Search

Mahubiri

Somo la 11: Maskani

[11-22] Mafumbo Manne Yaliyofichika Katika Mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 26:1-14)

Mafumbo Manne Yaliyofichika Katika Mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania
(Kutoka 26:1-14)
“Kisha fanya hiyo maskani iwe na mapazia kumi; ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya bluu, na ya zambarau, na nyekundu, pamoja na makerubi; kazi ya fundi stadi. Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa ishirini na nane, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne; mapazia yote yatakuwa ya kipimo kimoja. Mapazia matano yataungwa pamoja, hili na hili; na mapazia matano mengine yataungwa pamoja, hili na hili. Kisha utafanya tanzi za rangi ya bluu upande wa mwisho wa pazia moja katika ule upindo wa fungu lake, vivyo utafanya upande wa mwisho wa ile pazia iliyo, katika fungu la pili. Fanya matanzi hamsini katika pazia moja, na matanzi hamsini katika upande wa mwisho wa ile pazia ilio katika kuungana kwa pili; hizo tanzi zitaelekeana. Kisha ufanye vifungo hamsini vya dhahabu, na kuunganya hayo mapazia pamoja kwa vile vifungo; na hiyo maskani itakuwa ni moja. Nawe fanya mapazia ya singa za mbuzi yawe hema juu ya maskani; fanya mapazia kumi na moja. Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa thelathini, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne; hayo mapazia kumi na moja yatakuwa ya kipimo kimoja. Kisha utaunganya mapazia matano mbali, na mapazia sita mbali, na lile pazia la sita utalipeta hapo upande wa mbele wa ile hema. Fanya tanzi hamsini upande wa mwisho wa pazia lile lililo la mwisho katika hayo yaliyounganywa pamoja, na tanzi hamsini upande wa mwisho wa lile pazia lililo nje katika hayo ya pili yaliyounganywa pamoja. Tena ufanye vifungo hamsini vya shaba, na kuvitia vile vifungo katika zile tanzi, na kuiunganya ile hema pamoja, ili iwe hema moja. Na kipande kile kilichosalia, kile kiangukacho, cha yale mapazia ya hema, ile nusu ya pazia iliyosalia, itaanguka huko upande wa nyuma wa maskani. Na hiyo dhiraa moja upande mmoja, na ile dhiraa moja upande wa pili, ya urefu wa mapazia ya hema uliosalia, zitaanguka katika ubavu wa maskani upande huu na upande huu, ili kuifunika. Nawe fanya kifuniko cha ile hema cha ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.”
 


Mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania

 
Sasa tunageukia katika mapazia ya Hema Takatifu la Kukutania. Mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania yaliundwa katika sehemu nne. Wakati Mungu alipomwambia Musa kulijenga Hema Takatifu la Kukutania alimpatia maelekezo ya kina na ya wazi. Kipekee, paa la kwanza liliweza kuonekana toka tu ndani ya Hema Takatifu la Kukutania, ambalo ni paa juu ya mbao za Hema Takatifu la Kukutania na vyombo vyake vyote vya ndani. Paa hili lilikuwa limezifunika mbao za Hema Takatifu la Kukutania, Mahali Patakatifu, na Patakatifu pa Patakatifu na kutelemka hadi chini ya ardhi. Na lilikuwa limetengenezwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, na pia picha nzuri ya za makerubi zilikuwa zimefumwa juu yake. 
Paa la kwanza liliundwa kwa dazani kubwa mbili za mapazia yaliyokuwa yameunganishwa kila moja kwa jingine, kila pazia liliundwa kwa kuyaunga mapazia madogo matano yaliunganishwa kwa kila moja. Ili kuziunganisha dazani hizi mbili, basi vitanzi hamsini vya nyuzi za bluu vilitengenezwa katika kona zinazo yaunganisha mapazia. Vifungo vya dhahabu viliunganishwa katika vitanzi hivi vya nyuzi za bluu hali vikiunganisha zile dazani mbili za mapazia ili kulifanya paa moja kubwa. 
Pazia la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania liliundwa kwa mapazia kumi ambayo yalikuwa yameunganishwa katika seti mbili za mapazia mapana. Urefu wake ulikuwa ni dhiraa 28. Dhiraa ni sawa na sentimita 45 (futi 1.5), na hivyo urefu ulikuwa ni mita 12.6 (futi 41.6) katika vipimo vya kisasa, upana wa kila pazia ulikuwa ni dhiraa nne, ambazo ni sawa na mita 1.8 (futi 5.9). Mapazia matano yaliungwa kwanza pamoja ili kufanya seti mbili za mapazia, na kisha seti hizi mbili ziliunganishwa pamoja kwa vitanzi hamsini vya nyuzi za bluu na vifungo hamsini vya dhahabu. Hivi ndivyo paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania lilivyokamilishwa. Lakini kulikuwa na mapaa matatu zaidi. Paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania lilitengenezwa kwa kuyafuma mapazia kwa kazi ya fundi stadi kwa kuyafuma makerubi kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. 
Hii ilikuwa kwa ajili ya kutuonyesha njia kwenda katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa mfano, nyuzi za bluu zilizotumika katika paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania linaonyesha juu ya ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana ili kuzichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake. Kwa kubatizwa, Yesu alizichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake (Mathayo 3:15). Kwa sababu Yesu alizichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake mwenyewe kwa kupitia ubatizo wake, basi huu ubatizo kwa sasa umefanyika kuwa ni mfano wa wokovu (1 Petro 3:21).
Paa la pili la Hema Takatifu la Kukutania liliundwa kwa singa za mbuzi (Kutoka 26:7). Urefu wake ulikuwa ni mrefu zaidi kuliko lile paa la kwaza kwa sentimita 90 (futi 3). Katika dhiraa 30, urefu ulikuwa ni mita 13.5 (futi 45), na katika dhiraa 4, upana ulikuwa ni mita 1.8 (futi 5.9). Paa hili lilifanywa kwa mapazia kumi na moja yaliyokuwa yameunganishwa kila moja kwa jingine katika seti mbili za mapazia moja likiwa na mapazia matano na jingine likiwa na mapazia sita. Mapazia haya mawili yaliunganishwa pamoja kwa vifungo vya shaba. 
Paa hili la pili la Hema Takatifu la Kukutania, lililofanywa kwa singa za mbuzi linatueleza kuwa Yesu ametufanya sisi kuwa watakatifu kwa haki ya Mungu. Kwa kuja hapa duniani, Bwana wetu alipofikisha umri wa miaka 30 alibatizwa na Yohana kwa ridhaa yake mwenyewe, akazipokea dhambi za ulimwengu katika mwili wake. Kama matokeo ya hili, Bwana alizibeba dhambi za ulimwengu hadi Msalabani, alisulubishwa, akazitoweshea mbali dhambi zetu mara moja na kwa wote, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi wetu. Kwa hiyo paa la pili, paa jeupe la singa za mbuzi linatueleza sisi kuwa Yesu Kristo ambaye alifanyika kuwa mbuzi wa kisingizio alitufanya sisi kuwa tusio na dhambi kwa ubatizo wake na damu yake. 
Paa la tatu la Hema Takatifu la Kukutania lilitengenezwa kwa ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, hii inatueleza kuwa Yesu alizibeba dhambi zetu kwa kubatizwa, akazibeba dhambi zetu hadi Msalabani, akaimwaga damu yake na kuhukumiwa, na kwa hiyo ametukomboa toka katika dhambi zetu zote. 
Paa la nne la Hema Takatifu la Kukutania lilifanywa kwa ngozi ya pomboo. Maana ya ngozi ya pomboo ni kuwa Yesu Kristo anapotazamwa kwa mwonekano wake wa nje hakuwa na kitu cha kutamanisha. Lakini huyu Yesu alikuwa ni Mungu mwenyewe. Ngozi ya pomboo inatuonyesha sisi juu ya taswira ya Yesu Kristo ambaye alijishusha hadi chini katika kiwango cha wanadamu ili aweze kutuokoa toka katika dhambi za ulimwengu.
Hebu sasa tuyachunguze haya mapaa manne ya Hema Takatifu la Kukutania kwa kina zaidi.
 

Maana ya Kiroho ya Paa la Kwanza la Hema Takatifu la Kukutania
 
Maana ya Kiroho ya Paa la Kwanza la Hema Takatifu la Kukutania
Vifaa vya kwanza vilivyotumika katika paa la kwanza kati ya yale mapaa manne ya Hema Takatifu la Kukutania vilikuwa ni nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Lilifanywa katika njia ambayo rangi hizi nne ziliweza kuonekana kwa wazi kabisa toka ndani ya Hema Takatifu la Kukutania. Pia, urembo wa fundi stadi wa makerubi ulikuwa umefumwa juu yake ili kwamba makerubi haya yaliangalie toka juu lile Hema Takatifu la Kukutania. Maana ya kiroho inayojichika katika kila hizi nyuzi nne ni kama ifuatavyo. 
Fumbo la nyuzi za bluu linalodhihirishwa katika vifaa vya paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania ni kwamba Masihi alizipokea dhambi zote za ulimwengu mzima kwa kupitia ubatizo wake mara moja na kwa wote. Alikuja hapa duniani na alibatizwa na Yohana Mbatizaji ambaye ni mwakilishi wa wanadamu wote ili kuzibeba dhambi zote za ulimwengu kama ambavyo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa wa Agano la Kale alivyoyapokea maovu ya wenye dhambi yaliyokuwa yamepitishwa kwake kwa kuwekewa mikono. Pia linatueleza ukweli kuwa Yesu alizioshelea mbali dhambi zote za ulimwengu kwa kuibeba adhabu ya dhambi hizi mara moja na kwa wote. 
Kwa upande mwingine, nyuzi za zambarau zinatueleza kuwa Yesu Kristo aliyekuja hapa duniani ni Mfalme wa wafalme na Mungu mkamilifu kwetu. Nyuzi hizi zinatueleza kuwa Yesu ni Mungu mwenyewe katika ile hali yake. Nyuzi nyekundu zilizodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania zinatueleza sisi kuwa Yesu, baada ya kuwa amezipokea mara moja dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo wake ambao aliupokea toka kwa Yohana, aliimwaga damu yake Msalabani na kwa hiyo akabeba adhabu ya dhambi zetu hizi kwa haki badala yetu. 
Ubatizo wa Yesu na kifo chake Msalabani ulikuwa ni sawa na utaratibu wa sadaka ya kuteketezwa katika kipindi cha Agano la Kale ambapo sadaka zisizo na mawaa ziliyapokea maovu ya wenye dhambi kwa kuwekewa mikono na kisha kumwaga damu hadi kifo ili kubeba adhabu ya dhambi hizi. Vivyo hivyo, katika Agano Jipya, Yesu alibatizwa, akaenda Msalabani na akaimwaga damu yake na kufa juu yake. 
Biblia inamuelezea Yesu Kristo kuwa ni sadaka ya dhabihu. Jina “Yesu” maana yake ni “Yeye atakayewakomboa watu wake toka katika dhambi zao” (Mathayo 1:21). Na jina “Kristo” maana yake “mpakwa mafuta”. Katika Agano la Kale, watu wa aina tatu ndio waliopaswa kupakwa mafuta; wafalme, manabii, na makuhani. Kwa hiyo, jina “Yesu Kristo” linamaanisha kuwa yeye ni Mwokozi, Mungu mwenyewe, Kuhani Mkuu wa Ufalme wa Mbinguni, na Bwana wa ukweli unaodumu. Kwa kuja hapa duniani, kwa kubatizwa na Yohana, na kwa kuimwaga damu yake, Yesu amefanyika kuwa ni Mwokozi wetu wa kweli. 
Vivyo hivyo, paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania linaonyesha kuwa Masihi atakuja kwa kupitia nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa na kwa hiyo atawaokoa wale wanaomwamini toka katika dhambi zao na adhabu ya dhambi. Huduma hizi si nyingine bali ni ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani. Fumbo la wokovu linavyodhihirishwa katika nyuzi hizi za rangi nne ni kuwa Masihi alikuja hapa duniani, alizichukua dhambi za mwanadamu katika mwili wake kwa kubatizwa, alisulubiwa hadi kifo, kisha akafufuka tena toka kwa wafu. 
Kwa huduma hizi, Yesu Kristo amewaokoa wale wanaomwamini toka katika dhambi zao na amewafanya kuwa watu wa Mungu. Yesu Kristo ni Mfalme wa wafalme na sadaka ya kuteketezwa ambayo imeyatoweshea mbali maovu ya wenye dhambi, na amewakomboa wale wanaoamini toka katika dhambi zao zote na adhabu ya dhambi. 
 

