Search

Mahubiri

Somo la 11: Maskani

[11-20] Madhabahu Ya Uvumba (Kutoka 30:1-10)

Madhabahu Ya Uvumba
(Kutoka 30:1-10)
“Nawe fanya madhabahu ya kufukizia uvumba; utaifanyiza kwa mti wa mshita. Urefu wake utakuwa dhiraa moja, na upana wake dhiraa moja; itakuwa mraba; na kwenda juu kwake dhiraa mbili; pembe zake zitakuwa za kitu kimoja nayo. Nawe utaifunikiza dhahabu safi juu yake, na mbavu zake kando kando, na pembe zake; nawe utaifanyia ukingo wa dhahabu kuizunguka. Kisha utaifanyia pete mbili za dhahabu, chini ya ukingo wake katika mbavu zake mbili, katika pande zake mbili utazifanya; nazo zitakuwa mahali pa kuitia miti ya kuichukulia. Na ile miti utaifanya kwa mti wa mshita, na kuifunikiza dhahabu safi. Nawe utaitia mbele ya lile pazia lililo karibu na sanduku la ushuhuda mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, hapo nitakapokutana nawe. Na Haruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza. Na Haruni atakapoziwasha zile taa wakati wa jioni, ataufukiza, uwe uvumba wa daima mbele za Bwana katika vizazi nyenu vyote. Hamtafukiza juu yake uvumba mgeni, wala sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, wala hatamimina juu yake sadaka ya kinywaji. Naye Haruni atafanya upatanisho juu ya pembe zake mara moja kila mwaka; kwa damu ya ile sadaka ya dhambi ya kufanya upatanisho, mara moja kila mwaka ataifanyia upatanisho, katika vizazi vyenu vyote; ni takatifu sana kwa BWANA.”
 
 
Madhabahu Ya Uvumba

Madhabahu ya Uvumba Palikuwa ni Mahali pa Maombi

 
Madhabahu ya uvumba ilitengenezwa kwa mti wa mshita, na ilikuwa na umbo la mraba ikiwa na vipimo vya dhiraa (sentimita 45: futi 1.5) kwa urefu na upana wake na ilikuwa na kimo cha dhiraa 2. Hali ikiwa imewekwa ndani ya Mahali Patakatifu, madhabahu hii ilifunikwa kwa dhahabu sehemu zote hali ikiwa na ukingo wa dhahabu kuizunguka. Pete nne za dhahabu ziliwekwa chini ya ukingo huo ili kuweza kuishikilia ile miti ya kubebea sanduku hilo. Katika madhabahu hii ya uvumba, hakuna kitu kingine chochote kilichoruhusiwa zaidi ya mafuta ya upako na uvumba wa manukato (Kutoka 30:22-25). 
Madhabahu ya uvumba palikuwa ni mahali ambapo uvumba wa maombi ulitolewa kwa Mungu. Lakini kabla hatujaomba katika madhabahu ya uvumba, ni lazima tutazame kwanza ikiwa tunastahili kumwomba Mungu katika madhabahu hii au la. Yeyote anayetaka kustahilishwa ili aweze kumwomba Mungu mtakatifu ni lazima kwanza awe hana dhambi kwa kuzioshelea mbali dhambi zake kwa imani. Ili kufanya hivyo ni lazima mtu asafishwe dhambi zake zake kwa imani ya sadaka ya kuteketezwa na ile ya birika la kunawia. 
Mungu hayasikilizi maombi ya wenye dhambi (Isaya 59:1-3). Kwa nini? Kwa sababu Mungu anawapokea wale tu ambao wameoshwa dhambi zao zote kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Kwa sababu Mungu amezioshelea mbali dhambi zetu zote kwa ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa meneno mengine, Mungu anapendezwa kusikia maombi ya wenye haki tu (Zaburi 34:15, 1 Petro 3:12). 
 
