Search

Mahubiri

Somo la 9: Warumi (Maoni juu ya Kitabu cha Warumi)

[SURA YA 9-2] Ni Lazima Tufahamu Kuwa Kuchaguliwa Tangu Asili Kulipangwa Ndani ya Haki ya Mungu (Warumi 9:9-33)

(Warumi 9:9-33)
“Kwa maana neno la ahadi ni hili, Panapo wakati huu nitakuja, na Sara atakuwa na mwana. Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu, (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi al Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo bali kwa sababu ya nia yake aitaye), aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia. Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha! Maana amwambia Musa, Nitamrehemu nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani Mungu. Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote. Basi kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu. Basi utaniambia, mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake? La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u anani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, kwani kuumba hivi? Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima? Ni nini basi ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kwa kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu; tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu; ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia? Ni kama vile alivyosema katika Hosea: 
‘Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, 
Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.’ 
‘Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, 
‘Ninyi si watu wangu,’ 
Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.’ 
Isaya naye akatoa sauti yake juu ya Israeli, kusema: 
‘Hesabu ya wana wa Israeli ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari, 
Ni mabaki yao tu watakaookolewa. 
Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.’ 
Tena Kama Isaya alivyotangulia kunena: 
‘Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, 
Tungalifananishwa na Gomora.’ 
Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani; bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikilia ile sheria. Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwazalo, Kama ilivyoandikwa: 
‘Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; 
Na kila amwaminiye hatatahayarika.’”
 

Kuchaguliwa Tangu Asili Kulikopangwa na Mungu ni Nini? 
 
Hebu sasa tuweke umakini wetu juu ‘kuchaguliwa tangu asili kulikopangwa na Mungu”. Ili kuelewa kiusahihi juu ya maana ya kuchaguliwa tangu asili, basi tunapaswa kulizingatia Neno la Mungu lililoandikwa, na kisha tukajisahihisha sisi wenyewe ikiwa kuna kitu kibaya katika imani zetu. Katika hili, tunapaswa kwanza kutambua kuwa ni kwa nini Mungu alimpenda Yakobo huku akimchukia Esau. Pia tunahitaji kuchunguza ikiwa uelewa wa Ukristo wa sasa juu ya kuchaguliwa tangu asili kama haujatoka nje ya Maandiko. Sisi sote ni lazima tuwe na uelewa sahihi wa kuchaguliwa tangu asili kulikopangwa na Mungu. 
Ili tuweze kupokea baraka toka kwa Mungu, sisi Wakristo tunahitaji kufahamu jinsi kuchaguliwa tangu asili kwa Mungu jinsi kunavyoendana na mpango wa Mungu. Inapofikiriwa juu ya mpango wa Mungu, Wakristo wengi wa sasa wanafikiri kuwa majaliwa yao yalikwishapangwa kabla ya kuzaliwa kwao pasipokuwa na maana yoyote katika imani yao, kana kwamba hatima na majaliwa ya Yakobo na Esau yalipangwa na Mungu bila sababu yoyote ile. Lakini hali haiko hivi. Kupendwa na Mungu au la kunategemeana ikiwa tunaiamini haki ya Mungu au la. Huu ndio ukweli ambao Mungu ametupatia katika mpango wake. 
 

Ikiwa Unapenda Kufahamu Kuhusu Kuchaguliwa Tangu Asili Na Mungu, Basi Unahitaji Kuachilia Mbali Mawazo Yako Binafsi na Kisha Uizingatie Haki ya Mungu 
 
