Search

Mahubiri

Somo la 8: Roho Mtakatifu

[8-20] Mtu aliye na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake ndiye aongozaye wengine katika kumpokea Roho Mtakatifu (Yohana 20:21-23)

(Yohana 20:21-23)
“Basi Yesu akawambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapelekea ninyi. Naye akisha kusema hayo akawavuvia akawaambia, pokeeni Roho Mtakatifu wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote matakao wafungia dhambi wamefungwa.”
 

Ni mamlaka gani Bwana
Aliwapa wale wote wenye haki?
Aliwapa mamlaka ya kusamehe dhambi
za yeyote kwa njia ya Injili 
ya maji na Roho.

Yohana sura 20 inahabari ya ufufuko wa Yesu. Bwana wetu alifufuka tena toka kifoni na kuwaeleza wafuasi wake “Pokeeni Roho Mtakatifu”. Wafuasi wa Yesu walipokea uwepo wa Roho Mtakatifu kama zawadi toka kwake. Yesu alitoa uwepo wa Roho Mtakatifu na uzima wa milele kwa wale wote wanaoamini ubatizo wake na damu yake iliyo safisha dhambi zao zote. Biblia inasema kwamba ubatizo wa Yesu ni mfano wa wokovu ambapo ubatizo huo uliokoa wanadamu wote kwa dhambi zao (1 Petro 3:21).
 

Kwa nini Yesu alibatizwa?

Kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana? Jibu la swali hili litaweza kuonekana wazi toka kile Yesu alichosema katika Mathayo 3:15 “Hivi ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote”. Hapa neno “Hivi ndivyo” maana yake Yesu alichukuwa dhambi zote za ulimwengu pale alipo batizwa. Ubatizo wake ulifanyika kwa namna ile ilivyo kuwa tendo la kuwekea mikono kuliko fanyika katika Agano la Kale. Dhumuni la ubatizo wake lilikuwa ni kumtwika dhambi zote za ulimwengu.
Nini maana ya neno “haki yote”? Neno “ipasavyo” lina maana gani? “Haki yote” maana yake ilimpasa Yesu kuzichukua dhambi zote za ulimwengu kwa njia ya ubatizo wake. Na neno “Ipasavyo” linamaana kwamba kwa jinsi hii ndivyo ilivyo sahihi na njia sawia mbele ya macho ya Mungu.
Yesu alichukua dhambi zote za wanadamu kwa njia ya ubatizo wake na kuzifutilia mbali kwa kila amwaminiye. Yesu alibatizwa na kusulubiwa kwa hukumu ya dhmbi zao. Hii ndiyo Injili ya ondoleo la dhambi. Haki ya Mungu ni ondoleo la dhambi ambalo lilifuta dhambi zote za wenye dhambi.
Ikiwa watu wataelewa maajabu ya ubatizo wa Yesu kama ilivyo andikwa katika Mathayo 3:13-17 basi wataweza kupokea ondoleo la dhambi na pia kumpokea Roho Mtakatifu. Kila Yesu alichoweza kufanya katika huduma yake ya wazi ni kubatizwa, kusulubiwa na kufufuka. Ni katika kutupatia njia ya haki kuelekea wokovu, kama ulivyoletwa na Mungu. Kwa njia hii Yesu amekwisha kuwa Mwokozi wetu wa kweli kwetu sisi wenye dhambi. Injili ya ubatizo wake na damu yake ndiyo wokovu ambao ulitakasa dhambi zetu zote.
Watu wataweza kumpokea Roho Mtakatifu ikiwa tu wataijua na kuiamini Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake, kwa sababu ubatizo wa Yesu ulibeba dhambi zetu zote ulimwenguni kwa kumtwika. Kifo chake msalabani kilikuwa ni kwa niaba ya wanadamu wote na ndicho kifo changu pia. Ufufuko wake nao ndiyo ufufuko wangu. Kwa jinsi hii ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani ndiyo Injili ya ondoleo la dhambi na kupokea Roho Mtakatifu.
Natumaini utajifunza somo la ubatizo wa Yesu na kuwa na imani nalo na ndipo dhambi zako zitakapofutwa na kumpokea Roho Mtakatifu. Kwa nini Yesu alibatizwa? Ilikuwa ni kubeba dhambi zote za ulimwengu “Hivi ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15) Amina Haleluya!
Nyakati hizi, baadhi huamini kwamba kunena kwa lugha ndiyo ishara tosha ya kumpokea Roho Mtakatifu. Hata hivyo, uhakika wa kweli juu ya hili ndiyo imani ya thamani katika Injili njema ambayo imeandikwa ndani ya mioyo ya wale wote walio mpokea Roho Mtakatifu bayana.
 

