Search

Mahubiri

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-7] Injili iliyo njema inayowezesha Roho Mtakatifu kukaa ndani ya wanao amini (Isaya 9:6-7)

(Isaya 9:6-7)
“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa. Tumepewa mtoto mwanamume. Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake. Naye ataitwa jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani hayata kuwa na mwisho kamwe; kuuthibitisha na kuutengeneza kwa hukumu na kwahaki tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshu ndio utakaotenda hayo.”
 

Nini kinachowezesha 
Roho Mtakatifu kufanya makazi 
ndani ya wenye kumaini?
Injili njema ya maji na Roho.

Ili kumpokea Roho Mtakatifu tunahitajika kuwa na imani katika injili ya maji na Roho. Bwana wetu ameitwa wa Ajabu, Mshauri na Mungu mwenye Enzi. Bwana wetu amejitambulisha ndiye njia ya kwenda Mbinguni. Yesu Kristo amempatia kila mmoja zawadi ya Inijili njema. 
Hata hivyo katika ulimwengu huu wapo wengi ambao bado wanaishi gizani. Wanajaribu kutoroka katika kiza lakini kwa kuwa hawaijuia injili njema kamwe hawatoweza kukwepa dhambi zao. Badala yake wanatanga tanga na imani za mafundisho yao potofu. Kwa upande mwingine wale wanaotafuta ukweli ndiyo watakaokutana na injili njema hiyo na kuishi maisha yote wakiwa katika baraka ya Mungu iliyojaa. Naamini kwamba hii ni njia ya Mungu iliyo yapekee yenye kuwezesha mimi kuwasaidia watu kupokea injili njema na kutakaswa dhambi zao.
Hivyo basi uhuru toka dhambini usingewezekana endapo pasingekuwepo na njia hii ya Mungu. Ikiwa tumekwisha kutana na Bwana na kumpokea roho Mtakatifu, basi tumebarikiwa sana. Chakushangaza ni kwamba watu wengi hawafahamu kuwa baraka ya Mungu huja kutokana na imani katika injili njema. 
Baraka ya Mungu ni matokeo ya kuamini injili njema ambayo imeletwa kwetu na Yesu Kristo mwana wa pekee wa Mungu. Yesu ndiye pekee anaye tuokoa tokana na dhambi za dunia na hivyo kutubariki kwa rehema yake. Hakuna mwingine awezaye kutuokoa tokana na dhambi zetu au hata kutusaida kufuta hukumu iliyo ndani ya mioyo yetu. Ama kwa hakika ni nani ambaye angeweza kujiokoa binafsi tokana na dhambi zake na mateso ya kifo cha milele?
Mungu anatuambia “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu. Lakini mwisho wake ni njia za mauti” (Methali 16:25). Watu wameanzisha dini zao na kuziendesha kuelekea uharibifu na kifo. Wengi wa washika dini hujigamba kwamba wanatilia mkazo uadilifu na maisha ya haki, hivyo kuwaelekeza watu njia hizi zao katika kuwaokoa tokana na dhambi zao lakini, hata hivyo injili ya maji na Roho ndiyo pekee inayo weza kuokoa watu kwa dhambi zao zote. Ni Yesu pekee ndiye aliye mwokozi ambaye ataweza kuokoa wenye dhambi.
Katika Yohana 14:6 Bwana wetu alisema “Mimi ndimi njia na kweli, na uzima”. Ametoa mwili wake na damu yake kwa wale wote waelekeao katika mauti. Pia amejitambulisha kuwa yeye binafsi ndiye njia ya kweli ya uzima. Mungu anasema kwamba ikiwa watu hawatoamini injili njema ya Yesu, kamwe hawatoingia Ufalme wa Mbinguni.
Lazima tuamini injili ya maji na Roho kuweza kusamehewa dhambi zetu zote na kuamini kwamba, yeye ndiye mwokozi wetu, na hivyo kuweza kuingia katika Ufalme wa Mbinguni.
 

Hapo zama za kale za Israeli!

“Hata ikawa katika siku za Ahazi mwana wa Yothamu mwana wa Uzia mfalme wa Yuda Resini mfalme wa Shamu na Peka mwana wa Romalia mfalme wa Israeli wakapanda wakaenda Yerusalemu ili kupigana nao lakini hawakuweza kuushinda” (Isaya 7:1).
Kiasili Israeli lilikuwa ni taifa moja. Hata hivyo Israeli ikagawanyika kuwa kusini na kaskazini. Hekalu la Mungu lilikuwa Yerusalemu ya kusini mwa Yudea, ambamo Rehobamu mwana wa mfalme Sulemaini alitawala. Baadaye Yerobamu aliyekwa mtumishi wa Suleimani alianzisha taifa jingine katika kaskazini na hivyo Israeli ikagawanyika. Katika nyakati hizo ndipo imani katika Mungu iliporomoka. Kuporomoka kwa imani huko ndiko kulikoleta chanzo cha dini za uzushi hata kwa nyakati hizi za leo. Yerobamu kwa jinsi hii akawa mwanzilishi wa wazushi. Alibadilisha sheria ya Mungu kwa sababu alihitaji kuweka kiti chake cha enzi, na hivyo moja kwa moja akawa baba wa wazushi. Aliunda dini nyingine tofauti kwa watu wake wa Israeli, utawala wa kaskazini na hata kuthubutu kuivamia Yuda utawala wa kusini. Ni takribani miaka 200 imepita hadi sasa lakini hali hii isiyo ya kawaida katika uhusiano kati ya tawala hizi mbili haujabadilika.
Hata hivyo Mungu aliongea kupitia Isaya, “kwa kuwa Shemu amekusudia mabaya juu yako pamoja na Efraimu na mwana wa Remali wakisema, haya na tupande ili kupigana na Yuda na kuwasumbua tukabomoe mahala tupate kuingia na kummilikisha ufalme ndani yake hiyo mwana wa Tabeeli. Bwana Mungu asema hivi, neno hili halitosimama wala halitakuwa. Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameshi na kichwa cha Dameshi ni Resini na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande asiwe kabila ya watu tena, tena kichwa cha Efraimu ni Samaria ni mwana Remalia. Kwamba hamtaki kusadiki, bila shaka hamtathibitika” (Isaya 7:5-9).
Katika nyakati hizo Mungu alitabiri kupitia Isaya kwa mfalme Ahazi lakini hakumwamini. Ahazi alikumbwa na wasiwasi kwamba asingeweza hata kushindana na jeshi la Dameshi kwa uvamizi wakiungana na washirika wengine, hivyo Israeli ilitetemeka kwa woga. Lakini mtumishi wa Mungu Isaya alikuja na kumwambia mfalme, “si chini ya miaka sitini na saba Israeli ya kaskazini itavunjika. Na njama za uovu wa tawala mbili hizi kamwe hazitofanikiwa”.
Mtumishi wa Mungu alimwambai mfalme Ahazi kutafuta ishara ya Mugu “jitakie ishara ya Bwana Mungu wako; itake katika mahali palipo chini sana au katika mahali palipo juu sana” (Isaya 7:11). “Sikilizeni sasa enyi nyumba ya Daudi, je, ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia? Kwahiyo, Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama bikira atachukua mimba atazaa mtoto mwanaume naye atamwita jina lake Imanueli” (Isaya 7:13-14). Huu ni unabii wa Mungu ya kwamba ataokoa watu wake kwa dhambi zao.
 