Kwa kuwa watu wengi hawawezi kufikiri na kuamini katika haki ya Mungu iliyodhihirishwa kwa kupitia Yesu Kristo, basi watu hao wanaufikiria upendo wa Mungu kwa namna yoyote wanayoweza kuichagua, na baadhi yao wanadiriki kufikiri kuwa upendo wa Mungu si wa haki. Watu hao ni lazima watambue kuwa hawapaswi kufikiri kwa namna hiyo maana si sahihi. Tupanaswa kuachilia mbali mitazamo yetu isiyo sahihi ya kiimani ya kutoifikiria haki ya Mungu iliyodhihirishwa kwa kupitia Yesu Kristo. Ikiwa unafikiria kuwa Mungu anawapenda watu fulani na kuwachukia wengine, basi unapaswa kutambua kuwa hii ni imani potofu inayotokana na mawazo yako potofu. 
Akili za mwanadamu zimepata mapigo kutokana na mawazo potofu. Wakristo wengi wa sasa hawana imani sahihi kwa kuwa mara nyingi mawazo na akili zao zimefunikwa na fikra mbaya. Hii ndiyo sababu unahitaji kutupilia mbali mawazo yako mabaya na kuiweka imani yako katika njia sahihi kwa kulifuata Neno la Mungu na kuiamini haki yake. 
Kwa kuwa kuchaguliwa tangu asili kumepangwa ndani ya haki ya Mungu, basi kuchaguliwa huko kunaweza kueleweka na kuaminika vizuri wakati tunapoiamini haki ya Mungu. Hivyo ni lazima tuuamini mpango wake na tuiiamini haki yake. Mpango wa Mungu ni kuwavika wale wote wanaoamini katika upendo wake ndani ya haki yake katika haki. 
Hivyo, ukombozi wake ni kuwa Mungu atawafanya waamini kuwa watu wake kwa kuwafunika kwa wokovu wa ondoleo la dhambi, ambalo lililipwa na ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kwake. Tunapaswa kuuimarisha uhusiano sahihi na Mungu kwa kuwa na imani katika ukweli uliopangwa na Mungu ndani ya haki yake. Mungu amewafanya wale walio kama Yakobo kuwa ni vyombo vya rehema wakati wale walio kama Esau amewafanya kuwa ni vyombo vya ghadhabu. 
 

Kuchaguliwa Tangu Asili na Mungu Si Majaliwa.
 
Kuchaguliwa tangu asili ndani ya mpango wa Mungu kulianzishwa ndani ya haki ya Mungu. Upendo wa Mungu si kitu ambacho kimewekwa ovyo bila mpango. Ikiwa kila mtu alichaguliwa bila sababu kabla ya kuzaliwa kwake, kana kwamba maisha yalipangwa kwa majaliwa, basi inawezekanaje kwa mtu kama huyo kukombolewa toka katika dhambi kwa kuamini katika haki ya Yesu? Ikiwa majaliwa ya mtu yangelikuwa yamepangwa kabla ya kuzaliwa kwake kwa namna ambayo mtu kupendwa au kutopendwa na Mungu ni matokeo ambayo yalikwishapangwa zamani, ni nani basi ambaye angelifikiri kuwa Mungu ana haki? Na ni nani ambaye angelimwamini Mungu kama huyo? Hakuna hata mmoja ambaye angelipenda kumwamini Mungu dikteta kama huyo. 
Lakini mpango wa Mungu wetu si wa kidikteta na wala hauko ovyoovyo, bali unalenga katika kutukomboa sisi toka katika dhambi zetu zote kwa kupitia ndani ya haki yake na kutufanya sisi kuwa watu wake. Mungu alitupatia haki yake ndani ya mpango wake, na katika haki hii ya upendo ndipo Mungu alipotupatia msamaha wake. Mungu amejiandaa kuwafunika wale wote wanaoamini katika upendo wa haki yake, na pia atawapatia ghadhabu wale wasiouamini upendo wa haki yake. 
Ninapenda kusema yafuatayo kwa wale wanaokuchukia kuchaguliwa tangu asili na Mungu hali wakiwa chini ya kutokufahamu. Mpango wa Mungu ni kutufanya sisi ambao tuliumbwa kwa sura na mfano wake kuwa watu wake mwenyewe. Hivyo tunapaswa kuwa na shukrani kwa ukombozi wake. Hivyo ni vema kwetu sisi kuwa watu wa shukrani ambao tunaamini katika haki ya Mungu badala ya kuwa watu wenye chuki ambao wanamkana Mungu. Kila mtu anayemwamini Yesu kuwa ni mwokozi wake ni lazima awe na ufahamu sahihi na imani sahihi juu ya kuchaguliwa tangu asili ambako kulipangwa ndani ya haki ya Mungu. 
 