Bwana ametoa mamlaka ya kusamehe dhambi kwa wale wote wenye haki.

Bwana aliwapa wafuasi wake mamlaka ya kusamehe dhambi akisema “Wowote mtakao waondolea dhambi, wameondolewa na wo wote mtakao wafungia dhambi wamefungiwa” (Yohana 20:23). Hii inamana kwamba pale wafuasi wotakapo ihubiri Injili ya maji na Roho, dhambi za wale wote watakao isikiliza na kuiamini Injili hiyo zitasamehewa. Hata hivyo, hii haimaanishi kwamba wataweza kusamehe dhambi kwa yeyote bila kujali imani yao katika Injili ya maji na Roho.
Wafuasi wa Yesu wanamamlaka ya kusamehe dhambi ya yeyote kwa njia ya Injili ya maji na Roho tu. Hivyo ikiwa watafundisha kile kilicho andikwa yatupasa kuamini. Yakupasa uamini kwambaYesu Kristo amekupatia Injili ya maji na Roho ili kufuta dhambi zako zote. Hapo ndipo pekee utakapo weza kupata ondokeo la dhambi na kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Yesu pia ametupatia nguvu ya kuokoa watu wote kwa dhambi zao kwa njia ya kuihubiri Injili ya maji na Roho.
 

Nguvu ya Mtawala wa Ulimwengu

Hapo kale sehemu niliyo kuwa nikiishi, ilitupasa kupanda basi kupitia barabara isiyo ya lami. Wakati mwingine basi likikwama na abiria iliwabidi kushuka na kulisukuma kilimani. Siku moja raisi wa Korea alifika katika sherehe za uzinduzi wa mtambo wa umeme wa nguvu za mvuke na kupitia barabara hiyo. Watu walimkaribisha raisi kwa kuifagia barabara hiyo na kuweka miti kandokando pale walipo pata habari ya kuja kwake. Siku ilipowadia, piki piki ziliongozana njiani nyuma yake akifuatiwa raisi ndani ya gari lake. Umati wa watu ulijitokeza kumlaki wakiwa na bendera za taifa mikononi. Ilisemekana kwamba raisi alilalamika akisema, “Barabara hii ina mashimo sana inahitajika kuwekewa lami” Siku chache baadaye barabara hiyo iliwekwa lami.
Nini kilicho tokea hapa? Lalamiko moja tu la raisi lilitosha badiliko hili kubwa la hali ya barabara. Amri ya raisi inayo nguvu kubwa. Hata hivyo, tunafahamu vyema kwamba injili ya maji na Roho tuliyo pewa na Kristo ni zaidi ya nguvu. Yatupasa kuiamini injili hii ambayo ndiyo yenye nguvu katika kutuweka huru kwa dhambi zetu zote maishani.
 

Mamlaka ya kweli katika kusamehe dhambi.