Nani ni adui wa Mungu?

Adui wa mwanadamu ni dhambi na dhambi imetokana na shetani. Na ni nani mwokozi wa dhambi zetu? Mwokozi si mwingine bali ni Yesu Kristo mwana wa Mungu. Kimsingi mwanadamu ni dhaifu kimwili, hivyo hawezi kuacha dhambi. Yupo chini ya nguvu za shetani. Watu wa kuu na mashuhuri bado huenda kwa wapiga ramli na watabiri huku wakijaribu kuishi maisha vile wanavyo elekezwa na manabii hawa wauongo. Kwa hili ni uthibitisho wa moja kwa moja kwamba wamo chini ya utawala wa shetani.
Bwana alimpa Isaya uthibitisho wa wokovu, akisema kwamba, bikira atabeba mimba na kumzaa mwana, na jina lake ni Imanueli. Ulikuwa ni mpango wa Mungu kumtuma Yesu kwa mfano wa mwili wa mwanadamu ulio wa dhambi na kumfanya aweze kuokoa wenye dhambi tokana na mteso ya shetani. Kulingana na unabii huu, Yesu alikuja ulimwenguni akiwa mwanadamu aliyezaliwa na bikira Mariamu. 
Kama Yesu asingekuja kwetu, tungeendelea kuishi chini ya utawala wa shetani. Lakini Yesu alikuja ulimwengui na kubatizwa na Yohana, kufa msalabani ili kutupatia injili njema ambayo ingeliweza kuokoa wale wote wenye dhambi. Hivyo watu wengi walio amini injili walipokea msamaha wa dhambi na kuwa watoto wa Mungu.
Hata leo hii wanatheologia wengi hubisha kwamba endapo Yesu Kristo ni Mungu au mwanadamu. Wanatheologia wenyemsimamo husema “Yesu ni Mungu” lakini wale wa siku hizi hutahamaki kwa kupinga na kusema Yesu alikuwa ni mtoto halali wa Yusufu. Ni kauli ya kusikitisha!
Baadhi ya Wanatheologia wa nyakati hizi kusema kwamba, hawawezi kuamini ya kuwa Yesu alikuwa na uwezo wa kutembea juu ya maji. Husema “ukweli ni kwamba Yesu alitembea katika kina kifupi cha tambarare na hivyo wafuasi wake kwa kuona hivyo kwa mbali walidhani alikuwa juu ya maji ya kina kirefu akitembea.” Madaktari wa elimu juu ya Mungu waliomo katika shule za theologia ya kisasa si wote walio wanatheologia maarufu na wengi wao huchagua kuamini yale tu wanayoweza kuyaelewa katika biblia.
Kwa kutoa mfano mwingine Biblia inasema kwamba, Yesu aliwalisha watu wapatao 5,000 kwa samaki wawili na mikate mitano. Lakini wamebaki kulipinga kabisa jambo la muujiza huu. Huelezea kwa namna hii, “watu walimfuata Yesu huku wakiwa na njaa karibia kufa. Hivyo Yesu aliwaelekeza wafuasi wake kukusanya kwa pamoja makombo ya chakula. Ndipo akatokea mtoto mmoja na kumpa chakula chake kwa hiyari, kuona hivyo watu wazima wakaguswa mioyo na kuanza kutoa vyakula vyao. Walipo kusanya vyakula vyote kwa pamoja na kuvila, vikapu kumi na mbili vilibaki makombo.” Wanatheologia wa aina hii wanachoweza ni kujaribu kufanya maneno ya Mungu kutosheleza ufahamu wao ulio finyu.
Kuamini ukweli wa Mungu ni kuwa na imani katika injili njema ya Mungu aliyetupatia. Imani haina maana ya kujaribu kuamini jambo moja kwa sababu tu linaeleweka na kuwa na maana huku ukishindwa kuamini jingine kwa sababu halieleweki. Ikiwa tutaweza kuelewa au kutoelewa bado kunaulazima wa kumwamini Mungu na kuyakubali maneno yake kwa jinsi yalivyo andikwa.
Ukweli ni kwamba Yesu alikuja kwetu kama mwana wa Adamu na kwa maana hivyo alitumwa kutuokoa kwa dhambi zetu zote. Yesu aliye Mungu alikuja ulimwenguni kutuokoa. Isaya alikwisha tabiri kwamba angelikuja kwetu kama mwana wa Adamu na kuzaliwa na bikira.
Katika mwanzo 3:15, Bwana Mungu alimwambia nyoka “nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino”. Maana yake ni kwamba, Mungu alikwisha panga kumtuma Yesu kwa umbile la mwanadamu kama mwokozi wetu kutuokoa sisi wanadamu kwa dhambi zetu.
Katika biblia inaandikwa “kuwapi Ewe mauti kushinda kwako? U wapi ewe mauti uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu za dhambi ni torati” (1 Wakorintho 15:55-56). Uchungu wa mauti ni dhambi. Mtu anapotenda dhambi mauti humfanya awe mtumwa, lakini Bwana wetu ametuahidi “uzao wake huo utakupounda kichwa”. Hii inamaana kuwa Yesu ataharibu uchungu wa dhambi ambao shetani aliuleta.
Yesu alikuja ulimwenguni na kubatizwa ili kubeba dhambi zote za ulimwengu na kuhukumiwa kwa kusulubiwa kwa ajili ya dhambi hizo. Aliokoa wale wote wanao mwamini katika injili njema. Pale Adamu na Hawa walipotenda dhambi, Mungu aliahidi kuokoa wanadamu tokana na utawala wa shetani. Katika ulimwengu wa kisasa maadui wa Mungu ni wale wote wasio amini injili njema.
 