Kuchaguliwa Tangu Asili kwa Mungu Kulianzishwa na Yeye Anayeita
 
Kifungu cha leo kinasema, hasa ukianzia Warumi 9:9, “Kwa maana neno la ahadi ni hili, Panapo wakati huu nitakuja, na Sara atakuwa na mwana. Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu, (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo bali kwa sababu ya nia yake aitaye), aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.” 
Kifungu hiki kinatueleza sisi kuwa suala la Mungu la kuchaguliwa tangu asili ni lile lenye upendo, ambalo lilipangwa ndani ya upendo wa haki ya Mungu. Kama inavyooneshwa katika Mwanzo 18:10, ingawa kibinadamu ilikuwa ni vigumu kwa Sara kuzaa mtoto, Ibrahimu aliiamini ahadi ya Mungu kwa kuwa Mungu alikuwa amelitoa Neno lake. Hivi ndivyo Mungu alivyomhesabia haki Ibrahimu: Ibrahimu akamtolea Mungu mwanawe Isaka kwa kuwa alikuwa akimwamini Mungu, na Mungu akaikubali na kuithibitisha imani yake. 
Hivyo, tunapozungumzia kuhusu imani katika haki ya Mungu, tunazungumzia imani katika Neno la Mungu. Majadiliano yetu kuhusu mpango wa Mungu na kuchaguliwa tangu asili kunapaswa pia kuongozwa na imani katika Neno la Mungu. Wale ambao wanafanya kinyume na hivyo, kwa mfano wale ambao wanauchanganya msimamo wao wa haki ya Mungu kwa masuala ya uongo na ishara ambazo wanadai kuwa wameziona wakati walipokuwa wakisali au katika ndoto—watu wanaofanya hivyo wanafanya makosa makubwa sana katika imani yao. 
Paulo anaongezea kwa kusema kuwa, “Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu, (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo bali kwa sababu ya nia yake aitaye), aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo.” 
Maandiko yanatueleza sisi kuwa, Isaka alishindwa kupata mtoto kwa juhudi zake na hivyo akamwomba Mungu, na Mungu akamjibu kwa kumpatia mapacha. Tunaweza kuona kuwa kuchaguliwa tangu asili kulikopangwa na Mungu katika haki ya Mungu kuna uhusiano fulani na imani za wale wanaopendwa na Mungu. 
Itakuwa ni jambo jema kuirudia hapa aya ya 11 tena: “kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo bali kwa sababu ya nia yake aitaye” Ufunguo wa kuweza kuufahamu ukweli wa kuchaguliwa tangu asili na kuchaguliwa ndani ya mpango wa Mungu ni kwamba kusudi la Mungu lisimame “la Yeye aitaye.” Kwa mujibu wa kuchaguliwa tangu asili kuliko ndani ya mpango wa Mungu, kati ya Yakobo na Esau Mungu alimwita na kumpenda Yakobo. 
Kwa maneno mengine, wakati Mungu anapowaita watu na kuwapenda, Mungu anawaita na kuwapenda watu kama Yakobo ambao wako mbali na kule kuwa wenye haki. Mungu hakumuita Esau ambaye alijifikiria yeye mwenyewe kuwa mwenye haki na aliyekuwa amejawa majivuno. Katika mpango wa Mungu wa kuchaguliwa tangu asili ni wazi kuwa Mungu atawaita watu walio kama Yakobo. Nia ya Mungu katika kuwaita watu kama Yakobo ilikuwa ni kuwafanya wenye dhambi kuwa watoto wake mwenyewe walio huru mbali na dhambi. Yeye aitaye ili kuwavika walioitwa upendo wake ni Mungu, na kati ya Yakobo na Esau aliyeitwa alikuwa ni Yakobo. 
Ni lazima tuamini na kuamini katika haki ya Mungu ndani ya mpango wake. Yakobo anawakilisha aina ya wenye dhambi ambao Mungu amewaonyesha rehema zake ndani ya haki yake, kwa upande mwingine Esau anawawakilisha wale wanageuka na kuwa kinyume na Mungu kwa kuudharau upendo wake wa haki na kwa kuifuata haki yao wenyewe. Hii ndiyo sababu ufunguo wa kuweza kulifungua Neno la Mungu juu ya kuchaguliwa tangu asili kulipangwa ndani ya mpango wa Mungu ni kulifahamu dhumuni la nia ya Mungu “Yeye aitaye.” 
Ni lazima tujiweke huru toka katika imani potofu zilizoundwa kwa mawazo yetu binafsi. Katika haki ya Mungu, Mungu angaliweza kumpenda Yakobo na kumchukikia Esau. Maelezo ya mpango wa Mungu na kuchaguliwa tangua sili yanatolewa kwa kila mtu kwa kupitia tamko lake ambalo lwa hilo nia ya Mungu inasimama “ya Yeye aitaye.” Mpango wa Mungu ni ule ukweli wa upendo uliotimizwa katika haki yake. Wakati Mungu alipompenda Yakobo na kumchukia Esau, basi kule kuchaguliwa tangu asili kulimaanisha kuitimiza haki ya Mungu kwa mujibu wa mpango wake kwa wokovu. 
Si kama inavyodaiwa na dini nyingi, kwamba mtu anapendwa na kuokolewa na Mungu kwa sababu ya matendo mema, bali mtu anafanyika kuwa mtoto wa Mungu na kukombolewa toka katika dhambi zake kwa kuamini katika mpango na haki ya Mungu. 
 

