Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 8-11] Upendo wa Milele (Warumi 8:31-34)

(Warumi 8:31-34)
“Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.” 
 

Ikiwa Mungu alikwisha amua kutufunika sisi kwa haki yake katika Yesu Kristo hata kabla ya uumbaji, basi hakuna mtu anayeweza kusumbua na kuharibu mpango huo. Kwa kuamini katika haki ya Mungu, na wala si kwa kupitia katika Fundisho la Kuhesabiwa Haki kwa Imani, basi wale ambao wamekuwa hawana dhambi kiuhakika ndio watoto wa kweli wa Mungu. 
Kwa hiyo, sio kwamba watu wote wa kidini wapo sahihi. Siku hizi ni watu wachache ndio wanaoteswa kwa sababu ya kumwamini Yesu, lakini wengi wao wale wanaoifahamu haki ya kweli ya Mungu wamekuwa wakiteswa. Hata hivyo, watu waliofanyika kuwa watoto wa Mungu kwa kuamini katika haki ya Mungu hawawezi kutenganishwa na Mungu. Ni nani anayeweza kuwa kinyume nao wakati Mungu amekwisha wapatia injili ya haki yake? 
 

Mungu Ametupatia Kila Kitu Kama Zawadi 
 
“Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?” (Warumi 8:32)
Kwa wale walioipokea haki ya Mungu kwa kumwamini Mwanawe, Mungu amewapatia kila kitu kama zawadi—Ufalme wa Mbinguni, upendeleo wa kufanyika watoto wa Mungu, neema ya kulifahamu Neno lake, baraka ya kuwa tayari kuishi kama mtumishi wa haki, na baraka ya uzima wa milele. 
Mungu alitupatia Mwanawe ili kutufanya sisi kuwa watoto wake. Je, ni kitu gani basi ambacho Mungu hawezi kutupatia? Mungu amewapatia baraka zote za mbinguni na duniani wale wote ambao wameipokea imani ya kweli kwa kupitia haki yake. Waamini na watumishi wa Mungu wanamsifu Mungu milele kwa ajili ya haki yake. 
 

Ni Nani Atakayewashitaki Wateule wa Mungu? 
 
“Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea” (Warumi 8:33-34).
Hakuna anayeweza kuleta mashtaka dhidi ya watu ambao Mungu amewachagua kwa haki yake katika Yesu Kristo, kwa kuwa Yesu kwa kupitia haki ya Mungu amewafanya wao kuwa wasio na dhambi. Watu wanaoamini katika haki ya Mungu kwa kupitia Yesu Kristo hawana dhambi katika mioyo yao. Hii ni kwa sababu ya Mungu na wala si mwingine aliyewafanya wale wanaoamini katika haki yake kutokuwa na dhambi. 
Mwana wa Mungu Yesu Kristo alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, alibatizwa na Yohana Mbatizaji, akauchukua mzigo wa dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake, alikufa Msalabani na kisha akafufuka toka kwa wafu siku ya tatu, na amefanyika kuwa ni Bwana kwa wale wanaoamini. 
Hii ndiyo sababu hatuwezi kusema kuwa wale waliofanyika kuwa wenye haki kwa kuamini katika haki ya Mungu kuwa wana dhambi na watenda maovu. Hata sasa, Mungu anawatambua wale wanaoamini katika haki yake. Kama ushahidi wa jambo hili, Roho Mtakatifu anakaa katika mioyo yao. Hii ndiyo sababu hakuna anayeweza kuiasi haki ya Mungu au kwa wale ambao dhambi zao zimesamehewa kwa kuamini katika haki ya Mungu. 
Haki ya Mungu ilionekana kwa kupitia ubatizo wa Yesu Kristo, kuimwaga damu yake Msalabani, na kifo chake na ufufuko wake. Baada ya kuwa amekwisha kuitimiza haki yote ya Mungu, Yesu Kristo ameketi katika mkono wa kuume wa Mungu kama Mwokozi na mwombezi wetu.