Maana ya Kiroho ya Paa la Pili la Hema Takatifu la Kukutania
 
Maana ya Kiroho ya Paa la Pili la Hema Takatifu la Kukutania
Vifaa vilivyotumika katika paa la pili ni singa za mbuzi. Hii inatueleza sisi kuwa Masihi atakayekuja atawahalalisha wanadamu kwa kuwakomboa toka katika dhambi zao na adhabu ya dhambi hizi. Kwa maneno mengine inaonyesha kuwa ili mwanadamu aweze kupokea haki ya Mungu, basi ni muhimu sana kwao kuamini katika injili ya maji, damu, na Roho. Haki ya Mungu imeioshelea mbali mioyo yetu kuwa myeupe kama theluji, na kwa hiyo imetuwezesha kupokea ondoleo la dhambi zetu. 
 
 
Maana ya Kiroho ya Paa la Tatu la Hema Takatifu la Kukutania
 
Maana ya Kiroho ya Paa la Pili la Hema Takatifu la Kukutania
Vifaa vilivyotumika kwa paa la tatu la Hema Takatifu la Kukutania vilikuwa ni ngozi za kondoo waume zilizokuwa zimetiwa rangi nyekundu. Hii inadhihirisha kuwa Masihi atakuja hapa duniani, atazichukua dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa, atasulubiwa, na kwa hiyo atafanyika kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi za watu. Damu ambayo Yesu Kristo aliimwaga Msalabani ililipa mshahara wote wa dhambi ambao ni kifo kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. Kwa maneno mengine, inatueleza sisi kuwa Yesu Kristo mwenyewe alifanyika kuwa sadaka ya kuteketezwa na kwa hiyo amewaokoa watu wake toka katika dhambi zao (Mambo ya Walawi 16). 
Katika Siku ya Upatanisho, mbuzi wawili wa kuteketezwa waliandaliwa ili kuzichukua dhambi zote za watu wa Israeli. Mmoja wa mbuzi hao alikuwa ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ya upatanisho ambayo ilitolewa kwa Mungu kwa ajili ya dhambi zao. Kwa wakati ule Kuhani Mkuu aliiweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi wa kwanza wa sadaka ya kuteketezwa hali akizipitisha dhambi zote za watu wake juu ya mwanasadaka huyu. Kisha aliichukua damu yake, akainyunyizia upande wa mashariki mwa kiti cha rehema na mbele ya kiti cha rehema mara saba. Hivi ndivyo sadaka ya upatanisho wa Israeli ilivyotolewa kwa Mungu. 
Kisha, hali waisraeli wakishuhudia, yaani wale waliokuwa wamekusanyika kulizunguka Hema Takatifu la Kukutania, Kuhani Mkuu aliiweka mikono yake juu ya yule mbuzi mwingine wa kisingizio aliyesalia na akazipitisha dhambi za mwaka mzima za watu wa Israeli juu yake. Hii ilikuwa ni lengo la kuwapatia watu wa Israeli uhakika kuwa dhambi zao zote za mwaka uliopita zilikuwa zimechukuliwa mbali nao kwa kule kuwekea mikono kulikofanywa na Kuhani Mkuu. Kisha huyu mbuzi wa kisingizio alipelekwa jangwani ili kukutana na kifo chake hali akiwa amezibeba dhambi zao zote (Mambo ya Walawi 16:21-22). Hii ilikuwa ni ahadi ya Mungu kuwa Masihi atakuja hapa duniani, atazichukua katika mwili wake dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji ambaye ni mwakilishi wa wanadamu (Mathayo 11:11-13, 3:13-17), atabeba adhabu ya dhambi hizi kwa kusulubiwa kwa hiari yake na kwa hiyo atawaokoa watu wake toka katika dhambi zao zote.
 

Maana ya Kiroho ya Paa la Nne la Hema Takatifu la Kukutania
 
Maana ya Kiroho ya Paa la Nne la Hema Takatifu la Kukutania
Ngozi ya pomboo inatuonyesha sisi sura yetu wenyewe na pia juu ya sura ya Bwana alipokuja hapa duniani. Bwana wetu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu ili kuwaita wenye dhambi na kuwafanya kuwa wenye haki. Ngozi ya pomboo pia inatueleza sisi kuwa Yesu Kristo hakujikweza juu alipokuja hapa duniani bali alijishusha mwenyewe kama mwanadamu na akazaliwa kwa unyenyekevu. 
Katika kipindi cha Agano la Kale, Mungu alisema kwa kupitia manabii wake kuwa Masihi atakuja na kuwakomboa wenye dhambi wa dunia hii toka katika maovu yao. Tunaweza kuona kuwa Mungu alilitimiza Neno la unabii lililokuwa limezungumzwa kwa kupitia watumishi wake kwa ubatizo wa Yesu Kristo na damu yake Msalabani. Ahadi hii ya unabii ni Neno la agano kuwa Masihi atazibeba sio tu dhambi za watu wa Israeli bali dhambi zote na adhabu ya dhambi za kila mtu ulimwenguni, na kwamba atawaokoa waamini wake wote na kuwafanya kuwa watu wake mwenyewe. 
Kutoka 25 inazungumza juu ya vifaa vilivyotumika katika kulijenga Hema Takatifu la Kukutania. Vifaa hivi vya Hema Takatifu la Kukutania vilijumuisha nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa, singa za mbuzi, ngozi za kondoo zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi za pomboo, dhahabu, fedha, shaba, mafuta ya manukato, na mawe au madini ya thamani. Vifaa hivi vyote vinadhihirisha kuwa Masihi atakuja hapa duniani na atawaokoa watu wake toka katika dhambi zao kwa kupitia ubatizo na kuimwaga damu yake. Kwa hiyo, katika Hema Takatifu la Kukutania kumefichika mpango wa Mungu wa kina wa wokovu ambao Mungu aliufanya ili kuwaokoa watu wake toka katika dhambi zao. 
Kwa nini Mungu aliamuru zitumike nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu kutumika katika mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania? Na kwa nini aliamuru kutumia singa za mbuzi, ngozi za kondoo waume, na ngozi za pomboo? Ni lazima tuuzingatie mpango ambao aliufanya ili kuweza kutukomboa toka katika dhambi za ulimwengu. Ni lazima tuamini katika huduma zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ambazo kwa hizo Yesu amewaokoa watu wake toka katika dhambi zao kama walivyo, na kwa hiyo ni lazima tuokolewe toka katika dhambi zetu na kufanyika watu wa Mungu. Kwa maneno mengine, ni lazima tufahamu na kuamini katika mpango wa Mungu uliodhihirishwa katika mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania.
 

Kwa Mbinu Nne
 
Mapaa manne ya Hema Takatifu la Kukutania yanatueleza kwa kina juu ya mbinu au njia ambazo kwa hizo Mungu ametukomboa sisi toka katika dhambi zetu: Masihi atakuja hapa duniani katika mwili, atazichukua katika mwili wake dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana, atasulubiwa kwa adhabu ya dhambi hizi, na ataziondoa dhambi za watu wake na kuwaokoa toka katika dhambi zao kwa damu yake mwenyewe. Hata hivyo, wokovu huu unatimizwa tu kwa wale wanaoamini katika Masihi kuwa ni Mwokozi wao. Sisi sote ni lazima tuamini kuwa Yesu Kristo, kama alivyodhihirishwa katika vifaa ya mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania, alikuja kwa ubatizo na Msalaba na kwa hiyo ametuokoa sisi kwa hakika mara moja na kwa wote toka katika dhambi zetu zote. 
Kwa mujibu wa unabii wa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizodhihirishwa katika mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania, Mwana wa Mungu alikuja kwetu kama sadaka ya kuteketezwa ya kipindi cha Agano Jipya, alibatizwa, na akaimwaga damu yake kwa kusulubiwa Msalabani. Zaidi ya yote, kwa kuamini katika Masihi aliyefunuliwa katika mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania basi tunaweza kumpatia Mungu sadaka ya imani inayotuokoa sisi. 
Kwa hiyo, ni lazima tuamini katika ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Ikiwa mtu yeyote haji mbele za Mungu na anashindwa kutoa sadaka ya imani kwa kuamini katika huduma za Yesu zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, basi kwa hakika mtu huyo ataangamizwa kutokana na dhambi zake mwenyewe. Lakini ikiwa mtu ataamini katika ukweli huu, anaweza kwenda mbele za Mungu kwa imani yake katika wokovu wakati wowote kama mwana wa Mungu. Hema Takatifu la Kukutania linatuonyesha sisi kuwa hakuna mtu ambaye hamwamini Yesu Kristo ambaye alifanyika kuwa sadaka ya kuteketezwa na aliyedhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau na nyekundu anayeweza kuingia katika Ufalme wa Mungu. 
Kwa hiyo mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania yanatuonyesha sisi njia ya kwenda Mbinguni. Ni lazima tuitafute njia ya kuingilia katika Ufalme wa Mbinguni kwa kuamini katika ukweli uliofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Mtu yeyote anayetaka kuingia katika Ufalme wa Mungu ni lazima kwanza atatue tatizo lake la dhambi kwa kuamini katika ukweli wa ondoleo la dhambi uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Kwa hiyo, watu wanaweza kufanya uchaguzi wautakao yaani kuingia katika Kanisa la Mungu kwa kuamini katika ukweli huu au kukataliwa na Mungu kwa kutokuamini katika ukweli huu. 
Kwa kweli, dhamiri zetu ziko huru kuamini au kutoamini katika ukweli huu wa wokovu uliofunuliwa katika mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania. Lakini ni lazima utambue kuwa matokeo ya kutokuamini katika ukweli huu yatakuwa ni pigo kubwa kwa mtu yeyote. Hata hivyo, ili sisi tuweze kuingia katika Nyumba ya Mungu inayong’aa kwa mujibu wa mapenzi yake, basi ni lazima tuokolewe milele toka katika dhambi zetu kwa kuamini katika ubatizo ambao Masihi aliupokea toka kwa Yohana na damu yake Msalabani. Watu wote ni lazima wapokee na kukubali katika mioyo yao kuwa ubatizo huu wa masihi na damu yake ya Msalaba vimewaondolea dhambi zao zote. Ni hapo watakapoamini hivyo ndipo wanapoweza kupokea ondoleo la dhambi la milele na kuingia katika utukufu wa Mungu. 
Paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania lilifumwa kwa nyuzi za aina nne tofauti, na lilikuwa limelazwa chini ya paa la pili lililokuwa limeundwa kwa singa za mbuzi. Hii inatuonyesha ukweli kuwa sisi tuliweza kupokea ondoleo la dhambi kutokana na huduma za Yesu: ambazo ni ubatizo wake na damu yake. Kwa hiyo, ondoleo la dhambi ambalo tumelipokea kwa kuamini katika haki ya Mungu linajengwa katika imani yetu katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizodhihirishwa katika paa la kwanza. Ili kuona jinsi ambavyo ukweli huu ni wa msingi, hebu tuligeukie Neno la Biblia lifuatalo hapa chini. 
Isaya 53:6 inasema, “Na BWANA ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.” Waebrania 9:28 inatangaza kuwa, “Kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi.” Na 2 Wakorintho 5:21 iansema, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.” Kwa hiyo vifungu hivi vyote vinatueleza sisi kuwa wokovu wetu umetimizwa katika msingi wa huduma za Yesu zilizodhihirishwa katika kitani safi ya nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizotumika katika paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania. Kule kusema kuwa Kristo mwenyewe alisulubiwa msalabani kwa haki na akabeba adhabu ya dhambi zetu katika mwili wake mwenyewe kuliwezekana kutokana na ukweli kuwa alikuwa amekwisha kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, si kwamba ni pale Msalabani ndipo alipozibeba dhambi za ulimwengu wote. 
Wakati Yesu alipozichukua dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa na hivyo kubeba mateso ya kifo Msalabani ili kuzipatanisha dhambi hizo hakuwa na woga. Kinyume chake, Yesu alifurahi! Kwa nini? Kwa sababu ule ulikuwa ndio wakati haswa kwa yeye “kuitimiza haki yote” (Mathayo 3:15). Yesu alibatizwa na akaimwaga damu yake Msalabani ili kutukomboa sisi toka katika dhambi zetu. Yesu alifanya hivyo kwa sababu alitupenda. Hii ndio sababu alikuja hapa duniani, alibatizwa na Yohana, na kwa hiari kabisa akakinywea kikombe cha mateso ya kusulubiwa. Kwa kuwa Bwana alikuwa amezichukua dhambi zetu na mawaa yetu katika mwili wake kwa kupitia ubatizo wake ndio maana aliweza kuimwaga damu yake pale Kalvari kwa haki ili kubeba adhabu ya dhambi zetu hizi.
 