Je, Mungu Amekosea?
 
Mungu anawapenda wale wanaoamini na kuipenda haki yake. Kwa maneno mengine, hakuna kosa kuhusiana na ule ukweli kuwa Baba yetu aliamua kuwapenda na kuwafanya kuwa watoto wake wale wanaoamini katika haki ya Mungu katika Yesu Kristo. Mungu hakupanga kumpenda kila mtu katika Yesu Kristo, bali kuwapenda watu kama Yakobo. 
Basi, ni lazima tujiulize sisi wenyewe kwamba sisi tupo kama Yakobo au Esau. Lakini hata wale ambao wamejawa na matendo yao mema na haki yao binafsi bado wanataka wapendwe na Mungu, lakini hakuna anayeweza kuwazuia katika mbio zao za kuelekea upotofu. Hivyo, aina hizi mbili za watu zipo wakati wote zikipendwa au kuchukiwa na Mungu hata sasa tunapozungumza. 
Ni lazima tumtolee Mungu shukrani na tuutukuze utukufu wake kwa kuamini katika upendo wake wa haki na mpango wake wa wokovu. Pia tunapaswa kumshukuru Mungu kutokana na ukweli kuwa injili ya maji na Roho tunayoiamini inatoa ule mng’ao wa haki ya Mungu. Kila mtu ni lazima atambue kuwa ili kuweza kuvikwa katika upendo wa Mungu, basi ni lazima kwanza mtu atambue mapungufu na dhambi zake mbele za Mungu na kisha aamini katika haki ya Mungu. 
Tatizo ni kuwa, Wakristo wengi hali wakiwa hawawezi kuamini katika ubatizo wa Yesu na ukweli wa Msalaba ambavyo vimeitimiza haki ya Mungu, wanaamini kimakosa kuwa Mungu anawapenda kundi fulani la watu hali akiwachukia wengine na kuwaacha. 
Kuna tatizo zaidi kuwa kwa bahati mbaya aina hii ya imani isiyo sahihi bado ipo na inaendelea kuhubiriwa kwa watu wengi kwa msukumo mkubwa. Inaenea kwa haraka sana hali ikisababisha kuwepo kwa watu wengi ambao wanauelewa vibaya upendo wa Mungu ambao unaonekana katika mpango wa Mungu wa kuchaguliwa tangu asili. Kile ambacho Mungu anajaribu kutuambia kuhusiana na hadithi ya Yakobo na Esau ni kuwa haki ya mwanadamu haihitajiki ili kutufanya sisi kuwa watoto wa Mungu, bali kinachohitaji ni imani katika upendo wa haki ya Mungu uliopangwa kulingana na mpango wake. 
Maandiko yanatueleza sisi kuwa Mungu alimpatia Sara mtoto ambaye alimwahidia Ibrahimu. Hii inatueleza sisi kuwa ni wale tu walio na imani katika upendo na Neno la haki ya Mungu ndio wanaoweza kufanyika kuwa watoto wa Mungu. Ili kufanyika watoto wa jinsi hiyo ni lazima tuutambue ukweli ambao ulitolewa pamoja na imani yetu katika haki ya Mungu na mpango wake, na kisha kuuamini ukweli huu. Tunahitajika kuuamini upendo wa Mungu na haki yake. 
Upendo wa Yesu kwetu sisi na mpango wa Mungu kwetu ndio ukweli halisi na ndio upendo uliotolewa kwetu sote. Yesu alizichukua dhambi zetu zote katika mwili wake kwa ubatizo wake, alikufa Msalabani, na akafufuka toka kwa wafu ili kutuokoa toka katika dhambi zetu na kutupatia sisi tunaoamini uzima wa milele. 
Ukweli huu haumaniishi kuwa tunaweza kufanyika watoto wa Mungu kwa kuwa wanadini au kwa kuonyesha juhudi zetu binafsi, bali tunaweza kufanyika watoto wa Mungu kwa kumaini katika Neno la upendo na haki ya Mungu ambalo tumeelezwa na ambalo Mungu alilipanga kwa ajili yetu. Sisi sote ni lazima tutambue kuwa ni wale tu wanaoamini katika upendo wa Mungu na haki yake ndio waliovikwa katika upendo wa Mungu. 
Sasa, msimamo wetu uweje? Ni kuwa na imani katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. Ni lazima tumwombe Mungu ili aturehemu. Ni lazima tutambue mbele zake kuwa hatustahili kuitwa watu wake kwa kuwa sisi ni wenye dhambi. Ni lazima tutambue kuwa ni kwa kupitia mpango wa Mungu kwetu—ndipo tunapoweza kuufahamu upendo wake wa haki na kufanyika watoto wake. 
Wale ambao wanachukiwa na Mungu wanachukiwa kwa sababu hawauamini upendo wake na haki yake. Hivyo ni lazima tufahamu na kuamini katika mpango wa upendo wa Mungu ambao kwa huo Mungu ametuchagua tangu asili. Ukweli wa wazi ni kuwa wale wanaofahamu na kuamini katika upendo wa haki ya Mungu na wao pia watapendwa na Mungu na kuwa wale ambapo watakuwa wakiukataa upendo wake watachukiwa na Mungu. 
 

