mtakatifu kama sisi, baada ya kuisikia na kuiamini injili njema ya maji na Roho.
Mmoja wao, aliyekuwa ni mwalimu wa chuo kikuu cha Moscow, alitoa ushuhuda ufutao baada ya kusikia injili ya maji na Roho.
“Nilikuwa nikimwamini Mungu kwa takribani miaka 6, lakini nilimwamini pasipo kumwelewa. Hata hivyo, baada ya kusikia juu ya injili njema ya maji na Roho ambayo Mungu alitupatia, nikawa na imani madhubuti na faraja ilinijia moyoni. Hakika namshukuru Mungu. Niliwaza sana hadi pale nilipo weza kuishi maisha yaliyo na imani sahihi katika dini. Maisha yangu hapo awali yalikuwa katika msingi wa imani ya damu ya Yesu aliye kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Ingawa sikuwa na ufahamu kuhusiana na Mungu kutakasa dhambi zangu zote.
Ndipo nilipokutana na wachungaji na kuweza kuisikia injili njema mbayo Mungu alitupatia, na kugundua kuwa bado nilikuwa ni mwenye dhambi. Nilijaribu kutafiti juu ya injili hii na pia nini maana ya kuwa mwenye haki. Niligundua kwamba dhambi zangu zilitwikwa juu ya Yesu pale alipo batizwa. Hii ilikuwa ni injili njema. Niligundua pia kuwa si dhambi ya asili tu, bali hata zile za kila siku na zijazo nazo zili hamishwa kwake kwa njia ya ubatizo wake. Nilipata furaha kuu zaidi kwa kuzaliwa upya mara ya pili baada ya kuisikia na kuiamini injili hii ya kweli”.
Warusi wengi, pamoja na profesa huyu, walimpokea Roho Mtakatifu kwa kuisikia na kuiamini injili njema ya maji na Roho. Kwasasa kanisa la Roho Mtakatifu limepandwa mahala hapo, watu wengi kwa makundi wamekuwa wakiamini injili njema kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Ni Mungu diye aliye fanya yote haya, na nampa shukrani za pekee Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu aliye ndani yangu aliweza kunifanya niwe mkristo aliye zaliwa upya leo hii, kama vile wale wote wanao iamini injili njema ya maji na Roho, na kwasasa naihubiri injili hii ulimwenguni pote. Anawezesha vitabu vyetu vya injili njema kuweza kutafsiriwa kila mara si kwa kiingereza tu, bali hata kwa lugha nyingi mbali mbali ulimwenguni pote. Ametuwezesha kuihubiri ulimwenguni pote. Namshukuru Roho huyu. Nawe pia utaweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Mungu anapenda uwe na uwepo wa Roho Mtakatifu.
Watu wengi hujaribu kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuliita jina lake na kusali sala zisizo na kikomo mbele ya Mungu. Hata hivyo, kujaribu kumpokea Roho Mtakatifu pasipo injili njema ya maji na Roho, ambayo Yesu alitupatia, nimakosa makubwa. Kwakusema kwamba mtu ataweza kumpokea Roho Mtakatifu pasipo injili njema ya Yesu ya maji na Roho ni fundisho la uongo.
Je, wafuasi wa Yesu walimpokea Roho Mtakatifu pasipo kuamini injili njema ya Yesu waliyo pewa? Hapana, hakika sivyo. Yakupasa uelewe kwamba nyakati hizi Roho Mtakatifu huweka makazi ndani ya wale tu wano iamini injili ya maji na Roho, na maji ya uzima ya Roho Mtakatifu hububujika toka katika mioyo yao. Hata sasa, maji ya uzima ya Roho Mtakatifu hububujika toka katika mioyo pamoja na injili njema. Haleluya, namshukuru Bwana.