“Wote mtakao waondolea dhambi, wameondolewa nao wote mtakao wafungia dhambi wamefungiwa.” Wafuasi wa Yesu waliihubiri injili ambayo dhambi zao zote zili samehewa kwa walio isikiliza na kuiamini. Wali waambia watu “Yesu amekwisha zifuta dhambi zenu zote ulimwenguni kwa njia ya ubatizo wake na damu yake. Msifadhaishwe na lolote ingawa hatima yenu ilikuwa ni kutenda dhambi hata mbeleni, tayari Yesu alikwisha zichukua dhambi zenu za kila siku na kumwaga damu yake mslabani baada ya kubatizwa na Yohana. Yesu amewaokoa! Yakupasa muamini hili!”
Wenye dhambi wamepewa ukombozi kwa kuisikia na kuiamini Injili ya maji na Roho kwa kupitia wafuasi wa Yesu. Yesu aliwapa wafuasi wake mamlaka ya kusamehe dhambi kwa njia ya maji na Roho. Kwa kuwa wafuasi hao waliihubiri Injili ya maji na Roho kwa watu wote ulimwenguni basi walioamini waliweza kupokea ondoleo la dhambi. Yesu aliwapa karama hii pamoja na mamlaka ya kusamehe dhambi.
Watu wengi wamekwisha soma vitabu nilivyo kwisha chapisha hapo awali, na tayari wamekwisha okolewa kwa dhambi zao baada ya kuvisoma. Baadhi wamekiri kwamba wamegundua sababu ya kifo cha Yesu pale msalabani ilikuwa ni matokeo ya ubatizo wake uliobeba dhambi za ulimwengu huku waki nukuu “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu” (Isaya 53:5).
Baada ya ufufuko wake Yesu alisema “Pokeeni Roho Mtakatifu wowote mtakao waondolea dhambi wameondolewa na wo wote mtakao wafungia dhambi wamefungua” (Yohana 20:22-23). Tuliishi kwa mfadhaiko, utupu mioyoni na dhambi kabla ya kuaamini ukweli huu. 
Hata hivyo sasa tunayo imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake na tupo huru kwa dhambi. Nasi inatulazimu kuihubiri Injili hii kwa wengine. Zaidi ya yote, Bwana wetu aliwapa wafuasi wake amani. Aliwapa amani na baraka ya Roho Mtakatifu pia ili tuweze kupokea amani na Roho Mtakatifu toka kwa Mungu. Yatupasa kwanza kupokea ondoleo la dhambi kwa kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake msalabani.
Kile kituwekacho huru kwa dhambi ni Injili ya maji na Roho. Hii ndiyo imani ya kiroho ambayo hutupatia baraka za mbinguni. Lakini baraka isiyo rasmi itokanayo na msingi wa mawazo ya kibinadamu hupelekea uharibifu kwake. Yatupasa kutafuta ukombozi kwa kuamini Injili ya maji na Roho na hivyo kuweza kumpokea Roho Mtakatifu. Ili kuwa na imani hii ni lazima kutupilia mbali mawazo ya kidunia na kugeuza imani yetu kuielekea Injili ya maji na Roho.
Ili tuweze kuwa na imani inayo hitajika katika kumpokea Roho Mtakatifu mtu inamlazimu kuikubali Injili ambayo Yesu alibatizwa na kusulubiwa kwa ajili yetu sote. Bwana ametupatia ondeleo la dhambi amani na uwepo wa Roho Mtakatifu kwa sababu tunaamini Injili ya maji na Roho. Aliwapa wafuasi wake uwepo wa Roho Mtakatifu na mamlaka ya kusamehe dhambi kwa yeyote anaye amini Injili ya maji na Roho.
Tunapokea pia Roho Mtakatifu kwa kuiamini Injili hii. Injili ya maji na Roho inewasaidia wengi katika kufanya hivyo. Tunapo ihubiri Injili hii kwa majirani zetu na kwa ulimwengu wote watakao ichukulia moyoni wataweza kumpokea Roho Mtakatifu. Ikiwa Injili tunayo ihubiri haitowezesha watu kumpokea Roho Mtakatifu basi si Injili ya kweli. Kwa upande mwingine ikiwa Injili tunayo iamini itawezesha watu kumpokea Roho Mtakatifu, hakika hiyo ndiyo Injili ya kweli.
Kwa jinsi gani imetupasa kubarikiwa na kushukuru kwa kuwa na Injili hii. Injili ambayo tuliyo ihubiri mimi na wewe ndiyo Injili sahihi na iliyo tukuzwa, lakini kwa bahati mbaya ni vigumu kumpata mtu anaye ifahamu na kuiamini katika nyakati hizi. Hivyo inatupasa kuihubiri kwa bidii ulimwenguni pote na imetubidi kusaidia watu katika kumpokea Roho Mtakatifu.
 

Wale walio danganyika na shetani katika kuikana Injili ya maji na Roho.