 
Asili na Ukweli wa Wanadamu Wote
 
Tunapotazama kwa karibu, tunaona kuwa wanadamu wote tukiwemo mimi na wewe, kimsingi tulizaliwa na mbegu ya dhambi, na kwa hiyo ndio maana wote wanafanya dhambi. Kila mtu yeyote ni mbegu ya mtenda maovu. Kwa sababu watu walizaliwa kwa asili wakiwa na dhambi, basi watu hao hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kuishi maisha yao hali wakitenda matendo maovu. Hebu fikiria kuhusu wewe mwenyewe bila kujalisha kuwa wewe ni nani. Tunaweza kukiri mbele za Mungu kuwa tumekuwa ni waovu ambao tusingeweza kukwepa kutupwa kuzimu. Zaidi ya yote, tunapoyahukumu matendo yetu mbele za Mungu, ndipo tunapotambua kuwa kwa mujibu wa sheria ya Mungu inayosema mshahara wa dhambi ni mauti, basi tunaona wazi kuwa hatuwezi kufanya lolote ili kuikwepa hukumu yake ya haki kwa dhambi. 
Kwa sababu kile kinachotoka ndani ya mioyo ya wanadamu ni mawazo mabaya, uuaji, uzinifu, majivuno na ujinga, na mambo kama hayo, basi mara nyingi watu wanatenda mambo kama haya wanapopata nafasi (Marko 7:21-27). Je, inawezekanaje kwa mioyo ya wanadamu ambao kimsingi walizaliwa kama mbegu ya watenda maovu na ambao hawawezi kufanya loote zaidi ya kutenda dhambi pale mazingira na fursa zinaporuhusu kuwa na aibu mbele za Mungu? Kwa kweli haiwezekani kwa kuzitegemea jitihada za mwanadamu. Lakini kuna imani moja tu pekee ambayo inakuruhusu kutokuwa na aibu mbele za Mungu, na imani hiyo ni hii hapa. Sisi sote ni lazima tutambue na kuamini katika ukweli ulioundwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, ukweli ambao unatuwezesha sisi kuoshwa dhambi zetu zote na kusimama mbele za Mungu pasipo kuwa na aibu. Kwa hiyo, sisi sote tunaihitaji injili ya maji na Roho kikamilifu. 
Hakuna kati yetu anayeweza kuukana ukweli kuwa sisi sote tulikwisha fungwa kwenda kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu. Na kwa wale wanaotambua mbele za Mungu kuwa walifungwa kwenda kuzimu, basi si vigumu kwao kuamini katika mioyo yao juu ya wokovu ambao Mungu amewapatia. Tunapokutana na Mungu hali tukiwa na ukweli na unyenyekevu, basi hatuwezi kuificha mioyo yetu mbele zake kwa udanganyifu, na kwahiyo ndipo tunapokuja kuikubali haki ya wema wa Mungu. Kila mtu amepangwa katika mahali ambapo hawezi kukwepa zaidi ya kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake kwa hukumu ya haki ya Mungu. 
Sheria ya haki ya Mungu inayotangaza kuwa mshahara wa dhambi ni mauti si sheria ambayo wenye dhambi wote wanaweza kuikwepa kwa kuizunguka kwa kutegemea mawazo yao binafsi na imani zao za kidini. Kwa sababu Sheria ya Mungu ni ya kina, kamilifu, na ya haki, basi sheria hiyo inamlazimisha kila mtu anayesimama mbele ya sheria hiyo kukiri kuwa amepangiwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zake. Wenye dhambi wanafikia hatua ya kutambua kuwa hawawezi kuikwepa hukumu ya Mungu hata kwa zile dhambi ndogo wanazozitenda. 
Kwa hiyo, tunahitaji Mwokozi anayetuokoa sisi sote toka katika dhambi na ni sharti tumtafute Mwokozi huyu kuwa ni nani. Huyu ni Yesu Kristo, Mwokozi wa wanadamu wote. Yeye ni Mwokozi aliyekuja hapa duniani akabatizwa na Yohana ili kuzichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake, ambaye alibeba adhabu ya maovu yote ya wenye dhambi kwa kusulubiwa na kuimwaga damu yake Msalabani, ambaye kwa jinsi hiyo ametuokoa toka katika dhambi zetu zote. 
Sisi sote tulielewa vibaya kuwa kupokea ondoleo la dhambi kunaweza kuwa ni kitu kigumu sana. Kwa kweli tulifikiri kuwa tunaweza kuokolewa ikiwa tu tutaifahamu Biblia yote vizuri, au kuwa wokovu wetu unahitaji aina fulani ya matendo mema. Lakini ukweli wa wokovu uliotolewa na Mungu ulikuwa tofauti. Ukweli huu wa wokovu ulifungua na kutuonyesha njia ya kuokolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kuzichunguza dhamiri zetu mbele ya Sheria ya Mungu, kwa kuzitambua dhambi zote zinazopatikana katika mioyo yetu, na kwa kuamini katika injili ya maji na Roho. Ukweli huu ulionyeshwa kabla katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania. 
Ondoleo la dhambi la mwanadamu linatoka katika ukweli wa wokovu wa thamani uliotimilizwa kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Ni kwa kuamini katika ukweli huu ndipo watu wote wanapoweza kupokea ondoleo la dhambi la milele mara moja na kwa wote. Ili kufanya hivyo, kila mtu ni lazima atambue kuwa wote wamepangiwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zao na kuamini katika injili iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na hivyo kupokea ondoleo la dhambi zao zote mara moja. Injili ambayo Mungu ametupatia ni injili inayopatikana katika injili ya kweli inayoshikiliwa na nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. 
Wote ni lazima waamini katika injili hii ya kweli, kwa kuwa ikiwa hawataamini katika ukweli ulio ndani yainjili hii, basi hawawezi kuwekwa huru toka katika dhambi zao. Lakini wale wanaoamini katika ukweli huu wa wokovu ambao Mungu ameukamilisha kwa injili ya maji na Roho wanastahili kabisa kuokolewa toka katika dhambi zao zote na kufanyika watoto wa Mungu mwenyewe. Kwa hiyo, ili kufanyika miongoni mwa wale wanaoweza kwenda mbele za Mungu na kumwomba, basi kwanza ni lazima tuamini katika ukweli wa maji na Roho ambayo ni injili ya ondoleo la dhambi. Tunapokuwa tumeokolewa toka katika dhambi zote kwa kuifahamu injili ya kweli na kisha kuiamini katika mioyo yetu, basi hapo tutakuwa tumestahili kumwomba Mungu. Imani inayotuwezesha sisi kumwomba Mungu inapatikana kwa kuiamini katika mioyo yetu injili ya maji na Roho ambayo ni injili toka kwa Mungu. 
Ni makosa kujaribu kumwomba Mungu pasipo kuwa na imani inayofahamu na kuamini katika ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizodhihirishwa katika mlango wa kisitiri wa Hema Takatifu la Kukutania. Imani ya jinsi hiyo inaweza kusababisha kufanya dhambi ya kukufuru na kudhihaki dhidi ya Mungu. Je, inawezekanaje tukafanyika maadui wa Mungu kwa kukataa kuamini katika ukweli uliodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania ndani ya mioyo yetu? 
Unapokataa kuamini katika Yesu Kristo aliyekuja kwa kupitia ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, basi hiyo ni njia ya mkato kwako wewe kupata uadui na Mungu. Hili ni tendo la kutisha la kutokuamini ambalo linasimama kinyume na Mungu. Nafsi ambazo bado zinaendelea kufanya dhambi ya kuudharau utakatifu wa Mungu ni zile ambazo haziamini katika wokovu ambao Mungu ameutimiza kwa ajili yao bali zinaendelea kuamini kwa mujibu wa mawazo yao binafsi. Nafsi za jinsi hiyo ndizo zile ambazo zinajifunika na vazi la majani ya mzeituni liitwalo “unafiki”, na hivyo huudharau upendo wa Mungu na rehema zake. 
Lakini ni lazima utambue kuwa pamoja na kuwa watu hawa wanaweza kuidanganya mioyo yao, watu hao hawawezi kuikwepa hukumu ya Mungu. Watu wenye kutokuamini kama hao watahukumiwa adhabu ya dhambi ya kutisha na kuteseka kwa sheria ya haki ya Mungu. Kwa nini? Kwa sababu hawakufikiria kuifahamu injili ya maji na Roho ambayo kwa hiyo Bwana amezitoweshea mbali dhambi zao wala kuiamini injili hii. 
Wakati dhamiri zetu zinapokuwa chafu hata mbele ya macho yetu wenyewe, je tunawezaje basi kuzificha dhambi zetu mbele za Mungu mtakatifu? Kwa kweli hili haliwezekani! Kila mtu anayetaka kuzificha dhambi zake ataachwa nje ya upendo na rehema za Mungu. Wale wanaoidanganya mioyo yao binafsi wataishia kuwa ni watumishi waovu wa shetani ambao wanamdanganya Mungu na wanadamu wenzao. Ile dhana kuwa wanaweza kumdanganya Mungu kwa kuyapofusha macho yao huo ni mwangwi wa upotevu unaotoka katika mawazo yao machafu. Kwa kweli, wale wanaoyategemea mawazo yao binafsi ndio wale wanaoiletea changamoto injili ya maji na Roho, na ndio wale wanaotaka kuwa watumishi wa Shetani kutokana na uovu wao wenyewe. 
Watu ni lazima watambue kuwa ingawa wanaweza kuwa tayari kuidanganya mioyo yao, ukweli ni kuwa hawawezi kumdanganya Mungu. Na ni lazima wabadilishe mawazo yao ili waamini kwa mujibu wa Neno la Mungu. Je, inawezekanaje basi kila mtu akaoshelewa mbali dhambi zake pasipo kuamini katika injili ya maji na Roho? Kama ilivyoandikwa mshahara wa dhambi ni mauti, basi hakuna mwenye dhambi anayeudanganya moyo wake mbele za Mungu anayeweza kuikwepa hukumu ya Mungu. Ikiwa tutaikubali Sheria ya Mungu, basi ni wazi kuwa sisi sote tumepangiwa kuzimu kwa ajili ya dhambi zetu. Kwa hiyo, wale wote wanaotaka kumjia Mungu ni lazima waokolewe kwa kuamini katika ukweli wa injili uliodhihirishwa katika mlango wa Hema Takatifu la Kukutania. 
Hata hivyo, kwa kuwa wengi wameshindwa kuutambua ukweli kuwa watahukumiwa kwa dhambi zao, basi kwa sababu hiyo wameshindwa pia kuikubali katika mioyo yao injili ya wokovu ambayo imekuja kwa kupitia ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kama matokeo, wote hao wanaelekea kuzimu. Bila kujalisha kuwa watu hao ni Wakristo au la, wale wasioamini katika injili ya maji na Roho watakumbana na adhabu ile ile. Kwa hiyo, ni lazima tusijidanganye dhamiri zetu mbele za Mungu wetu, bali tuipokee katika mioyo yetu injili ya maji na Roho na kuikubali na kuuamini ukweli huu wa injili. 
 


