Search

Mahubiri

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-15] Utaweza kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu pale utakapo elewa kweli tu (Yoana 8:31-36)

(Yoana 8:31-36)
“Basi Yesu akawaambia wale wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru. Wakajibu, sisi tu uzao wa Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wa kati wowote wewe wasemaje, mtawekwa huru? Yesu akawajibu Amini amin nawaambia kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi wala mtumwa hakai nyumbani siku zote: mwana hukaa siku zote. Basi mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.”
 

Yatupasa tufanye nini 
ili tuweze kupokea uwepo wa
Roho Mtakatifu?
Yatupasa kuiamini injili njema ya 
majina Roho na kuishi 
kwa imani.

Je unaelewa ukweli ulivyo? Yesu alisema “mimi ndimi njia” (Yohana 14:6), hivyo kumjua Yesu ndiko kuijua kweli. Je, Roho Mtakatifu huweka makazi ndani yako kwa kuishukuru imani ya injili njema? Imekupasa ugundue kwamba ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ni taswira ya injili njema. Hivyo imekupasa kuiamini hivyo.
Siku hizi watu hutumia neno “kuzaliwa upya.” “Watu imewapasa wazaliwe upya. Siasa zizaliwe upya. Dini nazo zizaliwe upya” Neno hili hutumika kama kauli mbiu ya “uboreshaji.” Hata hivyo kuzaliwa mara ya pili haina maana ya uboreshaji wa asili kimwili. Kuzaliwa upya maana yake ni kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa kusikia na kuamini injili njema ya maji na Roho.
 

Ni maneno gani ya kweli yatuwezeshayo kuzaliwa upya?

Kwanini mwanadamu azaliwe upya? Mwanadamu si mkamilifu hivyo umembidi kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu ili aweze kuzaliwa upya akiwa mwana wa Mungu. Tunaweza kuona watu wengi wanao mwamini Yesu lakini hawana uwepo wa Roho Mtakatifu. Nikodemo alikuwa ni kiongozi wa Wayahudi. Nikodemo anaye onekana katika Yohana sura ya 3 alikuwa ni msayuni aliye jaribu kuishika sheria aliyopewa na Mungu. Hata hivyo alikuwa akitumika kama kiongozi wa dini ya watu, huku akishindwa kutambua juu ya uwepo wa Roho Mtakatifu.
Ili kuweza kupokea uwepo wa Roho Mtakakatifu, imetulazimu kuiamini injili njema ya maji na Roho Mtakatifu na kuishi kwa imani. Mwanadamu ataweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu pale tu atakapo kuja kuamini maneno ya kweli katika injili njema ya maji na Roho Mtakatifu. Yesu alisema “ikiwa nimeawaambia maneno ya duniani wala hamsadiki mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?” (Yohana 3:12).
Injili njema ya maji na Roho ni kama ifuatavyo: Bwana wetu alizaliwa hapa duniani alibatizwa na Yohana akiwa na umri wa miaka 30, baada ya miaka mitatu alikufa msalabani, alifufuka na hivyo alitukomboa tokana na dhambi zetu zote. Amekuwa mwokozi kwa wale wote wenye kuamini juu ya haya yote. Amewatunukia msamaha wa dhambi na uwepo wa Roho Mtakatifu kwa wale wote wanao iamini injili njema.
Wale ambao bado wanadhambi mioyoni mwao imewapasa kupokea msamaha wa dhambi zao kwa kuamini ubatizo huo wa Yesu na damu yake. Mwanadamu hawezi kamwe kujizuia kutenda dhambi mbele ya Mungu, na hivyo ina mlazimu kuokolewa kwa kumkubali Yesu kuwa Mwokozi wake. Yesu amesafisha dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya injili njema ya majina Roho. Wenye dhambi wote wataweza kuokolewa kwa kusikiliza na kuiamini injili njema ya maji na Roho. Wale wote wenye kuamini injili njema hubarikiwa na uwepo wa Roho Mtakatifu.
“Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani hivyo ndivyo Mwana wa Adamu hanabudi kuinuliwa” (Yohana 3:14). Katika Agano la Kale, ingawa watu wa Israeli walitenda dhambi nakugongwa na nyoka wenye sumu kali kule jangwani na kufa bila tumaini bado wengi walimudu kuishi kwa kuitazama ile sanamu ya nyoka wa shaba iliyo simikwa.
Vivyo hivyo nasi pia tunauwepo wa Roho Mtakatifu. Yesu ametupa uwepo wa Roho Mtakatifu kwa wale wanao amini injili njema. Shetani hutuwekea vikwazo katika kuifuata injili njema ya maji na Roho na kujaribu kutuzuia kumpokea Roho wa kweli. Hata hivyo Mungu alitubariki na msamaha wa dhambi na uwepo wa Roho Mtakatifu kwa kupitia imani katika injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake.
Utaweza pia kupoea uwepo wa Roho Mtakatifu ikiwa utaamini injili njema. Je, unaikubali injili hii njema kama ni ukweli mbele ya Mungu? Je, unaamini kwamba unaweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa kuamini injili njema?
Bwana ametuambia tuijue kweli inayo tuokoa tokana na dhambi zetu zote “Tena mtafahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). Je, unaufahamu ukweli wa injili njema ambayo hutuokoa na kutubariki kwa uwepo wa Roho Mtakafitu? Ikiwa utaikubali injili hii hakika utaweza kupokea uwepo huo wa Roho Mtakatifu.