Vifungo Vilivyoliunganisha Paa la Kwanza la Hema Takatifu la Kukutania Viliundwa kwa Dhahabu
 
Paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania liliundwa kwa seti mbili za mapazia ambayo yalikuwa yameunganishwa kwa vifungo vya dhahabu. Kwa kweli hii inatuonyesha kuwa tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mbinguni pale tu tunapoamini katika ukweli wa ondoleo la dhambi uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Kule kusema kuwa seti mbili za mapazia matano kila moja yaliunganishwa kwa vifungo hamsini vya dhahabu kunatuonyesha sisi kuwa tunaweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote pale tunapokuwa na imani ya kweli katika wokovu wake. Katika Biblia, dhahabu inasimama badala ya imani ya kweli inayoamini katika Neno la Mungu. 
Kwa hiyo, kila mmoja wetu ni lazima aamini katika Neno la Mungu lote. Ni muhimu sana kwetu kuwa na imani katika ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu. Kusulubiwa kwa Yesu pekee tu kunakuwa hakuna matokea sana katika wokovu wetu. Kwa nini? Kwa sababu kabla ya kusulubiwa kwake ni lazima kwanza kuwepo na mchakato wa ubatizo wa Yesu ambao kwa huo wenye dhambi wanaweza kuzipitisha dhambi zao juu ya Yesu Kristo. Msalaba unakuwa na muhimu sana kwa wokovu wetu pale tunapoamini kuwa Mungu Baba alimfanya Yesu Kristo kuzipokea dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa.
 
 
Je, Kitani Safi ya Kusokotwa Inatueleza Nini katika Hema Takatifu la Kukutania?
 
Inatueleza kuwa Mungu alifanya kazi miongoni mwetu kulingana na Neno lake pana na la ukweli. Kwa kweli Masihi alikuja hapa duniani na akabeba dhambi zetu na adhabu ya dhambi kwa kupitia ubatizo ambao aliupokea toka kwa Yohana na damu ya Msalaba. Na inatueleza kuwa wokovu wa Mungu umekwishatimizwa kama ambavyo aliahidi katika Neno lake. 
Katika kipindi cha Agano Jipya, kwa kweli Bwana wetu alikuja hapa duniani akazichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, aliimwaga damu hadi kifo, akabeba adhabu yote ya dhambi zetu, na kwa hiyo amezitunza ahadi zote za wokovu. Kwa kubatizwa na Yohana na kusulubiwa, Bwana wetu alikamilisha na kuyatimiza mapenzi ya Mungu Baba. Agano ambalo Mungu alikuwa amelifanya na watu wake wa Israeli lilitimizwa lote kwa kupitia Mwana wake Yesu. 
Je, ni nani basi anayepaswa kuweka mkazo na umakini katika ukweli huu? Je, ni watu wa Israeli tu? Au ni wewe na mimi? 
Ule ukweli kuwa paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania liliunganishwa kwa vifungo hamsini vya dhahabu unatutaka tuwe na imani ya kweli. Ukweli huu unatuonyesha kuwa tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mungu pale tu tunapofahamu na kuamini kwamba Yesu amezioshelea mbali dhambi zetu zote kwa kupitia huduma zake zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizotumika katika paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania. 
Kwa maneno mengine, inatuonyesha kuwa ondoleo la dhambi linapokelewa kwa kuamini tu katika Neno la kweli. Kwa kupitia Neno la Agano la Kale na Agano Jipya, Mungu anatuonyesha sisi kwa kina kuwa tunaweza kuupata wokovu wetu wa kweli kwa kuamini kuwa ubatizo na damu ya Msalaba vilivyodhihirishwa katika mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania vimetuokoa toka katika dhambi zetu zote. 
Kwa kweli Mungu ametuwezesha sisi kuoshwa dhambi zetu zote na kuwa weupe kama theluji kwa kuamini katika ukweli uliofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa zilizotumika katika paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania. Na Mungu amewaruhusu wale walio na imani hii tu kuingia katika Ufalme wake. Ni lazima tufahamu kuhusu mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania na kuyaamini. Kwa kumwamini Yesu Kristo ambaye amekuja kwetu kwa kupitia huduma za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu tunaweza kupata sifa za kufanyika watoto wa Mungu na kupokea utukufu wa kuingia katika Ufalme wa Mungu. 
Wakati Masihi ametuokoa toka katika dhambi zetu zote kwa kupitia kazi zake zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, tunawezaje basi kutoamini katika upendo mkuu wa Mungu wa wokovu na kuukataa? Tunawezaje kulikataa ondoleo la dhambi zetu na Ufalme wa Mbinguni ambavyo vinaweza kupatikana kwa imani tu? Sisi sote ni lazima tuamini katika Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wetu ambaye ametuokoa toka katika dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa na kuimwaga damu yake Msalabani. Ni hapo tu ndipo tunapoweza kufanyika kuwa watu wa Mungu. 
Wale wasioamini katika ukweli wa nyuzi za bluu, zambarau na nyekundu zilizodhihirishwa katika paa la kwanza la Hema Takatifu la kukutania hawawezi kuzioshelea mbali dhambi zao kwa imani. Wale wasioamini katika ukweli huu hawawezi kufanyika watoto wa Mungu. Hii ndiyo sababu ni lazima tuamini katika wokovu uliofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu za mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania, na hivyo ni lazima tupokee uzima wa milele. 
 

Paa la Singa za Mbuzi Lilifanywa Kubwa Kuliko Paa la Kwanza la Hema Takatifu la Kukutania
 
Paa la pili lililokuwa limetengenezwa kwa singa za mbuzi lilikuwa ni kubwa kuliko paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania. Hii ina maanisha kuwa wale wanaosimama kinyume na Mungu hawawezi kuona hata sehemu kidogo ya ule ukweli uliofunuliwa katika paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania. Hii inamaanisha kuwa wale wanaosimama kinyume na Mungu hawawezi kuona hata chembe ya ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Kwa kweli kulikuwa na uhitaji wa kulificha fumbo la ondoleo la dhambi katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu katika paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania. Hii ni kwa sababu Mungu alikuwa amepanga kuwa wale wanaotii na kumhofia yeye ndio wanaoweza kuingia katika Ufalme wake kwa kuamini katika huduma za Yesu zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu.
Hii ndio sababu pia Mungu aliweka makerubi mashariki mwa bustani ya Edeni na upanga uwakao moto uliokuwa ukizunguka pande zote ili kuulinda mti wa uzima mara baada ya kumfukuza mwanadamu aliyekuwa ameanguka katika dhambi (Mwanzo 3:24). Ukweli unaomwezesha mtu kuingia katika Ufalme wa Mbinguni hauruhusiwi kuonekana na yeyote yule pasipo kumwamini Mungu kwanza. Hii ndio sababu Mungu alilifanya paa la pili kwa singa za mbuzi ambalo lilikuwa kubwa kuliko paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania. 
Paa la pili la Hema Takatifu la Kukutania linatuonyesha sisi kuwa tunaweza kufanyika wenye haki pale tu tunapopokea ondoleo la dhambi lililodhihirishwa katika paa la kwanza. Kwa lugha nyingine, Mungu amewaruhusu wale tu wanaoamini katika Neno lake kwa hofu na utiifu, na ambao wanaishikilia injili ya kweli ili kufanyika watu wake. Kwa kuwa hivi ndivyo Mungu alivyoamua, basi hamruhusu kila mtu kuwa mtoto wake ikiwa mtu huyo hataamini kwanza katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ambazo ni ukweli wa ondoleo la dhambi uliopangiliwa na Mungu mwenyewe. Mapenzi ya Mungu ni kuwa wale ambao mioyo yao ni miovu basi hawawezi kutambua hata sehemu ndogo ya fumbo la nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu.
 

Paa la Pili la Hema Takatifu la Kukutania Liliundwa kwa Singa za Mbuzi na Vifungo Vyake Vilikuwa vya Shaba
 