Ni Lazima Tuzioshelee Mbali Dhambi Zetu Kwa Kuamini katika Neno la Ukweli

 
Watu wana dhamiri mbili: moja ni dhamiri ya mwili na nyingine ni dhamiri ya imani ikihusianishwa na injili ya ukweli. Ni lazima tuwe wakweli kuhusiana na maeneo haya mawili, lakini katika mambo haya mawili kwa kweli hatuwezi kushindwa kuwa na dhamiri ya imani ambayo inaitambua injili ya kweli. Ni lazima tuichunguze dhamiri ya imani yetu mbele ya Neno la Mungu; tuamini kwamba Yesu alizipokea dhambi zetu kwa kubatizwa, alihukumiwa Msalabani, na kwa hiyo ametuokoa sisi na kuzioshelea mbali dhambi za dhamiri zetu kwa imani hii. Inanikasirisha kuona kuwa hata pale inapofahamika kuwa huu ndio ukweli ambao hauna mpinzani bado inashangaza kuona kuwa kuna watu ambao hawaamini katika injili ya ukweli. 
Kuna utaratibu wa kiimani ili kuzisafisha dhamiri zetu. Kwanza, ni lazima tutambue na kuthibitisha ukweli kuwa sisi tumefungwa kuzimu, na pili, ni lazima tuamini katika mioyo yetu kuwa Mwokozi wetu alikuja hapa duniani, alibatizwa na Yohana kwa ajili ya dhambi zetu, alikufa Msalabani, akafufuka toka kwa wafu, na kwa hiyo ametuokoa sisi sote toka katika dhambi zetu zote. Wenye dhambi ni lazima waokolewe toka katika maovu yao na kisha wapokee uzima wa milele kwa imani yao katika injili ya maji na Roho ambayo imedhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. 
Pamoja na ukweli kuwa tunastahili kuokolewa toka katika dhambi zetu, bado kuna watu ambao hawaamini hata pale wanapolifahamu ondoleo la dhambi lililotimizwa kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Je, wanawezaje kufanya hivi? Kwa hakika ni lazima wawajibike kutokana na kutokuamini kwao. Ikiwa tungeufahamu ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu halafu tukawa hatujaamini, basi bado tungebakia kuwa ni wenye dhambi, na kama bado tungebakia kuwa ni wenye dhambi, je, tusingehukumiwa kwa mujibu wa sheria ya Mungu? Kila mmoja wetu, mwanamume au mwanamke, sote tulipaswa kuokolewa toka katika dhambi kwa kuamini mioyoni juu ya ukweli wa wokovu ambao Mungu ameutimiza kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. 
Watu ni lazima wawe na aina ya imani inayoweza kuwaokoa toka katika dhambi zao. Ni lazima wawe na imani inayoamini katika injili ya maji na Roho tu. Je, unaamini katika injili iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, ambayo inamaanisha kuwa Bwana alizibeba dhambi zetu zote kwa kubatizwa na ametuokoa sisi kwa damu yake aliyoimwaga Msalabani? Unapofikiria kuhusu wewe mwenyewe kwanza, je unakubaliana na ukweli kuwa ulipangiwa kwenda kuzimu? Je, unatambua kuwa hata pale tulipokuwa tumepangiwa kuzimu, bado Bwana alituokoa toka katika dhambi zetu kwa ukweli unaodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu? 
Ni lazima utambue kuwa Bwana alikuja hapa duniani ili kuzishughulikia dhambi zako zote, alibatizwa na kisha akaimwaga damu yake. Ili kuzitoweshea mbali dhambi zako na na zangu, Bwana wetu alikuja hapa duniani akafanyika mwili wa mwanadamu, akazipokea mara moja dhambi zote za wanadamu wote katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana katika Mto Yordani alipokuwa na miaka 30, kisha akabeba adhabu ya dhambi mara moja na kwa wote kwa kusulubiwa na kuimwaga damu yake. Mungu ameziondoa dhambi zote za wale wanaoamini mara moja. 
Tunaweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kuamini katika ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau na nyekundu. Ni lazima tuchunguze na kuthibitisha ikiwa tumeokolewa au hatujaokolewa kwa kweli toka katika dhambi zetu zote kwa ukweli huu. Ni lazima tuwe na imani inayoamini katika Yesu Kristo aliyekuja kwa nyuzi zabluu, zambarau, na nyekundu kuwa ni Mwokozi. Kama Biblia inavyosema, “Kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” (Warumi 10:10). Warumi 10:17 pia inasema, “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” 
Neno hili la Kristo linatueleza sisi kuwa tumeokolewa kwa kuamini katika wokovu uliotimizwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Ondoleo la dhambi si kitu kinachopatikana kwa kuamini kwa mawazo yetu binafsi, bali ni ni kitu kinachopatikana na kuchukuliwa kwa kuamini katika mioyo yetu katika wokovu ambao umekuja kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Imani inayoweza kutukomboa kwa kweli toka katika dhambi ni imani inayoamini katika injili ya maji na Roho. 
Je, ni lazima sasa tuombe kwa Mungu kwa kuiweka imani yetu katika ukweli huu? Kwa kweli ndivyo! Tunapaswa kutoa maombi yetu mara kwa mara katika Roho hali tukiwa tumejifunga viuno vyetu kwa ile kweli (Waefeso 6:14, 18). Lakini ukweli ni kitu gani? 
Ni injili ndiyo inayotueleza sisi kuwa Bwana wetu alikuja hapa duniani ili kutuokoa, alibatizwa na Yohana Mbatizaji alipokuwa na umri wa miaka 30, alizibeba dhambi zote za ulimwengu, alisulubiwa katika mikono na miguu yake, alitemewa mate, akaimwaga damu yake, na kwa hiyo amezioshelea mbali dhambi zetu. Ni lazima tukiri kuwa ni kwa imani yetu katika ukweli huu ndipo ondoleo letu la dhambi linapotimizwa. Bwana wetu alituokoa sisi toka katika dhambi zetu kwa kuadhibiwa kwa dhambi za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake na damu yake Msalabani. 
“Bwana, ulinipenda sana kiasi kuwa umenifanya kuwa mtoto wake Mungu.” Hivi ndivyo inavyotupasa kuikiri imani yetu. Hata wakati ule tulipokuwa na dhambi tu, Bwana wetu alitupa sifa za kutusatahilisha kuingia Ufalme wa Mbinguni kwa kuzitoweshea mbali dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo wake na kusulubiwa kwake. Ni lazima sisi sote tuamini katika ukweli huu na kisha tupokee uzima wa milele. 
