Search

Maswali ya kila mara juu ya Imani ya Kikristo

Somo la 1: Kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho

1-23. Nitawezaje kusema “mimi ni mwenye haki” hali kila siku Ninaanguka dhambini?

Sisi kama wanadamu tutaendelea kutenda dhambi siku hadi siku mpaka kifo chetu. Kama ilivyo ukweli huu, hii ni kutokana na asili ya msingi wa maisha yetu; ya kwamba tulitenda dhambi tokea mwanzo Biblia inasema “Hakuna mwenye haki hata mmoja” (Warumi 3:10). Na ndiyo maana Mtume Paulo alikiri mbele ya Mungu kwamba “Ni neno la kuamini, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi ambao wa kwanza wao ni mimi” (1 Timotheo 1:15).
“Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana kuna tofauti kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu” (Warumi 3:21-24).
“Haki” hii ya Mungu maana yake ni Yohana Mbatizaji kumbatiza Yesu Yordani. Alipo taka kubatizwa alimwambia Yohana “Kubali hivi sasa kwa kuwa ndivyo itupasavyo kutimiza haki yote” (Mathayo 3:15). Alibeba dhambi za ulimwengu katika namna ya haki na ifaayo alipobatizwa na Mwakilishi wa wanadamu wote, Yohana Mbatizaji na kwa jinsi hiyo Yohana akaja kushuhudia baada ya ubatizo huo ya kwamba “Tazama! Huyo ndiye Mwanakondoo wa Mungu azibebaye dhambi za ulimwengu” (Yohana 1:29).
Sasa basi, nini maana ya “dhambi za ulimwengu.” Hii inawakilisha dhambi zote za wanadamu tokea Adamu na Eva, wanadamu wa kwanza duniani hadi yule mwanadamu wa mwisho kuishi hapa ulimwenguni. Watu wa kale ni wa ulimwengu huu, watu wa nyakati hizi ni wa ulimwengu huu pia na hata wale wajao majaliwani ni wa ulimwengu huu. Yesu, Alpha na Omega, alitoa sadaka moja kwa dhambi za wakati wote, kwa kubeba dhambi za ulimwengu mara moja za wote kwa ubatizo wake Yordani na kufa msalabani. Na “hivi ndivyo” tumetakaswa.
Kwa uwazi Biblia inatamka “katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu” (Waebrania 10:10). Angali kwamba hii sentensi ni ya wakati uliopo. Tumetakaswa kwa hakika na hatuna dhambi, toka pale tulipo mwamini Mungu hadi sasa na siku zote itakuwa hivyo. Kw kuwa Mungu ni mwenye Enzi, anauweza wa kuona mbali ttoka mwanzo hadi mwisho wa dunia. Ingawa yapata miaka 2000 sasa iliyopita alipobatizwa Yesu, alibeba dhambi zetu zote wanadamu tutendazo toka mwanzo hadi mwisho wa ulimwengu. Hivyo, kabla ya kufa kwake Yesu pale msalabani alisema “Imekwisha!” (Yohana 19:30). Alibeba dhambi zetu zote ulimwenguni miaka 2000 iliyopita na kufa msalabani ili kututakasa.
Bado tunaendelea kutenda dhambi hata baada ya kuokoka kwa sababu miili yetu ni dhaifu. Kwa namna hiyo Yesu ametukomboa sisi sote tokana na dhambi zote za zamani, sasa na za nyakati ijayo kwa kubeba dhambi zote juu ya mwili wake kwa ubatizo na kuhukumiwa nazo msalabani. Hii ni haki timilifu ya wokovu wa Mungu.
Ikiwa Yesu asingebeba dhambi zetu zote hata zile tutakazo tenda mbeleni, basi pasinge kuwepo mwanadamu yeyote aliyekombolewa kwa dhambi za kila siku, “kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23) wakati Yokobo na Esau walipokuwa bado tumboni mwa Mama yao, Mungu aliwatenganisha kuwa mataifa mawili hata kabla hawajatenda mema au mabaya mbele zake, na alimpenda Yakobo na kumchukia Esau na alisema “Na mkubwa atamtumikia mdogo” (Mwanzo 25:23). Ujumbe huu una maana kwamba wokovu wa Mungu hauna lakufanya juu ya matendo yetu ya sheria, bali hutolewa kwa wale wenye kumwamini Mungu kwa usahihi katika wokovu wake ulio kwenye ubatizo wa Yesu na kusulubiwa kwake.
Sisi wanadamu tumewekewa mwisho wetu kuwa motoni kama viumbe waovu toka mwanzo tulipozaliwa hadi tutakapo kufa lakini Mungu alitangulia kuona dhambi zetu kabla ya yote, na kuzisafisha zote mara moja kwa wote kwa ubatizo wa Yesu na msalaba wake kwa sababu anatupenda tunaishi kipindi cha baraka. Nabii Isaya alisema “Semeni na moyo wa Yerusalemu, kawaambieni kwa sauti kuu ya kwamba, vita vyake vimekwisha uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi zake zote” (Isaya 40:2). Kipindi cha utumwa wa dhambi kimekwisha kwa kupitia ubatizo wa Yesu na msalaba wake, hivyo, yeyote aaminiye Injili ataokolewa na dhambi zake zote. “Hili ni agano mtakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, nitalia sheria zangu mioyoni mwao na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo, dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa. Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi” (Waebrania 10:16-18).
Mungu hatuhukumu kwa dhambi za kila siku tena kwa sababu alikwisha tutakasa sisi wanadamu na kuhukumiwa nazo kupitia Yesu.
Na kwa matokeo hayo tutaweza kumsubiri yule ajaye, Bwana na kufuata Neno lake, kama aliye mwenye haki asiye na dhambi, ingawa bado tunaendelea kutenda dhambi maishani.