Maana ya kiroho ya vifungo vya shaba ina maanisha juu ya hukumu ya dhambi za watu. Vifungo vya shaba vinatueleza sisi kuwa dhambi zote zinahitaji malipo ya mshahara wa haki yake. Kwa hiyo, vifungo vya shaba vina ukweli kuwa Masihi alipaswa kuimwaga damu yake Msalabani kwa sababu alikuwa amekuja hapa duniani na kuzibeba katika mwili wake dhambi za ulimwengu mara moja na kwa wote kwa kubatizwa. Kwa kuwa Masihi alikuwa amekwisha kuzichukua kwanza dhambi zetu kwa kupitia ubatizo wake ambao aliupokea toka kwa Yohana, ndio maana basi aliweza kuibeba adhabu ya dhambi hizi za ulimwengu kwa damu aliyoimwaga Msalabani. 
Toka katika vifungo vya shaba tunaweza kuigundua sheria ya Mungu inayotuambia sisi kuwa mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23). Kwa hiyo, ni lazima tutambue kuwa Mungu aliitimiza hukumu ya dhambi zetu kwa kupitia Masihi. Kwa kuwa Yesu Kristo alibatizwa na Yohana na kisha akaimwaga damu yake hadi kifo Msalabani, basi hukumu ya dhambi zote za mwanadamu ilikamilika kikamilifu.
Tunapokwenda mbele za Mungu, wewe na mimi ni lazima tufikirie katika dhamiri zetu kuhusu ukweli huu ulivyo. Tunaishi katika ulimwengu huu hali tukitenda dhambi nyingi halisi kila siku katika mioyo yetu, mawazo yetu, na matendo. Hata hivyo, Masihi alizipokea dhambi hizi zote tunazozitenda kila siku, akalipa mshahara wa dhambi hizi kwa gharama ya uhai wake mwenyewe na kwa hiyo ameukamilisha wokovu wetu. Ikiwa hatuna imani katika ukweli wake basi dhamiri zetu zimefungwa kunyauka na kisha kufa. Kwa hiyo, sisi sote ni lazima sasa tuamini katika ukweli huu ili kwamba nafsi zetu zinazokufa ziweze kuokolewa na kuishi tena.
Je, mioyo yetu inatamani kuamini katika ukweli uliodhihirishwa katika vifungo hivi vya shaba? Ukweli ambao vifungo hivi vya shaba unatueleza ni kuwa wakati tulipokuwa hatuwezi kukwepa zaidi ya kuhukumiwa kwa sababu ya dhambi zetu, Masihi alizichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa na kuhukumikiwa adhabu kwa haki kwa ajili ya dhambi hizi kwa niaba yetu. Kwa kweli Yesu alibeba adhabu yote ya dhambi mara moja na kwa wote kwa ubatizo wake na damu yake Msalabani. Kwa kufanya hivyo, Yesu Kristo ametupatia imani inayotuwezesha kuingia katika Ufalme wa Mungu. 
Wakati mtu anapokuwa na dhambi katika moyo wake mbele za Mungu, basi mtu huyo ni lazima atupwe kwenda kuzimu. Kile ambacho tulistahili kukipokea kwa sababu ya dhambi zetu ilikuwa kifo cha milele. Lakini Masihi alifanyika sadaka ya haki kwa ajili ya dhambi zetu na kwa hiyo ametuokoa sisi sote toka katika adhabu ya dhambi. Sisi sote tulistahili kuadhibiwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu, lakini kwa kuamini kuwa Masihi aliadhibiwa kwa niaba yetu tunaweza kuingia katika Ufalme wa Mungu. 
Kwa kuamini katika ukweli huu katika mioyo yetu basi ni lazima tuweze kuondolewa dhambi zetu za ulimwengu na kukwepa adhabu ya dhambi zetu. Ilikuwa ni kwa nia ya kuzifanya hizi kazi za wokovu ndio maana Masihi alizipokea dhambi za ulimwengu kwa kubatizwa na Yohana, na alisulubiwa kwa sababu ya dhambi hizi za ulimwengu. Kwa kufahamu na kuamini katika ukweli huu basi ni lazima tupokee ondoleo la dhambi na ni lazima pia tuokolewe toka katika adhabu ya dhambi. 
Ni lazima tuamini kuwa Masihi angaliweza kuzipokea hizi dhambi zetu katika mwili wake na kubeba adhabu ya dhambi hizi kwa kuja hapa duniani na kuupokea kwanza ubatizo wake katika mfano wa kuwekea mikono. Ikiwa Masihi alizichukua dhambi zetu zote za ulimwengu kwa kupitia ubatizo ambao aliupokea toka kwa Yohana, na kama alisulubiwa ili kulipa mshahara wa dhambi hizi, basi ni lazima sisi tuamini hivyo. Hivyo, kwa wale ambao wanaamini hivyo Mungu anawapatia maisha mapya. 
Kwa sababu tulifungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu, Masihi alizipokea dhambi zetu na akafa kwa niaba yetu na hivyo akabeba adhabu ya dhambi zetu wenyewe. Kwa sisi ambao tulipaswa kufa kutokana na adhabu ya dhambi zetu, basi Bwana wetu alibeba adhabu hiyo kwa niaba yetu na kwa ajili yetu. Ikiwa Bwana alisulubiwa hadi kifo ili kutuokoa toka katika hukumu ya dhambi zetu, basi ni lazima sisi tuamini hivyo. 
Ni lazima tuupokee wokovu wa Bwana katika nafsi zetu, katika vina vya mioyo yetu, si kwa kule kutii kwa midomo yetu bali imani yetu ya kiroho katika Neno lake. Kila mmoja wenu ninyi ambaye ameusikia ujumbe huu ni lazima aamini katika ukweli huu katika moyo wake. Kwa kuwa Masihi ametuokoa kwa ubatizo wake na damu yake, basi wale wanaoamini kwa kweli wanaweza pia kuokolewa. 
Ikiwa watu hawaamini kuwa wamefungwa kuzimu, basi hawawezi kuona umuhimu wa kuokolewa na kumwamini Masihi aliyekuja kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Lakini ikiwa watu wanaamini kuwa kwa hakika walikuwa wamefungwa kuzimu, basi watu hao wataona kwa hakika umuhimu wa wao kuokolewa kwa kuamini katika Masihi huyu aliyekuja kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Hii ndio sababu Yesu alisema, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi” (Marko 2:17). Kwa hiyo wanapoamini katika ukweli huu katika mioyo yao basi kwa hakika watapokea ondoleo la dhambi zao katika mioyo yao. 
Ikiwa tutajiangalia sisi wenyewe hali tukijipima kwa Sheria mbele za Mungu, basi kwa hakika hatuwezi kukana kuwa sisi ni wenye dhambi kabisa na kwamba tunapaswa kulaaniwa kabisa kwa sababu ya dhambi zetu. Si kwamba tunapaswa kukiri tu kwamba tumefungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu, bali ni lazima pia tuwe na nia ya dhati ili kuiepuka hukumu kama hiyo ili kwamba tuweze kuoshelewa mbali dhambi zetu zote kwa kuamini katika ujumbe huu. Hii ndio njia pekee ya maisha ya kubeba hukumu ya haki ya dhambi zetu zote kwa imani. 
Pasipo kuwa na imani katika huduma za Yesu zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu zilizotumika katika Hema Takatifu la Kukutania, basi kwa hakika hivi sasa tungekuwa tunakaribia kabisa kukutana na kuzimu. Ubatizo ambao Masihi aliupokea na damu aliyoimwaga Msalabani kwa kweli vinahusiana kwa undani sana katika wokovu wa nafsi zetu. 
Kwa kuwa tulizaliwa kama wazawa wa Adamu na wenye dhambi, basi sisi tulikuwa tumefungwa kuzimu. Hivyo ni lazima tukiri mbele za Mungu kuwa sisi sote ni wenye dhambi ambao tunaelekea kuzimu moja kwa moja, lakini unaukubali ukweli huu? Wakati Mungu anapotuangalia sisi anaona kuwa tulikuwa tumefungwa kuzimu, na sisi tunapojitazama mbele za Mungu tunajiona wazi kuwa tulikuwa tumefungwa kuzimu pia. Mwokozi wetu alikuja hapa duniani ili kutuokoa sisi toka katika dhambi zetu kwa sababu mimi na wewe tulikuwa tumefungwa kuzimu. 
Kwa kuja hapa duniani, kwa kubatizwa, na kuimwaga damu yake na kufa, Bwana wetu amezitimiza kazi zake za kutuokoa sisi. Kimsingi, ikiwa tungekuwa hatujafungwa kuzimu, basi Bwana wetu asingekuwa na sababu ya kuzifanya kazi za wokovu. Lakini ukweli ni kuwa pamoja na kuwa sisi tuliozaliwa upya hatuna dhambi katika mioyo yetu sasa, lakini ukweli unabakia kuwa tulikuwa na dhambi hapo kabla. 
Yeyote aliye na dhambi ni lazima aende kuzimu. Mshahara wa dhambi ni mauti. Hii ina maanisha kuwa wenye dhambi kwa hakika wametupwa kuzimu. Lakini wale ambao kwa imani wamepokea ondoleo la dhambi lilitolewa na Bwana Yesu Kristo wanaweza kuupata uzima wa milele. Wakati wewe na mimi tulipoamini katika Yesu Masihi kuwa ni Mwokozi wetu, basi Bwana alituokoa sisi toka katika dhambi zetu zote na adhabu ya dhambi katika upendo wake kwetu. Amin! Halleluya!
 
 
Ni Lazima Tujichunguze Sisi Wenyewe Ili Tuone Ikiwa Tuna Imani ya Kweli Iliyotolewa na Bwana katika Mioyo Yetu
 
Hebu tujiangalie sisi wenyewe. Je, wewe na mimi tumeamini kwa mujibu wa sheria ya Mungu? Ikiwa ndivyo, je ni nini basi ambacho kingetutokea sisi mbele za Mungu? Je, hatukuhumiwa sisi kwa sababu ya dhambi zetu? Mungu wetu si Mungu asiye na haki ambaye hawaadhibu wenye dhambi. Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu na mwenye haki, basi yeye hawezi kuivumilia dhambi. Mungu ametueleza sisi kuwa atawatupilia kuzimu wale wote wenye dhambi mbele yake kwa sababu ya kutokuamini. 
Mungu amesema kuwa atawatupa katika moto wa kuzimu mkali unaowaka kwa makaa ambapo hata minyoo haiwezi kufa. Mungu atawatupa kuzimu wale wote wanaojaribu kuzioshelea mbali dhambi zao kwa jitihada zao wenyewe na wanaojifariji mioyo yao wao wenyewe. Hii ndiyo sababu Bwana alisema kwa watu wa jinsi hiyo, “Tokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!” (Mathayo 7:23).
Kwa hiyo, ni lazima tuamini katika Masihi, na ni lazima tuamini katika ubatizo ambao Yesu aliupokea alipokuja hapa duniani, na katika damu ya Msalaba, na ufufuo wake toka kwa wafu. Kwa nini? Kwa sababu kimsingi, sisi sote tulikuwa ni wenye dhambi mbele za Mungu na kwa hiyo sisi sote tulikuwa tumefungwa kuzimu. Hii ndio sababu Masihi alikuja kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, akatoa sadaka ya kuteketezwa ya wokovu kwa mwili wake mwenyewe, na kwa hiyo amezitoweshea mbali dhambi zetu zote. Hivyo ni lazima tuamini kuwa Bwana alibatizwa na kusulubiwa kwa ajili yetu. Ikiwa sisi hatuwezi kutambua kuwa tulikuwa tumefungwa kuzimu, basi hatutakuwa na kitu chochote cha kufanya na Bwana wetu. 
Hata hivyo, watu wengi hawafikirii kuwa walipaswa kufungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zao. Wanafikiria kuwa wanafanya vizuri kuwaulizia madaktari wao. Watu wa jinsi hiyo ni wale wanaomchukulia Yesu kuwa ni mtu mpole na mwenye tabia nzuri, mwenye kuheshimiwa na mwalimu, na pia ni watu wanaomwamini Yesu ili kujifanya tu kuwa wao ni watu wenye tabia njema. Bwana wetu alisema kwa watu wa jinsi hiyo, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi” (Mathayo 9:12). Ni lazima waichunguze mioyo yao kwa upana toka katika mtazamo wa kibiblia sasa hivi ili kwamba wasije wakaishia kuzimu. 
Sababu inayotufanya tuamini katika Masihi ni ili kwamba tuweze kuondolewa dhambi zetu zote kwa kumwamini yeye kuwa ni Mwokozi wetu. Sisi hatumwamini Masihi ili kujenga heshima zetu. Bali, ni kwa sababu ya dhambi zetu ndio maana ni muhimu sana kwako wewe na mimi kumwamini Masihi. Hii ndiyo sababu tunaamini: kwamba Yesu Masihi alizaliwa hapa duniani; kwamba alibatizwa na Yohana alipokuwa na umri wa miaka 30; kwamba alizibeba dhambi za ulimwengu na kuimwaga damu yake kwa kusulubiwa kwake; kwamba alifufuka tena toka kwa wafu baada ya siku tatu; kwamba alipaa mbinguni; na kwamba sasa anakaa kuumeni kwa mkono wa Mungu Baba—mambo haya yote yanabeba ushuhuda kwa ondoleo letu la dhambi. Kwa kuwa vitu hivi vyote vilikuwa ni kazi za Mwokozi aliyetuokoa sisi toka katika dhambi zetu zote, basi kwa hakika sisi tunapaswa kuziamini hizo kazi zote bila kuacha hata moja. 
Inaweza kuonekana sawa katika mawazo yetu binafsi kuyatengeneza mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania kwa kufuma tu nyuzi fulani nzito, lakini katika Biblia Mungu anatoa vipimo maalum juu ya jinsi ambavyo mapaa hayo yalivyopaswa kutengenezwa, inakuwaje baadhi ya vifungo vilipaswa kutengenezwa kwa dhahabu na vingine kwa shaba. Unafikiria ni kwa nini Mungu aliamuru hivyo? Aliamuru hivyo kwa sababu vitu vyote vililenga kumaanisha maana ya kiroho kwetu sisi. Hii ndiyo sababu hatuwezi kukidharau hata kimojawapo.
 