Je, kuna sababu gani ya wewe kutokuamini katika ukweli huu? Kama mimi, nisingekuwa na kitu cha kusema hata kama Bwana hakubatizwa ili kuniokoa mimi toka katika dhambi zangu, na lakini kwa ajili yangu, Bwana alibatizwa, akamwaga damu yake, na kwa hiyo ameniokoa mimi toka katika dhambi zangu zote. Na kwa hiyo ninaamini! Hakuna sababu inayotufanya sisi sote tusiiamini injili hii. Ni wazi kuwa ikiwa wenye dhambi hawaamini katika ukweli wa injili ya maji na Roho, basi ni hakika kuwa watatupwa kuzimu. Lakini ninapenda kila mmoja wenu aokolewe toka katika dhambi kwa kuamini katika injili ya nyuzi za bluu, zambarau na nyekundu.
Kulikuwa na wakati ambapo mimi mwenyewe nilibakia nikiwa mwenye dhambi hata pale nilipokiri kuwa namwamini Yesu. Hali nikipenda kuwa Mkristo mzuri, nilijitahidi sana kutokuwa na aibu chini ya Mbingu. Lakini kinyume na mapenzi yangu, niliendelea kutenda dhambi kwa nyakati mbalimbali; lakini kitu pekee ambacho kilinifariji ni kuwa nilipojilinganisha na wenzangu nilijiona kuwa angalau nina nafuu kuliko wao. Hata hivyo, dhamiri yangu iliendelea kuniambia kuwa bado nilikuwa na dhambi, na kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti kwa mujibu wa sheria ya Mungu, basi mimi nilikuwa nimefungwa kwenda kuzimu kwa sababu ya maovu yangu. 
Baada ya mwongo mmoja wa maisha yangu ya taabu na kujitakia haki, basi nilijikuta kuwa nimekufa kiroho kabisa. Hata hivyo, Mungu aliniamsha kwa neema kwamba Yesu Kristo alibatizwa kwa ajili yangu na kuzibeba dhambi zangu katika mwili wake. Si kwamba alizichukua dhambi zangu tu bali na dhambi za kila mtu katika ulimwengu wote. Kisha akabeba adhabu ya dhambi hizi kwa kuzibeba Msalabani na kusulubiwa na kufa juu ya Msalaba huo, kisha akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa ni Mwokozi wangu wa kweli na aliye hai hata sasa. Nilipokuja kuifahamu injili hii ya ukweli sikuweza kufanya lolote zaidi ya kuiamini. Na kwa kuamini kuwa Yesu Kristo amefanyika kuwa Mungu wa wokovu wangu kwa kupitia ubatizo wake na damu yake aliyoimwaga Msalabani, dhambi zangu zote zimeoshelewa mbali. Nimepokea ondoleo la dhambi katika moyo wangu kwa imani. 
Si kwa sababu nililifahamu vizuri Neno la Mungu ndipo nikapokea ondoleo la dhambi bali niliondolewa dhambi zangu kwa sababu nilizifahamu dhambi za dhamiri zangu, kisha nikazipitisha dhambi hizi katika mwili wa Yesu Kristo kwa ubatizo wake, na nikaamini katika moyo wangu kuwa Yesu alihukumiwa na kuadhibiwa Msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi zangu. Ni kwa sababu nimepokea ondoleo la dhambi zangu ndio maana sasa ninaishi maisha yangu hali nikiihubiri injili. Wewe na mimi tupo sawa; kwa kweli hakuna tofauti kati yetu. 
Kama ilivyo kwako, mimi pia nilikuwa nikielekea kuzimu, na kama ilivyo kwako, nimepokea pia ondoleo la dhambi kwa kuamini katika injili ile ile ya maji na Roho. Kwa kuamini katika injili ambayo kwa hiyo Bwana amezitoweshea mbali dhambi zetu, wewe na mimi kwa pamoja tumeokolewa kwa imani. Kwa hiyo ninatoa shukrani zangu kwa Bwana. Ni kwa sababu kwa njia hii tunayo ile dhamiri ya imani kwa kupokea ondoleo la dhambi kamilifu kwa kupitia maji na Roho na ndio maana tunaweza kwenda mbele za Mungu na kumwomba kama watoto wake ambao tumepokea ondoleo la dhambi. 
Kama Biblia inavyotueleza kuwa manukato ya madhabahu ya uvumba yaliundwa kwa mafuta ya upako na uvumba wa manukato, Yesu ametufanya sisi kuwa safi kwa kuzioshelea mbali dhambi zetu zote kwa injili takatifu ya ukweli. Katika zama za kale za Agano la Kale, watu wa Israeli walipaswa kuutengeneza uvumba huu na kisha kuuchoma juu ya madhabahu kwa usahihi kama Mungu alivyoamuru. Kwa hiyo ndani ya Mahali Patakatifu, uvumba ulichomwa na harufu yake nzuri ilikuwa ikisikika kila siku. Uvumba huu unamaanisha ni kumwomba Mungu. 
Katika kipindi cha Agano Jipya, ili wewe uweze kuuchoma uvumba huu Mahali Patakatifu ni lazima kwanza uamini katika injili ya ukweli na kisha upokee ondoleo la dhambi katika moyo wako. Kwa maneno mengine, ni kwa kuamini katika injili ya ukweli ndipo mtu anapoweza kuuchoma uvumba wa maombi. Je, tunawezaje pia kuuchoma uvumba kwa namna ile ile kama ilivyofanyika katika kipindi cha Agano la Kale? Wakati ambapo vyombo vya Hema Takatifu la Kukutania kama vile madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na madhabahu ya uvumba havipo pamoja nasi tunawezaje basi mimi na wewe kuufanya uvumba na kuuchoma juu ya madhabahu? Tunaweza kuchoma uvumba wa maombi kwa imani, kwa kuwa Yesu Kristo amezitoweshea mbali dhambi zetu na ametuokoa. Kwa sababu mioyo yetu imesafishwa kwa imani wakati tulipopokea ondoleo la dhambi, sasa tunaweza kuuchoma uvumba ukapaa kwenda kwa Mungu kwa maombi yetu ya kina. 
Tunaamini kwamba kwa imani ya kina ndani ya mioyo yetu katika injili ya maji na Roho dhambi zetu zote zilipitishwa kwa Yesu Kristo, na kwamba Yesu Kristo alibeba adhabu ya dhambi hizo pasipo hatia kwa niaba yetu. Kwa hiyo mioyo yenu na mioyo yetu imefanywa kuwa misafi. Kwa kuwa dhambi zetu zote katika mioyo yetu zilipitishwa kwa Yesu, basi mioyo yetu imefanyika kuwa misafi kikamilifu mara moja kwa imani. Ikiwa dhambi zako zote zilipitishwa kwa Yesu kwa kupitia ubatizo wake ambao aliupokea toka kwa Yohana, basi dhambi zako zote zilioshelewa mbali na kutoweshewa mbali mara moja na kwa wote. Hakuna dhambi yoyote iliyoachwa katika mioyo yetu. Kwa kuwa dhambi zetu zilitoweshewa mbali na kusafishwa kwa kule kuiamini injili, basi sasa tunaweza kwenda mbele za Mungu mtakatifu na kisha kumwomba msaada wake. Kule kusema kuwa tunaweza kumwomba Mungu ni kitu ambacho kimejengwa katika imani yetu, kwamba tumepokea ondoleo la dhambi kwa kuamini kikamilifu katika injili, ambayo kwa sasa ni msingi wa mioyo yetu myema. 
Kaka na dada zangu, nenda katika madhabahu ya uvumba na uombe maombi yanayonukia. “Baba, tafadhali nisaidie mimi. Hii ndiyo hali ambayo nimo hivi sasa, na hivi ndivyo nitakavyo. Ninapenda kuihubiri injili ya kweli na kuishi kwa haki. Ninapenda kuishi maisha safi yanayomfaa mtu ambaye amepokea kwa kweli ondoleo la dhambi. Ninapenda kuzaa matunda ya haki. Nipatie imani katika wewe Baba. Ninapenda kuishi maisha yangu kwa mujibu wa mapenzi yako.” Vivyo hivyo, hivi ndivyo ilivyo hata pale tunapoomba juu ya mahitaji. Maombi yanahusu kuomba msaada wa Mungu kwa mujibu wa haki yake. 