Tunawasaidia hata wale ambao tayari walikwisha mwamini Yesu wengi wao bado hawajampokea Roho Mtakatifu ingawa wamemwamini Yesu. Hivyo tunawasaidia kwa kuwahubiria Injili na hivyo kuwaongoza katika kumpokea Roho Mtakatifu.
Ikiwa mtu bado hajampokea Roho Mtakatifu ingawa ana mwamini Yesu panaweza kuwepo na matatizo katika imani yake. Ni wale tu ambao wamekwisha kumpokea Roho Mtakatifu kwa njia ya imani katika Yesu ndiyo watakao weza kuchukuliwa kuwa ni watu walio na imani ya kweli. Hivyo imetupasa sote kuwa na imani inayo tuwezesha kumpokea Roho Mtakatifu. Yatupasa kuijua Injili ya maji na Roho kwa sababu ndiyo ukweli pekee katika Injili utakao weza kutupa Roho Mtakatifu.
Tunaihubiri Injili ya maji na Roho ili kwamba wengine waweze kumpokea Roho Mtakatifu. Hata hivyo wale wanaoihubiri Injili hii wanalazimika kukutana na taabu nyingi maishani. Baadhi ya wakrisho hudhani wataweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuweka jitihada zao binafsi kwa muda mrefu. Watu hawa hukumbana na matukio mengi ya kuchanganyikiwa ambayo hayahusiani kabisa na swala la kumpokea Roho Mtakatifu. Kwa aina hii ya watu inahitajika muda mwingi na kujitolea ili kuweza kuwabainishia kwa njia ya Injili ya maji na Roho.
Ni nani basi asingeamini Injili ya maji na Roho ikiwa kila mtu angedhani kwamba mtu aweza kupokea Roho Mtakatifu kwa njia ya imani katika Injili hii? Shetani ndiye anaye walaghai watu kwa njia tofauti kabla ya Injili ya kweli kuwafikia. Watu aina hii hushangaa na kuona ni kipi zaidi katika kuamini ikiwa tayari wamekwisha jichukulia kwamba wao nao wanaimani katika Injili ya Yesu. Hivyo matokeo yake kuikana na kuikataa Injili ya maji na Roho.
Watu wengi nyakati hizi na miaka hii hawakubali ujumbe wa Injili ya maji na Roho, kwa kuwa shetani amekwisha wapofusha. Matokeo yake hudhani kwamba kumwamini Yesu ni kazi rahisi tu. Hata Injili hii si jambo rahisi hivyo. Injili ya kweli ya maji na Roho imewekewa pazia la Injili ya uongo. 
Watu wanafikiria kuwa kuna mtu yeyote anaweza kuingia katika Ufalme wa Mbingu ikiwa wataenda kanisani na wanadai kwamba wana mwamini Yesu. wengi wanaamini kuwa kuishi na Roho Mtakatifu hupewa kupitia juhudi zao wenyewe, kama vile kuomba na kufunga. Walakini, imani kama hizo ni mbali na ukweli wa kupokea Roho Mtakatifu. Wanadhani kwamba kunena kwa lugha na miujiza mingine ni ishara za kumpokea Roho Mtakatifu.
Hivyo ni vigumu kwao kuelewa kwamba ili kuweza kumpokea Roho Mtakatifu ni muhimu kuamini injili ya kweli ya maji na Roho. Hata hivyo Biblia inasema kwamba mtu ataweza kumpokea Roho Mtakatifu ikiwa tu ataamini neno la Mungu. Mungu ameficha maajabu ya kumpokea Roho Mtakatifu ndani ya maneno yake.
 

Wale wanye kuhitaji uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yao.