Ni Lazima Kwa Hakika Tuamini Katika Ubatizo na Damu ya Yesu Kristo Aliyefanyika Kuwa Masihi

 
Sisi tulipaswa kutupwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu, lakini Yesu Kristo Masihi alikuja hapa duniani na ametuokoa toka katika dhambi zetu. Kwa kweli Yesu alibatizwa, akasulubiwa, na akamwaga damu yake. Kwa hiyo, ni kinyume cha sheria kwetu sisi kusema kuwa hatuna dhambi pasipo kwanza kuamini katika mioyo yetu juu ya ubatizo wa Yesu na damu ya Msalabani. Yesu ambaye amefanyika kuwa Masihi, kwa kweli alikuja hapa duniani ili kutuokoa, kwa kweli alizipokea dhambi za mwanadamu katika mwili wake mwenyewe kwa kupitia ubatizo wake, alibeba adhabu yetu na akafa, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo amefanyika kuwa Mwokozi wetu wa milele. Yesu ametuokoa kwa njia hii na ndio maana tunaweza kuondolewa dhambi zetu zote kwa kuamwamini huyu Yesu. 
Ili kuzikamilisha kazi za wokovu, Masihi alipaswa kubatizwa na Yohana Mbatizaji na kisha kufa Msalabani. Hii ina maanisha kuwa tangu mwanzo, sisi tulipaswa kuhukumiwa kwa sababu ya dhambi zetu. Lakini kwa kweli, kwa sasa hatuhitaji tena kuibeba adhabu hii. Kwa nini? Kwa sababu Masihi ambaye alikuwa hana dhambi na ambaye hakupaswa kuhukumiwa adhabu ya dhambi alizipokea dhambi zetu zote zilizopitishwa kwake, na akahukumiwa kwa haki kwa ajili ya dhambi zetu zote. Kwa hiyo, ni kwa kuamini kwa moyo wote katika ubatizo wa Yesu na damu yake ya Msalaba ndio maana tumeweza kuokolewa wote toka katika adhabu ya dhambi zetu.
Tunaweza kuona stika zimeandikwa katika madirisha ya nyuma ya vioo vya magari mengi “upendo wa Mungu kwako!” Je, ni hilo tu ndilo ambalo Yesu anapenda wewe ulifahamu? Wokovu wa Bwana wetu si kitu ambacho kilitengenezwa kwa maneno matupu kama hayo. Yesu anataka ufahamu kuwa, “Ninakupenda sana. Kwa hiyo, nimezisamehe dhambi zako. Wewe niamini tu, nami nitakufanya kuwa mtoto wangu.” Kwa kweli masihi alibatizwa na kusulubiwa, na akamwaga damu yake na kufa, alifanya haya yote ili kutukomboa toka katika dhambi zetu. Kwa kweli Bwana ametuokoa sisi na kutukomboa toka katika adhabu inayotusubiri. 
Bwana alifanyika kuwa daktari wetu ili kuutibu ugonjwa wa dhambi zetu. Kwa kuja hapa duniani, Yesu alizipokea dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa, alisulubiwa na kuimwaga damu yake hadi kifo, akafufuka tena toka kwa wafu na kwa hakika ametuokoa sisi. Wakati tulipokuwa tumefungwa kwa hakika kwenda kuzimu kwa ajili ya dhambi zetu, Bwana amekwisha kutuponya sisi toka katika ugonjwa wa dhambi. Ni lazima tuponywe dhambi hizi kwa kupitia imani sahihi. 
Ikiwa watu wasingetupwa kuzimu hata pale walipofanya dhambi, basi kungekuwa hakuna haja kwa Masihi kuja hapa ulimwenguni na kuimwaga damu yake. Lakini sababu ambayo inatufanya tulazimike kumwamini Yesu ni kwa sababu tulikuwa na ugonjwa wa kutisha wa dhambi ambao ulikuwa unatupeleka kuzimu. Kwa hakika watu wenye ugonjwa huu wa kutisha wa dhambi hawawezi kufanya lolote zaidi ya kutupwa kuzimu, na hii ndiyo sababu inayowafanya pasipo maswali yoyote kuamini katika ubatizo na damu ya Yesu ambaye amefanyika kuwa masihi wetu. 
Wale wote wenye dhambi katika mioyo yao kwa hakika watapokea adhabu ya kuzimu kwa sababu itakapofikia katika sheria ya Mungu, mshahara wa dhambi ni mauti kwa kila mtu. Kwa lugha rahisi, ikiwa mtu ana hata ile dhambi ndogo katika moyo wake, basi mtu huyo atatupwa kuzimu. Hii ndiyo sababu Yesu alipaswa kuja kwetu. Kwa hiyo tunapoamini kwa kweli katika Masihi ambaye amezitoweshea mbali dhambi zetu kikamilifu, basi tunaweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote. Ni lazima tuamini katika Yesu kuwa ni Mwokozi wetu na ni lazima tuamini kikamilifu kwa mujibu wa yale aliyoyatenda kwetu. 
Kwa kweli Yesu ni Mungu mwenyewe. Yeye ni muumbaji wa kweli. Lakini aliuweka mbali utukufu wake wa kimungu na akafanyika mwili wa mwanadamu kwa kitambo ili aweze kutukomboa mimi na wewe ambao alitupenda sana toka katika adhabu ya kutisha ya dhambi na mauti, maangamizo, na laana. Na kwa kweli alibatizwa, akasulubiwa, akafufuka, na kisha akapaa Mbinguni. Huu ni ukweli. Hatuwezi kuuchukulia ukweli huu kiurahisirahisi kana kwamba ni mzaha. Suala la kuuamini ukweli huu mkamilifu si suala la hiari kuchagua. Sisi sote ni lazima tuamini kwa hakika katika ukweli huu halisi katika mioyo yetu na ni lazima tuufahamu kwa hakika. 
Je, kondoo na mbuzi waliotumika kama sadaka ya kuteketezwa walikuwa na dhambi? Hakuna hata mnyama mmoja anayefahamu kuwa dhambi ni kitu gani. Lakini kwa sababu wanyama hawa walizipokea dhambi za watu wa Israeli katika Agano la Kale kwa kule kuwekewa mikono, basi walipaswa kuuawa kwa haki kwa niaba yao. Kwa nini? Kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti na hivi ndivyo Mungu alivyokuwa amedhamiria. Kwa hiyo sadaka ya kuteketezwa ya Siku ya Upatanisho ambayo ilikuwa imezipokea dhambi zote za watu wa Israeli pia ilipasa kufa kwa hakika. Vivyo hivyo ni kwa sababu hizo hizo ndio maana ilimpasa Yesu Kristo kufa kwa kuwa alikuwa amezibeba dhambi zote za ulimwengu kwa kupitia ubatizo wake.
Je, kazi hizi zilifanywa kwa ajili ya nani? Kazi hizi zilifanywa kwa ajili yako na yangu. Je, hiki ni kitu ambacho tuna uhuru wa kukiamini au kutokukiamini? Watu hawaamini kwa sababu hawafahamu vizuri juu ya madhara ya ugonjwa wao wa dhambi zao. Ikiwa wangefahamu ukweli kuwa watatupwa kuzimu hata kwa ile dhambi ndogo, basi wasingeweza kuufikiria wokovu wa Yesu kuwa ni kitu cha kuchagua wanachoweza kuamini au kutoamini pasipo madhara yoyote.
Ikiwa watu wana dhambi hata kama ni ndogo kama punje ya mbegu, basi watu hawa watatupwa kuzimu. Wataangamizwa. Kila kitu wanachokifanya hapa duniani kitaishia katika laana ya milele. Wale wanaofikiria kuwa ni sahihi kuwa na dhambi nina hakika kuwa wanachanganyikiwa. Kwa kweli matokeo ya dhambi ni kifo. Kwa kweli, kuna watu wengi wanaoishi maisha ya kufanikiwa pamoja na kuwa wana dhambi katika mioyo yao. Vijana wako sahihi kuwaabudu watu mashuhuri huku wakiota ndoto kukutana nao siku moja. Lakini je, maisha yao ya kifahari yatadumu milele? Baadhi yao wanageuka kuwa watu wa kuhuzunisha sana mara baada ya huo umashuhuri wao wa dakika kumi na tano kuyeyuka.
Kuna baadhi ya watu ambao kila wanachokifanya kinageuka kuwa kibaya. Kabla hujaonana na Bwana, wewe pia bila shaka ulikuwa mtu wa aina hiyo ambapo karibu kila kitu kilienda vile ambavyo hukupenda. Kana kwamba ulikuwa ukiishi katika maisha ya laana, kila ulichokifikiria kilikuwa ni kitu cha hakika ambacho hakikugeuka kuwa kitu ulichokitaka, na kila ulichodhania kuwa kinaenda vizuri hatimaye kiliishia vibaya. Bila shaka ulikuwa ukiota ndogo kubwa lakini hakuna kitu kilichotokea na ndoto zako ziliendelea kuwa ndogo zaidi na zaidi hadi pale zilipotoweka. Ulipotambua kuwa hata ndoto zako ndogo haziwezi kuwa halisi basi hatimaye ndoto zako zilitoweka kabisa.
Kwa nini hali ilikuwa hivi? Ni kwa sababu ya dhambi zilizokuwamo katika moyo wako. Watu walio na dhambi katika mioyo yao hawawezi kamwe kuwa na furaha. Mungu hawabariki watu wa jinsi hiyo hata wakijitahidi kiasi gani. Hata kama kuna watu ambao wanaonekana kufanikiwa pamoja na kuwa ni wenye dhambi, basi ni lazima utambue kuwa Mungu amewaacha kabisa wao. Ni lazima ufahamu kuwa ingawa maisha yao ya sasa yanaweza kuonekana kuwa na mafanikio, lakini ukweli ni kuwa Mungu amewakatia tamaa na anasubiri kuwatupa kuzimu. Ikiwa ulimwengu huu mzima ungekuwa umejazwa na wasio na dhambi basi kusingekuwa na uwepo wa kuzimu. Lakini kwa kweli Mungu aliitengeneza kuzimu na ameifanya hiyo kuzimu kwa ajili ya watu walio na dhambi katika mioyo yao.
Mungu aliamuru kulitengeneza paa la kwanza la Hema Takatifu la Kukutania kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ili aweze kutoa ondoleo la dhambi katika mioyo yetu. Pia inafunua kuwa wakati kipindi cha Agano Jipya kitakapokuja, Yesu Kristo atazichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kwa kubatizwa na Yohana, na kwamba kisha atasulubiwa hadi kifo ili kubeba adhabu ya dhambi hizi. Kwa hakika Bwana wetu amefanyika kuwa Mwokozi wa wenye dhambi. 
Hii ndiyo sababu Yesu ametoa ondoleo la dhambi kwa wenye dhambi kwa kupitia kazi zake za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Je, unatambua hili sasa? Kwa kweli Yesu Kristo alibatizwa katika Mto Yordani ili kuzichukua dhambi zetu katika mwili wake, na alisulubiwa na kuimwaga damu yake ili kulipa mshahara wa dhambi hizi. Kubatizwa kwa Yesu kulikuwa ni kwa sababu ya kuzibeba dhambi zetu. Je, unaamini kuwa Yesu alikufa Msalabani kwa sababu kwanza alikuwa amezichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana? 
 