Bila shaka una matamanio mbalimbali pia. Kwa kuwa tumefanywa kuwa ni wenye haki kwa imani katika injili ya maji na Roho ambayo imetuhesabia haki, basi kwa sasa inawezekana kabisa kumwomba Mungu vitu vyote kwa maombi yetu. Wale ambao wanaweza kumwomba Mungu ili awape msaada wake ni watu ambao wanafuraha. Kwa sasa hakuna shaka kwa sababu sisi sote tunaweza kumwomba Mungu kwa sababu tumeamini katika injili ya maji na Roho. 
Wale ambao kwa imani yao katika Mungu na katika injili ya maji na Roho wamepokea ondoleo la dhambi katika mioyo yao basi kwa kweli wamestahilishwa kumwendea Mungu mtakatifu na kisha kumwomba msaada wake. Na wale waamini wote waliozaliwa upya tena bila kukwepa wanakuja kuomba kwa ajili ya msaada wa Mungu katika maisha yao, kama ambavyo mtoto analia anapohitaji msaada kwa wazazi au anapokuwa katika shida. Imani yao ambayo imewaletea ondoleo la dhambi si imani inayowawezesha kumwita Mungu kuwa ni Baba tu, bali ni imani inayowawezesha pia kumwomba Baba msaada katika nyakati zote tukiwa kama wana na mabinti zake. Kwa kuwa Mungu amefanyika kwa kweli kuwa Baba yetu kwa imani, basi sasa tunastahili kabisa kumwomba msaada wake kwa kupitia maombi yetu kwa mujibu wa mahitaji yetu. 
Kwa kweli sifahamu jinsi ambavyo maombi yako binafsi yamekuwa au jinsi ambavyo Mungu amejibu maombi yako baada ya kuwa umepokea ondoleo la dhambi zako. Lakini ninachofahamu ni kuwa wakati tunapoomba kwa Mungu ili atuwezeshe kuungana na Kanisa lake na kuihubiri injili, kwa hakika Mungu anajibu maombi yetu. Ni katika mchakato huu ndipo tunapokuja kuombeana. Mara ya kwanza, kila mtu anaomba kwa ajili ya mahitaji ya mwili wake. Lakini kwa kazi ya Roho Mtakatifu tunakuja kujikuta kuwa tunaomba pia kwa ajili ya mahitaji ya watu wengine, na ndipo tunapojitoa kuomba kwa ajili ya wokovu kwa nafsi zingine na kuenea kwa injili ya maji na Roho katika ulimwengu mzima. Kwa nini? Kwa sababu maombi ya watakatifu waliozaliwa upya tena yanaongozwa na Roho Mtakatifu. Mungu ametuambia sisi kuwa, “Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake” (Mathayo 6:33).
Lakini miongoni mwa waliozaliwa upya tena, wale ambao bado hawajakomaa kiroho hawajui namna ya kuomba kwa vitu sahihi, kwa kuwa bado hawajayazoea majibu ya Mungu katika maombi yao. Hii ni kwa sababu bado hawafahamu jinsi ambavyo imani ina nguvu katika haki ya Mungu. Wale wenye imani ndogo wakati mwingine hawajui ikiwa maombi yao yamejibiwa au la na wakati mwingine wanakuwa na mashaka. 
Kwa hiyo, watu hao ni lazima waombe pamoja na wale walioamini kabla yao. Wale ambao imani yao bado ni changa wanakuwa na mashaka ya kumwomba Mungu. Na wanapoomba, wanaoomba tu juu ya yale wanayoyataka—“nipatie, nipatie, nipatie.” Lakini wale walio wachanga katika imani wanapounganika na Kanisa hata pale wasipokuwa na imani kubwa katika Mungu, bado wanaweza kujifunza kuwa maombi ya kweli ni yapi, kwa kuwa watangulizi wake katika Kanisa wanaomba kwa ajili ya haki ya Mungu. Pia kwa sababu Roho Mtakatifu anatoa imani ya kuomba kwa wale ambao wameunganishwa na Kanisa, basi hatimaye wanajikuta wanaomba pia kwa ajili ya haki ya Mungu. “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana” (Yakobo 5:16).
Maombi yenye imani ya waliozaliwa upya tena ambao wana haki ya kumwomba Mungu yanafaa sana. Maombi ya wale walio na imani katika Mungu kwa kweli yanajibiwa na Mungu. Wakati watu wanapomwomba Mungu, na ili kwamba maombi yao yajibiwe na Baba, basi ni lazima kwanza waamini kuwa Mungu ni Baba yao na kwamba anayajibu maombi yao sawasawa na imani yao. Kwa hiyo, wakati watangulizi wa imani wanapoungana pamoja na kuwaombea wale wanaozifuata nyayo zao na kwa ajili ya kazi ya haki ya kuieneza injili, basi wanafikia hatua ya kupata matendo makuu. Ikiwa utasimama karibu na mtangulizi wako ambaye anaamini katika Mungu, basi unaweza kusaidiwa sana katika imani yako. Kwa kuwa Mungu anafahamu kuwa tunahitaji msaada mkubwa si kwa neema ya wokovu tu bali hata katika mambo mengine ya kimaisha, basi Mungu anajibu maombi yetu. Hii ndio sababu kuwa sisi sote tunahitaji imani ambayo imeunganishwa na Kanisa la Mungu. 
Tunapoomba kwa ajili ya vitu ambavyo vinamfurahisha Mungu, basi imani yetu inaimarishwa sana. Kama watoto wa kiroho tunaiga na kufuatisha kuomba basi hatimaye tunafikia hatua ya kuomba maombi hayo kama ya kwetu binafsi na yaliyokomaa, pia tunaweza kuja kuomba mbele za Mungu Baba juu ya matatizo yetu binafsi baadaye kidogo. Wale ambao kwa kufanya hivyo wanamwamini Mungu basi wanafikia mahali pa kutembea kwa imani katika njia hali wakiufuata ukweli halisi. Kama ambavyo Biblia inavyotueleza kwa wenye haki wataishi kwa imani tu, basi hawataishi kwa ajili yao tu bali na kwa ajili ya wokovu wa nafsi zingine. 
Je, tumepataje tena sifa za kumwomba Mungu? Tumezipata sifa hizo kwa kuzaliwa upya tena kwa kupitia imani yetu katika injili ya maji na Roho iliyotolewa na Mungu. Ni kwa wale tu ambao wamepokea ondoleo la dhambi kwa kuamini katika injili ya maji na Roho ndipo ujasiri wa imani unaomwezesha mtu kumwomba Mungu Baba unapotolewa. Imani ni karama toka kwa Mungu. Kupata sifa za kuomba ni kupokea baraka kubwa za imani toka kwa Mungu. 
Miongoni mwa Wakristo wengi waamini katika sayari hii, je, ni wangapi miongoni mwao ambao unafikiri wanastahili kuomba kwa imani hiyo? Kwa kweli sio wengi! Moja ya karama zilizobarikiwa toka kwa Mungu ni kuwa, kwanza, tumefikia hatua ya kuwa na imani ambayo imetuokoa sisi toka katika dhambi zetu kwa ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau na nyekundu. Na la pili ni kuwa tumepokea nguvu na sifa za kumwomba Mungu kama watoto wake mwenyewe; na tatu, kwamba tumefikia kuwa na imani inayoturuhusu kuishi kama watenda kazi wa Mungu.
 