Siku moja nilikwenda Taiwan nikiwa na baadhi ya watenda kazi wetu. Watu wa huko walituomba vitabu vinavyo husu Roho Mtakatifu. Hivi ndivyo pia ilitutokea tukiwa Japan na Urusi. Sababu ya watu wengi kuhitaji vitabu juu ya uwepo wa Roho Mtakatifu ni kwamba, watu wa nyakati hizi wana hamu na kiu ya kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Wengi huamini juu ya Yesu na wakati mwingine hawana uhakika ikiwa kweli wamekwisha mpokea Roho Mtakatifu, kwa sababu hawana uwepo wa Roho Mtakatifu.
Wapo watu wengi wanao mwamini Yesu na kudai kwamba wamekwisha mpokea Roho Mtakatifu. Hata hivyo watu waliokwisha mpokea Roho Mtakatifu moja kwa moja kwa kudumu milele ni wachache. Watu wengi hawawezi kufikia hili ingawa wana mwamini.
Kati ya wakristo wa ulimwenguni wapo wengi wanaodhani wamekwisha kuwa na Roho Mtakatifu. Baadhi utawasikia wakisema kuwa wanakutana na Yesu katika ndoto na baadhi hudai kuwa wanaye Roho Mtakatifu ndani yao kwa sababu eti wameweza kukemea pepo. Kwa jinsi hii basi, wapo wengi ambao imani zao zimejengwa katika msingi wa matukio yao binafsi. Hata hivyo nadra sana kwa watu wa aina hii kuweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa imani ya Injili ya maji na Roho.
Hapo mwanzo nilishangaa kuona kwamba hakuna vitabu vyovyote hapa duniani vinavyoelekeza juu ya kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa njia ya imani ya Injili ya maji na Roho. Watu wengi wamebaki kuzungumzia matukio yao binafsi na Roho Mtakatifu, lakini kwa nini hakuna vitabu vinavyo husu neno la kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu? Vitabu vya aina hii ni vigumu kupatikana ingawa utavitafuta kwa marefu na mapana ulimwenguni pote.
Wale wote wanao sisitiza kimakosa kwamba wamekwisha mpokea Roho Mtakatifu hudai kuwa wamekwisha tokewa hata na Yesu mwenyewe binafsi na wamekwisha tembelea Ufalme wa Mbinguni na kupaona motoni kwa ndoto na maono. Husisitiza kwa kusema wameambiwa “Umekuja huku mapema kabla ya muda wako. Umeacha mengi katika kuyakamilisha huko duniani kwenu, hivyo haraka sana rudi uliko toka”. Matukio ya aina hii si rahisi kabisa kutokea, ataweza kweli kuwa ni Yesu wa kweli? Je Yesu angeweza kweli kukutana nao huku wakiwa bado wana dhambi mioyoni mwao? Je Yesu kweli hushikamana na wenye dhambi?
Ni kweli kwamba Wakristo wengi nyakati hizi hawana uwepo wa Roho Mtakatifu ingawa wanajaribu kujiwekea kiwango cha imani ya juu kwake. Hivyo sisi tulio na Roho Mtakatifu imetupasa kueneza Injili ambayo itawapelekea wengine kuweza kupokea karama ya Roho Mtakatifu toka kwa Mungu.
Yatupasa sisi sote kumshukuru na kumsifu Bwana kwa kutupatia Injili ya maji na Roho. Nimekwisha kuwa na furaha ya Roho Mtakatifu wakati anapodumu nami katika kuandika kitabi hiki. Wakati kitabu hiki kinachapishwa wengi mtapokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa njia ya imani zenu katika Injili ya maji na Roho “Je mlimpokea Roho Mtakatifu mlipo amini?” (Matendo 19:2) alisema Paulo kwa wafuasi watarajiwa katika Efeso.
Lazima sote tumpokee Roho Mtakatifu. Wakristo ulimwenguni pote wanahamu ya kumpokea Roho Mtakatifu katika nyakati hizi za mikanganyiko ya historia ya dunia. Nahubiri njia ya kibiblia namna ya kumpokea Roho Mtakatifu, kama Roho Mtakatifu aniongozavyo kufanya hivyo. Ili kuishi maisha yenye kuridhika lazima uamini ukweli wa uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako kwani hii ndiyo nafasi yako ya mwisho katika kumpokea Roho Mtakatifu moyoni mwako.
Najisikia msukumo mkubwa katika kueneza Injili ambayo itamsaidia kila mmoja kuweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa sababu Yesu Kristo amenipatia Injili ya maji na Roho na kunijaza karama ya Roho Mtakatifu.
 

Watu wa Mataifa nao lazima wawe na imani katika Injili ya maji na Roho.