Katika Mwili, Mimi na Wewe Tulikuwa Kama Ngozi za Pomboo
 
Paa la nne lilitengenezwa kwa ngozi za pomboo. Neno hili pomboo limetafsiriwa toka katika aina ya mnyama wa kundi la mamalia anayeitwa “Tachash” kwa kiebrania cha Agano la Kale. Mnyama huyu ametafsiriwa katika majina mengine ya wanyama wa kundi la mamalia—kwa mfano, “ng’ombe bahari” (NIV), “sili” (ASV), “ngozi safi ya mbuzi” (NLT), na “pomboo” (NASB). Hatuwezi kusema kwa kina kuwa mamalia huyu yuko vipi. Wanafalsafa wa kibiblia wanasema kuwa asili ya neno hili “Tachash” pengine linatokana na maneno mageni yaliyoazimwa nje ya lugha ya kiebrania. Kwa vyovyote vile, mnyama Tachash ni mnyama ambaye ngozi yake ilitumika katika kutengenezea paa la nne la Hema Takatifu la Kukutania. Na ni vema kusema kuwa paa hili halikuwa la kupendeza na halikuwa na sifa zozote za kuvutia. 
Paa hili la nne la ngozi ya pomboo linaonyesha kuwa Yesu Kristo alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu. Yesu hakuwa na kitu chochote cha kuvutia katika mwonekano wake. Biblia inauelezea juu ya mwonekano wake kwa kusema, “Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani” (Isaya 53:2). 
Kule kusema kuwa Mwana wa Mungu alikuja hapa duniani katika mwili wa mwanadamu na wa kuzaliwa kwa unyenyekevu ilikuwa ni kwa lengo la kutuokoa sisi sote ambao tusingeweza kufanya lolote zaidi ya kuendelea kuishi maisha ya aibu ya dhambi hadi kifo. Wakati Mungu anapotutazama sisi wazawa wa Adamu anatuona pia kuwa hatupendezi kama ambavyo ngozi ya pomboo isivyopendeza. Zaidi ya yote, sisi tunapenda kufanya dhambi tu. Kama ambavyo pomboo ni wachafu, wanadamu wanafurahia kuyalisha matumbo yao tu tangu wanapozaliwa hadi wanapokufa. Hii ndiyo sababu halisi iliyomfanya Yesu kuja katika mwili wa mwanadamu na akateseka kwa mateso. 
Ni wale tu wanaofahamu hatari ya hali yao ya dhambi ndio wanaoweza kumwamini Masihi na kisha kuokolewa toka katika dhambi zao na adhabu ya dhambi. Kwa hiyo, wale ambao hawazifahamu dhambi zao, na wale wasiofahamu na kuamini katika adhabu ya dhambi, basi watu hawa hawastahili kupokea ondoleo la dhambi. Mungu anatueleza sisi kuwa watu wa jinsi hiyo si wengine bali ni kama wanyama (Zaburi 49:20).
Pamoja na kuwa tumeumbwa katika sura na mfano wa Mungu, sio wote wanaoupokea upendo wa Mungu. Wale wasioamini katika mpango wa Mungu wa wokovu hawawezi kupokea ondoleo la dhambi katika mioyo yao na kwa hiyo wataangamizwa kama vile wanyama wanaopotea. Mungu alimuumba mwanadamu katika sura na mfano wake kwa sababu alikuwa na mpango juu yake. 
Hebu jaribu kuangalia kwa karibu juu ya kile ambacho kila mtu anakifikiria au kukitazamia. Sisemi wewe mwenyewe, bali ninazungumzia juu ya wanadamu wote. Watu wengi hawamfahamu hata muumbaji wao aliyewaumba. Zaidi ya yote, wengi wao wanadai kuwa hawatendi dhambi na kwamba wao ni bora kuliko mtu mwingine yeyote. Je, wanadamu hawa ni wajinga kiasi gani? Wale wasiomfahamu Mungu wamejawa na ujinga. Tunapojilinganisha sisi wenyewe na wenzetu wengine, ni tofauti gani hasa tunayoweza kuiona? Je, sisi ni wazuri au wabaya kwa kiwango gani? Halafu kuna watu wanawadhuru wengine ili tu kuzifikia tamaa zao binafsi—hili ni kosa sana.
Hatuwezi hata kufikiria juu ya dhambi ngapi ambazo kila mtu anatenda kinyume na Mungu katika kipindi cha maisha. Sisemi hivi kwa maana ya kuidharau tabia ya mwanadamu, bali ninachofanya hapa ni kuonyesha bayana ule ukweli kuwa ingawa Mungu amewaumba wanadamu kuwa wenye thamani, kuna wengi wao wasiofahamu kuwa wamepangiwa kuangamizwa kwa sababu ya dhambi zao. Watu hawafahamu namna ya kuzitunza nafsi zao; hawawezi kuandaa wakati ujao kwa ajili yao; hawalitambui Neno la Mungu; na hawataki kumwamini Mungu pamoja na kuwa hawana chaguo jingine la kuweza kukwepa maangamizo yao ya milele. Ni watu wa jinsi hii ndio ambao si bora kuliko wanyama wapoteao.
 

Lakini Mungu Hakutuacha Katika Maangamizo Yetu
 
Kwa kweli ili kutuokoa toka katika dhambi, Yesu alikuja hapa duniani, na ili kuzitoweshea mbali dhambi zetu zote, Yesu alibatizwa, akaimwaga damu yake Msalabani, na akafufuka tena toka kwa wafu. Kwa hiyo Bwana amefanyika kuwa Mwokozi wetu wa kweli. Je, unaamini? Kwa namna yoyote ile na kutokana na kutoifahamu Biblia hausemi kuwa, “kuna maana gani? Ikiwa tunaamini katika Yesu kwa kiwango fulani, je sisi sote tutaenda Mbinguni”? Pia kuna wale wanaosema, Ikiwa tutaamini tu katika damu ya Msalaba, basi Mbingu itakuwa yetu.” Je, hii ni aina ya imani iliyosahihi? 
Kwa kweli Mungu ni Mungu wa ukweli. Yeye ndiye aliyezungumza nasi kuhusu mipango yake, na ambaye alizitimiza kazi za wokovu vizuri kabisa kulingana na Neno lake, ambaye ametupatia ondoleo la dhambi, na anayekutana nasi kwa kupitia ukweli wake. Mungu yuko hai. Mungu yupo hapa hata sasa na yupo na kila mmoja wetu. Watu walio na dhambi katika mioyo yao wasijaribu kumdanganya Mungu. Ikiwa watu wana dhambi katika mioyo yao na dhamiri zao zinawashtaki na kuwatafuna, basi ni lazima walitatue kwanza tatizo hili kwa kuamini katika ubatizo ambao Yesu aliupokea na damu ambayo aliimwaga. Wenye dhambi ni lazima waamini katika ukweli kuwa kwa sababu walikuwa wamefungwa kuzimu, Bwana amewaokoa toka katika dhambi zao zote kwa kupitia ubatizo wake na damu yake Msalabani.
Hakuna hata mmoja ambaye hawezi kulishughulikia tatizo la dhambi kwa kuamini katika maji na damu. Lakini hata kama Bwana wetu ametuokoa sisi kwa kupitia maji, damu, na Roho (1 Yohana 5:6-8), ikiwa kwa upande wetu hatutambui na kuamini katika ukweli huu na tukaangamizwa, basi sisi tutawajibika kwa matokeo haya. Sisi sote ni lazima tukiri mbele za Mungu, “Nimefungwa kuzimu kwa kuwa mimi ni mwenye dhambi. Lakini ninaamini katika injili ya maji, damu, na Roho.” Ni lazima tuwe na imani kama hiyo. Ni lazima tuamini katika mioyo yetu kuwa Bwana ametuokoa sisi toka katika dhambi zetu zote kwa kupitia maji, damu, na Roho. Ni lazima tuungane na ule ukweli uliodhihirishwa katika injili ya maji na Roho hali tukiwa na mioyo ya kweli na yenye imani. Ni mpaka hapo ndipo tunapoweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote.
Kwa hiyo, ni lazima tuvifahamu hivi vitu vyote, na ni lazima tuamini katika ukweli wake. Baadhi ya watu wanaamini kuwa “Kwa sababu ninaamini, basi ninakwenda mbinguni pamoja na kuwa nina dhambi” wakati hawaufahamu ukweli uliodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania na injili ya maji na Roho. Lakini Mungu alisema kuwa wote walio na dhambi watatupwa kuzimu; Mungu hakusema kuwa watu wenye dhambi hawatatupwa hata pale wanapokuwa na dhambi ati kwa sababu tu wanamwamini Yesu. Huu unawezekana ukawa ndio ujinga mkuu kuliko wote. Kule kusema kuwa watakwenda Mbinguni ati kwa kuwa tu wanamwamini Yesu, wakati kusema kweli wanamwamini kwa namna yoyote wanayoitaka wao, basi huo ni mwangwi wa ujinga, uzembe, na upofu wa kiimani.
Baadhi wanasema, “sijamuona hata mtu mmoja ambaye alitupwa kuzimu, wala sijamwona mtu yeyote aliyeingia Mbinguni. Hatuwezi kufahamu chochote hadi Siku ya Hukumu.” Lakini kwa kweli kuna kuzimu na Mbingu. Je, humu duniani ni vitu vyote tunaweza kuviona kwa macho yetu ya kawaida? Kwa kweli kuna ulimwengu usioonekana. Wenye dhambi wote wasioamwamini Mungu ati kwa sababu hawamwoni ni kama wanyama wapoteao.
Kwa hiyo, watu ni lazima watambue kuwa ikiwa wana dhambi katika mioyo yao basi kwa hakika wata angamizwa, na kwa hiyo ni lazima waamini katika injili ya maji na Roho ili waweze kuikwepa hukumu ya Mungu. Watu wenye busara ni wale ambao wanatambua kuwa pamoja na kuwa hawajawatendea watu mabaya katika jamii yao inayowazunguka lakini bado wanatambua kuwa wana dhambi nyingi mbele za Mungu, na kwa jinsi hiyo wanakiri kuwa watahukumiwa mara watakapokwenda kusimama mbele za Mungu.
Hatupaswi kupotea kwa sababu ya ujinga wetu na kutomzingatia na kumheshimu Mungu na hukumu yake ya haki. Kwa hakika Mungu atawaadhibu wenye dhambi wote kwa moto wa milele wa kuzimu. Ikiwa watu wataangamizwa kwa sababu ya kutoamini katika ukweli uliodhihirishwa katika Hema Takatifu la Kukutania hata pale ambapo wameusikia ukweli huo, basi watu hao ni lazima watakuwa ni watoto wa Shetani. Kitu ambacho Masihi anakitaka toka kwetu ni kwetu sisi sote kuwa na imani inayotuwezesha kupokea ondoleo la dhambi na kuingia Ufalme wa Mbinguni.
 