Ni Nani Anayeweza Kuipokea Injili ya Maji na Roho?
 
Injili ya maji na Roho iliyotolewa kwetu na Mungu ndio ukweli pekee ambao unaifunua haki yake. Je, ni aina gani basi ya watu ambao ndio wanaoupokea ukweli huu katika mioyo yao? Hawa ni wale wanaotambua kuwa hatima yao ipo katika maangamizi ya milele na kwamba ni wenye dhambi mbele za Mungu na mbele za Neno lake na kwamba wanaomba rehema za Mungu. “Bwana, mimi ni mwenye dhambi, ambaye siwezi kuishi kwa kuzifuata sheria yako kabisa. Ninautoa moyo wangu kwako na kujisalimisha kwako.” Watu wa jinsi hii ndio wale ambao Mungu amewapatia ondoleo la dhambi la upendo katika haki yake. Imani katika injili inayoidhihirisha haki ya Mungu ni ya muhimu sana kwa wenye dhambi wote. 
Mungu hakutupatia sheria yake ili kwamba tuweze kufuata kila kipengere, na huo ndio ukweli ambao wengi hawafahamu. Dhumuni la sheria ilikuwa ni kutuongoza ili tuweze kuzitambua dhambi zetu. Kwa nini basi wenye dhambi wanajaribu kuifuata sheria? Ni kwa sababu kila nafsi ya mwenye dhambi inajaribu kuupata ukombozi na suluhisho la dhambi zake. 
Lakini hakuna anayeweza kuzitii na kuzifuata sheria zote. Majaribio yote ya kuifuata sheria yalikuwa ni kama maigizo tu, kama kufuatisha kwa kihisia ili kujaribu kuzifunika dhambi zao katika hali ya kukata tamaa—kitu ambacho ni imani ya udanganyifu mbele za Mungu. Hii ndio sababu wenye dhambi wanapaswa kuiachilia mbali imani ya udanganyifu kama hii, na kisha waigeukie imani katika haki ya Mungu ili kwamba wafunikwe na upendo wa Mungu. 
Ili kuweza kutufunika sisi katika upendo wake, Mungu alimtuma Yesu kuja hapa duniani, ambaye baada ya kubatizwa na Yohana, alizichukua katika mwili wake dhambi zote za ulimwengu na akazitoweshea mbali dhambi hizo kwa kuimwaga damu yake Msalabani. Mungu amezitambua imani za wale wanaoamini katika upendo wa haki ya Mungu. Tunapokombolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kupitia imani katika injili ya maji na Roho, ambayo ni utimilifu wa haki ya Mungu, basi sisi tunavikwa ule upendo wake. Huu ndio ukweli ambao uliahidiwa kwa ajili yetu katika mpango wake. 
Mungu atawachukia wale ambao wanajitegemea wao wenyewe. Kuna watu wengi wa jinsi hiyo wanaotuzunguka. Lakini unapaswa kuokolewa toka katika dhambi zako zote kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake ambavyo vimeutimiza upendo wa Mungu na haki yake. Hapo ndio kwa hakika utakapofunikwa katika upendo wa Mungu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya wale ambao Mungu anawaita. Mara nyingi watu wanajaribu kufanya vitu kwa kujitegemea wao wenyewe kwa ajili ya Mungu ili waweze kuupata upendo wake na msamaha, lakini juhudi za jinsi hii pasipokuwa na haki ya Mungu ni kujidanganya. 
Mungu alimwita Yakobo tu ili aweze kufunikwa katika upendo wake, na wala si Esau. Mbele za Mungu, Yakobo alikuwa ni mlaghai na mwongo, lakini kwa kuwa aliuamini upendo wa Mungu na haki yake, Yakobo alifanyika kuwa mmoja wa mababa wa imani. Sisi pia tunapaswa kuupokea upendo wa Mungu kwa kuamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani kama ukombozi wetu, vitu ambavyo ni utimilifu wa haki ya Mungu. Kwa kuwa Esau alijaribu kubarikiwa na baba yake kwa mawindo yake mwenyewe, basi yeye alifanyika kuwa ni alama ya wale ambao hawawezi kuzipata baraka za Mungu. Tunahitaji kutumia muda fulani kufikiri kwa uangalifu juu ya jambo hili. Ni akina nani katika ulimwengu huu ambao wapo kama Esau? Je, sisi si kama Esau? 
Watu kama Yakobo ni wale ambao wanajivika upendo wa haki ya Mungu. Sisi pia tunajitambua kuwa ni wadhaifu kama Yakobo alivyokuwa. Mungu ambaye ametuita hata kabla hatujazaliwa ili tusimame si kwa matendo yetu bali kwa wito wake ametueleza kuwa tuuamini upendo wake na haki yake ili tuweze kulipata pendo lake. Mungu alimtuma Yesu, ambaye aliitimiza haki ya Mungu ndani ya mpango wake kwa ajili yetu sote. 
Wakati Mungu alipotuita mara ya kwanza, alikuja kwanza ili kuwaita wenye dhambi na si wenye haki. Wale wambao wanachukiwa na Mungu ni wale ambao wanajifikiria kuwa wamejawa na haki yao binafsi na wasiouamini upendo wake wa rehema. Wale walio na imani potofu kama hizo wanachukiwa na Mungu na hawawezi kufunikwa katika upendo wake ili kuwa watu wake. Mungu alikwisha uchagua ukweli huu tangu asili kwa ajili yetu ndani ya moyo wake. Hivyo, Paulo anaeleza wazi kuwa, “Tuseme nini basi? Kuna udhaifu kwa Mungu? Hasha!” (Warumi 9:14).
 