Biblia inahusisha namna wafuasi wa Yesu walivyoweza kuwasabishia watu wengine kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Hata watu wa mataifa nao iliwapasa kuwa na imani sawa na ile ya wafuasi wa Yesu ili nao waweze kumpokea Roho Mtakatifu. Zaidi ya yote, watu wa Mataifa kwa nafasi yao walihitajika kuwa na imani ya Injili ya maji na Roho ambayo mitume walikuwa nayo ili waweze kuingia katika ulimwengu wa Mungu. Hivyo sisi tulio watu wa mataifa yatupasa pia kuamini Injili ya kweli ili tuweze kumpokea Roho Mtakatifu. Mungu alimtuma Petro kwenda kwa Kornelio ambaye alikuwa ni mtu wa Mataifa ili kwamba aweze kupokea nuru ya Injili ya maji na Roho, ambayo ni muhimu kwa ajili ya kumpokea Roho Mtakatifu.
Wayahudi wanao amini walishangaa kusikia kwamba karama ya Roho Mtakatifu pia ilishushwa hata kwa watu wa mataifa. Petro alipo rudi katika kanisa la Yerusalemu baada ya kuihubiri Injili ya maji na Roho, wote walio kwisha kutahiriwa walimpinga wakisema “Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao” (Matendo 11:3) lakini Petro alielezea yote toka mwanzo hadi mwisho.
Maelezo yake kwa kina yamo katika Matendo 11:5-17, “Nalikuwa katika mji wa Yafa nikiomba roho yangu ikazimia nikaona maono; chombo kinashukua kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia. Nikakitazama sana nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne na wa angani. Ni kasikia na sauti ikiniambia ondoka Petro ukachinje ule, nikasema, Hasha Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijaingia kabisa kinywani mwangu. Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni. Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi. Jambo hili likatendeka mara tatu kisha vitu vyote vikavutwa tena juu mbinguni. Na tazama mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyo kuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisare. Roho akaniambia nifuatane nao nisione tashwishi, Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami tukaingia katika nyumba ya mtu yule akatuelekeza jinsi alivyo mwona malaika aliyesimamia nyumbani mwake na kumwambia. Tuma watu kwenda Yafa akamwite Simoni aitwaye Petro atakaye kuambia maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote. Ikawa nilipoanza kunena Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo. Nikalikumbuka neno lile la Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?” 
Petro alisema kwamba, hakwenda katika nyumba ya wasio tahiriwa kula tu bali pia aliwaeleza juu ya Injili ya shukrani kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu na waliposikia mambo haya walinyamaza kimya, na kumtukuza Mungu aliye wapa toba na uzima kwao wote - Kornelio, jamaa yake na watu wa karibu yake.
 

Injili ya Kitume kwa ajili ya kumpokea Roho Mtakatifu.

Upi uliokua mkakati mkuu 
wa Mitume?
Kuihubiri injili ya maji na Roho ili 
watu waweze kumpokea 
Roho Mtakatifu.