Mungu Hakutufanya Sisi Kama Midori
 
Wakati Mungu alipotuumba sisi wanadamu, lengo lake lilikuwa ni kutuwezesha kuishi pasipo kuteswa na dhambi na kufurahia uzima wa milele, ukuu, na utukufu pamoja na Mungu kama watoto wake mwenyewe. Ili kutufanya sisi tusipelekwe kuzimu, Masihi alibatizwa, akazichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake, akaimwaga damu ya Msalabani, na kwa hiyo amezitoweshea mbali dhambi zetu zote. Wakati Mungu ametupenda kiasi hiki, ikiwa basi hatutaukiri upendo huu na kisha tukaamini nusu nusu juu ya wokovu ambao ametupatia, basi kwa hakika hatuwezi kuikwepa hasira ya Mungu.
Mungu ametukomboa sisi toka katika dhambi zetu kwa kumtoa dhabihu Mwana wake. Masihi ametuokoa sisi kikamilifu toka katika dhambi zote za ulimwengu kwa kubatizwa na kubeba dhambi zote katika mwili wake na kujitoa ili kuwa sadaka ya dhambi zetu. Ni kwa sababu tulikuwa tumefungwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zetu, ndio maana basi Bwana wetu alituonea huruma, ndio maana akabatizwa, akaimwaga damu yake hadi kifo, akafufuka tena toka kwa wafu, na kwa hiyo ametuokoa sisi sote toka katika dhambi zetu zote na ametufanya kuwa watoto wa Mungu. Mungu hakutufanya sisi kuwa kama midori yake.
Zamani kidogo, wakati dada mtawa wa kanisa langu alipokuwa chuoni, nilipata bahati ya kuhudhuria mahafali yake. Nikiwa pale katika ukumbi wa maonyesho niliweza kuyaona mabango mbalimbali. Moja ya bango ambalo lilikuwa limechorwa na darasa la wahitimu lilikuwa na bango lililoonyesha Adamu na Hawa wakila toka katika tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya, bango hili liliandikwa, “Je, Mungu aliwafanya wanadamu kama midori?” Mtu mmoja aliandika jibu lake kwa swali hili chini yake akisema, “Mungu alikarahika, na kwa hiyo alituumba sisi kama midori yake.” 
Hakuna kitu ambacho kilikuwa ni kosa kubwa kama jibu hili. Kwa nini basi Mungu aliuumba mti wa ujuzi wa mema na mabaya na kisha akamwambia Adamu na Hawa wasiule mti ule? Zaidi ya yote, Mungu alifahamu kabla kuwa watakwenda kula matunda ya mti ule, lakini bado Mungu aliuumba mti na kisha akawaambia wasile matunda yake. Wakati walipokula matunda ya mti huo, Mungu aliwafukuza kutoka katika Bustani ya Edeni kwa kuanguka katika dhambi. Kisha akasema kuwa wenye dhambi watatupwa moja kwa moja kuzimu. Kwa nini Mungu alifanya hivyo? Je, ni kweli kuwa Mungu alituumba sisi kuwa midori yake ati kwa sababu tu alikuwa amechoshwa? Je, ni kweli kuwa Mungu alimuumba mwanadamu kwa sababu tu alikuwa amechoshwa na upweke na hivyo akaamua tu kutuumba? Kwa kweli sio hivyo!
Kaka zangu na dada zangu, kitu ambacho Mungu alitaka kukifanya ilikuwa ni kutubadilisha sisi kuwa watu wake mwenyewe, kutufanya tusioharibika, na kuishi pamoja nasi kwa furaha milele. Majaliwa ya Mungu katika kuruhusu haya yote kwa mwanadamu ilikuwa ni kutufanya sisi viumbe wasioangamia ambao wanafurahia ukuu wa milele na utukufu na ambao wanaishi milele wakiwa na utukufu. Kwa hiyo, wakati wewe na mimi tulipodanganywa na Shetani, basi tulianguka katika dhambi na tukapangiwa kuzimu, Mungu alimtuma Mwanawe pekee katika dunia hii ili kutuokoa. Mungu ametuokoa sisi toka kwa Shetani kwa kumfanya Mwana kubatizwa na kuzichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake, na kuimwaga damu yake, na kufufuka tena toka kwa wafu. 
Hata hivyo, kuna idadi kubwa ya watu ambao wana mtazamo huu uliopotoshwa kuwa Mungu kwa kiasi fulani alituumba sisi kuwa kama midori yake ili kukipamba chumba chake. Miongoni mwa wale ambao waliacha kumwamini Yesu na wale ambao hawakumwamini kabisa tangu mwanzo, wapo baadhi yao wanaosema katika uchungu wao kwa Mungu kuwa, “Kwa nini Mungu aliniumba na kunifanya niteseke? Kwa nini anasisitiza kuwa ninapaswa kuamini? Kwa nini anasema kuwa atanipatia wokovu mpaka nitakapoamini na si kinyume chake?” Wanasema mambo ya jinsi hiyo kwa sababu hawayafahamu majaliwa makubwa ya wokovu ambayo Mungu amewapatia wanadamu. 
Hii bahati kuu ya Masihi ilikuwa na lengo la kutupokea sisi kama watu wa Mungu na hivyo kutufanya sisi kama watoto wake mwenyewe na kuturuhusu kufurahia utukufu wote na ukuu wa Mbinguni kama familia yake. Hili ndio dhumuni la Mungu la kumuumba mwanadamu. Mimi pia sikuweza kuufahamu ukweli huu mpaka pale nilipozaliwa kwa maji na Roho. Lakini baada ya kupokea ondoleo la dhambi na kuzaliwa tena upya ndipo nilipokuja kutambua, “Ahaa! Kwa hiyo hii ndio sababu Bwana aliniumba mimi!”
Je, Masihi alifanya nini ili kuzichukua kwa kweli dhambi zetu katika mwili wake wakati alipokuja hapa duniani takribani miaka 2,000 iliyopita? Alifanya nini ili kuzibeba dhambi zetu? Aliupokea ubatizo na kuimwaga damu yake! Na haya yalikuwa ni matendo ya haki na dhabihu ya haki ambazo zilimaanisha kuzitoweshea mbali dhambi zetu. 
Hapa kuna sababu kuwa ni kwa nini ni lazima tumwamini Mungu, na kwamba ni kwa nini tumwamini Yesu Kristo kuwa ni Mungu Mwokozi wetu. Ni kwa sababu wewe na mimi tulikuwa tumefungwa kuzimu ndio maana Mungu mwenyewe alikuja hapa duniani ili kutuokoa sisi. Kwa maneno mengine, Yesu alipaswa kubatizwa na Yohana na kisha kufa Msalabani, na kisha kufufuka tena toka kwa wafu. Sababu inayotufanya tuamini katika ondoleo la dhambi lililofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ni ili kwamba tuweze kuondolewa dhambi zetu zote. Ni lazima tuwe na imani ili kuyatimiza majaliwa ya Mungu kwetu. Na tunapoamini katika wokovu wa Bwana hatufanyi hivyo kwa faida ya mtu fulani bali ni kwa faida yetu binafsi. 
 

Sasa Ni Wakati wa Kuamini katika Ukweli wa Wokovu wa Mungu
 
Ikiwa mtu yeyote anataka kuufikia ukweli huu, basi mtu huyu ni lazima aachane na imani yake yenye makosa sasa hivi na kisha aamini katika injili ya maji na Roho katika moyo wake: “Sikufahamu kuwa nilikuwa nimefungwa kuzimu. Nilikuwa ninaamini tu kwa sababu niliambiwa kuwa Yesu alizitoweshea mbali dhambi zetu zote. Lakini imani yangu yote ilijengwa katika uelewa wenye makosa! Sasa ni lazima nijifunze kile kilicho sahihi na kisha niijenge imani yangu katika elimu sahihi. Hadi sasa, nimekuwa nikiamini kwa makosa, lakini bado sijachelewa. Kitu ambacho ninapaswa kukitambua toka sasa na kuendelea ni kuwa nimepangiwa kuzimu kwa sababu ya dhambi zangu, na kuamini katika moyo wangu kuwa Masihi ameniokoa mimi kwa kupitia ubatizo wake na damu yake aliyoimwaga, na hivyo kupokea ondoleo la dhambi zangu. Kwa hiyo nilikuwa nimefungwa kuzimu!”
Kusema kweli, ni Wakristo wachache sana ambao walikuwa na uelewa sahihi juu ya injili ya maji na Roho walipoamini kwa mara ya kwanza. Mimi mwenyewe ilinichukua takribani miaka 10 tangu nilipoanza kuwa Mkristo hadi kufikia hatua ya kufahamu kikamilifu kuwa Yesu alizichukua dhambi za ulimwengu zote katika mwili wake kwa ubatizo wake na kwamba alisulubiwa hadi kifo Msalabani, na ni wakati huo tu ndipo nilipoweza kuokolewa kwa kuamini tena katika Yesu kuwa ni Mwokozi wangu. Kwa hiyo ni baada ya miaka 10 tangu nilipokuwa Mkristo ndipo nilipoweza kuitupilia mbali imani isiyo sahihi na kisha kuja katika ufahamu sahihi wa injili ya maji na Roho na kisha kuiamini kwa usahihi. Lakini kwa wengine, pengine imeshachukua miaka 20 hadi kufikia kuufahamu ukweli na kisha kuuamini. 
Wakati watu wa jinsi hiyo wanapofikia kutambua hata baada ya miaka 20 kwamba Mungu alikuwa amepanga kuwaokoa kwa kupitia maji na Roho, basi ni lazima waamini kuwa Yesu alibatizwa na kusulubiwa kwa ajili ya dhambi zao. Hakuna kitu kinachoweza kuwa ni uovu mbele za Mungu kama kuufahamu ukweli na kisha kukataa kuuamini. Lakini kama wangaliweza kuamini katika injili ya maji na Roho sasa, hata baada ya kuwa wameishi miaka 10, 20 kama Wakristo, basi jambo hili si baya. Hakuna makosa kabisa katika hali kama hii wala hakuna aibu yoyote ile. Wakati watu wanapofahamu kwa kweli na kuamini katika ondoleo la dhambi lililofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, basi kwa hakika watu hao wataokolewa. Imani katika injli ya maji na Roho ndiyo imani inayomfurahisha Mungu. Ninaamini kuwa ninyi nyote mtaamini katika wokovu huu ambao umefikiwa, ambao utimilifu wake ulikuja kwa kupitia nyuzi za bluu na nyekundu. 
Mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania yalikuwa yametengenezwa kwa mafafanuzi ya kina. Kwa kuangalia tu katika ule ukweli kuwa ngozi ya kondoo waume iliyotiwa rangi nyekundu ilikuwa imewekwa juu ya paa la singa za mbuzi, na kwamba ngozi za pomboo zilikuwa zimewekwa juu ya haya yote, basi hapo tunaweza kuona tangazo la wazi la ukweli kuwa sisi sote tulifungwa kuzimu, lakini Bwana wetu alikuja hapa duniani akazichukua dhambi zetu katika mwili wake kwa kubatizwa, na akafanyika kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi zetu hizi kwa kuimwaga damu yake na kufa Msalabani. Sisi sote tunaweza kuamini katika injili ya maji na Roho. Kitu ambacho Bwana ametuokoa kwa hicho ni kazi za Yesu ambazo zinadhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania yanalishikilia fumbo hili la wokovu na si vinginevyo.
Kitu ambacho ni muhimu si tu kule kuisoma Biblia. Kitu kinachomfurahisha Mungu si tu kule kujifunza, bali ni kuamini kwamba ikiwa Biblia inatuambia kuwa Mungu alidhamiria kutuokoa sisi kwa kupitia kazi za Yesu zilizofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, basi wewe na mimi ni lazima tuupokee ukweli huu katika mioyo yetu na kisha tuamini hivyo. Hivi ndivyo tunavyoweza kumpendeza Mungu. Ikiwa tunalisikiliza kwa kweli Neno la Mungu katika mioyo yetu, na ikiwa tunazitambua dhambi zetu, na kisha kuamini katika ubatizo wa Bwana na damu ya Msalaba, basi tunaweza kupokea ondoleo la dhambi zetu. Lakini ikiwa hatuamini katika ondoleo hili la dhambi lililotolewa na Bwana, na badala yake tukamwamini yeye kama suala la kinadharia tu, basi tutaendelea kuteseka kwa dhamiri zenye hatia.
Ikiwa hatulitatui tatizo la dhambi zetu halisi kwa kuamini katika injili ya maji na Roho, basi dhamiri zinazoshitakiwa zitaendelea kuitafuna mioyo yetu. Hata hivyo, ikiwa tunaamini katika injili ya maji na Roho, basi tunaweza kuwekwa huru toka katika dhamiri hizi zenye hatia, kwa sababu wakati tunapofanyika tusio na dhambi kwa kupokea ondoleo la dhambi kamilifu, tunawezaje basi kusumbuliwa tena na dhambi? Hivi ndivyo tunavyopaswa kuamini. Ni lazima tuamini katika injili ya maji na Roho na kulifanya tatizo la dhambi zetu kutatuliwa. Wale wanaoshindwa kufanya hivyo hawana la kufanya bali kuendelea katika kifungo cha dhambi. 
Maisha ni mafupi sana na yaliyojaa mateso. Mungu anaruhusu mateso kwa kila mwanadamu. Kwa nini Mungu anaruhusu mateso ili yatupate? Ni kwa sababu kwa kupitia mateso yetu ya dhambi anataka sisi tutambue uthamani wa injili ya maji na Roho, kuamini katika injili hii, na hivyo kutoweshewa mbali dhambi zetu. Mungu alileta mateso kwako ili kwamba uweze kuamini katika moyo wako kuwa Masihi amezioshelea mbali dhambi zako zote kwa kupitia ubatizo wake na damu yake Msalabani. Kutoamini katika injili ya maji na Roho kuwa ni ukweli ni kitu cha kijinga zaidi kukifanya. Dhambi za mwanadamu zinaweza kuoshelewa mbali na kuwa safi kwa imani inayoamini hasahasa katika injili ya maji na Roho. 
Mungu anatueleza sisi kulitatua tatizo la dhambi kwa kuamini katika injili ya kweli. Hivyo, ni lazima tuamini katika Yesu, Mwokozi wa kweli. Wewe pia ni lazima uamini katika Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wako katika moyo wako. Ni lazima uzikiri dhambi zako mbele za Mungu, uamini katika injili ya maji na Roho, na hivyo kuokolewa. Wakati unapoamini katika moyo wako juu ya ubatizo wa Yesu Mwokozi na damu yake Msalabani, basi kwa hakika utaondolewa dhambi zako zote. Ni pale tu tunapoamini katika ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani kuwa ni kweli ndipo tunapoweza kuokolewa toka katika dhambi zetu zote.
 