Wale Wanaopendwa na Mungu ni Wale Walio Kama Yakobo
 
Wakati Mungu anapokuangalia unaonekana kuwa ni mtu ambaye Mungu atakuonea huruma? Je, ni sababu gani ambayo Mungu anaihitaji ili aweze kumrehemu yule amrehemuye? Na ili amchukie yule amchukiaye? 
Kuna watu wengi sana wanaoishi katika ulimwengu huu. Wengine wanapendwa na Mungu na wengine hawapendwi. Je, hii ina maanisha kuwa Mungu amewakosea? 
Mungu pia ni Mungu wa haki anayezihukumu dhambi za wale ambao wapo kinyume na haki yake. Ni lazima tuepuke namna yoyote ya kutoelewa katika jambo hili kwa kuufahamu mpango wa Mungu uliodhihirishwa katika haki yake kwa imani yetu katika haki ya Mungu. Kuna Wakristo wengi ambao wanapotoshwa ambao mioyo yao ni kama Farao, yaani mioyo yao imefanywa kuwa migumu. Hawa ni aina ya watu ambao wanachukiwa na Mungu, kama aya ya 17 ya sura hii inavyoeleza: “Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.”
Sisi sote tuna mapungufu mbele za Mungu. Hivyo hatupaswi kuwa kama Farao. Je, Mungu atuchukie sisi ambao ni wagumu kama Farao kwa kutokuamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani kama ukombozi wetu? Ndiyo. Watu kama Farao wanageuka na kuwa kinyume na Mungu. Watu wa jinsi hiyo wanajidai na kutegemea haki yao wenyewe, lakini haki yao wenyewe haiwezi kuwakomboa toka katika dhambi zao. 
Je, Farao alitegemea kitu gani? Farao aliutumainia na kuutegemea Mto Naili. Alifikiri kuwa kwa kuwa maji ya Mto Naili yanaendelea kutiririka kwa wingi, basi kila kitu kitakuwa shwari. Hii ndio sababu Mungu anawachukia watu kama Farao. Mtu yeyote ambaye moyo wake ni mgumu kama ule wa Farao atachukiwa na kulaaniwa na Mungu. Hupaswi kuwa kama Farao. Badala yake unaweza kufanyika kuwa mtoto wa Mungu kwa kuupokea upendo mkuu wa Mungu ambao amekupatia bure. 
 