Kwa nini Yesu alizaliwa ulimwenguni? 

Mungu alitupa sheria (torati) pamoja na injili njema ili kutuokoa dhambini. Chini ya sheria (torati) watu walikuwa ni wenye dhambi mbele yake. Kwa jinsi hiyo pia sheria (torati) ililetwa ili watu waweze kufahamu dhambi zao. Watu walipo kuwa watumwa wa dhambi na kwa sheria (torati) yenyewe, Bwana akaja ulimwenguni kutimiza hitaji la haki ya sheria hiyo.
Yesu alizaliwa chini ya sheria (torati). Alizaliwa kipindi cha sheria (torati). Sababu amabayo watu walihitaji sheria (torati) ni kwamba walihitaji kuelewa juu ya dhambi zao ili hatimaye waweze kupokea msamaha wake. Watu husafisha uchafu toka katika nguo zao ikiwa tu wameweza kuungundua uchafu huo. Hivyo ndiyo pia kwao kugundua dhambi zao kumewapasa kufahamu sheria ya Mungu. Kama pasinge kuwako na sheria pasinge kuwako maana ya dhambi; na Yesu asingelihitajika kuja ulimwenguni.
Ikiwa unafahamu sheria ya Mungu, basi unayo nafsi ya kukutana naye. Sisi tulifahamu juu ya sheria na hivyo tumeweza kutambua juu ya dhambi zetu. Nipale tu tulipo fahamu juu ya dhambi zetu ndipo Yesu Kristo alipo leta injili njema kwetu ili tuiamini. Ikiwa Mungu asingeli tupatia sheria, basi tusingeweza kuwa wenye dhambi na hukumu isingelikuwapo. Kwa haya yote Mungu ametupa sheria (torati) na kutuletea injili njema kuokoa wote toka dhambini. 
Sheria (torati) iliyo muhimu kuwepo kati muumba na viumbe wake ni sheria ya Mungu ya wokovu. Hii ni sheria ya Upendo. Mungu alimwambia mwanadamu “walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika” (Mwanzo 2:17). Hii ilikuwa ndiyo sheria ya Mungu aliyo tupatia, na sheria hii ndiyo ikawa msingi wa upendo ambao Mungu alituokoa sisi sote kwa dhambi zetu. Mungu anatueleza kwamba yeye ndiye muumba wetu na hivyo kila kitu kimekuwepo kulingana na mapenzi yake. Hii ina maana kwamba, hakika Mugu yu hai na hivyo watu imewapasa kuamini sheria ya wokovu ambayo ilikamilishwa kupitai injili njema.
Mungu aliye hai hakika ni mwema. Upendo wa Mungu kwa ulimwengu huu ndiyo ulio msukuma yeye kumtoa mwana wake wa pekee na kuwa mwokozi wa wenye dhambi wote. Ikiwa Mungu alituumba, na ikiwa asingetupatia injili njema na kutuokoa kwa dhambi zetu, hakika tunge mlalamikia. Lakini Mungu alipenda kutuokoa tokana na kuangamia na hivyo kuweka sheria ya wokovu. Kwasababu ya torati, tumeweza kutambua dhambi zetu na kuziona moja kwa moja, na hivyo kuanza kuiamini injili njema ya Yesu. Tunapokwenda kinyume na neno la Mungu tunaonekana wazi kama wenye dhambi mbele ya torati na baada ya yote sisi wenye dhambi tunapiga magoti kwa kusihi rehema ya Mungu kwa ajili ya msamaha wa dhambi mbele yake.
Yesu alizaliwa na mwanamke na kuja ulimwenguni kuokoa wanadamu kwa dhambi zao. Yesu alikuja ulimwenguni akiwa mwanadamu kutimiza mpango wa Mungu kwetu. Tunaiamini injili yake njema. Hivyo basi tunamsifu Bwana.
Wengine hulalamika, “kwanini Mungu aliniumba kuwa mdhaifu namna hii ambapo mara kwa mara naanguka kirahisi katika dhambi na hata kateseka sana kwa uovu wangu?” Lakini hakika kamwe Mungu hakupenda sisi tuteseke, bali ameruhusu iwe hivyo kwa sababu tumekuwa kinyume na injili ya Yesu. Mungu ametupatia mambo mawili, mateso na injili njema ili tuweze kuwa na nguvu kama yake tukiwa wana kwake. Na huu ndiyo aliokuwa mpango wake.
Lakini pepo husema ndani yako “Hapana! Hapana! Mungu ni mtawala wa kimabavu! Wewe endelea kuishi vile utakavyo. Uwe huru! Tafuta bahati yako kwa uwezo wako.” Pepo hawa pia hujaribu kuzuia wanadamu kumwamini Mungu. Lakini wale wote wenye kuchagua kuishi mbali na Mungu ndiyo kwazo kwa mpango wake wa wokovu. Yesu alikuja ulimwenguni na kuwaita wale wote walio chini ya utawala wa shetani kutubu dhambi zao. Tusijaribu kamwe kuishi mbali na Mungu.
 

Mwanadamu amezaliwa akiwa mwenye dhambi na mwisho wake ni motoni.

Hakuna ukweli usio badilika hapa ulimwenguni. Lakini injili njema ya Yesu ni ukweli ulio madhubuti usio badilika. Hivyo watu wanaweza kutegemea ukweli wake na hatimaye kukombolewa tokana na nguvu za shetani. Wanadamu wamerithi dhambi ya Adamu na Hawa na hivyo pasipo Kristo kuingilia kati wangeangamia motoni. Badala yake namshukuru kwa kujitoa kwake, na kwa jinsi hiyo basi mwanadamu alibarikiwa na nguvu ya kuweza kuwa mwana wa Mungu. “Lakini yeye aliyekuwa katika dhiki hatokosa changamko” (Isaya 9:1). Mungu alimtuma mwana wake ulimwengu hivyo kuwatukuza wale wote wenye kuamini wokovu ulio mwema.
“Watu wale waliokwenda katika giza wameona nuru kuu; wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewaangaza” (Isaya 9:2). Leo hii andiko limekuwa kweli kwako na kwangu. Kwa kuamini injili njema tumebarikiwa na uzima wa milele ambao hakika hatuwezi kuupata hapa ulimwenguni. Yesu Kristo aliokoa wanadamu kwa dhambi zao zote za ulimwengu na kwa wale wote watakao amini injili hii njema amewapa uzima wa milele na Ufalme wa Mbinguni.
 