Je ni kweli Mitume waliihubiri Injili ya maji na Roho? Yatupasa kwanza kupata uhakika endapo Mtume Petro alikuwa akiamini Injili ya maji na Roho. Katika Biblia Petro alisema “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi” (1 Petro 3:21). Mtume Petro kwa uwazi alikuwa akiamini kwamba Yesu aliokoa wenye dhambi na dhambi zao kwa ubatizo wake na kifo chake pale msalabani, pia aliamini kwamba wakati Yesu alipobatizwa (Mathayo 3:15) dhambi zote zilitwikwa juu yake, hivyo alisulubiwa na hatimaye kufufuka ili kutuokoa sisi sote.
Nyakati hizi wapo watu walio na imani kama hii ya Petro. Wale wenye kuhubiri Injili ya maji na Roho ni wale wenye kuihubiri Injili aliyo ihubiri Petro. Ukweli huu unatosha kabisa kuwezesha wanao usikiliza kuweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu.
Kama ilivyo kwa watu wengi walivyo mpokea Roho Mtakatifu wakati Petro alipo hubiri Injili ya maji na Roho, nasi pia tunawaona watu wenye kuiamini Injili hii na kuweza kumpokea Roho Mtakatifu pale tunapo hubiri ukweli ule ule. Mtu kamwe hampokei Roho Mtakatifu kwa kuamini atakavyo au kwenda mbinguni ikiwa ana mwamini Yesu kuwa ni Bwana tu, bali kwa kuamini Injili njema ya maji na Roho.
Petro wakati mmoja aliwachukulia watu wa Mataifa kwa hadhi ya chini akidhani walikuwa sawa na wadudu watambaao tu kulingana na sheria ya Torati. Walikuwa sawa na wanyama najisi mbele ya Yesu kabla hajabatizwa kufa msalabani na kufufuka. Hata hivyo, hao watu wa mataifa waliweza kubarikiwa na uwepo wa Roho Mtakatifu kwa kuamini Injili ya maji na na Roho. Hivyo sauti ilinena na Petro ikisema “Vilivyo takaswa na Mungu usiviite wewe najisi” (Matendo 10:15).
Sisi tukiwa watu wa Mataifa hatukuweza kumpokea Roho Mtakatifu, lakini leo hii tutaweza kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu kwa kuwa na imani ya Injili ya maji na Roho. Tunapoihubiri Injili kwa subira ya wale walio jawa na fikra zao, mara nyingi tunaweza kuwaona baadaye wanakuja kuiamini injili hiyo na hatimaye kumpokea Roho Mtakatifu. Tunaweza kuwasikia pia wakikiri kwamba hawana tena dhambi mioyoni mwao baada ya kuamini ubatizo wa Yesu na damu yake. Hapo ndipo Roho Mtakatifu anapo weka makazi ndani yao.
Lengo letu kuihubiri Injili si kuwafanya watu waielewe tu bali kuwaongoza katika kumpokea Roho Mtakatifu. Ukweli kuwa wale wenye kuamini Injili tunayo ihubiri hupata msamaha wa dhambi zao zote ndiyo muhimu zaidi. Na ukweli wa kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu wakati huo ni muhimu zaidi. Hatuihubiri injili kwa watu wa dunia hii tu bali pia kuchukua hatua moja mbele na kuwaongoza katika kumpokea Roho Mtakatifu kwa wakati mmoja.
Yatupasa kuibubiri Injili ya maji na Roho katika mtazamo huu kwa wale wenye uhitaji wake. Ikiwa tutasinyaa baada ya kuihubiri Injili hii, maana kamili ya juhudi yetu itapotea. Yatupasa kuwa makini kwamba Injili hii ndiyo ipelekayo watu kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Tunapo ihubiri Injili huku tukiwa na mawazo haya, cheche za Roho Mtakatifu zitasambaa kama moto msituni duniani pote.
Mwinjilisti anapoamini kwamba Injili hii itaweza kuongoza watu wa dunia kumpokea Roho Mtakatifu, hugundua ya kwamba huduma hii si kuhusiana na kushawishi watu kumwamini Yesu Kristo tu bali ni kuwaongoza katika kumpokea Roho wakati huu.
Mtu anapaswa kusikia kwa masikio yake na kuiamini kwa moyo wake wote Injili tunayo iamini ili kuweza kumpokea Roho Mtakatifu. Kwa uwazi Injili tunayo ihubiri ina gusa maisha ya watu. Nguvu ya Injili ni mamlaka na baraka inayo tolewa na Mungu.
Petro alikuwa ni mwinjilisti wa Wayahudi, wakati Paulo alikuwa ni wa mataifa. Wakati Petro akiomba katika chumba cha juu, aliona mbingu ikifunuka na kitu kama kitambaa kikiwa na pembe nne kikituwa mbele yake. Juu yake palikuwa kila aina ya wanyama najisi ambao Biblia imekataza kuliwa. 
Petro hakuwahi kula kitu chochote kilicho najisi. Hata hivyo, Mungu alimwamuru achinje na kuwala Petro alikataa akisema “Hasha Bwana kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi” na sauti ikamjibu “Vilivyotakaswa na Mungu usiviite wewe najisi” Hii ina maana gain? Mungu hapa anasema, Yesu alikwisha takasa dhambi zote za ulimwengu, hata zile za watu wa mataifa pale alipo batizwa na kufa msalabani.