Mungu Hajibu Maombi ya Wenye Dhambi

 
Baadhi ya wenye dhambi hata pale wanapokiri kumwamini Yesu, wanamwomba Mungu ili kuzitoweshea mbali dhambi zao kwa kupanda baadhi ya milima na kwa kupiga kelele kwa jina la Bwana. Hata katika nyakati za usiku zenye baridi na zenye upepo, bado wanapanda mlima hali wakiwa wameifunika miili yao kwa mashuka ya plastiki, na pamoja na kuwa wanaogopa, bado wanaoomba kwa juhudi sana kwa kujitoa kwao kwote. Lakini maombi yao yanatoa tu mlio wa kutisha katika eneo lisilo na kitu. 
Pamoja na kuwa wanaomba usiku kucha, watu hawa hawana imani ambayo kwa hiyo Mungu atawajibu maombi yao. Sababu inayowafanya kuomba kwa nguvu na juhudi kiasi hicho pamoja na kuwa hawana imani ni kwa sababu wanataka kujionyesha kwa watu wengine, ni kama maonyesho tu. Maombi yao ni maombi yasiyojibiwa. Kwa kweli, wanafahamu wazi katika dhamiri zao kwamba maombi yao hayamfikii Mungu, kwa sababu wana dhambi katika mioyo yao. Kwa sababu bado hawajapokea ondoleo la dhambi zao, basi hakuna jibu kwa maombi yao mengi bila kujalisha kuwa wanaomba kwa kiasi gani, wanalia na kupiga kelele, wanaunguruma, na kufanya kila aina ya vitu ili kumwomba Mungu kwa yale wanayoyataka. 
Wanachohitaji kutambua ni kuwa sifa za kumwomba Mungu zinapatikana pale tu mtu anapopokea ondoleo la dhambi kwanza. Lakini kwa sababu wenye dhambi wengi hawana la kufanya hadi pale wanapokuja kuifahamu injili ya maji na Roho, basi hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kuishi katika maisha yao ya imani kama wenye dhambi. Wakati watu wanapokuwa hawajasafishwa mara moja kwa kuamini katika mioyo yao juu ya injili ya maji na Roho iliyotolewa na Bwana, basi kwa kweli maombi yao yanaishia katika utupu. Kila wenye dhambi wanapojaribu kumwomba Mungu, dhamiri zao zinawapigia kelele, “Unafikiri maombi yako yatamfikia Mungu? Ota ndoto! Maombi yako yote ni utupu tu!” Kwa hiyo hata pale wanapoendelea kumwomba Mungu, “Nipatie hiki, nipatie kile,” kwa kweli maombi yao ni kujichosha tu. 
“Kabla hujaniomba Mimi, kwanza pokea ondoleo la dhambi zako.” Haya ni mapenzi ya Mungu. Wakati wale ambao hawajapokea ondoleo la dhambi wanapomwomba Mungu, wanatambua kutokana na uzoefu wao kwamba dhamiri zao hazikubaliana na yale wayasemayo. Wakati wenye dhambi wanapoomba, wanaendelea kusema, “Nipatie hiki, Bwana, na pia nipatie kile,” lakini hakuna jibu kwa maombi yao. Mbali na hilo, dhamiri zao zinawaambia wao kuwa, “Hakuna njia! Majibu yako hayatajibiwa, kwa sababu wewe ni mwenye dhambi!” Wakati hata katika dhamiri zao wenye dhambi hawawezi kuivumilia imani yao, wanawezaje basi kumdanganya Mungu, wanawezaje kuthibitishwa na Mungu, na maombi yao yanawezaje kujibiwa? Wenye dhambi kwa kweli hawastahili kumwomba Mungu. Mbali na hilo, hata mioyo yao haiyaamini maombi yao. 
 