Ameweka nuru njema ya injili kwa wale wote walio poteza tumaini.

Mwanadamu ni kama ukungu unao kuwepo juu ya ardhi kwa muda na punde kupotea. Maisha yake ni kama mazao au nyasi katika msimu wa mwaka. Nyasi huwa na nguvu ya uhai kwa miezi michache tu wakati wa kipindi cha mwaka mmoja na kupotea kulingana na mapenzi mema ya Mungu. Kwa maisha yetu, yote huwa ni bure na yasiyo na maana kama ilivyo katika nyasi hizi. Lakini Mungu ametupatia injili njema kwa roho zetu zilizo choka na kwa haki yake ametufanya kuwa watoto wake. Hakika hii ni neema ya ajabu! Uhai wetu usio na maana umegeuka kuwa uzima wa milele. Tunaushukuru upendo wa Mungu na pia tumebarikiwa na haki ya kuwa wana wake.
Hapa upo ushuhuda wa nafsi iliyobarikiwa kwa neema ya Mungu kwa kuamini injili njema.
“Nilizaliwa katika familia ambayo haikuwa inamwamini Mungu. Hivyo nililelewa katika mazingira ya kuona kuwa ilikuwa ni jambo jema kwake mama yangu kuomba kwa miungu ya mbinguni na duniani kwa ustawi wa familia yetu kila siku asubuhi akiwa na bakuli la maji mbele yake. Umri uliposogea wakati huo sikuweza kuelewa thamani yangu au sababu ya mimi kuishi ambapo kulinifanya niamini kwamba haikuwa na maana endapo nitakuwa hai au kuishi. Hii ni kutokana na kwamba sikuwa nimetambua uthamani wangu hivyo kuishi katika hali ya upweke.
Maisha ya aina hii yalinichosha na hivyo nilikimbilia kuolewa. Maisha yangu ya ndoa yalikuwa mazuri. Sikuwa na chakutamani hivyo niliishi kwa amani na furaha. Baadaye nikawa na mtoto na kuanzia hapo nikaanza kuona upendo ukichomoza ndani yangu. Nikaanza kupoteza hali ya ubinafsi ndani yangu lakini pia nikahofu kuwapoteza wale walio karibu nami.
Kwa yote haya nikaanza kumtafuta Mungu. Nilikuwa mdhaifu nisiye jiweza na hivyo nilimhitaji mwenye enzi aliye hai kuweza kulinda nilio wapenda. Hivyo nikaanza kuhudhuria kanisani lakini imani yangu ilikuwa tofauti kidogo dhidi ya mama yangu kwa jinsi alivyokuwa akiomba mbele ya bakuli la maji, kwani maombi yangu kimsingi yalihusika zaidi na maono ya hofu na matumaini.
Wakati mmoja nilipata kuhudhuria mkutano fulani katika moja ya makanisa ya eneo langu, na wakati nilipokuwa nikiomba machozi yalianza kumiminika nilifedheheka na kujaribu kujizuia kulia lakini wapi, machozi yalizidi kunitiririka. Watu walio kuwa karibu yangu waliniwekea mikono juu ya kichwa changu na kuanza kunipongeza kwa kumpokea Roho Mtakatifu. Lakini nilipotoshwa, sikuwa naelewa hata kidogo maneno ya Mungu na imani yangu kwake ilikuwa ni hisia tu, hivyo sikuwa na uhakika endapo nguvu hizo kweli zilikuwa ni za Roho Mtakatifu.
Kanisa nililohudhuria lilikuwa likijihusisha na vuguvugu la uamsho wa Kipentekoste na wengi walitokewa na hali hiyo iliyonipata na hivyo karibia wote walikuwa wakinena kwa lugha. Siku moja, nilialikwa katika mkutano wa uamsho uliokuwa ukiongozwa na mchungaji mmoja ambaye watu walikuwa wakihadithia kuwa alikuwa amejazwa na Roho Mtakatifu. Mchungaji huyo alikusanya makundi ya watu katika kanisa na kusema angeliweza kumponya mtu mwenye matatizo ya kupumua kwa kupitia uweza wa nguvu za kiroho. Hata hivyo nilidhani kwamba ugonjwa huo ungeweza kuponywa hospitalini kirahisi zaidi, hivyo nilikuwa na hamu ya kuona ni kwa kiasi gani mchungaji huyo alivyo pokea upako wa Roho Mtakatifu. Lakini baada ya kuona kuwa alifanikiwa kuponya alianza kujigamba kwamba angeliweza pia kutabiri ikiwa wanafunzi wa sekondari wangeliweza kufaulu mtihani wa kuingia chuo kikuu au la. Watu wengi walisifu nguvu alizo nazo utadhani zilikuwa ni za Mungu.
Lakini sikuweza kumuelewa. Na hivyo sikuhitaji kutathimini juu ya nguvu alizonazo mchungaji huyo ikiwa zina husika na Roho Mtakatifu au la. Sikuona kwamba palikuwa na umuhimu kati yakuweza kwake kuponya ugonjwa huo au kutabiri mafanikio ya mtihani wa mtu. Hivyo sikuchukulia moja kwa moja juu ya miujiza hiyo kuwa ni nguvu za Roho Mtakatifu. 
Nguvu na upendo wa Mungu nilio kuwa nao moyoni ulikuwa ni tafauti na nilio uona. Kwasababu hiyo nilikoma kuhudhuri kanisa hilo nahivyo kuwakwepa wale wote waliokuwa wakiamini nguvu za mchungaji huyo. Baada ya hapo nilianza kuhudhuri kanisa jingine tulivu ambalo nililolichagua kwa sababu ndipo mahala neno la Mungu linapohubiriwa zaidi. Nilijifunza kuhusiana na sheria na kwa kupitia hilo nikajitambua sina haki ndani yangu. Ndipo hapo basi Mungu akawa kigezo cha hofu kwangu na nikagundua kwamba sikuweza kuonekana mwenye hadhi mbele yake na hivyo Roho wake alionekana kunitenga kabisa.
Katika Isaya 59:1-2 imeandikwa “Tazama mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na Mungu wenu na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone hata hataki kusikia”. Hili lilionekana kuwa sawa na hali yangu. Ni jambo lisilowezekana kwangu kuwa mwana kwake na kumpokea Roho Mtakatifu kwa sababu yote niliyofanya au kuwaza yalikuwa ni uovu tu.
Nilimhofu Mungu na hivyo nikawa nikifanya sala za toba kila mara. Hakuna aliye niambia kufanya hivyo lakini nilitaka kusimama nikiwa na hadhi mbele ya Mungu. Kwakuwa nilikuwa ni mwenye dhambi, niliendelea kufanya sala za toba kwa bidii zaidi. Lakini sala hizi zilishindwa kutakasa dhambi zangu. Yote niliyo yafanya yalikua ni kumwonyesha Mungu mawazo yangu na uaminifu hivyo dhambi zangu bado ziliendelea kuwepo. Kuanzia muda huo nilianza kutoa malalamiko dhidi ya Mungu nilitamani kuwa mkamilifu mbele ya macho yake lakini sikuweza kuwa hivyo moja kwa moja, hivyo malalamikio yangu na dhambi zangu zilirundikana.