Kiroho amri hii ya Mungu kutaka achinje na kula wanyama hao najisi ili kuwa ni kumfundisha Petro kwamba, hata watu wa Mataifa wataweza kuwa watoto wa Mungu kwa kumwamini Yesu aliye letwa ulimwenguni, kubatizwa ili kubeba dhamba zao zote na kusulubiwa ili kuhukumiwa kwa niaba yao.
Petro alikuwa bado akifuata taratibu za sheria badala ya kuyaona haya kwa macho ya imani ya kiroho, hata baada ya kumpokea Roho. Lakini Petro alikiri kosa na kuamini kwamba Mungu tayari amekwisha safisha hata dhambi za watu wa mataifa. Petro alikuja kugundua thamani ya Injili njema kwa undani zaidi. Alishuhudia Roho Mtakatifu akiwashukia wasikilizaji pale alipo hubiri maneno ya Mungu.
Tutawezaje kutambua ikiwa wainjilisti wa nyakati hizi tayari wamekwisha kumpokea Roho Mtakatifu au la? Inategemea ikiwa wanaikubali Injili ya maji na Roho. Mtu yeyote anaye iamini Injili njema pale wakati mwinjilisti anapo hubiri maneno ya Mungu, basi atakuwa kapokea uwepo wa Roho Mtakatifu. Yule Roho Mtakatifu aliye ndani ya moyo wa mwinjilisti huja pia ndani yake na kufanya makazi. Mwinjilisti na msikilizaji wataweza kuwa na usharika kati yao kama urafiki wa kitoto. Wataweza kuona upendo wa Mungu ukiwa nao daima kati yao. 
Tunapo ihubiri Injili tunaweza kumwona Roho Mtakatifu akishuka juu ya wale wanao amini mara moja pale tu wanapo amini Injili ya maji na Roho. Hili si tukio la pembeni au baada ya wokovu. Hii ndiyo sababu ya msingi kwa nini tunaihubiri Injili ya maji na Roho. Injili tunayo ihubiri ni ile inayo wawezesha wengine kuweza kumpokea Roho Mtakatifu. 
Wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu ni watoto wa Mungu Injili ya maji na Roho si fundisho la kinadharia katika dunia na hivyo tunapo ihubiri kwa wengine wanakuja kuwa na imani, kumpokea Roho Mtakatifu na kuwa watoto wa Mungu. Ni baraka iliyoje! Na ni kazi njema iliyoje! Wale wanao ihubiri Injili hii husaidia kujenga Ufalme wa Mungu. Sisi tunacho weza ni kuibubiri Injili tu, lakini wao hupokea Roho Mtakatifu. 
Badhi ya watu hudhani kumwamini Yesu ni jambo moja na kumpokea Roho Mtakatifu ni jingine. Hivyo wakristo huomba wajazwe Roho Mtakatifu. Hata hiyo Biblia yasema kwamba Roho huyo huja juu ya wale walio isikia na kuiamini Injili iliyo hubiriwa na mtumishi wa Mungu. Injili tunayo ihubiri huongoza watu kutimiza haja za mioyo yao. Ndiyo maana tunalo jukumu la kuieneza duniani pote. Sisi ni watoto wa Baba na warithi kwake tulio waaminifu kwa agizo kuu.
Yatupasa kuihubiri Injili kwa imani huku tukiwa makini kwamba lengo letu ni kuwezesha watu kumpokea Roho Mtakatifu. Injili hii ni ile ambayo wainjilisti wote lazima waiamini kabla ya kuihubiri kwa wengine. Ndipo wasikilizaji wataweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuiamini. Kwa njia hii ndipo tunapotoa pumzi ya uzima wa milele kwa wote wenye kuimamini. Lengo letu ni kuwezesha wao wakombolewe toka nguvu za giza na kugeukia Ufalme wa Mungu. Wainjilisti ndiyo hubadilisha mwelekeo wa wenye dhambi chini yanguvu za giza kuelekea Ufalme wa Mwana wa Mungu. Ni muhimu sana hii kazi ya kubadilisha wenye dhambi kuwa wana wa Mungu.
Wengi hawajui ufunguo wa kumpokea Roho Mtakatifu na hivyo kujaribu kumpokea kwa juhudi binafsi. Hata hivyo hili litathibitisha kushindikana. Ni imani ya Injili pekee inayo hitajika, kwa kua ndiyo imwekayo huru kwa dhambi zote.
Je, wewe umempokeaje Roho Mtakatifu kwa maombi? Au labda kwa kuwekewa mikono? Hapana, hii si njia sahihi. Tunaweza kumpokea pale tunapo amini Injili ya maji na Roho. Yatupasa kusali na kuihubiri Injili ili watu wa dunia hii wampokee Roho Mtakatifu.
Neno “mtume” maana yake “mtu aliye tumwa na Mungu” Mitume hufanya kazi gani? Huihubiri Injili ya maji na Roho ili watu wapokee Roho Mtakatifu. Je utapenda kushiriki nasi kwa kazi hii? Wote yatupasa tuwe na uwepo wa Roho Mtakatifu ili tuihubiri kwa watu wote. Haleluya! Tuusifu ukweli halisi wa Injili ambayo Bwana alitupatia ili tuweze kumpokea Roho Mtakatifu.