Maombi Yetu Yanaanza Kujibiwa Pale Tunapofanyika Wenye Haki kwa Imani

 
Lakini maombi ya wengi ambao wamekuwa ni wenye dhambi hapo kabla yanaanza kujibiwa pale wanapopokea ondoleo la dhambi zao kwa kuamini katika injili ya maji na Roho iliyodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu za Hema Takatifu la Kukutania. Wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho katika mioyo yao wanaweza kuwa na mapungufu yao binafsi, lakini wanaweza kumwendea Mungu kwa imani, na kwa imani wanaweza kumwomba Mungu, hali wakimwomba mahitaji yao. Wakati wale waliopokea ondoleo la dhambi kwa imani wanapomwomba Mungu kwa mujibu wa mapenzi yake, basi ndipo wanapoweza kuomba kwa ujasiri. 
Lakini wanapoomba kwa ajili ya miili yao, basi kwa nyakati fulani wanajisikia kuwa hawastahili. Sisi wenye haki ni watu wenye furaha sana pale tunapoomba juu ya kuenea kwa injili ya maji na Roho kwa ajili ya nafsi za watu wengine. Tunapoomba kwa ajili ya nguvu ya kuenea kwa injili, hali tukiwa hatuzuiwi na kizuizi chochote cha mwili, basi tunaweza kukishinda kizuizi cha ukomo wetu kwa kupitia maombi yenye imani. Lakini kwa nyakati fulani, tunajisikia kama tumechanganyikiwa hasa pale tunaposhindwa kuvishinda vizuizi hivyo kwa imani. Katika nyakati kama hizi tunachotakiwa kukifanya ni kuomba na kuamini kuwa hatimaye Mungu atatujibu. Na kwamba utafika wakati ambapo tutashuhudia kuwa Mungu ametujibu kwa hakika. 
Kitu ambacho ni lazima tukifanye ni kuomba na kisha kusubiri, na sio kushangaa kutokana na kutokuwa na subira na kusema kwa nini maombi yetu hayajajibiwa pale pale. Mungu anatutaka sisi kuomba kwa imani, na kuamini kuwa ikiwa maombi yetu yanapatana na mapenzi ya Mungu, basi Mungu atayajibu maombi yetu wakati utakapowadia. Na wakati tunapopokea ondoleo la dhambi kwa imani, na wakati tunapoomba kwa imani katika maisha yetu, basi kwa hakika tutashuhudia sisi wenyewe kuwa maombi yetu yanajibiwa. 
Lakini je, umeishi kwa imani kama hivi? Kama ndivyo basi unaweza kumwomba Mungu kwa hakika. Wakati tunapojichunguza sisi wenyewe zaidi na zaidi, ndipo tunapotambua kuwa sisi tumefungwa kwenda kuzimu, na pia tunatambua tena kuwa tunaweza kustahilishwa kuomba kwa kupokea ondoleo la dhambi kwa kupitia imani yetu katika injili ya maji na Roho. Kwa hiyo, ni lazima tukumbuke kwa hakika kuwa wale wanaoweza kuomba ni wale ambao wamepokea ondoleo la dhambi kwa kuamini kwamba Bwana amezitoweshea mbali dhambi zao zote katika kipindi walichoishi kwa injili ya maji na Roho. 
Kuna watu wengi miongoni mwa wale ambao hawajazaliwa tena upya ambao wanajivuna sana. Vipi kuhusu wewe? Je, una kitu chochote cha kujivunia? Je, mikono yako ina nguvu? Je, miguu yako ina nguvu? Haijalishi ni kwa kiasi gani miili yetu inaweza kuwa na nguvu, ukweli ni kuwa miili hii haiwezi hata kushindana na virusi waletao mafua na kikohozi, wala haiwezi kupingana na nguvu kinzani ya kimwili kwa muda mrefu, hapo ndipo udhaifu wa miili hiyo unapoonekana. Je, unatambua jinsi ambavyo wanadamu ni wadhaifu? Tunaweza kufa kutokana na kung’atwa na mbu mara moja tu, au kuanguka na kufa pale tutakapogongwa na jiwe lililoporomoka wakati tunatembea barabarani. Sisi si kitu. Ikiwa mtu anatamka sentesi moja ambayo inajeruhi majivuno yetu, mara nyingi mioyo yetu inaweza kuumia sana kiasi kuwa tunakuwa kama ni nusu wafu. Je, hivi si ndivyo ilivyo? Kwa kweli ndivyo ilivyo! 
Je, ni watu wangapi wanakufa hata kabla ya kufikisha miaka 60? Kuna watu wengi wasio na hesabu ambao wanakufa hata kabla ya kufikia miaka 30. Viumbe wanyonge kiasi hicho si wengine bali ni wanadamu wenyewe. Nguvu ya kudumu ya mwanadamu haiwezi kupatikana popote. Je, viumbe wadhaifu kama hao wanaweza kuifanya migumu mioyo yao na kutoamini katika Neno la Mungu ndani ya mioyo yao? Sisi wanadamu hatuna kitu cha kujivunia wala kujifanya kuwa tuna nguvu katika hicho. 
Kwa hiyo, ni lazima tuutambue udhaifu wetu binafsi, tutambue mapungufu na dhambi, na kisha tuamini katika injili ya ukweli iliyotimilizwa kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu katika mioyo yetu na hivyo kupata sifa za kumwomba Mungu. Ni lazima tuwe na imani katika Mungu. Ili kuwa na imani hii inayomfurahisha Mungu katikati ya mioyo yetu, ni lazima watu waamini katika injili ya maji na Roho, lakini kuna watu wengi ambao hawaiamini injili hii. Je, ungeweza kupata haki ya kumwomba Mungu toka katika injili nyingine zaidi ya hii injili ya maji na Roho? Je, dhambi zako zingeliweza kutoweshewa mbali ikiwa kama Yesu asingelikuja hapa duniani na kuzibeba dhambi zako katika mwili wake kwa kubatizwa kwa ajili yako? Je, ungeliweza kuzipitisha dhambi za moyo wako kwa Yesu na kuzioshelea mbali pasipo kuamini katika ubatizo ambao Yesu aliupokea? 