Wakati wa kipindi hiki chote cha kuchanganyikiwa kidini baba yangu akapatwa na kiharusi. Aliteseka kwa muda wa siku 40 hospitalini katika chumba cha mahututi akiwa kitandani kabla ya kufariki. Lakini sikuweza kumwombea hata kidogo. Nilikuwa ni mwenye dhambi, hivyo niliwaza ya kwamba kama ningeliomba kwa ajili ya baba yangu maumivu yake yangeliweza kuwa mabaya zaidi. Nilichanganyikiwa na kukata tamaa kwa kukosa imani na nilitamani kumfuata Mungu lakini sikuweza, hivyo niliendelea kulalama na hatimaye kumhasi. Maisha yangu ya kidini ndipo hapo yalipo komea. Nilidhani kwamba ikiwa nitamwamini yeye, Roho wake ataweka makazi ndani yangu na hivyo kupata amani lakini hilo halikuwa ni sababu. Baada ya hapo maisha yangu hayakuwa na maana kabisa na nilianza kuishi kwa hofu na huzuni.
Lakini Bwana hakunitelekeza. Alisababisha niweze kukutana na muumini ambaye kwa hakika amempokea Roho Mtakatifu kupitia maneno ya Mungu. Nilijifunza kutoka kwa mtu huyu kwamba, Yesu alizichukua dhambi zetu kupitia ubatizo wake kwa Yohana na hivyo alihukumiwa kwa dhambi hizi msalabani. Kwa hiyo, dhambi zetu zote ulimwenguni, pamoja na zangu, zilisamehewa. Niliposikia na kuweza kuelewa hili niliweza kuona kwamba dhambi zetu zote zilitakaswa. Mungu alinisaidia kupata msamaha wa dhambi zangu zote na kunipa baraka ya Roho Mtakatifu na kunitunukia maisha ya amani. Taratibu aliniongoza akanipa kuelewa mabaya na mazuri na hivyo kunivika nguvu ya kushinda majaribu ya ulimwengu huu. Alijibu maombi yangu na kunisaidia katika kuishi maisha yaliyo ya haki na yenye thamani. Kwa kweli namshukuru sana Mungu kwa kunipatia Roho Mtakatifu.”
Kila mmoja wetu amebarikiwa na neema ya Bwana na anauwezo wa kumpokea Roho Mtakatifu. Namshukuru Bwana kwa kunipatia injili yake njema. Mungu alibariki wenye haki kwa furaha hii. Mioyo ya wenye haki ni yenye furaha. Bwana ametutunukia furaha ya milele. Tunajua ni kwa vipi wokovu wa Mungu ulivyo wa thamani, upendo na neema, hivyo tunamshukuru kwa yote hayo. Bwana ametupatia furaha kupitia injili njema ya mbinguni. Hiki ni kitu ambacho hakiwezi kamwe kununuliwa kwa fedha. Mungu alimtuma kwetu Roho Mtakatifu pamoja na injili njema ili kutufanya washindi na waadilifu. Injili hii njema ndiyo ifanyayo maisha yetu yabarikiwe. Bwana ametupatia injili njema na anafarijika kwa kuwa wale wote wenye haki watayafurahiya maisha ya baraka. 
Kama ilivyo andikwa katika Luka, Mariamu alisema, “Kwakuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu Mariamu akasema, tazama mimi ni mjakazi wa Bwana na iwe kwangu kama ulivyosema” (Luka 1:37-38). Wakati ule tu Mariamu alipoamini maneno mazuri ya Mungu kama yalivyo nenwa na malaika wake ndipo hapo mara mimba ya Yesu ikatungwa. Kwa jinsi hiyo pia kwa imani wenye haki hutungwa mimba ya injili njema mioyoni mwao.
“Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake na fimbo yeke yeye aliyemwonea kama katika siku ya Mediani” (Isaya 9:4). Shetani alisababisha mafarakano, magonjwa na mateso katika maisha yetu hivyo sisi niwanyonge kuweza kumshinda. Lakini Mungu anatupenda na hivyo alipigana vita na shetani na hatimaye kumshinda.
“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa tumepewa mtoto mwana mume na uweza wa kifalme utakuwa begani kwake naye ataitwa jina lake mshauri wa ajabu Mungu mwenye nguvu baba wa milele mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake. Kuuthibitisha na kuutegemeza kwa hukumu na kwa haki tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndiyo utakaotenda hayo” (Isaya 9:6-7).
Mungu aliahidi kututukuza kama watoto wake kupitia injili nzuri ambayo Yesu alileta. Alimshinda Shetani kulingana na ahadi Yake na akatukomboa kutoka kwa nguvu za Shetani.
Bwana alikuja duniani na kwa nguvu Yake aliahidi kuondoa giza lote la dhambi. Kwa hivyo sisi pia tunamwita Bwana wetu Mzuri. Ametufanyia mambo mengi mazuri. Uamuzi wa Mungu kuja ulimwenguni kama Mwana wa Adamu ulikuwa wa kushangaza. Bwana anasema, “Njoo sasa, na tuungane pamoja. Ingawa dhambi zako ni kama nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji; ingawa ni nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu ”(Isaya 1:18).
Bwana aliahidi kutuokoa tokana na dhambi zetu na kutupatia msamaha wa milele. Yesu anaitwa hapa kuwa ni “Waajabu” na kwa jinsi hiyo alifanya kazi yamiujiza kwetu “jina lake ataitwa Mshauri, Mungu mwenye enzi”. Mungu akiwa mshauri, alipangilia wokovu wetu kwa injili njema hivyo kupanga kutuokoa milele kwa dhambi zetu.
Upumbavu wa Mungu ni hekima kubwa zaidi ya mwanadamu. Ilikuwa ni hekina yake kwa Yesu kubatizwa na Yohana na kufa msalabani ili kutuokoa kwa dhambi zetu zote. Hii ni kazi ya ajabu aliyo ifanya kwetu kwa sheria ya upendo ambao ulituokoa kwa dhambi zetu zote. Sheria ya upendo ni injili ya kweli ambayo hutuongoza katika kumpokea Roho Mtakatifu kupitia maji na damu yake.
Bwana anasema katika Isaya 53:10, “lakini Bwana aliridhika kumchubua amemhuzunisha” Yesu aliifanya nafsi yake kuwa sadaka ya dhambi ili kuyatimiza mapenzi ya Mungu. Mungu alitwika dhambi zote za ulimwengu juu ya mwana wake, Yesu Kristo, na kuruhusu ateseke kwa kusulubiwa ili iwe hukumu kwa ajili ya dhami hizo. Hii ndiyo injili njema iliyo okoa wanadamu kwa dhambi zao mara moja na kwa wote. Kristo alitoa uhai wake kwa ajili yetu na kulipa mshahara wa dhambi na kutubariki kwa wokovu.
 