Je, Unakubalina Kwa Furaha na Mpango wa Haki ya Mungu?
 
Je, moyo wako umejiandaa kuupokea upendo wa haki ya Mungu uliopangiliwa kwa ajili yako katika mpango wake? Kuna baadhi ya watu ambao pamoja na kuwa wanamwamini Yesu, wanaendelea kuteseka kwa huzuni kwa kuwa wameuelewa vibaya mpango wa Mungu. Watu wa jinsi hiyo wanashangaa, “Ninamwamini Yesu, je, ni kweli kuwa Mungu amenichagua? Kama hajanichagua imani yangu ina faida gani? Sasa nifanye nini? Siwezi kuacha kumwamini Yesu; nifanye nini? Kwa kweli ninamwamini Yesu, lakini nini kitatokea ikiwa simo katika chaguo lake?” 
Kisha wanaweza kuanza kujifariji wao wenyewe kwa kufikiria, “Kwa kuwa ninamwamini Yesu na ninahudhuria Kanisani, basi ni dhahiri kuwa Mungu amekwisha nichagua mimi. Kwa kweli huo ndio ukweli wenyewe!” Lakini wanapoangukia katika dhambi wanajikuta wakishangaa tena, “Inawezekana kuwa Mungu hajanichagua! Pengine huu ndio wakati wa mimi kuacha kumwamini Yesu!” Kwa maneno mengine, wanajifikiria wao wenyewe, wanahitimisha wao wenyewe, na wanamalizia kila kitu wao wenyewe. Watu hawa wanahitaji maalum la kuufikiria upya uelewa wao wa mpango wa Mungu ili waweze kupata ufahamu sahihi na kuamini katika Yesu kuwa ni Mwokozi wao. 
Kwa upande mwingine, wale wanaoyaamini zaidi mafundisho ya watheolojia kuliko Neno la Mungu mwenyewe wanaweza kusema, “Je, Mungu hakusema kuwa mkubwa atamtumikia mdogo, na kwamba alimpenda Yakobo huku akimchukia Esau hata kabla hawajazaliwa? Kwa kuwa sasa tunamwamini Yesu, basi ni dhahiri kuwa tulipangiwa kuokolewa hata kabla ya kuzaliwa kwetu.” Lakini Mtume Paulo anatueleza kuwa kuchaguliwa tangu asili kulikopangwa na Mungu ni “kusimama, si kwa sababu ya matendo bali kwa sababu ya nia yake aitaye.”
Kuifuata sheria hakumfanyi mtu kuwa mtoto wa Mungu. Tunaweza kufanyika watoto wa Mungu kwa kuwa na imani katika haki ya Mungu na rehema zake na upendo ulioonyeshwa na ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. 
Kutokana na mafundisho ya dini yaliyowekwa na watheolojia, watu wengi hawawezi kuuamini ubatizo wa Yesu na damu yake, ambavyo ni udhihirisho wa haki ya Mungu kuwa wokovu wao. Wale ambao wameusikia upendo wa injili ambao kwa huo Mungu ameionyesha haki yake bado hawaamini kama Farao. Mungu anawachukia wale ambao wanajaribu kufanyika watoto wa Mungu kwa kumwamini Yesu kulingana na fikra zao wenyewe hali wakishindwa kuiamini haki ya Mungu iliyofunuliwa katika Yesu Kristo. 
Ikiwa huuamini upendo wa haki ya Mungu ulioonyeshwa kwa kupitia Yesu Kristo, basi sasa ni wakati wako kufanya hivyo. Hapo ndipo utakapoweza kuvikwa upendo wa Mungu. Kwa asili sisi sote tulikuwa kama Esau, lakini kuna wakati mmoja tuliokolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kuamini katika upendo wa haki ya Mungu. Sisi tumeupokea upendo wa Mungu wenye baraka kwa kuiamini haki yake. 
Mungu ameiruhusu baraka kwa Waisraeli na Wamataifa wanaoamini katika haki yake kufanyika watoto wa Mungu. Kama Mungu alivyosema, “Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.” Mungu ametupatia injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake na pia ametupatia sisi tunaoiamini injili hiyo upendo wa haki yake. 