Mpangilio wa Mapaa Unawiana Kikamilifu na Mpango wa Wokovu Wetu
 
Inapofikia katika hatua ya wokovu wetu, basi kipaumbele kinakuwa ni kutambua kwanza kuwa tangu mwanzo kabisa tulizaliwa hapa ulimwenguni, na kwamba sisi sote tumekuwa ni wenye dhambi kama pomboo, yaani wanyama wapoteao. Na ni lazima tuamini kuwa tulipaswa kuuawa kwa hakika na kutupwa kuzimu kutokana na dhambi zetu. Zaidi ya yote, ni lazima pia tuamini kuwa ili kukombolewa toka katika dhambi zetu, basi kwa hakika tunahitaji sadaka ya kuteketezwa, na kwa hiyo, Masihi amekuja na kuzibeba dhambi zetu kwa kubatizwa. Ni lazima tuamini kuwa Mwokozi wetu kwa hakika si mwanadamu bali ni Mungu mwenyewe. Na ni lazima tuamini kuwa Yesu Mwokozi kwa kweli ametuokoa toka katika dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo wake na Msalaba. 
Ikiwa isingekuwa hivi, basi Mungu angelitengeneza mapaa mawili tu juu ya Hema Takatifu la Kukutania. Ikiwa wokovu ungefikiwa kwa kuuacha ubatizo wa Yesu, basi kusingekuwa na sababu ya kuwekwa mapaa manne tofauti juu ya Hema Takatifu la Kukutania, na Mungu angelikuwa amelifunika hema hilo kwa ngozi za pomboo na zile za kondoo waume tu. Lakini, ni mapaa haya mawili tu ndiyo yaliyotumika? Hapana! Hema Takatifu la Kukutania lilipaswa kufunikwa kwa mapaa manne tofauti; mapazia yaliyokuwa yamefumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa; na paa jingine liliundwa kwa singa za mbuzi; na bado paa jingine liliundwa kwa ngozi za kondoo waume; na paa la mwisho liliundwa kwa ngozi za pomboo. 
Ni lazima tuamini katika ukweli kama ulivyo kwamba Yesu alizipokea dhambi zetu zote kwa kubatizwa, akafa Msalabani, na kwa hiyo ameziokoa nafsi zetu chafu na zenye huzuni toka katika kifungo cha kuzimu kutokana na dhambi zetu hali akitufanya kuwa watu wa Mungu mwenyewe. Hili ni fumbo lililofichwa katika mapaa manne ya Hema Takatifu la Kukutania, na ule mpangilio wa jinsi ambavyo mapaa haya manne yalivyowekwa si kitu kingine bali ni mpangilio ule ule wa Wokovu wetu. 
Ili kuunganisha paa la kwanza na paa la pili pamoja, yaani yale mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania, basi vifungo vya dhahabu na shaba vilihitajika. Na katika kila kona ya hizi seti mbili za mapazia ambayo kwa pamoja yalilifanya kila paa kulikuwa na kitanzi cha nyuzi za bluu. Lakini kwa wale wanaoamini katika damu ya Msalaba tu, basi ni vigumu sana kwao kufahamu maana ya vifungo hivi vya dhahabu na shaba vilivyoambatanishwa katika vitanzi vya nyuzi za bluu. Ni wale tu wanaoamini katika injili ya maji na Roho ndio wanaoweza kufahamu na kuamini katika ukweli uliofichwa katika mapaa haya manne. 
Vitanzi vya nyuzi za bluu vina maanisha ni ubatizo wa Yesu alioupokea katika Mto Yordani. Kwa nini basi watu hawaamini katika ubatizo ambao kwa huo Yesu alizipokea dhambi zote za ulimwengu katika mwili wake na badala yake wanaamini katika damu ya Msalaba tu? Ni kwa sababu hawaliamini Neno la Mungu kama lilivyo. Tunapokiri kuwa tunamwamini Yesu hatuwezi kumwamini kwa usahihi kwa kuongeza au kupunguza toka katika Neno la Mungu. Ni lazima tuliamini Neno la Mungu kikamilifu kama lilivyo na kulikubali “ndiyo.”
Miongoni mwa watu wengi wanaodai kuwa wanamwamini Yesu, wengi wao wanaamini katika damu tu iliyomwagika Msalabani hali wakiuacha ubatizo ambao Yesu aliupokea. Hii ndio maana Wakristo wengi hawawezi kulifahamu fumbo la ukweli uliodhihirishwa katika mapaa ya Hema Takatifu la Kukutania. Na hii ndio sababu Wakristo wa leo hawaamini katika ondoleo la dhambi kamilifu ambalo Masihi amelitimiza. Wanamwamini Yesu katika hali ya utupu tu kama mmoja wa waanzilishi wa dini za ulimwengu huu. Kwa hiyo, Wakristo wengi wanatembea katika njia potofu. Wanatenda dhambi kila siku, na bado wanadai kuwa wanaweza kwenda Mbinguni ati kwa sababu ya kutubu kila siku. Hali hii inaonyesha jinsi watu wengi wa kidunia wanavyoukataa Ukristo kila siku. 
Tunapowauliza Wakristo, “Ni kwa imani ipi na kwa vipi tunaweza kulitatua tatizo la dhambi zetu?,” basi wengi wao wanasema, “Tunaweza kutatua tatizo hili kwa kutoa maombi ya toba wakati tunapoamini katika damu ya Yesu iliyomwagika Msalabani.” Halafu tunapowauliza tena, “Je, ni kweli kuwa dhambi zako zimetatuliwa na kuondolewa mbali katika moyo wako?,” wanajibu, “Kwa kweli, bado nina dhambi zilizosalia katika moyo wangu.” Watu ambao bado wana dhambi katika mioyo yao basi watu hao si watu wa Mungu. Watu wa jinsi hiyo wapo nje ya Yesu Kristo. Ni lazima waje kwa Yesu Kristo kwa kuamini katika injili ya maji na Roho mara moja. 
Ni lazima tutambue kwa kina kuwa ni kwa mbinu ipi kamilifu ambayo kwa hiyo Bwana wetu amezitoweshea mbali dhambi zetu. Bwana wetu aliweza kuzitoweshea mbali dhambi zetu zote kwa kuzichukua dhambi za ulimwengu hadi Msalabani kwa kupitia ubatizo ambao alioupokea kwa kweli toka kwa Yohana na kisha kwa kuimwaga damu yake. Ikiwa tunapenda kuingia katika uwepo wa Mungu, basi ni lazima tuingie kwa kuamini katika wokovu wetu uliofumwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. Haijalishi ni kwa kiasi gani mtu anaweza kuwa amemwamini Mungu, bado inawezekana kabisa kwa mtu huyo kuamini vibaya na kutofahamu vizuri wakati huo wote. Ili sisi tuweze kuingia katika Ufalme wa Mbinguni ni lazima tuupokee wokovu uliotengenezwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu ambao kwa huo Masihi amezitoweshea mbali dhambi zetu zote kuwa ni ukweli halisi na kisha tuuamini. 
Ikiwa imani yetu mbele za Mungu ina makosa, basi ni lazima tuirekebisha na kuamini tena kwa usahihi hata kama ni mara nyingi. Ni lazima tuamini katika wokovu kwamba kwa kweli Bwana alizichukua dhambi zetu katika mwili wake na akazioshelea mbali dhambi hizi kwa ubatizo wake. Ni lazima tuamini kwa kweli kuwa Bwana alizichukua dhambi zetu katika mwili wake mara moja na kwa wote kwa kupitia ubatizo wake, na kwamba alibeba adhabu yote ya dhambi hizi kwa kupitia damu ya Msalaba. 
Kwa kuwa na imani halisi katika huduma za Yesu zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau na nyekundu za Hema Takatifu la Kukutania, basi sisi tunaweza kuonana na Masihi. Kwa kupitia Hema Takatifu la Kukutania, sasa tumeweza kuipata injili ya maji na Roho kwa upana zaidi na kisha kutambua kuwa imani yake inajengwa katika ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Imani ya muhimu sana ambayo sisi sote tunatakiwa kuwa nayo ni ile inayoamini kwa moyo juu ya wokovu ulioundwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu. 
Kwa sasa tunasikia na kujifunza juu ya ukweli ambao unashikiliwa katika Hema Takatifu la Kukutania ulioundwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Baada ya kuwa amezitoweshea mbali dhambi zetu kwa kupitia kazi zake zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, basi Masihi anatungojea hivi sasa. 
Mungu anakutia nguvu na kukuimarisha wewe kuamini katika ukweli huu kwa moyo wako wote. Je, bado una dhambi katika moyo wako? Basi, ni lazima ninyi nyote mtambue mbele za Mungu jinsi ambavyo dhambi zenu ni nyeusi na chafu, mzikiri dhambi zenu, muamini katika ukweli uliofunuliwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na hivyo mpokee ondoleo la dhambi zenu zote. Unapoamini kwa kweli kuwa Yesu amekwisha kukuondolea dhambi zako zote, basi unaweza kuzipitisha dhambi zote zinazopatikana katika moyo wako kwake na kisha ukapokea ondoleo la dhambi kamilifu toka kwake. 
Sisi sote ni lazima tuamini katika mioyo yetu juu ya ondoleo la dhambi lilifanyizwa kwa nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa ambalo Mungu alilipanga kwa ajili yetu. Mungu ametupatia injili iliyofanyizwa kwa huduma hizi za Yesu za kushangaza za nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na ametuwezesha sisi kupokea ondoleo la dhambi na kuufurahia ukuu wake na nguvu zake na mamlaka kama watoto wake mwenyewe. Mungu ametuwezesha sisi kuokolewa toka katika dhambi zetu zote na adhabu ya dhambi, na kisha kupokea uzima wa milele kwa kuamini katika kazi za wokovu tulizopewa na zilizodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu.
Ninamshukuru Bwana kwa kufanya iwezekane kwetu sisi kuokolewa kwa kuamini katika ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Kwa kuamini katika ukweli huu, basi tunaweza kuokolewa dhambi zetu zote na kuingia katika Ufalme wa Mbinguni kwa imani. Helleluya!