Mpangilio wa sadaka ya Mungu.

Ni dhambi ngapi Yesu alibeba
Kwa kubatizwa kwake na Yohana?
Dhambi za zamani, sasa na wakati ujao 
kwa kuanzia Mwanzo hadi mwisho 
wa ulimwengu.

Biblia huzungumzia juu ya sadaka ambayo hapo zamani za kale iliweza kuleta msamaha wa dhambi za kila siku. Mwenye dhambi ilimpasa kuleta mnyama asiye na doa na kumwekea mikono juu ya kichwa chake ili kumtwika dhambi zake. Ndipo ilimpasa aichinje shingo sadaka hiyo na kuikabidhi damu yake kwa kuhani. Naye kuhani alichukua kiasi cha damu hiyo na kukiweka katika pembe za madhabahu ya kuteketezwa na iliyo salia alimwaga chini ya madhabahu hiyo.
Kwa njia hii mtu huyo aliweza kusamehewa dhambi za kila siku. Tendo la kuwekea mikono lilikuwa ni njia ya mwenye dhambi kumtwika dhambi mnyama huyo wa sadaka. Wale waliotoa sadaka kulingana na mpangilio huu waliweza kupokea msamaha wa dhambi zao. Mpangilio huu ndiyo iliyokuwa njia tuliyo patanishwa kwa dhambi zetu nyakati zile kabla ya Yesu kubeba dhambi zote.
Pia Mungu aliweka siku maalumu ya upatanisho ili kwamba watu wa Israeli waweze kufanya upatanisho kwa dhambi zao walizotenda kwa kipindi cha mwaka mzima. Utoaji wa sadaka hiyo ulifanyika katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Mungu alimteua Harumi Kuhani mkuu kuwa ndiye pekee atakayetwika dhambi zote za Israeli kwa mwaka mzima juu ya mnyama wa kafara. Ibada hii ilifanyika kulingana na mpangilio wa Mungu. Msamaha wa dhambi ulikuja kwa hekima na kwa upendo wake kwa wanadamu. Hii ndiyo nguvu yake.
“Pembe za madhabahu ya sadaka za kuteketezwa” humaanisha “kitabu cha hukumu” (Ufunuo 20:12) ambamo dhambi za wanadamu zimewekwa kumbukumbu. Sababu ya kuhani kuweka damu ya sadaka ya dhambi katika pembe za madhabahu ya sadaka za kuteketezwa, ilikuwa ni kufuta majina na makosa yaliyo andikwa katika kitabu cha hukumu. Damu ni uhai wa mwili. Sadaka ya mnyama ndiyo iliyo beba dhambi za Waisraeli hivyo ilibidi ichinjwe kulipia mshahara wa dhambi. Mungu aliruhusu ichinjwe ili iwe ni hukumu ya dhambi zao. Hii ilikuwa ni ishara ya hekima na upendo wake kwetu.
Yesu Kristo alikuja hapa ulimwenguni kama sadaka ya dhambi ili atimize mpango wa Mungu. Yesu alichukua dhambi za ulimwengu kwa njia ya kujitoa kwake. Ikiwa tutaangalia maneno ya ahadi yake tutaona “lakini Bwana aliridhika kumchubua amemhuzunisha” (Isaya 23:10) au “alibeba dhambi ya ulimwengu” (Yohana 1:29).
“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa tumepewa mtoto mwanaume na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake naye ataitwa jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe, katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake kuuthibitisha na kuutegemeza kwa hukumu na kwa haki tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo” (Isaya 9:6-7).
Miujiza na maajabu ya ahadi ilikuwa ni Yesu atakaye fanya mapenzi ya Mungu na kuwapa wale wote wanao amini amani kwa kubeba dhambi zote za ulimwengu. Ahadi ya Mungu ilikuwa ni ahadi ya upendo ambao aliupanga ili kuleta amani kwa wanadamu wote. Hili ndilo Mungu alilotuahidi na ndilo alilotimiza.
Mathayo 1:18 inasema, “kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribina alionekana ana mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”. “Yesu” maana yake Mwokozi yeye atakaye waokoa watu wake kwa dhambi zao. “Kristo” maana yake Mfalme mpakwa mafuta. Yesu hakuwa na dhambi, na ndiye mfalme wetu na Mwokozi wetu aliyezaliwa na mwanamwali ili aokoe watu wake kwa dhambi zao.
“Naye atazaa mwana nawe utamwita jina lake Yesu maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa manabii” (Mathayo 1:21-22).
 

