Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-21. Ni nani mzushi katika Biblia?

Mzushi ni yule mwenye dhambi moyoni huku akimwamini Yesu. Katika Tito 3:11 inasema “akijua yakuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hata yeye mwenyewe.”
Yesu alizichukua dhambi zetu kwa ubatizo wake, lakini mzushi haamini juu ya baraka ya Injili ya maji (ubatizo wa Yesu, ubatizo wa ukombozi) ambao ni zawadi ya thamani kwa Mungu, bali yeye hujihukumu mwenyewe kama mwenye dhambi huku akikataa wokovu kamili.
Biblia inaeleza aina hii ya watu kama “wazushi” wenye kumwamini Yesu lakini wakiendelea kujihukumu kuwa wenye dhambi (Tito 3:11) utaweza kushangaa ikiwa wewe nawe ni “mzushi” au la. Ikiwa una mwamini Yesu, huku bado ukijiita mwenye dhambi, basi hujaelewa ukweli wa kiroho wa Injili ya maji na Roho.
Ikiwa utaamini katika Yesu, lakini bado unajichukulia kuwa ni mwenye dhambi asiye na tumaini, hivyo wewe ni mzushi. Maana yake ni kwamba, unadhani Injili ya kweli katika maji na Roho ni dhaifu mno katika kufuta dhambi zetu zote na kutufanya watoto wa Mungu. Ikiwa wewe ni mmoja kati ya hawa waitwao wazushi wenye kukiri imani kila siku mbele ya Mungu ili wasamehewe na kukubali kwamba ni wenye dhambi, basi wewe ni hatari kwa kufikiria upya imani yako.
Utaweza vipi kuwa mwenye dhambi ikiwa Yesu alikwisha beba dhambi zako zote? Kwa nini unaendelea kujaribu kulipia deni ambalo tayari lilikwishalipwa na Yesu kama zawadi kwako? Ikiwa utaendelea kusisitiza kulipia deni hilo binafsi wew ni mzushi! Kwa sababu imani yako ni tofauti na ile aliyo kupa Mungu kila Mkristo aaminiye katika Yesu, lakini hajazaliwa upya ni mzushi. Yakupasa ujue kweli hii. Mungu alizichukua dhambi zote za ulimwengu, na ikiwa utadharau wokovu wake wewe ni mzushi.
Mzushi ni yule ajiitaye yeye ni mwenye dhambi, kwa maneno mengine, mwenye kujihukumu nafsi yake mwenyewe. Je, unadhani ni rahisi kwa Mungu aliye Mtakatifu atakubali mwenye dhambi awe mtoto wake? Ikiwa unajiita wewe ni mwenye dhambi hali una mwamini Mungu Mtakatifu, wewe ni mzushi. Ili usiwe mzushi, yakupasa uamini ubatizo wa Yesu na damu yake Msalabani kama mambo ya kweli.
Utaweza kuokoka ikiwa utaamini yote haya kwa wakati mmoja: ubatizo wa Yesu na damu yake.