Kifungu kifuatacho, “Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, ‘Ninyi si watu wangu,’ Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.” Ni Neno la Mungu ambalo limetimizwa kwetu hivi leo. Hivyo, tunaweza kutambua kuwa kwa kuwa tulikuwa na mapungufu mbele za Mungu, Mungu alituokoa kwa kuja kwetu katika mwili na kuufanya upendo wa haki yetu kupatikana kwetu. 
Kule kusema kuwa wewe na mimi tumeokolewa toka katika dhambi zetu mbele za Mungu ni upendo wa ukombozi ambao ulikuwa umepangwa ndani ya haki ya Mungu. Kukombolewa toka katika dhambi zetu zote kwa kuuamini upendo wa haki ya Mungu pasipo kuifanya mioyo yetu kuwa migumu, kunawezekana tu kwa imani katika ukweli. Mbali na na njia hii ya imani, hakuna njia nyingine inayoweza kutusaidia kupokea ondoleo la dhambi. Sisi sote tunazaliwa tukiwa na mioyo migumu, lakini Neno la Mungu linaweza kuishinda mioyo yetu. Hapo ndipo mioyo yetu inapoweza kuongozwa na amani ya Mungu. Ikiwa unamwamini Mungu, basi haki ya Mungu itakuwa yako. 
Ikiwa injili ya ukweli ambayo ina haki ya Mungu haipo, basi kila mtu katika ulimwengu huu atakuwa akikabiliana na maangamizi yake. Pasipo kuwapo wale wanaoihubiri injili ya maji na Roho basi wanadamu wote wangekuwa wamepoteza matumaini yao. Na kama isingekuwa kwa ajili ya wale ambao wamefunikwa katika upendo wa haki ya Mungu, basi ulimwengu huu mzima ungelikuwa umeshafikia mwisho wake hali kila mtu akihukumiwa adhabu kwa sababu ya dhambi zake. Lakini Mungu ametuacha sisi hapa duniani, sisi tunaoamini katika upendo wa haki yake. Sisi tunaweza kumshukuru Mungu kwamba anafanya kazi kupitia sisi pamoja na kuwa tuna madhaifu na mapungufu mengi. 
Imani ambayo imefunikwa katika upendo wa haki ya Mungu ndiyo haki ambayo ambayo inatoka katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. Imani katika haki ya Mungu inapatikana katika moyo ambao unaamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake. Sisi tunakombolewa toka katika dhambi zetu kwa imani yetu katika haki ya Mungu. Ukweli huu ndio mpango, kuchaguliwa tangu asili, na uchaguzi ambao Mungu ameuweka kwa ajili yetu. 
Mungu amesema kuwa yeyote anayeliamini Neno la Mungu ambalo linaitimiza haki yake katika Yesu Kristo ataokolewa toka katika dhambi zake. Mtu anaweza kukutana na maangamizi si kwa sababu haki ya Mungu haijaondolea dhambi zote, bali kwa sababu ya moyo wake mgumu ambao haujaiamini haki ya Mungu. 
Tunapaswa kuifanya mioyo yetu kuwa minyenyekevu mbele za Neno la Mungu na kuamini katika injili ya maji na Roho. Mioyo yetu ni lazima ipige magoti mbele zake. Sisi tulibarikiwa kwa kuamini katika upendo wa haki ya Mungu. Mungu alituokoa toka katika dhambi zetu zote kwa kuwa alikuwa akituonea sana huruma. Tunamshukuru Mungu. Sisi ambao tunaamini katika haki ya Mungu hatuna kitu tunachoweza kukionea aibu. Na badala yake tuna kila sababu ya kujivunia haki yake. 
Mungu ametuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi zetu kwa sababu sisi tumepungukiwa mbele zake—tumsifu Bwana kwa wokovu huu! Ili tuweze kupendwa na Mungu basi ni lazima tuweze kuiamini haki yake. 
Je, unaifahamu hii yaki ya Mungu? Ikiwa ndivyo, basi iamini haki hiyo. Hapo ndipo upendo wa haki ya Mungu utakapokuja katika moyo wako. Imani yako katika upendo wa haki ya Mungu na iwe mbali na kuelewa vibaya. 
Upendo wa ukombozi ambao Mungu ameuwekwa kwa jili yako na uje katika moyo wako. Halleluya! Ninatoa shukrani kwa Mungu utatu ambaye ametufanya sisi kuwa watoto wake katika haki yake.