Yesu alibeba dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya ubatizo wake.

Imeandikwa katika Mathayo 3:13-16, “Wakati huo Yesu alikuja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana iliabatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, mimi nilihitaji kubatizwa na wewe nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini na tazama mbingu zikamfunukia akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua akija juu yake, na tazama sauti kutoka mbinguni akisema huyu ni mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye.”
Yohana mbatizaji anaonekana katika kifungu hiki. Kwanini Yesu ilimpasa abatizwe na Yohana? Yesu ilimpasa abatizwe ili aweze kubeba dhambi zote za ulimwengu na iwe kwa mpango wa Mungu.
“Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake” (Isaya 9:6). Hapa “Uweza wa Kifalme” maana yake Yesu ndiye pekee aliye na mamlaka na nguvu kama Bwana wa Mbinguni, Mfalme wa ulimwengu. Hii ni mamlaka aliyo tunukiwa Yesu Kristo pekee. Yesu alifanya jambo zuri katika kubeba dhambi zote za wanadamu. Jambo hili zuri lilikuwa ni kwake kuweza kubatizwa na Yohana. Kile Yesu alichomaanisha anaposema “ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” ni katika kuzichukua dhambi zote za ulimwengu kwa usawa na kwanamna ipasayo.
Warumi 1:17 inasema, “Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani”. Haki ya Mungu inadhihirishwa katika injili. Je, injili ya kweli katika maji na Roho imedhihirisha haki ya Mungu? Ndiyo! Injili ya kweli ni ile ambayo Yesu Kristo alichukua dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya ubatizo wake na kusulubiwa kwake. Injili ya maji na Roho ni injili iliyo njema ambayo haki ya Mungu imedhihirishwa. Ni kwa njia gani Yesu alichukua dhambi ya ulimwengu? Alichukua dhambi zote za ulimwengu pale Yohana Mbatizaji alipo mbatiza katika mto Yordani.
Kwa lugha ya Kigiriki neno “haki yote” ni “πᾶσαν δικαιοσύνην (pasan dikaiosune)”. Hii inamaana kwamba Yesu alibeba dhambi zote za wanadamu kwa njia ya haki na iliyo njema. Pia inamaana kwamba Yesu kutakasa dhambi zote za ulimwengu kilikuwa ni kutendo kilichostahili na chenye haki. Ilimbidi Yesu abatizwe na Yohana ili afute dhambi za ulimwengu.
Mungu alijua kwamba ubatizo wa Yesu ulikuwa ni muhimu hakika ili kuleta amani kwa wanadamu. Yesu asingeliweza kuwa mwokozi ikiwa kama asingelibatizwa na Yohana na kumwaga damu yake msalabani. Yesu alijitoa kama sadaka ya dhambi kwa kubeba dhambi zote za ulimwengu.
Mungu anasema katika Isaya 53:6 “Sisi sote kama kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote”. Ilimbidi Yesu azikubali dhambi za ulimwengu wote ili atimize mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo sababu kwamba Yesu alikuja akiwa kama sadaka ya dhambi katika mwili wa mwanadamu na kubatizwa na Yohana.
Yesu alikubali dhambi zote za wanadamu na kuhukumiwa kwa ajili yake ili aweze kutimiza mapenzi na mpango wa Mungu hivyo kuweka bayana upendo wake usio na kikomo. Yesu alipotoka majini baada ya ubatizo wake, Mungu alisema, “huyu ni mwanangu mpendwa wangu ninayependezwa naye” (Mathayo 3:17).
 

Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa.

“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake. Naye ataitwa jina lake Mshauri wa ajabu Mugu mwenye nguvu Baba wa milele, Mfalme wa amani” (Isaya 9:6). Yesu ni mwana wa Mungu. Yesu ni Mungu muumbaji aliye umba ulimwengu wote. Si tu mwana wa Mungu mwenyezi, yeye pia ni Mumba na Mfalme wa Amani. Yesu ni Mungu aliye wapa wanadamu furaha.
Yesu ni Mungu wa kweli alibeba dhambi zetu zote, akatuokoa na kutupa amani. Je, ipo dhambi tena duniani? Hapana hakuna dhambi. Sababu ya kuweza kuwa na uhakika wa kusema haya kwamba hakuna dhambi tena, ni kuwa tunaamini injili njema ambayo inasema kwamba Yesu alitakasa dhambi zote za ulimwengu kwa kupitia ubatizo na damu yake pale msalabani. Yesu hakutudanganya. Yesu alilipa mshahara wa dhambi kwa ubatizo na damu yake. Amewezesha wale wote watakao amini haya, kuweza kuwa watoto wa Mugu na kutupatia amani sisi sote. Alitufanya kuishi tukiwa watoto walio takaswa katika imani milele. Namsifu Bwana na kumshukuru. 
 

Tazama mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!

Yohana 1:29 inasema, “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake akasema, tazama mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” Yesu Kristo alionekana tena mbele ya Yohana Mbatizaji siku iliyo fuata baada ya kubeba dhambi za ulimengu kwa njia ya ubatizo wake. Yohana Mbatizaji alishuhudia juu Yesu kwa kusema, “tazama mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” Alishuhudia kwa mara nyinge tena katika Yohana 1:35-36 “Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake akamtazama Yesu akitembea, akasema, tazama mwana kondoo wa Mugu.”
Yesu alikuwa ni Masihi aliyekuja kama mwana kondoo wa Mungu kwa jinsi ile Mungu alivyo ahidi katika Agano la Kale. Masihi Yesu Kristo aliyekuja kwetu akiwa Mshauri wa Ajabu na Mwenyezi Mungu, na alibatizwa ili kutuokoa sisi sote na dhambi zetu. Mtoto alizaliwa kwa ajili yetu. Alikubali kujitwika dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya ubatizo wake kwa Yohana na kulipa mshahara wa dhambi hivyo kuwa Mfalme aliyetupa amani na ondoleo la dhambi zote. “Tazama mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.”
Hapo awali watu hawakuwa na jinsi yoyote bali kufa kwa sababu ya dhambi zao. Wanadamu hutenda dhambi zisizo na idadi hadi mwisho wao kutokana na asili ya dhambi, na matokeo yake kuhukumiwa kwenda motoni. Kwa kuingia katika lindi hilo la maovu; hakuna yeyote kati yao angeliweza hata kuota kuingia Ufalme wa Mungu kutokana na udhaifu huo. Yesu Kristo aliye Mungu wetu alizikubali dhambi zao pale alipo batizwa na Yohana katika mto Yordani, na alisulubiwa kwa hukumu ya makosa yao. Wakati wa kifo chake Kristo alisema “yamekwisha!” (Yohana 19:30) Kupaza huku kwa sauti kulikuwa ni ushuhuda wa ukweli kwamba Yesu aliokoa wanadamu wote kwa dhambi zao na kifo chake, na hivyo kwa ukamlifu alileta ukombozi kwa yeyote yule atakaye amini injili njema.
“Tazama mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Je, unafahamu ni wapi dhambi za ulimwengu zilipo? Je, hazipo juu ya mwili wa Yesu Kristo? Ni wapi zilipo dhambi na makosa yote yanayo tudhohofisha sisi hapa ulimwenguni? Yote yalitwikwa juu ya Yesu Kristo. Dhambi zetu zote zipo wapi? Zote zipo juu ya mwili wa yule aliye na mamlaka mabegani mwake; zipo katika mwili wa Mwenyezi Mungu.
 