Majibu ya maswali hayo hapo juu ni hapana, hapana, na hapana kabisa! Yesu alisulubiwa na kubeba adhabu ya dhambi zote kwa damu yake, hii ni kwa sababu Yesu alikuwa amezibeba dhambi za ulimwengu kwa ubatizo alioupokea toka kwa Yohana. Je, ungeliweza kuokolewa basi pasipo ubatizo wa Yesu na Msalaba? Kwa kweli sivyo! Ubatizo wa Yesu ulilenga kumfanya Yesu kuzichukua dhambi zetu zote mara moja na kwa wote na kisha kuzioshelea mbali na kuzisafishilia mbali dhambi hizo. Na kule kusema kuwa alisulubiwa, kulilenga katika kuibeba adhabu ya dhambi zetu. Ni kwa kuamini katika ukweli huu wa injili ya maji na Roho ndipo tumeweza kuondolewa dhambi zetu zote. 
Kwa hiyo, tunaweza kwenda mbele za Mungu na kisha kukiri kwa ujasiri, “Bwana, nina mapungufu kiasi hiki, lakini kwa sababu umeniokoa kwa maji na damu yako, kwa sasa sina dhambi. Ulikuja hapa duniani, ukazichukua mara moja dhambi zote katika mwili wako kwa kubatizwa, ukazibeba dhambi hizi za ulimwengu hadi Msalabani, uliadhibiwa kwa sababu ya dhambi hizi, na kisha ukafufuka tena toka wa wafu. Na kwa kufanya hivyo, Bwana, umefanyika kwa kweli kuwa Mungu wa wokovu wangu. Ni kwa kupitia imani yangu katika ukweli huu ndio maana ninakuamini wewe.” Kwa maneno mengine, tunapoitunza imani yetu basi tunaweza kwenda mbele za Mungu na kumwomba bila kujali mapungufu yetu. Tunaweza kuomba kwa ajili ya kupanuka kwa Ufalme wa Mungu, tunaweza kuomba kwa ajili ya kaka na dada zetu, pia tunaweza kuomba kwa ajili ya nafsi nyingine ambazo bado hazijapokea ondoleo la dhambi. 
Ni pale tu watu wanapoamini katika injili ya maji na Roho ndipo wanapoweza kuwa hawana aibu chini ya mbingu. Lakini pasipokuwa na imani hii ya injili ya maji na Roho baadhi ya watu wanaweza kujitahidi kuliziba pengo hilo kwa kitu kingine—ni lazima utambue kuwa jitihada za jinsi hiyo ni bure kabisa. Hii ndio sababu mioyo yao ina huzuni na inateswa hali ikiyafanya maisha yao kuwa yasiyobebeka. Kila mtu anapenda kuamini katika kitu fulani bila kujalisha kuwa kitu hicho ni cha kweli au cha uongo. Naomba utafakari wewe mweneywe. 
Jichunguze wewe mwenyewe ili kuona kuwa ikiwa unamwamini kweli Bwana kwa imani inayoamini katika injili ya maji na Roho, au ikiwa huamini katika injili hii ya maji na Roho. Bwana amezitoweshea mbali dhambi zako kwa maji na damu—ikiwa unaamini katika hili, je, kutakuwa na dhambi iliyosalia katika moyo wako? Ikiwa kweli unaamini toka katika kina cha moyo wako na roho yako, basi kwa hakika hakuna dhambi katikati yako kabisa. Kwa imani yako kamilifu katika ukweli huu, pokea ondoleo la kweli la dhambi sasa hivi. 
Kwa sababu Mungu ametupatia ondoleo la dhambi kwa kupitia ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, basi kwa sasa tumepokea hili ondoleo la dhambi la milele. Na kwa sababu ya hili, wale wanaoamini katika ukweli huu wamefanyika wana wa Mungu mwenyewe, wamevishwa neema ambayo inawawezesha kwenda mbele za Mungu. Kwa hiyo, ni lazima tupendane sisi kwa sisi na tuyafahamu mapungufu ya kila mmoja wetu, tuitumikie kazi ya Mungu hadi mwisho, na kisha twende kwake na kusimama mbele ya uwepo wake. 
Wale ambao wamepokea ondoleo la dhambi wanawapenda wenye dhambi wote. Mioyo ya wenye haki inatamani kila mwenye dhambi kuufahamu ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kisha wazaliwe tena upya. Lakini kuna baadhi ya aina ya watu ambao hawawezi kwa kweli kuwapenda watu. Hawa ni wenye dhambi wagumu—ambao ni Wakristo wanaozidanganya dhamiri zao za imani na kujilaghai wao wenyewe kwa kufikiri kuwa wanaamini katika Mungu hata pale wanapobakia kuwa ni wenye dhambi. 
Kwa kuamini katika injili ya maji na Roho na kwa kupokea ondoleo la dhambi katika mioyo yetu, basi ni lazima sisi sote tuzilinde dhamiri zetu za imani. Hebu tukimbie vizuri katika mashindano yetu hadi mwisho, hali tukitunza dhamiri zetu za imani na pasipo kuipoteza imani yetu. Na inapotokea kuwa mtu mmoja anaonekana kupitia katika kipindi kigumu kiroho, basi tusaidiane sisi kwa sisi na kisha tushikane sisi kwa sisi kwa ukakamavu. Bila kujalisha kinachotokea, wenye haki hawatakiwi kuliacha Kanisa. Ikiwa wenye haki wanaliacha Kanisa la Mungu, basi watakufa mara moja. Kuliacha Kanisa la Mungu ni sawa na kuiacha nyumba yako binafsi. Kuiacha nyumba yako ni sawa na kuliacha kimbilio lako, na kwa hiyo moyo wako hauwezi kamwe kupata mapumziko wala raha mahali popote, na hatimaye mwishoni utakufa.
Kanisa la Mungu ni mahali ambapo kondoo zake wanalishwa na kupewa mapumziko. Kwa hiyo, wakati kondoo wanapopoteza nguvu zao na kuwa wachovu, Kanisa la Mungu linaisaidia mioyo yao kuimarishwa kwa kulisikia Neno. Unapolipokea Neno kwa kuamini katika moyo wako, basi Roho Mtakatifu aliye ndani yako atafurahi na kwa hiyo moyo wako utatiwa nguvu, na kama matokeo ya mwisho utapokea uzima wa milele.
Sisi sote wenye haki tunatoa shukrani zetu kwa Mungu. Tunamshukuru Bwana kwa sababu ili aweze kutustahilisha sisi kuomba ametupatia sisi injili ya maji na Roho. Halleluya! Ninamwomba Mungu aliye hai ili kwamba atuwezeshe kumwamini yeye na kuishi kwa imani.