Dhambi zote kuanzia kuzaliwa hadi kaburini! 

Tunatenda dhambi maishani mwetu mwote. Tunatenda dhambi kuanzia siku tuliyozaliwa hadi tunapofikisha umri wa miaka 20. Niwapi dhambi hizo tunazo tenda tukiwa na umri kati ya miaka 21 hadi 40? Nazo pia zilitwikwa juu ya Yesu. Haijalishi ni miaka mingapi mtu ataishi, dhambi atakazo tenda kuanzia mwanzo wa maisha yake hadi mwisho zilikwisha twikwa juu ya Yesu Kristo. Dhambi zote za wanadamu kuanzia Adamu hadi mtu wa mwisho hapa duniani zilikwisha twikwa juu ya Yesu. Hata zile dhambi za watoto wetu na wajukuu wetu wote, tayari zimekwisha tikwa juu ya Yesu. Dhambi zote zilitwikwa juu ya Yesu pale alipo batizwa.
Sasa basi, je, bado kunadhambi ulimwenguni? Hapana hakuna hata moja iliyo achwa. Hakuna dhambi iliyo achwa ulimwenguni kwa sababu tunaamini injili njema ambayo Yesu Kristo ametupatia. Je unadhambi moyoni mwako? Hapana. Amina! Tunaamini injili njema ambayo inasema Yesu Kristo alituokoa kwa dhambi zetu zote. Tunamsifu Mwenyeenzi Yesu kwa kufanya kazi hii njema kwa ajili yetu.
Yesu Kristo amerejesha maisha yetu yaliyopotea. Sasa tunaamini injili njema, hivyo tunaweza kuishi na Mungu. Hata wale waliokuwa ni maadui wa Mungu wenye dhambi ambao hawakuwa na jinsi bali kujificha gizani leo hii wataweza kuokolewa toka dhambini mwao kwa kuamini injili njema.
Injli njema hutufundisha kwamba Bwana alitakasa dhambi kwa kusafisha pale alipo batizwa na Yohana, akasulubiwa na kufufuka. Tumekuwa watoto wa Mungu tulio takaswa kwa kuamini injili ya Yesu. Yesu aliutoa mwili wake kuwa sadaka ya dhambi. Yeye Mwana wa Mwenyezi Mungu, ambaye hakutenda dhambi kamwe hata mara moja akiwa hapa duniani alibeba dhambi zote za ulimwengu na kuokoa kila mtu atakaye mwamini. Isaya 53:5 inasema, “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu.”
Yesu alibeba dhambi zote za ulimwengu zikiwemo zote mbili, yaani dhambi ya asili na zakila siku maishani. Hakuacha uovu wowote. Alilipa mshara wa dhambi kwa kifo chake msalabani na kwa hivyo alituokoa sisi sote na dhambi zetu zote. Yesu amesafisha dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya injili njema. Tumepata uhai nafsini kupitia Yesu. Wale wote wenyekuamini habari hii njema kamwe si nafsi zilizo kufa tena. Sasa tunauzima mpya wa wamilele kwa kuwa Yesu amesafisha dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya injili njema. Tumepata uhai mpya kupitia Yesu. Sasa tunauzima mpya na wamilele kwa kuwa Yesu alilipa mshahara wote wa dhambi. Tumekuwa watoto wa Mungu kwa kuamini injili njema ya Yesu Kristo.
Je unaamini kwamba Yesu Kristo ni mwana wa Mungu? Je, pia unaamini kwamba ni mwokozi? Ndiyo ninaamini. Yesu Kristo ni uzima kwetu. Tumepata uzima mpya kupitia kwake. Hatima yetu ilikuwa ni kifo kwa sababu ya dhambi na uovu wetu. Lakini Yesu alilipa mshahara wa dhambi kwa njia ya ubatizo wake na kifo chake pale msalabani. Alitukomboa toka utumwa wa dhambi, toka nguvu za kifo na vifungo vya shetani.
Bwana ni Mungu aliyetuokoa toka dhambini na kuwa mwokozi wa yeyote amwaminiye Yesu. Tunapo angalia katika Waebrania 10:10-12, 14 na 18 tunaweza kuona kwamba, Bwana alitutakasa hivyo kwamba, hapatakuwepo tena na hitaji la ondoleo la dhambi. Tunaingia Ufalme wa Mungu kwa kumwamini Yesu. Hatima yetu ilikuwa ni kifo kwa sababu ya dhambi zetu na uovu wetu, lakini leo hii tunaweza kuinga mbinguni na kufurahiya uzima wa milele kwa kuamini ubatizo na damu ya Yesu.
“Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo” (Yohana 10:11). Bwana wetu alikuja hapa ulimwenguni kutuokoa kwa dhambi za ulimwengu kwa njia ya ubatizo wake, kifo chake msalabani na ufufuo wake. Pia ametoa awepo wa Roho Mtakatifu ndani ya wale wote wenye kuamini ondoleo la dhambi zao kwa kuamini ukweli huu. Nakushukuru Bwana kwa Injili yako njema ambayo inauwezo wa kuwapa wanaoamini, uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao. Haleluya! Namsifu Bwana.